[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 01" 0746638941 Whtsp.
UTANGULIZI.
Siku zote katika maisha unaambiwa upendo wa mtu, ndugu, rafiki au Mpenzi alieko mbali na wewe mahusiano yake muda mwingi huwa ni ya kawaida kuliko mtu aliye karibu yako! Wanasaikolojia wamejaribu kufatilia swala hili na kulipa asimia kadhaa! Huku watafiti mbalimbali wanaosoma maisha ya mwanadamu na wao wakathibitisha hilo! Kuwa upendo wa mbali huwa umepoa kuliko upendo wa karibu! Ili kujua mengi Ungana nami katika mkasa huu naimani utajifunza mengi zaidi.👇👇👇 ( Ukifatilia vizuri simulizi hii ndio utagundua Simulizi ya IKAWE KHERI MY DUFFER Kiini chake kilianza Huku)
Jijini Mwanza alionekana ni Binti mmoja muda wote alikuwa na simu yake ndogo akijaribu kuandika meseji kwenye simu yake baada ya kumaliza kuandika Aliishia kufuta ule ujumbe Huku akifunga macho yake kwa uchungu Sana! Huku akitafuta namna ya kufuta kumbukumbu za nyuma zilizowahi kumpata!
Muda huo Ilikuwa ni majira ya usiku! Baada yakuona maumivu aliyonayo hawezi kuyavumilia, alishuka chini Huku akikumbatia mto wake alitoa Sara kwa Muumba wake Huku akisema" Eee Mwenyezi Mungu nipe Amani ya moyo" baada ya kumaliza Sara yake alirudi tena kitandani Huku akiutafuta usingizi kwa Mara nyingine mpaka kukapambazuka!
Asubuhi Kuna mtu alikuja kwenye mlango wake kumgongea hodi ilibidi aamke akafungue, Alipofungua mlango akabaki kustaajabu kwanza baada ya kumuona Binti mmoja kamnyoshea mkono mmoja Huku mkono wake wa pili kauweka kiunoni, na kichwa chake alikibinua kukielekeza Upande wa pili, ilibidi amhoji kwanza;
"" Falaja! Ndo Asubuhi hii umeijia pesa!? Nimekwambia ungoje mwisho wa mwezi nitakugaia tu!"
'" kunigaia tenaa!? Si mtu chake apewe! Hafu mbona wajidhalilisha you are the Doctor! Watu wote wanakujua mtaani Doctor! Doctor afu pesa ndogo hiyo ushidwe kuipata kweli!?"
"" Please Falaja! Mbona wewe huwa NI rafiki yangu Sana! Sahii huniamini kweli!?"
"" Nakuamini! Ila nimepita kukumbushia tu! Na kesho nitapita tenaa! Ila sio ka nakuchukia usijisikie vibaya!"
Baada ya falaja kuondoka, Binti huyo Aliingia ndani Huku akishika simu yake tenaa aangalie Kama Kuna ujumbe umeingia, alikutana na meseji moja ikimuita aende sehemu alijaribu tena kuitizama vizuri Ile namba make ilikuwa kuwa ngeni, ilibidi arudie tena kusoma ule ujumbe.
"Dr. Janerose! Njoo hapa karibu na Ofisi ya kata! Nina mazungumzo na wewe!"
Ujumbe ulioingia ndio ulitujulisha moja kwa moja Majina ya Binti huyo ni Janerose! Ilibidi afate njia haraka huenda itakuwa ni dili la kazi zake, baada ya kufika hapo alikaa Kama dakika tano haoni mtu ilibidi amtumie mtu yule aliyemhitaji, muda kidogo alitokea. Janerose alikuja kupiga jicho hivi na kubaki akitabasamu kwanza.
"" Aaah! Kumbe ni wewe Hussein!? Mbona umetumia no ngeni tenaa!? Nakwaminia kwa madili upo vizuri! Haya Dili gani Hilo?
"" MVA!?" ( kusafisha mimba iliyoharibika tumboni, au mtu alikuwa ana abot mimba ikakataa kutoka ndio humfanyia MVA)
"" Sangapi!? Na wapi!?"
"" Kazini kwetu! Harafu ni usiku itakuwa! Nmekutonya mapema! Leo usiku naingia Night Hafu niliyekuwa nategemea kuingia nae Dr. Jayce mwanae mgonjwa wewe fanya mawasiliano nae ili umshikie zamu tumake money!?"
"" Usijali, ngoja nimtafute make nimefurumishwa asubuhi tu na Falaja!"
Janerose alitafuta namba haraka akaongea na Jayce, walielewana vizuri make hata Jayce alitaka ampigie simu amuombe msaada! Baada ya kumaliza kuwasiliana alibaki kufurahia tu, lakini Kuna Huzuni ilimwingia tena ikamfanya anyong'onyee.
Hussein aliliona Hilo ilibidi amshike mkono Huku wakielekea kwenye mgahawa mmoja, Hussein alimuagizia supu na yeye akaagiza, lakini alishangaa baada ya kumuona Janerose kailudisha ilibidi amhoji.
"" Vipi tenaa!? Mbona wairudishaa!?"
"" Situmiagi bhana Nyama ya Ng'ombe", umesahau!?"
"' Daaah sorry!" "Mhudumu tofauti na supu ya Ng'ombe una supu gani nzuri nzuri! Mchumba wangu apate.
"" Hamna! Labda Maharage!"
Janerose Aliishia kutabasamu kwanza make utani wa Hussein ni mwingi.
"" Hapana! Nitatumia chai ya maziwa na vitafunwa!"
"" Daaah! Pole Sana! Ani Mimi huwa nawahurumia watu ambao hawali Nyama ya Ng'ombe! Mnajua huwa mnakosa vitu vizuri nyiee!?" Okay! nambie mbona huna furaha tenaaa au mmeanza tenaa na Mwenzako!?"
"" Muda mwingine naona Kama nakukosea kuwa nakuelezea haya yote! Ani Kila Siku kukicha ni toleo jipya utafikili wasoma.. "Magazeti leo!?"
"" Pole!! Yataisha tu Ila hutakiwi kuwa mnyonge kiasi hicho!? Harafu punguza stress utakonda shauri yako!?"
Janerose Aliishia kumuangalia Hussein Huku akiangua kicheko, make NI rafiki yake wa karibu Sana muda mwingi akipata shida humpelekea ili amliwaze hata Na huu utani utani ulikuwa ukimjenga kwa namna moja au nyingine.
+++++++++++++
( Janerose ni Binti kaajiliwa kwenye kituo Cha afya, anafanya kazi na Hussein, Falaja na Jayce pamoja na watumishi wenzake kadhaa. Hussein ni mtu wa karibu Sana na Janerose Ani ni marafiki walioshibana muda wote huelezeana shida zao na umri wao wamepishana Miaka miwili Ani Hussein ndio mkubwa.
Janerose yupo kwenye mahusiano na mkaka mmoja( Shamsi) anaekaa mkoa mwingine tofauti na makazi alipo yeye.
Kuhusu Hussein mahusiano yake huwa hayaweki wazi Sana japo huwa anamdokeza Janerose huyu ndie wifi yako, Mara yule na ndio maisha yao walivyokuwa wakiishi, Ila urafiki wao ulikuwa ni wakuheshimiana Sana kwenye serious huwa NI serious kweli na Kama ni utani hutaniana,
Kwenye Mahusiano Upande wa Janerose mchumba wake( Shamsi) alikuwa Kama anamzingua hivi make wamedumu kwenye mahusiano takribani Miaka mitano ahadi zao zilikuwa hazitimii japo mawasiliano yalikuwepo, ni Kama mwaka kesho nitakamilisha kufika nyumbani, na hii ilipelekea Janerose kuzoea maneno ya shamsi ni Kama ya kawaida Sana ani kumuamini Ni pale kakanyaga kwao.
Mbaya zaidi muda mwingi walikuwa wakitofautiana na Shamsi kwasababu ya wivu, muda wote Shamsi alikuwa hamuani Janerose pindi yupo mbali nae kama hamsaliti? Na muda mwingi alikuwa akiziunganisha simu zake ili kuangalia watu wanaowasiliana nae, na huwa wanazungumzia Nini muda mwingi huo akiongea na simu.
Lakini kwa maisha ya nyuma kabisa kabla hawajawahi kakutana wakawa wapenzi, Kila mtu alikuwa na mpenzi wake kwa Shamsi alikuwa na mdada mmoja mwalimu wakaachanaga kiaina, Huku kwa Janerose alikuwa kwenye Mahusiano na mkaka mmoja walikuwa tayari wameachana ndio akaja kuwa na Shamsi na hii ni miezi sita ilipita ndio akawa na Shamsi.
Lakini kwa Shamsi Aliingia kwenye mahusiano Huku mguu mmoja Bado upo nje akiendelea kuwasiliana na mtu wake wa zamani japo alimhakikishia Janerose kashaachana nae, mahusiano yake yalianza kunoga mpaka ikapelekea kutokumjali tenaa Janerose, bila Janerose kumtafuta ndio imeisha hiyo, Khari hii ilimpelekea Janerose kuchoka akaamua kumnyamazia pasina kumtafuta mpaka miezi mitatu ikapita akaamua kuvunja mahusiano kimya kimya hata hivyo alikuwa keshachoka na ahadi zake, akawa amepata mkaka( Denison) na yeye ana fani Kama yake(Dokta) wakaanza urafiki baadae mahusiano yakazaliwa yalikuwa ni mahusiano Moto moto lakini haikuwa bahati yake, kijana huyo alihamishwa kazi akapelekwa Morogoro ule ukaribu wa awali ukawa umepungua ikawa ni kuwasiliana kwa simu tu Huku wakipeana ahadi nyingi watakuja kuonana na wakakaa karibu tena.
Upande wa Shamsi aliendelea kumfatilia Janerose akaja kugundua kwasasa tayari ana mtu, aliamua kujirudisha kwa Kasi Huku akiomba msamaha wa hapa na pale, Janerose ilibidi amsamehe make hata yule kijana aliyekuwa akimpa kampani kwasasa hayupo ilibidi kurudiana na Shamsi make hata hivyo alikuwa kamzoea Sana! maisha yakaendelea japo kelele za nyuma zilirudi vilevile Huku akijitahidi kumvumilia huenda atakuja kubadilika mbeleni akaishi Kama wanaume wengine wanavyoishi na haya ndio yalikuwa matumaini yake.
Tuendelee tulipoishia.....
Baada ya kumaliza kunywa chai waliachana Huku Kila mtu akimuahidi mwenzake kuwahi. Janerose aligeuka mdogo mdogo Huku akiondoka lakini Hussein alimuita tena Huku akimuendea..
"" Sorry! Nlisikia kwenye Mazungumzo yako ulimtaja Falaja vipi anakudai? Make Falaja muda wote akimtafuta mtu ujue ni pesa yatafutwa tu!"
Janerose alitingisha kichwa Ishara ya kukatataa lakini alitamani hata kumuomba amsaidie pesa ili amludishie Falaja, lakini hofu ilitanda juu yake Huku akifikilia Kama atamuomba Hussein pesa si atajiuliza huyo Bwanako huwa hakuhudumii hata balance huna?
"" Vipi mbona hunijibu tena!? NI anakudai!?"
"" Mhu mhu! Huku akitikisa kichwa chake!"
Hussein Aligundua kabisa Janerose itakuwa anadaiwa Aliingiza mkono wake mfukoni akatoa wallet Kisha alichomoa elfu kumi tatu Kisha Alimpatia Janerose.
"" Itakusaidia hii! Mimi huwa naumia kukuona unakosa furaha kiasi hicho! Ani mpaka napata hasira natamani nimjue huyo jamaa anaekufanya ukose furaha!"
Janerose alibaki akimtizama Hussein mpaka anaishilia na yeye alianza kurudi mdogo mdogo nyumbani kwake, njia nzima alibaki akijibizana na sauti pamoja na mwili Huku akiwa na furaha pindi anapokumbuka wema wa Hussein.
....... Itaendelea.......
Usikose sehemu ya 02.
Simulizi yetu mpya ndio tumeianza! Naomba Ushirikiano wenu wa Dhati mpaka tufikie tamati!
Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 02" 0746638941 Whtsp.
Janerose alibaki akimtizama Hussein mpaka anaishilia na yeye alianza kurudi mdogo mdogo nyumbani kwake, njia nzima alibaki akijibizana na sauti pamoja na mwili Huku akiwa na furaha pindi anapokumbuka wema wa Hussein.
ENDELEA.....
Ilikuwa ni Siku nyingine tenaa Janerose siku hiyo Aliingia kazini kutimiza wajibu wake, ikiwa ni pamoja na ahadi yake walivyokubaliana na Hussein wanasema Dili lilitiki vizuri! Akawa amepata pesa ilibidi apitilize moja kwa moja kwa Falaja kumumalizia pesa yake!
Majira ya jioni aliamua kumtembelea rafiki yake Hussein, alimkuta yupo nje akifua fua nguo ilibidi aanze kumsaidia kwa nguo zilizobakia.
"" Vipi sahii unae furaha!? Hafu ulikuwa wakataa Falaja hakudai, mida Ile tu tumeachana nilikutana nae akanambia! "Vipi umemlipa ukabakiwa na chochote!?" Hussein Alimhoji.
"" Achana nae bhana! Sa hii hanidai tenaa!? Vipi lini tena tu make money!?
"" Kumbe wapenda pesaa ee!?"
"" Kawaida ila sio Kama Falaja! Hafu naona uko busy sana na kuchart, Ni wifi Nini?"
"" Aaa! Siku nikimpata nitaringa! Wewe washa data Uone Stutus yangu ilivyochafuka. ( Huku akicheka)
Janerose Aliingia mtandaoni haraka Kisha Aliingia Stutus ya Hussein kuangalia kitu alichoweka, Aliishia kucheka tu, baada ya kukutana na neno "Special My Valentine's" Huku picha ake imewekwa.
"" Kwahiyo muda wote upo unahangaika kuni edit!?"
""Yaah! Coz ni my valentiner!" Vipi wapenzi wako wamekupost au ni Mimi tu ndie nliyebakia muwakilishi wao!?"
"" Umeanza bhanaa!! Ama ndio Sina kabisa!"
Janerose aliamua aangalie kwenye akaunt ya Shamsi Kama kweli kampost, alikutana na picha ikiwa ni watu watatu, Dada zake wawili na wa katikati alikuwa ni mchumba wake wa muda mrefu aliwahi kuwa nae, Kisha alimalizia kusoma caption kwa chini, "" My Valentine's" ilimchanganya kiasi chake lakini aliamua kuipotezea.
"" Vipi mbona mnyonge tenaa!? Au ndio makusudi tena kakufanyia!?"
"" Nia yake nisiwe na furaha tu, anajua kabisa huyu mwanamke huwa twazozana Kila Mara lakini anamuweka makusudi tu, Et wao kwasasa washabaki marafiki wakuheshimiana, Hadi kwao huwa anaenda kusalimia wazazi! Hivi hata Wewe Hussein ukiwa na mtu utakuwa wamfanyia hivyo!?
"" Aah! Siwezi Ani nikapata mtu Kama Wewe afu nifanye ukatiri kiasi hicho hapana kwa kweli!"
"" Mwenzako ndio anafanya!"
"" Achana nae harafu leo nataka nikutoe Out!"
"" For sure!!?"
"" Sinaga ahadi zisizotimia siku zote! Hasa kwa rafiki yangu nmpendae!"
Janerose aliishia kumtizama Hussein Kisha alimshika mkono nakuingia nae ndani Kisha aliwasha TV aangalie kinachoendelea na hi NI baada ya kusikia Kuna kipindi Cha wasafi Kuna msanii anahojiwa.
"" Daah!! Kumbe ni yeye kabisa! At alikuwa na yule msanii! Wakaachana kisa wivu! Daah!"
Hussein alibaki akimtizama Janerose aliona akili yake iko mbali Sana aliamua kuzima TV Kisha akafungulia music, hafu mkono mmoja alimshika Janerose akiomba waDance.
"" Kucheza wajua kumbe, Harafu nikawaza leo waenda kuniaibisha Pup!"
"" Mimi siendi huko bhana! Hafu naona aibu kucheza mbele ya watu nisiowajua!"
Mziki ulikatishwa na mwito wa simu ilibidi Hussein akapokeee, aliishika ile simu Huku akiangalia mtu kapika alimsev Resious( Rehema)
"" Vipi mbona hupokei tenaa! Au ndio wanawake wako unaotaka ukanikutanishe nao Pup!"
"" Huyu ni Resious! Ni rafiki yangu pia!"
"" Mhuu! Sawaaa!"
"" Sawa Nini!?"
"" Recious!!?"
"" Una matatizo...!"
"" Hata Wewe unayo..!""
Utani wao uliendelea baadae Janerose aliamua kuondoka ili ajiandae na mtoko wa jioni, wakati akiwa anatoka ndani alikutana na Falaja pamoja na Jayce wakija kwakee!
"" Vipi leo, huo ndio mtoko wa pamoja na yule rafiki yako Hussein!? Jayce aliuliza.
"" Ndio manake, ngoja tukaoshe machoo leo!!"
"" Mi nikajua Shamsi kaja kumbe ni Hussein!?' Ila itakuwa nyie mwapendana na huyo rafiki yako ee!?"
"" Si kweli....!!!"
Janerose aliamua kuondoka lakini alikuwa ni mtu mwenye mawazo Sana baada ya kusikia jina la Shamsi! Alifungua tena simu yake akiangalia huenda Shamsi kamuweka kwa Stutus alikutana na maua ya Valentine's yaliyoeditiwa vizuri huku Caption ilifata "Kwako my son" aliview nakuachana nayo, Kuna kumbukumbu za nyuma zilimuijia ghafra alipomkumbuka Denison! Aliishia kutabasamu Huku machozi yakimtililika.
"" Kweli vitu vizuri huwa havidumu alikuja kwangu kwa mda mfupi tu akanifanya niwe na furaha leo sipo naye tenaa!! Alikuwa kijana mzuri mwenye tabasamu lake zuri! Hana makuu na mtu lakini walimuhamisha! Mbaya zaidi hata simu yake haikuwahi kupatikana tenaa hata rafiki zake na wao hawampati tenaa!!?"
Muda huo huo Simu yake iliita alikuwa ni Doctor Sharifu rafiki yake na Denison alipokea simu kwa umakini akisikilizia.
"" Naam! Doctor Sharifu!! Kuna chochote kile umesikia kuhusu Denison!!?"
"" Fanya hivi..!! Una muda sahii tuonane!?"
Janerose aliangalia saa yake Huku akiwa bado kaweka simu sikioni.
"" Ndio! Nipe location tu!"
Baada ya kupewa Location ilibidi aondoke haraka Hadi ile sehemu walipoahidiana. Alimkuta tayari Sharifu kafika Huku akishushia Wynne yake taratibu.
"" Vipi? ni Nini umepata kuhusu Denison!? Ni, amerudi!?"
Sharifu Alimpatia Karatasi mbili nyeupe mbili, alizifungua kuzitizama kwa ndani ndipo anakuta picha yake imechorwa kwa penseli, alitizama vizuri Huku akisoma ujumbe uliofuata kwa chini ilikuwa ni "" Utatunza kumbukumbu yangu nitakapokuwa mbali na Wewe!?"
Alichukua karatasi ya pili ndipo anakutana na picha ya Shamsi imechorwa, aliangalia picha ya kwanza ikamthibitishia mchoraji atakuwa ni mmoja ndipo alibaki akijiuliuliza.
"" Ina maana Denison alikuwa akimfatilia Shamsi? Mbona Ni yeye kabisa kamchora alikuwa na maana ipi!?"
Baada ya kumaliza kutathimini pasina majibu alimrudishia picha Sharifu, Huku akiwa amemtolea macho;-
"" Nini manake hii!?"
"" Wewe si unamtafuta Denison!? Mimi nimefanikiwa kupata hivi vitu kwenye fille lake la kuhifadhia Documents nikaona nikushilikishe huenda majibu utakuwa nayo Wewe!?"
"" Ani kuniita kote huko ulitaka kunionesha picha tu, wakati hata Wewe hujui kinachoendelea!"
"" Okay! Nilitaka kukukalibisha kwenye hii party ujumuike na Wewe! Basi agiza chochote uoshe ulimi kwanza!"
Janerose ilibidi atulie aangalie Party ilivyokuwa ikiendelea! Kwa mbali alimuona Falaja akiingia Huku akiwa ameupala lakini pembeni yake alikuwa na Hussein na mdada mmoja waliingia na kukaa pamoja! Janerose ilibidi akae kimya make alikuwa kwenye sitofahamu alibaki akijiuliuliza. "" Inamaana Hussein alikuwa akimleta pale!? Na huyo Binti ndie alimpigia simu!? Sasa kwanini ulitaka kunikutanisha na wanawake zako!?"
Maswali yalizidi kuwa mengi Huku akizidi kutoa macho angalau aone vizuri, huenda macho yake yalikuwa yana ukungu! Ilibidi asimame kwanza ili aone vizuri huenda muda mwingine aliona ni Kama kawa mfupi.
Sharifu na yeye alikuwa akimtizama tu, lakini moyo wake pia uliuma Ghafra, kabla hajaona kinachoendelea alifanya kumvuta mkono Huku akimkalisha chini, alichukua Juice akamumiminia kwenye Grass Kisha alinyanyua mkono wake wenye Grass akimpatia.
"" Tafadhari hebu kunywa kwanza! Achana na Mambo ya watu!!"
.... Inaendelea....
Usikose sehemu ya 03.
Kipi kinaendelea baina ya Hawa watu? usikose kufatilia simulizi hiii naimani utajifunza vingi.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 03" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Sharifu na yeye alikuwa akimtizama tu, lakini moyo wake pia uliuma Ghafra, kabla hajaona kinachoendelea alifanya kumvuta mkono Huku akimkalisha chini, alichukua Juice akamumiminia kwenye Grass Kisha alinyanyua mkono wake wenye Grass akimpatia.
"" Tafadhari hebu kunywa kwanza! Achana na Mambo ya watu!!"
ENDELEA....
"" NI kipi kinaendelea kwanza!!? "
"" Mbele yako....!!" Akitumia Ishara ya kichwa kumuonesha
Janerose aliinua kichwa tena ili atizame kinachoendelea alimuona Shamsi akiwa kabebelea mtoto wa Jayce wakiingia, waliingia na kukaa sambamba na Jayce kwa mahaba mazito kabisa! Kitendo hiki kilimuacha mdomo wazi Janerose;
"" Inamaana Jayce na Shamsi wanafamiana? Inakuwaje Shamsi ahudhulie party ya Birthday ya mtoto wa Jayce ( Patricia) Au ndio kazaa nae?"
Upande wa Hussein kumbe na yeye alikuwa haelewi kinachoendelea mbaya zaidi hata Shamsi alikuwa hamfahamu Kama ndie yupo mbele harafu ni mchumba wake Janerose! Aliishia kupiga makofi Huku akiwa na Falaja pamoja na Resious.
"" Daaah! Naona mlitaka kuni suprise leo! Mmening'ang'aniza kweli nifike hata hivyo nlikuwa na mtoko na rafiki yangu! Sijui kwanini hakupokea simu zangu tu! Au ana Dharura nimcheki tenaaa!!?"
Resious aliwahi kumshika mkono ili asichukue simu akampigia Janerose.
"" Wewe nae!! Janee katolewa out na mchumba ake mpya! Wewe si ni rafiki tu kwake? mbona unajari Sana kuhusu yeye!!?"
Hussein hakuwa na usemi tena hata hivyo hakuwa na kosa, ila tatizo ni Janerose kutopokea simu zake na kumjulisha kwanini kagailisha out yake!?"
Huku kwa Janerose muda wote alikuwa akiugumia moyoni, maumivu aliyokuwa nayo yalikuwa hayabebeki, Alimtizama tena Sharifu ambae alikuwa kakaa nae alimuuliza;
"" Kwanini Sasa hukuwahi kuniambia mapema Kama Shamsi kazaa na rafiki yangu Jayce? Harafu kwanini umetaka nione kinachoendelea Kati yao! Shamsi ni Mwanaume wangu nilimpenda na nilitegemea Siku moja tuishi mke na mme! Kwanini yote haya yanatokea lakini!?"
Janerose alibaki akilaumu muda wote alitamani aondoke lakini alishidwa. Wakati huo Jayce alimuomba Hussein amsaidie kufungua Shampen, Hussein bila hiana pamoja na manjonjo yake alianza kucheza nayo kwa umaridadi mkubwa baadae aliifungua Huku watu wote wakipiga makofi pamoja na kelele za shamrashamra za Sherehe.
Muda huo Janerose hakuwa na ujasiri hata wakuinua mguu tena kuondoka pale alibaki ameegama mezani Huku machozi yakimtililika tu.
Upande wa Falaja pamoja na Resious walikuwa wanajua Kila kitu kinachoendelea mbaya zaidi hata sehemu alipokuwa amekaa Janerose walimuona.
Hussein baada ya kufungua alikuja kukaa pamoja na Resious na Falaja, baadae kabisa Falaja aliamua kumnong'oneza sikioni Hussein.
"" Unamuona huyo Bwanake Jayce! Ndie mchumba wake na Janerose na huyo ndie Babake na Patricia."
"" Aaah! Ani mchumba wake Janerose anaemsemaga Kila Siku Shamsi! Shamsi! Ndie huyo mbele!!?"
"" Ndio, mbona Ni muda umekuwa! na mwezi kesho anaenda kumalizia kutoa mahari kwao!!""
'" Serious!!? Make Wewe utani mwingi at!!"
"" Ayaa! Shauri yako na Janee yupo hapa anashuhudia tukio! Sa sijui yupo na Nani!? Nimemuona yupo na mkaka fulani smart hivi!!"
" Wapi..!?" Huku akisimama kuangaza.
Falaja na yeye aligeuka kutizama lakini hakukuwa na mtu tenaa.
'" Itakuwa wameondoka make walikuwa kwenye viti vilivyo wazi hapo nyuma!"
Hussein hakuamini kabisa Kama ni kweli Janerose kushuhudia tukio mbele yake, alitoka Nje Huku akitafuta simu yake ili ampigie kumbe aliisahau sehemu alipokuwa amekaa! Alirudi na kuikuta ipo mikononi kwa Resious.
"" Nitakutafuta baadae ngoja nikaongee kwanza na Janerose! Ila mmemfanyia ukatiri Sana mwenzenu! 'Sijapenda!"
Hussein alichukua simu yake Huku akiendelea kumtafuta, simu iliita tu pasina kupokelewa alijaribu Kama Mara tatu baadae namba ikawa haipatikani kabisa.
"" Kwanini tenaa hupatikani Janerose! Hebu niambie Nani atakufariji kwa wakati huu, washa simu angalau nijue wapi ulipo!?"
Alichukua usafiri Hadi nyumbani kwake na Janerose, alikuta mlango umefugwa na komeo ilibidi akae kwanza akitafakari ni wapi atakuwa.
Huku kwa Janerose aliondoka na Sharifu wakaelekea nyumbani kwake, Janerose alifika akapumnzika sebuleni Huku akiwa amejilaza kwenye Kochi, kichwa chake alikiangalizia juu ya singboard Huku akizidi kuyarudia matukio kwa kuyapangilia tangu anatoka kwake akutane na Jayce na Falaja kumbe ndio ilikuwa ni safari ya kuja kwenye Birthday.
"" Vipi wajisikiaje kwasasa!? Naomba Achana na Mambo uliyoyaona Sasa ni wakati wa kumove on! Kila Jambo huwa Lina wakati wake, chukulia huu Ni Wakati wa kufanya maamuzi sahihi!"
"" Doctor Sharifu!! Kweli moyo wangu unauma! Naona hata mwili nao unauma! Wazani sahii Nina maamuzi basi!! Hata Hussein nae kawa mchochezi na Alijua kabisa Jambo hili ila hakuwa muwazi kwangu! Daaah! Naumia Sanaa!"
"" Basii!! Pumnzika kwanza! Mie pia ngoja nijinyoshe ukiamka nambie!"
Sharifu Aliingia chumbani kwake kupumnzika Kama robo Saa, mlango ulisikika Kuna mtu alibisha hodi, Janerose alishituka alitizama mlango wa Sharifu wa Chumbani Kama anaamka baada ya kusikilizia ana koroma ilibidi akafungue, ile anafungua alikutana na mdada akiwa na begi pamoja na mkoba Aliingia Hadi ndani Huku akimkata jicho la kwanini!
Janerose alibaki akimtizama Huku akiwa na hofu Sana.
'" Itakuwa Ni mkewe Sharifu ama ikoje hafu mbona kaniona akawa na hasira na Mimi !?"
Binti yule Alipitiliza Hadi chumbani kwa Sharifu, alimkuta Sharifu akiuchapa usingizi alimfurumusha kwa makelele;
"" Nilijua tu, huwezi kuwa na subira na Mimi Mara hii tu ushaanza kuniletea wanawake humu ndani, Haya kamtoe huyo mwanamke wako nje kabla sijamharibu sura!"
Sharifu ndio anaamka Huku akipikicha macho yake, kutokana na usingizi aliokuwa nao.
"" Nurazy Please!! acha makasiriko hebu kaa chini kwanza niulize kwa ustaarabu tuongee kwanza tufikie mwafaka!"
"" Mwafaka upi!? Sahii saa mbili usiku unae mwanamke ndani, Mie nimekaa kwangu nikaona nimeboeka nikaona nije nipumnzike huku! Ayaaa nambie wataka kuniongopea Nini!?"
Maongezi yaliendelea Chumbani, Janerose alikuwa akiyasikia vizuri masikioni kwake Alijua moja kwa moja yeye ndio chanzo kaja kuharibu mahusiano ya watu, aliona huenda ana mkosi katika Maisha yake Kila kukicha mikosi inazidi kumuandama, aliwaza akimbie msara lakini aliona atamuacha Sharifu katika wakati mgumu ilibidi akae sebuleni akisubili mwafaka itakuwaje!?"
Muda kidogo alimuona Sharifu akitoka akiwa sambamba na Nurazy walionekana kuwa kwenye position nzuri kuashilia hakuna makasiriko tenaa!
"" Vipi waendeleaje kwasasa!? Harafu nilisahau kukutambulisha huyu Ni Mchumba wangu! Huwa anakaa Daslamu! Na ndio anafanyia kazi huko japo Nyumbani kwao Ni Huku, leo kaja kunitembelea!""
"" Ooh! Waoo Wifi! Mie naitwa Janerose, Sharifu Ni rafiki yangu pia Ni mfanyakazi mwenzangu na mie nimepita kumsalimia."
Sharifu alibaki akimtizama Janerose Huku akicheka, make kujichanganya et kapita kumsalimia usiku ule! Hili Ni wenge kweli!"
"" Nashukuru kukufahamu wifi yangu! Kwa kuwa Sharifu Ni rafiki yako Basi mie wifi yako! Ila pole kwa changamoto!!?"
Janerose aliduwaa kidogo Huku akifikilia. "" Sa Sharifu umemwambia yote hayo ya Nini!? Mbona nakuwa Kama Cinema tenaa!? Ndio kunihurumia hivo!?"
"" Janeee! Are you here!?" Sharifu Alimhoji baada ya kumuona hayupo sawa!!
"" Abee!!! Nipo sawa! Naomba niondoke nirudi Nyumbani!!?"
Nurazy alibaki akimtizama Janerose mpaka akawa na hofu.
"" Mbona Kama anajishuku usikute Ni Mwanamke Wake Sharifu!"
"" Sa' Wifi uondoke usiku huu kweli!? Kama wahofia malazi usijari! Mie nitaanza kujishuku au nimewaingilia maongezi yenu Hadi utake kuondoka?."
Sharifu Aliishia kumpiga jicho Nurazy, Linalotafsiri kitu ndani yake.
.... Itaendelea.....
Usikose sehemu ya 04.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 04" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
"" Sa' Wifi uondoke usiku huu kweli!? Kama wahofia malazi usijari! Mie nitaanza kujishuku au nimewaingilia maongezi yenu Hadi utake kuondoka?."
Sharifu Aliishia kumpiga jicho Nurazy, Linalotafsiri kitu ndani yake.
ENDELEA....
"" Aaa! So hivyoo! Kwangu usalama hautoshi!"
Sharifu aliona isiwe kesi alimtafutia usafiri Hadi kwake make hata Mchumba wake alionekana kutokufurahia uwepo wa Janerose!
Upande wa Hussein baada ya kuzunguka Sana aliamua kurudi tena kwa Janerose, ile anakaribia kufika alimuona Janerose akishushwa na pikipiki alikaa pembeni akimtizama mtu aliyemshusha Kama atakuwa anamfahamu lakini hakuiona sura yake make alikuwa amevalia koti lenye kofia, Janerose alimuaga Kisha Aliingia ndani kwake, muda huo Hussein alikuwa akimtizama tu mpaka anaingia ndani, baada ya kuhakikisha kaingia aliamua kurudi nyumbani kwake kuhofia Kama ataenda mgongea atamsumbua.
Siku iliyofuata Hussein, Jayce pamoja na Falaja walikuwa kazini lakini Janerose hakuingia Siku hiyo! Hussein aliamua kumuulizia Mkuu wake wa kazi Kama Kuna chochote kile, majibu aliyoyapata Janerose kaomba ruhusa ni mgonjwa Siku hiyo hatofika kazini!
Majira ya jioni Hussein aliamua akamuone Janerose nyumbani kwake!! Alikuta mlango uko wazi Kuna maongezi baina ya watu watatu wanaongea! Ilibidi arudi kwake atakuja wasaa mwingine.
Ndani kwa Janerose alikuwa ni Nurazy pamoja na Sharifu walimtembelea ili kumjenga vizuri ki saikolojia! Sitori za hapa na pale ziliendelea mwisho kabisa waliaga wakaondoka! Baada ya kuondoka Janerose alishika simu yake na kukuta ujumbe toka kwa Hussein.
"" Vipi naweza kukuona!!?"
Alitaka kuijibu ile message lakini aliishia kuandika na kufuta Huku akikumbuka matukio ya jana'ke, kuwa Hussein alikuwa akifungua shampeni kwa ustadi mkubwa mbele ya adui yake!
Wakati bado anafikilia Hussein aliamua kumpigia kabisa, lakini Janerose hakupokea! Alivyoona hapokei alimwachia ujumbe wa message.
"" Please Janerose! Pokea simu zangu huenda unafikilia Mimi Ni mtu mbaya kwako Mimi nilialikwa tu, hata hivyo Sikujua Kama yule ndie Shamsi mchumba wako! Nakuomba tenaa pokea simu yangu tafadhari!''
Janerose alitizama ule ujumbe tenaa! Ndio akaamua kumpigia simu Hussein, simu iliita mpaka ikakata muda huo Hussein aliweka simu chaji akatoka.
++++++
Nchini Kenya alionekana kijana mmoja amekaa sebuleni Akiwa amefungwa kitambaa cheupe machoni, Huku mkononi alikuwa ameshikilia fimbo ya kumuongoza njia akijaribu kuigonga gonga Ishara ya kutaka msaada Kama Kuna mtu karibu.
Kuna Binti mmoja alifika pale akawa amekaa Huku akizidi kumtizama jinsi anavyohangaika kutafuta msaada ilibidi amuongeleshe.
"" Ka Denison!! Ni Mimi Merry! Wamtaka ka Khamisi!?"
"'' Niletee maji ninywe kwanzaa!! Kwani yeye Kaenda wapi!?"
"" Kamfata Doctor! Aje akuangalie macho yako kwanza."
Muda kidogo Khamisi Aliingia akiwa na Doctor!
"" Doctor! Mgonjwa wetu ndio huyu naona kwasasa yupo vizuri anaweza kutembea! Angalau Kama nusu saa! Kuliko kipindi kile analetwa Hapa!"
"" Leo itakuwa Ni Mara mwisho kumfanyia surgery ya macho! Tunamuomba Mungu angalau tufanikiwe kwa leo make haturuhusiwi tenaa kurudia surgery labda baada ya mwaka mmoja!!"
Doctor aliwaomba wampishe kidogo alimchukua Mgonjwa wake nakumuingiza kwenye chumba Cha matibabu! Alifanya kumfungua zile bandage Kisha alimwamuru afungue machoo!
Denison alijitahidi kufungua macho, lakini macho yake yalibakia kuona ukungu na muda wote yalikuwa yakimuuma Sana alianza kuyapikicha lakini Doctor alimzuia. Alitoka Nje kumuita Khamisi na Merry.
Waliingia kwa haraka Huku Kila mtu aliwahi kumtizama Denison Kama kweli anaona! Merry aliwahi akachukua bomba la sindano lilokuwa pale Kisha alisogeza karibu na macho ya Denison alimuuliza;-
"" Kaka! hii Ni Nini!?"
Doctor alibaki akicheka, aliona Ni jinsi gani wanatamani ndugu Yao aone!
"" Hampaswi kumsumbua hivyo! Kadili Siku zitakavyozidi kusogea na ndivyo atazidi kuona! Kwasasa anaona ukungu tu! Ila tumefanikiwa zoezi letu!"
Denison alikuwa akisikiliza majibu ya Doctor, hata yeye pia alitamani Sana aone! Khamisi alimchukua Denison nakumtoa nje Angalau azoee mwanga wa Nje! Denison alikuwa akijitahidi Sana kutizama mwanga lakini ulizidi kumuumiza aliamua kurudi ndani!
Sitori zilizidi kuendelea Kati yake na Khamisi Huku Merry yeye alikuwa akiandaa chochote kitu.
"" Vipi ulisema ukipona warudi Tanzania ulikokuwa wafanyia kazi!? Waweza niambia NI kipi Cha muhimu Sana mpaka urudi tenaa!?"
"" Daaah!! Ninae rafiki yangu sikumuaga vizuri pindi nahamishwa! Harafu nilitaka nimjulishe kitu kilichonisibu nikashidwa kumtafuta! Nikishamuaga tu basiii, ndio sitakuja kumuona tenaa make nategemea nikipona narudi shule tenaa! Ila nataka nimpatie taarifa hizi.'"
"" Daaah! Nawewe wapenda kuchezea pesa! Kwani Ni muhimu Sana!! Ayaaa huyo rafiki yako Ni Nani vile! Make tangu upate ajari imekuwa Ni rafiki yangu rafiki yangu! Atakuwa wa kike ee!!?"
Denison aliishia kutabasamu tu, Ni kweli alimkumbuka Sana Janerose na muda wote alikuwa akimuwaza.
"" Ni rafiki yangu niliemzoea kwa muda mchache Sana! Lakini hata sikufaidi uwepo Wake kwangu! Ila natamani nimuone tu! Huyu rafiki.
'" Sawa nishajua! Rafiki! Rafiki nahisi Ni wa kike harafu unavyokuwa ukimtaja Mara kwa Mara inaonekana uliwahi kuvutiwa nae Sana!!"
"" Basi naomba unisindikize Tanzania! Ukamuone huyo rafiki yangu! Harafu ndio nije nijiandae niende shule.'"
+++++
Huku Kwa Janerose baada ya kukaa muda mwingi bila amani aliomba uhamisho ahamishiwe sehemu nyingine huenda itamsaidia kupunguza Maumivu! Barua yake ilikubaliwa kutokana na yeye kuhitaji kuhama kwa uharaka alipewa sharti la kujihamisha mwenyewe pasina sapoti yoyote ya pesa! Ilibidi akubaliane na Gharama yoyote! Hata hivyo na Hussein aliamua kumuongezea pesa kidogo katika maandalizi yake ya kuhama.
Leo ndio ilikuwa Ni Siku ya kuhama! Alichukua gari(fuso) ilipakia vitu vyake vyote! Wafanyakazi wenzake walifika kumuaga akiwemo na Jayce! Wakati anamaliza kuwaaga ghafra mtoto wa Jayce (Patricia) Aliingia Huku akimkimbilia Janerose! Ilibidi amnyanyue juu Huku akizidi kumtizama! Alimkiss shavuni Huku akimuaga anaenda kumletea Chocolate! Mtoto alionekana kufanana na Jayce Sana lakini baadhi ya vitu alifanana na Shamsi Kama Macho, midomo na masikio vilimfanana kweli Shamsi.
Janerose aliangaza Huku na kule akimtafuta Hussein, alichungulia kwenye Gari ndipo anamuona Hussein kajinamia kwenye usukani ilibidi aingie kwenye gari Kisha alifunga vioo Tinted Huku akibaki kumtizama Hussein! Alivyo na Huzuni na yeye alishidwa kuvumilia machozi yalianza kutililika Huku kilio kikifatia.
Hussein aliamua kuwasha Gari Huku wakitoka eneo hilo, make wafanyakazi wenzake wote walikuwa wakiwaangalia! Na wao walikuwa na Huzuni Sana Kila wakikumbuka uwepo wa Janerose jinsi alivyokuwa akijituma kufanya kazi kwa bidii hata ule ucheshi wake hii iliwauma zaidi.
Mganga mkuu alikaa Ofsini kwake Huku akijilaumu kwanini kakubali kutoa kibali Janerose ahamishiwe, Mganga msaidizi Aliingia akiwa na Matron na Patron! Wakihitaji kulijadili swala hilo.
"" Maskini Binti wa watu mchapa kazi! Kashidwa kuvumilia maumivu Kila muda akimtizama Mtoto wa Jayce! Muda wote imekuwa Ni kulia tu! Ila nyie wanaume nyie mtakuja kuua watu!
Patron aliongea Huku akikaa mkao wakusikiliza kikao!
.... Itaendelea.......
Usikose sehemu ya 05.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 05" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
"" Maskini Binti wa watu mchapa kazi! Kashidwa kuvumilia maumivu Kila muda akimtizama Mtoto wa Jayce! Muda wote imekuwa Ni kulia tu! Ila nyie wanaume nyie mtakuja kuua watu!
Patron aliongea Huku akikaa mkao wakusikiliza kikao!
ENDELEA.......
Baada ya kikao kumalizika Huku upande wa Janerose alikuwa njiani akiondoka Huku Hussein akimpatia kampani.
Wakati wapo njiani Kuna gari ilipaki mbele Yao nakuziba njia! Hussein ilibidi afunge break kwanza Ili amgoje mtu aliesimama mbele Yao, hakuwa mwingine Bali Ni Shamsi alishuka kwenye Gari Huku akielekea kwenye Gari Yao.
Janerose alibaki ameduwaa akimtizama Shamsi! MOYO wake uliraluka muda wote hasa pale anapomuona Shamsi huwa anakosa ujasiri. Shamsi alimsogelea karibu kabisa na kioo Kisha Alimpatia Ishara ashushe kioo, Hussein alibaki ameganda tu Huku mikono yake bado kashikilia usukani akitizama aone kipi kinaenda kufanyika.
"" Janee! Ndio umeamua kujitenga mbali na Mimi!! Naona vile unavyoniona Mimi Ni mkosefu kwako lakini sio hivyo!!?"
Janerose alibaki akimtizama Shamsi Huku kifua chake kikizidi kufura hasira! Alifungua kinywa chake azungumze lakini Hussein aliwahi akaziba mkono Huku akimpa Ishara akae kimya.
Shamsi ilibidi amgeukie Hussein ili ajue Ni Nani anaingilia penzi lake, akisema kitu na Janerose asiongee.
"" Wewe ndie Hussein!? Upo kwaajili ya watu walioumizwa kuwapa furaha! Je! Ushawahi kujiuliza Why kaumizwa bila sababu, Anyway una ukaribu mzuri Sana na Janerose! Vipi kuhusu Denison na Mimi huwa unatuchukuliaje kwa Janerose!?"
"" Shamsi!! Inatoshaa sipo radhi nimuone Janerose anaumia mbele yangu! Hata Kama mlitofautiana hukupaswa kumchukua rafiki yake mpaka uzae nae! Unajua Janerose anajisikiaje Kila akimuona Jayce? Kwaajili yako leo kashidwa kuvumilia maumivu anahama kikazi!"
"" Okay! Vizuri Wewe ndie wamjua vizuri Janerose! Wewe hujaona alinisaliti akatoka na Denison tena mfanyakazi mwenzake isipokuwa vituo vya kazi tu ndio wanaachana na mie nimemchukua mfanyakazi mwenzake ka Ni vizuri!"
"" Hapana Shamsi!! Unaongopa!! Mimi sikutaka kuwa na Denison Ila Wewe ndio chanzo!! Ulikuwa na Mimi ukaendelea kuwa na mwanamke wako wa zamani wakati uliniahidi mmeachana, bado ukaendelea kuwa na wanawake wengine, isitoshe hata mdogo wangu ukamtongoza bado Dadangu mtoto wa mamkubwa nae ukataka upite nae! Mimi Ni mtu gani nikavumilia upuuzi huu!? Ndio ninae Denison na ninampenda Sana japo nmempoteza Ila Moyoni anaishi.
Janerose aliongea kwa paniki mpaka alitoa Siri ambazo hakuwahi kumwambia Hussein, Hussein alichukia Sana alistua gari ili waondoke lakini gari ya Shamsi ilikuwa imepaki mbele yake hii ikamfanya ashidwe ku overtake.
Shamsi Alijua kweli kumhadaa Janerose alinyanyua mkono wake Kisha alimshika shavuni Huku akiongea nae taratibu.
"" Najua una hasira na Mimi, Ila hukupaswa ukae mbali na Mimi! Mimi na Wewe huwa twapendana Siku zote hata ungekimbia mbali na Mimi Ila hisia zako zote zi ndani yangu na hizi Ni hasira tu mpaka tumefikia huku! Ila Mimi bado nakuhitaji Sanaa katika Maisha yangu!"
Wakati akiongea hayo yote Jayce alikuwa kafika Huku akiangalia parangano linavyopelekwa, mwanzoni alikuwa akichekelea Ila maneno ya mwisho yalimuumiza sana, Aliishia kuita...
"" Hapana Ba Patricia!! Unampendaje Janee, wakati unae mtoto na mie?" Janerose anae mtu wake kwasasa wewe muache aende Ni mwanamke gani Kama anampenda mmewe hata akamkimbia!?"
Maneno ya Jayce yalizidi kumuongezea hasira Janerose! Alimsisitiza Hussein waondoke.
Shamsi alibaki akimtizama Hussein Huku akimind kweli, alimshika mkono Jayce Kisha akampelekea kwenye Gari yake ili waondoke, waliondoa gari wakawa wameondoka lakini kwa pembeni kidogo alionekana Resious akiwa anakuja anakimbia kuelekea Walipo.
Janerose Alimuonea Resious kwa saint miror, alimwambia Hussein asiondoe gari kwanza amsikilize Resious.
Hussein nae alimuona Resious akiwa anakuja ilibaki aking'ata midomo yake Huku akiongea kimya kimya.
"" Kwanini nakuwa na kigugumizi kumwambia ukweli Janerose kuhusu Resious! Daaah! Hapa nafanyaje Sasa!?"
Janerose Aligundua hilo huenda Kuna kitu Kati ya Resious na Hussein make hata Siku Ile mawasiliano Yao yalikuwa na kitu ndani yake ilibidi amulahisishie kazi.
"' Mchukue pia Resious tuondoke nae! Siku ukiwa warudi upate mtu wakusema nae njiani."
Hussein hakuwa na jibu, Alimtizama Resious Kisha alimpa Ishara apande, japo alibaki akimtizama tu.
"" Sasa mbona hupandi!? Au hutaki tuongozane!?
"" Nataka hapooo!!"
"" Mhuuu mbele!!?"
"" Ndioo!!"
Janerose alibaki kuwatizama Huku akicheka tu.
"" Ani huyu Hussein! Ni wanapendana kumbe Ila hataki kuweka wazi! Ona mtoto kapanda zake na sitori zimeanza kukolea."
Hussein aliendelea kuendesha Gari Alimtizama Janerose kwenye kioo aliona kasinzia, ilibidi amgeukie Resious make muda huo alikuwa akicheka cheka ovyo.
"" Wewe vipi mbona umenifuata tenaa!? Afu nilikwambia nampeleka Janee harafu nawahi kurudi, unavunga Kama hukuona ujumbe wangu we mwanamke!?"
"" Weee!! Kila mtu akae na mtu wake karibu, make Siku hizi ikishakuwa Love Distance! Ndo matokeo yake yakuwapata kina Jayce tenaa! Ila Shamsi sio mwaminifu kweli!?"
"" Mhuu sio mwaminifu... Hata Wewe kakutongoza amaa!?"
Resious ilibidi acheke kwanza.
"" Kumbe unae wivu ee! Hata Mimi nahisi umemtongoza Janerose, Why wamganda hivyoo!?"
Hussein ilibidi ageuke nyuma kumtizama kwanza Janerose Kama anawasikia Kisha alifanya kumsina Resious mkononi.
"" Hata Wewe nae muuaji tu! Kwanini ulikuwa wajichezesha ovyo ovyo kwenye Birthday ya Patricia!? Au kwakuwa ulimuona yule mkaka aliyekuwa na Janerose karibu!!?"
"" Ooh! Wamuongelea Sharifu ee!? Yule si rafiki yake na mtu wake Janerose!? Hafu walionekana kumechi hivi!!?"
'" Mhuuu! Wewe mwanamke! Mkaka aliyekuwa na Janerose na yeye wamjua mbona Kama mbea Wewe!!?"
"" Aaah! Ushaanza kuniita majina yako ya ajabu! Si nimesema tu lakini!?"
"" Mhuuu! Harafu sitaki hao rafiki zako uwe nao karibu, Sio Jayce Wala Falaja! Kama umekosa rafiki nifanye Mimi niwe rafiki yako zaidi Yao!"
"" Eee! Masharti yako hayo! Wao si wao" na mie si Mimi! Mimi hata Sina habari nao kwenye Mambo Yao!"
"" Nawewe si huwa hunyamazi!? Haya hapo kazini kwako naona Kuna wadada wenye sifa nzuri tu! Ile Siku ulikuja nao kwangu ukawatambulisha mbona wanaonekana Ni wazuri tu!"
"" Ooh! Yaani wamzungumzia Mariam na Agape!? Itakuwa na Wewe wawamendea!!"
Huku kwa Janerose ndio anaamka usingizini Huku akiota Ndoto Kama vile anakimbizwa aliita..
"" Shamsiiii.....!!!"
........ Itaendelea...........
Usikose sehemu ya 06.
Usisahau kulike na kukoment hapo chini! Kwa wale ambao bado hamja join kwenye Group langu hakikisha unajiunga Kwa hii link chini Make inaweza tokea tatizo nikaacha kuonekana kwenye Group Kama hajajiunga ndio utakuwa umenipoteza hivyoo.
https://facebook.com/groups/263417295228138/
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 06" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Huku kwa Janerose ndio anaamka usingizini Huku akiota Ndoto Kama vile anakimbizwa aliita..
"" Shamsiiii.....!!!"
ENDELEA.....
Hussein pamoja na Resious walishituka nakubaki wakimtizama Janerose.
"" Vipi umeamka!!?"
Janerose aliendelea kuuchapa usingizi kumbe ile ilikuwa Ni Ndoto!
Majira ya Jioni waliingia Mkoani Arusha! Walifikia hadi sehemu alipokuwa amechukua chumba walisaidiana kwa pamoja kushusha mizigo Huku wakipangilia sehemu husika. Siku iliyofuata Hussein pamoja na Resious walirudi nyumbani.
Baada ya Mwezi mmoja kupita Janerose alikuwa tayari kashazoea mazingira ya kazini kwake! Alianza kusahau kumbukumbu za Shamsi Huku akiendelea kuwasiliana na Hussein Kama rafiki yake wa karibu!
Kuna Siku alipokea simu kutoka kwa Sharifu alimpigia Huku akiongea nae!
"" Vipi habari za huko!? Mbona uliondoka kimya kimya? harafu Nina mapya kwako! Rafiki yako anakuja bhanaa!""
"" Rafiki yangu Nani!? Hussein si kanisusa kweli at anadai kuja Huku mpaka namie nije huko ila kwasasa mi kuja huko Ni mapema mnoo!"
"" Aaah! Achana na Hussein Kuna rafiki yako yule mwingine!!'"
Kabla hajamuuliza vizuri Kuna mfanyakazi mwenzake alifika, ilibidi akate simu kwanza ili amsikilize.
"" Doctor Janerose! Matron anakuita ofsini kwake!"
"" Doctor! Umeniita!?"
"" Nataka uongozane na wenzako kesho Asubuhi mpeleke chanjo ya pepopunda kwa watoto kijijini! Make Hawa wengine Ni wanafunzi bado, ni vizuri kuongozana nao Ili uwapatie mafunzo zaidi"
"" Sawa Doctor! Ngoja nianze kuandaa mapema!!"
Baada ya kumaliza kuandaa vizuri, Alirudi nyumbani kwake, alichukua simu ili amtafute Sharifu lakini hakupatikana kwenye simu aliamua kujipumnzisha.
Kesho yake Asubuhi waliamkia safarini kupeleka chanjo, walifika kule lakini mtandao ulikuwa Ni washida sana mpaka kutafuta sehemu yenye mwiinuko na hii ilimfanya Janerose kutowasiliana na rafiki yake pamoja na ndugu zake wa karibu, zoezi hili lilichukua Siku kadhaa kusambaza chanjo kutokana na vijiji kuwa mbali mbali.
Huku Jijjini Mwanza Denison pamoja na rafiki yake Khasani waliingia Mwanza Kama walivyokubaliana walimtafuta Sharifu akaja kuwapokea! Siku hiyo ilikuwa Ni furaha Sana kwao kuonana. Walipiga sitori mbalimbali lakini Sharifu muda wote alikuwa akimtizama Denison make Kama alikuwa akihangaika kutizama hasa pale anapoona kitu Cha mwanga ilibidi amhoji.
"" Vipi jamaa angu Siku hizi umekuwaje au upepo wa Huku unakuchanganya Sana make Kama wahangaika kutizama vile!"
"" Daaah! Ni sitori ndefu ujue! Harafu hukanitambulisha Tuliemkuta hapa ndie shemeji!?"
"" Shemeji yenu ndio, Sema alipigiwa simu Nyumbani kwao! Nikawa nimeshidwa kumtambulisha kwenu!"
'" Ooh! Mrembo kweli! Naona umechagua UA!! Muda wote litachanua! Hata jina husemii!?"
"" Aaa! Wewe nae bado unao utani wako tu! Anaitwa Nurazy ila hata rafiki yako na yeye ukimuona wanafanana miili Kama shemeji yako!"
"" Yupo wapi kwani? Au amepuuzia uwepo wangu!?"
"" Mhuu! Ila samahani kwanza! Janerose nilijaribu kumdokeza kuhusu ujio wako harafu muda huo nlikuwa sijamaliza kumpa taarifa kamili nikasikia kaitwa ilibidi akate simu atanitafuta baadae! Lakini nimekuja kumtafuta leo asubuhi hakupatikana tenaa!?"
"" Sasa si umfuate! Au kahamia mtaa wa pili!?"
"" Bora hata mtaa wa pili! Janerose alihama kituo Cha kazi kwasasa yupo Arusha ndiko anafanyia kazi!"
''" Masihara mengi ujue!! Nimekuja kwaajili yake Et!!?"
Sharifu baaada ya kumuona Denison yupo sereous ilibidi amweleze Kila kitu kilichomfanya mpaka akahame! Baada ya kumaliza kuongea alimpigia simu Hussein angalau waje waongee! Hata hivyo Hussein alikuwa akimfahamu vizuri Denison.
Kitendo Cha kusikia changamoto alizozipata Janerose zilimuuma Sana lakini pia zilimvunja Moyo, muda wote Alijua Janerose atakuwa amemsubili hii ya kusikia alirudiana na Shamsi ndio ilimralua Moyo! Alitamani aondoke hiyo hiyo Siku lakini ilikuwa Ni ngumu.
"'' Vipi mbona Umebadilika ghafra! Kuna sehemu umekwazika!? Hussein Alihoji Baada ya kugundua hilo.
'" Hapana! Sema nimekumbuka mbali Sana! Kipindi nafanyia kazi hapa kulikuwa bado hakujachangamka ila sahiii ni amsha amsha!?"
Hussein Alimtizama mpaka akatikisa kichwa! Ilibidi amuulizie kuhusu Macho.
"" Vipi Siku hizi waumwa macho nimeona una miwani ya Lenzi kwenye mfuko wako!?"
"" Daaah! Naona mmeniandama leo kwa hili swali!? Okay kwanza niseme Namshukuru Mungu tu kwakuwa ninaishi! Kwa Mara ya mwisho niliondoka hapa kuelekea masomoni ndio nilivyowaaga! Siku hiyo nilichukua usafiri kuelekea Airport lakini kabla hata sijavuka mkoa tulipata ajari mbaya nikawa nimeumia vibaya kwani Nyonga zangu pamoja na mguu sehemu ya kiungio mifupa iliweza kuvunjika! Wakati naanguka nilienda kupigiza kichwa chini kikapelekea kuzima nilikuja kuamka nipo hospital ya Kenya nahisi Ni Kama Siku tano kupita ndio nilianza kujitambua.
Siku niliyokuja kuamka niliona kiza, miguu yangu mikono yangu haikuweza kumove sehemu yoyote mbaya zaidi hata macho yangu hayakuweza kuona! Nilimuita mtu aliyekuwa karibu yangu nikasikia sauti ya huyu rafiki yangu niliyeambatana nae hapa akiniongelesha neno la kwanza baada ya kuniona tu alisema " Mungu Mkubwa" maneno haya nilianza kuyatafakari Sana Huku nikivuta taswira ilivyokuwa ndio nikakumbuka nilipata ajari muda huo nilimuuliza; "" Kwahiyo Mimi Ni kipofu na sitaweza tena kutumia mikono yangu Wala miguu yangu kutembea!!?"
Hutaamini Khamisi Alinijibu kwakuwa naweza kuongea tu, Kila kitu kitakaa sawa kikubwa walikuwa wakiangalia akili yangu Kama nitaamka itakuwaje!? Niliendelea kufanyiwa matibabu pale Kila Siku zilivyozidi kwenda nilianza kufanyishwa mazoezi ya viungo mwishowe kabisa nikawa nasukumwa kwenye Wheelchair na muda huo ujue nilikuwa sioni! Nilikaa miezi Kama Sita ndio Siku hiyo nilimsikia Baba yangu mdogo alikuja kuniona! Kumbe wakati napata ajari Babangu alikuwa nje za nchi hakuweza kupata mawasiliano na hii Ni baada ya kurudi ndio akapata taarifa japo yeye muda huo Alijua nipo masomoni.
Babangu Mdogo alinisimamia Sana mpaka Mimi nikawa katika khari hii! Pia Nashukuru uongozi wa wakufunzi wa chuo( Kenya) baada ya kusikia nimepata ajali wasamalia wema waliona anwani yangu yakuja Kenya ndio wakatoa taarifa na wao ndio wakafanya utaratibu wa Mimi kufika kwao nakuanza kunifanyia huduma na hii Ni baada ya kumkosa Babangu hewani.
Wakati nikiendelea kupata huduma sikupewa ruhusa ya kutumia simu yeyote! Ndio maana hata nyie jamaa zangu wa karibu nilishidwa kuwajulisheni! Harafu spesho kabisa alikuwa Ni Janerose maake alikuwa Ni rafiki yangu mzuri pindi nipo nafanya kazi zangu, Nilijua atakuwa amenitafuta Sana lakini nilivyofikili kumbe sivyo! Mie nilifunga safari yangu angalau nimshukuru kwa muda aliokuwa na Mimi pia nilitaka nimuage kwasasa ndio nirudi rasmi masomoni hivyo hataniona kwa uharaka vile ila mpaka nitakapomaliza miaka mitano ndio nitamuona! Kwakuwa na yeye alihama Basi mkimpata mfikisheni taarifa zangu na mmwambie chanzo kilichofanya nishidwe kumtafuta na hiki ndio kitu nlikuja kumtaarifu tu basiii!"
Denison alimaliza kuongea Kisha aliinamisha kichwa chake chini, aliwaachia nafasi watu waliokuwa pale waanze kutafakari neno moja moja la Denison!
Hussein yeye alibaki na maumivu Sana Kila akimkumbuka Shamsi alivyomfanyia Janerose ndio maana yote yanatokea, Alimtizama Resious muda huo nae alikuwa amejiinamia akifikilia kivyake, Pia upande wa Sharifu alikuwa katulia na yeye akisononeka, pembeni alikuwepo Nurazy alifika mida Denison akiendelea kuelezea, na yeye pia aliamua kuegama miguuni kwa mmewe mtarajiwa akisononeka.
.... Itaendelea.....
Usikose sehemu ya 07.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 07" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Hussein yeye alibaki na maumivu Sana Kila akimkumbuka Shamsi alivyomfanyia Janerose ndio maana yote yanatokea, Alimtizama Resious muda huo nae alikuwa amejiinamia akifikilia kivyake, Pia upande wa Sharifu alikuwa katulia na yeye akisononeka, pembeni alikuwepo Nurazy alifika mida Denison akiendelea kuelezea, na yeye pia aliamua kuegama miguuni kwa mmewe mtarajiwa akisononeka.
ENDELEA.....
Ilikuwa Ni Siku iliyofuata Denison aliondoka na Khamis kuelekea kwao! Siku hiyo hiyo Janerose na yeye alikuwa njiani akirudi kazini kwake! baada ya kufika aliacha utaratibu kwa mkuu wake Huku akimwelezea kazi yake alivyoweza kuisimamia.
Baada ya kukamilisha Kila kitu alirudi nyumbani kwake! Aliamua kuwasha simu yake ili awasiliane na rafiki yake Hussein make alimumisi kweli, ile anafungua alikutana na sms nyingi zikiingia kwa kufuatana aliamua kusoma sms kutoka kwa Hussein akilalamika kweli.
''' Kweli leo umeniboa mno! Hata Kama upo busy unashidwa hata kutuma ujumbe nikajua sababu! Siku zote napenda uwe na furaha lakini Wewe ndio hutaki kuiona furaha yako! Umepigiwa simu na Sharifu kakupa taarifa mapema rafiki yako kaja lakini umeishia kumkatia simu! Hivi unajua jinsi alivyojisikia alipokukosa!?"
Janerose alimalizia kusoma ujumbe wa Hussein Kisha alifungua ujumbe wa Sharifu.
"" Kwanini hukunitafuta tenaa baada ya kukata simu!? Rafiki yako Denison kesho yupo Mkoani kwetu! Naomba tuwasiliane ukimaliza kazi zako!"
""Khaaa! Denison kaja Mwanza!!?
Alichukua simu yake ili apige lakini hakuwa na salio, ilibidi amtumie ujumbe Hussein ampigie. Hussein baada ya kuona sms ya Janerose aliamua kuipuuzia alichukua simu nakuamua kuizima kwa muda, wakati anaizima Resious alikuwa pembeni akimtizama tu.
"" Kwanini unazima simu tenaa!? Ni rafiki yako atakuwa ee!?"
"" Aaa Janee! Sijui Ni utoto! Aya mkaka wa watu katoka mbali kaja kwaajili yake Hafu mtu hapokei simu, akaona haitoshi aliamua kuzima kabisa sahii anataka nmpigie tuongee Nini Sasa!!?"
'" Nawewee hebu acha roho mbaya hivyo! Msikilize kwanza ndio ujue shida iko wapi!?"
Hussein aliishia kumkata jicho Huku akiuma midomo yake kwa hasira! Kimya kilipita Kama dakika kumi alishangaa kusikia sauti ya mtu akilia ilibidi amchungulie vizuri Ni analia kweli au anaekit, Ni kweli Reseous alikuwa akilia ilibidi amsogelee karibu Kisha alinyanyua mkono wake nakumshika kichwani.
"" Nambie my! Kipi hasa kinakuliza au Mimi kukataa kupokea simu ya Janerose ndio ulie!?"
Reseous ndio alizidi kulia, Mpaka Hussein akachanganyikiwa alimuinua kwa mikono yake Kisha akamuegemeza miguuni kwake Huku akizidi kuchezea Nywele zake.
"" Basii samahani!! Ngoja nimpigie Janerose nijue kipi kimemsibu hata Mimi naumia kweli pale ninapomkosa hewani! Sijui ilikuwaje tu aniii!!?"
"" Nilijua tu lazima uumie kuhusu rafiki yako ningeshangaa et Wewe ndio wakumzimia simu Janee kisa ulimpigia hakupokea, najua unaempenda rafiki yako kuliko hata Mimi, na muda wote umekuwa ukinitenga kisa Janerose!!'
Reseous aliongea Huku akizidi kulia, Hussein alibaki akishusha pumnzi na kuivuta Kisha alishika mkono mmoja kichwani Huku akizidi kumtizama Reseous alibaki akijisemea;
"" Daah hapa nimekwisha! Muda wote kamejaa wivu! Ani wanawake bhana hata sioni sababu kinachomliza muda wote! Ndo maana Mimi mahusiano huwa siingii kwa pupa! Anyway liwalo na liwe!"
Aliamua kumbemba Reseous Kisha alimpeleka chumbani, Alirudi tenaa sebuleni alitizama simu yake nakukuta missed call tatu za Janerose aliamua kumpigia.
Janerose alipokea simu Huku akiwa anazunguka zunguka ndani misri kapoteza kitu Huku akiongea.
"" Aaa Hussein!! Jamaniiii Denison Upo nae hapo!?"
"" Ameshaondoka Siku nyingi! Mbona hukuwa wapokea simu yangu!?"
"" Kaenda kwa Sharifu ee!? Nampigia Sharifu hapokei simu yangu sijui wamelala!? Au nitumie namba yake moja kwa moja nimpigie mimi! Naona kanimisi kweli!"
"" Harafu Janee! Hebu punguza mihemko hiyoo! Naona unaongea ongea tu pasina kunisikiliza Mimi! Sasa Ni hivi; Denison alikuja Huku akiwa ameambatana na rafiki yake! Kuja kwake Huku alikuja kutuaga pia alikuja kutupatia taarifa za yeye kutokupatikana hewani! Kwakifupi Siku anatoka Tanzania anaelekea masomoni alipata ajari mbaya iliyopelekea baadhi ya viungo vyake vya mwili vishidwe kufanya kazi! Mbaya zaidi hata macho yake yalijawa upovu wa muda mwingi, na hicho kilipelekea kushidwa kutumia simu tukampata hewani, japo alifanyia matibabu kwasasa yupo vizuri ila hajawa sawa kivile macho bado yanamsumbua Mpaka atumie miwani.
"" Kilichomleta Huku Ni kuwasalimia ndugu na jamaa! Nakutuaga upya kuwa hatarejea tena Huku Hadi miaka mitano ipite! Ila Wewe ndio ulikuwa spesho Sana! Alikuulizia Sana Hadi taarifa zako Mpaka akajua chanzo Cha kuhama Ni kuhusu Shamsi kuzaa na Jayce! Kilichomuuma zaidi nikusikia Wewe ulirudiana na Shamsi! Hiki ndio kilimkatisha tamaa hata tulipojitahidi kukutafuta alisema tukufikishie Salamu tu! Kwa kifupi Denison keshaondoka Tanzania tayari.
Janerose aliyasikia vizuri maneno Huku yakipenya masikioni kwake barabara! Alishusha simu yake chini toka sikioni Kisha alikata simu Huku akibaki amepiga magoti kwa Huzuni Huku akijaribu kuufariji moyo Wake taratibu.
"" Nilijua tu haya yote yangetokea tu! Mara ya kwanza alikuja kwangu akanifanya niwe na furaha tele! Kwa Mara ya pili aliondoka Ghafra pasina kuniaga akaniaga kwa simu Huku akiniahidi atarudi harafu nimgoje lakini hakuwahi hata kupatikana kwa simu yake, kwa Mara ya tatu kwasasa alikuja kwangu Kama alivyoondoka tu, team hii karudi kinyume chake kaja na taarifa zote kuhusu kutopatikana kwenye simu, matatizo yaliyomkuta yote alitaka kunielezea lakini hakunikuta tenaa! Hata Mimi najua haya yote ungenihadithia mbele yangu ningeumia Sana hasa pale ungemalizia lile neno la mwisho sitakuona tena labda miaka mitano ipite umalize masomo yako ndio nikuone hapo nisingevumilia kulipokea mbele yako!"
"" Natamani nikupigie simu huko uliko nikwambie kwanini sikupokea simu yako ila nitakuwa Ni mtu wakujieleza Sana wakati Wewe tayari umeshaondoka na majibu tofauti na yangu! Sina zaidi yakusema ili niufurahishe moyo wako ila Nahisi Wewe nilikupenda zaidi na zaidi! Na Kama Ni mpango wa Mungu tutaja onana tenaa!"
Janerose alimaliza kuongea maneno Huku moyo wake unae maumivu, Aliingia chumbani kwake Kisha alivuta Droo iliyokuwa kabatini, Kuna picha alipatiwa Siku ile na Sharifu hotelini alizichukua na kubaki akizitizama Kisha alianza kusema nazo kwa kuziongelesha na kucheka.
"" Hivi Denison kwanini alikuwa akikuchora Wewe!( Mimi) ndio alimaanisha u moyoni mwake au Ni vile aliwaza Kuna siku atakuja kukuacha ubaki na hizi picha! Harafu kwanini ulimchora huyu Shamsi kwenye picha ya pamoja na Wewe!? Hukupaswa kabisa umuweke pembeni yako na ndie huyu huyu kanifanya Mimi niwe mbali na Wewe muda wote!"
Muda kidogo simu yake iliita, aliangalia mtu aliyepiga alikutana na namba ngeni alipokea na kuisikilizia sikioni baadae ilikatwa lakini Kuna sms iliingia.
''" Bado una hasira na Mimi Maama!? Naomba Basi tuyamalize! Kweli nimekumisi Sana, Ni wakati wetu wa kutimiza ndoto zetu kwani wazazi wangu wanakungoja wewe wakuone mkwe wao!"
....Itaendelea......
Usikose sehemu ya 08.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 08" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Muda kidogo simu yake iliita, aliangalia mtu aliyepiga alikutana na namba ngeni alipokea na kuisikilizia sikioni baadae ilikatwa lakini Kuna sms iliingia.
''" Bado una hasira na Mimi Maama!? Naomba Basi tuyamalize! Kweli nimekumisi Sana, Ni wakati wetu wa kutimiza ndoto zetu kwani wazazi wangu wanakungoja wewe wakuone mkwe wao!"
ENDELEA....
Janerose alirudia Mara mbili kusoma message Kisha alikaa chini akimfikilia Shamsi tangu waanzishe mahusiano Yao mpaka kufikia pale, alionesha Bado anampenda lakini kwa vituko anavyomfanyia ndivyo vilipunguza upendo aliamua kufuta ujumbe Kisha aliibrock ile namba!
Ni miezi kazaaa ilipita leo katika hospital aliyokuwa akifanyia Janerose Kuna ugeni ulifika pale ilikuwa Ni kampuni linalojihusisha na utoaji wa misaada kwa watoto wadogo wanaosumbuliwa na saratani pamoja na Manjano, kampuni hii ilimilikiwa na Wazungu!!
Kwa Janerose alipewa kitengo Cha mapokezi Ni pamoja na kupokea dawa make kwenye lugha ya kingeleza alikuwa akifuzu vizuri hata kuongea na wazungu kwakee haikuwa changamoto! Japo hata hao Wazungu walikuwa wakiongea kingeleza.
Walifanya taratibu zote baada ya kukamilisha zoezi hilo ilikuwa Ni mapumnziko walikaa sehemu ili kupata lunch time. Stori mbalimbali ziliendelea Kuna kijana Aliingia hotelin Kisha alikaa karibu na mzungu mmoja wakiongea nae baada ya maongezi Alimtizama Janerose Kisha akatabasamu, Huku akiinuka ili aondoke.
Janerose nae alianza kujisitukia make Mzungu muda wote alikuwa akimtizama, na yeye alikuwa akimtizama chini chini mwisho walikutanisha macho ikabidi wote wacheke tu! Mzungu ilibidi amuongeleshe.
"" You smile good!! Hafu unafanya kazi kwa moyo wako wote! Hongera kwa Hilo!!"
"" Thanks Doctor!!"
Muda wa Lunch uliisha walitawanyika wote! Janerose alikuwa akipanga vitabu vyake kisha aliweka kwenye begi lake la mgongoni Ili aondoke! Wakati anaondoka pale Kuna sauti aliisikia ikitaja jina lake ikitokea kwenye gari ilibidi atizame, baada ya kutizama Kuna mtu alimuita kwa Ishara ikabidi amfuate, alikuwa Ni yule Doctor aliyetoka kuongea na Mzungu pindi wanakula.
"" Hellow Doctor Janerose!( Huku akimpatia mkono) Pole na Majukumu ya leo! Naona tunaonana onana tu lakini hatufamiani Niite Doctor Brighton! I'm come from USA! Ndio nafanyia kazi kwenye hii kampuni ila Mimi Ni Mtanzania Kama Wewe! Nipo kiutaftaji zaidi! Vipi naweza kukujua zaidi!?"
Janerose alibaki akitabasamu Huku akiutazama mkono wake Bado Umeshikiliwa na Brighton hauachii, alijaribu kuutoa taratibu Kisha alibaki ameshikilia mikono yake kwenye begi lake Huku akichezea mikanda ya begi.
"" Naona umekuwa kimya nipe Contact yako nitakucheki midaa! Huku akimpatia simu yake aandike namba.
Alichukua simu Kisha alimuandikia namba akaaaga kuondoka.
Janerose alitoka kimya kimya Huku akitafakari Ndoto yake ilienda mbali Sana tangu ujio wa wazungu wafike pale yeye aliingiwa na Ndoto ya kujiunga kwenye kampuni hiyo akafanyie kazi na ikiwezekana ahamie kabisa Marekani ili amsahau mazima Shamsi.
Hata usiku alipoenda kulala kitandani alianza kukumbuka jinsi Mzungu alivyomwambia ana tabasamu zuri! Bado Brighton alimuomba namba hii ikamthihilishia kabisa wamemuelewa alishika simu kuangalia Kama Kuna ujumbe wa namba ngeni umeingia lakini hakukuwa na ujumbe baadae aliamua kusinzia ili apunguze hiyo mihemko ya Ndoto za Marekani.
Asubuhi yake kulikucha alijiandaa ili aingie kwenye Majukumu yake lakini alipokea simu kutoka kwa Sharifu!
'"" Vipi mbona upo kimya Siku hizi! Harafu hautumii Sana mitandao ya kijamii Siku hizi? Make juzi nilimuona Denison akiwa anahojiwa na waandishi wa Habari! Kuna Operation alifanikiwa kuifanya imewaacha watu midomo wazi! Inakuwaje kijana mdogo kafanikiwa kawazidi hata wafanyakazi wenzake na wametangulia kazini? ila yupo vizuri Siku hizi na hapa ni miezi kadhaa tu imepita!! Vipi hujazipata?"
Janerose ilibidi ashushe pumnzi kwanza alikumbuka Kwa Mara ya mwisho alivyokataa hata asipigiwe simu ila ajulishwe tu kuwa Denison alikuja Tanzania kwa ajili yake, Hafu mbaya zaidi alifatilia mahusiano yake na Shamsi kuwa walirudiana hii ikamfedhehesha sana, aliamua kumjibu.
"" Hapana sijaona! Harafu simu yaku inazingua Siku hizi ila na kazi zimenibana kwasasa!"
"" Pole Sanaa!! Hussein anakusalimia pia! Naona haishi kukuongelea muda wote sijui ulimlisha nini!!?"
"" Hahahaa!! Muache Bhana huyo ndie Mimi kabisa alifaa awe pacha wangu sema Sasa likawa Ni dume ndo maana nakuwa nae mipaka!!?"
"" Sawaa Bhana!! Denison akizingua basi muoane nyie!!"
"" Weeee! Muone...! sa Reseous utamfanya awe mke wa pili kwako? Na huyo mkeo anae wivu kweli Siku yenyewe kidogo nichezee makofi!!"
"" Hana shida huyoo!! Niwaktuliza tu! Si unajua Mimi ndie mwanaume rijali bhanaa!!"
"" Wewe tenaa!? Na si Hussein au Denison ama Bra.... Aah sorry Bhana sijui nitake kusema kipi tenaa!?"
"" Malizia tu huyo Braa...! Ndo Nani tenaa!?"
"" Mekosea bhanaa! Harafu Denison hata huwa haniulizii!? Huku akivunga.
"" Jamaa yupo busy na kitabu sahii!! Kumpata Ni kwa Nadra sanaa!! Ngoja nikimpata nitajaribu kumuingizia hili Hafu nitakupa majibu!"
"" Au acha tu! Inaonekana keshanisahau Ani mpaka Mimi niwe maada kwake ndio aanze kunielezea!"
"" Wewe nae kwa kujishuku Daah!! Ila Mimi napigania muwe wote Siku moja! ''Sawaa!?"
"" Mhuu! Sawaa!" Baadae naona nimefika kazini! Ahsante kwa kunisindikiza!"
"" Muone!!! Kumbe nilikuwa nakupatia kampani!! Basi baadae na kazi njema.
Wakati anakata simu! Ndio anainua uso mbele yake ndio anakutana na Brighton mbele yake Huku mkono wake mmoja alikuwa kashikilia miwa imemenywa Huku akiwapatia watoto waliokaa wakimzunguka!! Aliendelea kugawa Hadi ilipoisha ndio anainua uso wake nakumuona Janerose kasimama akimtizama, alimpatia Ishara kwa kutumia macho yake ili asogee!!
"" Hongera Sana naona upo careling! Watoto wanafurahia uwepo wako! Na bafo unafanya tiba ya ugonjwa wa Manjano; Vipi lakini umzima!?"
Brighton aliamua kumtoa mbali kidogo ili wazungumze.
"" Vipi lakini Jana ulifika salama! Make nasikia Arusha kuna vijana wahuni wanakula bange hatari!"
"" Mara ya kwanza walijua kunisumbua sijui walijua mi wa mkoani ila sahii twaenda nao sambamba!!"
"" Mhuu! Kweliii!?"
"" Ila sio useme natumia..!! Make umeniuliza kwa makini!"
"" Sio hivyo!! Nakutizama tu kwasababu leo unaonekana kuwa Happy Sana! Basi kaendelea na Majukumu.
''" Okay! Baadae pia!!
Aligeuka na kupiga hatua Kama tatu lakini alisikia akiitwa tenaa! Ilibidi ageuke..kumbe Ni simu aliisahau mezani
"" Kweli leo una furaha! Isiyoelezeka Hadi wasahau simu!?
"" Khaaa!! Sorry bhana! Nimekusumbua but Nashukuru!"
"" Hukunisumbua! Sema nisingekuletea ingenisumbua Kuna Hawa Shemeji zetu wangepiga simu balaa!"
"" Alitabasamu tu Kisha aliaga aondoke!"
.... Inaendelea.....
Usikose sehemu ya 09.
Like, comments zenu ndio zinanifanya niendelee kuandaa zaidi Simulizi hii. Tusiangushane🤝✍️ leo ndio tarehe ya mwisho kwa kuchangia SAPOTI KWA MWANDISHI ambao bado naomba tujitahidi Basi 🙏
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 09" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Khaaa!! Sorry bhana! Nimekusumbua but Nashukuru!"
"" Hukunisumbua! Sema nisingekuletea ingenisumbua Kuna Hawa Shemeji zetu wangepiga simu balaa!"
"" Alitabasamu tu Kisha aliaga aondoke!"
ENDELEA...
"" Daaah!! Hata hivyo Janerose Ni mcheshi kweli. Brighton alibaki akimtizama Janerose mpaka anaishia.
Huku kwa Janerose aliendelea na pilika za hapa na pale baada ya kukamilisha kazi zake alitafuta sehemu nzuri akapumnzika Huku akishushia Pepsi ya baridi.
Kuna Mzungu mmoja alimfuata alionekana Ni kijana mwenye makamo ya Kati, alivuta kiti akaketi nae Huku wakiendelea na sitori.
"" Doctor Janerose! Naona kazi yetu imeisha! Vipi umefurahishwa na kazi za kampuni yetu"
"" Of course! Mpo vizuri Sana mpaka nimetamani kazi zenu na jinsi mnavyozidi kuendesha hasa kutoa misaada kwa watu wasiojiweza hii inanifanya nikumbuke mbali sana!!"
"" Kama wapi vilee!!!?"
"" Kuna Siku nilikuwa namhudumia mgonjwa alikuwa Ni mtoto wa miaka Kama sita hivi! Alikuwa ana tatizo la upungufu wa Damu ( sikoseli) wazazi wake walikuwa na maisha Duni! Muda huo mtoto alikuwa kaishiwa Damu! Mbaya zaidi mama wa mtoto huyo nae alikuwa ana juma moja kalazwa hapa hospital! Isingewezekana kumuongeza Damu mwanae, Tulijaribu kufanya utaratibu wa hapa na pale ili kunusuru maisha yake! Ikabidi niende stoo ya kuhifadhia damu nakuta Hakuna damu yenye group lake make ilikuwa Ni AB, niriludi nikiwa Ni mnyonge ile nikawapa taarifa labda awapigie ndugu zake wamsaidie, alijaribu kutafuta mawasiliano ya nyumbani wakamuahidi watafika haraka.
Tulikaa tukisubili Kama lisaa limoja Kuna Babake mdogo alifika akafanyiwa utaratibu akatolewa Damu ya kumuongeza mtoto, wakati huo ndio nimemuandaa mgonjwa wangu nimtafutie mshipa ili Ni connect ile damu iingie mwilini kwake nikawa nimefanikiwa! Lakini Ghafra tu khari ya mgonjwa ilibadilika alianza kutupa tupa mikono na miguu mithili ya mtu anaetetemeka kwa baridi! Baadae kabisa niliona baridi limeanza kumpata khari hi ikanichanganya ikabidi nimuite Doctor! Ile anafika amfanyie matibabu alimshika kifuani Huku akipima mapigo ya moyo aliishia kutikisa kichwa Kisha akasema " Dearth"
Nilibaki nikimtumbulia macho Huku mwili wangu ukiwa umepigwa baridi, nilitizama ile damu nloitundika juu nikatamani hata niichukue nimpelekee mtu aliyejitolea ani katoka kijijini kwa baskeli ili kunusuru maisha ya mgonjwa lakini Mungu alimpenda zaidi. Niliufunika ule mwili Huku natetemeka nikawa siamini kabisa kumbe mwanadamu akipoteza pumnzi ndio huwa anaogopesha kiasi hicho! Nilipata ujasiri tena nikamfunua kwa Mara nyingine ili nione sura yake nikagundua damu imeanza kuganda! Nilimfunika kwa woga Huku nikitoka mbio kumfuata Doctor nikamueleza, Ni kweli niliogopa kumwambia mamake ambae muda wote yupo nje akizunguka mbaya zaidi alikuwa na mtoto ananyonyesha Kama nikimwendea pasina maarifa anaweza hata kumuumiza mwanae au yeye kupoteza maisha.
Doctor alitoka Nje nakumuita ndugu yake alieambatana nae Kisha alimueleza kwa umakini zaidi.
"" Ninapenda kutanguliza pole kwanza kwa familia kabla sijaongea! Sisi Kama waauguzi tumejitahidi kutumia Kila namna ili Mgonjwa wetu awe na Afya njema lakini Ni mapenzi ya Mungu Mgonjwa wetu ametuacha! Naomba tujikaze kwa hili!"
Doctor baada ya kufikisha ujumbe! Kwa mwangalizi ukimya uliitanda kwakuwa Ni mwanaume nilimuona akikuna kichwa kwanza Huku akiondoka! Namie sikuona kuendelea kufatilia kipi kilifuata, Siku iliyofuata walibeba mwili wao kwenda kumsitili.
Janerose alimaliza kuongea na kuweka nukta kidogo! Huku ukimya ukitanda baadae alimuuliza Mzungu.
"" Harafu sorry lakini! Wewe waitwa Nani make natamani nikuite Wewe Mzungu!"
"" Naitwa Henny!!"
"" Waooo Doctor Henny!! Tuachane na sitori zilizopita kwahiyo mkitoka hapa mwaenda wapi tenaa!?"
"" Sasa hivi twazunguka Tanzania nzima! Ila nimeona hapa Kuna changamoto nyingi Sana! Kama itapendeza tunataka tuweke Branch hapa!! Vipi tukuweke kuwa msimamizi!!?"
'" Haaa!! Itapendeza ila hapa wazani nitapaacha!?"
"" Shauri yako! Kitu masirahi ndio huwa twaangalia!"
Muda kidogo Alifika Brighton akawa amekaa Huku akishusha pumnzi.
"" Vipi Brighton! Umemuona Binti Dangote! Anafaa kuwa wife material, au Ni macho yangu tu. Henny alitania Huku akimtizama Janerose.
Janerose alibaki akitabasamu tu Huku akimtizama Brighton, Huku akifikilia kitu.
"" Au inawezekana kweli akawa Brighton! Ila hapana Denison atanitafuta tu, mbona nakuwa Kama Sina msimamo! Ayaaa! Macho yake Duuuh!!?"
Muda huo Brighton alibaki akimtizama Janerose Kisha alimuita;
"" Janerose!! At ni ukweli au Wewe waonaje!?"
"" Aaah!! Achaeni Mambo yenu mi nataka nifanye kazi kwenye kampuni yenu kwanza!"
"" Tukuoe kwanza ndio ufanye kazi!
Henny aliongea na kuwafanya wenzake wacheke kwa pamoja.
"" Unajua Nini Janerose! Tuache matani ila unajibidiisha katika utendaji kazi, Kama kampuni yetu itapata mfanyakazi Kama Wewe tutaendelea Sana! Naona Hadi meneja wetu amekukubali Kama upo sereous tufanye kumtongoza akuunge kwa kampuni! Sijui umelizia!!?
Brighton aliongea akionesha u sereous kwenye maongezi yake Huku akimuachia Janerose atoe jawabu.
"" Nipo tayari hata hivyo niliwaza Siku nyingi niwe mbali na baadhi ya watu!"
Janerose aliongea kwa hisia mpaka akabaki anajisitukia sijui hata aliwaza Nini kusema vile.
"" Okay! Kesho asubuhi nitakupatia majibu kamili! Au utakuwa Ni mwangalizi wa hapa!!?"
"" Kivyovyote tu nitafanya! Ila mshahara uwe mnono tu.
Baadae waliachana Kila mtu aliendelea na Majukumu yake, lakini kwa Janerose Kila akishika kazi wazo linamuijia la kwenda USA tu.
Upande wa Brighton alikuwa amekaa kwenye hotel room walipofikia alichukua simu yake Huku akiangalia picha.
"" Huyu Mtoto jamani! Ananifanya Ni muwaze muda wote! Sa' sijui nimwambie ukweli! Mbona Ni mapema lakini!? Anyway when I see u a'm happy!"
Wakati Janerose amelala alikuwa akichezea simu yake Huku akichart kwenye Group la Ma Doctor wakipeana mafundisho mbalimbali Huku wakichangia hoja! Kuna Message iliingia ilibidi aiview
" Hey!?'
"" Mbona ni namba ya Nchi za nje hii! Asije akawa Mkulugenzi wa kampuni kapewa Details zangu ananikalibisha kazini!"
Alirudisha kwa Kureplay "" Hellow "
Kwa mood aliokuwa nao aliamua akae kitandani Huku akisubili majibu kwa shauku, baadae alifungua ujumbe japo ulikuwa mfupi.
"" Rafiki haujambo!?"
"" Sorry Nani!!?"
Kabla hajatuma aliona Kuna picha zinatumwa ilibidi azifungue kwanza, ilikuwa Ni picha yake akiwa na Denison! Aliangalia ile picha ikamkumbusha mbali Sana Kuna Siku walitoka out na Denison kuosha macho ndio wakawa wanapiga picha wakiwa ufukweni.
"" Oooh!! Ni Wewe Denison kweli!!?"
Janerose aliamua kumpigia akawa amepokea, kweli alikuwa Ni Denison akiwa amelala kitandani Huku akichezea laptop. Janerose hakuamini kabisa walibaki wakitazamana na Denison pasina kuongea! Uzalendo ulimshinda Janerose mpaka machozi yalianza kumtililika.
Denison ndio akafungua kinywa chake aongee nae;
"" Mbona hukutaka kuonana na Mimi!? Au kwa kuwa umeolewa na Brighton ndio maana ulikataa kutokea!?"
"" Haaaa! Nimeolewa na Brighton? Brighton yupi huyo tenaa!? Kwanini Wewe ulikataa kuongea na Mimi hata kunipa muda wa kujieleza kwako Napo hukutaka! Unajua Mimi niliishije pale nilipokukosa! Harafu unakuja na vitu visivyoelezeka.
"" Sawaa!! Nilimisi nikuone tu! Sikukupa muda kwasababu hata Wewe hukuthamini muda wangu niliokuwa nikikungoja nikuone angalau robo Saa ningelizika tu! Nimekupigia simu kwaajili ya Sharifu tu make kanisihi nikutafute angalau Mara moja namimi nimefanya hivyo kwa kumheshimu Sharifu, ila nafurahi kwakuwa umzima na umekuwa mrembo kweli! Umepata Mwanaume mwenye pesa!
.....Itaendelea.....
Usikose sehemu ya 10.
Like, comments and suggestions 👍✍️🤝🙏❤️
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "11" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
'"' Aliniuliza Kama nakufahamu! Baada ya kuweka picha tupo wote aliona. Jana kipindi kile mwapiga sitori na Henny na mie nilikuja kukaa pale nikapiga picha moja Kisha nikaipost! Denison akanifuata akaniuliza ikabidi nimueleweshe! Aninieleza vizuri jinsi mlivyofahamiana Nahisi Ni Kama Wewe ulivyoeleza basii! Ila Kuna kitu nimegundua.
ENDELEA....
Janerose alibaki akimtizama ili amalizie kile anachotaka kumalizia kuongea.
"" Vipi wataka nimalizie kuongea!!?
"" Yaaah!! Akikubali kwa kichwa lakini Brighton aliishia kutabasamu tu, Kisha alichukua maji ya kunawa.
"" Vipi lakini! Utafanya kazi DHB?
"" Natamani Sana Hafu Kama ningeenda USA ingefana Sanaa!"
"" Ani wataka tukakae meza moja na wewe! Sa si Nita...!! Au Basi tu.
"" Mbona Wewe humalizii sentesi zako muda wote? Utanifanya niache kusema na Wewe!"
"" Mimi mgeni ujue! Harafu itakuwa picha mbaya!"
"" Makusudi hayoo!"
'" Basii ngoja nimalizie...."Nitakuoa!"
Huku akiinuka kufata remote iliyokuwa kwenye meza ya TIV! aliwasha Huku akiconnect simu yake kwenye Bluetooth akiachia ngoma ya Amapiano.
Janerose alibaki akimtizama Brighton kipi anakifanya, baadae Bry alimnyoshea mikono Huku akimuuliza;
"" Vipi unaweza kuchezaa!!? Au nikuwekee Gospel!"
Janerose alibaki akitabasamu tu, Kila akimuona Bry Aliona Ni mtu simple Hafu Charming tu.
"" Mhuu!! Fanya Wewe!"
Brighton alibadilisha wimbo nakuweka wa Justin Bieber "Every minute" Kisha alisimama na kumshika mkono Janerose Huku mkono mwingine akiupitisha kiunoni nakubaki akimtizama usoni.
"" Dance with me! Be Free for anything!"
Janerose alikuwa Kama anaota muda wote mwili wake ulikufa ganzi! Hasa ule ukaribu wa Bry ndio ulimchanganya nakubaki akimtizama tu.
Brighton alibaki akimtizama pia Huku akicheza nae taratibu akisikiliza maneno ya Justin Bieber yalimkumbusha mbali Sana nakumfanya azidi kuzama kwenye ulimwengu mwingine! Ghafra simu yake iliita nakumfanya imtoe uweponi! Alimwachia Janerose taratibu Huku akipokea simu.
"" Nipo karibu tu hapa nakuja!
Janerose alibaki amekaa kwenye kiti Huku akitafakari Ni kitu gani kimemfanya mpaka akawa kwenye mood wa kucheza.
"" Sorry Janeee! Nahisi nimekukwaza kucheza na Wewe huenda hukutaka! Naomba niwie radhi kwa hiki kitu kilichotokea!!"
"" U usijalii!!! Sema hata Mimi Huwa napenda kuchezaa!!"
"" So kweli unaongopa!? Au kwakuwa hukunizoea ndio maana hukutaka kunipa sapoti!"
"" Muda mwingine tutacheza zaidi!"
Janerose Aliingia chumbani nakumuacha Brighton kakaa sebuleni! Alifika na kujitupia kitandani Huku akifunga macho yake kwa mikono yake.
"" Mungu wangu Aibu! Aibu hii, Brighton kanishika kiuno changu! Maskini naogopa tenaa! Kwanini nilimkalibisha Chai leo!? Aaa Hapana sio kawaida!"
Alisimama nakusogea karibu na kioo Huku akitizama sura yake! Alipiga picha jinsi Brighton alivyokuwa akimsogelea at! ""Dance with me" ana balaa huyu mkaka Hafu ndio kanitizama na hayo macho yake kayalegeza.
Alitoka Hadi chumbani akawa akimchungulia Brighton kupitia upenyo wa Pazia alimuona yupo Busy akichezea simu yake Huku akitabasamu.
"" Sijui anaangalia Nini hapo!? Au Ni picha zile tulizopiga."
"" Oyoo Janeee!! Ndio hutoki huko chumbani nataka nitoke mie!"
Brighton aliongea baada ya kuona ukimya.
Janerose alishituka nakurudi chumbani haraka alianza kuruka ruka.
"" Au kaniona nilivokuwa nikimchungulia!!? Ngoja niende."
Ghafura simu yake iliita muda huo alikuwa ameiacha mezani Brighton aliishika Huku akitizama ilikuwa Ni namba ngeni! Wakati kaishika Janerose aliwahi akawa ameishika nakujikuta wote waimeshika, Brighton alinyanyua kichwa chake Huku akimtizama Janerose.
"' vipi Ni wanaume wako wanakupigia ee!?' Make umewahi Kama risasi!"
Muda huo simu ilikata, alichukua pasina kusema kitu kisha alikaa kwenye korch Huku akisubili ipigiwe tenaa! Baadae iliita alipokea simu nakusikiliza.
''" Vipi naweza kukuona leo!?
Ni sauti ya kiume ilisikika, Janerose Alimtizama kwanza Brighton kabla hajajibu, Aliinuka nakuingia chumbani.
"'' Wewe mtu gani muda wote hauishi kunitafuta, nishakwambia kwasasa Nina Mambo yangu harafu nimempata mwanaume wa Ndoto zangu! Si Wewe una Jayce kulikoni kunifatilia Kila Siku! Nimechoka jamanii! Kila ninaposikia sauti yako Huwa wanipa maumivu hata hivyo Sitaki nikumbukie ya Nyuma! Kwangu Huwa Ni mwiba unaochoma moyoni mwangu!"
''" Please Janerose...! Najua kwasasa hunipendi, una maisha yako Ila Mimi ninachotaka kwako nikukuona tu, nimefika Jana Arusha nataka kujua uwapi? Au nipe sehemu yakukutana na Wewe ninamazungumzo nawe!"
"" Hapana sihitaji kabisa! Kazungumze na Mama Patricia! Sio Mimi!"
Janerose alikata simu Huku akiwa na hasira, Alirudi sebuleni Huku akionesha khari ya Furaha kwa kumchangamkia Brighton.
"'' Nimekuacha mwenyewe! Harafu na Wewe nikipigiwa simu unaniambia Ni wanaume zangu tu, sa sijui ninao wangapi!?
"" Si Denison na Shamsi....!?"
''" Shamsi...!!?"
"" Nitoe nje Bhana mimi nataka niende..!"
"" Yaani huyu Mjinga kweli nikikaa na furaha Huwa ananiletea Huzuni Siku zote!?"
"'' Vipi tena Janerose!! Mbona wazungumza mwenyewe!? Who's Shamsi!?"
Janerose alishidwa kujibu machozi ndio yalitoa majibu. Brighton alimuwahi nakukaa karibu yake Kisha alimkumbatia kwa kumuegemeza kwenye miguu yake.
"" Naogopa Sana kumuona mwanamke akitoa machozi mbele yangu! Moyo wangu unauma!! Tangu Siku nakuona niliona Ni mtu unayejitahidi kutoa furaha kwa nje ila moyoni mwako una machungu! Hata Siku Ile unasahau simu niliona reaction yako haukuwa Sawa! Ila Pole Sanaa Kuna Siku utakuwa Sawa!!"
"" Sorry Bry natamani kuficha maumivu ninayoyapata lakini nashidwa! Sikutaka nifanye haya yote kwako lakini inatokea tu! Nisamehe kwa hili.
Janerose aliinuka Huku akifuta machozi yake alisimama ili akalilie chumbani, lakini Bringhton alisimama na kumvuta Huku akibaki amemkumbatia.
"" Leo Lia mbele yangu ili nithamanishe machozi yako kadri yanavyomwagika ndio nikutafutie ujazo wa yale Yale machozi yawe furaha kwako!"
Brighton alichukua kitambaa chake Kisha alianza kumfuta taratibu Huku akimbembeleza baadae alimkalisha kwenye korch Huku akimuachia kitambaa aendelee kujifuta Kisha yeye alisimama.
""" Naomba uwe na amani! Ngoja nikamuone Henny Mara moja! Naomba unihakikishie unakuwa salama.
Aligeuka Huku akimtizama na kumuachia tabasamu 😊.
"" See you later Doctor Janerose! Byeeeeee! Naimani utakuwa mwenye furaha!"
Janerose alimpungia mkono Huku akimsindikiza kwa macho na tabasamu kwa mbali.
.... Itaendelea.....
Usikose sehemu ya 12.
Nasubili like na comments zenu nipo nawazoom tu😌.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "10" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Sawaa!! Nilimisi nikuone tu! Sikukupa muda kwasababu hata Wewe hukuthamini muda wangu niliokuwa nikikungoja nikuone angalau robo Saa ningelizika tu! Nimekupigia simu kwaajili ya Sharifu tu make kanisihi nikutafute angalau Mara moja namimi nimefanya hivyo kwa kumheshimu Sharifu, ila nafurahi kwakuwa umzima na umekuwa mrembo kweli! Umepata Mwanaume mwenye pesa!
ENDELEA....
Denison alimaliza kuongea Kisha alikata simu.
"" Khaaa!! Nini hiki tenaaa!!? Mimi nimeolewa na Brighton? Brighton yupi au huyu huyu kaja Hospitalini kwetu? Kwani wanafahamiana?"
Janerose alikuwa akizidi kutafakari lakini hapati mwafaka Kuna kitu alikumbuka muda ule wamekaa na Henny! Brighton alikuwa akipiga picha!!
"" Au Brighton picha zile ulizipost? Harafu watumia Jina gani kwenye mitandao ya kijamii!?"
Alikumbuka jina la kampuni DHB HEALTH ORGANIZATION! Aliingia mtandaoni akawafollow alianza kuangalia picha moja baada ya nyingine ndipo akakutana na picha ya Henny akiwa na meneja wa kampuni! Alizidi kupekua ndipo anakutana na jina la Brighton kapost na kushare kwenye page ya kampuni aliamua kumfollow kwa jina la "Official Health Bry" alikutana na picha za kazini zimepostiwa, Kuna picha ya karibuni kabisa alikuwa Ni yeye akipokea Dawa, na Kuna picha nyingine ilikuwa ya pamoja wakiwa kwenye kikao team nzima ya kazini!
"" Oooh! Au Ni Kweli Denison anafahamiana na Brighton! Mbona sijaona Kama wana urafiki au Kuna akaunt nyingine anatumia Bry mbona hii Ni kazi zake tu kapost!?"
Siku hiyo ilikuwa Ni Siku ndefu kwa Janerose mpaka Kuna pambazuka alikuwa na shauku Sana akutane na Brighton angalau amuulize kwa kina, lakini Siku hiyo alikuwa off alikuwa nyumbani tu!
"" Brighton nae tangu achukue namba yangu hakuwahi kunitafuta sa nitampata vipi sijui!?"
Muda kidogo aliona simu yake ikipigiwa aliwahi kupokea kumbe Ni video call, ile anatizama vizuri ndio anamuona Brighton akiwa bado kitandani kavaa singled na pensi! Janerose alianza kuona aibu Huku akiangalia pembeni kwa aibu.
"" Vipi chai tayari? Leo nataka ninywe chai iliyopikwa kwa mikono ya Doctor Janerose! Sijui nakalibishwa? Au nijiombee tu!"
"" Hapana! Sio ujiombee hata Mimi nilitamani kukalibisha sema namba ndio sinaa!"
"" Ooh! Sorry! Hafu sikuwahi kukutafuta ee!? Mie nae sijui nafeli wapi make nikajua tushabadilishana namba! Samahani kwahilo!"
"" Usijali! Basi karibu chai make nipo naandaa hapa! Ukiwa tayari nambie nikupe location!"
"" Sawaa! Ngoja nipige maji kwanza!"
Janerose alifanya maandalizi haraka Huku akiweka mazingira Safi baada ya kuona kakamilisha Kila kitu ndio alimpigia simu Brighton akampa Direction! Alichukua marashi nakupulizia nyumba chake Huku akimsubili mgeni wake afike.
Muda kidogo Brighton alifika akaishia getini Huku akimtumia ujumbe Janerose aje kumchukua.
"" Waooo! Karibu Doctor Brighton! Umefika kwa wakati sahihi. Huku wakiingia ndani.
"" Daah! Mazingira yanavutia humu ndani! Ni Kama alivyo Janerose tu!"
"" Aaa! Acha kuniongopea bhana! Karibu mezani tupate!"
"" Nashukuru Sana! Hatimae leo nimefika kwa Janerose! Najua huko Henny akiamka ataniulizia mno! Kumbe nishaanza kujua mitaa!"
"" Kawaida tu! Harafu Bry Siku ile ulinambia Wewe Ni mzawa wa hapa! Sijajua Ni wapi make Tanzania kubwa!?"
"" Et Tanzania kubwa! Ni vizuri naweza kusema Babangu Ni mtu wa Uganda ila mamangu Ni mtu wa Kilimanjaro! Tumezaliwa watoto watatu Mimi ndie mkubwa wadogo zangu wanaonifuata Ni wakike sema wao naona hawataki kuja Tanzania wanakaa zao Uganda! Mama na Baba walitengana kidogo, Mama anaishi Pwani kwasasa yupo kikazi ila makazi yetu nikitoka hapa lazima nipumnzikie Kilimanjaro! Na ndio tumejenga huko! Nahisi nimeeleweka!
"" Hayaa! Unajua kujieleza Ani umefanya ku summarize tu! Lakini nimeelewa umejibu kutokana nilivyokuuliza. "swali jingine Umesomea wapi shule na umeingiaje kwenye hili kampuni!?"
"" Elimu yangu nimesomea nje kidogo! Shule ya upili nimesomea Uganda Hadi namaliza! Baada ya kumaliza nilichukua course ya Afya katika kampuni lililopo Kenya baada ya kumaliza nikaona matangazo ya ajira katika kampuni ya DHB HEALTH ORGANIZATION! Nikawa nimefanikiwa nikaanza kufanya kazi jijini Dar es salaam! Make ndio office zao zipo baadae nikaunganishwa moja kwa moja na Mzungu nikapewa kazi ya stoo, mwishoe Kabisa nikasajiliwa rasmi Kama msambazaji wa hii huduma Africa mashariki yote.
"" Daah! Hongera Sana! Wewe tayari umetoboa Maisha! Hapo unakula shavu tu!"
"" Wee kawaida tu! Naona maswali umeishiwa! Siku ile nilikwambia nataka nikufahamu zaidi! Sijui Ni wakati sahihi kukufahamu!?"
"" Waweza nifahamu! Mbona Mimi nimekuuliza!?"
"" Okay! Sorry lakini Kama utanichukulia Mimi mfatiliaji Sana! Kuna picha nimeiona hapo juu sio ngeni kwangu! Kama nilishawahi kuiona sehemu! Au macho yangu tu!"
Janerose alishituka kwanza Huku akitizama picha zilizokuwa ukutani alikumbuka maneno ya Denison huenda itakuwa Kweli.
"" Picha ipi hiyo make zipo nyingi tu!?"
'''' Hiyo ya katikati naona upo Wewe pamoja na wafanyakazi wenzako wanne! Ila Nahisi sijakosea au nikuulize Direct tu nikipata majibu ndio nitaamini Ni Kweli. "" Unafahamiana na Denison!?"
"' Ani De e.. Denison!!!?"
"' Ndio!! Kuna kijana nilisoma nae O level! Nikaja kupotezana nae! Nimekuja kuonana nae Kama mwaka mmoja umepita ila alionekana kapata ajari mbaya hakuwa na uwezo wa kutembea! Kama kampuni letu tulikuwa tumeenda chuoni kutoa semina ya magonjwa mbalimbali baadae tukawa twapita kusalimia wagonjwa ndio nikakutana nae! Kama kawaida kampuni letu lilijitoa kumfanyia matibabu na hii Ni baada ya kugundua tuliwahi onana Ani tumesoma wote sema Mimi nilimzidi madarasa mawili ikabidi tutoe huduma! Majuzi Kati tena niliweza kuonana nae akiwa chuoni naona kwasasa kaimalika inaonekana anapitia njia nzuri Ni Daktari mwenye upeo wa kufikili kwa uharaka zaidi, Siku hiyo alinikalibisha kwake tukapata chai Kama hivi ndio nikaiona hii picha akaanza kunipa sitori kupitia hio picha naona tukio limejirudia tenaa! Naomba nipate majibu kwako kwa hii picha! Mna ukaribu gani na hii picha na ile nilioiona kwa Denison!?
Janerose alishusha pumnzi kwanza Huku asiamini kile kitu anachokisikia Kisha alielekeza macho kwa Brighton ili amjibu.
"" Daah! Milima haikutani ila binadamu hukutana! Kwanza nikushukuru kwa kujitoa kutetea maisha ya Denison! Ulichoongea Ni sahihi Wala hukukosea labda na Mimi nifanye surmarize kidogo! Denison nimefamiana nae kikazi kipindi nafanyia mwanza Mimi nilikuwa nikifanya kazi Mwananchi hospital (private) harafu yeye alikuwa Bugando! Muda mwingi nilikuwa nikiagizwa kwenda kuchukua baadhi ya vifaa vya matibabu na bosi wangu! Katika kwenda kwangu ndio nikafahamiana na Denison Mara nyingi nilikuwa nikienda nakutana nae nikawa nimemzoea na ndio chanzo Cha kufahamiana nae mpaka tukawa marafiki wa karibu ila tumekuja kutenganishwa na yeye alipoenda kusoma Kenya ndio tukawa mbalimbali!"
"" Vizuri! Make ungeniongopea ningejua tu! Kwahiyo Hadi Sasa mwawasiliana!?"
"" Mara moja moja tu!"
"" Sawaa! Vipi hajakuuliza kuhusu Mimi!?"
Janerose alitia kigugumizi kidogo! Make akikumbuka palangano la usiku lilivyokuwa ilibidi ajibu kiaina.
"" Kwani sahii Wewe na Denison mna ukaribu gani!? Mimi sijui Kama anaweza kukuulizia make hajui hata Mimi Nawewe twafahamiana, harafu Kwanini umeuliza hivyoo!?"
'"' Aliniuliza Kama nakufahamu! Baada ya kuweka picha tupo wote aliona. Jana kipindi kile mwapiga sitori na Henny na mie nilikuja kukaa pale nikapiga picha moja Kisha nikaipost! Denison akanifuata akaniuliza ikabidi nimueleweshe! Aninieleza vizuri jinsi mlivyofahamiana Nahisi Ni Kama Wewe ulivyoeleza basii! Ila Kuna kitu nimegundua.
.....Itaendelea.......
Usikose sehemu ya 11.
Like, comments and suggestions 👍✍️🤝🙏❤️.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "12" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Janerose alimpungia mkono Huku akimsindikiza kwa macho na tabasamu kwa mbali.
ENDELEA...
Brighton alivyoondoka tu, Janerose aliwasha simu yake Huku akitegeshea huenda Shamsi angempigia tenaa! Baadae Kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake ulitoka kwa Shamsi.
''" Kama utaamua leo kunilaza mtaloni Basi amua, hutaki hata kuniona ukajua Ni kipi nimekuitia!? Mbona Siku hizi umeanza tabia mbaya!?"
Janerose alimaliza kusoma ujumbe Huku akifikilia kitu Cha kumjibu Kuna kitu aliwaza kutoka kwa rafiki yake Hussein muda mwingi alikuwa akipenda kutumia neno moja pale Janerose anapopata appointment na mtu.
"" Kubali wito kataa maneno."
Alibaki akitabasamu kwanza, "" Daaah nakumisi Sana Hussein acha niende na msemo wako ila nitaufanyia kazi.
Alimtumia ujumbe Shamsi akimpatia location ya kukutana nae, baada ya hapo alijiandaa nakuelekea sehemu walipokubaliana wakutane.
Shamsi alikuwa kawahi kabla ya muda waliokubaliana, Janerose alifika sehemu ile aliangaza Huku na kule baadae alimuona, alifika pale na kukaaa.
"" Habari yako Shamsi!!?"
'" Njema tu za kunisusa!?"
"" Kawaida tu!" Okay nambie make nimeupokea wito wako"
"" Unanichukia!!?"
"" Wewe sema Bhana! Ulichoniitia.'
''" Okay! Hongera kwasasa jina lako linazidi kuwa kubwa! Nasikia kwasasa umerudiana na Denison! Na Kuna mkaka mmoja toka Marekani picha zenu zimeanza kusambaa kwenye mitandao! Lakini hao watu unajua wapo serious na Wewe!? Harafu usipende kuwa mrahisi kwa wanaume, wanaume wote mzazi wao Ni mmoja kwahiyo kuwa makini Kuingia kwenye mahusiano mapya!"
"" Mhuu! Sahiii Wewe ndio umekuwa msemaji wangu, vipi kuhusu Wewe na yule mwanamke wako mwalimu? Vipi tena kutoka kwenye mahusiano ukaenda kuanzisha na Jayce mfanyakazi mwenzangu sahii Wewe ndio unataka kunishauri Nini, Ani Mimi na Wewe are the same!"
"" Kwahiyo unajilinganisha na Mimi!? Mimi Ni mwanaume Siku zote harafu hakunaga mwanaume Malaya! Shauri Yako utapoteza Kila kitu!"
"" Ni sawa tu...!!" Kikubwa mi najitambua na bado najielewa!"
''" Okay! Tuachane na hayo ila Mimi nilichokuja kukwambia kwasasa hivi nataka nilee watoto wangu hata Jayce kwasasa simuhitaji nataka kulea mwanangu tu! Kuhusu Mambo ya zamani kwasasa nimeacha! Ila nataka nitulie na mwanamke mmoja Ani nioe kabisa! Kwasasa nataka nirudi kumswalia Arah' itapendeza Sana Kama Wewe ndie utakuwa mke wangu! Nimefikili kwa kina Sana naona Wewe ndie unafaa kuwa mama wa watoto wangu ni mtu tumetoka mbali tumepitia Kila aina ya changamoto lakini tunazisov zinaisha hafu tunaendelea, Naomba hata huu utofauti Kati yangu Mimi na Wewe uishe make siyo Ugomvi huu Janerose.
''" Lakini Shamsiii....!!"
''" Sorry ishia hivyohivyo kuniita sitaki uongee zaidi! Naomba ufikilie hilo na huu ndio ulikuwa wito wangu kwako."
Janerose alibaki akimtizama Shamsi huku akimfikilia Sana.
"" Sijui kwakuwa Mimi Ni mpole ndio maana Huwa ananifanya hivi! Au kwakuwa Sina ujasiri kwake ndio maana ananibuluza tu, Ni kweli nilimpenda lakini kwasasa Basi tenaa!"
"" Naona upo mbali kimawazo ila Mimi nataka nikuache! Lakini Janerose Mimi nishabadilika siyo Kama yule wa kipindi kile! Kwasasa starehe zote za ujanani nimeacha kwasasa namswalia mtume wangu tu."
Janerose alibaki akimtizama tena Shamsi make alikuwa akiongea kwa hisia kweli kumaanisha kitu anachokisema.
"" Shamsi Ni yule yule Huwa Ni Ector mzuri tu! Sio Mara yake ya kwanza kusema maneno haya japo leo kaonesha usereous Sana lakini Hapana!"
Shamsi alisogea karibu alipokaa Janerose Kisha alinyanyua mkono wake akamshika Janerose mikono yake akiiminya, huku akibaki kumtizama usoni.
'"' Nimekumisi Sanaa Janerose! Nisamehe kwa kitu kilichotokea hapo nyuma! Naomba uniamini kwa hiki ninachokiongea natamani kujieleza Sana kwako lakini naomba unielewe kipi namaanisha kwa ninachokiongea.""
Janerose alibaki akitizama mikono ya Shamsi jinsi anavyochezea kucha zake Kuna kitu kilimfanya afikilie.
"" Hata zamani alikuja hivi hivi kwa kuchezea vidole vyangu! Sijui kwakuwa ndio napendaa...!!?"
"" Janee! Naomba unisamehe tenaa!! Sema kitu chochote namimi nitekeleze juu ya msamaha wako."
Shamsi aliongea baada ya kumuona Janerose bado yupo kimya.
"" Hapana Shamsi... naweza kuondoka sahiii? naona tumefikia tamati katika Mazungumzo yetu."'
Shamsi alimwachia baaada ya kuona Janerose kasimama aondoke.
'" Mbona upo haraka hivyo! Niruhusu basi nikuage angalau Mara moja!"
Alibaki akimtizama Shamsi Ni kipi anataka amuage.
Shamsi alifanya kumkumbatia Janerose Huku akisemezana nae.
"" Naomba ufungue moyo wako tuyamalize! Hakuna ugomvi usioisha Janee hata Mimi Namisi ukaribu wako... namisi hata sitori zako pia Nimemisi tabasamu lako ni muda mrefu sijaliona!"
Kama kawaida ya Janerose Huwa Ni mdhaifu Sana kwa Shamsi, isitoshe ndie mtu aliewahi kumpenda alijikuta akiendelea kumkumbatia Huku machozi yakimlenga lakini alijikaza ili asioneshe udhaifu wake mbele yake.
""" Naomba kuondoka Shamsi.!"
Shamsi alimwachia Huku akibaki amemushikilia mikono huku akizidi kumtizama usoni.
"" Umezidi kuwa mrembo Sana! Naona Kuna watu wanatunzisha Mali yangu! Okay nakutakia Majukumu mema! Naomba usiendelee kunichukia kiasi hicho nitumie hata message ya salaam moyo wangu utafarijika Sana!"
Janerose hakutoa majibu zaidi ya kuchukua mkoba wake aondoke, aliondoka na kumuacha Shamsi bado kakaa mezani Huku akizidi kumtizama.
Alipiga Hatua mbele kidogo nakugeuka ili ajue Kama Shamsi kaondoka na yeye ile anageuka alikutana uso kwa uso na Shamsi, Shamsi aliishia kumkonyeza Huku akimpatia dole kwa mkono wake. Janerose alijisahau akaachia tabasamu baada ya kukumbuka alirudia kumtizama tena huku akikunja sura, Shamsi aliliona hilo nakubaki akizidi kutabasamu Mara mbili yake.
"" Tabasamu ulilonionyeshea hapo awali haliwezi kuzibwa na muonekano wa Mara ya pili, ila nimeipenda hiyo ingependeza muda wote ungenioneshea tangu nimekaa na Wewe ningefarijika Sana!"
Huku kwa Janerose baada ya kufika nyumbani aliona kabisa anaelekea kuchanganyikiwa ingali Ni mwenye akili yake timamu.
"" Huku ndio kupotea mazima kabisa! Mbona Sina maamuzi tenaa! Et Shamsi kanikumbatia tena Kama Brighton! Harafu nimetulia tu! Ni Nini hatima yake lakini!?"
Wakati bado ametulia aliona ujumbe ulikuwa waingia WhatsApp aliufungua na kukuta Documents zimetumwa, Huku zimeambatanishwa kwa ujumbe.
"" Karibu DHB, Mkurugenzi kakubali kujiunga na kampuni, Na hizi Ni baadhi ya nakala za mkataba waweza zipitia harafu kesho ujaze mkataba rasmi!"
Janerose aliruka ghafra Huku akiwa amejaa furaha tele.
"" Waooo Mungu kanikumbuka hatimae Ndoto ya kwenda USA imetiki! Jumapili nitaenda kumtolea Mungu Shukrani mbele ya Madhabahu.'"
Muda huo alishidwa hata kumjibu Brighton aliishia kupekua page moja baada ya nyingine, wakati bado anaendelea kupitia Brighton alimpigia simu.
"" Vipi upo sawa lakini!? Make nilikuja kazini Mambo yakawa mengi Hadi nikakusahau!"
"Umepitia mkataba lakini?"
"" Mimi nipo Freshi tu! Ndio namalizia kupitia hapa mkataba! Yaani leo nipo na furaha natamani niweke mziki nicheze kuthibitisha furaha yangu!"
Brighton aliishia kucheka kwanza, furaha ya Janerose ilimthibitishia kweli Hana Huzuni tenaa.
"" Okay Enjoy! Basi cheza Kama hutacheza tenaa!"
Alimaliza na kukata.
"" Yaani nikienda kule Marekani nitakuwa nikivaa Earphones Hafu napiga pamba kali, then naingia kitaa kuzuga kidogo najichanganya sehemu yenye upepo mzuri naagiza zangu juice Kisha naanza kunywa Huku nikichezea laptop! Harafu natafuta marafiki wazungu nakuwa nikibadilishana nao mawazo! Sijui nitakuwa nikikaa ghorofa la namba ngapi huenda Ni ya mia huko, nakuwa juu juu nawatizama watu wa chini harafu nachukua simu nampigia Hussein simu video call tena nasubili akiwa lunch na hao kina Reseous, Falaja na huyo Jayce! hakika watanikoma wataanza kuitana njoo, Njoo umuone Janerose yupo USA kwasasa Ni Doctor mkubwa anakaa na wazungu tu!! Daaah! Naona vile naenda kuwa na furaha ya Moyo isiyokoma😌.
.... Itaendelea.....
Usikose sehemu ya 13.
Like comments and suggestions 👍✍️🤝🙏❤️.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "13" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Baada ya Janerose kutoka kwenye Tafakuri yake aliinuka kitandani nakuchukua simu ili amjuze Hussein kuhusu Habari mpya zilizojiri kuhusu kuonana na Shamsi hatimae kuhamia Marekani kikazi.
"" Lakini Janerose! Unaliamini Hilo kampuni usije ukapoteza kazi yako namna hii hii, Harafu kuhusu Shamsi hapo siwezi kusema make naweza kukuzuia lakini Wewe bado ukawa na hisia kwake! Kama humtaki hebu vunja mawasiliano nae leo amekuita na Wewe ukafunga safari! Sahii unakuja kuniambia nikushauri Nini hapo? Anyway Kama hutakuja kuniaga jitahidi likizo inayokuja tuonane.
"" Sawa Hussein nimekuelewa lakini sikwenda kuongea nae kuwa Ni upande wake! Alinisihi ana Mazungumzo namie ila hakuna chochote kilichotokea baina yetu."
''" Haina shida ila ukienda huko hakikisha unakuwa busy na masomo! Jisimamie mwenyewe katika kazi yako.
++++++++++++++++++++
Habari za Janerose zilizagaa kwa Kila mtu aliyekuwa akimfahamu, Habari hizi zilifika Hadi kwa viongozi wake wakuu, wengi walizipokea vizuri nakumpongeza kwa hatua nyingine ya mafanikio.
Ilikuwa Ni jioni moja leo faraja alimtembelea Jayce kumjulisha kuhusu Habari za Janerose.
"" Sasa shoga angu Janerose huyo USA! Ulimchukulia Bwanake sahii naona anaenda kusahau yote ya nyuma ndio utakuwa ukimuona mtandaoni yupo na Mzungu, muda huo Wewe umebaki na Patricia! Harafu nikupe umbea."
"" Ushaanza kuninanga! Wewe si ulishadadia nimkubali Shamsi harafu sahii waniletea Habari gani hizo!!?"
"" Mimi nilikwambia ingia taratibu mguu mmoja ndani mwingine nje! Wewe Sasa ndio ukadumbukia Hadi kichwa, Wewe ulikosea pale ilikuwa Ni kula pesa tu matokeo yake umetengeneza na copy yake! Ila Hongera make wakwangu nikimuomba pesa tu anachomoa et napenda pesa mno nitakuja kumfilisi Sasa sijui anataka kuziweka stoo!?"
"" Hahaahaaa!! Ila Wewe harafu Siku Ile ulinambia ulienda kumtembelea Resious!!! "Hana usemi kweli make Bwanake na Janerose Ni marafiki wa kufa na kuzikana."
"" Daah!! Nilisahau ndugu yangu!! Tatizo Resious akimuona huyo Bwanake utasikia My! My Mara ooh naumwa! Hadi Huwa naboeka anavyodeka! Haya huyo Hussein nae yupo Pole bibie! Nikuletee Nini Jioni!! Ndo akatoka Sasa tukaanza sitori zetu, kumbe baba Patricia alienda Arusha kumuomba msamaha Janerose! Janerose nae si akachomoa kwahiyo shoga angu Wewe ndie baba, mama kwa Patricia jiandae kisaikolojia kulea."
"" Kuwa Sereous basii!!
"" Eee wenzio Hadi picha tunazo walipiga picha wamekumbatiana baada ya kuwekana sawa."
Faraja alichukua simu yake nakumuonesha Jayce, kumbe Siku yenyewe alipomtembelea Resious aliiona ile picha make Janerose alichati na Hussein kupitia simu ya Resious na picha ilitumwa kwake hivo kwa Faraja ilikuwa Ni rahisi kuipata. Jayce hakuamini kabisa Kama Ni kweli Shamsi kafunga safari kwenda kumtembelea Janerose.
"" Vipi mbona umekaa kimya hausemi!"
"" Kuna kitu nawaza kufanya, Kama kweli ataniacha huyu mwanaume atakuja kunilaumu bure!!"
"" Isije kusema waenda kumchawia??"
Jayce aliishia kutabasamu tu Kisha alimuita mwanae Patricia alikuwa akilia.
"" Pati!! Njoo mwanangu unalilia Nini!?"
"" Baba ameniachaa!"
Faraja Alimtizama Patricia Huku akongea kimoyo Moyo.
"" Baba kaenda kwa mtu ampendae mamako si alifata pesa tu, hakujua Kuna matokeo mengine yangetokea."
"" Faraja!!! Jayce alimwita baada ya kuona yupo mbali kimawazo.
"" Ooh nambie,,,!"
"" Nisaidie Basi kufatilia Habari za Shamsi na Janerose Kama Ni kweli wapo ote!"
"" Una shingapi hapoo!!?"
"" Mhuu!! Nawee!!' Hata haunaga urafiki, Wewe huwezi fanya kwa rafiki yako jamaniiii!"
"" Wewe wasema unajua huko Ni kujitoa mhanga harafu si wajuaga Hussein akiwepo anavyotuchukiaga! Inahitajika hata pesa ya soda Nikiwa naongea nashushia Pepsi ya baridi ili nipate umbea."
"" Ten tu, ndio itakutosha ukifanikiwa nitakutoa out twende kwenye chimbo la kitimoto."
+++++++++++
Huku upande wa Sharifu leo alikuwa kakaa sebuleni akichart na Denison What's up Kuna picha nyingi walikuwa wakitumiana Huku akiangua kicheko chenye Emoji kadhaa.
Nurazy alikuwa Jikoni baada ya kumuona Sharifu akizidi kucheka Huku amejisahau, alinyata taratibu Hadi kwenye kotch akawa akichungulia charting aliona Ni picha za Janerose zimetumwa, Sharifu nae alimtumia picha ya Nurazy Huku akimalizia caption.
"" Natarajia nikamimbe kwanza si unajua nataka mtoto sahiii!"
"" Harafu kwao itakuwaje!?" Denison alihoji.
"" Kwao hawataki mwanaume mwislamu wazani nisipofanya hivyo watanidhibiti, ila hata Nurazy Hana shida make tunapendana."
"" Kuwa makini! Asichomoe harafu muwekee mipaka! Make wanawake ukiwapa Uhuru huwa wanataka kutuendesha!"
Nurazy alimaliza kusoma mpaka akaishiwa Nguvu nakubaki akicheka Huku akiondoka kimya kimya.
"" Wanaume mnajua kutusema! Yaani Denison anashabikia mie nipigwe mimba na Sharifu! Anashidwa kusema tukaongee nao wazazi watakubali tu."
Huku kwa Sharifu hakushituka walaa Kama charting Yao imesomwa na Nurazy. Aliendelea kuchart na Denison Mara ya mwisho alimuuliza kuhusu ujio wa Janerose Kama wataonana nae, Denison alimjibu.
"" Sema nimemumisi kweli Janerose! Nitajitahidi nimuone live angalau Mara moja! Ila kwakuwa yupo Huku nitajaribu kusema nae kuhusu urafiki wetu! Hivi unajua yule Binti niliishi nae Kama rafiki tu, kuhusu mahusiano sikuwahi kumtamkia ila urafiki wetu ulikuwa Ni zaidi ya wapenzi! Siku nimekuja Tanzania unajua nilikuja kumwambia live nimuweke wazi kuwa nampenda sema Mambo yaliingiliana tu."
"" Mwaambie bhana! Unajua sahii mtoto anarukaruka Kama kuku anayetaka kutaga! Kuna Brighton huyo asije kutupia ndoano akaibuka na samaki."
"" Hivi unajua Siku yenyewe nimemuona Janerose yupo na Brighton moyo wangu ulilipuka ukafanya Hadi nimpigie simu pasina kutaka Hafu nikaanza kumjaji kweli! Ila alinipa majibu mpaka nikajilaumu kwanini sikumpa nafasi yakujitetea! Harafu nimekuja kufatilia kumbe alifanya vile ili awe mbali na Shamsi! Next time nitamuomba msamaha."
"" Mhuu Sharifu! Mnachart na Nani muda wote mpo Busy hata huniulizii Kama kumeiva!!?
Nurazy aliamua akatishe Mawasiliano namna ile make aliona Ni Kama wanazidi kumjadili Kama Ni kumibwa sahii wamefikia Hatua ya kulea Mtoto wanaelekea na kusomesha.
"" Mhuu! My kwa wivu jamani! Nachati na Denison bhana! Si unajua wenzetu wako kwenye upepo wa mjapan muda wote Ni kiyoyozi."
"" Aah! Mmetosha basiii!! Harafu kumbe ulikuwa ukipita na Janerose ee!?'' Make mazoea yenu yalizidi Sasa hivi nitapumua kwa huo ukaribu Duuu!!"
"" Umeanza ee! Ani Mimi nipite na mtu wa rafiki yangu kweli! Namheshimu Sana ujue."
"" Mbona nilisikia Bwanake Janerose alipita na rafiki yake tena mfanyakazi mwenzake kabisa!!"
"" Kwa wasiojitambua ndio hufanya hivyoo Siku zote!""
"" Eee! Ndo wanavyosemaga ila Mimi sitaki nimuachie rafiki yangu azoeane na mchumba wangu hio hapana! Kama Ni kukutana labda huko mtaani kwangu aje usipokuwepo!"
"" Kwa wivu Wewe mwanamke unaongoza! Ndo maana rafiki zako siwaonagi hapa nyumbani kumbe ushawakataza!?"
"" Kabisaaa! Agape, Mariam na wao Wana waume zao! Mbona wao hawajawahi kunitambulisha kwa waume zao! Basi tuishi hivyo!"
..... Itaendelea..........
Usikose sehemu ya 14.
Like, comments and suggestions 👍✍️🤝🙏❤️.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "14" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Kabisaaa! Agape, Mariam na wao Wana waume zao! Mbona wao hawajawahi kunitambulisha kwa waume zao! Basi tuishi hivyo!"
ENDELEA..
Leo ndio ilikuwa Ni safari rasmi kwa Janerose kuondoka kwenda USA kujiunga na kampuni la DHB HEALTH organization.
Waliondoka na uongozi wote wa Brighton, Henny na wengineo ili kwenda kuweka mikakati ya kazi rasmi. Majira ya Jioni ndege ilitua Airport walikuja kupokelewa na baadhi ya wafanyakazi wenzao.
Hatimae ilikuwa Ni wakati wakupata chakula Cha usiku, Janerose alikuwa akitoa macho Huku akiwatizama wenzake ambao muda wote wapo busy kula, mbaya zaidi muda wote wanaongea kingeleza Cha ndani alibaki akiwatizama Huku akifikilia chinichini.
"" Nilifikili nakijua kingeleza kumbe Huku wanakingeleza Cha mafumbo na wao yaani ni Kama kunisekenya nipo hafu nisijielewe, lakini Brighton mwenyewe kaenda wapi? Bado Henny nae yupo busy na vitabu vyake anapita anarudi Daaah! Huku ndio kupatikana hasua!"
Wakati akiendelea kutafakari Ghafura aliisikia kicheko Kuna wadada wawili waliingia sebuleni Huku wakiwa wamevalia vipensi na vitop! Walifika nakukaa Huku wasimsalimie, waliendelea kupeloose mtandaoni Huku miguu yao wameweka nne Huku wakiachia vipaja vyao wazi.
Muda kidogo Aliingia Brighton Huku kapiga pensi alipofika tu, vile vidada vya kizungu vilimuwao Huku vikimpatia kiss kadhaa. Kuna mdada mmoja aliongea kiswahili na kumfanya Janerose atoe jichoo.
"" Waooo my lovely Doctor! I miss you Honey! Tanzania kuzuri make umezidi kupendeza."
Brighton kabla hajajibu alikaa kwanza kwenye kiti huku akimtizama Janerose, Kisha aliendelea kuongea nao.
"" Shamy! Unajua vile nilikumis afu una bad behavior hata kuona ur phone number hamna!'"
"" Sorry! I'm busy Bry na my business! Si unajua nilienda tafuta customer ili Ni make money and then tuenjoy!"
"" Waooo! Good idea!"
Janerose aliona kuboeka aliamua kutoka nje angalau akatulize akili, wakati yupo nje alianza kuangalia vidada vilivyovaa uchi uchi ilibidi ajitizame vizuri kwanza na yeye make alipiga suruali kubwa na t-shirt pana Kama swaga! Aliishia kujicheka tu.
"" Sijui ningevaa kigauni kifupi ndio ningeonekana wa USA kwasasa naonekana Tanzanian people! Lakini Sasa ningejuaje watajijua wao bhana!! Hafu Brighton Tanzania alikuwa akivaa tofauti Huku Sasa ndio kafanana nao kabisa hafu vidada vipo uchi uchi hafu vinashikana shikana ovyo na Bry, afu nae katulia tu et anacheka.
Wakati akizidi kushangaa watu wanavyopita aliamua kumpigia simu Hussein akawa amepokea video call.
"" Hellow Doctor Hussein! U see me?"
"" Muone peleka kingeleza chako huko! Mhuu unaenda Kasi Wewe sahii tu waniongelesha kingeleza okay I see you so!?"
"" Hahaahaaa! Utani bhana! Nimefika Jioni ila Sasa hata sielewi rafiki yangu! Bry yupo Busy na vidada vya kizungu harafu chakula Chao Sasa mi kimenishinda Ani sijui wamekoroga tambi na minyanya! Jamanii Nahisi kukonda Mimi na nilivomwembamba hapaa Labda ngoja tuone!?"
Kabla Hussein hajajibu Reysious alisogea.
''' Aaah! Na Wewe ushaanza wataka kuchungulia Nini Sasa! Au ukawaambie rafiki zako ndoto ya Janerose imetimia!?"
Hussein alibaki akiongea na Reysious baada ya kumuona anazidi kumsumbua.
"" Mpe simu Bhana niongee nae wifi yangu!"
Reysious aliongea ilibidi Hussein amuachie simu.
"" Yaani wifi una roho mbaya Wewe ukaona usituage kabisa ukaenda kimya kimya hata taarifa hamna! Mhuuu hata rafiki yako wa Dhati kabisa hukumuaga!?"
"" Wewe hebu tulia kwanza niongee nae si umemsalimia Basi inatosha!!"
"" Ayaaa! Ongea nae ulizike si unaonaga Kama Mimi ulikosea kuwa na Mimi ila ulifaa uwe na Janerose!!?"
"" Please Reysious! Unanikosea Sana!"
"" Sa Hussein' baadae Sasa make mkeo anae wivu huyo! Mpe simu niongee nae kwanza."
"" Wifi yangu mbona unakuwa haujiamini kiasi hicho, Hussein Ni rafiki yangu Mimi ningekuwa namtaka ningemchukua toka zamani make alikuwa hakujui hata Wewe! Isitoshe nikwambie huyo Hussein ndio nilimshawishi awe na Wewe kwahiyo naomba ubalance shobo na hiyo mihemko yako! Wewe Kama unapendwa hebu tulia Basi mapenzi yako yawekee mipaka watu hawaishi hivyo! Kama utaendelea kunichukia Ni sawa! Harafu wape taarifa na hao rafiki zako wanaokutuma Kila Siku ujue Janerose anaendeleaje tulieni majibu mtayaona wenyewe pasina kutumia nguvu! Naomba mtulize midomo yenu! Wafikishie na wenzako Habari zangu.
Janerose alimaliza nakukata simu make aliona Kama Reysious anataka kumpanda kwa kichwa. Huku kizaazaa kwa Hussein kiliendelea.
'"' Hussein unaona Sasa!?' Unakataaga hukudate na Janerose! Umeona alivyonitukana lakini!? Shida mwanamke mkishare tu anakuzalau et Mimi ndie niliemshawishi Hussein awe na Wewe! Hivi kumbe ulitafutiwa mwanamke na huyo rafiki yako! Na hukunipenda kumbe!!?
Hussein aliishia kumtizama Reysious nakubaki akicheka Huku akirudia maneno ya Reysious aliyoyaongea Janerose.
"" Et nilitafutiwaga mwanamke na Janerose! Ndio nilitafutiwa kwasababu alikupenda jinsi ulivyo mrembo, tabia yako, umbile lako hili lilimvutia Kila muda aliongea sifa zako! Naweza kusema hakuchoka kukukuelezea jinsi ulivyomteka akili yake! Na kwangu ikawa hamasa zaidi kuwa na Wewe make kwako sioni kasoro yoyote ila punguza marafiki wanaokuulizia Habari za Janerose muda wote! Ndio sio inayopungua kwako.
Hussein alimaliza kuongea nakuingia bafuni kupiga maji. Reysious alibaki ametulia pale Huku akitabasamu mwenyewe.
"" Kumbe napendwa hapa! Ila Janerose Ni kweli ulikuwa ukinisifia hivyo kwa Hussein!? Daaah nimejikuta natabasamu tu.'"
Aliinuka nakuingia chumbani alifika kwenye kioo Huku akitizama sura yake kupitia kioo alibaki akicheka.
"" Harafu ninae dimpo kumbe! Harafu na kasura kazuri jumlisha rangi Ani nikicheka nakuwa mrembo kweli!"
Muda huo Hussein alitoka bafuni nakumkuta Reysious yupo busy nakioo alifika nakumkumbatia kwa nyuma Huku wakibaki wote wakitizama sura zao kwenye kioo.
"" Unapenda kujisifia Wewe mwanamke! Ni mrembo ndio! Ila wivu Sasa daah! Ndio unakufanya ufubae, Harafu usiwe wamchukia Janee ni mtu wangu wa thamani ujue!!"
"'' Simchukii hata hivyo! Ila sipendi kuwa wamsema mbele yangu! Yule Ni mwanamke mwenzangu afu wamsifia!"
"" Basiii! Umekataa kabisa kukubali ombi langu la kudhibiti wivu kwa Janee, Harafu natoka nikuletee Nini!!?"
"" Oohoo!!!! Nileteee... Mhuu! Sijui Nini tu! Basi tutoke wote leo."
"" Wewe mwanamke! Utanichelewesha bhana! Si hujaoga!?"
"" Nia yako hutaki kwenda na mie tu!
"" Ndio umenuna Sasa!!?'"
''" kimya... hunisemeshi!!?"
"" Wewe si hutaki tuondoke wote!?'"
"" Basi dakika kumi tu za kujiandaa!!! Sio ndio upendezee utazani waenda kwenye kitchen party! Make nyie wanawake mkiingia ndani mpaka twasahau."
"" Angekua Janerose anajiandaa usingesema ila Mimi Sasa , na mabango juu!! Ayaa natoka Kama napeleka rejesho kwenye kikoba."
Hussein ilibidi acheke tu.
"" Daaah! Wanawake bhana Huwa wanataka waongee tu muda wote! Kabla muda huo kautumie hata kusugua mguu ila kanaongea balaa!!?"
.... Itaendelea......
Usikose sehemu ya 15.
Like comments and suggestions 👍✍️🤝🙏❤️.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "15" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Hussein ilibidi acheke tu.
"" Daaah! Wanawake bhana Huwa wanataka waongee tu muda wote! Kabla muda huo kautumie hata kusugua mguu ila kanaongea balaa!!?"
ENDELEA....
Janerose alimaliza kuongea akawa amekata simu yake. Brighton alitoka nje kumuangaza baada ya kumkosa muda mrefu sebuleni.
"" Janeee.. unahisi kuboeka!!?"
Janerose ndio alisituka na sauti ya Brighton make akili yake ilikuwa mbali Sana.
"" Oooh! Umenifata kumbe!!? Mimi nilikuwa siwaelewi nikaona ngoja niwaache."
"" Nikuwazoea tu Hawa wadada! Wanaishi kizungu Sanaa! Ndio hujisikia Vizuri!"
"" Mhuu! Huku Akiitikia kwa Ishara.
'"' Daaah! Ila umependeza kwa hiyo swaga! Umejisitili vizuri!''
"" Umeanza utani wako! Harafu Meneja nitamuona lini make na hamu kweli nimuone!!"
'" Hutamuogopa!? Harafu Ni jitu Nene linapumulia juu juu hafu lavaaga miwani! Ila linaongea ujinga lile! Au ndo mijitu minne ndio inapenda kuongea hivyo!"
"" Sikweli!! Nani kakwambia?"
"" Wewe mwanasayansi kabisa hujui saikolojia ya watu! Ni utafiti uliofanyika ndio iko hivyo watu wanene wanapenda kuongea matusi Sana!"
Muda kidogo Shamy alitoka nje aliwakuta wakiendelea kuongea pale alisogea Hadi kwa Brighton Kisha akimnong'oneza sikioni huku akimshika mkono na kumvuta. Brighton aliamua kumuaga Janerose.
Muda huo wanaingia ndani Henny alikuwa akitoka nje Huku akipangusa mikono yake iliokuwa imejaa vumbi la dawa, alitazama pembeni yake akawa amemuona Janerose yupo busy na simu.
"" Doctor Janerose! Mbona unajitenga kiasi hicho! Njoo unifungulie bomba kwanza!"
"" Oooh!! Umemaliza kazi zako! Make umekuwa busy tangu tufike hapa!?"
"" Unajua dawa zilikuwa zimetuishia hapa tulikuwa twaandaa dawa kwanza!"
"" Heee! Hadi dawa huwa mwaandaa nyinyi! Mi nikajua mwachukua sehemu! Lakini mpo vizuri!?"
Henny alibaki akimtizama muda huo alikuwa akifuta mikono yake na kitambaa, aliamua kumkoa kidogo kichwani.
'"' Muone kwahiyo huduma zetu huziamini pia!? Hapa Kuna mkemia mkuu huwa anakagua kwanza!"
"" Hapo sawa! Huku akicheka.
"" Naona umeboeka leo! Wenyeji wamekutenga! Basi nisindikize sehemu!"
"" Mhuu wapi?
"" Jiandae kwanza!!"
Janerose alienda kubadili nguo na kuvaa kigauni kifupi kilionekana kumpendezea sana, alipita sebuleni nakumkuta Brighton akiwa mezani akiandika kana kwamba anajisomea. Janerose alifika sebuleni akawa amesimama Huku akiwaza jinsi ya kumuuaga.
"" Sogea Basi nikuone ulivyopendeza! Nimesikia marashi yako yametanda sebule nzima ndio watumia Burhan!?"
Brighton aliamua kusimama Kisha alimfuata Janerose Hadi alipokuwa amesimama mlangoni, alifika nakumsogelea Huku akizidi kumkagua vizuri! Alinyosha mkono wake na kamtengenezea Nywele zilizokuwa zikikaribia Kuingia machoni lakini alimuuliza;
"" Vipi leo una mtoko na Henny!?
Janerose alishikwa na kigugumizi Huku akifikilia atoe jibu gani baadae alijibu.
"" Hatukawii kurudi! Kuna sehemu namsindikiza tu!"
"" Vizuri! Ila Nahisi mtakuwa mnaenda kudate!"
"" Ku ku u date!!?"
"" Yaah! Hafu umeshangaa kweli ila msiende kucheza mziki! Kumbuka uliniahidi Kuna Siku tutacheza wote Siku ile nilipokuja kwako."
Janerose aliinamisha kichwa chini kwanza, make alikumbuka Siku yenyewe Bry alivyojiachia kwake mwisho aliishia kutabasamu tu.
'"' Basi nendaa!!!"
Alinyanyua Hatua kazaa kusonga mbele, Brighton alimuita tenaaa. Ilibidi ageuke make alikuwa akimfuata.
"" Kuwa na amani! Kwa vitu ulivyoviona Jana naomba visikuwazishe Sana! Vichukulie vya kawaida tu!"
"" Oooh!! Unazungumzia kuhusu Shamy!? Mbona kawaida tu au Kuna kingine!?"
Brighton alibaki akicheka tu Kisha alimshika Shavu.
"" Sahii unaenda kutengeneza Maisha mapya! Ni muda tu unaenda kusahau yote yaliyopita.'"
"" Thanks Bry! Mimi pia natamani iwe hivyoo! Byee nitakuona baadae!"
Alitoka Huku akikimbia baada ya kusikia mlio wa pikipiki, Alifika Hadi nje nakumkuta Henny kavaa zake pensi na jezi nyeupe, Henny Alimtizama Huku akimuachia tabasamu.
"" Wewe Ni bomba kweli! Siko kwa kupendeza huko.'
Janerose aliachia tabasamu Huku akipanda.
"" Henny Mimi naogopa eti, naona huku Kila Kona magari yamejaa Sasa utaendeshea wapi!?"
"" Wewe tulia nikupeleke uswahilini si umekalili uswahilini Ni huko kwenu tu!?"
Siku hiyo walitembelea sehemu nyingi Sana Henny alijitahidi kumtembeza Kila sehemu ili kumfanya Janerose asijihisi mpweke tena. Majira ya Jioni walirudi na mapocho pocho kibao! Walifika Hadi nyumbani Huku wakisaidiana kuingiza ndani, Janerose Aliingia kwenye chumbani chake Huku akitizama baadhi ya vitu walivyonunua hakili yake ilimkumbuka Hussein make aliwaza huenda wangetumia wote na Hussein Huku wakifurahi aliona kabisa Hana mtu wa kufurahi nae kwasasa angekuwepo Hussein Siku ingeenda vizuri Sana.
Ghafra mlango uligongwa ilibidi akafungue alikuwa Ni Shamy kaja kulala.
"" Ni Wewe Jenny! Leo hii Night Sina pakulala naomba tulale wote, make huko nje siwaelewi."
Janerose hakuwa mgumu alimkalibisha lakini aliwaza moyoni mwake.
"" Inamaana Siku zote huyu Shamy huwa analala wapi? Au anakaa wapi? Hata sikaelewi tu."
Muda huo alifunga mlango lakini alisitushwa na kelele zikitoka sebuleni.
"" Kama hataki kurudi nyumbani basi huyo kijana amuoe!"
"" Mhuu Nani tenaa? Ina maana Shamy kaja hapa kwaajili ya mkaka! Sa' atakuwa Nani!?"
Kidogo alisikia akiitwa nje ilibidi aende alikuwa Ni Henny.
"" Unae Shamy huko!? Mwambie atoke asituletee kesi hapa! Babake anamsubili."
Shamy nae alitoka nje baada ya kusikia Babake kaja. Janerose alimfuata Henny nakumuuliza;-
"" Kipi kinaendelea lakini!?"
"' Si Shamy! Huwa anampenda Brighton Ndo maana anang'ang'ania hapa muda wote! Mbaya zaidi Brighton nae kama vile hamuelewi!"
Janerose hakuwa na usemi teena alibaki akimtizama Shamy ambae alipita mbele yake.
""Sorry Daddy!! Niache kwa Leo nikae hapa ila kesho nitarudi nyumbani!"
Shamy aliongea nakumfanya Babake aanze kumtizama Brighton juu chini huku akimthaminisha na Binti yake, alimshika mkono Shamy huku akimpeleka kwenye gari yake.
Janerose alibaki amedata Huku akijiuliza amekuja kufanya kazi au Ni sehemu ya maigizo, mbaya zaidi hiyo ndio Siku ya kwanza tu tangu afike Mambo yamekuwa vururu vururu! Aliamua kujiondokea lakini Brighton alimuomba waonane kwanza.
Walitoka nje wakawa wamekaa Huku Kila mtu akiwa kimya, Brighton alikuwa amejiinamia muda wote Huku akifikilia kitu Cha kufanya baadae alinyanyua kichwa Huku akimtizama Janerose ambae muda huo alikuwa akitizama urefu wa Ghorofa ilokuwa karibu na pale, Kuna kitu alitaka azungumze lakini aliposikia Brighton anaongea aliishia kuita Bry! Huku na Brighton nae akimuita Janee!"
"" Wataka kusema Nini Janerose Make umeniita tu?."
"" Zungumza kwanza Wewe huenda nikizungumza utaishia kucheka kwanza...!!"
"" Basi sema kwanza ili nicheke hafu tumalizie kwa kilio.!"
"" Ni kuhusu Ghorofa lilivo refu make Tanzania hamna Kabisa!!!"
""" Hahaahaaa! Kweli umekaa kuwaza ujinga tu!"
"" Mhuu! Ni kweli lakini! Aya sema hivo vilio vyako tulie kwa pamoja! Make Mimi nimechekesha!"
"" Ni kuhusu huyu Shamy, kwa kitendo kilichotokea sa hii au tangu tufike hapa" Wewe unanichukuliaje kwanza!!?"
......Itaendelea......
Usikose sehemu ya 16.
Like, comments and suggestions 👍✍️🤝🙏❤️.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "16" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
"" Ni kuhusu huyu Shamy, kwa kitendo kilichotokea sa hii au tangu tufike hapa" Wewe unanichukuliaje kwanza!!?"
ENDELEA..
"" Kawaida tu!!"
"" Najua wanionea aibu kuzungumza, ila iko Hivi Huyu Binti tangu nije hapa amekuwa akining'ang'ania ati ananipenda lakini Mimi sivutiwi nae kabisa!!"
"" Lakini Bry si ni Mzungu yulee!!?"
""Mzungu Ndio, wamaanisha!!?"
''" Upendane nae."
'" Kumbe Wewe akiwa Mzungu ndio wataka nipendane nae!? Na vipi Kama nataka kupendana na Mtanzania mwenzangu nitakuwa na kosea? Au Wewe sahii wataka kupendana na Henny kwakuwa ni Mzungu?"
Janerose alijikuta akiangua kicheko, kilichomfanya Brighton Abaki kumshangaa na kumuona Kama kituko baadae Janerose alimjibu.
"" Daah! Nimecheka kwa sauti Hata sijui kipi nachekea! Ila naona kabisa Kuna watu relation zetu Hata hazijulikani huwa Ni relation zinazohusiana na Nini ama love relation, au relationship isiojulikana imeegamia wapi!?"
Brighton nae alibaki akimtizama Janerose kutokana na maneno yake Huku akifikilia hiki ndio kimemfanya acheke.
"" Mhuu! Kwahiyo hapa tunasaidianaje kwahilo!?"
"" Nakushauli tu Upendane nae! Sizani Kama anaweza kuja kukucheat make anakuwa kapenda kweli! Ani inafikia hatua natamani nimpate mtu atakae nipenda mpaka nimuonee kelo! Anitafute muda wote, aniliwaze, aniambie sorry baby, yaani namaanisha anipende kweli kweli."
"" Khaaa!! Humu kichwani kunae Mambo mengi kweli."
"" Ndo unikoe Sasa!?"
"" Yaani nimekuja kushare mawazo kwa mtu anaetaka kushare na yeye! Mimi ushauri wangu kwako.... fanya kazi Kwanza Kila Jambo Lina wakati wake! Ila ushauri wako kuhusu kupendana na Shamy hio Hapana Labda tupendane na Wewe Mimi nitatimiza Kila kitu ulichoongea hapa!!"
"" Mjinga Wewe! Kamwee swezi pendana na Wewe! Kumbe ulikuwa wanisikilizia tu."
'"' Leo tunaongea kimasiala ila Kuna Siku nitakuja live! Wewe kapumnzike nitakuona kesho."
Ilikuwa Ni Siku nyingine leo Janerose alikuwa akireport kwa mkuu wake wa kazi, Siku hiyo alikutana na meneja wake live! Alimsainisha mikataba ya kazi pamoja na kuelewana kiasi Cha mshahara na hapo ilikuwa Ni ofsini kwa meneja nje na Kampuni.
Kesho yake alipelekwa moja kwa moja kwenye Kampuni la DHB HEALTH organization. Lilikuwa Ni Kampuni kubwa lililojaa Kila aina ya wafanyakazi wazungu, kwa waafrica.
Majira ya jioni aliandaliwa Party ndogo ya kukalibishwa rasmi kwenye Kampuni! Brighton na Henny wao walimwandaliwa zawadi ndogo iliyomfanya Janerose awe na Furaha zaidi hasa kwa kwmpani yao.
Ilipita Kama Mwezi mzima Janerose alikuwa tayari amezoeana na baadhi ya wafanyakazi Na hii ni kutokana na yeye kuwa mcheshi Sana ilimpa urahisi kuzoeana nao,
Kati ya Siku hizo zote hakuweza kuonana na Brighton make Hata makazi yake alikuwa amepangwishiwa sehemu nyingine tofauti na alipofikia, Maisha ya Janerose yalizidi kuwa mazuri Hata mwili wake ulinawili na kumletea shape Furani ilioanza kuwachanganya wafanyakazi wenzake.
Vijana walianza kutuma maombi yao, Huku wakitumia maneno mazuri ya kumshawishi lakini Janerose aliwakatia mbali, kwaujumla aliamua kufokasi na kazi zaidi mpaka baadhi ya viongozi wake walianza kumpongeza kwa kupitia Brighton wakisema kweli kawaletea mchapa kazi mzuri.
Ilikuwa Ni Siku moja Brighton aliomba appointment ya kumtembelea Janerose kwake, baada ya muda mrefu kutokuonana! Janerose alifanya kumkalibisha vizuri Huku akimuandalia chochote kitu.
Brighton Kama kawaida muda wote huwa Ni mtu wakuzingatia muda kwahilo alijaaliwa, alifika kwa wakati kwa Janerose Huku akipokelewa vizuri sitori ziliendelea! Katika kupiga sitori za hapa na pale Brighton alionekana Kama kabadilika Sana! Hakuwa na ule utani utani wa hapa na pale. kitendo hiki kilimchanganya Sana Janerose alishidwa kuvumilia ilibidi amuulize;
"" Hivi Brighton! Kuna kitu kimetokea kwenye maisha Yako? Ninavyokujua na ninavyokuona kwa Sasa Ni tofauti Sana! Harafu naona umekuwa tofauti hata kunitafuta tu imekuwa changamoto.""
'"' Aah! Sorry lakini ndio maana nimekuja ila nilikuwa busy sana na kazi! Harafu nataka niache kazi!!"
"" Mhuu! Wewe!!?' kwanini Sasa? Kwani kumetokea Nini mpaka uache!?"
"" Daah! Ni makubwa!! Kwakuwa Wewe Ni mtu wangu wa karibu nitakwambia! Iko hivi; Kipindi Cha nyuma nilichukua mkopo kwenye Kampuni kwaajili ya kumuuguza mama yangu alikuwa Ni mgonjwa! Pesa nyingine nilifungua Dhahanati huko nyumbani kwetu nikawa nimemuweka ndugu yangu! Nikafungua akaunti ya Bank ili mauzo awe ananiwekea huko! Sasa sijui kashawishika na Nini Ani kaenda Bank kutoa pesa zote ni zaidi ya billion mbili! Na hapa nimejitahidi kumtafuta Kama wiki moja sijampata! Ani nachanganyikiwa Doctor."
"" Pole Sanaa! Kumbe una makubwa kiasi hiki yaani billion mbili zote? Harafu ndugu Yako? Kwahiyo Kuna watu umewaweka wakusaidie kumpata! Lakini hii sio sababu ya Wewe kuacha kazi! Wewe ndie umenifanya Mimi niingie kwenye hii Kampuni Kama utaacha na Mimi sitakuwa najiamini katika kazi Kila nikikumbuka Wewe haupo lazima nikose morali ya kazi! Au Kuna sababu gani mpaka uache kazi? Mimi naona hizo sababu ulizozitaja sizani Kama zinakufunga kufanya kazi!
"" Janeee! Huenda zisiwe sababu kubwa kwako! Ila ni kwaupande wa meneja wa Kampuni hawezi kukubali Mimi niwe natoka kufatilia Mambo yangu hafu kazini nisionekane! Kwaujumla kazi za kuajiliwa zinachosha nataka nikafanye kazi zangu."
Janerose alibaki kimya Huku Huzuni ikimshika aliwaza Kama Brighton ataacha kazi kwa yeye kuaminika pale inakuwa ngumu make kujulikana kwake ilikuwa Ni kupitia mgongo wa Brighton.
"" Vipi naona umewaza Sana! Ila kuhusu Wewe na kazi usijali, Henny atakuwa upande wako!"
"" Aaa! Sikubaliani na Wewe Brighton! Kama kutafuta hizo pesa na Mimi nitakusaidia! Nipe muda Kama Siku tatu nikaongee na meneja nimuelezee kwa kina naamini atakubali tu! Atakupa likizo ukafatile kazi yako itabaki pale pale! Labda Kama Wewe unataka kuacha kazi useme tu.''
"" Nataka kuachaa kazi!!"
Janerose aliamua kuondoka kwanza, nakuelekea nje make aliona Kama Brighton hamuelewi. Brighton aliamua kumfuata Kisha alisimama pembeni yake.
"" Ndio umechukia Hadi umenisusia kukaa na mie ndani!?"
"" Ukweli unaboa Sana! Naona Kama Sina jipya tenaa lakukushawishi!"
"" Basi nimeamua... Siachi kazi tenaa! Ila nitabaki kwaajili yako."
Janerose alibaki ameduwaa Huku asiamini kabisa.
"" Bry Ani unasemaa.....!?"
"" Nabaki kazini, Inamaana huamini?"
"" Ewaaaa!!!! Hapo ndio umekuwa Mkubwa. Huku akimkumbatia.
Brighton alimuachia Huku wakielekea ndani.
"" Kumbe huwa unanikubali ee!?"
"" Sio kivile Sasa..!"
"" Harafu hebu sogea hapa uone hii picha!"
Janerose alisogea Huku akitizama vizuri, lakini alishituka Huku akimtizama Brighton.
"" Ndio amekwambia anakuja wiki hii!?"
"" Eeh! Wanakuja semina ya wiki moja si huwa wasema Ni rafiki yako Denison? Kama Ni uongo nitajua tu."
"" Aah! Wewe nae... eti utajua tu!! Hata hivyo Ni Siku nyingi sijamuona Najikuta natamani Sana kumuona! Sa sijui atafurahi kuniona make aliondokaga kwa hasira Yule!!?"
"" Wewe!! Huku akimsitua.
" Ndio unazama kwenye fikira kiasi hichoo!! Sa' Unataka nikueleweje!?"
.... Itaendelea......
Usikose sehemu ya 17.
Like, comments and suggestions 👍✍️🤝🙏❤️.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "17" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
"" Wewe!!
Huku akimsitua.
" Ndio unazama kwenye fikira kiasi hichoo!! Sa' Unataka nikueleweje!?"
ENDELEA...
"" Nimewaza tu...!!''
"" Ni Kama unampenda Hivi!?"
"" Si kweli!!!''
Brighton aliamua kuondoka make Hata muda ulikuwa umeenda Sana! Janerose alifanya kumtoa kwa kumsindikiza.
Hatimae ile Siku iliyokusudiwa leo ilitimia! Maandalizi yalifanyika vizuri Siku hiyo make ilikuwa ikifanyikiwa kwenye kampuni la DHB HEALTH organization. Maandalizi yalienda vizuri ilikuwa Ni muda wakuwangojea Wageni! Brighton alikuwa amepangiwa kitengo kimoja na Janerose wao walikuwa kwenye kamati ya vinywaji.
Baada ya kupanga vizuri kamati yao walikaa pembeni Huku wakizungumza na Brighton.
"" Naona ulivyo na shauku ya kukutana na rafiki yako wa muda mrefu Karibuni anaingia hapa. Harafu unaona kule Wageni wameanza kufika."
Janerose alinyanyua uso wake akitizama lakini macho yake yalikutana na Henny akifika pale ilibidi wamsikilize.
"" Hii Ni Oder kutoka kwa Meneja Brighton na Janerose mtaingia kwenye semina! Kuna vitu vipya vya kujifunza!"
"" Heee! Tenaa?" Janerose alihoji.
"" Tuliza kichwaa! Hutaki kujifunza Wewe?. Brighton aliongea Huku akisimama.
"" Sa' Ndio waondoka kienyeji hivyo!?"
Janerose aliuliza huku akimwendea Brighton.
"" Wewe hujui kumbe!? Ani kwenye semina huwa Kuna posho nzuri! Harafu wanakula mle!?"
Janerose ilibidi acheke tu Huku akimvuta mkono.
"" Kwahiyo Furaha yote hiyo Ni Pamoja na msosi?"
Brighton alimgeukia Kisha aliunganisha mikono yake na Janerose.
"" Unavyozidi kunifuata utazani twaenda kujiandaa kwa Pamoja!?"
"" Sio eti, Basi ngoja nikajiandae."
"" Hapo sawaaa! Ila usijiachie Sana kwa rafiki Yako.
Wakati wakizidi kuongea Shamy alifika pale Huku akimwendea Brighton alifika nakumshika mkono akimtizama Brighton usoni, na mikono yake aliiachia huku akimkagua Brighton, Janerose alibaki akiwatizama tu.
"" Sorry Bry kwakuwa mbali na Wewe Baba alinifungia ndani! Ila leo kaniachia nihudhurie kwenye Semina harafu nimefurahi kusikia Hata Wewe utakuwepo!"
"" Basii!! Ila Babako akikuona bado upo na Mimi atakuadhibu tenaa! Ni vyema uwe mbali na Mimi kwasasa nisije leta matatizo!"
"" Don't fear Bry! But I no Ni kipi nimeplan! Harafu nimekuandalia breakfast kwa leo! Tafuta sehemu tukae kwanza."
Janerose aliamua kujiondokea make aliona Brighton hafurahishwi kabisa na hicho kitendo Cha Shumy kuwa pale. Ile anaondoka tu Shamy alimuita Huku akimsalimia.
"" Hey Janee! Are you okay!? Your welcome tujoin kwa pamoja kwa Meeting!"
"" Thanks Shamy! I hope tutakuwa wote!"
Janerose alielekea nyumbani kwake kujiandaa! Baadae alirudi nakuingia kwenye meeting aliandaa daftari lake pamoja na pen! Muda kidogo Aliingia Brighton akiwa na Henny pamoja na Shamy. Brighton alitafuta seat ya kukakaa Huku na Shamy nae alikaa karibu yake! Kwa Henny aliamua kukakaa karibu na Janerose.
"" Vipi mbona unacheka Janee!?"
"" Nafurahi tu jinsi Brighton alivyogandwa na Shamy Ani naenjoy! Harafu kumbe Shamy nae ni mtaalamu wa afya?"
"" Ndio! Na yupo vizuri Sana hasa kwenye Operation sema Ni mapepe yake tu! Sema Brighton naona Kama anakuelewa Wewe ndio maana anamuona Kama Shamy Ni mzigo kwake!"
"" Hapana!! Ananichukulia Kama rafiki yake tu!"
"" Kwani hajawahi kukwambia kuwa anakuelewa? Au Wewe wazani Kila mwanaume anapenda kuwa rafiki tu?
'" Mhuu! Sijajua make huwa anakuwa na maneno mengi ya kuongea sijui Hata huwa anamaanisha Nini!?"
"" Shauri yako! kumbe ujumbe ushakufikia Ila unaweka ngumu!! Harafu nitakutafuta baadae nikueleweshe naona Wageni hao."
Janerose aliinua kichwa hakuamini kumuona Denison yupo miongoni mwa wageni wanaoingia, Mbona alidata nakubaki akimtizama Denison jinsi muonekano wake ulikuwa ukivutia japo alikuwa amevaa kofia kichwani alijitahidi kumchungulia ili amjue zaidi, Kuna furaha ilimvaa mwilini mwake ikapelekea mpaka mwili wake kumsisimka nakubaki akitabasamu ovyoo! Huku akiongea pekee.
"" I hope nimpate Huyu mwanaume ifeel nitakuwa in love kwake! My Dream zitakuwa tamati if nikimpata tenaa!!?'
Muda huo Brighton alikuwa akimtizama kwa jicho la wizi wizi aliona kabisa Janerose kuchanganyikiwa aliamua kumtumia message.
"" Are you here!? I see unavyo mu enthous this man!""
Janerose alifungua ujumbe akawa ameusoma Huku akibakia kucheka aliamua na yeye kumchallange.
"" I'm here! Vipi Wewe na Shamy kwa hio position!?"
Brighton ilibidi akae kimya Alimtizama Shamy muda huo alikuwa ameegamia begani kwake Huku akijifanya yupo busy kusikiliza kinachoongelewa mbele, aliamua kumuacha tu.
Huku semina iliendelea make wenzetu wanajua kwenda na muda, baada ya maada kuisha kulikuwa Kuna maswali yakuuliza! Shamy alionekana kuwa vizuri Sana kwa majibu! Mwishoni kabisa Mkufunzi wao aliuliza swali akampoint Janerose ajibu make swali lilimhusu yeye! Janerose nae alikuwa vizuri Sana kwa upande wake make kujiunga na lile kampuni haikuwa Hivi Hivi tu, mpaka waangalie ufaulu wako Huku vigezo na masharti kuzingatiwa.
Baada ya maswali kuisha ilikuwa Ni muda wa mapumnziko Kila mtu alitoka nje kupunga upepo! Janerose alibaki akimtizama Denison huenda angemtafuta wakasalimiana lakini haikuwa hivyo yeye alibaki busy akiongea na Ma daktari wakubwa katika kampuni yao. Baadae kabisa alimuona kasimama na Shamy wakiongea walionekana Ni Kama wanafahamiana kwa ile ongea yao Hii ikamchanganya pia.
Walikusanyika wote tenaa kwaajili ya lunch! Make chakula kiliandaliwa pale, kwa bahati nzuri katika kukaa walichangamana lakini kwa Denison alikuwa Badoo yupo nje Aliingia nakukuta kalibia seat zote zimejaa. Doctor mwenyeji alitoa kiti chake Huku akiangalia meza ambayo Haina watu Sana ambapo anaweza kuweka chakula Cha mtu mmoja kikaenea pale.
Alielekezea kiti chake mezani kwa Janerose huku akimkalibisha Denison aketi, Janerose yeye alikuwa akiangalia chini chini Hata alipomuona Denison kakae pale alijitahidi kubalance shoobo na kuwa busy kumtenganisha samaki kwa mikono yake ilimradi aingie kinywani.
Denison alikuwa akimtizama kwa kuibia ibia mwisho kabisa alimuuliza kwa sauti ya chini kabisa.
"" Hujaacha tu kupenda samaki!?"
Janerose alisita kidogo nakubaki amekalisha kijiko mdomoni! Kana kwamba hajasikia vizuri.
"" Wewe kula upungue kwanza! Naona umenenepa!?"
Ilibidi ashushe kijiko chake chini Huku akipaliwa na punje za wali kadhaa nakumfanya akohoe bila kupenda. Denison aliwahi nakumpatia maji kwenye Glass apate kunywa.
"" Pole rafiki! Jikaze basii mwishoe wasema nakusemesha Sana mpaka umepaliwa."
Baada ya kunywa maji kikohozi Cha kupaliwa kilikata nakubaki kakaa kimya Huku akiwatizama watu Kama bado wanamwangalia, alipojilizisha wapo busy na kula alibaki akichekea moyoni Huku akimtizama Denison kwa kuibia ibia.
"" Kumbe bado ananikumbuka kuwa mie Ni rafiki yake! Inamaana hajasahau chochote kunihusu Mimi! Harafu inakuwaje unaniambia Nile harafu nipungue au alisema kinyume chake kuwa nipunguze kula nimenenepa?"
..... Itaendelea......
Usikose sehemu ya 18.
Like, comments and suggestions 👍✍️🤝🙏❤️.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "18" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Baada ya kunywa maji kikohozi Cha kupaliwa kilikata nakubaki kakaa kimya Huku akiwatizama watu Kama bado wanamwangalia, alipojilizisha wapo busy na kula alibaki akichekea moyoni Huku akimtizama Denison kwa kuibia ibia.
"" Kumbe bado ananikumbuka kuwa mie Ni rafiki yake! Inamaana hajasahau chochote kunihusu Mimi! Harafu inakuwaje unaniambia Nile harafu nipungue au alisema kinyume chake kuwa nipunguze kula nimenenepa?"
ENDELEA....
"" Wewe zinduka ndotoni! Ndo wasahau Hadi kula? Harafu Mbona husemi na Mimi?"
"" Ni vile unanichukia!!"
"" Wewe ndo unaniwazia hivyoo kumbe!?"
Muda wa kula uliisha waliendelea na semina tena, mnamo majira ya jioni semina ilimalizika wafanyakazi wote walitawanyika makundi makundi Huku wakibadilishana mawazo.
Janerose hakuona hata maana yakuendelea kujizungusha pale! Baada ya kumuona Denison yupo busy na Shamy aliamua kujiondokea. Brighton alimfuata angalau waongee nae.
"" Ndo unaondoka kimya kimya naona Ni vile unae wivu kwa Denison! Sema tukueleweshe kuhusu Shamy!"
"" Hayanihusu Jamanii! Kwani Mimi nimesema kitu?."
Muda huo simu ya Brighton iliita alipokea nakuisikilizia, baadae alimuwekea simu Janerose sikioni.
"" Nitachukua namba yako kwa Brighton!"
Janerose aliitikia Huku akiondoka! Alifika nyumbani kwake nakukaa kwanza Huku akifikilia.
"" Ina maana Denison hakuwa na namba yangu muda wote huo Hadi aichukue kwa Brighton!?"
Muda kidogo simu yake iliita ilikuwa Ni namba ngeni alipokea nakusikilizia.
'"' Madaam Janerose! Mi Denison! Naomba tupate chakula Cha usiku kwa pamoja!"
'" Siko vizuri najisikia kuumwa!"
"" Basi nataka nije nikusalimie, nipe location, au Sahii unae mme?"
"" Wewe njoo bhanaa!!" Kuna mtu namuagiza aje akuchukue!"
"" Powa! Ila nitakuletea chakula!!"
Muda si mrefu Denison alifika Hadi nyumbani kwa Janerose alibisha hodi akawa amekalibishwa moja kwa moja Hadi sebuleni, muda huo Janerose alivunga Busy kuandaa juice kwa blender.
Denison alikaa karibu Kisha alimshika mkono na kumzuia asiendelee kusaga Juice.
"" Unaumwa tena tumbo?" Huku akimwangalia usoni.
"" Ndivyo ulivyonizoea!!?"
"" Kawaida yako ila nilijua ushapona!"
"" Badoo!"
"" Magonjwa ya wanawake hayo!"
"" Ayaaa! Umeniletea Nini kwanza!?"
"" Nilisikia Siku hizi hushibi chakula Cha huku! Kuna sehemu huwa wanatengeneza chakula Cha kitanzania nikiendelea kukaa huku nitakupeleka ukapaone! Ila umenenepa.
"" Ninenepe mi Ng'ombe kwani!? Huku akicheka.
Aliuchukua mfuko alokuja nao Denison Kisha alifungua nakutoa hot pot ndogo, alifungua nakukuta supu ya kuku ikiwa ya Moto, Muda huo Denison alikuwa akimtizama tu jinsi anavyofunua. Janerose alikuwa yupo Busy Sana alikuja kuinua kichwa nakukuta Isha nae akimwagilia mpaka akaona aibu.
Denison alipiga jicho nakuona Kuna kabati ya vyombo alichukua Bakuri na kijiko Kisha alimimina ile supu, alichukua Bakuri nakumsogelea karibu akitaka kumnywesha. Janerose aliona aibu na kumshusha mkono.
"" Hapana nitafanya Mimi pekee!"
"" Come down! Wewe si waumwa!? Nikikuangalia Sana Nakumbuka nyakati Zile Mambo mengi mazuri tulifanya! Nilitamani kufanya zaidi lakini muda ndio ulinitupa mkono! Nilimisi kampani yako japo nilikuja Tanzania nikatoka nimekuchukia kumbe nilikosea Sana kwani nilishidwa hata kuvumila kwanini sura yako sikuitia machoni kwa muda ule! Nliambiwa kuhusu Wewe kurudiana na Shamsi hii iliniuma Sana mpaka nilipopata taarifa zako unaenda USA kufanya kwazi Hutaamini moyo wangu ulijawa furaha, daima nilijiona Ni mshindi katika Ndoto zangu japo Mwanzoni tuliishi Kama marafiki ila Mimi nilikuwa napata picha tu wapenzi, huenda hata Wewe unajua tuliishi vile ila leo nataka kukwambia kwasasa Ni zaidi ya marafiki! Itoshe kusema Janerose Nakupenda Sana, nipo tayari kuunganisha familia zetu kwa pamoja ziwe familia moja Kama utaniunga mkono kwa hili.
Denison alimaliza kuongea! Muda huo hata supu ilikuwa imeisha, alimuachia Janerose na yeye azungumze kitu lakini muda huo alikuwa akiendelea kumuonea aibu. Denison ilibidi amuache kwanza Huku akiulizia uwani.
Janerose alimuelekeza akawa amerudi sebuleni Huku akitoa vyombo mezani, alianza kukumbukia hiyo ayaa iliyoshushwa na Denison alihisi hata tumbo lake kupona! Alianza kutafuta kitu chakuzugia Huku akitafuta channel angalau yenye michezo make akiweka sehemu yenye Tamthiliya ilionesha kinachoongelewa Ni kilekile alichoongea Denison hii ikamnyima kujiamini.
Muda huo Denison alifika Kisha alichukua ile remote nakurudisha kwenye Tamthiliya Kisha alimpatia Remote Janerose Kama atataka kuitoa Ni yeye Sasa.
"" Vipi mbona waniogopa hivyoo!? Harafu kwanini ulimzuia Sharifu asiniambie Kama unaniulizia kwake!?"
"" Niliogopa kwasababu Siku yenyewe umekuja! Hussein na Sharifu walipotaka kunipigia ili niongee na Wewe uliwazuia!"
"" Ni hicho tu! Au Kuna kingine?"
"" Tangu uende kule hukuwahi kunitafuta, hata kuniulizia tu napo hukutaka, Niliwaza hata urafiki wangu kwako ulikuwa hufurahishwi nao ndio maana yote haya yalitokea.""
"" Basii!! Lakini si rafiki zako walikwambia kilichotokea! Haikuwa matakwa yangu ila samahani kwa yaliyotokea, na pia nisamehe kwa kukuchukulia vibaya Siku yenyewe nimekuja Tanzania huenda nilikuwa nikiwuiwa na wivu mkali juu yako! Ila now I'm happy nimepata kitu nilichowekea matumaini nacho kwa Ndoto zangu."
Janerose alibaki akifurahia tu, alitamani hata amwambie na yeye kuwa anampenda Sana! Lakini mdomo ulikuwa mzito ila Ishara ndio zilionesha kuwa Binti kazama, Denison aliamua kumsogeza kifuani kwake akawa ameegamia Huku akimchezea Nywele zake.
"" Vipi lakini umenisamehe make nategemea nisikie angalau neno moja litoke kwako!!"
"" Hukunikosea ila nilikumisi Sanaa! Kwa muda ulionitenga mbali na Wewe, kweli nimekutana na changamoto nyingi Sana! Ila kwakuwa nimekupata naimani nitakaa sawa! Nauchukia ule wakati wa nyuma nilivyootaabika na Shamsi huenda Ni kwakutokuwa na maamuzi sahihi ila kwasasa nimeamua kuwa na Wewe hata Mimi Nakupenda Sana.
"" Nami nitatimiza Ndoto Yako! Na nitazidi kuwa mwaminifu kwako, mapungufu yaku, udhaifu wangu naomba unilindie! Harafu vipi kuhusu Brighton hakusumbui?"
"" Hapana Ni rafiki yangu tu, sema yeye anae Shamy! Japo naona Kama hawaelewani."
"" Ni kwasababu yako Najua! Shamy kanieleza Mambo mengi kuhusu Wewe na Brighton! Mara ndie kakuunganishia kazi, huwa anakuja kwako kukusalimia! Na out nyingi huwa mwatoka, ila kwasasa mumiliki harali amerudi Yule Ni rafiki yangu nampenda pia twaheshimiana, Ni mtu spesho kwangu hata kwenye maisha yangu alipigania uhai wangu mpaka Sasa naishi! Ila nataka heshima iwepo japo sikukatazi kuzungumza nae.
Denison aliweka kituo Huku akibaki kumtizama Janerose make kijasho chembamba kilimpitia, hasa akikumbuka ujio wa Brighton Siku ile, ndio picha ikaja moja kwa moja Brighton huwa anampenda alikumbuka hata maneno ya Henny ajiongeze bado alimuomba Siku moja waongee. Ilibidi ainuke hata miguuni kwa Denison make hamtendei haki kabisa.
'"' Please Janerose!! "Unaenda wapi? Naomba leo ukae karibu yangu nibaki nakutizama jinsi ulivyozidi kuwa mrembo! Ni muda mrefu sura hii ilitoweka machoni kwangu ila leo nataka nikae nayo karibu kwa muda nitakaokuwa huku nataka nikufaidi.
..... Itaendelea......
Usikose sehemu ya 19.
Like, comments and suggestions 👍✍️🤝🙏❤️.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "19" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
'"' Please Janerose!! "Unaenda wapi? Naomba leo ukae karibu yangu nibaki nakutizama jinsi ulivyozidi kuwa mrembo! Ni muda mrefu sura hii ilitoweka machoni kwangu ila leo nataka nikae nayo karibu kwa muda nitakaokuwa huku nataka nikufaidi.
ENDELEA...
"" Nakuja Mara moja!!"
Denison alibaki akimtizama mpaka anaishilia, moyo wake ulizidi kufarijika Sana, baadae Janerose alirudi akawa amekaa.
"" Vipi bado unaniogopa tu!? Huku akizidi kumtizama.
"" Sikuogopi hataa!!!"
"" Basi funga machoo Kuna suprise Yako."
Janerose alifanya vile, Denison akamshushia kiss kwenye paji la uso! Huku akiongea nae.
"" Vipi utaniimbia tena Kama awali ulivyokuwa ukiimba!?"
Alibaki kucheka tu, make Ni muda mrefu tangu achanganywe na stress za mapenzi hata mood ya kuimba iliishaga.
"" Sizani Kama naweza kwasasa! Ni muda mrefu imekuwa sijafanya vile!""
"" Unaweza bhana! Hebu jaribu.
'" Utanicheka...!"
"" Basii Mimi nimemisi kucheza na Wewe!"
"" Fanyaa...!"
"" Mwenyewe hapana! ( Huku akimnyoshea mkono asimame ).
Waliweka Nyimbo za Zero distance Huku wakizidi kucheza kwa hisia, baadhi ya kumbukumbu za nyuma zilianza kuwaijia Kila wakikumbuka ukaribu wao jinsi ulivyoanza mpaka kufikia pale, Kwa Janerose muda mwingi alikuwa akikumbuka maisha ya nyuma alivyohangaika kwenye mahusiano! Hakuamini kabisa Kama kwenye mahusiano Kuna Siku na yeye atapata muda wakufurahia mapenzi yake alibaki akitabasamu Kila Mara anapozidi kumuona Denison mbele yake feeling zake zilizidi kwenda mbali, hata upande wa Denison nae Akili yake aliielekeza kwa Janerose ikawa miili yao na nafsi zao zinasemezana kwa pamoja.
Siku zote unaambiwa Mapenzi Ni furaha pale unapompata mtu wakuendana nae Akili pamoja fikra ziwe kwake huku zikibwebwa na kitu kinachoitwa hisia! Hisia zitakuongoza pale unapomuona au mnapokaribiana na mwenzako Kuna hisia unazipata ( stimulation). Japo wengi hawajapata chaguo sahihi wamebaki kulaani na kutowa lawama kuhusu wenzi wao na hii Ni kwasababu ya kutopata mtu wakuendana nae! Zaidi muombe Mungu akupe mtu wa kuendana nae naamini utaenjoy hata hizo sababu za kumuona mwenzako kasoro hizi zitaisha.
Siku hiyo upande wa Janerose na Denison ilikuwa Ni Siku Yao nzuri! Hata kulipopambazuka walijiandaa na kuelekea wote kazini japo walienda kwa kutangulizana kuhofia maneno ya hapa na pale kwa upande wa kazi Ni fedheha mbaya.
Janerose alifika nakuendelea na Majukumu yake! Aliienda Kuwaangalia wagonjwa Huku akisubili muda wa semina! Baada ya kukamilisha kuona wagonjwa Aliingia kwenye semina Huku akiendelea kuwasubili wenzie watimie waendelee na semina.
Upande wa Denison muda wote alikuwa akiitizama chombo yake jinsi inavyo present inapoulizwa swali alibakia kutabasamu tu, aliona asiishie kushare furaha peke yake aliamua kumtumia message.
"" Doctor wa viwango! Hiyo kichwa yako umemeza matirio!?"
Janerose alifungua ile message nakubaki akicheka kwanza alimtumia Emoji za kushangaa na kucheka! Baadae alimalizia kuandika.
"" Nitazima simu naona Unanichanganya!"
""Basii!!! Nimeacha... Ayaa tega sikio kwa makini ukishidwa kuelewa note sehemu nitakufundisha nyumbani.''
"" Niache bhanaa!"
Baadae kipindi kuisha ilibidi wakapumnzike kwanza. Siku hiyo Brighton aliamua kumfuata Janerose baada ya kumuona kakaa peke yake kwenye Garden.
'" Vipi nikae!? Au ndio rafiki kaweka order Hapa!?"
"" Bila kunitania huwa hujisikii kabisaa!
"" Kweli Ati, si Ni rafiki ndio."
"" Leta stori Achana na hio maada kwanza!
Brighton alisogea akawa amechukua kitabu chake, Kuna topic alifungua na kumpatia Janerose.
"" Naomba leo tukiingia kwenye semina ulizia kuhusu hii topic Kuna magonjwa huwa tunakutana nayo Ni vigumu hata kuelezea yanaambukizwa vipi!?"
Janerose alikuwa akizidi kupekua kurasa baada ya kurasa baada ya kumaliza alichukua pen akawa amenote baadhi ya maswali Huku akingoja waingie kwenye semina.
Baada ya kumaliza kunote, sitori baina yake na Brighton ziliendelea japo Denison alimpiga biti kuhusu mazoea kwa hilo lilikuwa gumu kumuepuka make Brighton Ni mcheshi kwake na muda mwingine humfanya awe na furaha bado Ni mwenyeji wake katika kampuni.
Wakati sitori zao zikizidi kuendelea Brighton alimsitua nakumuonesha upande wa pili, Alikuwa Ni Denison yupo na Shamy wakipiga picha! Si unawajua wenzetu na vinguo vyao hata kujali hawajali wapo kizungu zungu hata zile picha zilizopigwa Ni za kizungu tupu.
Janerose hakuamini kwanza moyo wake ulilaruka! Nakubaki ameshikilia tumbo lake kwa maumivu! Japo alionesha kujikaza kwa Brighton asijue Kama anaumia lakini Brighton alimgundua baada ya kubadilisha hata maongezi Yao yakawa ya mkato! Ilibidi amhoji.
"" Janeee! Na Wewe unamuonea wivu rafiki?"
Janerose alishidwa hata kujibu! Alibeba begi lake nakuingia class akisubili muda wa kipindi kianze! Baada ya kumaliza kipindi alijiondokea mapema kuelekea kwake.
"" Hapana!! Hii too much imekuwa! Shamy Ni Nani kwako mbona ipo kwa position hiyo! Kama Ni rafiki tu ndio muwe karibu kiasi hicho? Mbona Ni Jana tu nilikuwa na furaha leo hii tu nishaanza kuikosa furaha!?"
Alamua kuchukua simu yake na kumpigia Hussein, akamwelezea yote kuhusu ukaribu wa Denison na Shamy! Majibu aliyoyapata kwa Hussein hakuyapenda kabisa kwani alimjibu, " mbona Mimi na Wewe tu marafiki tu! Kwa mtu asiyejua kuhusu hilo lazima afikilie tofauti Ni Kama Reysious anavyokuwa akikuchukulia wewe kingine chunguza kwanza au ampigie Sharifu akupe majibu make Ni watu wa karibu.
Alimnyokea simu Sharifu akamuelezea yote majibu aliyoyapata kwa Sharifu Ni;
"" Kweli sahii ushapenda kima ukwelii, ila punguza wivu! Shamy Ni rafiki yake wamesoma nae Chuo! Pia huyo Shamy alikuwa akitoka na rafiki yake na Denison! Sema walikuja kutenganishwa chuo, Babake na Shamy alimhamishia shule tofauti kutokana na umbali harafu mchumba wake alikuwa na maisha Duni ikawa ngumu kuonana! Ila Najua mpaka Sasa huwa anamtafuta japo hata kwenye simu hakupatikana! Ila nilisikia Kama ameanza kumsahau kapata mkaka wa Huku Tanzania ndio kitu alichoniambia Denison! Kwahiyo Wewe jiamini maama."
Janerose baada ya kujilizisha na majibu ya Sharifu alikata simu huku akichukua Grass ya maji akishushia alibaki akimtizama Shamy katika kumbukumbu Huku akimuonea huruma sana! Alichukua kitabu chake pamoja na daftari lake alivuta kalamu iliyokuwa mezani Kisha aliandika neno
"" Because of LOVE DISTANCE" isingekuwa hili neno haya yote yasingetokea, Mwanzoni nilikuwa na kijana kabla ya kuwa na Shamsi aliniacha kwasababu ya kuwa mbali nae! Alishidwa kuniamini matokeo yake akatafuta mtu mwingine nikaachwa vibaya, Mbaya zaidi nikaja kumpata Shamsi yeye ndio Alijua kunivuruga alianza kuchukua wadada ovyo harafu ananijibu kwa dharau eti Mimi nitaishije wakati Wewe umbali na Mimi, akaona arudiane na huyo mwalimu wake kisa wapo sehemu moja kikazi, akaona haisitoshi akaja kumchukua rafiki yangu,
Baada ya kuchoshwa na tabia zake nikaamua kuaachana nae lakini aliona aje kuniadhibu mbele yangu, haikutosha tu akaendelea kunifatilia Kila Hatua mpaka nilipoamua kuwa na Denison.
Nikaangia nae kwa mahusiano kwa muda mchache nikamzoea na yeye tena wakamhamisha! Ikawa Ni love Distance again, na yeye alikuja kunisahau tena japo yeye Ni kwaajali, bado katika kuhangaika nimekuja kujuana na Brighton tenaa vipi Kama miaka ingezidi pasina kumuona Denison huenda ingekuwa tumepotezana tena.
Ninachojifunza kumbe sio kwangu tu, Mwangalie Shamy Ni mrembo anavutia nae alikuwa na mchumba wake wamepotezana kimazingira, kamtafuta hampati mwishoe amechoka ameamua kumganda Brighton na hii imesababishwa na love Distance! Ndio maana mtu hushidwa kumuamini mtu nakupelekea kuchukua maamuzi yake mwenyewe kisa umbali wa mahusiano.
Haya Ni baadhi ya maneno aliyokuwa akiyaongea Janerose kwa kuyaandika na kuyarudia kisha kuyakoleza Huku akibubujikwa na machozi.
.... Itaendelea....
Usikose sehemu ya 20.
Nini hatima ya mkasa huu! Usikose kufatilia mwanzo Hadi mwisho wa Simulizi hii.
Like comments and suggestions 👍✍️🤝🙏❤️.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "20" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Haya Ni baadhi ya maneno aliyokuwa akiyaongea Janerose kwa kuyaandika na kuyarudia kisha kuyakoleza Huku akibubujikwa na machozi.
ENDELEA.....
Muda huo Denison alikuwa akija na hii Ni baada ya kuongea na Brighton akamuelezea jinsi Janerose alivyojisikia akimuona na Shamy! Baada ya kufika alipitiliza Hadi sebuleni na kumkuta Janerose Kuna karatasi alikuwa akiisoma alinyanyua kichwa chake ili atizame aliishia kusoma.. "" Because of love Distance"
Alimtizama Janerose ambae macho yake yalikuwa mekundu Ishara alikuwa akilia, alimsogelea nakumkumbatia kwa dakika kadhaa Kisha alimuuliza.
'"' Hii Ni kwasababu ya love Distance tu! Au Kuna kingine?"
Alishidwa Hata kumjibu nakubaki akiongeza Kasi ya kulia.
"" Basi nisamehe kwakuweka mbali na Mimi kwa mda mrefu ila nimerudi kwaajili yako tenaa! Natamani nikufanye uwe na furaha muda wote, Najua vile unavyojisikia Ila niamini Mimi! Kama unaona nakuumiza kuhusu Shamy! Yule Ni rafiki yangu upande mwingine Ni shemeji yangu! Hata nae anapitia situation hii muda mwingine najaribu kumfanya awe na furaha! Naomba uniamini Janee!' hakuna mwanamke ninae hisia kwake zaidi yako, isitoshe kusema "Nakupenda sana' Harafu sipendi kukuona unakuwa unalia muda wote nitashidwa kuyalipa machozi yako na upande mwingine utanifanya nilie pia.
Denison alimwachia toka kwenye kumbatio nakubaki akimtizama baadae alicheka tu, baada ya kumuona Janerose anatabasamu kwa mbali Huku akimuonea aibu.
"" Nafurahi unavyocheka kwa aibu! Harafu unapendezea ukiendelea kunionea aibu make hutakuwa na ujasiri wakunipinga nikitaka kitu!"
"" Wewe jaribu tuone! Sikuogopi sema nakuheshimu tu."
Alimtizama huku akishika vidole."" Mbona una vidole vyembamba hivi! Ani havina supu ila sema huwa unapenda kutunza kucha zako Ni Safi kweli! Ila sizani Kama tutapata Pete ya kutoshea hivi vidole."
"" Tutachongesha kwa Sonara! Au una jingine?"
Denison Alicheka Huku akizidi kubinya vile vidole, Kisha alijilaza miguuni kwa Janerose akimtizama vizuri usoni.
"" Ani huwa napenda ngozi nyeupe! Mie mweusi harafu nioe mwanamke mweusi hiyo Hapana! Ila tumefanana Kila kitu!"
"" Ushaanza Uongo hapo kwenye kufanana Kila kitu umenipiga! Ila sahii umekua hadi vindevu vimekuota!"
"" Harafu si vinanipendezea!! Denison alidakia.
"" Mhu mhu! Havina Ushirikiano."
"" Wivu huo, si Wewe kipindi Cha nyuma ulikuwa ukinisifia eti unapenda mwanaume mwenye ndevu fupi, Mara kimzuzu Cha wastani! Ayaa ninavyo sa wataka mwanaume yupi tena!?"
"" Mnene awe na tumbo!!"
"" Mjinga Wewe! Eti nataka mwanaume mrefu mwembamba, kapanda hewani harafu awe mweusi, nyie wanawake nyie mna mibaraa!"
"" Basii!! Inua kichwa chako Mimi niingie Jikoni."
"" Tutaandaa wotee!!"
Janerose alibaki akimtizama Denison Huku akicheka make alitangulia Jikoni, wakaanza kuandaa kwa pamoja huku wakizidi kuelekezana, Chakula kilipoiva walijumuika mezani nakuanza kutumia.
Nje kidogo na kazini, kunako Hotel kubwa kulionekana Kuna viongozi wakubwa wa kampuni wameketi Huku wakijadili kuhusu ujio mtoto wa Bosi nchini Marekani. Kikao hicho kilikuwa Ni faragha pasina kumshilikisha kiongozi wao! Hoja zilikuwa zikiongelewa Ni kuhusu kumilikisha kampuni.
"" Hapa inatakiwa tuanze kuandaa mikataba yetu mapema kabla Chris hajafika hapa! Kiongozi wetu anaelekea kustaafu, uzee umemvaa tayari na hapa lazima amrithishe kijana wake! Hii lazima tuipinge make kijana wake atakuwa akitubania Sana! Najua atakuja na usomi somi wake lazima atuangamize!"
Mzee mmoja aliongea, kwa upande wa kampuni alikuwa Kama mhasibu.
"" Hapo sawa nakuunga mkono!! Kila pesa itakayoingia kwenye kampuni lazima iandikwe! Na Huyu kijana akifika Mara tu baada ya kuanza kazi lazima tumfatilie. Mhazini aliongea.
Baada ya kumaliza kujadili kikao kiliisha, lakini muda huo huo Brighton alikuwa akiingia kwenye hiyo hotel akiwa na Henny! Wakawa wamefanikiwa kuwaona ila bahati mbaya Mazungumzo Yao hawakuyasikia.
"" Brighton! Yule si Mhasibu wa kampuni! Kwanini wapo hapa na wale watu wake wa karibu!?"
"" Itakuwa wanakula bata! Si mshahara umetoka majuzi tu!""
"" Nahisi Kuna kitu! Mara nyingi bata zao hufanyia hotel zenye changanyikeni hapa Ni Kama spesho issue! Harafu nimekumbuka hivi kumbe Doctor Janerose na Denison Ni wapenzi na inasemekana Brighton unajua ila sikuelewi kwanini ulianza kumpenda Yule Binti?"
'" Aaah! Henny! Kupenda Ni kupenda tu! Kwani kunachagua Basi Kama Yule pale Ni mtu ya mtu, au Ni mke wa jamaa!? Hii inakuja tu, sema ukweli nilianza kuvutia na Janerose baada ya kuonana nae Tanzania na nilichokipenda kwake Ni ile careling tu! Hafu havungi pia Ni mcheshi yaani mtu wa watu."
Henny ilibidi acheke tu Huku akimuegamia begani.
"" Kwahiyo hapo unaugumia maumivu ukiwaona wapo pamoja?
"" Inategemeana hata hivyo!"
""Wakati kazi ndogo tu leo nataka kukufanyia suprise naomba ujifunze kumpenda mtu anayekupenda!"
"" Acha zako Wewe utaniambia Nini wakati hapo huna msichana wakupoteza nae muda!"
"" Wewe tulia leo ni suprise hivi husitukii why tumependeza hivi, ngoja nipokee simu kwanza nakurudia."
"" Utazani simu ya maaana!!' hupaswi kuaga hata hivyo!"
Brighton aliamua aagize kinywaji angalau achangamshe kichwa. Kama dakika kumi zilipita Henny alikuwa bado hajarudi! Brighton aliamua kumpigia simu wakati simu yake ikiendelea kuita alishangaa mlangoni kumuona Henny anaingia akiwa na wadada wawili, alikaa vizuri Huku akiwatizama.
"" Yule si Shamy! Au macho yangu hayaoni vizuri!?"
Henny alisogeza viti viwili katika meza Kisha aliwakalibisha wageni wake, Kama kawaida Brighton alivyomzoea Shamy muda wote huwa anamshobokea kwa kumkumbatia lakini Siku hiyo ilikuwa tofauti sana! Alikuwa ametulia tu Huku akiwa busy na simu ilibidi amsemeshe.
"" Shamy! Are you here?"
"" Yaaah!"
"" Alimtizama kwa Yale majibu akaamua kukaa kimya."
"" Mbona unamuuliza hivyo wazani yupo wapi?"
"" Ni tofauti na nilivyomzoea!!"
"" Unaishi kwa kukalili Sana!"
"" Nitambulishe kwanza! Naona unarukaruka!"
Henny Alimtizama Binti aliyekuwa karibu yake Kisha alinyanyua mkono wake na kuuweka begani Huku akimtizama Binti huyo Kisha alimtambulisha.
"" Brighton, Shamy!' Huyu ndie mke wangu mtarajiwa anaitwa Minnah Siku za usoni tunaenda kuwa wanandoa! Mara nyingi umekuwa ukijiuliza huenda mi sinae mwanamke ila leo ndio utajua ninae, yeye anaishi Nairobi japo familia yake ipo hapa ila huko yupo kikazi! Kachukua likizo ya kuja kuwaona ndugu zake! Sa' sijui na Mimi nikiwemo au laah! Au ajibu...!"
Minnah alibaki kucheka Huku akimtizama Henny.
"" Because of you!" Kisha alitulia nakuanza kumtizama Shamy.
Shamy nae alimuona jinsi anavyomtizama kama ana kitu anataka kusema, baadae Minnah alimshika mkono na kuzungumza nae.
"" Mnapendezea kuwa wawili hasua! Kweli mmependeza."
Kitendo hicho kilimshangaza Brighton Minnah kaongea vile kumaanisha Nini, harafu kumbe anaongea kiswahili.
"" Ooh! Usijali Shemeji yangu Shamy Ni rafiki yangu wa karibu harafu Ni niii.."
Kabla hajamalizia kuongea make alitaka kusema Ni mfanyakazi mwenzake lakini Minnah alimuwahi.
"" Means Mchumba wako!! Ni mrembo Sana! Harafu kapata ngozi adimu hii!"
Upande wa Henny alibaki akicheka Moyoni make alitaka Brighton awe na Shamy, mtoto wa watu anateseka kwaajili yake.
Muda huo Minnah alisimama kuaga Huku na Henny akisimama.
"" Shem ngoja tuwaache kidogo! Ngoja nimchukue huyu jamaa Kuna sehemu twataka kufika! Kuna sehemu nataka tuzunguke make muda mrefu hatujafika! " Shamy Byee!"
Shamy alimpungia mkono Huku akimtizama Brighton make alikuwa akimtizama kwa kuibia ibia.
..... Itaendelea.......
Usikose sehemu ya 21.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "21" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Shamy alimpungia mkono Huku akimtizama Brighton make alikuwa akimtizama kwa kuibia ibia.
ENDELEA...
Ukimya ulitawala pale Kila mtu alikuwa busy akiendelea kunywa, Brighton ilibidi ashushe Grass yake chini huku akimtizama Shamy.
"" Ndo mlipanga hivyo na wenzako?"
"" Niambie live Kama hunitaki Kabisaa nijue! Nimekuja kufata Mapenzi yangu na si kwaajili yao."
"" Wewe Shamy!" "Mbona hivyo Babako atanifunga Mimi! Nategemewa na wazazi wangu ujue!?"
"" Ni Hilo tu, au Kuna kingine!? Mimi pia wazazi wananitegemea ila kwenye kuandaa maisha yangu wazazi wangu hawatakuwa na Mimi tenaa! Kwanini Wewe u hofu?"
"" Utakuwa umekunywa Wewe sio bure! Make unavoongea kwa kujiamini leo yaani nakushangaa!?"
"" Nachekesha Sanaa! Ani nimekuwa mdori wamaanisha?"
"" Endelea kabisa kutumia Kama leo sitokuacha hapa."
Shamy aliagiza kinywaji kingine Huku akizidi kuchanganyia! Pombe ilianza kumvaa hasua na kubaki akiongea maneno mengi ya kufikisha hisia zake kwa Brighton mwisho kabisa alizima.
"" Heee! Wewe mwanamke Ni Nini Sasa wafanya lakini!? Babako hatanielewa nikikurudisha kwenu upo hivi!"
Alichukua simu nakumpigia Henny amjulishe kilichotokea.
"" Hapo hamna ujanja Bry! Wewe fanya mchukulie room ulipie ili apumnzike ukimpeleka nyumbani alivyolewa hivo lazima ataongea Mambo mengi kuhusu Wewe, Bora akipumzika hapo ataamka pombe zimemuisha!"
Brighton alibaki akipumulia juujuu Kila akimtizama Shamy, ilibidi aite mhudumu pale ampatie chumba alichofanya Ni kumbeba Shamy Hadi chumbani, alimlaza kitandani Huku akizidi kumtizama kweli Shamy Ni mdada mrembo Sana na anavutia kwa Kila mtu hasa amtazamapo, sijui kwanini tu Brighton hamuelewi?'
Aliinuka kitandani kuelekea Bafuni lakini Shamy alimvuta kwa nguvu Huku akiinuka, Brighton aligeuka Huku akimtoa mkono. Shamy alibaki akimtizama huku akiongea kilevi kwa bahati mbaya alihisi kutapika akawa amemtapikia Brighton kwenye suruali yake.
""Shamy!!!! Ni Nini hiki wafanya! Mtu Hata kunywa pombe huwezi ona Sasa unavyonichafua! Wazani nitavaa Nini kukicha!?"
"" I'm sorry Bry! Forgive me! Huku akimfuta kwa kutumia mikono yake.
"" Sio bure Wewe hujielewi Kwanza unazidi kunipakaa uchafu! '' upoje lakini!?" Khaaa! Tayari na Wewe ushajitapikia."
Shamy alibaki akicheka tu huku akimwambia " because I love u''
Muda kidogo Shamy alipitiwa usingizi, Brighton alibaki amekaa kitandani Huku akijiinamia aliangalia muda ilikuwa Ni saa mbili usiku.
"" Sa sijui nifue hi suruali, Huyu nae kajitapikia! Hiyo kesho sijui tunatokaje hapa!?"
Alimkagua Shamy nakumuona kapitiwa na usingizi, Alivua suruali yake huku akibaki kwenye pensi na singled Kisha alielekea bafuni kuoga Huku akifua nguo zake, baada ya kumaliza alirudi kitandani Huku akimkagua Shamy kibode chake kilivyochafuka huku akiwaza jinsi ya kumvua akifue.
Alimvua taratibu huku Shamy akiwa hajielewi na kwenda kukifua kisha alirudi kitandani na kuchukua shuka akajifunika.
Asubuhi yake kulipopanzuka Shamy ndio alikuwa wa Kwanza kuamka make aliwahi kulala, Aliona kawa Kuna mkono umemshika kiunoni ilibidi ageuke ndio anakutana na Brighton akikoroma kabisa hana habari, alivuta kumbukumbu jinsi alivyokuwa amelewa akawa amepata picha huenda Brighton ndio alichukua chumba, aliendelea kumtizama usoni huku akitizama vizuri jinsi alivyomshika akawa ameshituka baada ya kumuona Brighton yupo na singled na pensi. Alipiga kelele huku akijua kafanyiwa kitu mbaya.
Brighton ndio anasituka usingizini kwa zile kelele japo kwa mbali alihisi Ni zile kelele za kwenye mziki, aliamua kujikunyata akawa amemkumbatia Shamy pasina kujua kumbe huwa Ni tabia yake akiwa amelala huwa anagalagala kitanda kizima.
Shamy alidata Kabisaa, akaona isiwe shida hata yeye alisubili apate angalau kumbatio toka kwa Brighton aliamua kumkumbatia pia huku akimtizama.
Brighton ndio anagutuka kufungua macho baada yakuona utofauti katika mwili wake, alikutana na Shamy akiwa akimtizama nakubaki akikumbukia kwanini yupo pale, Alimwachia huku akifanya kumkoa kichwani.
"" Jana ulilewa kweli, harafu kumbe sio mzoefu wa kunywa?"
Aliinuka kitandani nakuelekea bafuni kuoga baadae alirudi kavaa nguo, mkononi alishikilia kishifoni Cha Shamy alimletea.
"" Usiku ulinifanya niwe house girl wako, kufua nimefua basi kaoge bosi wangu!"
Shamy alibaki akimtizama Brighton muda huo alikuwa akivuta simu akitoa maelekezo kwa mhudumu alete supu.
"" Bado unanitizama tu, au huogi?"
Shamy alijiondokea Bafuni, aliporudi alikuta supu ya kuku pamoja na chai, alikaa pembeni Huku akimtizama vizuri Brighton ambae muda huo alikuwa akimsogezea supu.
"" Kunywa supu ushibe! Make Jana ulilewa Sana!?
"" Shamy alibaki akimtizama zaidi baada ya kumuona akiinua kijiko kumnywesha!"
"" Basi malizia! Nilikuwa nakukaribisha tu, hamchelewagi kusema tumewawekea Dawa!"
Shamy alishidwa kujizuia aliachia kicheko Huku akinyanyua kijiko nae akifanya vilevile kumnywesha.
"" Naomba unisamehe kwa kile kilichotokea Jana usiku! Pole pia kwa kunifulia nguo yangu na Ahsante pia."
"" Inatoshaa malizia hiyo supu! Harafu tusubili muda kidogo uende ikifika saa tano tuondoke! Ukiulizwa na Babako mwambie nilikuwa na Brighton."
"" Wewe! Serious? Mimi siogopi kumwambia, tena natamani ajue kabisa kuwa Binti yake anampenda Mtanzania."
Brighton aliishia kuguna huku akipanda kitandani, Alichukua simu yake akiendelea kuchati na Henny.
"" Vipi usiku wenu ulikuwa vizuri!?"
"" Acha zako, Harafu nitachelewa kufika kazini! Nataka nitafute mbinu yakumfindisha Huyu manzi anaenda kujibu vipi kwa babake! Harafu nasikia Chris anaingia leo jioni tutawahi kumpokea.
"" Sawaa! Harafu Janerose alikuulizia make hajakuona kazini."
"" Ananiuliziaje wakati alikuwa na Denison!?"
"" Acha wivu bhana, si unae Shamy hapo!? Anataka msaidiane kazi make mmepangwa wote kupokea ugeni kwahiyo uwahi."
"" Aaah! Ni sie tenaa!?' mbona wanataka kutuzoea Sanaa!"
"" Kwasababu mpo shapu katika utendaji kazi! Fanya uwahi kufika mengine yatajili huku!"
"" Mnapendana Sana na Henny ee!?'
( Shamy alihoji Huku akipanda kitandani)
"" Kwanini umeuliza vile!?"
"" Hamuachani muda wote! Harafu mkiwa karibu huwa naona nyuso zenu zinavokuwa na furaha."
"" Sawaa!!! Harafu unapenda kucheza game la jungle marble!?" Huku akitizama jinsi anavyocheza.
"" Nikiwa nimeboeka huwa napenda kuchezaa! Vipi tuchezee!?"
"" Na leo umeboeka!?"
"" No, I'm happy!"Alimnyanganya simu huku akiendelea kucheza lakini, game lilimgomea kete zote zilimezwa.
Shamy Alimtizama huku na Brighton anafanya vile, baadae walicheka kwa pamoja wakivutana masikio.
....Itaendeleaa....
Usikose sehemu ya 22.
Like comments and suggestions 👍✍️🤝🙏❤️.
[9/19, 21:09] Tinner 1: SIMULIZI: LOVE DISTANCE 💔. MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: "22" 0746638941 Whtsp.
ANZA NAYO.
Shamy Alimtizama huku na Brighton anafanya vile, baadae walicheka kwa pamoja wakivutana masikio.
ENDELEA.
"" Umefurahi kwa raha zako kwamba nimeshidwa!?"
"" Kabisa, make umeonesha kuweza lakini hauwezi."
"" Basi tuondoke muda umefika! Harafu unaenda kuwaambia Nini wazazi wako umelala Nje!"
"" Usijali!! Sitaki uwaze kuhusu mimi! Hapa nishaongea na Rhita rafiki yangu nikitoka hapa nampitia kwao anisindikize nyumbani make nishampanga atasema tulikuwa kwenye Birthday ya mdogo wake! Ila baba mtata ataomba Hadi picha ila sio mbaya Hata picha tutatumia za mwaka Jana si hakuziona!"
"" Duuuh! Wewe mwanamke Kama Baba utamdanganya hivyo! Je, Mimi utakuja kunidanganya vipi nikisimama Kama mmeo?"
Shamy alicheka Huku akibeba mkoba wake waondoke lakini akiwa kwenye gari ndio alimjibu.
"" Sitafanya hivyoo kwa mtu aliyebeba Ndoto zangu!"
Brighton aliishia kutabasamu Huku akimwangalia.
"" Mimi nakushushia hapa huko kwenu sifiki.".
Huku kwenye kampuni la DHB HEALTH organization! Wafanyakazi walikuwa kwenye shamra shamra za kumpokea Chris.
Kuna wadada watatu walikuwa wakizungumza faragha.
"" Chris Ni kijana msomi anasura nzuri ila huwa anajisikia Sana! Letty aliongea.
"" Yaaani iwe isiwe Mimi lazima nitoke nae yule mkaka!" Regina alijibu.
"" Wewe tulia Janerose anapita! Harafu huyu Binti wanamshobokea Sana sijui kawapa Nini tu! Yule Doctor mgeni kafika juzi tu leo hii keshaanza kutoka nae Ani Ni mrahisi huyu Binti Hadi Brighton nae kapita hapo."
"" Mhuu Naomi! Wewe nae kwa umbea utasutwa vibaya!"
Huku kwa Janerose alikuwa akipita mitaa ile aliwasalimia nakuwapatia kazi ya kufanya make walikuwa wamekaa pale wakimsubili awape maelekezo.
Baadae aliwaacha nakuendelea na majukumu Aliingia kwenye stoo ya dawa Kuna kitu alikuwa akikiendea, baada ya kukipata alirudi, muda huo na Denison alikuwa akija stoo walikutana mlangoni. Denison aliangalia pembeni Kama Kuna watu baadae alimshika mkono Janerose na kumrudisha ndani.
'" Denison! Ni Nini lakini unafanya!?"
Denison alikuwa bado akimtizama Kisha alicheka na kumshushia kiss.
"" Nimekumisi tu! Harafu nilikukosa Ghafra nikawaza utakuwa wapi kumbe upo huku!"
"" Ila Wewe! Doctor mkubwa unanivuta chemba tutakutwa humu."
"" Kwani nazini!? Wewe Ni wangu tu!"
"" Baadae basi! Subili tutoke kazini tutaongea!"
"" Kuwa makini! Harafu Kama utachoka Sana punguza kazi! Ona mpaka umesweat!"
"" Usijali! Ni kazi ndogo nafanya! Sema nipo peke yangu! Nilipagwa na Brighton naona kanitelekeza."
"" Nitakuja kukusaidia! Nenda kajiandae Kwanza! Nguo zako zimechafuka vumbi tayari."
Maandalizi yalizidi kupamba moto, taarifa zilifika tayari Chris katua Airport! Muda si mrefu ataingia.
Janerose baada ya kumaliza kazi zake alienda kujiandaa na kuanza kusogea mdogo mdogo kuelekea ukumbini, Kuna Ujumbe uliingia toka kwa Denison akimuomba amsubili make wataingia double.
Denison alifika Hadi sehemu walipokubaliana wakutane huku akiwa na gari yake alisimamisha gari huku akimuita Janerose aingie.
"" Hivi Ni Wewe kweli!? " mbona umekuwa mrembo kiasi hiki! Yaani umependeza kweli!"
"" Nashukuru ila umemechi na Mimi nguo! Au ulipanga toka awali ulivyonitumia Kama Nina gauni la gold nivae, ulitaka tumechi!?"
"" Tulia basii, huenda Kuna watu wanajua Wewe hunae bwana, au mie sinae mwanamke leo nataka wajue kwamba Janerose na Denison wanadate!"
Janerose alicheka huku akiegemea kwenye bega.
Walifika Hadi kwenye tukio Denison alishuka Huku akimshika mkono Janerose wakiingia ukumbini, Kuna mtu alikuja kuwapokea huku Janerose asielewe kwanini wanapatiwa nafasi hiyo ya upendeleo.
"" Tulia basi mbona unaogopa tenaa!? Alimhoji Janerose baada ya kuona anakuwa mzito kutembea.
Walienda kukaa mbele kabisa VIP ndio nafasi zao zilikuwa huko. Muda huo huo Hutaamini Brighton Aliingia akiwa na Shamy na wao walikaa upande wao huku wakifatiwa na Doctor Henny akiwa na Minnah!
"" Unatoa mno macho! Hebu kaa kwa mapozi! Harafu ulikuwa watangulia kwenye Sherehe ulitaka Mimi nije niaibike Sinae mtu."
"" Hukuniambia mapema Kama tutakaa wote Kama hivi! Unajua sijazoea.
"" Ndo uanze kuzoea jinsi ya kukaa na mmeo karibu."
Ilikuwa Ni muda wa kumkalibisha Chris, Aliingia na marafiki zake wawili, Huku mbele yao alikuwepo Mkurugenzi wa kampuni yaani mwanzilishi. Watu wote walisimama kumpatia heshima mpaka pale alipokaa.
Minongono ya chini chini ilizidi kuendelea, Huku wakimjadili mtoto wa kampuni kwa mwonekane wake, wazee wakubwa katika kampuni wao walikuwa wakiangalia masrahi tu, mzee mmoja aliongea.
"" Hapa hamna kitu! Mtoto mwenyewe anaonekana kalala sana! Harafu hao aliongozana nao ndio body guard!?"
Meneja wa kanda alisimama kutambulisha wafanyakazi wake, huku Kila mtu akijitambulisha kwa nafasi yake pamoja na cheo chake.
Mwanzilishi wa kampuni alisimama Kuna maneno machache aliongea, kwa lugha ya kingeleza huku mkalumani alikuwa akitafsiri kwa kiswahili.
"" Nawapongeza watu wote wanaondelea kuniunga katika kazi za kampuni, juhudi zenu zimekuwa kubwa na mnaendelea kunitia nguvu! Kwasasa naona naelekea uzeeni Mara nyingi nitakuwa sishiliki kwenye vikao ila nitakuwa nikiwakilishwa na meneja wa Kanda! Pia katika uandaaji wa takwimu nitamuachia Chrishtom ndio atakuwa akinisaidia baadhi ya majukumu yangu.
Watu wote walishangilia lakini Kuna baadhi ya watu hawakupendezwa Chrishtom kuwekwa katika kile kitengo.
Sherehe iliweza kuishaa Kila mtu alielekea kwake. Na Siku ya kesho yake majukumu ya kazi yaliendelea.
Siku hiyo ilikuwa Ni Siku ya kuhitimisha semina, Chris aliamua aje kuwasikiliza kipi kinachoongelewa zaidi huku akijaribu kunote baadhi ya Maada zilizoongelewa.
Mwisho kabisa Aliingia katika ofsi yake huku akikagua baadhi ya documents! Kama Kuna tatizo alikuwa akimuita mhusika mmoja anahesuka na kitengo kile aongee nae, baadae alimuita Janerose akawa ameingia na file zake alimkabizi.
"" Ooh! Wewe ndio Janerose unahusika na magonjwa ya watoto wenye matatizo ya manjano pamoja na sikoseli!?"
Muda huo Chris alikuwa akiongea Huku akiendelea kukagua file baada ya kumaliza kukagua aliinua kichwa huku akimwangalia Janerose alipomuona alishituka kidogo Kisha Alimhoji.
"" Wewe ndie Mrs Denison!?"
"" Ndio!"
"" Sawa! Naona unajitahidi katika utendaji kazi! Hongera pia unae mwanaume anaekupenda!
Janerose ilibidi akae kimya make hakutegemea Kama angesikia maneno yale toka kwa Chris.
"" Okay!! Niitie Brighton, Henny waje kwa pamoja! Wewe waweza kwenda"
Janerose Alichukua File zake na kuondoka, huku kwa Chrishtom alibaki akimtizama Sana! Kisha aliendelea kujaza taarifa zote.
.... Itaendelea....
Usikose sehemu ya 23.