Safari Ya Ndoto

 SIMULIZI: SAFARI YA NDOTO.                                             MTUNZI: TINNER ROBER.                        SEHEMU: '31 'FINAL' . 0746638941 Whtsup.


ANZA NAYO.




Hapo hapo Norah alifika akiwa na farasi wake Huku akitoa tamko.

  "" Mimi namwamini Alfred atafanya vizuri make nimeshampa mbinu zote za kivita nahisi kashaanza kuzifanyia kazi! Hapa inatakiwa Askari wazunguke Tokyo Hafu wengine waende Sakhalin! Hakikisha Kila walinzi waliobakia kulinda Ufalme mnawakamata na kuwaweka ndani! Kuhusu wananchi wao msiwadhuru make wao siku zote hufuata Sheria tu, nataka pambano likiisha Kila kitu tuwe tumemaliza kukiweka sawa! Naomba mtekeleze kwa wakati huu.

ENDELEA...


Huku Upande wa Alfred alikuwa akiendelea kupambana na Ngwasamo muda huo alikuwa kawekwa chini, Ngwasamo alinyanyua Upanga wake ili amchinjie mbali! Watu wote waliokuwa pale walifunga macho ili wasione tukio linavyoenda kutokea.


Upande wa Brighton alibaki amemkumbatia Dadake Huku akimfunga macho asione kinachotokea! Kama dakika tano zilipita kulisikika sauti ya kilio Huku wengine wakiuliza mbona imekuwa hivyo tenaa! Hapo hapo kukaanza kelele Huku watu wakianza kupigana wao kwa wao, Brighton hata hakuelewa kipi kiliendelea make ilikuwa ni kelele tu! Alimchukua Pacie pamoja na Degner Huku wakitafuta namna ya kuokoa maisha yao walikimbilia kunako msitu mkubwa wakawa wametulia huko, Huku baadhi ya wanakijiji na wao walikimbilia pia.


Wakati wametulia walisikia wanakijiji wakijadili ilibidi watege sikio wajue kipi kiliendelea!

  "" Unajua Ngwasamo alitaka mwenyewe kupoteza maisha! Alfred alikuwa amelegea muda huo Kama kushusha upanga angemshushia haraka! Lakini kwa majigambo aliyokuwa nayo Alfred alimtriki inaonesha alimtegua mguu mmoja ile anaanguka Alfred alimtega lile jiwe lenye ncha Kali akawa ameliangukia! Daah! maskini damu nyingi zilimumwagika bado na lile panga aliloshikilia lilimkata vibaya mkonononi! Hutaamini amekata roho Huku akiwa amekunja ngumi akimwangalia Alfred kwa hasira!"


Brighton, Pacie na Degner waliposikia hivyo Hutaamini Pacie alishidwa kujizuia kwa furaha aliyonayo aliruka ruka Huku akipiga kelele, lakini Brighton alimuwahi na kumziba mdomo.

   "" Ani wewe unaonesha furaha yako mbele ya watu! Huoni Kama hapa Kuna vikosi viwili watakuja kutuchinjia mbali"


Pacie alikaa kimya! Ndipo akili yake ikarudi alimkumbuka Babake kwanza.

  "" Kaka! Baba atakuwa wapi muda huu au na yeye keshauwawa tayari make hii vurugu iliyopo hapa sizani Kama Kutakuwa sawaa!"


Wakati wakiwa pale Kuna Wababe walionekana wakizunguka Ishara wanamtafuta mtu.

   "" Soyona, Alfred na wewe Prince Lee toka Shantar naomba mjitokeze!"


Sauti ile iliwafanya washituke kwanza kumbe wenzao wanatafutwa, na hapo hapo wakagundua kweli Alfred anaishi..


++++++++


Nje kidogo na mji kulionekana Kuna watu wengi walikuwa wamevalia mavazi meupe Huku wakitoa heshima zao za mwisho kumuaga Ngwasamo, baadhi ya viongozi toka Sakhalin walikuwa wakiongoza ibaada ya mazishi mwisho kabisa waliuchoma mwili wa Ngwasamo Huku wakibaki kuongea.

  "" Mtukufu wetu Ngwasamo! Hakika ulikuwa shujaa Sana, daima tutakukumbuka siku ukizaliwa upya katika Dunia nyingine! Naomba uje kukomboa taifa letu tenaa na uliongoze vyema!"


Siku zote wenzetu huwa wanaimani mtu akifa leo, kesho yake atazaliwa tena mpaka Mara tatu ndio hufa mazima kwahiyo nafsi yake huwa inaishi mpaka afikie umauti kwa Mara ya tatu ndio nafsi yake hupotea na haiwezi kurudi tena Wala kuzaliwa upya!


Wakati yakiendelea hayo Hutaamini Soyona alikuwa pembeni Huku akiwa na jeshi lake, muda huo walikuwa wakiwasubili wamalize ibaada Yao ya mwisho, ni kawaida katika Mila zao kuheshimu ibaada hata Kama watakuwa wapo vitani husubili ibaada iishe  ndio vita iendelee. 


Baada ya kuona wamemaliza ibaada ile wanaondoka tu tayari Wanajeshi waliwazunguka na kuwachukua mateka kiulaini, waliwapeleka Hadi mji wa Tokyo kwenye himaya yao, ile wanafika walimkuta Baba yake Soyona pamoja na wafanyakazi wenzake wote wamewekwa chini ya ulinzi, Soyona hakuonesha kujali alimwangalia Babake Kisha aliachia tabasamu aliangalia jua kisha alishusha macho chini Huku akiangalia  kimvuli kwa mbali alisikia sauti ya farasi wakija pale alibaki akiwatizama Wanajeshi wa Sakhalin Huku akiachia tabasamu.


Muda kidogo Norah, Noely pamoja na Prince Lee walifika pale Huku wakiwa na kikosi kikubwa! Watu waliokuwa pale walibaki wakitoa macho hasa wale Wanajeshi hawakuamini kuona familia zao pamoja na watoto wao wadogo wamefugwa kamba walipowaona tu Kila mtu aliachia siraha  chini huku akipiga magoti kuomba msamaha wasiguse familia zao.


Soyona alitoa amri! Iliyopelekea wote wabaki wakimkimbilia.

  "" Wasogezeni hao watoto wadogo mbele ya Baba zao na Mimi nitashusha upanga wangu juu ya vichwa vyao!"


Kuna sauti ilisika ilyopelekea Soyona abaki ameinua upanga wake juu. Alikuwa ni Brighton ( mmewe) pamoja na Pacie.

   "" Hapana Soyona usifanye hivyo tafadhari! Mimi nipo tayari kukufuata wewe pamoja na watu wangu! Nipo chini ya miguu yako."


Wale Wanajeshi walipomuona Brighton kapiga magoti na wao waliishia chini Huku wakimuinamia! ( Soyona alibaki akicheka kimya kimya kumbe ni triki iliandaliwa toka awali Brighton afanye vile ili Babake Brighton asalende kwa hiari yake) 


Muda huo Babake na Brighton alikuwa akiangalia Huku akijitia ushindi Kuna Wanajeshi wake alikuwa akiwategemea alishangaa kuwaona na wao wanaletwa mbele yake Huku wakiwa mateka na Alfred alikuwa akiongoza kikosi alitoa macho akiwatizama Hutaamini walishuka kwenye farasi Huku wakimwomba msamaha na kuahidi kuungana na Alfred.


Babake Brighton alishuka chini nguvu zilimuishia, Pacie pamoja na Brighton walikimbilia kumsaidia! Make kifua kilikuwa kimebana! 


Huku kwa Noely pamoja na Norah Kuna ujumbe walikuwa wameuandaa walitoa na kumpatia Alfred ausome! Alfred alimaliza kuusoma nguvu zilimuishia alishuka chini taratibu Huku akibaki kuongea.

  "" Kumbe Norah na Noely ni wajukuu wa Babu!? Babu alikosea kumbe walizaliwa watoto mapacha kwanini Norah alinificha ilikhari alifahamu ukweli!?"


Aliinuka kwa hasira Huku akimuelekea Norah alimshika na kumkaba Huku akizidi kulia kwa uchungu kwanini hakumwambia mapema! Wakati hatima yake alipewa kumtafuta mjukuu tu! Angejitokeza mapema Wala Vita Isingetokea.


Norah alibaki akilia na yeye Huku akimuomba msamaha Noely nae alifika akamkumbatia Huku akimuomba radhi.

   "" Nisamehe Mimi Alfred! Mwanzoni nilijua tayari ushaanza kumpenda Norah! Nilitafuta muda wa kuongea nae ikabidi Mimi na Norah tufanye uchumba ili tukukatishe tamaa! Make tungekuacha ungeshidwa kukamilisha Safari ya Ndoto uliyoachiwa na Babu! Nasisi ilikuwa ngumu kukwambia kuwa tu wanandugu tungefanya hivyo usingeweza kupigania taifa lako, Hapa tayari umekomboa mji wa Sakhalin na Mimi nilienda kukaa Saka Ili nipate nguvu kwa Wanajeshi wa Saka Ili kwenye Vita tutoe msaada kwenye taifa letu! Hata Upande wa Norah nae alienda kukaa Harbin awe Kama Dokta baadae kiongozi wa jeshi Nia na malengo yetu ilikuwa ni kutafuta nguvu ya kupigania taifa letu. Naomba utusamehe Sana ila kwasasa tumeshinda Vita na tutarudi kukaa kwenye taifa letu Kila kilichofanyika kipindi Cha nyuma kinyume na Sheria kwasasa kinaenda kuzaliwa upya! Taifa letu halitaongozwa kimabavu tenaa!


Alfred Alibaki kufurahia Alijua tayari kwasasa kapata familia yake! Furaha yake ilimfanya Babake Soyona atabasamu alimsogelea na kumpatia ujumbe wa maandishi ulioachwa na Babu yake! Kumbe Babu  alikuwa ni Babake mkubwa yeye alikuwa ni mtoto wa mdogo wake na Babu! Kuhusu Noely na Norah wao walikuwa ni watoto wa Babu mkubwa! hii ilizidisha furaha kwao.


Upande wa Soyona alikuwa akipiga makofi mpaka Babake yake alibaki akimshangaa! Alimpatia Ishara aende kwa mmewe! Soyona alimfuata Brighton kwa pamoja walikumbatiana, Huku kwa Alfred alimfuata Pacie pia.


   *******


Baada ya Miaka miwili kuisha  Alfred alitawazwa kuwa kiongozi wa taifa la Sakhalin akiwa na mkewe Pacie! Soyona nae alimkabidhi uongozi Brighton Huku wakishilikiana kuongoza kwa pamoja, Norah alienda kuanzisha taifa jingine, alijipatia mme toka taifa la Saka alikuwa ni mtoto wa waziri mkuu(Hussein) Huku na Noely na yeye alifanya vivyo hivyo, alimchukua Degner akamfanya mkewe. Mataifa yote yaliyoanzishwa yalizaliwa kutoka Sakhalin, Na mshauri alikuwa ni Babake Soyona pamoja na Babake Brighton japo walikuwa wamezeeka ila walibadilika na kuwa watu wema na hi ndio ilikuwa  SAFARI YA NDOTO YA WATOTO WAO.


     ..... MWISHO.......


Huu ndio mwisho wa simulizi yetu ilikuwa ni Korea love story (Pori) 


Nawashukuru wale mliokuwa mkifatilia simulizi hii naimani mmempata kitu Cha kujifunza.


Usikose kufatilia simulizi zangu katika Group langu bonyeza link hii kujiunga kwa yule ambae bado hajajiunga.

://facebook.com/groups/263417295228138/ BY TINNER ROBER.

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi