Mashabiki wa Simba walia na utegemezi

 Na Mwanahabari wetu


Simba Fans


Simba ni Chama na Chama ni Simba. Kila mmoja anamtegemea mwenzake. Mechi mbili amekosekana timu imekosa ubunifu katikati ya uwanja. Wapinzani wenyewe wanafurahia kucheza na Simba isiyokuwa na Chama. Akiwepo Chama kikosini kila mchezaji unamuona yuko safi. Naelewa kelele za mashabiki wetu. Simba tumezoea kuona timu yetu ikishinda na kumtawala adui, sio kuongoza mechi kisha kutamani mpira umalizike haraka. Hii sio afya.
 
Hayo ni maneno ya wadau wa soka walioyatoka katika mtandao wa kijamii wa Facebook mara baada ya mchezo wa Timu yao ilipocheza na Namungo na kuweza kuvuna ushindi wa alama 3 zilizowasogeza juu kabisa na kushika nafasi ya pili chini ya watani wao Young Africa ambao wako kileleni wakiwa na uongozi wa tofauti ya alama tano.
 
Naye Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally alipohojiwa na wanahabari juu ya matokeo na msimamo wa timu kwa ujumla alikiri kuwa timu  yake ni kweli imeshuka kiwango sio kama simba ya zamani maana kuna kitu kimepungua. 
 
na katika duru za kombe la dunia nimekusogezea uchambuzi kama huu
 
 

Yahya Njenge wa PAGE 4 ya Amplifaya @CloudsFMTZ anasema tangu kuanzishwa kwa kombe la dunia mwaka 1930 mpaka kwenye Kombe la dunia 2018 mara zote Mabingwa wa kombe hilo walikuwa ni Nchi zilizokuwa chini ya Makocha wazawa.

Unaambiwa pia katika World Cup ya mwaka huu inayoanza nchini Qatar hivi karibuni kati ya Timu 32 zinazoshiriki….. 23 zinaongozwa na Makocha Wazawa huku 9 pekee zilizobaki ndio zina Makocha wa kigeni.

 

 

Katika Burudani tunaangalia FULL INTERVIEW YA INSPECTOR HAROUN AKIONGELEA MZEE WA BUSARA RMX3 /KUHUSU EP YAKE NA #JUMANATURE /UJIO WAO MPYA /USHIRIKINA HAUWE KUISHA /UFALME WA TEMEKE HAUWEZI KUPOTEA ...

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi