DARUSO ni neno lenye ufupisho wa Dar es Salaam University Student Organization ambayo ni serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar Es salaam. Hivi karibuni mpekuzi wenu alizama na kukutana na Mmoja wa wabunge wanaounda serikali hiyo Mhe. SAID KHARIM MSHANA na tulipata nafasi ya kufahamu mambo mengi kuhusu yeye masuala ya siasa na hata masuala mengine kadha wa kadha.
Mshana alianza kwa kutuelezea ni kwa namna gani aliweza kupiga hatua hadi kuingia katika siasa za chuo hiko ambapo alibainisha changamoto mbalimbali alizokumbana nazo
Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:-
Msakuzi wetu: Ok Brother Can you tell us in short who is Mshana?
Mshana: 🙏in briefly *Mshana Said* is a University of Dar es Salaam student studying Bachelor's Degree with Education is also a Novel and History Writer and Blogger Content Producer Also He is a leader who got the chance to be elected as the Daruso CoHU second year MP 2021/2022 also He is Chairman of the Standing Committee of the Daruso Parliament Order 2021/2022. Mafanikio haya yote nimeyapata kutokana na ushirikiano mkubwa ninaupata kutoka Team kubwa Team Humanities. Hivyo niwashukuru sana Mhe. Akida Omar Mwenyekiti ndaki ya Insia na Ismail Kaminambeo katibu mkuu ndaki ya Insia bila kusahau Watendaji wote (Excom's) Wa ndaki ya Insia na Wabunge makini ambao wako bega kwa bega nami kuhakikisha Changamoto zote zinashughulikiwa kwani hakuna mtu mwenye uwezo wa kuyafanikisha yote hayo kwa uwezo wake binafsi isipokuwa lazima kuwe na watu waliotayari kufanya mabadiliko
Msakuzi wetu: Ok hongera sana Mhe. Said sasa uliwaza nini hadi kuingia katika siasa
Mshana: Sababu kubwa ya kuingia katika siasa ni ili Kuwawakilisha walio wengi na kuwa msemaji wao katika masuala mbali mbali kwa ajili ya kuhakikisha tunaijenga jamii iliyo imara kwa kutatua kero mbali mbali zinazoikumba jamii yetu
Katika hilo pia Mhe. Said Kharim Mshana aka Tajiri wa CoHU aliweza kubainisha changamoto mbalimbali alizowahi kuzipitia akianzia katika kuomba hata walau awe muwakilishi wa Darasa katika baadhi ya masomo anayosoma lakini alikosa uwakilishi huo kitendo kilichomfanya anyanyuke na kwenda kuwafuata wahadhiri kuwaomba wampe nafasi hizo kama muwakilishi wa madarasa na hapo ndipo gari la siasa kwa upande wake likawaka ambapo Mhe. Mshana anasema
".......Binafsi nilipenya katika siasa za Chuo kwa sababu ya uthubutu na kutokukata Tamaa. Nakumbuka Nilithubutu Kujaribu Kuomba U cr wa GE ila sikuteuliwa nikabahatisha kuwa cr wa DS 112 & 113 Chini ya *Cordinator Iman Majenda* Na Cr wa Semina ya LL 102 Chini ya *Dr Kimambo*. Nakumbuka Hapo ndo safari ilipoanzia. Hata ilipofika Mwezi May wakati wa Chaguzi niliomba nafasi ya Ubunge Ndaki ya Insia na nilikuwa mtu wa 30+ kuchukua Fomu ila sikukata Tamaa, Mkeka unatoka nikawa miongoni mwa watu watu 14 walioitwa kwenye interview Na baadae Tume ya *Mhe. Yusuph* ikaniamini na nikawa miongoni mwa watu wanne waliopitishwa ili kuja kuomba ridhaa kwa wanafunzi wenzetu na walio wengi waliniamini na kunipa nafasi japo upinzani ulikuwa mkubwa.
Kwa vijana wengi hapa ndio sehemu ya kujifunza mengi haswa uthubutu na uvumilivu. Kijana hakuwahi kuwa katika orodha ya wateuliwa wa kuwakilisha darasa lakini juhudi zake zikamletea faida na leo anapepea na kitu chenye utepe wa blue. Angekata tamaa sidhani kama leo hii tungemwita Mheshimiwa hivyo basi jambo tunalopaswa kulifanya au kujifunza kutoka kwake ni uvumilivu na uthubutu wa kila jambo.
Msakuzi wetu hakuishia hapo tu aliingia ndani zaidi kutaka kufahamu zaidi ni kwa namna gani wameweza kuzitekeleza ahadi zao viongozi na hapa ndipo mhe Mshana alisema
Binafsi si sehem ya serikali ni sehem ya Bunge ila kama Bunge nina wajibu ya kuhoji juu ya Utekelezaji wa Ahadi za serikali hata hivyo mpaka sasa Hatujakaa kikao chochote cha Bunge Cha kuhoji juu ya utendaji wa serikali kufuatia Kuvunjwa kwa baraza la mawaziri hivyo kila kitu kilisimama Ikiwemo vikao vya Bunge mpaka Mambo yalipokaa sawa. Hata hivyo Tutahoji suala hilo katika kikao kijacho cha Bunge🙏
Ebhana Mshana kaubonda mwingi sana. Lakini pia ikumbukwe kuna watu walionekana wakimpost kumtakia matashi mema mapema mwezi Machi mwanzoni katika hili Mshana alisema
Nooo All day's that Am happy its like my birthday I CELEBRATE but my real birthday is 13/4.
Hii ndio inakuja kutuambia kale kalikuwa kama ni ka (Pre-Birthday) flani kenye unyama wa kimwaisa flani hiviii. Lakini wewe unayewazia kuwa sera za viongozi hao hazikufanikiwa amini kwamba SERVICE AT PASSIONATE LEVEL inaenda kukamilisha sera zake katika kipindi hiki kilichobaki.
Niandikie maoni yako ni nani tena weekend ijayo asakuliwe na tukuletee mambo yake hapa ndani.
Pia waweza kunitafuta Instagram @lugembeblog
Ama kwa kutuma pendekezo lako kwenda namba 0678772962 ukianza na #MSAKUZI kisha jina la mtu ungependa tumnyapie na kukuletea taarifa zake humu