Mbowe na wenzake wameachiwa baada ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali, DPP, kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo.
Mbali na Mbowe, wengine ni Adam Kasekwa, Halfani Bwire na Mohamed Ling’wenywa waliokuwa makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando ameieleza Mahakama kwamba, “Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri anaomba kuwasilisha taarifa ya kutokuwa na nia na kuendelea na shauri hili.”
Amesema, taarifa hiyo tunaitoa chini ya Kifungu cha 91(1) kwa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Mawakili wa utetezi, wakiongozwa na Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi, Peter Kibatala walidai hawana pingamizi juu ya ombi hilo na kuiachia mahakama.
Nje ya viunga vya Mahakama, shangwe zimetawala kwa baadhi ya wanachama wa Chadema waliojitokeza kusikiliza kesi hiyo.
Hata hivyo, Mbowe na wenzake hawakuwepo mahakamani wakati kesi hiyo ikifutwa.
Na mara baada ya kuachiwa huru alipata wasaa wa kukutana na Amiri Jeshi mkuu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samiah Suluhu Hassan.
Rais Samia Suluhu Hassan leo Machi 4, 2022 amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugwnzi ya mawasiliano Ikulu leo, Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki.
Aidha, taarifa imesema kuwa Freeman Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taila la Tanzania ni kusimama katika haki.
Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Tags
Kitaifa