[1/25, 17:16] Tinner 1: MWANDISHI; TINNER ROBER. SIMULIZI; UPENDO USIOTARAJIA. SEHEMU; 01
UTANGULIZI.
Majina yangu naitwa Tinner "22", ni mtoto pekee kwa wazazi wangu, mzaliwa wa mwanza, Wazazi wangu wanajishughulisha na biashara, Baba yangu ni muuza dagaa maarufu huwa anachukua dagaa, ziwani anasambaza mikoani, mama yangu ni fundi cherehani pia Ana duka la vitambaa makoroboi, anauza jumla na rejareja, Wazazi wangu wamenipa kipaumbele Sana katika masomo yangu mara tu Baada ya kumaliza kidato Cha nne.
Wazazi wangu walipenda Sana nikajiunge na chuo Cha uuguzi kibiti Nursing school, kilichopo Lindi. Chuo hiki walikipa kipaumbele Sana kutokana na baba yangu mdogo ni daktari bigwa wa maswala ya "Physiology" na hii imempa umaarufu Sana kwa hapa Bugando. Na matumaini yao yalikuwa ni makubwa sana kwangu hata kama ajira zingekosekana walikuwa radhi kunipa mtaji nikajiajiri mwenyewe, Baba aliependa Sana muda wote kuniambia;
" " Mwanangu elimu ni hadhina kubwa kama wazazi wako wakikupa hadhina hii ihifadhi ili badae uje kuitumia mbeleni na hii itakupa ufunguo wa maisha yako""
Nakumbuka ilikuwa ni siku moja ni siku iliyovutia machoni kwangu, kumbumbuku za furaha, na huzuni Kila ninapovuta taswira haikosi jirudia Tena, ni siku ambayo ilikuwa ni kumbukumbu yangu ya kuzaliwa ilikuwa ni tarehe 23,12 ni siku watu walikuwa wameanza maandalizi ya X-mas na mikesha hasa katika makanisa mbalimbali ya kikristo yalikuwa yamepamba Moto, Nyumbani kulijaaa na shamra shamra za Kila aina , Mimi nlikuwa ndani na rafiki yangu Jescar, tunapiga story za hapa na pale huku tukiandaa mavazi yetu. Jescar, alikuwa ni rafiki yangu wa karibu Sana aliweza kunisapot siku ya birthday yangu kuwa kama partiner siku hiyo, na urafiki wetu ulikuwa ni urafiki wenye furaha siku zote ulijaa amani, na upendo na siku zote ulizidi kuchanua.
"" Mara Baada ya maandalizi yetu kumaliza, tulielekea sehemu ya tukio, Kila mtu aliekuwa mahali pale kiukweli aliweza kupendeza na sherehe ilipamba Moto, muda ulizidi kwenda ilikuwa ni muda wa zawadi mbalimbali Kila mgeni alileta zawadi yake,
"""mama aliniletea zawadi ambayo sikutegemea kabisa, walikuja na baba wameshikilia kibox Cha Kati baba,
"" akasema "" Mwanangu,, Mimi na mama yako tunakuachia muongozo wa Vitabu hivi vikawe mwongozo wa maisha yako itabidi ufungue hapa mbele za haraiki hii Kila mtu aone zawadi hii.
""Taratibu nilifungua box lile nilikuta Kuna vitabu viwili Cha Kwanza ni Anatomy( kinazungumzia Sana sehemu ya mwili wa binadamu kwa ujumla), Cha pili ni Midwifery (ukunga)
Mimi binafsi sikuamini kama wazazi wangu wangenipa zawadi hiyo, watu wote walishangaa kwa mtu ambae hakuwa mwelewa aliona kama kitu Cha ajabu sana, kwa waelewa walishangilia.
Muda kitogo kuna vijana wawili walivaa nguo nyeusi, waliingia huku wameshikilia zawadi zao ikiwa ni pamoja na keki, moja kwa moja Hadi sehemu nilipokaa, waliweka mezani Kisha kuchukua mshumaa, na kuwashaa, watu wote walikuwa wakiwatazama bila majibu yoyote, Baada ya kuvuta Moshi ule wa mshumaa nilianza kuhisi mwili wangu unakuwa mzito, nikaanza kuwasikia kwa mbali wakiongea;
""mama, baba tayari huko wameuwawa!!!,
sijui ni kumbukumbu zangu tu nilizipelekea huko, baadae nilimuona mama povu linatoka mdomoni, na baba alikuwa pembeni damu zikimtoka puani na mdomoni. Nilisituka ghafura na kusema ""
''Hivi naota!!!,, Tinner hebu gutuka rudisha akili hapa nataka kuchanganyikiwa'' hivi naota???
"Jescar""" hivi na wewe ninavyoota Mimi na wewe unaona hivyohivyo, hebu niambie ni ya kweli haya lakini!!!??
"""Baada ya kufumbua macho, yangu nilimkuta 'Jescar kanikumbatia kwa nguvu huku hofu ikiwa imetanda neno la mwisho alisema""
" Tinner, tukimbie mama, Baba wote wameuwawa, tutoke hapa watu wote wamekimbia wamebaki wachache tu na wao ni wafu, tuondoke, halafuuu,,,,,,,
""Kabla hajamaliza kuongea nilimuona mtu mwenye nguo nyeusi alimpulizia Moshi machoni Jescar" na hapohapo alizirai Kisha alinivuta kwa nguvu na kunitupia kwenye gari kama mzigo na kuwashaa gari, kwa sipidi Kali muda huohuo Baada ya kunitupia kwa gari nilijigongeza kwenye paji la uso na kuzrai.
,,,,,,,Itaendelea usikose sehemu ya pili.
MWANDISHI: TINNER ROBER.
SIMULIZI: UPENDO USIOTARAJIA.
SEHEMU:02.
""Kabla hajamaliza kuongea nilimuona mtu mwenye nguo nyeusi alimpulizia Moshi machoni Jescar" na hapohapo alizirai Kisha alinivuta kwa nguvu na kunitupia kwenye gari kama mzigo na kuwashaa gari, kwa sipidi Kali muda huohuo Baada ya kunitupia kwa gari nilijigongeza kwenye paji la uso na kuzrai.
"" Ile nakuja kuzinduka tayari nlikuwa Airport, na ndege muda huo inaondoka, nikaanza kupiga kelele, nilikuja kuangalia watu wote wapo busy na mambo yao wengne wanasoma gazeti, pembeni yangu alikuwepo mzungu mmoja kakaa na mwanae na muda huo yupo busy wanacheza game kwenye laptop,
" Ikabidi nimsemeshe "" how are you? Mzungu yule, aliniangalia tu akatabasamu Kisha akasema "" Fine"
" Daaah!! Moyoni nikajisemea na kutabasamu kote anaishia, fine" tu kweli watu weupe wanadharau Sana, sasa nitamuanza vipi tena, nimwambie unajua nlikotoka, au ninapoenda , au abiria wote wanaelekea wapi?? make wanafuraha Sana utazani wanaenda kwenye sherehe, mbona nikikumbuka mara ya mwisho nilikuwa kwenye gari na watu wenye nguo nyeusi au ndo nipo kwenye surprise ya birthday.
"Wazo liniijia nikawaza ngoja nimfinye mtoto au nmkanyange niseme bahati mbaya, ili akilia Baba atakuwa busy kumbembeleza mtoto, na akishanyamaza mtoto hatakuwa na mud Tena wakucheza game, atambembeleza mwishoe atalala akilala huyu mzungu atanisikiliza vizuri make atakosa kampani Tena lazma nitafanikisha tu hapa.
"" Nilijisogeza karibu, na mtoto nikajifanya kama nasinzia, taratibu nilimkanyanga mguuni kwa kumkwarua kucha zangu za mguuni muda wote nilipendaa kufuga,
Mtoto kweli alilia huku akisema Daddy!! Daddy!! Huku akininyoshea kidole akinielekezea Mimi.
Mimi, ndo nkajistua daaaah sorry, sorry, excuse me, sorry please!!
Mzungu, aliniangalia tu,,nikaona tayari nimesha muungia kingeleza ndo maana kaniangalia, na kunishangaaa tu.
Matokeo yake nilichofikilia ndio nilifell kabisa, alimnyamazisha mwanae Tena kwa kumdanganyia acheze game la kukimbizana, na ndo game likanoga wakawa watu wakucheka tu baadae wakapitiwa usingizi wote wakalala,
"""Tayari upande wangu nkabaki kushangaa tu abiria wenzangu muda wote wanachezea laptop nikaona ngoja nilale tu sioni hata mtu anayetaka kuwa karibu yangu.
"" Nasinzia hivi, nashangaa, mdada wa kitanzania akaja na kukaa karibu yangu, vipi Madam unanjaa? Kwa haraka kweli nilimjibu Tena Sanaa kama ukileta sato, mkubwa mkavu, na ugali ntashukuru.
"" Dada yule, aliondoka, hakunijibu chochote , baadae aliniletea samaki mkavu, na ugali pamoja na juice ya embe Kisha aliondoka. Akili yangu ikanituma aaah kumbe nipo Tanzania tu itakuwa naenda Dar, mbona vyakula vya Nyumbani tu wameleta na nmeagiza makusudi tu wasingeleta ningejua sipo sehemu sahihi,
******
Safari ilizidi kuendelea, taratibu usingizi ulinichukua, ile naamka tayari ndege imetua Airport, muda huo natoatoa macho, sielewe zaidi ni watu wamebadilika kabisa kimuonekano, mpka mavazi kuliko watu wa kitanzania wanavyovaa, walivaa mavazi kama ya kikorea, ni mavazi yenye heshima, Tena walikuwa wanaheshimiana kweli salamu zao walisalimiana kwa kusujudiana,
"" Muda kidogo alitupokea mama mmoja wa makamo hivi alitoa ishara tu tumfuate, muda huo nlikuwa nmevaa gauni langu la birthday, na pembeni nilikuwa na wale vijana waloniteka japo tyari walibadilisha mavazi yao na kuvaa mavazi ya kule, niliamini tu watakuwa ndio wenyewe wamebadili nguo,.
''' Tayari tulifika kwenye jumba moja lililokuwa limepambwa vitu vyenye thamani, vilivutia muda wote na sehemu hiyo ilionesha kutakuwa na tukio litafanyika punde.
"" Alitokea mdada mmoja ,umri kama tunalingana, alikuja kwa heshima akiniinamia, kama salamu za hapo walivyokuwa wakifanya hata kwa wengine,, akisema ""ewe princess mtukufu,; Mtukufu wetu markia anakuita yupo kwenye jumba la ibaada, tafadhari fuatana na Mimi princess nikupeleke.
Nilimfuata kwa unyonge, mpaka kwa malkia, nikasimama, muda Huo nimeshikilia gauni langu lilikuwa refu, ishara ya kutaka balance ya kusimama kisha, kumtolea macho.
"" Malkia unaniita!!??,
"" Keti Kwanza tuongee""
"" Taratibu niliketi, ""Malkia nakusikiliza''
"" Malkia aliniangalia tu hakusema chochote, alichukua birika lililokuwa na kahawa na kunimiminia Kisha alinipatia akisemaa, "" Princess"" pole na uchovu, tumia hii itakupa nguvu.
"" Nilinyanyua kikombe nikanywa ile nakunywa tu niliibunda mdomoni kusikilizia Radha yake, ilinishinda ikabidi niiteme, ile natema tu bahati mbaya nkamtemea Markia.
""Haraka walikuja warinzi wa Malkia kumfuta na kumpa pole
."" pole Malkia, naona hajazoea, hada mavazi yake yanasadifu hajawahi tumia.
""Muda huo, Malkia alikuwa kimya tu, akijifuta.
"" Taratibu nilianza, kuogopa na kusema, "" mbona wanamcare hivo, hafu Mimi nimemtemea sijasema hata samahani??
""" Taratibu, Nilipiga magoti mbele ya Malkia, nikamwinamia huku Naropoka kwa sauti na kusema,
""'samahani Mtukufu Malkia, kweli ilikuwa bahati mbaya, kiukweli nakubaliana na mlinzi wako Mimi sijawahi tumia vitu hivi hata mavazi yangu ni tofauti na yenu.
"" Malkia, aliniinua kwa mkono wake mmoja kunishikisha, "" nimekuelewa princess, sawa keti.
"" Akaamuru nitengenezewe chai, namimi nikasapot hapo sawa Malkia, huwa natumia baba yangu alipenda Sana kunitengenezea chai.
"" Hapo, hapo fahamu zilinirejea na kuanza kulia Huku nikikumbuka Wazazi wangu.
,,,,,Itaendelea,,,,,,
usikose sehemu ya tatu..
Vipi Tinner Rober kapelekwa nchi asiyoifahamu Kuna Nini nyuma ya pasia???
[1/25, 17:16] Tinner 1: MWANDISHI: TINNER ROBER
SIMULIZI:UPENDO USIOTARAJIA.
SEHEMU:03
"" Hapo, hapo fahamu zilinirejea na kuanza kulia,
""Kwanini, mmenitenga mbali na wazazi wangu, mbaya zaidi naishi nchi, hata nisiojua ni nchi gani?, Mmeua wazazi wangu naomba mnirudishe Nyumbani kwetu, Tanzania, sizani kama hii, ni nchi yangu hatuna Mila kama hizi mbaya zaidi Rais wetu nmeacha kafariki, huku naona Bado mna utawala wa kifalme.
""" Niliendelea kulia, bila matumaini yoyote, """ basi nawataka wale vijana waliokuwa wamevaa nguo nyeusi, wanipeleke wao ndio wanapajua Nyumbani, nipelekeniiiiii!!!
"""Ikawa ni patashika sehemu hiyo, Nilivunjavunja Kila kitu Cha udongo, na maua yote nilitupa kulee.
""" Malkia, aliamuru nipelekwe ndani, nioge na nibadilishiwe nguo nifanane kama wao.
"""" Ukweli niliandaliwa, chumba kizuri, kilichokuwa na mazingira mazuri, chumba, kilijaa nguo Kila aina Tena zilikuwa na matrio ya dhahabu, muda ule zilikuwa zikimetameta.
""" Kijakazi, mmoja alikuwa karibu Sana na Mimi tokea nilipofika kwenye jumba lile alijitambulisha"" princess niite piniety, ntakuwa mwangalizi wako muda wowote, ukiwa na shida niambie, naahidi kuwa karibu na wewe muda wote ukikosa wewe niazibiwe Mimi, na hii ndio kazi yangu niliochagua. "" Basi ukimaliza kuoga niite, nikusaidie, kukuweka sawa upendeze mi nipo jikoni nakuandalia chakula.
"" Samahani Tena princess, niahidi basi, kama hautatoroka utabaki, na Mimi, usiniharibie kazi nakuomba tafadhari.
""Muda wote nlikuwa mbali kimawazo, baadae nasituka hivi, nikakuta nmekubali "" kweli ntakaa mikononi mwako siku zote!!"
""Piniety, "alinikumbatia kwa hisia Kali na kusema ahsante Sana princess, nimefurahi kusikia hivo Basi tufurahi kwa kinywaji.
***** ****** ****** ******* ********
Upande wa Malkia, alionekana akizunguza, na mwanamama mmoja umri wake ulikuwa umeeda kukoma kuzaa, mazungumzo yao yalikuwa hivi""
"""Malkia "" Mimi tayari nimeshaanza kuwa na wasiwasi na hii kazi tunayoifanya, hivi kwa mfano prince Nillylan, akitoka masomoni akifika akampenda princess itakuwaje , na mpango wetu, tunajua hawezi kumpenda kweli mTanzania, na option ya mwisho sisi lazma tumchague binti yako aolewe awe princess, na akishaolewa tayari ntapata fungu hapo.
""Wewe usijali, Mtukufu Malkia, kwa kuwa hujapata mtoto, na hauna uwezo wa kumzalia mfalme, naamini tukifanikiwa kwa hili, Malkia wa Nillylan, kumuondosha ni vyepesi, isitoshe haoni, ni kipofu.
""Malkia, akadakia kwa kusema, "" hakika nakukubali Sana, kama uliweza mwagia tindikali na hakuna aliyetuhisi, lazma tutafanikiwa hata na kwa hili.
"""Vipi, kuhusu na huyu prince Nicklan, mdogo wake prince Nillylan""
""'hahaaaaa!! Bado mdogo Sana, si itakuwa tayari, ufalme upo mikononi mwetu, yule ni kumbeba tu.
""" Basi, usiniangushe, ngoja nikaaongee na mfalme, tuweke sawa maandalizi, imebaki wiki moja tumpokee prince, tayari masomo kamaliza, harusi ifungwee tuvute shavuu.
"""" Malkia, na mshauri wake , waliagana kwa kicheko, kilichojaa, ushindi, wakiamini tayari ufalme upo mikononi mwao!!"
***** ***** ****** *******
Kwa upande wa mfalme alikuwa, na wake wawili, mke wa Kwanza ni Malkia Cheness, hakubahatika kuzaa, hivo mfalme ilibidi aoe mke wa pili ambae ni Malkia wa Nillylan au Nicklan alibahatika kuwa na watoto wawili wakiume, Mfalme Ana matatizo ya moyo muda wote yeye anashinda kwenye ufalme, zaidi nchi yake inaongozwa zaidi na mawaziri, yaani serikali ya uongozi ndio inashikilia zaidi madaraka ya kuongoza, kwa upande Wa Malkia wa Nillylan, alipata tatizo la kutokuona mara baada ya kumwagiwa Tindikali na mhusika mkuu, ndio tumeona ni Malkia Cheness na mpango mzima ni mama mshauri wake nia na malengo nikupata madaraka kumuuangusha Mfalme, prince Nillylan aoe kwa mshauri wake, kwa kuwa hakupata mtoto, atakatiwa kiasi Cha hadhina katika ufalme, je itawezekana?? Mimi na wewe hatujui Basi songa nayooo Hadi mwisho.......
******* ****** ********
Upande Wa prince Nillylan, alionekana, kakaa na rafiki yake Nellyson, sitori zao zilikuwa hivii;
""Nillylan, sasa naona, tumefikia, tamati hapa, tumemaliza masomo yetu, tayari unarudi, kutumikia nchi yako, na tayari mwali kaandaliwa, siamini kama unaenda kumumiriki princess hafu naskia princess, mwenyewe mTanzania, hahaaaaa!!, Hivi upo tayari kumuacha princess pinty wa kifalme Tena falme yao ina nguvu, Kwanza mnajuana tangu uanze chuo, na mnamaliza wote Sasa, Hivi kweli upo tayari???
""Kiukweli Nellyson, sizani Mimi ntaenda kufanya ndoa fake, harafu narudi kumchukua princess Pinty'' siwezi kuoa, Mtanzania Mimi, harafu mtu mwenyewe simjui!!!"
Baadae alionekana Pinty" anakuja alifika na kusimama nyuma ya Nillylan, na kuanza, kumtengenezea kora ya t-shirt ake, huku akiachia maneno kwa prince Nillylan nakusema """""
""Nillylan, kwahiyo unaondoka, kweli?? na utatimiza ahadi yetu??, Nimeambiwa tayari umeletewa princess wa Kitanzania, na ndio mtegewa awe ubavu wako, je utapingana na falme yako kisa, Mimi?, Kama unajua kabisa ni ngumu, niambie mapema, nianze kukusahau, namimi tayari nimeshaandaliwa prince wa kunioa, nianze kumpenda taratibu japo haitafikia kama wewe ninavyokupenda, niambie please na Nellyson awe shahidi.
"""Prince Nillylan,,, alisimama, na kuinamisha kichwa chini, alimshika mkono Pinty, ishara ya kukubaliana, "" Ndiyo ntafanya hivyo usibadili maamuzi nitakufata katika falme yako na nipo tayari kuunganisha falme yangu na yako liwe taifa moja lenye nguvu moja.
""Naahidi itakuwa ni siku moja utakapoona karibuni ""Anga siku hiyo jua litachomoza, halafu kutatanda giza, na hio siku ni ya kupatwa kwa mwezi, ndio itakuwa ni siku nitakayofunga Safari nakuja kwako princess Pinty!!
""Kwa furaha walikumbatiana wote ishara ya kufurahia ahadi yao, waliagana kwa furaha na hatimaye Kila mtu alierekea kwenye falme yake, Pinty na Nellyson walikuwa wanakaa falme moja, Nillylan yeye alikuwa peke yake kwenye falme katika chuo hicho.
******** ********* ******
Siku hiyo ufalme ulikuwa, umechangamka tayari, kumpokea prince takribani miaka mitatu alikuwa masomoni, na huku mipango ya harusi ikiendelea, ratiba ilikuwa ni prince apumnzike siku moja kesho yake harusi na siku inayofuata tayari kutawanzwa, na kuwa mfalme na hii kutokana na mfalme alikuwa kazoofika na maradhi na nchi kupelekea kuendesha zaidi na serikali ya kifalme na kusababisha mambo mengne hasa biashara za jirani na ufalme na falme kwa falme kusitishwa kwa kukosekana kiongozi wa kusimamia biashara hizo.
"" Upande Wa Tinner" ilimlazimu kaandaliwa kuwa princess tayari alikuwa kashajikatia tamaa, na matumaini kabisa ya kurudi Nyumbani hayakuwepo tenaa.
""Siku ya harusi iliwadia ni siku ya huzuni kwa prince Nillylan, muda wote alikuwa kavaa vazi la harusi lakini akili yake ilikuwa muda wote ikimuwaza princess Pinty, pamoja na ahadi walizowekeana, alishikilia nembo aliopewa na Pinty! Mkononi na kunuia kwa kusema""
"""Siamini princess Pinty, kwani mpka muda huu naenda kuoa sijui una khari gani huko?? Mimi ni mtoto tu nafata sheria za ufalme wetu kama ntaweza kunusurika nitakuja kwako, naiweka nembo hii kwa kuifukia chini sehemu ya chumba changu kwa sasa naenda kukaa siku zote katika falme na siku nikirudi hapa nkafukua nikapata nembo hii hakika nitaamini kuwa wewe ni wangu, na nisipoiona Basi haukuwa riziki yangu, nisamehe kwa maneno magumu niliyoyazungumza lakini naamini itakuwa hivyo.
"" Prince Nillylan baada ya kumaliza maagano Yale alierekea tayari kwenye jumba la kifalme kusubiri ndoa.
""" Tayari, Princess Tinner alikuwa kashaandaliwa tayari kupelekwa kwa prince alifungwa kitambaa machoni, asiweze mtambua prince mpka watakavyoamliwa amfunue na kwa prince ilikuwa vivyohivyo.
"" Muda ulifika tayari, prince, princess, waliambiwa Kila mtu ashike kitambaa Cha mwenzake kwa nyuma afungue taratibu kwa ustadi mkubwa, na sisi tunahesabu, moja,mbili, tatu, mtafungua kwa pamoja, baada ya hapo Kila mtu amfunue mwenzake kwa wakati mmoja.
""Moja, mbili,tatu"""
Macho ya prince, na princess yaligongana kwa pamoja Kila mtu akaingiwa na fikra juu ya mwenzake, wote waliduwaaa!!!!!!
,,,,,,,,,,,,Itaendeleeaa,,,,,,,,,
Usikose sehemu inayofuata.
Je, Prince Niylan atakamilisha ahadi yake na Pinty?
Na kuhusu Princess Tinner nini hatima yake katika nchi nyingine itakuwaje? Na vipi kuhusu malkia Cheness?
[1/25, 17:16] Tinner 1: MWANDISHI: TINNER ROBER. SIMULIZI: UPENDO USIOTARAJIA. SEHEMU: 04.
ANZA NAYO.
""Moja, mbili, tatu!! "" Macho ya prince na princess, yaligongana kwa pamoja Kila mtu akaingiwa na fikira juu ya mwenzake wote waliduwaa!!!
"" Upande wa princess Tinner, alizidi kuwaza, daaaah! Mbona prince ni mzuri hivi nywele zake tu daah! Uso wake ndo kabisaa!!!
hivi kweli ndo naolewa na kijana huyu kweli inaonekana ni mzuri kwangu, aaa aah!! Simtaki Tena narudi zangu Tanzania nmemuacha Joelly'' ananisubili"
Upande wa prince Nillylan pia muda huo alimfikilia Tinner, huyu Mtanzania na macho yake madogo, makubwa hata hayaeleweki, ngozi yake nyeusi japo ana kirangi hivi, uso wake sijui hajapakaa vizuri mafuta mpka vidoti vyaonekana, nywele yake inaonekana ngumu daah!! Lazima ntamfanya kuwa mtumwa wangu na huyu ndio ataniletea pinty wangu.
***
Sherehe zilizidi kupamba Moto zawadi mbalimbali zilizidi kutolewa, hatimaye sherehe ilifika ukingoni tayari prince na princess walipelekwa katika jumba lao zuri liliandaliwa kwa wapendanao, chumba maalumu kiliandaliwa kwa usiku wa wanandoa, Kila aina ya chakula kiliwekwa mahali pale, mapambo mengi ya dhahabu yalisheheni sehemu hiyo na mavazi yaliandaliwa maalumu kwa wanandoa kwa ujumla Kila kitu hakikukosekana katika chumba hicho.
"Mazungumzo kati ya wanandoa yalianza;
Nillylan
"" Wewe Mtanzania, (alipenda kutumia jina hili akimanisha Princess Tinner) kilichokutoa huko kwenu, huku umefata nini huku? Au Kwenu mna dhiki et?, halafu nasikia Tanzania ni nchi maskini Sana ndo umeamua kuja kuomba msaada huku?, Hivi Una wazazi kweli wewe??
Harafu Kwenye sherehe sijaona ndugu zako zaidi ya kubebwa na Malkia Cheness? Na hapa unazani ukiolewa na Mimi ndo utaondokana na umaskini wa huko kwenu? Sawa nataka nkupatie kazi, nataka wewe ndo uniletee mwanamke nmpendae yupo Korea kusini anaitwa pinty ukinisaidia kwa hili tayari utaishi na Mimi kama kijakazi wangu, lakini ukinifurahisha kwa kazi zangu ntakupa cheo uwe mlinzi wangu sawaa Mtanzania!!?
''Huku akimshika Tinner sikio, nataka sikio lako liwe pana na uweze kunielewa kwa Kila nikisemacho na hii kichwa yako iwe
inatunza kumbukumbu vizuri na ndio sifa ya kuitwa princess, sio unakujakuja tu hujui hata sheria za maprincess, umenielewa ee!, Kisha alimwachia kwa kumsukuma huku akiachia tabasamu na kujitupia kitandani.
,,,Upande wa Tinner, muda wote machozi, yalizidi kutililika na kusababisha macho yake kuwa mekundu, na uso wake ulilowa hata makeup yote ilififia kwa machozi Yale na kuacha uchumvichumvi, kwake ilikuwa ni huzuni na majonzi, alikumbuka Nyumbani wazazi wake walivyouwawa kiukatili pamoja na ndugu zake na wageni walioalikwa kwenye sherehe siku hiyo na kusababisha kuwapoteza wote, pamoja na rafiki yake wa dhati Jescar, na zaidi hakujua kilichoendelea baada ya kutoka kule. Alijitahidi kuficha huzuni yake lakini ilishindikana nakumpelekea kupaza sauti huku akilia nakusema """
""Mama, baba kwanini mmeniacha nikiwa katika wimbi la huzuni siku zote au nlikosea kuwaambia mnifanyie sherehe ya kuzaliwa kwangu?, na hi ndio siku ilionisababishia kwangu iwe ni siku ya huzuni siku zote, sitamani hata nisikie siku na mwezi niliozaliwa kama siku hi ifike tena.
""Yuko wapi rafiki yangu kipenzi Jescar, niliekuwa nacheka nae, tukitaniana nae kwa furaha, nlipokuwa na huzuni alikuja akinitania Mwanabudagala, nayeye namtania mwanalena, hapo hapo furaha inarejea,
""najua Jescar, nlikuacha umezrai hebu Rudi leo unitanie Tena, najua unanimisi kipenzi chako, nakumisi pia na hayo macho yako makubwa ulikuwa ukiyatoa darasani mpka mwalimu anaogopa kukuuliza swali, nakumisi karembo kangu, tafadhari nakungoja uje unipe ujasili wa kuishi na hiki kiumbe kinachoanza kunivuruga mapema ningali Bado nawaza wazazi wangu na ndugu zangu wote waliopotea siku hiyo,
""umenifundisha ujasili et dawa ya Moto ni Moto je nmuwashie huyu Nillylan? Na nikiwasha je, hiki kiumbe Cha huku korea' kinajuaga Moto wa huko Tanzania??
Muda huo Tinner alilia Sana bila matumaini yoyote mpaka sauti yake ilianza kukwarua na kubaki machozi yakimtililika tu.
""""Prince Nillylan, muda wote alikuwa akimsikilizia Tinner, kama hasikii kwa kile alichokuwa anakizungumza taratibu aliinuka na kumwangalia huku akitikisa kichwa Kisha alichukua Tauro na kuelekea bafuni kuoga.
Tinner, alijivuta taratibu kuelekea kwenye kabati la nguo nakutoa mavazi Yale ya harusi na kuvaa mavazi ya kawaida, aliamua Bora hata atoke nje kupunguza msongo wa mawazo, apunge upepo lakini tayali chumba Chao kilifungwa kwa nje, kiliwekwa kwa imani za wanandoa. Ilibidi arudi na kujipumnzisha kwenye sofa hatimaye usingizi ulimchukua kutokana na uchovu wa hapa na pale mwili na akili kwa pamoja ziiihitaji mapumnziko.
""Prince Nillylan, alitoka bafuni, na kuelekea kwenye kabati lake la nguo ili abadilishe mavazi ya harusi avae vazi la kawaida, Kisha Alikaa kitandani alale, kwa pembeni alimuona Tinner kapitiwa usingizi kalala kwenye sofa, taratibu aliinuka na kuchukua blanketi na kumufunika huku akimfuta machozi na kusema "" Inaonekana una shida kweli kwani kipi kimekusibu mpaka uwe katika khari hii!!??"
SONGA NAYO NO 5.
MWANDISHI; TINNER ROBER. SIMULIZI: UPENDO USIOTARAJIA. SEHEMU: 05.
*** Upande wa Ufalme, siku hiyo kulikuwa na kikao Cha Baraza la kifalme walikuwa wakipangilia katiba ya nchi pamoja na uongozi mpya utakaofatia wa prince Nillylan na jopo la kumsaidia ikiwa ni pamoja na wazee wenye busara.
Mfalme alitoa hotuba yake, " ndugu zangu wote mliokusanyika hapa na viongozi wa nchi yangu khari yangu naona naelekea kudhoofika kwa maradhi ni siku yoyote mwenyezi mungu atasimamisha uhai wangu, ninaomba kabla haijafika Prince Nillylan mmpe ushirikiano najua akili yake bado haijakaa vizuri kiutawala naomba na prince Nicklan( mdogo wake na Nillylan) mara tu atokapo masomoni afundishwe sheria za kifalme pia naomba princess Tinner, apewe urinzi wa kutosha kama mtawala wa prince halafu naomba kiongozi wa Siri afatilie kuhusu Malkia Cheness nimeanza kuwa na mashaka nae taarifa zake nizipate haraka iwezekanavyo. Na Kikao chetu kwa leo tunaishia hapa.
Upande wa Tinner, tayari aliamka na kukaa kwenye sofa Kisha alianza kuangaza huku na kule alimuona prince bado kalala, alitabasamu tu nakusema kumbe unajali ulinifunika blanketi usiku!!? taratibu aliinuka na kuelekea bafuni kuoga.
""Mlango ulisikika mtu akigonga hodi, princess alielekea mlangoni, kumbe alikuwa ni mtumishi wake Piniety,
" U khari gani mtukufu princess?, tafadhari muandae Prince, pia karibuni chai tayari na leo ni siku ya kunywa pamoja na mfalme na Malkia kwa pamoja wanawasubili.
Tinner, alielekea moja kwa moja Hadi kwa prince na kukaa kitandani, muda huo alikuwa bado kalala, alifika na kuanza kumwangalia tu aliinua mkono wake amuashe lakini alisita kutokana na maneno makali alimpatia ilibidi akae tu asubili atakapoamka lakini nafsi yake ilimuuma taratibu alimgusa begani kumuamsha lakini tayari prince alikuwa kaamka na yeye mbaya zaidi kashikwa bega tayari kiliwaka,
"" We mtanzania, unanipenda ee, unanitaka kwa lazima, mara hii unataka kunichungulia Tena umekaa kitandani kwangu, kitanda Cha gharama? Kwenu mnacho kweli? Jana kukufunika blanketi ndio uanze kusogea karibu yangu haya sogea huko nipishe nioge nivae hafu weka vizuri sura yako tunaenda Kula na mfalme twende ukamuone na mamangu umjue vizuri halafu sitaki mazoea na wa kwetu kama hauna wa kwenu tulia mi ndo nitakuwa wa kwenu et, si Mimi ndo mmeo natakiwa nijue vingi vyako ? namimi ujue vingi vyangu!? ok jiandaee vizuri mrembo wangu wa kitanzania sawa.
" Sawa, nmekuelewa. Prince!!!,
""kwanini lakini muda wote umekuwa mtu wakunionea tu, mara kwetu maskini, nmekuja kwenu kwa matajili, nimekimbia kwetu kisa umaskini hivi wazani ni mtu gani hapendi kwao, hapendi kukaa na wazazi wake, ndugu zake, rafiki zake halafu aje kunyanyasika hivi, tangu nmekaa hapa umewahi kuona nimeingiza utajili gani kwenu, zaidi ya kukaa kama mtumwa tu, wewe Leo hii tumeoana sio kwa ridhaa yako Wala yangu wazani Kila mtu anafurahia ndoa hii?" sawa Sina pakwenda, Sina nauli, sijui hata nyumbani napanda gari au ndege kwenda, Sasa ni hivi na nyumbani sitaenda tena. Najua hakuna furaha zaidi ya majonzi tu, nikheri niwe mtumishi wako kama ulivyosema nikutumikie huenda nitasahau hata vifo vya wazazi wangu.
"Tinner"" alisimama kwa hasira na kuondoka,
"" prince alimuwahi na kumshika mkono na kumsogeza hadi ukutani alichukua kitambaa chake kumfuta usoni machozi yale.
""Naomba uniache, nyie muda wote mnataka nilie Kila siku aya, mna nia gani na Mimi kunitoa kule Tena kwa mateka Hadi hapa mna njama gani hasua malkia Cheness muda wote anataka kuwa upande wangu?
""" Kuwa mpole, unaongea kwa sauti Sana, futa machozi mtanzania, uso wako utakuwa hauvutii Tena kama princess, hebu tabasamu Kwanza nione kabla hatujafika kwa mfalme kweli utavutia kama princess(Pinty) wangu japo wewe ni mtanzania tu!!"".
""Hasira zilizidi kumpanda tinner, kweli prince maneno yake yalikuwa ni yenye kebei kubwa, na kumsababishia kukosa amani hasua alimchukulia Tinner kama taswira ya mwanamke Pinty muda wote Kila kitu kizuri alikifanya kwa kuweka muonekano wa pinty, na zaidi alimchukulia tinner kama mwanamke asielizika na maisha, na muda wote kamkuta Tinner katika falme hajaambiwa kwa undani zaidi ilikuwaje akafika sehemu hiyo.
"'Ilikuwa ni muda wa kupata chai, mfalme, pamoja na wake zake wote waliketi huku prince na princess wakiwa wameki kwenye kiti Cha pamoja,
" Malkia wa Nillylan, alizungumza kwa kusema;
""hongera mwanangu prince Nillylan umeniletea princess Tinner, japo sitamuona kwa macho yangu nina imani ni mtu sahihi anastahili kwako ni mcheshi, mpole hasua katika watanzania huwa ni wavumilivu Sana naimanii ukimshika hakika mtashikamana, vivyohivyo na nchi yetu itakuwa na mshikamano!!".
Upande wa malkia Cheness yeye muda wote, alikuwa akibinua midomo yake huku akimtolea jicho Tinner, moyoni alijisemea kwa kusema ungejua tumekufanya kama chambo tu hapa, nasisi ndo tumeshika ndoano muda wote tunawaloa wote na malkia hajui mchezo unavyoenda hapa mbona ataturahi tu.
""Mfalme hakuwa na maneno mengi ya kusema zaidi alimchagua princess Tinner, awamiminie chai Kisha waendelee na kifungua kinywa na hi huwa ni heshima tosha kwa princess kupewa kazi hii humanisha ni jinsi gani wamekuamini katika falme hiyo.
.
********
Ni miezi mitatu ilipita baada ya prince Nillylan kukabiziwa falme hiyo ikawa mikononi mwake, ni siku nyingine Tena mdogo wake na prince Nillylan yaani Nicklan alikuwa akirejea nyumbani mara tu yakutoka masomoni, walimwandalia tafrija ndogo ya kumpongeza na masomo, pia na kumshukuru kwa kumaliza vizuri masomo yake.
Nillylan, alijitahidi kuhamasisha walinzi kuweka mazingira sawa,
"'Muda huo Tinner alikuwa kakaa na mtumishi wake Piniety alimpenda kweli walipga stori mbalimbali,
Piniety alimuuliza Tinner;
"" Hivi kweli princess usitake kuniambia wewe na prince mnaishi ndani kama kijakazi wake, siku moja nilimuona prince akikuamuru Tena anofoka kwa bahati mbaya kumbe aliniona alinifuata na kunikanya nisimwambie mtu kwa kile nilichokiona, nmekuwa nafanya upelelezi nimegundua kumbe ndo mnavyoishi humu ndani.
"Piniety, "" kwa kuwa umegundua Hilo tafadhari usimwambie mtu yeyote nakuamini Sana lakini mi nishazoea naona kawaida tu.
""Sawa nimekuelewa princess, hivi unajua kuwa mdogo wake Prince, Nicklan anakuja leo? Na huwa ni mcheshi kweli, we utamuona tu, tatitizo lake yeye hapendi kukaa katika falme muda wote anapenda kucheza na watoto wa kike yeye ni kurukaruka tu, yuko kule, yuko hapa, yaaani ukipewa uwe mlinzi wake nawewe utakuwa kama yeye.
Walicheka kwa pamoja,"" hahaha hahaaa! Unajua siku hizi nimekuzoea nakuchukulia kama Jescar rafiki yangu wa huko Tanzania alikuwa akinichekesha kama wewe!""
""Huenda ni Mimi, nimerudi kama yeye" sitori ziliendelea kati ya princess na Piniety zikipamba Moto.
Prince, alifika sehemu ile aliketi Tinner, ""haraka alimshika mkono na kumvuta faragha, nakusema, "" Naona umesahau majukumu yako ya uprincess hujitambui vizuri nyie ndio wale mnaoolewaga wake wapili ili akusaidie majukumu naona umeshidwa.
""Fanya haraka nifate chumbani, nikupe kazi ambayo tangu ufike hapa sijawahi kukupatia.
,,,,,,Itaendelea,,,,,,,,,,,
Usikose sehemu ya 06!!
Nini hatima ya prince Nillylan kwa Tinner ???
[1/25, 17:16] Tinner 1: MWANDISHI: TINNER ROBER. SIMULIZI: UPENDO USIOTARAJIA. SEHEMU: 06.
SONGA NAYO
"Fanya haraka nifate chumbani kwangu, nikupe kazi ambayo tangu ufike hapa sijawahi kukupatia."". ENDELEA
""Tinner, aliongozana na prince Hadi ndani, prince muda wote alikuwa akifoka, "sijui wewe ni mwanamke gani muda wote hujali, hujitambui kama ni princess kiukweli unanichosha, umekaa kaa kama kijakazi tu, sawa nenda kaandae kile chumba Cha pili ndio atakachokuwa anakitumia Nicklan halafu jiweke sawa, Nicklan akifika asinicheke hujapendeza, bora Anicheke nimeoa mtanzania lakini sio umepauka.
" Muda kidogo prince Nicklan, alifika moja kwa moja alienda kumsalimia mfalme na malkia ni siku nyingine alikuwa hajaonana nao, sitori zilikuwa nyingi za hapa na pale.
"Malkia alimsihi akamuone shemeji yake mke wa kakake amsalimie pia.
"Princess alikuwa tayari, kashajiandaa, alimfuata mmewe chumbani kwake, '"" Prince, tayari nakungoja twende.
"Macho ya Prince, yalitua moja kwa moja kwa princess na kubaki kaduwaaa, siku hiyo Tinner alipendeza Sana, alivaa gauni refu liloushika vizuri mwili wake na urefu aliojaliwa nao pamoja na umbo lake lilionesha vizuri hipsi zake, na nywele yake ndefu aliibana kwa mtindo, ni kweli Tinner alikuwa bomba Sana.
"" Sawa nisubili, ndipo Prince anazinduka kwenye mawazo, Kisha aliendelea kutengeneza nywele zake, lakini moyoni aliingiwa na hisia zaidi baada ya kumuona princess, alibaki akitabasamu muda wote na kucheka huku akiendelea kuchana nywele.
" Moja kwa moja walielekea kwenye sherehe iliyokuwa imeandaliwa kumpokea Nicklan, shamrashara za hapa na pale zilizidi kupamba moto.
"Muda huo Prince Nillylan na princess Tinner walikuwa wakiingia sehemu hiyo kwa kwa madaha zaidi Prince alimshika sawasawa mkono Tinner,
"" Tinner alitoa macho tu na kumwangalia Prince usoni, hakuamini kama siku moja angeshikwa mkono namna ile.
""Prince, Nicklan muda wote, alikuwa na hamu Sana amuone shemeji yake, macho alikuwa kakodoa kwa udadisi huku moyoni akisemea " mtanzania huyo anakuwaje Kwanza!? Anakuwa na muonekano gani!?. "" Ile anatazama hivi, hakuamini alimuona kakake anaingia, kwa pembeni kashikilia manzi mrembo, Nillylan alivaa suti ya duck blue, na huku Tinner alivalia gauni lake la gold muda wote lilikuwa likimetameta na kuzidi kumpendezea zaidi, kwa Kila mtu aliekuwa mahali pale wote walivutiwa na muonekano wao kwani ni watu walioendana Sana.
""Moja kwa moja Nicklan, alimuwahi kaka'ke na kumkumbatia kwa furaha huku akimnongoneza sikioni "kweli Kaka umekuwa mkaka mkubwa hadi umeoa lakini ni mrembo kweli, sitaki nisikie Tena unawasiliana na Pinty, laaah! hivyo ntamuoa princess.
""Nillylan muda huo alitabasamu hakuongea chochote, " Nicklan, " mbona umemuogopa shemeji yako?
""Nicklan kama vile alimchelewesha alimsogelea Tinner, na kumkumbatia kwa hisia kweli huku akimnongoneza, ""Hakika kweli we ni mrembo huku akiachia tabasamu kubwa liliojizihilisha wazi ndani yake limejaa upendo.
******
Sherehe iliisha huku Prince Nicklan, aliomba akae pamoja kwenye jumba anapoishi Prince Nillylan na Princess ili wasaidiane katika kazi mbalimbali za kifalme. Nillylan hakuwa mgumu alifurahi Sana kuishi pamoja na ndugu yake, na akiiangalia ni siku nyingi hajakaa nae kwake ilikuwa ni furaha tu.
"" Siku zilizidi kwenda, lakini muda wote Prince Nicklan, alikuwa karibu Sanaa na Princess Tinner, alijitahidi kumuweka upande wake, japo Tinner muda wote alikuwa ni mtu mwenye huzunii siku zote alikumbuka Sana wazazi wake hakumpa muda wa ukaribu tayari alikuwa ameshamuelewa Prince Nicklan alichokuwa akihitaji.
"Siku moja Tinner, aliamua angalau atoke nje ya ufalme, kwa siri na kuwatoloka walinzi wake kwenda kuzuru nje ya Ufalme. Kulikuwa na bustani nzuri ya maua pamoja na swimming pool ilikuwa sehemu ile. Waliweza kuitumia kama ukiona haupo sawa unaenda kulia sehemu ile na kuomba furaha ishamili kama bustani ilivyostawi na furaha ikasitawi vile. Taratibu alifika pale na kukaa huku miguu yake akaiwekea kwenye maji huku akichezea maji Yale, na kusema"
"" Leo nafuta kumbumbuku zote, za wazazi wangu, ndugu zangu, rafiki zangu, wote mliotangulia hakika tutaonana Tena paradiso, nataka nisimame imara sihitaji kulia Lia Tena kuanzia leo ntakuwa mtu wa furaha kama Maua haya yachanuavyo na kupendeza ndivo hivo moyo wangu utakuwa. Alitoa kidani, kilichokuwa shingoni kwake na kukitupa kwenye maji na kusema,
"napoteza ushahidi wa birthday yangu Sasa nmebaki mtupu Sina kumbumbuku hizo Tena.
"Baada ya kumaliza hapo alisitushwa na kishindo kilichokuwa kinafuata sehemu ile alipokaa, aligeuka na kumwona Prince Nicklan, akisogea sehemu aliyokaa,
""Nicklan alikaa karibu na Tinner, huku miguu yake akaiwekea kwenye maji.
""Vipi princess; uliogopa; Baada ya kusikia nakuja hapa!?, muda wote nlikuwa na wewe nakuangalia muda ule unatoka kimya kimya kwenye Ufalme nilitaka nikupe urinzi maana walinzi wako walikuwa mbali na wewe. Hivi huoni hii ni kesi kubwa wakisikia princess yupo nje ya Ufalme huku hauna walinzi mbaya zaidi hata Prince Nillylan hajui kama upo huku, huoni unampa wakati mgumu kakangu?
""Nicklan, najua yote unayoyasema na Mimi nimetoka nikiwa nimefikilia kwanza, nakuomba haya yote niachie mimi najua Kukabiliana nayo.
""Inaonekana una wasiwasi Sana, japo unajiamini, je? unavyojiamini hata mme wako anakuamini? Au uaminifu huu ndo umekuja kuuaminisha kwenye bustani hii?
""Muda wote Tinner, alimuangalia Nicklan asiweze kumumaliza, alisimama na kuondoka.
""Nicklan, alimuvuta mkono Tinner, kwa bahati mbaya alidondokea kwenye maji, na kuanza kutapatapa akihitaji msaada. Taratibu Nicklan alijitupia kwenye maji kuwahi kumuokoa.
'"Tinner hakuwa mtaalamu wa kuogelea tayari alianza kunywa maji, jitihada zilizidi hatimae Nicklan aliweza kumtoa kwenye maji na kumpa huduma ya Kwanza, lakini hazikusaidia kuyatoa maji. Wazo lilimuijia Ilibidi ampatie pumzi kwa njia ya mdomo hi ingesaidia kunusuru maisha ya princess.
"Taratibu alimuweka chali na kuibinya midomo yake sawa kumpatia pumzi, alikutanisha kinywa chake na kinywa Cha Tinner na kumpulizia pumzi kabla hajamaliza;
""sauti ilisikika upande wa pili ikisema, Nicklan, """ Achaaa!!!!!!
,,,,,,, Itaendelea,,,,,,,,
Usikose sehemu ya Saba, unahisi atakuwa nani huyo?.
[1/25, 17:16] Tinner 1: MWANDISHI: TINNER ROBER. SIMULIZI: UPENDO USIOTARAJIA. SEHEMU:07.
SONGA NAYO
""Sauti ilisikika upande wa pili ikisema, "Nicklan, Achaaaa!!!!.
Alikuwa ni Prince Nillylan alifika sehemu hiyoo, Kisha kusogea taratibu alimbeba mke wake na kumuweka kwenye gari huku Tinner akiwa bado hajitambui vizuri.
"'Nicklan, tuondoke sehemu hii siyo nzuri panda upesi"
"Walifika moja kwa moja Hadi nyumbani, Nicklan alimbeba mke wake Hadi chumbani aliamuru mlinzi wake princess amubadilishie nguo.
"'Muda wote yeye alikuwa nje alionekana Ana mawazo Sana, inakuaje Nicklan awe karibu Sana na Tinner, hajui kama yule ni mke wangu hata kama hatuna mahusiano ya ndoa, si lazima amheshimu na Mimi pia aniheshimu lakini huenda ni jinsi anavyohitaji kumfariji muda wote Tinner ni mnyonge tu na Mimi kwake simpi furaha yoyote ile ingali kweli anahitaji kufarijiwa na kujegwa kiuhalisia akae sawa.
Piniety, alifika Hadi kwa Prince, ""Mheshimiwa tayari nimemaliza kazi yangu iliyonituma." "Sawa kaandae chakula cha mgonjwa Kisha niletee hapa upesi.
""Chakula tayari kilifika, Tinner tayari kumbumbuku zake zilimrejea aliikaaa kwa kitako kitandani na kuanza kukumbuka matukio ya siku hiyo, aibu ilimjaa usoni inamaana Prince Nicklan, Leo kagusisha kinywa chake na changu, hasira ilimuingia " ngoja niwe sawa ataniona na yeye.
Prince, alisogea moja kwa moja Hadi kitandani na kukaa, Kisha alisogeza ile meza ya chakula.
"" Vipi Princess, unaendeleaje? Nilikuwa na hofu juu yako et, Basi Kula Kwanza, Alichukua bakuli lililokuwa na supu na kuanza kumnywesha taratibu huku akimsindikizia maneno kadhaa.
" Unaonekana umelia Sana leo, lakini kwanini hukuniambia twende wote bustanini,
""wewe wazani mimi siku zote Nina furaha tu, Nina vitu vingi vya kuwaza hata huu Ufalme nauendeshaje na kwenye huu Ufalme Kuna watu wanahitaji madaraka wanatamani hata kuniangamiza Mimi wachukue madaraka.
"Hivi Kwenye kuomba mazuri umenikumbuka na Mimi? Sawa lakini Muda mwingine ukienda naomba tuongozane ili ukiangukia kwenye maji na mimi nikuokoe.
Prince, alimaliza kumnyeshwa supu ile. "Basi malizia nawewe kwa hii iliyobaki na vitafunwa hivi.
""Muda wote Tinner, alikuwa kimya akimsikiliza Nillylan maongezi yake, aliendelea kunywa supu na vitafunwa,
"'
""mbona unaniangalia Sana leo una muda gani hujaniona, au na Leo unaniona kama mwanamke wako Pinty?
""Nillylan, alibaki kimya tu, Kisha alishusha macho yake chini pasipo majibu yoyote.
""Nimekugusa penyewe mpaka umeanza kuweweseka macho ee, lakini unampenda, hakai na wewe, huna mawasiliano nae, hujui mpka Sasa huko anakufikiliaje, hivi ushawahi jiuliza Nini maana ya mahusiano na upendo, Au kati ya mahusiano na upendo kipi kinaanza na mtu akajua Anapendwa? Najua kwenye UPENDO siku zote hujengwa na vitu vitatu yaani, Mapenzi, hisia, na Matamanio ya kitu unachokiwaza kifanyike!! Vipi hata Wewe unalitambua Hilo???
""No, wewe Mtanzania!!, Usinifundishe, usinipangie hi ni biashara yangu na matumizi yangu ya moyo, Tena Basi umetoshaaa!!!, Aliinuka kwa hasira na kuondoka lakini kwa bahati mbaya alipamia chupa ya chai iliyokuwa chini na kumwagika moja kwa moja miguuni kwa Tinner,
"Tinner, alipiga kelele kwa maumivu Yale,Maaaaaa!! Nakufaaaa!! " Haraka Prince, aligeuka upesi kumsaidia tena alichukua Asali na kumpakaa mguuni, Huku akimfokea" Muda mwingine jilinde nawewe, kwa khari hi utakuwa Kila muda ni wakulia tu, Leo tu umeenda kuomba furaha kwa khari hi furaha utaipata kweli? Ona Sasa utabaki wauguza mguu ndani mpka upone.
""Niombe samahani Kwanza maana wewe ndio chanzo na maneno yako uliokuwa ukiongea na Mimi ndio nikutake radhi kwa kukuunguza na kukupa jeraha hili, Si umekosa Furaha Tena siku ya leo na mpka utakapopona ndo utaipata Tena?
"Sikuomba furaha nipatiwe na mtu Bali nimeomba furaha nitafute mwenyewe, sitegemei furaha kwa mtu kama ndo Kwanza mtu kanikatia furaha yangu mpka kufika hapa ni hila za mtu, wazani huyo mtu nikimtegemea anipatie furaha atanipa?
"Inategemeana na wewe unataka furaha gani, mtu anaweza kukupa furaha pale inapositahili na sio kwa Kila kitu ataweza kukikimu vingine itabidi wewe mwenyewe furaha itoke kwako uzibe sehemu hiyo. Sawa princess"
""Wewe endelea na biashara yako, hapa Kila mtu Ana biashara yake kijakazi na awe kijakazi, mtumwa na awe mtumwa, mtumishi na atumikie serikali yake Basi, mengine ni maneno tu yatabakia na hayatamuinua mtu isipokuwa yatamfikisha sehemu yakutokea lakini Hana wakumvuta akatoka.
******. Korea kusini.*******
Alionekana Dada mmoja muda wote alikuwa kashikilia nembo ya taifa la kina Nillylan, machozi yalikuwa yakimtililika lakini uso wake ulijawa na furaha.
"Mlinzi wake(Peless) alimfuata na kusema, ""leo unaonekana unafuraha Sana Nini chanzo Cha furaha yako Pinty?
"Peless!! "Kweli moyo wangu umejawa na furaha kwani siku niliokuwa naisubili siku nyingi hatimae Leo imewadia.
"Ni siku kama ya leo niliweka maagano na Mtu nimpendae hakika anga na mtume wetu amejibu "Ona leo ni siku ya kupatwa kwa mwezi ni kiza kimetanda naona Prince Nillylan atakuwa anakuja kakamilisha ahadi yake leo.
"Naomba Leo usiku unisindikize tuvuke mto Jabanah japo tutaondoka kwa Siri sana, sitaki Mtu yeyote kwenye Ufalme atuone, kajiandae tafadhari.
,,,,,Itaendelea,,,,,. Usikose sehemu ya nane, Je Nillylan anakumbuka ahadi ile?
[1/25, 17:16] Tinner 1: MWANDISHI: TINNER ROBER. SIMULIZI: UPENDO USIOTARAJIA. SEHEMU: 08.
"'"Songa nayo""
""Naomba leo usiku unisindikize tuvuke mto Jabanah, japo tutaondoka kwa Siri Sana, sitaki Mtu yeyote kwenye Ufalme atuone, " Kajiandae. ENDELEA
''Upande wa Nillylan alikuwa kapumunzika Muda wote aliwaza mambo mengi yaliyopita nyuma mpaka alipofikia, aliwaza mambo mengi mpaka maneno alioyoambiwa na Tinner, lakini fikira zake ziliendelea mbali Kila akijaribu kuwaza zilikuwa zinampeleka moja kwa moja kwa Tinner,
""Unaonekana ni mrembo kweli, mpole lakini mbona Tena unakuwa mkorofi???"
""Alisimama na kuelekea nje kiza kilitanda ingali ni mchana, hapohapo alikumbuka ahadi yake na Pinty, aliingia ndani na kubadili mavazi aanze Safari ya kumtafta Pinty.
""Ghafura Malkia Cheness alifika moja kwa moja kwenye nyumba ya Prince akiwa na mshauri wake.
"" Prince, inaonekana unaharaka Sana wapi unawahi?
"" Samahani Malkia nataka nielekee moja kwa moja kwenye mipaka wa nchi yetu, nikaangalie usalama zaidi nmesikia Kuna taifa linataka kuchukua sehemu hiyo.
'"'Mbona umejiandaa peke yako na Princess yeye yupo wapi?? huyo ni mkeo na anatakiwa ajue mipaka ya nchi yake ili akulinde pia.
Nillylan, aliona wasimshitukie Sana ilibidi amwambie mkewe ajiandae aongozane nae yeye atajua jinsi ya kufanya akifika huko.
HUKU kwa Malkia Cheness na mshenga wake walifurahi Sana baada ya princess na Prince kuondoka.
""Sasa ni wakati wetu huu Malkia, tazama Prince kuondoka hapa tutengeneze mipango yetu kama nilivyokuahidi, binti yangu (Petty) kwa Sasa amekuwa mkubwa nmeshaongea nae japo anaonekana kuwa mgumu kukubaliana, muda wote anasema Nillylan hampendi anamke wake hawezi kumpenda, Sasa nataka Malkia tumia umalkia kumshawishi kwa vitisho vingi mpka ampate Prince, tuweke sawa siku akiludi tu tayari jitihada za Petty kumpata Prince zitakuwepo.
""Tena kwa Mimi, Petty mapema tu atakuwa amenielewa yule ni mtoto tu na yupo chini ya nyanja zangu kwa Hilo usijali.
** **
Upande wa Petty muda wote hakuwahi kabisa kuwa na ndoto ya kuolewa na Nillylan, yeye muda wote alimpenda Nicklan, malengo yake yote yalimuwaza Nicklan kwa kuwa ni Mtu aliesoma nae na wamekuwa wote umri wao ni sawa japo hakuwahi kumwambia. Nicklan yeye alimchukulia Petty rafiki yake na mwanafunzi mwenzie pasipo kujua kuwa Petty anahisia nae mpka muda wote kaweka malengo ya kuolewa nae.
••••••****••••
Upande wa mfalme leo alionekana akizunguka zunguka nje na mkewe kwenye bustani ya maua, mkewe alikuwa haoni ilibidi amshike mkono wakiendelea na mazungumzo.
"Malkia, Kila siku zinavyozidi kusogea naona maradhi yangu ndo yanazidi najitahidi kutumia dawa, lakini bado magonjwa nyemelezi yanazidi na umri nao unachangia ona mwili wangu umezoofika hata hauna nguvu, naumia siku nikiondoka nitakuacha katika wakati mgumu najua tunamaadui wengi nao wapo katika ufalme huu, utanyanyasika Sana lakini mkombozi wako atakuwa ni Princess Tinner, hakikisha anapata urinzi wa kutosha.
Mfalme khari yake ilikuwa mbaya alianza kukohoa na kutapika damu. Walinzi walikimbia na kumpeleka katika nyumba yake, aliitwa daktari wa mfalme tayari kumpa huduma ya Kwanza.
Malkia aliita mtumishi wake amuitie walinzi wa himaya ya kifalme kuweka urinzi zaidi, " Naomba pia uniitie Nicklan na Nillylan mapema iwezekanavyo,
" majibu yalikuja Malkia mtukufu samani yupo Nicklan tu, Nillylan ametoka na Prince wameelekea mpakani kukagua mipaka iliyopo karibu na kaskazini
""Naomba tafadhari afatiliwe na arejeshwe mapema ni ombi la Mfalme"
••••••***•••••
Malkia Cheness alikuwa ndani kakaa na mshauri wake mlango uligongwa, ""Nani huyo Tena?
""Ni Mimi Askari wa kifalme, Kuna shida kidogo Malkia khari ya mfalme sio nzuri tafadhari unaombwa ufike Kuna mazungumzo.
""Sawa najiandaa mapema nakuja""
Malkia alimgeukia mshauri wake kwa furaha na kusema,
"" Kweli dawa ile imefanya kazi, itakuwa ni unga wa mti gani huu? mwanafunzi wetu kajitahidi kufikisha mzigo wetu na huyu tutamtumia vizuri siku zote mpka Prince awe upande wetu.
Prince na Princess walizidi zaidi kutokomea na kuingiwa msituni, huku walinzi walizidi kuwafatilia kwa kasi Sana wakiongozwa na Nicklan.
Walifika kwenye bonde moja pembeni yake Kuna mto na mto ule ndio walipanga kukutana na Pinty, ilibidi washuke kwenye gari na kutembea, Tinner muda wote alikuwa mwenye furaha Sana akifurahia upepo na mandhari ya mazingira Yale pasipo kujua Prince kaja pale kwa malengo yake binafsi.
"Prince, alimgeukia Tinner, " Naomba unisubilie hapa Kama robo saa nakuja tafadhari usitoke hapa.
""Wewe nenda tu hata ukikaa lisaa kwangu sawa tu, mazingira yenyewe yanaruhusu hata kuhamia kabisa.
Nicklan, alivuka mto ule kwa boti, nakuelekea mpkani mwa nchi jilani, alifika pembeni na huo mto baada ya kuuvuka alikaa kwenye mti waliokubaliana watakutana na Pinty, alisubili Sana bila matumaini yoyote Giza lilizidi kutanda huku akivuta subira.
Upande wa Tinner, aliona muda unazidi kwenda aliamua aanze kumfata Nillylan alipoelekea huku akipaza sauti yake akiita Nillylan!!! Nillylan!! Nillylan!! Upo wapi tafadhari nilitania tu uludi baada ya lisaa mi sikumanisha hivo bhana, Njoo Basi tazama imekuwa kiza,
""Alizidi kuita pasipo matumaini yoyote kiza lilizidi, hofu nayo ikazidi kuingia na kuanza kuogopa Kila kitu kilichokuwa mbele yake aliamua kupumzika kwenye mti akaegama baridi nayo ilizidi kumuingia fikra zilienda mbali matukio ya vifo vya wazazi wake vilianza kujirudia kichwani kwake, aliona mama yake siku ya birthday alivokuwa akitokwa na damu pamoja na babake povu lilivokuwa linamtoka, nafsi yake alimuona mama na baba wanakuja kumchukua
""Mama kumbe haukufa siku hiyo, nilijua tu unaigiza wewe na baba leo mmeniijia twende wote, mliniacha nikachukuliwa na huyu Nillylan ona Sasa kanileta msituni niuwawe na wanyama wakali, si bora tu angeniacha nikaendelea kuwa mtumwa wake.
""Tafadhari Mama, Baba Leo twende wote nitoke kwenye hii nchi, "alisimama kumkumbatia mama yake akizani Kweli wapo sehemu ile, " alikutaa anakumbatia hewa ndipo kumbukumbu zinamuijia kumbe naota alizidi kulia kwa sauti, lakini hofu ndio inazidi, hapa niliendelea kulia kwa sauti wanyama wakali watanifuata, alinyamaza na kuanza kutembea usiku huku kawasha simu yake na kuelekea sehemu asipokujua.
Nillylan, alizidi kumgonjea Pinty, pasipo na mategemeo yoyote, tayari alikuwa kachoka ndipo ufahamu wake unamurudia na kukumbuka alikuwa na Tinner, alianza kukimbia usiku ule akiwa na tochi huku akiita Tinner!! Tinner!! Tinner!!, Pasipo na matumaini yoyote, alienda mpka sehemu ile aliyomuacha lakini hakukuta mtu, alizidi kumtafta Kila sehemu mwishoe alikutana na kipande Cha nguo kimeninginia juu ya mti wenye miiba.
,,,,, Itaendelea,,,,,
Usikose sehemu ya Tisa.
[1/25, 17:16] Tinner 1: MWANDISHI: TINNER ROBER. SIMULIZI: UPENDO USIOTARAJIA. SEHEMU: 09.
ANZA NAYO.
Kwa upande wa Pinty, alionekana akiwa na gari akiwahi Kweli akiwa na mlinzi wake Peless,
""Ongeza mwendo Peless, Kama huwezi niachie Mimi usukani.
" Usijali princess nawahi Sana nikiongeza spidi tutaumia, kumbuka itakuwa shida kwenye Ufalme na hapa tumetoloka.
"" Sawa jitahidi Mimi namjua vizuri Nillylan huwa ni mtu wa kuzira siku zote nina hofu et.
"" Hofu gani Kama anakupenda kweli lazima asubili Hadi kupambazuke, lakini Kama hakupendi ataondoka,
"" Ikiwa ataondoka, kwanini lakini asisubili akajua kipi kimenisibu mpka nichelewe kufika. "" Halafu Nina hofu nahisi Kuna mtu anatufatilia ilikuwaje gari wakati naenda kuangalia Ile Usiku ilikuwa haina pancha hafu tuikute ina pancha Tena na hamna mtu alietoka nayo.
"" Mhuuu, au atakuwa Nellyson, maana huwa anakupendaga Sana toka mme chuoni amekuwa mtu wakukuchukulia uangalifu siku zote.
""Ushaanza, Mimi Nellyson, anajua kabisa nampenda Nillylan, Hadi niliamua niwaunganishe wawe marafiki ili asiendelee kunisumbua, nahisi atakuwa ni yeye na hakuna mtu aliekuwa anajua siku Kama ya leo tutakutana hapa na Nillylan na yeye alikuwepo kama mashahidi siku yenyewe twaahidiana.
""Basi ndo ushaharibu, unazani yeye Kama anakupenda atavumilia hili tukio alione mbele ya macho yake na wakati na yeye ni mwanaume Kama Nillylan tu. Halafu mbona Nellyson ni kijana mzuri tu anaonekana ni handsome Kila mtu kwenye utawala wetu wabinti hati kinamama wanampenda isipokuwa wewe tu sijui unashida gani.
"Kwahiyo na wewe Peless, unampenda Nellyson?
"Ndio, natamani hata Sasa hivi aniambie ananipenda nitafurahi Sana, nimefanya Kila njia kumuoneshea nampenda lakini hakujari hisia zangu hata kidogo, mtu muda wote yupogi siliazi tu.
"'Makubwa!!! Nellyson kwangu hata siku moja sijawahi kuwa na hisia nae hata kidogo, hata kumuwaza tu siku niwe nae sijawahi waza, wewe mpende tu nitakuunganisha nae najua kwangu waga ni zaifu usiwaze kwa hilo.
"" Nitafurahi sana, Kama utafanya hivo lakini naona tayari tumefika mti wenyewe ule pale mie nitakungoja hapa nenda mkamalizane ukirudi njoo na Pete ya uchumba tu, Mimi nipeleke kwa Nellyson.
Pinty, alifika kwenye mti ule alianza kuangaza huku na kule haoni mtu alianza kuita kwa sauti "" Nillylan!! Nillylan!! Nillylan!! Ni Mimi Pinty nimefika.
Aliendelea kusubili pasipo majibu yoyote muda ulizi kwenda mpka Peless alichoka kumsubili aliamua kumfuata sehemu ile,
""Vipi haijafika bado??, Hapohapo Pinty alianza kulia, nilikuambiwa Nillylan ni mtu wa kuzira ona Sasa tayari ameondoka kashidwa kunisubili matokeo yake kaacha kitambulisho chake tu,
"' Nillylan wewe mwanaume gani hauna subira, hujui kusubili, kichwa yako waga inawaza nini? hivi haraka gani hiyo uliokuwa nayo au Umeanza kumpenda Mtanzania wako? Inaonekana kakuvutia ee, kwani Mimi sio mzuri hata usiniwazie!!, siku zote nilijua tu una utani mwingi nikakuchukulia ndivyo ulivyo kumbe uliniigizia unanipenda kupitia utani wako? Hivi Mimi kukwambia nakupenda ulijua natania, aliendelea kulalamika.
Pinty, inatosha huyo kaenda, jikaze twende atarudi Tena Kama anakupenda, usilie huenda Kuna kitu kimemsibu hebu angalia yeye huko hajui Kama sisi gari yetu ilikuwa mbovu tukakawia kufika vivyohivyo hata kwake.
Safari ilianza kurudi kwenye Ufalme, njia nzima Pinty alikuwa akilia kwa huzunii Sana mpka walifika ingawa khari yake haikuwa nzuri ilimpelekea kuugua homa, alipatiwa dawa za kutuliza maumivu Hadi akawa sawa.
Upande wa Nicklan, alifika sehemu ile akiwa pamoja na walinzi ilikuwa ni asubuhi kumepanzuka walikuta Kuna gari ya Nillylan, imepakiwa alichungulia kwenye gari lakini hawakuona mtu, Nicklan aliamulu walinzi wake wasambae huku na kule kuwatafuta.
Msako wa hapa na pale uliendelea bila matumaini yoyote, walitafta huku na kule matokeo yake walikutana wao kwa wao, Prince Nicklan aliamulu wazidi kuingia polini Kila mtu ajichukulie ungalifu wake.
Princess Tinner, muda ule alichoka kutembea aliamua apumnzike kwenye mti taratibu usingizi ulimchukua alikuja kuzinduka ni asubuhi njaa inamuuma, aliangaza huku na kule aliona mti wa mbuyu ulikuwa na matunda yake tayari yaliwiva, aliokota yaliokuwa chini na kuanza be Kula, kiu nayo ilianza kumsumbua alikumbuka mto sehemu alipouacha ni mbali ilibidi aanze kurudi taratibu akijivuta mwili wake ulikuwa umechoka Sana.
Nillylan yeye muda wote alikuwa akihangaika huku na kule akiaangaza Kama atamuona Tinner, alizidi kujilaumu "" Nisamehe Tinner sikujua kwa kile nitakachofanya kitanipa wakati mgumu Kama huu, najilaumu hata kukuleta huku si bora ningehangaika mwenyewe, " Hebu mwangalie Pinty nayeye hakutokea matokeo yake nimepigwa baridi, sijajua kwako una khari gani au wanyama wakali wamekuzuru nimeona nguo yako umeniachia kitambaa tu tafadhari Naomba uishi tu mpka nkupate Kuna kitu nataka nkwambie, nguvu zilianza kumuishia hapo hapo alianguka chini na kuzimia.
Mlinzi mmoja alikuwa anaelekea usawa wa Nillylan, alitupa jicho pembeni alimuona Nillylan kalala, alimsogelea na kumushika mkono kifuani mapigo yake yalikuwa chini Sana ilibidi amuinue na kumbeba moja kwa moja kumpeleka kwenye gari. Alifika pale na kuwakuta walinzi wawili wakiwa wamechoka Sana
" " Vipi Prince Nicklan yupo wapi yeye? ,
" mpaka Sasa hatujamuona pamoja na princess pia hajapatikana. Me
" Itabidi tusubili hapa Kama robo saa tusije potezana akikawia tumufuate kwa pamoja.
"Nicklan yeye alizidi kumtafuta ndugu yake kwa bidii moyo wake ulijawa na hofu muda wote aliwaza huenda kaliwa na wanyama wakali, ni mtu aliekuwa akimtegemea Sana na hata falme muda huo inamuhitaji hapo hapo alichanganyikiwa machozi yalitililika, alijipa ushujaa na kuanza kumuomba mungu anusulu uhaii wa kakake. Mbele kidogo aliona nyani wakiwa wanacheza huku wakiruka ruka aliamua asogee kalibu kuwashangaaa.
""Ghafura aliduwaa alimuona Tinner, kalala chini halafu watoto wa nyani walikuwa wakimchezea huku wakimshikashika mashavuni na kumkwarua kwa makucha alichukua mti na kuanza kuwalushia Kisha walisambaa wote, alifika mpka pale na kuanza kumwangalia tu Tinner, huluma ilimwingia na kuanza kumfuta machozi pamoja na damu zilizokuwa zikimtoka kwenye mikwaluzo, alishika mapigo ya moyo yalikuwa chini Sana na joto lilikuwa limepanda alifanya upesi alimbemba na kumpeleka kwenye gari.
Nillylan aliamka, na kuanza kuwasumbua walinzi, " Niacheni nikamtafute Tinner, halafu mdogo wangu yupo wapi? Mumewateka? Walinzi walizidi kumzuia asitoke mahali pale, Mlinzi mmoja alimuona kwa mbali Nicklan anakuja lakini alionekana kachoka Sana aliwahi kumfuata pamoja na Nillylan lakini Nicklan alikuwa tayari kachoka alianguka chini na kuzimia.
""Haraka walinzi walimuwahi kumubeba kumpeleka kwenye gari, kwa Nillylan akili yake ilikuwa kwa Tinner, alifika na kuanza kulia Kila akimtazama alizidi kuchanganyikiwa hasua akiangalia uso wake umejaa mikwaluzo, Alimuinamia na kumkiss kwenye paji la uso na kusema, " Tinner nahisi kukupenda, hakika huu ni "UPENDO USIOTARAJIA"
"""" Itaendelea""""""
Usikose sehemu ya 10.
[1/25, 17:16] Tinner 1: MWANDISHI: TINNER ROBER. SIMULIZI: UPENDO USIOTARAJIA. SEHEMU:10
Songa nayo.
Safari ilizidi kusogea, Nicklan pamoja na Tinner walikuwa bado wamezimia. Lakini muda wote Nillylan alikuwa macho aliikaa katikati huku alimuegemeza Tinner kwenye paja lake la kushoto na Nicklan kwenye paja la kulia alikuwa muda wote alikuwa akiwatazama kwa huluma huku akiwapepea na mkoti wake na kusema,
"" wote mmeumia kwaajili yangu lazima muwe sawa, nitahakikisha nawapambania mpka afya zenu ziimalike".
Hatimaye walifika kwenye Ufalme Kila mtu alikuwa na hamu kuwaona, hasa mfalme alihofia Sana angewapoteza wanae ilihali anategemea wawe watawala. Moja kwa moja tabibu wa kifalme aliitwa na kuamliwa na mfalme awaangalie afya zao maana wote walikuwa wapo hoi pamoja na njaa Kali,
""Kila Mtu alihoji kipi kilijili mpka wamekuwa katika khari ile, walinzi wote walikatazwa na Prince Nillylan wasiseme kilichokuwa kule na hi ilibaki sili yao tu, maana wangesema wangemchafua Prince ingali ndio mtawala anategemewa leo hii ameenda kwa mwanamke asiejulikana katika Ufalme na si mke wa ndoa ingeleta taharuki. Hata Mfalme nayeye hakujua Prince be alienda kufanyanini zaidi alienda kuzuru mpakani na kukagua mipaka na mkewe.
Matibabu yalizidi kuendelea, Prince Nicklan na Nillylan wao walikuwa wanaendelea vizuri isipokuwa kwa Tinner yeye alikuwa bado hajazinduka ni siku ya nne alikuwa amelala kitandani, kumbukumbu zilianza kumrejea hasa za marehemu Baba na mamake alianza kulia na kusema
'"Tafadhari mama baki na Mimi usiniache Tena na leo Kama ulivyoniacha polini,
""Muda wote Nillylan alikuwa karibu akiangalia usalama wa mkewe, alimuona akiweweseka alisogea karibu zaidi kumutazama. Tinner alifungwa macho yake huku na kule akishangaa mazingira, alimuona Nillylan yupo karibu na kumuuliza;
Nipo wapi hapa?,
"" Upo mahali salama tayari tupo kwenye Ufalme.
"" Nani kakwambia nataka nikae ufalmeni,
""Wewe ulitaka ukae wapi?
""Polini.
Nillylan alizidi kuumia Sana kutokana na majibu ya Tinner, aliona asiendeleze mjadala wangefika mbali Sana,
""Naona bado akili yako haijakaa sawa pumunzika Kwanza nakuja.
Alitoka nje na kumuita Mlinzi wake, Piniety!!, tafadhari Tinner ameamka mwandalie chakula umpelekee hakikisha anakula vizuri na anashiba.
"" Sawa mheshimiwa nitafanya Kama ulivyosema, Piniety alikuwa na maswali mengi ya kujiuliza inaonekana dhahiri kwa Sasa Prince unajali Sana kuhusu Princess,
"" Hawa watapendana tu, naona Kuna utarajio wa wawili Hawa kupendana""
Muda kidogo Prince Nillylan, walipishana Na Nicklan akiwa anatoka na yeye anaingia kujua maendeleo ya mgonjwa.
"Vipi Kaka, Princess anaendeleaje?
'"Mungu anasaidia kwa Sasa kaamka pita umsalimie.
""Ni Jambo jema muda wote nimekuwa nikiwaza Sana juu yake, badae Kaka nikuone Nina maongezi na wewe.
""Nipo hapa nje, utaniulizia ukinihitaji. Nillylan alikaa nje kwenye jiwe kubwa muda wote alikuwa na mawazo Sana. Akijiuliza mambo mengi Sana "" Nifanye kitu gani kwako Tinner uniamini, Hata nikikueleza hisia zangu kwako sizani Kama utanielewa.
"Alisitushwa na sauti nyuma yake ikimuita Nillylan mbona umekaa pekee, alikuwa ni Petty.
"""Oooh!!! Kumbe ni wewe karibu tuketi, sema nilikuwa naota jua la asubuhi ndo maana umenikuta hapa.
"" Tunaweza kuongozana na wewe tukiota jua woteee?
"""Haina shida Basi twende!! ( Prince alimchukulia Petty Kama Dada yake kutokana na ukaribu wa mama yake Cheness kwa mamake Petty Ani mshauri wa Malkia Cheness halafu ni rafiki yake na Nicklan, pasipokujua kuwa yupo mtengoni )
Nicklan, alifika moja kwa moja kitandani alipokuwa amelala, princess Tinner, unaendeleaje khari yako?
" " Naendelea vizuri kwa Sasa ingali bado mwili una maumivu.
Nicklan; alimshika Tinner, mkono na kuuelekeza kwenye mkono wake na kuanza kumbinya binya inaonekana damu yako imepungua jitahidi ule matunda ya kuongeza damu pamoja na chakula. Kisha aliuludisha mkono wake kitandani na kuchukua parachichi nakumenya alimaliza na kuchukua kipande,
"inaonekana hauli Sana nataka ule na Mimi naona, Basi achama ule kipande hiki.""
"Tinner, aliachama taratibu Nicklan alimlisha, kwa pamoja walicheka; Hapo sawa nimefurahi Basi malizia peke yako vipande hivi.
""Nicklan Kuna kitu nataka nikuulize?"
""Naam!'' Ulizaaa.
""Hivi siku ile ni wewe uliniokoa katika pori lile? Kumbukumbu zangu Kila nikiwaza naona ni Kama wewe ulinibeba, unaweza niambia muda huo Nillylan alikuwa wapi mpaka unaniokoa??"
Nillylan, alikuwa tayari amerudi alikuwa akiangalia Kila kitu kilichokuwa kinaendelea mahali pale,
kwa Nicklan alihisi Kuna mtu sehemu ile, alibadilisha maada kabisa na kumjibu Tinner.
"" Kweli kumbukumbu zako hazijakaa sawa aliekuokoa alikuwa ni Nillylan, ndio aliekubeba mimi, nilitumwa na Mfalme kuja kuwarudisha khari ya mfalme haikuwa vizuri aliamuru mtafutwe na mrudishwe ufalmeni ile nafika kuwasaidia Prince alikuwa amekubeba mgongoni, kutokana na umbali alichoka na kuanguka Mimi na walinzi tulitoa msaada wa kuwabeba Hadi kwenye gari Kisha kuwaleta hapa.
(Nicklan aliamua abadilishe ukweli kuwa uongo baada ya kumuona kakake amesimama akiwaangalia, aliweza kutambua dhahiri kwa Sasa Nillylan anampenda Tinner, toka watoke porini hisia zake zipo kwake )
,,,,,, Itaendelea,,,,
Usikose sehemu ya 11.
SONGA NAYO......
MWANDISHI: TINNER ROBER. SIMULIZI: UPENDO USIOTAJIA. SEHEMU: 11
Songa nayo.
Taratibu usingizi ulimpitia Tinner, Nillylan alifika mpaka kitandani na kumuuliza mdogo wake Nicklan,
"Inaonekana kwa Sasa yupo vizuri mgonjwa anaweza hata kucheka.
""Ndio kwa Sasa yupo vizuri akiendelea hivi atakuwa kapona.
Nillylan aliuchukua mguu wa Tinner, na kuuweka taratibu kwenye kiti, huku akimuonesha Nicklan, naona mguu wake bado hajapona ni muda umekua tangu aungue chai ngoja nimuoshee dawa leo akiwa bado kalala.
"Nicklan, alimtania kaka yake,
" we nae muoga kweli kumuoshea mpka alale subili aamke ndo umuoshee, hutaki mchumba akuone unavyo mgusagusa!!!.""
Huyu mchumba, Ananichukia Sana nataka nimtongoze upya, tuanze uchumba mwishoe ndoa halali.
" Naona kwa Sasa Kaka unampenda Sana Tinner, umekuwa ni mtu unaejali Sana kuhusu yeye, sawa ngoja nikuletee boksi la huduma ya Kwanza uendelee na matibabu, nitakutafuta baadae tuongee.
Huduma iliendelea huku Nillylan alikuwa bize Sana akisafisha kidonda,
Tinner aliaamshwa kwa Yale maumivu ya dawa,
"" kumbe ni wewe!!!, mbona hujaniamsha wakati unataka kunioshea??"
"" Sikutaka nikuhalibie usingizi, wewe tulia nikuhudumie Kisha upumunzike.
""Basi, fanya taratibu naumia et,
""Usijali, Hivi Tinner, Unaweza kunipenda tenaa?
""Kukupenda vipi?
""Siku zote unanichukulia Kama Prince, au Nillylan, vipi siku ukinichukulia Kama mme, na ukaacha kuniita majina unayoniita utakuwa umekosea???"
""Mbona umekaa kimya tu nimekuuzi? sawa!!! pumunzika mi nishamaliza kazi yangu kesho jiandae ninakurudisha nyumbabi kwako, Dokta kaniambia umekuwa sawa atanipa dawa za maumivu utatumia, ni siku nyingi zimekuwa tangu utoke porini upo hapa kwa Dokta na Mimi nakuhitaji kwangu kwa sasa nikakuuguze!!!"
"'Nitarudi vipi ningali siwezi kutembea vizuri, ni bado natumia mti kutembea halafu mti Dokta bado hajanitengenezea.
""Wewe jua kesho kwako, hata Mimi ninaweza kuwa mti wa kutembelea, una hofu Nini badala niwaze Mimi unaenda kuishije huko??"" Harafu wewe ndo unataka kunipangia ratiba??"
""Ayaa Prince, isiwe kesi naona muda wote umeandaa mgongo wa kunibeba, mbona utachoka tu.
***
Muda kidogo aliingia Malkia Cheness, akiwa na mtoto wa mshauri wake (Petty)
"Siku nyingi sijakuona Princess, u khari gani lakini??"
"" Namshukuru Mungu naendelea vizuri isipokuwa nasikia mguu wangu bado una maumivu.
""Pole sana, kesho unaruhusiwa utaenda kwako, Mimi nimeona ulinzi wa Piniety pekee hautoshi kwako utampatia majukumu mengi yaani akuandalie chakula, bado akuangalie afya yako itakuwa mzigo kwako. Petty kajitolea kwa msaada zaidi utaenda nae kwako yeye atakuwa zaidi akikuhudumia kuhusu afya yako Piniety yeye atabaki na kazi zake,
""Tinner alifurahi kweli, akimshukuru Malkia mara mbilimbili.
""" Nashukuru Sana Malkia kwa upendo wako hakika niliwaza kweli itakuwaje, nilijua naenda kuwa mzigo kwa Piniety Sasa acha apumnzike na kazi zake."""
Siku iliwadia ya Tinner kurudi kwake. Prince tayari alikuwa amefika mapema sehemu ile lakini alishangaa baada ya kumuona Malkia Cheness akiwa na Petty huku wakitoa mizigo na kuleta kwenye gari.
"" Prince, mbona unashangaa, nimeamua nikupatie Petty uende nae yeye atakuwa anamsaidia mkeo katika ugonjwa wake siku akipona tu atarudi nyumbani.
""Malkia, Mimi pia naweza kumchukulia uangalifu Tinner, Wala nisingehitaji msaada wa mtu mwingine, najua hawezi nisumbua kwanini nianze kuwaingiza watu wengine kwenye kazi zisizostahili.
Kaka Nillylan, usiwaze nimeamua Mimi mwenyewe kujitolea usiwe na shaka.
Nillylan alikubali kwa shingo upande, aliwasha gari na kuondoka mpaka kwake, muda wote alitamani nafasi hiyo angeipata ya kumuuguza Tinner angempata haraka, wangewekana kasoro zao wazi, kwa ujio was Petty hapa aliona ni mtihani mwingine.
Moja kwa moja walifika , Piniety alikuwa wa Kwanza kuwapokea na kuwakalibisha ndani, alichukua begi na kuingiza ndani,
Prince, alimuita Piniety, Naomba unisaidie kazi, hamisha vitu vyote vya Tinner chumbani kwake Kisha peleka chumbani kwangu hapa tutamwachia Petty, atakuwa akitumia chumba hiki, Naomba unisaidie kaongee na Tinner akapumunzike chumbani kwake sawa.
Sawa, mheshimiwa nitafanya Kama ulivyosema, Piniety alifanya Kama alivyoagizwa Kila kitu kilikaa mahali pake , kulibakia na vitu baadhi visivyoweza kuhamishika pamoja na vitu vya Petty.
wakati wakupumzika ulifika, Petty alioneshwa chumba chake Cha kupumzikia. Upande wa Tinner yeye alikuwa amekaaa sebuleni akicheki movie, Piniety alimfuata na kusema, Princess twende, ukapumzike tazama ni usiku umeingia.
""Piniety, Kama ndo chumbani kwa Nillylan Mimi siendi, nitalala hapa.""
""Petty nayeye alifika kumbembeleza kwenda kulala, mwishoe alikubali walimpeleka Hadi chumbani Prince alikuwa tayari kalala, alijua angeumiza kichwa tu kumbembeleza Tinner maana ni watu wasioelewana, alifika Petty na Piniety walimsaidia kumpandisha na kulala kitanda chake.
""Chumbani kwa Petty, alionekana ni mtu mwenye furaha Sana alikuwa akirukaruka kitandani na kucheza huku akisemaa;
Hakika hii ndio nafasi niliokuwa natamani niipate Sasa imenikuta hapa lazima nimpate Nicklan ndo mwanaume wa maisha yangu Sasa anaenda kuwa mikoani mwangu, Hizi njama za Malkia na Mama Mimi siziwezi kikubwa mi kumpata Nicklan tu Basi lakini mbona Prince Nillylan na Tinner wanaonekana ni watu wanapendana tu hafu leo hii Mimi nivunje mahusiano yao ntafaidika na nini!, ""Siku zote ndege wafananao huruka pamoja""
( Upande wa Petty ulikuwa mtihani mgumu kuja kuvuruga ndoa ya Prince muda wote alikubali aiingizwe kwenye mpango wa Malkia alikubali lakini Nia yake ilikuwa apate nafasi ya kukaa kwa Nillylan, kigezo Cha kuharibu uhusiano wao lakini wazo lake lilikuwa ni kukaa hapo ili ampate Nicklan kwani na yeye alikuwa akiishi pamoja na Nillylan )
Asubuhi kulipambazuka Petty, alikuwa wa Kwanza kuamka alienda kumgongea Piniety chumbani kwake alimkuta ndo kaamka, walisaidiana kwa pamoja kuandaa chai na kuweka mezani.
Nicklan nayeye aliamka, alikuwa anakimbia akifanya mazoezi mara Petty alimuona dirishani akifanya mazoezi, macho yake yalimtoka na kusema;
"''hakika Umejaaliwa muonekano mzuri kwa Sasa tunaishi wote lazima nifanye kitu kwaajili yako."
Nillylan yeye aliamka mapema, aliinuka na kuelekea Hadi kitanda Cha mkewe, na kuanza kumtengenezea nywele zake zilizokuwa zikikaribia kuingia machoni.
.
"Tinner; " Hivi tutaishi hivi mpaka lini? Hutaki mazoea kabisa na Mimi!! mpaka uniogope kiasi hiki halafu unakataa mbele ya watu kuja chumbani kwako, ukweli Tinner nimeumia Sana usiku wa leo, wewe Njoo ulale Kama hivi Mimi sio msumbufu furaha yangu nikukuona karibu yangu Kama hivi, nataka wewe ndo ugundue Nakupenda kiasi gani huenda na wewe Utafungua moyo wako kwangu.
,,,,Itaendelea,,,,,
Usikose sehemu ya 12.
👇👇👇👇👇