MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: 22. "0746638941"what'sup
ANZA NAYO!!
Leo katika kitengo Cha Utafiti.
Joanyther alikuwa ametulia katika Chumba chake, huku alikuwa amepatiwa kazi ya kukusanya mafile pamoja na specimen zilizokuwa zimetumika siku hiyo.
Wakati yupo Busy kukusanya baadae Mdogo wake Movick alifika pale na kuanza kumsaidia, ilibidi kwanza amuulize swali la kizushi.
"" Hivi Dada Joany!! Ni Nini hatima ya maisha yetu kwa Sasa!! Au maisha yetu siku zote yatazidi kuwa hapa!!??""
Joanyther ilibidi amtizame Mdogo wake kwa Huruma Sana.
"" Hapanaa!! Movick naimani Kuna hatima mbele yetu inakuja!! Wewe usikate tamaa tu.""
"" Sawaa!!! Hafu umejipanga vipi kuhusu ujio wa huyo Maneger anayekuja!! Make katoa order Wewe ndio utampokea, vipi hatakuzuru au Wewe umejipanga vipi??""
"" Movick!!! Naomba uniombee tu!! Sina Cha kufanya na hapa Sina wakunisaidia nikamuepuka huyo Maneger.""
""Daa Joany!!! Mimi ikitokea hivyo naona Ni bora nife tu, sitaki kuona ukatili huo unafanyika mbele yangu!! Vipi ukiniruhusu nimfate Baba!! Haya mengine nisiyaone, naomba useme kitu basiii!! ""
Joanyther ilibidi amtizame Movick alimuona Kama kapandwa na kichaa, ilibidi amkumbatie tu huku akimtia moyo.
"" Niamini Mimi!! Sitaki uniache tena Mdogo wangu!! Baba!! Mama wote wametukimbia tumebaki Mimi na Wewe!! naomba ishi kwa ajili yangu na Mimi niishi kwaajili yako naimani tutafika tu! Swezi kukuangusha Mdogo wangu!! Nikuahidi hakutatokea kitu.""
Muda kidogo Kuna mfanyakazi mmoja alifika pale kumuijia Joanyther. Alimpeleka moja kwa moja Hadi kwenye ofsi kubwa Kisha alimuacha na kuendelea kuzungumza na maboss wake.
"" Joanyther Kuna mgeni kafika hapa anakuomba ukamsaidie kazi, naomba uandae syringe pamoja na dreep za maji Kuna mgonjwa yupo kule anahitaji huduma, nenda ukasaidiane nae pia uwe unakalili kitu anachokuelekeza!!! "Sawaa!!!?""
Joanyther hakuwa na budi Aliondoka na kuelekea Hadi sehemu aliyokuwa kaagizwa, Alifika na kuweka vifaa vyake huku akizidi kuangaza huku na kule.
"" Mbona Hakuna mtu hapa!! Na huyo mgonjwa yupo wapi au Ni mtego!!???""
Mara mlango ulifunguliwa, Aliingia Mbaba mmoja alionekana Ni mtu aliejazia Sana kwa umbo lake, Alifika na kumtizama Joanyther Kisha alimuuliza.
"" Ndio Wewe Joanyther??"
"" Ndio Mimi!!! Kwani ndio Wewe nimeambiwa nakuja kukutana nawee!! Wewe ndio Mr. Jacob???""
"" Yaah!! Hujakosea!! Ndio mimi, Okay nifuate, njoo na vifaa vyako!! ""
Waliondoka Hadi kwenye chumba kimoja, walifika na kuingia, Lakini Mr Jacob alimuaga Joanyther afate baadhi ya vifaa vyake Kwanza kavisahau.
kitandani kulionekana Kuna mtu mmoja alionekana kuwa Ni mgonjwa kalala huku kajifunika shuka gubi.
Joanyther ilibidi amusogelee karibu huku akimtizama yule mgonjwa, alimfunua Taratibu Shuka ile huku Akiwa kajaa hofu Sana.
Lakini alipigwa butwaa Baada ya kumuona Jolvin ndio kalala pale, Woga ulimshika na kutaka kuanza kupiga kelele. Jolvin alimuwahi na kumziba mdomo.
"" Joanyther!!! Nipo kwaajili yako, japokuwa nitakuwa Mbali na Wewe!!, Lakini sitakuacha kamwee!! uharibikiwe katika maisha yako, naomba kaa kimya jifanye Mimi na Wewe hatujuani hata akija Mr Jacob!! Wewe msikilize kwa kila kitu atakachosema, akienda kinyume Mimi nitakusaidia!!"
Muda kidogo Mr.Jacob aliingia huku akiwa ameshikilia vifaa vyake!! Alifika na kuviweka Kisha alichukua BP na kuanza kumpima Mgonjwa wake presha!!, Baada ya kukamilisha vipimo vyake aliingia Ofsini na kukaa huku akiwa anajiuliza maswali mengi Sana.
"" Mbona huyu mgonjwa Presha ake ipo normal tu, hafu haumwi kivile au Kuna kitu kinaendelea hapaa!!??""
Ilibidi amuite Joanyther kwanza Kisha alimpatia Bp mashine na yeye ampime mgonjwa huenda hakili yake haikuwa sawa!!!
Joanyther alimuacha Mr. Jacob akiwa amekaa, Alichukua BP mashine na kuondoka nayo Hadi kitandani kwa Jolvin, Lakini alikuwa akitafakali ujio was Jolvin Sehemu hiyo.
Lakini kwa ile haraka aliyokuwa nayo alijikwaa chini na Kuangusha ile Bp mashine. Sauti ya kuanguka kwa Joanyther ilifika Hadi kwa Mr. Jacob huku akisikika akisema;
""" Kuwa makini Binti!!! Utaharibu hiyo mashine, hafu pima haraka uniletee majibu, ngoja niegeshe kidogo mezani!! Naona usingizi unanielemea.
Baada ya kusikia hivyo, hiyo ikawa pona pona yake, Alifika kitandani kwa Jolvin na kuanza kumgombeza.
"" Sasa!! Inakuwaje? Kwanini umekuja Wewe!!?, kuwa kama mgonjwa Huoni Kama Ni hatari kwa maisha yako, kwani Wewe ulihofia Nini Mpaka umekuja?? Mr. Jacob Ni mtu mzuri mbonaa!! Hawezi nifanyia baya........ Halafu umepona????......"
Jolvin alimwangalia Joanyther, huku akiwa anajiuliza maswali mengi sana. Alimvuta Joanyther na kumsogeza karibu na uso wake huku akiwa amemkazia macho.
"" Wewe!! Utakuwa kipofu Hadi lini Joanyther!!??' Mbona mwepesi Sana kuamini kila mtu!! Mimi nilijua kwa akili yako nisipokuja nitakupoteza tenaa katika maisha yangu, Sitaki umwamini mtu kiurahisi hivyo!! Naomba unipime Presha kwanza !! Hebu leta hio mashine Kwanza,,,,,,
Jolvin alichukua ile BP mashine, Kisha alilifungua na kuifunga na kumpatia Joanyther,
"" Majibu yatasomeka presha ipo chini!! Hapa tayari nishamaliza kuiset hivyo!! Okay!! Peleka majibu.""
Joanyther ilibidi amuite Mr. Jacob, aje ajionee majibu, Baada ya kufika pale Mr Jacob alichukua vipimo na kumpima upyaa.
""" Daaaah!!! Kweli nimepewa mwanafunzi mzuri anayejua kupima, kumbe akili yangu ilikuwa mbali Sana!! Hapa utampatia dawa mgonjwa wetu, halafu presha ake ikikaa normal naomba kesho nitamaliza kazi yangu niliyoijia!!, Now Ni muda wa kupumzika naomba tukapumnzike, mgonjwa yeye atakuwa sawa TU baada ya kunywa dawa!!""
"" Hapana!! Mr. Jacob!! Mgonjwa khari yake sio nzuri!; Nikuombe Kama unauzingizi Wewe kapumnzike tu!! Mimi nitabakia namwangalia.""
Mr. Jacob ilibidi amsogelee Joanyther kwa karibu.
"" Wewe!! Katoto!! Inaonekana hujui Sheria za hapa!! Mgonjwa akifa ndio siku yake imefika!! Mbona tuna akiba nyingi kwenye store!! Tutachukua akiba nyingine!! Kwani yeye haogopi kufa? Kama anaogopa atajisaidia ili anusuru afya ake, Mpaka tutakaporudi!!""
Joanyther alibaki akimshangaa Mr. Jacob, "" Mbona kawa katili hivyo mwanzoni hakuwa hivyoo, sa' huko tunakoenda Si atanizuru!!!? ""
Muda huo huo Mabodyguard wa Mr. Jacob walifika pale na kupaki gari ya kifahari Kisha waliingia Hadi kwenye chumba Cha mgonjwa na kukuta , usitofahamu unaendelea pale.
Bodyguard mmoja alifika pale na kutoa salamu kwa Mr. Jacob.
"" Boss!! Usafiri tayari!! Twakungoja Wewe tu.""
"" Mchukueni huyu Mwanamke mtangulie nae nipo nakuja, ngoja Kwanza nimpatie Dawa huyu mgonjwa!!"
"" Lakini boss!!! Ingependeza tukusubili muende wote!! Make Muda umeenda Sana!! Kurudi tenaa itakuwa Ni usiku Sana!!""
""Basi twende wote tu!! Kwanza naona huyu Binti! Kanichanganya mpaka nimekuwa na hofu!! Mchukueni na huyo mgonjwa, muwekeni kwenye buit ili kesho!! Nitamaliza nae hukohuko!! Sina Muda wakupoteza kwenye mji huu, nataka Sample yake ichukuliwe mapema ipelekwe kwenye chuo Cha uchunguzi haraka!! ""
Msafara wa Mr. Jacob ulifika Hadi kwenye hotel moja kubwa, walifika na kushuka Kisha walimchukua Jolvin na kumbeba na kumpeleka Hadi kwenye chumba kimoja kilichokuwa kimekodiwa siku hiyo. Waliingia Hadi ndani Kisha walimtupa Chini Jolvin Kama mzoga na kuondoka.
Huku Joanytherna yeye Alifika akaingizwa ndani huku kwa chini kabisa Alikuwepo Jolvin kalala Kama mgonjwa, Muda wote Alikuwa akimtazama tu na kuongea pekee.
"" Mbona unateseka Sana kwaajili yangu!! Muda wote unapenda matatizo yakukute, nishakwambia kaa mbali na Mimi lakinii hautaki!! Ona Sasa unahangaika kiasi hiki!!""
Mr. Jacob, Alifika na kuingia na yeye Kisha alichukua dawa na kuichanganya na maji Kisha alimpatia Sindano Joanyther.
""" Naomba umchome Dawa hiyo mgonjwa Presha yake iwe normal.
Baada ya kumaliza kuchanganya dawa Aliingia bafuni kuoga.
Upande wa Joanyther, Alikuwa bado kashikilia ile sindano huku akizidi kutetemeka na machozi yakianza kumtoka.
Ilibidi ajikaze Kisha alimsogelea Jolvin huku kaandaa Sindano tayari kumchoma. Alimtikisa Kwanza Jolvin na kusema.
"" Jolvin Sitaki kuwa msababishi wa matatizo kwako!! Naomba kujitoa kwako kunilinda Mimi!! Naomba huo urinzi unaojitahidi kunipatia Mimi!!! " siku ya leo mpatie Mdogo wangu Movick.""
Kisha aliigeuza ile Sindano Upande wake ili aweze kujidunga, Jolvin akawa amemuwahi Joanyther na kuchukua ile Sindano na kuidunga kwenye Godoro!!
Mr. Jacob aliamua kufungua mlango wa bafuni baada ya kuona Kukulukakala nyingi.
"" Vipi mgonjwa anasumbua kudugwa sindano???""
Joanyther ilibidi ajikaze huku akiwa na hofu kubwa Sana.
"" Alikuwa anasumbua lakini tayari kwa Sasa!!!""
Joanyther alitoka pale na kukaa kwenye sofa huku akiwa analia Sana, kila akimtazama Jolvin alijihisi Ni mkosaji tu kwake.
Mr. Jacob alisikia ile sauti ya Joanyther akiwa analia, Alitoka haraka bafuni na kuvaa nguo zake, Kisha alimsogelea Joanyther mpaka sehemu aliyokuwa kakaa.
"" Ushaanza kulia mapema!! Wazani nitakuacha kwa kuigiza kwako!! Unaonekana Ni kanjanja Sana Wewe!!
Joanyther alizidi kulia huku moyoni akisema. " Mdogo wangu Movick!! Nilikuahidi nitajirinda mwenyewe!! Naimani Hakuharibiki kitu.
Upande wa Mr. Jacob!! Taratibu alianza kupunguza mavazi yake huku akizidi kumsogelea Joanyther na kuanza kumpapasa.
Upande wa Jolvin Alikuwa akishuhudia Mambo yanavyozidi kuendelea hapo. Moyoni alibaki akijisemea."" Hapa nitakuwa mjinga Kama nitashidwa kumsaidia Joanyther, Tena nitakuwa mjinga hata Muda nilioupoteza kuja kunusuru maisha ya Joanyther Kama leo hii nitashidwa kutimiza ndoto yake.
Mr. Jacob alizidi kumsumbua Joanyther kwa ubabe wake aliamua kumbeba na kumpeleka Hadi kitandani huku Joanyther akizidi kupika kelele kuomba msaada
"" Jolvin!! Jolvin!! Mbona naaibishwa huku na Wewe waona Hivi wanipenda kwelii Jolvin??" Niwewe tu nakutegemea Sina mtu mwingine zaidi yako!! Fanya kitu kwaajili yangu please!!!""
Sauti za kuomba msaada zilizidi kupenya masikioni kwa Jolvin.
Jolvin aliamka pale chini Kisha alianza kuangaza huku na kule