Tinner 1: MWANDISHI: TINNER ROBER. SIMULIZI: UPENDO USIOTARAJIA. SEHEMU: 12
Songa nayo,
******
Ni siku nyingne kwenye Ufalme, khari ya mfalme ilikuwa mbaya. Malkia wa Nillylan muda wote alikuwa karibu Sana na mfalme akimwangalia.
""Mfalme baada ya kuona khari yake inazidi kuwa mbaya iliwaita watoto wake pamoja na familia yake kwa ujumla iwe karibu nae.
Prince Nillylan na Nicklan pamoja na Princess Tinner, walihamia kwa mfalme Kama alivyoamulu walifanya hivo. Zilipita siku tatu khari ya Mfalme ilizidi kuwa mbaya, alionekana akikohoa Sana muda huo Mfalme alikuwa peke yake walinzi walikuwa nje.
Malkia wa Nillylan muda huo alikuwa na princess Tinner wakipuga upepo na sitori mbalimbali walikuwa wakiongea, ""'Malkia alifurahishwa Sana na uwepo wa Tinner, alitokea kumpenda Sana na kumuona mfariji mzuri Sana kwake.
Tinner;
"" Malkia hivi unaamini siku moja utaona muda wote najua unatamani unione, halafu mi mwembamba tu Kama wewe, si unamfahamu Petty, najua uliwahi kumuona kabla ungali unaona. Basi na mwili Kama wa Petty, ila yeye Ana nywele nyingi na rangi yake Kama yako kwa Mimi Nina rangi ya Kitanzania tu.
"""Princess, umetoshaaa Hata siku nikikuona upo tofauti mi Nakupenda tu.
Alikuja mlinzi wa Mfalme, alionekana ni mtu mwenye huzuni Sana, ""Malkia mtukufu tumeingiwa na huzuni kubwa mtawala wetu Mfalme ametuyangulia Tafadhari jikaze ukamuone.
""Malkia alipokea taarifa hiyo ilimsitua ilipelekea kupoteza fahamu, haraka Mlinzi na Tinner walisaidiana kumpeleka ndani na kupatiwa huduma.
Upande wa Maprince wawili wote walijawa na huzuni Sana walikuwa wakilia tu na kufarijiwa , Na upande wa Malkia Cheness, alionekana ni mtu mwenye furaha moyoni japo machoni alikuwa akilia sana, kwa watu waliomuona hakika walijua kaguswa Sana na msiba, kwa ujumla Ufalme wote uliingiwa na majonzi Makubwa, Harakati za mazishi zilipangwa kustili mwili wa Mfalme zote zilifanyika mpaka msiba ulimalizika wanakijiji waliendelea na majukumu yao zaidi msiba ukabakia Ufalmeni.
Nillylan, alionekana ni mtu mwenye majonzi Sana akiangalia utawala kwa sasa umebaki mkononi mwake, alikuwa akiwaza Sana mpka Hata hamu ya chakula ilikosekana, khari ile ilimpelekea kuumwa kichwa na kubaki mtu mwenye kulia siku zote na mwili wake kazoofika. Mtu pekee aliyebakia kumfanya awe na furaha alikuwa ni Tinner tu. Tinner alimuonea huruma Sana Nillylan ilibidi achukue majukumu Kama mke amufariji mmewe taratibu alimfuata ili kumuliwaza zaidi.
""Nillylan, utakuwa hivi mpaka lini mmewangu, tazama imeshatokea na nchi yote inakuangalia wewe, wewe ukiwa na huzuni kiasi hiki wazani Nicklan yeye atafanyaje ingali ni mdogo anakuangalia wewe, jikaze mmewangu futa machozi, Mama mwenyewe bado anaumwa muda wote anaamka na kuzimia tumebaki Mimi wewe na Nicklan tushirikiane kwa pamoja amani iludi Tena Kama zamani kufiwa kusikufanye ushindwe kutimiza malengo yako,
""Nakumbuka wewe ulikuwa mshauri wangu pale nilipokosa furaha, uliniambia furaha unaweza kupewa na mtu lakini Kuna furaha ambayo huwezi kupewa isipokuwa inatoka moyoni mwako kwa kuziba pale ambapo mtu anashidwa kupaziba Basi fanya hivyo leo itafute furaha niliyoshidwa kuiziba.
Nillylan,; maneno Yale yalimuingia, alisimama na kumukumbatia Tinner kwa hisia Kali huku akilia na kusema,
'" kweli Tinner sikutambua uchungu wa kupotelewa na wazazi, Mimi nimepoteza mzazi mmoja tu lakini naumia kiasi hiki, wewe umepoteza wazazi wako wawili pamoja na ndugu zako kumbe na wewe ulikuwa unaumia hivi, Nisamehe kwa pale nilipokuuzi nimetoa maneno machafu juu yako, pamoja na familia kwa ujumla Naomba unisamehe, pia nawaombea wazazi wetu wapumunzike mahali salama mwenyezi Mungu awapunguzie na adhabu ya kaburi.
"" Nicklan yeye yupo wapi?? Nina siku sijamuona?
"" Nicklan, yupo na Petty, nimewaona wametoka pamoja.
"" Sawa, Naomba tuongozane twende kwa Malkia nikamjulie khari, sijajua maendeleo yake kwa Sasa.
*****
Malkia Cheness, leo alionekana akiwa na Jopo lake la Siri wamekaa wakijadili, mipango kazaa katika Ufalme wakiongozwa na mshauri wake(Mama Petty). Malkia Cheness alisema; "Jamanii nawashukuru Sana wale wote mliokuwa katika kazi yetu, tumefanikiwa kwa ustadi mkubwa Sana kumuuangusha Mfalme kwa Sasa tumebakiwa na kazi ndogo Sana, naombeni ushirikiano Tena kazi yetu bado haijaisha, tunataka Prince Nillylan amuoe Petty Kisha awe princess na baada ya hapo atamuua Prince Nillylan na utawala wote utakuwa mikononi mwetu, Tumefanikiwa kwa kidogo tumemtuma Petty, akakae kwenye jumba la Prince, mpka amteke Prince amuingize kwenye mahusiano. Naahidi nimeandaa zawadi kubwa tukifanikiwa kazi yetu Kila mtu aliyepo hapa atakuwa kwenye uongozi wa kifalme, Tujipigie makofi kwa hatua hi, nitawaiteni Tena Naomba Kila mtu aendelee na kazi zake na mkumbuke hii Siri Kila mtu akae nayo moyoni kwake.
"'Upande wa Nillylan na Tinner, walionekana Mona kwa moja wakiingia kwenye jumba la Mfalme, lakini kwa muda huo alikuwepo pekee Malkia, waliingia Hadi chumbani, Malkia alikuwa bado kapumunzika walifika na kuketi kitandani, ""Malkia!! Ni Mimi mwanao Nipo hapa na Princess amuka nikuone angalau.
'"'Malkia baada ya kusikia sauti ya mwanae aliamka kwa kujivuta taratibu na kumshika shavuni, akili ilienda mbali muda wote aliwaza ni Mfalme yupo mahali pale, Tafadhari usiniache Tena Mfalme baki na Mimi unanikimbia kisa Mimi sioni, Princess Tinner kaniahidi kuona Tena usikae mbali na Mimi Tena.
""Kweli akili za Malkia zilikuwa mbali Sana, Nillylan alimkumbatia mama yake na kumjibu;
""sawa Malkia sitakuacha Tena Nipo hapa kwaajili yako siku zote.
""Nicklan nayeye aliingia akiwa pamoja na Petty, alifika moja kwa moja nakumuita mama yake alimkumbatia kwa hisia huku akilia;
""Mama hatuwezi kukutenga tazama Mimi Nillylan na Tinner, Tumebakia upande wako hakika hatutakuacha kwa Sasa tumebaki Kama ndugu wa nne naimani Tinner ataziba pengo la upweke lililokuwa limebakia kuwa ni watatu kwa Sasa tuwanne,
""Nillylan, aligeuza shingo na kumuona Tinner, muda wote alikuwa akifurahi na kucheka kwa sauti kwa sauti ya chinichini; "" alimvuta na kumkumbatia kwa furaha,
""Sasa na wewe ni mwanafamilia wa kifalme sogea tujumuike pamoja na Malkia tupate baraka, Malkia aliweka mikono yake juu ya meza na kusema Kila mtu atakae kuwa Upande wangu aweke mkono wake juu yangu Kama ishara ya kuungana, wote walifanya hivo na kufurahia kwa pamoja, furaha ilirejea tena.
""Nicklan, muda huo ndo anakumbuka alikuja, akiwa ameongozana na Petty, Aliamua kumuuliza Tinner. """" Tinner; "mwenzako yupo wapi???.
""Daaah!! Kwa furaha, hii mpka tumemsahau. Lilikuwa Ni jibu la Tinner.
Nillylan, Alijibu.
""Atakuwa ameenda kwenye familia yake na yeye huoni hapa wote tuwanafamilia tu.
""Wote walicheka kwa pamoja"
Petty, kwa Upande wake alikuwa, kaegemea ukutani huku machozi yakimtoka. Aliumia sana muda ule alikuwa pale hasa Nicklan hakuonesha kumjali zaidi alipotambulisha familia kuwa ni wa nne ndio wamebakia mbaya zaidi Tinner, kachukua nafasi ile ya Mfalme kuziba pengo,
""kwanini lakini Nicklan unanifanyia hivi, hisia zangu nakuonesha hujali nmejitahidi kuwa Upande wako wa msiba kukufariji lakini fadhira zangu huzioni.
Nicklan, muda huo alikuwa akimtafuta Petty, huku na kule hatimae alimuona akiwa kaegama ukutani,
""Mbona unalia?; kwaniniii uliondoka hukunisubili wakati tulikuwa wote??"
Petty hakutoa jibu zaidi aliondoka.
Nicklan alizidi kumufuata,
" Sasa ndo uninunie kiasi hiki Hata Kama nilikuacha, Nisamehe basi, nilikuwa na hofu na Mama muda wote ndio maana nimeshidwa kukujali; "Bado umenuna na haunisikii tena sawa" nisikusumbue naona haunijari Tena kwakuwa haujui uchungu wa msiba kwa kuwa haupo kwako. Nicklan aligeuka na kuanza kurudi kwa wenzake.
Petty, aliona ukimya umezidi Nicklan haongei Tena aligeuka na kumuona Nicklan anaishilia, alimkimbilia wangu wangu, Kisha alimurukia kwa kumkumbatia kwa hisia huku akilia na kusema Nicklan;
""Nakupenda""
,,,,,, Itaendelea,,,,,,
Usikose sehemu ya 13.
MWANDISHI: TINNER ROBER. SIMULIZI: UPENDO USIOTARAJIA. SEHEMU: 13.
Songa nayo.
Petty aliona ukimya umezidi Nicklan haongei tena, aligeuka na kumuona Nicklan anaishilia, alikimbia wangu wangu, Kisha alimurukia na kumkumbatia kwa hisia huku akilia na kusema;
""Nicklan, Nakupenda" ENDELEA
Nicklan muda huo alibaki kaduwaaa tu, asiseme chochote alimuachia na kumfuta machozi, sawa Mimi nilikuwa natania tu nilijua ungenifuata.
""Wewe chukulia unatania lakini Mimi sitanii, "Ukweli Nakupenda" wewe nenda lakini ujumbe wangu nimekifisha Naomba ufikilie.
Nicklan alikuwa na mawazo Sana, Mimi nilijua unanitania tu, bado unaendelea kuniambia nizidi fikiria wewe utakuwa kichaa, Mimi muda wote hisia zangu zipo kwa Tinner japo kakangu kashaniwahi lakini tutampenda wote kuliko nikupende wewe.
Leo asubuhi Prince Nillylan aliamua atoke na Princess Tinner, nje kidogo na Ufalme alielekewa katika milima iliyokuwa ikizunguka falme walifika sehemu kulikuwa na nyumba ilionekana kuchakaa, walipaki gari na kuelekea mpka sehemu hiyo walifika na kuingia Hadi ndani.
Tinner; Alihoji, "" mbona kumechakaa Sana japo kwa ndani kunaonekana bado ni pazuri?
"" Mfalme muda mwingi alipenda kuja kuzuru mahali hapa, alifanya vile kipindi kile wakiwa na Malkia (mama yangu)alikuwa akija hapa muda wanapokuwa wametofautiana kidogo katika maongezi na Malkia, lakini Kila siku wakiludi mama alionekana Ana furaha Sana kuliko akiwa anatoka, nimeona nije na wewe hapa nifanye utafiti zaidi kipi kilimfanya mama arudi akiwa na furaha, Naomba uketi unisubili kidogo nakuja.
""Unaniacha Tena na leo unataka unitelekeze Kama siku ile porini?, Lakini bora Hata ukinitelekeza leo nina sehemu ya kupumzika sitaogopa tena na baridi haitaniingia isipokuwa njaa ndio itajiludia kama siku ile. Naomba unitafutie chakula kwanza ndio uende.
""Kuwa na amani na mimi, sitachelewa Tena Kama siku ile nilikusababishia matatizo leo nataka uludi nyumbani ukiwa na furaha. Nillylan aliondoka na kumuacha Tinner akiwa akishangaa mandhari ya jumba lile.
Punde kidogo alirejea akiwa na ndoano mkononi kashikilia samaki wa tatu,
Tinner alimuona Nillylan anakuja alianza kucheka tu,
""kumbe nawewe ni mvuvi? Nilijua Hata maji unaogopa mpka siku ile naokolewa na Nicklan kwenye swimingpool na wewe ulikuwa umefika muda tu inaonekana ulikuwa ukitufuatilia si et?
""Unaonekana siku zote wewe una maneno mengi kunizidi mimi, ila Mimi leo Nina kitabu changu nimekiandika siku nyingi tangu Mtanzania kaingia Korea nilikuwa nakiandika na hapa nataka nielezee vitu nilivyojifunza katika kitabu hicho. Upo tiyari kusikiliza?
""Daaah!!!, Hii itakuwa babu kubwa tangu lini Nillylan akawa mwandishi wa kitabu, yeye muda wote waga ni msikilizaji tu, ayaaa kitabu chenyewe umekipa jina gani Kama wewe ni mwandishi?
""Unataka jina tu, hutaki kujua wahusika waliomo, ok, jina la kitabu nimelipa ""UPENDO USIOTARAJIA"" Umefurahi kusikia hivyo?
""Kawaida tu mbona. Nataka nijue ujumbe uliobeba neno hilo Basi.
Nillylan alianza kuwaandaa samaki wale na kuwachoma kwenye Moto."" Vipi unapenda na wewe samaki wa kuchoma?
"Napenda ndio, lakini muda umeenda tunaondoka sangapi huku?
""Tutaondoka tu lakini mpaka nijue furaha ya mama ilikuwa inatoka wapi ndio tuondoke.
""Tazama ni baridi imekuwa tuondoke. Nillylan, aliona Kama Tinner anazidi kumsumbua alivua koti lake na kumfunika.
""Aya sema Nini Tena unataka??
"" Leo ni siku ya kupatwa kwa mwezi, majira kama haya niliwahi kufanya upuuzi kwa kutokujua hisia zangu nilitaka niende nchi nyingne nikaoe nilitumia ufahari tu wa kwenda kuoa pasipo kusikiliza moyo wangu kipi unataka nilipeana ahadi na mwanamke aitwae Pinty tulikutana chuoni muda wote yeye alikuwa akinipenda Sana Mimi nilimchukulia hivohivo na kumpa kampani ili asiumie muda huo sikuwahi kuwaza kabisa kuwa na mwanamke zaidi ya masomo yangu, siku yenyewe niliamua kwenda nikaonane nae nimwambie ukweli aendelee na mipango yake Mimi bado sijaamua kuwa na mwanamke ndipo alikawia baadae ndo nakuja kukumbuka nimekuacha ukweli nilikuwa na hofu Sana juu yako unajua nilikuwa nakutafuta huku nikiombaje?
"" Unataka niongope, wakati wewe ndo unaongea??"
""Ngoja nikwambie, muda huo nilikuwa nikiomba, Ee Mwenyezi Mungu Naomba umnusuru Tinner na wanyama wakali awe mzima na nikimpata tu lazima nimwambie nampenda.
Na leo ndio nimekuja kukamilisha ahadi yangu nilikosa muda wakusema nimeona niseme leo Tinner,
""Nakupenda"" nimejua hili tangu siku ya harusi yetu ulipofungua kitambaa niliona moyo wangu umekuwa tofauti kabisa hisia zilinijaa Kila nikizikataa zilikuwa zinajiludia, muda wote nimekuwa na hofu nawewe nahisi wivu Sana mpaka kwa mdogo wangu Nicklan sitaki ukaribu huo naumia. Hivi unakumbuka siku yenyewe umeenda bustanini kutafuta furaha, na siku anakulisha kipande Cha parachichi ulivokuwa unacheka kwa furaha, bado siku yenyewe porini Mimi muda wote nilianza kukutafuta baadae nilichoka nikawa nimezimia halafu anakuja Nicklan kakubeba mgongoni ulijua Mimi nilikuwa naumiaje?
""Lakini si Nicklan, alinambia muda wote wewe ulikuwa umenibeba, mpka unaanguka Nicklan ndio alijitokeza kunisaidia?
""Ukweli ndio niliousema hapa;" Nicklan, alifanya hivyo kwa kuwa alijua Nakupenda!! Ila wewe ndio hunielewi!!"".
""Ningekuelewa vipi? Wakati muda wote unamuwaza Pinty mpaka unaanza kunifanya Mimi nisimame Kama mdori wa Pinty unaishi nao???"
""Sikufanya makusudi, muda wote nilitaka nijue unajali kiasi gani kuhusu Mimi lakini ni tofauti hukuumia hataa; zaidi ya kunihamasisha nimfate Pinty. Tuachane na hayo yote hapa tu wawili tu mwanamke na mwanaume Tena ni mke na mme japo tumefunga ndoa muda huo Kila mtu alikuwa hana hisia na mwenzake kwa Sasa naomba turudie harusi yetu tenaa. Au unasemaje?
""Maneno mengi unazani mimi ndo wa kunipimia upendo, harafu ndo uzalishie upendo tena kwangu yaani utoke kwa Pinty uje kwangu!!! harusi sahau Tena Mimi nitabaki kuwa mtumwa wako tu sina hisia na wewe Nina hisia zangu tu pekee.
""No, Tinner inatosha, alisogea karibu na kumukumbatia kwa nguvu, Niamini Sina maana hiyo, Nakupenda ndio zawadi niliyonayo kwako Tafadhari usiendelee kusema maneno makali Kama hunipendi nyamaza nitajua mwenyewe, Lakini Nataka tukitoka hapa tukajiandae nikupeleke nyumbani kwenu ukawaone ndugu zako, japo naomba uniahidi, mama yangu apate kuona pia turudi wote uendelee kukaa na Mimi tena Kama Mlinzi wangu nakupandisha cheo angalau nizidi kukuona japo hunitaki Na hii ndio itakuwa fadhira yangu kwako kukulipa kwa mengi uliyoyafanya katika Ufalme huu.
Huruma ilimwingia Tinner, kumbuka muda wote na yeye alikuwa akimpenda Nillylan, japo walikuwa wanakosana, alikumbuka wema wote aliokuwa akimtendea Hata pale alikuwa kwa daktari Ana mwambia twende nyumbani, anasema Sina mti wa kutembelea, Nillylan alimwambia Hata Mimi nitakuwa mti wako wakutembelea alijikuta anatabasamu na kucheka mwenyewe, moja kwa moja alimufata Nillylan alikuwa ndani akipanga nguo tayari waondoke, alimufata mpka sehemu ile na kumushika kiunoni kwa nyuma huku alimkumbatia, ;"
"Nillylan Nakupenda pia" Sitaki nikupoteze nimekuzoea Sana Sina furaha nyingne zaidi ya wewe.
Nillylan, hakuamini alimkumbatia Tena Tinner kwa furaha Kisha alimbeba na kuanza kumzungusha, " Hakika ndoto yangu ni kuwa na wewe tu na hi ni furaha tosha; naona Kama siku zinachelewa tukitoka tu Tanzania tufanye bonge la harusi nakumiliki mazima mpaka kifo.
Stori ziliendelea mpaka kesho yake walianza Safari ya kurudi njiani kote walikuwa na furaha pamoja na utani wa hapa na pale.
Nillylan alikuwa akiongea pekee.
""" hakika nimeamini kwanini Mfalme alirudi na furaha akiwa na Malkia tazama leo, Prince na Princess Leo wanarudi na furaha Tena.
,,,,,, Itaendelea,,,,
Usikose sehemu ya 14, ambayo ni Final.
MMOJA WENU AGUSWE VOCHA YA VODA AJE INBOX NA NO YA VOCHA TUMALIZIE SIMULIZI 🙏🙏
[1/25, 17:16] Tinner 1: MWANDISHI: TINNER ROBER. SIMULIZI: UPENDO USIOTARAJIA. SEHEMU: 14 FINAL.
Songa nayo.
Upande wa Nicklan, alikuwa sebuleni kakaa akiwa anachezea gem, Petty alifika na kukaa pale Kisha alichukua remote na kuzima Kisha alichomeka frash na kuweka igizo la The general,
""Nicklan""Inaonekana unapenda gem Sana leo tuangalie igizo hili wote.
Nicklan muda wote, alikuwa akimwangalia tu Petty vituko vyake pasipo kuongea lolote, alisama na kuondoka Moja kwa moja Hadi kitandani kwake huku akisemaa;
""Petty nimechoka kweli hakika wewe ni msumbufu Sana Kaka na yeye sijui anarudi lini tu humu ndani sipumu kabisa.
Kidogo alisikia mlango uligongwa, "" Wewe Petty mi nimelala kwa Sasa sihitaji usumbufu jamani. ""Alijibu akijua ni Petty""
Wewe Nicklan, ni Mimi Nillylan naona unamuwaza Sana Petty sahizi!"
""Kaka mmerudi? Namuwaza wapi ungejua muda wote nafanya dua muwahi kurudi humu ndani nimepachoka kwa kweli mmeniachia Petty ananiendesha Kama gari bovu, halafu Kaka Tinner ameshapona naomba umurudishe kwao.
"' wewe nae hujui kujiongeza tu Petty anakupenda.
""Atanipenda wakati Mimi sijataka mpenda, halafu huyu ni rafiki yangu pia dada yangu na ndo ninavyo muchukulia tu
""Kazi kwenu Mimi tayari napendana na mtanzania wangu hapo ndio nimekufa nikaoza.
""Lakini Kaka kwani hakuna mtanzania mwingine mdogo wake na Tinner na Mimi nikaoa. Harafu Imekuwaje lakini mpaka kwa Sasa unampenda mtanzania???
"""Ni historia ndefu mdogo wangu lakini naona ni moyo wangu ndio umenituma hivo, mwanzoni sikuwaza kabisa Mimi kuoa mtanzania tangu Nipo shuleni tulikuwa tukipiga sitori nyingi kuhusu Tanzania daaah!! Ngoja niishie hapa ukweli sikumpenda mtanzania lakini naona ni Kama UPENDO USIOTARAJIA, Ndo umenikuta.
"" Hivi Kaka Wajua Hata Mimi nampenda Tinner!?
Ila sema kwa kuwa wewe ni Kaka yangu tu, nimekuachia "lakini nilijua Tinner nayeye anakupenda Sana wewe angekuwa ananipenda mimi nahisi tayari angekuwa mikononi mwangu mpaka Sasa, muda wote amekuwa akikuhofia wewe na hapo ndio nilijua hisia zake zipo kwako.
""Na wewe Tena unampenda Tinner?
Kwaniniii Sasa unampenda ungali unajua ni mke wangu. Nilijua mapema hili toka zamani umekuwa ukijaribu kumweka Upande wako lakini nashukuru kwa kuwa umezijali hisia zangu naomba uzidi kumheshimu vivo hivyo nawewe utampata mwanamke utakayempenda na yeye akakupenda mkaendana wote.
" Sawa Kaka usijali lakini siku ya kwenda Tanzania naomba tuongozane kwa pamoja angalau nikaione hio nchi iliyotuletea princess katika taifa letu.
"" Sitakuacha wiki kesho ndio Safari nitaenda kukata tiketi mapema maana wasafili ni wengi na huu msimu wa Christmas's inabidi niwahi.
*****
Nje kidogo na Falme alionekana Malkia Cheness alikuwa na hasira Sana akimfokea Petty,
""wewe tangu uende pale hakuna kilichobadilika zaidi uwefata mapenzi kwa Nicklan muda wote imekuwa ni mtafutano, tumekwambia sie twataka umuteke Nillylan akupende wewe matokeo yake unaenda kumung'ang'aniza Nicklan akupende wewe.
Alipigwa bakora zote huku akilalamika na kuomba msamaha; "Malkia naomba unisame tena haitajirudia lakini kelele zile hazikumsaidia. Walinzi walizidi kumuazibu.
Malkia aliamuru baada ya kichapo kile Petty alilegea Sana mpka alizirai, Kisha aliamuru baada ya hapo akatupwe katika mto Jabanah aliwe na Mamba, walinzi walifanya vivo hivyo.
Tinner alionekana muda huo amekaa na daktari wakifalme leo hi alikuwa akifanya jaribio la kuparua macho ya kondoo, kwenye zizi moja walimuchukua kondoo mmoja Kisha walimumwagia Tindikali na kuanza kumtibu kwa kutumia dawa mbalimbali zilizokuwa zikitumika kutibu wagonjwa katika Ufalme, walifanya juu chini lakini kondoo huyo hakuona tena, jitahada za hapa na pale ziliendelea mpka kukapanzuka hamna dalili yoyote, majira ya mchana walienda kumwangalia kondoo yule kwenye zizi hakika hawakuamini walimkuta kondoo akila majani, wote walifurahi kwa pamoja na kusema hapa Tumefanikiwa. Imetuchukua muda yapata siku tatu Sasa naimani Malkia atapata kuona.
Upande wa Petty alienda kutupiwa mtoni lakini kwa bahati nzuri walinzi walimuonea huruma walimsogeza mpka kwenye barabara iliokuwa inaingia nchi kaskazini kwa kina Pinty,
""Siku hiyo alionekana Nellyson alikuwa akipita eneo Hilo akiwa anawinda sungura kwa bahati nzuri aliona Kuna mtu kalala kwenye kichaka alisogea karibu mpaka sehemu hiyo alishangaa kumuona binti kalala mwili wake umetapakaa damu pamoja na alama za fimbo alisikilizia mapigo ya moyo aliona bado anapumua aliamua kumsaidia na kumchukua mpaka kwenye Ufalme wake na kuanza kutibiwa japo matibabu Yale yalifanyika kwa Siri Sana Mfalme asijue Kuna ujio wa mgeni tofauti na nchi yao maana wao waliamini ukileta mgeni tofauti na nchi yao nikuleta mkosi.
Siku ilifika ya kumfanyia Malkia upasuaji wa macho kwa vitendo Muda huo Tinner alikuwa makini na kazi yake alikuwa akipita huku na kule nenda Rudi baadae Malkia aliingizwa kwenye chumba Cha upasuaji na kuanza kufanyiwa huduma. Kwa Upande wa Nicklan na Nillylan muda wote walikuwa wakizunguka zunguka kwenye chumba Cha upasuaji kwa nje huku na kule wakimuomba mungu, Kila mtu aliwaza lake.
Malkia Cheness, Leo alikuwa akizozana na mshauri wake;
"" Namtaka mwanangu Petty, nilikwambia umuonye tu na si kwenda kujichukulia maamuzi ukamtupe mtoni mwanangu kwa Sasa kaliwa na Mamba najua umefanya hivi kwakuwa wewe hujui uchungu wa mtoto nitahakikisha nakuweka bayana kwa Kila kitu ulichokuwa umepanga kufanya katika Ufalme na Kila mtu atajua kuwa wewe ndio umemuua Mfalme hakika nakwambia lazima ulipe kwa kifo Cha mwanangu. Mizozano ilizidi kuendelea Kila mtu akisema lake
Malkia; "'sasa hivi unanituhumu Mimi tu wakati wewe umejitoa Hata kumtoa mwanao Petty, akaharibu ndoa ya Nillylan ili aolewe matokeo yake "Wewe Kama unataka kusema kaseme tu na Mimi Nina vitu vyako vingi.
Ni siku tatu zilipita Malkia alikuwa bado kalala khari yake bado haijakaa sawa mwishowe kwa upande wa Tinner alianza kuingiwa na hofu muda wote alikuwa akimwomba mwenyezi Mungu amufariji kwa kile alichokuwa amekifanya, lakini Nillylan alilitambua hili alimfuata na kusema;
" Vipi naona unahofu Sana kweli wewe ni daktari?
""Tinner alisituka Sana kwa swali lile na kuanza kutetemeka, Nillylan alichukua koti lake na kumfunika hakika umefanya kazi nzuri Sana sikutegemea mama yangu ataona Tena, naomba upumunzike na wewe ni siku tatu hujalala leo nitakuwa macho kukuangalia wewe mpaka utakapolala.
Mama kwa Sasa yupo kwenye uangalizi wa Nicklan na daktari kaniambia leo nishinde na wewe usiku kucha Usihofu tena kuhusu mama sawa.
""Hakika Tinner, hakuamini hivi ni kweli Malkia anaona? Nillylan.
"" Ndio anaona wewe pumunzika kesho atakuwa anaona vizuri. Tinner alifurahi Sana, siku hiyo ndio alipata usingizi akiwa na amani alilala fofofo kutokana na kukosa usingizi wa siku tatu. Lakini Nillylan muda wote alikuwa akimwangalia tu Tinner alisogea kitandani na kuegama kifuani kwa Tinner huku akimwangalia usoni
"" Hakika wewe ndio chaguo sahihi kwangu siku zote unanipa furaha,"" Kisha alimbusu kwenye paji la uso, unaonekana umechoka sana basi pumunzika.
*****
Asubuhi kulipambazuka.
Tinner alienda kumuona Malkia, hakuamini macho yake kumuona Malkia anatazama vizuri alimkumbatia Malkia kwa furaha na kusema hakika kazi yangu nilioachiwa na Mfalme nimeikamilisha "" Naomba Mfalme uliko pokea Dua yangu kazi yangu nmeimaliza uliyonituma tazama Malkia anaona kwa Sasa.
Malkia alifurahi Sana alipomuona Tinner zaidi alizidi kumpenda Hata muonekano wake sura na ucheshi wake, aliamuru aombe chochote kile kwenye Ufalme afanyiwe lakini Tinner, hakuwa na tamaa aliomba,
""Malkia Mimi naomba; "UPENDO tu kwa mwanao zaidi akinipenda ndio itakuwa furaha yangu, chapili, naomba ruhusa niende kuiona nchi yangu Kama wiki moja Naomba niambatane pamoja na Nillylan na Nicklan nitarudi nao pamoja.
""Sawa;. ""kwa Hilo tu usijali, nimewaruhusu muwahi kurudi Mimi nitakuwa tayari nafanya maandalizi ya harusi yenu wewe na Nillylan, nawewe Nicklan kwa Sasa Mimi mama yako naona vizuri kwa Sasa, kwahiiyo nataka mkwee ""sawa baba!!!.
*****
NCHINI TANZANIA
Leo alionekana Jescar, akiwa anaandika orodha ya mahitaji yake ya duka lake la dawa muhimu zilikuwa zimepungua baadhi, alikuwa na wafanyakazi wake wakisaidiana kuorodhesha.( Jescar baada ya tukio lililopita yapata Kama miaka mitano katika birthday ya Tinner yeye alinusurika pekee katika tukio hilo baada ya kuanguka chini, polisi walikuwa tayari wamefika katika tukio walimchukua na kumpeleka kufanyiwa vipimo katika mwili alienda kutibiwa uingeleza mwaka mmoja akawa kapata wadhamini wakumsomesha baada ya mwaka kupita alimaliza elimu yake na kuja kufungua pharmacy kubwa nchini Tanzania )
Baadae aliagiza mzigo lakini kichwa chake hakikuwa sawa siku hiyo alionekana Ana huzuni Sana akaamua akapumunzike nyumbani, kumbukumbu zake zilienda mbali Sana siku hiyo alianza kumkumbuka rafiki yake Tinner Kila Mara.
*****
AIRPORT MWANZA.
Alionekana ni Tinner, Nillylan pamoja na Nicklan wakishuka moja kwa moja walikodi tax Hadi Jb, hotel ndio walipumunzika hapo kesho yake walianza Safari moja kwa moja Hadi igoma walifika mpka mtaa ule aliokuwa anakaa Tinner walikuta nyumba yao tayari imebomolewa kumejengwa kiwanda kikubwa kinachomilikiwa na mzungu,
zaidi ilibidi kumtafuta Jescar ndio angekuwa msaada mkubwa kwao, walianza kumtafuta huku na kule kumuulizia Jescar, bahati nzuri walikutana na kijana mmoja aliwapa address ya nmtaa mpaka nyumba, Jescar alikuwa akiishi kapirpoint,
walifika moja kwa moja, Jescar alikuwa anamiliki mjengo mkubwa na alikuwa na usalama wa kutosha muda wote nyumba yake ilizungukwa na walinzi,
moja kwa Moja walinzi waliwakalibisha ndani, Jescar alikuwa jikoni akiandaa chakula Cha mchana, aliamua atoke nje kumwaga uchafu, ile anatoka hakuamini macho yake kumuona rafiki yake kipenzi akiwa kaambatana na vijana wawili.
Walikumbatiana kwa furaha lakini machozi na kilio kilianza upya Kila walipokumbuka matukio yaliotokea nyuma walianza kulia tu.
Kazi ilibaki kwa Nillylan na Nicklan kuwabembeleza. Nillylan yeye aliamua kumbembeleza Tinner. Nicklan akaona sio mbaya na yeye alikuwa Upande wa Jescar akimubembeleza.
Baada ya kulia Sana walinyamaza Tinner, aliulizia habari ya wazazi ilikuwaje Jescar alimhadithia vyote ilivyokuwa. Zaidi na Tinner alimwambia maisha alivyoishi mpka kufikia hapo Alimtambulisha Nillylan kuwa ni mchumba wake na hivi karibuni wanaenda kuoana.
""Jescar alifurahi sana, na kumpongeza rafiki yake, Tinner Alihoji mbona wewe hunitambulishi shemeji yangu!!
""Jescar alisituka kidogo, Daah Tinner, naumia kweli, nilikuwa na mchumba wangu siku moja nilifata mzigo Dar nikawa nimemuachia duka ile nimerudi nimekuta nusu ya duka kabeba nimejitahidi kufatilia lakini sijafanikiwa nikaamua kumpotezea ndo maana mpaka Sasa Nipo pekeyangu tu sihitaji Tena mwanaume.
Pole Sana, Hivi Nelly alipotelea wapi?
""Daah yule bwanako nahisi kalioa tatizo kalikuwa kanajikuta ni kazuri Sana Kila siku kanabadilisha wasichana nahisi kamekufa na Corona.
"Walicheka kwa pamoja, Et amekufa na Corona, vipi lakini J, unamuonaje Nicklan ni kijana mzuri anaweza kuziba pengo lakini.
""Sitaki bhana, Mimi mwanaume tenna, Nicklan anajikuta mzuri Sana ni mwendo wa kuumizwa tu itakuwa Kama natonesha donda.
"kwani Hana mke?
"" Ndio, hajaoa muda wote kaja Tanzania kutafuta mchumba, na ndoto yake ni kuoa mtanzania hutaamini nyumbani kakataa kuoa anataka mtanzania laa hivo anioe Mimi na kakake wote niwe mke wao. "Kaa uzungumze na moyo siku tunaondoka unipe majibu, hapa nimeshaona tayari Nicklan ameanza kukumezea mate.
""Muone, wewe Tinner kumbe haubadiliki siku zote tu huishiwagi maneno, Tena ya kumtoa nyoka pangoni. Acha Mimi niingie jikoni Kwanza
Nicklan muda wote alikuwa akimsumbua kakake, Nillylan nifanyie mpango Basi na Mimi nataka nitoke na Jescar, nioe kabisa kumbe watanzania ni wazuri tu, ongea na Tinner Basi au Mimi nikaaongee nae japo ushanikataza mazoea na mchumba wetu,
""Huyo sio mchumba wetu sema mchumba wangu,
""Usipofanya Basi Tinner, atakuwa mchumba wetu tu.
"""Una kelele kweli sawa nitafanya kwaajili ya Tinner tu, ukae nae mbali sawa.
***
Siku iliyofuata walionekana Jescar na Nicklan katika hotel moja ya kitalii wakiongea mambo ya hapa na pale lakini jibu la mwisho tulisikia ni ""sawa tutaenda wote"" Alisema Jescar.
Safari ilifika siku hiyo walikuwa Airport tayari kuelekea Korea wakiwa ni Nillylan, Nicklan, Tinner na Jescar, walifika Korea na kupokelewa vizuri.
Nicklan alimtambulisha Jescar Kama mchumba wake, Malkia alifurahi Sana aliamua awafanyie bonge la harusi wanawe wawili waliokuwa wakioa pamoja ndani ya siku moja. sherehe ilfanyika ilikuwa kubwa Sana.
Upande wa Malkia Cheness baada ya kusikia taarifa ya harusi Nillylan anamuoa Tinner, na Nicklan anamuoa Jescar halafu wote ni wanawake wa kitanzania, mapigo yake ya moyo yalienda mbio na kusababisha tatizo lake la presha yake ilipanda moja kwa moja na kusababisha kifo chake.
Baada ya Ndoa Nillylan alifurahi Sana kumpata mke mwema , moyo wake ulijawa na furaha Sana alimuahidi ahadi nyingi Tinner ambae kwa Sasa alikuwa ni mke wake wa ndoa halali, walishilikiana kwa pamoja kuongoza Ufalme na mwenyezi Mungu hakuwatupa mkono utawala wao ulikuwa wenye neema na amani ya kutosha.
Nicklan na yeye baada ya Ndoa alirudi Tanzania na mkewe Jescar, walifungua miradi mbalimbali iliokuwa ikiwaingizia hela na kuwapa umaarufu mkubwa jijini mwanza.
,, FINAL,,,,,
Nawashukuru sana kwa wale wote ambao wametoa muda wao kufatilia SIMULIZI hii ( UPENDO USIOTARAJIWA)na imani umejifunza mengi zaidi tukutane Tena kwenye simulizi zijazo. Na hii Ndio ilikuwa Ni simulizi yangu ya kwanza kuandika ndani ya mwaka mpya 2022!! Naamini makosa hayakosekani ila umejitahidi rekebisha😂
Hadithi zangu hizi zinapatikana katika blog yetu pendwa ya LUGEMBE BLOG ambapo utakutana na habari na hadithi zangu nyingine nyiingi. Pia kama utakua na matangazo ya Biashara wasiliana nae kupitia mawasiliano yaliyopo katika blog hii
By TINNER ROBER.