Ikawe Heri My Duffer 1

 SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER .                            MTUNZI: TINNER ROBER.                          SEHEMU: 01. 0746638941 (Wtsp).


ANZA NAYO.


Katika Nyumba Moja kulionekana Kuna Mabinti wawili walikuwa wakizozana hapa na pale wakirushiana matusi mpaka ya nguoni.


Alikuwa Ni Lunah!! Na Ennah. Lunnah Alikuwa akiishi kwa shangazi yake( Mamake na Ennah ) Mara TU Baada ya Wazazi wake kupoteza Maisha huko kijijini. Alichukuliwa na Shangazi yake na kuletwa mjini ili aendelee na masomo yake, Lakini alivyotegemea ikawa sivyo matokeo yake aliwekwa kuwa mfanyakazi wa Ndani. 


Upande wa Ennah hakuwahi kabisa kumpenda ndugu yake hata siku moja, muda wote ilipelekea kushidwa kupatana ikawa ni kila siku kutukanana na kupigana.


Lunnah! Alikuwa Tayari kashayazoea maisha ya shangazi yake muda wote alikuwa akifanya Kazi kwa ziada japo masimango yalikuwa Ni mengi hata kwa shangazi yake. Siku moja Alikuwa kakaa Chumbani kwake alichukua vitabu(4m2) baadhi alivyokuwa katoka navyo kijijini akijaribu kujisomea.


Muda kidogo aliingia Ndugu yake Ennah. Alifika na kumnyanganya kile kitabu huku akimtupia maneno.

   "" Siku zote Wewe Ni mtoto wa maskini tu!! Hapa unapoteza muda wako kujisomea, Tena una bahati yako Ancle anakuja leo ndio utapumua humu Ndani!!!""


Ghafura mlango uligongwa Alikuwa Ni shangazi akiingia.

 "" Wewee Lunnah!! Huna adabu ee toka umpokee shangazi yako!! Huoni Kama Kuna wageni wengine nimekuja nao!!!""


Lunnah alitoka huku akikimbia.

 '" Samahani Shangazi nilikuwa namalizia Kazi.""


   "" Mama muongo huyo!!! Hakuwa na Kazi yoyote Zaidi ya kuchezea vitabu vyangu!! Ennah alidakia.


Lunnah hakujari yote hayo alichukua mizigo na kuingiza Ndani.


Baadae Shangazi yake alimuita Lunnah sebuleni ili waanze kuzungumza nae pamoja na wale wageni.


  "" Shangazi yangu!! Muda wote naona unatamani Sana ueende shule Lakini naona majukumu ya hapa Ni mengi!! Leo Mjomba wako kanipigia simu anataka ueende shule na Hawa ndio utaondoka nao, naomba ukawaheshimu na ukawachukulie Kama  Wazazi wako!!""


Lunnah Alibaki kaduwaa asiamini Kama Leo angepata neema ya kwendaa shule.

Alimkumbatia Shangazi yake nakusema.

   "" Shangazi!!! Ahsante Sana!! Sikutegemea Kama siku moja nitarudi Shuleni.""

  

  "" Usijali Shangazi!! Haya Ni matakwa yangu nikusomeshe Wewe!! Na niahadi niliyoachiwa na Wazazi wako nihakikishe unasoma kwa bidii!!  Basi kajiandae hakikisha Nguo zako zote unabeba""

   

   """ Shangazi nguo zote Tena na wakati nitakuwa narudi likizo kuja kumsalimia!!""


""" Ukija nitakununulia nguo nyingine mpya!! Au wataka kuziacha ukirudi ukute nimezichoma Moto!!!""


"" Aaaah!!! Hapana Shangazi!! Nabeba zote!! Nitakuwa navaa nguo mpya kila nikija bhana!!!""


Lunnah aliingia ndani na kuanza kukunja nguo zake na kuweka kwenye Begi kubwa, Kisha alitoka nalo Hadi sebuleni.

  "" Shangazi Tayari nishamaliza!!!""


  """ Hapo sawaa!!! Na upo haraka kwelii!! Nikutakie Safari njema na masomo mema kumbuka heshima ndio kila kitu shangazi!!""


  "" Sawa!! Shangazi!! Sitakuangusha.


Lunnah Alichukua begi lake Lakini Alitaka Kwanza kumuaga Ndugu yake Ennah. Alimgeukia na kumfungia mkono.

   "" Ennah!! Nitakumisi Sana!! Nikutakie Masomo mema!! Na ubaki salamaa!! Zaidi Tukutane likizo ijayo.""


Ennah muda wote alikuwa akimtizama tu, Kisha Aliibinua midomo yake na kuifyonza na kuingia chumbani.


Huku Safari ilianza ilichukua Kama masaa kumi na mbili kufika. Mnamo majira ya usiku walifika kwenye jumba Moja kubwa lililokuwa limezungushiwa fence.


Mlinzi wa Getin alifungua mlango na kuingia Moja kwa Moja na kupokelewa na wadada wawili walifika pale na kupakua ile mizigo na kuingiza Ndani.


Mdada mmoja Alimpokea Lunnah na kuingia nae Hadi ndani na kumuonesha sehemu ya kupumnzika.

  " Alimuita kwa jina la utani!! "" Kadogoo Wewe waitwa Nani??""


   "" Naitwa Lunnah!!!"


   """ Basiii niite. Da! Angela!! Nikutakie usiku mwema, ukitaka kutoiletika Ni huko kwa mlango!!""


"" Sawaa!!! Ahsante! Da Angela!!""


Usiku uliisha hatimae ilikuwa Ni asubuhi kumepambazuka. Angela na Rechoh waliamka mapema wakiandaa kifungua kinywa!!


Huku kwa Lunnah siku hiyo hakupata usingizi aliamka mapema na kufanya usafi wa Mwili Kisha alifungua pazia kwa nje akiwa anatazama mazingira. Aliona mji ulivyokuwa na Maghorofa mengi yamepangana alibaki kutabasamu na kujisemea.

   "" Nitoke hapa niende wapi Sasa!!! Maisha si Ndio haya!!!


Mara mlango uligongwa na kumfanya Lunnah ashituke kidogo.

 "" Karibu Da Angela!!""

   

 ""Ooh!! Uliamka mapema Sana!! Mbona ushamaliza kujiandaa mapema hivyo!!""

 

 "" Kawaida tu!! Nilizoea pindi Nipo Nyumbani!!""


Walifika Hadi mezani na kukaa. Rechoh muda huo yeye Alikuwa akimimina chai.


Muda kidogo Lunnah Ndio anamuona mamake aliyemchukua alisimama na kumpokea Kisha Alimsalimia kwa heshima zote.


Huku upande wa Rechoh na Angela walibaki wakikonyezana.

 "" Naona hajui kitu kinachoenda hapa!! Atazoea tu!! Naona hajamtambua Madam vizuri!!!""


Madam Baada ya kumaliza kunywa chai. Alimuita Angela pembeni na kuongea nae maneno kadhaa.kisha aliwaaga na kuondoka.


Angela baadae Alimchukua Lunnah na kumpeleka kwenye chumba kimoja Kisha alimpatia mavazi tofauti na kumwambia.

   "" Lunnah!! Madam kanambia uvae mavazi haya!! Harafu usiwe unamuita mama!! Muite Madam, ""sawa!!;""


Lunnah Alichukua mavazi Yale na kuyakunjua, Aliamua kumuuliza Angela!!

  "" Una uhakika haya Ni mavazi yangu???""


Angela alitaka amjibu lakini alisitushwa na kelele mlangoni za wadada wakicheka, ilibidi aende Mlangoni kuwasikiliza.

   "" Nyie mnataka Nini hapa!! Mbona mna vihelehele hivyo!!""


  "" Nataka tumuone huyo kigori!! Anayekuja kutoka na mtoto wa kibosile mkubwa hapa Nchini, Et anataka bikra kwani Bikra mwenyewe Ana mvuto gani?!"


Angela aliamua kuufunga mlango lakini wakawa wamemzidi nguvu na kuingia Hadi Ndani.


Lunnah Alisituka Baada ya kusikia kelele zinazidi kuingia ndani Ile  anageuza kichwa hivi Ndio anawaona wadada warembo wamevaa Kama vazi alilopatiwa avae na Angela.


Aliwaonea Aibu na kujifunika Macho yake na mikono. Huku wale wadada walibaki wakisonya na kutoa maneno machafu.

   "" Mbona hasemi!! Mbona haongei!! Harafu Ana kipaja kimekomaa Kama Cha bwana afya huyu nae asitutishe tu, lazima akataliwe huyo.""


Walitoka na kuelekea Hadi kwenye Vyumba vyao na kuendelea na maandalizi ya hapa na pale ili usiku waingie kwenye Cassino!!


Angela Alimsihi mpaka Lunnah akawa amevaa Lile vazi, aliamua kumuuliza Kwanza.

   "" Da Angela!!!! Kwani Ni kipi kinachoendelea hapa!!?


   "" Kwani Madam hakukwambia mpaka ukafika hapa?? Wewe umemjuaje Kwanza Madam?!""


   "" Mimi nilikuwa naishi kwa shangazi yangu Mara TU Baada ya Wazazi wangu kafariki shangazi alinichukua na kunilea ila Nia ya kuja kwa shangazi ilikuwa Ni kupata ELIMU tu, Ndipo juzi alikuja na Madam na kuniambia nije nae I'll nisomee huku na hiki ndio kilichoniletaa!!!"


   """ Duuuh!!!! Pole Sana hapa Umeliwa!! Hapa Hakuna Cha shule Wala Cha Elimu!! Hapa unakuja na mtaji wako unatumika Kama miaka miwili unapatiwa pesa yako!!;"


  "" Sa Da Angela!! Mbona sikuelewi Ani Mimi tayari na mtaji wakati hata Kazi niliyoifanya ya kuniingizia pesa sijapata??""


   "" Ayaa!! Kalia hivyo hivyo!! Mtaji Ni Mwili wako Ndio utakuwa unaufanyia Kazi harafu Baada ya miaka miwili unapewa pesa uliyoingiza ila kwa madaam yeye huwa anakata asilimia 10% TU kila Baada ya miezi sita.


Lunnah Alichoka kabisa na kuanza kulia.

   "" Kwanini shangazi umeamua kunivua hivi Mimi!! Hata Kama nilikukosea hukupaswa unifanyie hivyo. Bora ningebaki kuwa mtumishi wako nikakutumikia siku zote!!""


Angela ilibidi amkumbatie TU kumtia moyo.

  "" Usiwe na hofu kiasi hicho!! Ukizoea  Utazoea TU, hata Mimi nilikuwa hivyo lakini kwa Sasa nmezoea na hii nafanya Kama Kazi zingine tu.""


Muda kidogo walisikia sauti ya Madam akiongea huku akiwapangia Kazi za kufanya wadada!! Mara alisikika akimuulizia Angela na Lunnah!!""


Angela alitoka haraka na Lunnah Hadi kwenye Meeting. Madam Alifika na kuanza kumkagua Lunnah Kama kapendeza.


Alimuita Rechoh na kumuamuru amchukue Lunnah akamfanyie Make-up Kwanza. Baadae Lunnah alirudi akiwa kapendeza huku kavalia Weaving na kigauni kifupi Cha pinki na kiatu kirefu, sio Siri Alikuwa Ni Beauty kutokana na rangi yake Nyeupe Ndio ilizidi kumng'alisha zaidi.


Kwa wale wadada kila wakizidi kumtizama Lunnah alionekana Ni bomba kabisa walibaki wakisema chinichini.

  "" Kumbe nakenyewe kakipodolewa kanakuwa karembo hivyoo!!""


Madam alimaliza kugawa majukumu kila mtu akaendelea na Kazi zake. Alimchukua Lunnah na kuondoka nae.


Alifika na kuanza kuongea nae.

 "" Lunnah!! naimani Angela ameshakwambia kila kitu ila Wewe utakaa hapa Kuna mtu utaonana nae Kama nusu saa atakuwa hapa!!""


Lunnah Alibaki akitikisa kichwa asiseme chochote!! baadae Madam Aliitwa na kutoka Nje, kuonana na mtu aliekuwa kamuita.


Kuna Gari ya kifahari ilishuka pale walionekana wakaka wawili walishuka  na kuonana na Madam, Madam aliwapa maelekezo na kuwaelekeza Hadi kwenye chumba Cha Lunnah.


Walifika na kuingia kwenye chumba kile na kumkuta Lunnah kakaa kwenye sofa kajiinamia tu huku machozi yalikuwa yakimtoka.


Mkaka mmoja Aliitwa Imlany, Alifika na kumsogelea Lunnah na kumuinua kichwaa.

   "" Mbona huna Raha kiasi hicho!! Ongea Basi na rafiki yangu anaitwa Rich, angalau umsalimie.


   "" Mambo vipi Lunnah!!!!?? Unaonekana mtoto mubichi kweli!! Hadi unaogopa kuongea na wanaume!!?? Alikuwa Ni Rich muda wote huwa anakuwa na mawenge ya hapa na pale. Tena akiona ngozi Nyeupe Ndio anachanganyikiwa kabisa!!!""


Lunnah Baada ya kusikia hivyo ndio alizidi kulia mfululizo.

 Imlany aliamua kumtoa Rich na kubaki na Lunnah huku akijaribu kumbembeleza.


   "" Rich nikukute Nje Kama Nusu saa hivii!! Huyu Manzi nitamfanya afurahie TU,na hatojuta kuniona siku zote Kama nakuwa mbali nae....""


   ,,,,, Itaendeleaa.....  

Usikose sehemu ya 02.


Unazani nini kitafuata kwa Lunnah, Je, Imlany  Atamuacha salama????'''


Like, comments, Share Ndio saport yakunifanya nijue mnaikubali simulizi hii kiasi gani!!!!??

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi