SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER . MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 05. 0746638941 (Wtsp).
ANZA NAYO.
Ilikuwa Ni siku nyingine Tena siku hii Ilikuwa Ni siku ya Kazi kwa upande wa Lunnah!! Ndio Alikuwa anaanza kazi rasmi!!
Rich aliamua awe bega kwa bega na Lunnah huku akimfundisha jinsi ya utendaji kazi.
Muda kidogo Maneger Tonny!! Alifika na kumuomba Lunnah afike Ofsini kwake, Lunnah aliingia Moja kwa Moja Hadi Ofsini kwa Tonny!!
Tonny alifika na kumkabidhi Mafile amsaidie kupanga lakini Alikuwa na maswali mengi ya kuuliza.
"" Hivi Lunnah!! Wewe na Imlany man siku nyingi mwafahamiana!!?!""
"" Ni muda mwingi imekuwa!! Vipi mbona wauliza??""
"" Nimeuliza tu!! Make Imlany huwa Ni mgumu kuingiza wafanyakazi kiurahisi hivi!! Hata kama ukiingia hiyo Interview utakayofanyiwa utatamani usirudie kuomba kazi Tena!! Ila kwako nimeshangaa umefanyiwa Hadi party harafu bila Interview!!!""
""" Usijali bhana!! Hata hivyo Duffer wangu hanaga roho mbaya!! Akishakuamini tu Hakuna kinachoharibika!!""
Muda kidogo Imlany Alikuwa anakuja Ofsini kwa Tonny.
"" Vipi Tonny!!! Unamfundisha majukumu Duffer!! Ni vizuri lakini naomba nimchukue kidogo make kwa sasa Ni Lunch time!! Akishiba Ndio utamuelekeza vizuri!!!""
"" Sawa!!! Haina Shida Boss!!!""
Imlany Alimchukua Lunnah na kuelekea kwenye hotel nzuri huku wakipata Chakula, Lunnah Aliamua kumuuliza Duffer wake!!"
"" Kwanini Duffer!! Hunishirikishi kuhusu Ndoa yako!! kumbe Wewe msiri kiasi hicho na Mimi nitakuwa nakuficha Mambo yangu!!""
"" Ooh!!! Nilitaka tupate siku tuongee!! Ila kwasasa nitakueleza pia!! Rayna Ni Mchumba wangu! Pia Ni mke wangu mtarajiwa hapo baadae na tunategemea Mnamo mwezi wa kumi na mbili itakuwa Ni harusi!! Hivyo Karibu Sana na Samahani sikukwambia mapemaa!!!""
"" Ndo uniambie leo!! Baada ya kukuuliza Okay!! Nikutakie maandalizi mema na Ndoa yenye Kheri!!;""
"" Sa' Ndio wataka kuondoka??? Au Nini wamaanisha!!??""
"" Niondoke kabisa!! Wakati Badoo sijala!! Thubutuuu!!!""
"" Hahahahaaaa!!! Harafu Na Wewe una tumazoea!! Sahii unataka ukaribu na Tonny tenaa!!!?""
"" Kwahiiyo hutaki wataka niwe naongea na Wewe TU!! Wakati muda huo unakuwa chumbani kwako so wataka nikae tu ka Sina mdomo!!;??""
"" Ayaaa!! Hongera pia!! Na endelea!!""
Lunnah Alichukua nyama na kumpatia Imlany!! "" Basii!! Leo nimejua Duffer wangu Ana wivu!! Hataki nitafute Duffer mwingine!! Sijui Ndio ataniona yeye??" Lunnah Alikuwa akijisemelesha ili azidi kumkela Imlany!!
""" Ayaaa!! Kula haraka twende kazini!! Unaongea Sana!! Kisha alisimama na kwenda kulipia hella ya Chakula!!"
Lunnah alitabua kuwa Duffer wake kachukia alisimama na yeye na kufika kumkumbatia kwa mgongo.
"" Samahani Duffer!! Duffer mzuri Ni yule anayegundua haraka kuwa kamkwaza rafiki yake huwahi na kumtaka radhi!!!" Nisamehe Basi Duffer!! Nimekukosea at!!""
Imlany alimgeukia Lunnah na kumtizama kwa karibu. Alichoamua Ni kumfinya mashavu.
"" Bado TU Duffer unanikosea, ona kwa Sasa unakuja hata hujanawa!! Nyama nyama zako mkononi!! Badoo mafuta harafu wanishikia kwa unform huoni Kama umenikosea bado!!""
Lunnah Ndio anatazama mikono yake na kuona Kweli Ni michafu, Aliondoka pale na kwenda kunawa Kisha alichukua tishu na kuja Moja kwa Moja na kuanza kumfuta!! Imlany muda huo Alikuwa akimtazama TU Lunnah!! Make aliona anachokifanya pale Ni kuzidi kumchafua TU.
Alimshika kwa nguvu na kumkokota na kumpeleka Hadi kwenye gari!! Kisha Alifunga mlango na kumgeukia.
"" Unachofanya Ni Nini hicho muda wote naona hata upeo wako wa kufikili Ni ziro!; Sijui hata utaweza kazi!! Hapa umenichafua Mara mbili yake na bado waendelea, kifuatacho Ni Nyumbani ili ukafue hizi nguo, sawaa!!??"" Kisha aliwasha gari Moja kwa Moja Hadi Nyumbani.
Huku Njiani Lunnah Alibaki na maswali mengi ya kujiuliza!!
"" Shida Ni Nini kwani!! Mbonaa hata ulichonunia Mimi sikioni?? Hayaa nitaenda kufua harafu kunambia Sina upeo wa kufikiri Kama Kazi sitaweza Ni sawa TU Mimi Sina akili!!' Tena hata Wewe umeniuzi pia!!!""
Walifika Hadi Nyumbani. Imlany alishuka na kuingia chumbani kwake Kisha alibadili mavazi yake na kumletea zile nguo Lunnah!! Azifue Kisha aliondoka na kurudi kazini!!""
Ratifa Alikuwa akiandaa Chakula baadae alitoka Ndani na kumkuta Lunnah akiwa nje anafua, alifika nakumuuliza.
"" Kwanini Umetoka mapema hivyo kazini!! Na sikawaida kurudi saa hii!! Au kazi imekushinda umezoea kukaa nyumbani!! Ratifa Alikuwa akiongea kiutani utani.
Huku kwa Lunnah alivyolipokea ikawa Ni tofauti kabisa Alianza kuongea peke yake Kwanza.
"" Mimi Sina upeo wa kufikili!! Harafu kazi imenishinda!! Badoo nimezoea kukaa nyumbani!! Sijui Ndio kupenda kulala Ndio unamaanisha??""
"" Una Nini Lakini Lunnah!! Waongea peke yako au Duffer wako amekuuzi leo? Au kina Rich na Tonny!!!? Make Jana walikuwa wanakumezea mate Kweli!!""
"" Hayakuhusu bhana!! Wewe endelea na kazi zako!!
Ratifa aliona akizidi kukaa hapo atasababisha vingi aliamua kupeleka miguu yake jikoni. Muda kidogo alimuona Lunnah kaja pale na Hotpot lake akipakua Chakula Kisha aliondoka na kuelekea Chumbani kwake.
"" Yaaani Lunnah!! Huwa wanichekesha TU!! Na bwebwe zako!! Sa' Chakula kingi hivyo wakula na Nani au Ndio Hadi usiku shosti!!""
Imlany Alirudi majira ya usiku, alifika na kupakua chakula na kuondoka nacho Hadi chumbani kwake, Alifanya hivyo alitegemea Lunnah atakuja kula mezani akaona Bora akalie chumbani ili amuepeke na huku kwa Lunnah alifanya vivyohivyo ili amuepuke.
Asubuhi kulipopambazuka Imlany alijiandaa kuelekea kazini Kisha alimuita Ratifa na kumpatia hella ya nauli ampatie Lunnah akiwa anaenda shule yeye Alikuwa na pitapita nyingi siku hiyo.
Majira ya saa tatu Lunnah Ndio anaamka akiwa Hana haraka kabisa' na kazi, Alifika sebuleni na kuangalia Kama Kuna kifungua kinywa, Kisha alikaa mezani ili aendelee kula, alipotizama pembeni aliona Kuna karatasi ikiwa na ujumbe.
"" Duffer wako kakuachia hella ya nauli!! Leo yeye anapitapita nyingi hivyo chukua hio elfu tano Kama usafili!!""
""" Oooh!! Wewee bado waniepuka hutaki kuniona!! Basi na Mimi hutaniona kabisa na kazi nimeacha si Mimi Sina upeo wa kazi!! Basi sitakuja tenaa!!!""
Huku Ofsini kwa Imlany. Alionekana Rich akiingia.
"" Imlany upo powa Lakini?? Naona Kama leo umeboeka hivi!! Harafu Lunnah anaumwa make sijapata taarifa zake na wakati ulinikabidhi nimfundishe Kazi!!""
Imlany Ndio anasituka, muda wote alijua Lunnah yupo kazini kutokana na ubusy was hapa na pale yeye hakutoka Ofsini tangu aingie.
"" Lunnah hayupo?? Naona huenda hajisikii vizuri!! Hebu Rich Jaribu kufanya mawasilino nae Kwanza, muulizie Shida Nini!!""
Muda huo huo aliona Ujumbe unaingia kwenye simu yake. Alikuwa Ni Lunnah.
"" Boss!! Kuanzia Leo Mimi Nimeacha Kazi!! Harafu nataka nirudi kwenye Cassino nikaendelee na maisha!!!""
Imlany Alisituka kidogo baada ya kusoma Ujumbe, ilibidi amwambie Rich aachane nae kwani angeongea nae yeye Kama yeye!!
Huku upande wa Lunnah muda huo anatuma Msg Alikuwa kakaa na Ratifa. Ratifa aliamua kumuuliza Lunnah!!
"" Hivi kwanini unafanya hivyo Lakini?? Unajua Duffer wako anavyokukubali na kiasi gani anakuelewa Wewe??
"" Mimi Ni mtoto yatima nisie na sehemu ya kukaa!! Hapa nitakuwa mzigo kwenu harafu Imlany atakuwa anamficha Ancle Hadi lini Mimi nataka Ancle akija nimwambie jinsi tulivyokutana na Imlany Tena nasubili tukiwa wote yaaani Mimi, Wewe, Ancle na Imlany!! Si yeye alimdanganya kuwa Mimi Ni ndugu yake na Rich!! Basi Sasa na nitamwambia Leo usiku akija tu Ancle.""
Upande wa Imlany siku hiyo alikuwa Hana furaha kabisa aliamua kuondoka kazini mapema na kuelekea Nyumbani, alifika na kujipumnzisha. Lakini alisitushwa na mlio wa simu Ilikuwa ikiita, aliangalia na kukutana na Rayna akipiga.
"" Imlany!! Why siku hizi upo kimya Sana mpaka nkutafute lakini!! Au Ndio uko busy na Duffer muda wote Hadi unanisahau Mimi mkeo!!!""
"" Hapana mamangu!! Majukumu tu ya Kazi yamekuwa mengi, si unajua kwa Sasa tunaenda kugunga mwaka!! Wateja Ni wengi lakini pia inahitajika umakini kwenye mahesabu ya kufunga mwaka!! Usijali hata hivyoo nakukumbuka Sana Malkia Wangu!! Pia Sina mtu mwingine nimpendae Zaidi yako!!
"" Ahsante!! Nakupenda pia mme wangu!! Pole pia na Kazi!! Naona umepumnzika Ngoja nikuache Kwanza!! Tutaongea kesho!!
"" Okay!! Usiku mwema pia!! Bi harusi wangu!!!
Imlany aliweka simu yake pembeni, Kisha alijigeuza ili aendelee na usingizi, lakini alisitushwa na sauti ya Ratifa ikimuita.
"" Kaka!! Ancle kaja anakuhitaji sebuleni!!!""
Imlany aliamka na kuelekea Hadi sebuleni, alifika na kumsalimia Baba yake, Kisha alimtizama Lunnah akaona akimuacha itakuwa Shida kwa Ancle.
"" Duffer za majukumu!!??""
"" Njema TU!!!
Lunnah alianza kuzungumza.
"" Samahanini kwausumbufu nimewaiteni leo hapa!! Kuna kitu nataka nikiweke wazi kila my ajue!! Ancle Samahani tena!! Na Imlany Samahani pia!!! Ukweli wangu leo nataka mjue ujio wangu.""
"" Mimi kufika mpaka kwenye Nyumba hii!! Ilikuwa Ni siku moja Wazazi wangu walipoteza maisha Kijiji nikawa nilichukuliwa na aunt nikalelewa lakini malezi ya Shangazi yalikuwa sivyo nilitegemea nitasoma shule Lakini matokeo yake ikawa sivyo mpaka siku Mona Shangazi aliamua kuniuza kwa mmama mmoja anayemiliki Cassino nikawa Ni mikononi mwake ndipo siku Mona yule mama alinitafutia jibaba nitembee nalo wakati huo Alikuwa amepatiwa pesa Ndefu na siku hiyo nikawa nimesaidiwa na Imlany ikawa Ndio ponapona yangu ilibidi anichukue, mpaka Sasa nikawa kwenye familia yenu.
"" Kwa Ancle Nilitaka TU nikujulishe Mimi siyo Ndugu yake na Rich, Wala Ndugu yenu hapa Ila Ndugu zangu niliokabiziwa Ni wale wa kwenye Cassino yaani Madam!!
Imlany alimaliza kuongea Kisha Alimkazia jicho Ancle nayeye aliamua kukwepesha jicho, Huku Lunnah Alibaki akijisemea moyoni.
"" Ancle najua kea Sasa!! Hautakuwa na Nguvu ya kuninyanyasa na Wala hautoweza kuniludisha kwenye Cassino!! Siku Madam akijua kuwa Mimi nakaa kwako harafu na Imlany aliyenitoa huko Ni mwanao!! Siku ikijulikana kwa tajiri mkubwa hivyo kuwa wachukua watoto wadogo hii Ni Aibu kubwa!!""
Imlany aliamua kumuuliza Lunnah!!
"" Sasa Lunnah Baada ya kuongea haya yote!! Nini maana yake au tukusaidieje??"
Lunnah Aliamua kumjibu.
"" Imlany kwakuwa Mimi Ni mtoto wa Kwenye Cassino na ndugi zangu walinichagulia hii kazi wakaona inanifaa!! Na pale wamenipeleka ikawe nyumbani Haina budi kubaki sehemu ambayo siyo himaya yangu!! Hapa nimeandaa kila kitu begi Hilo hapo Mlangoni nikuombe Imlany Wewe uliyenitoa kule Ndio utakaenirudisha!!""
Imlany, Ratifa na Ancle ile wanatupa jicho wanaona Kweli Lunnah kaandaa kila kitu.
Ancle alisimama Kwanza kisha, alimwambia Ratifa arudishe begi chumbani, Kisha alimshika mkono Lunnah na kuondoka nae mpaka Nje.
"" Hivi Wewe mtoto!! Unataka kuniumiza akili yangu!! Yaaani nishidwe kuwaza biashara zangu nikae nikukuwazia Wewe!!! Hivi ukirudi Cassino wazani siku yule Madam akijua wakaa kwangu harafu Imlany alikutoa pale siku ile na wakati alikununua ili umtengenezee pesa itakuwaje?! Bado Imlany Ni mwanangu Mimi! Akiyajua haya yote atanichukuliaje?? Bado Mimi Ni mtu maarufu wataka taarifa ziandikwaje kwenye magazeti huoni Kama heshima itaisha Hadi biashara yangu itarudi nyuma!! Ninachotaka Ni Wewe maisha yako yatakuwa hapa siku zote Mimi Nipo tiyari kukufanyia chochote kile!! Aya rudisha mizigo yako ndani na ukae utulie na kazi utaendelea si umemtumia Imlany hutaki Kazi kisa wataka niaibisha!! Ayaa endelea...
Ancle alimaliza kuongea na kuchukua gari yake na kuondoka kuelekea kwenye Cassino akapunguze mawazo.
,,,,,,,,, Itaendelea,,,,,,,,,
Usikose sehemu ya 06!!
Lunnah tayari kalinukisha hivyoo. Usikose mkasa huu!!!