SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER . MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 06. 0746638941 (Wtsp).
ANZA NAYO.
Baada ya Ancle kuondoka Imlany aliamua amfuate Lunnah Hadi Nje, alimkuta kakaa akionesha Kama Ana huzuni Kweli, lakini moyoni anae furaha. Imlany alifika pale na kuchuchumaa Karibu yake kabisa.
"" My Duffer!! Najua nimekukosea Sana!! Mimi ndie nimesababisha haya yote mpaka tumefikia huku!! Nisamehe Basi kwanza Mimi!!!!
Lunnah Ndio kwanza, anakumbuka jibu la Imlany siku ya Jana ile kumwambia Hana Upeo wa kufikili na hawezi kazi aliamua kuondoka kwa hasira na kuelekea Chumbani kwakee. Imlany na yeye aliamua kumfuata nyuma nyuma!!
Alifika hadi Mlangoni na kuingia chumbani kwake huku Imlany na yeye alikuwa akisukuma mlango lakini kwa bahati Mbaya aliweza kumbana Lunnah na mlango Ndio kukampelekea aachilie Mlango. Lunnah alishuka Hadi chini huku akiwa ameshikilia kidole chake na mkono mwingine, Alikuwa akisikilizia maumivu yasiolezeka.
Imlany alimuwahi na kumshika mkono!! Kutokana na hasira alizokuwa nazo Lunnah Aliangalia kwa pembeni kidogo aliona Kuna rula alichoamua Ni kuchukua ile rula na kumpiga nayo Imlany usoni mpaka kukaacha mchubuko ulioanza kutoa damu, lakini kwa Imlany hakujali hayo yote Alikuwa Busy akimfunga kitambaa kwenye kidole chake. Alizidi kumwambia TU.
"" Fanya ufanyavyo ila Wewe kwangu bado Ni Duffer wangu!! Siku zote nilitoa ahadi ya kukulinda muda wote!! Kama Wewe utashidwa kunilinda Mimi Basi fanya zaidi!! But Mimi Ni bado upande wako sitakuacha kamwee!!!""
Lunnah Ndio anasituka baada ya hasira zake kuisha, Alimtizama Imlany usoni na kumuona damu zinamtoka!! Alisimama haraka na kutafuta boks la huduma ya kwanza, Kisha alifungua na kuanza kumhudumia Imlany. Muda wote Alikuwa akiomba msamaha.
"" Duffer nisamehe basi!! Najua hauna kosa !! Mimi si Ndio namakosa sawa Mimi nimekusamehe ila Wewe usinisamehe si nimekuumiza zaidi!!??""
Imlany muda huo Alikuwa akimsikiliza vizuri TU Lunnah!! Aliamua kumshika mkono.
'" Sitaki tenaa uendelee kunisaidia najua Mimi ndio na makosa kwako natakiwa nijiazibu mwenyewe!! Najua hasira yote uliyonayo Ni kwasababu ya maneno yangu ya jana, Najua Jana nilikuwa na hasira tu sijui hata zilitoka wapi nikakuta nakwambia hauna upeo wa kufikili na bado nikakwambia hautoweza Kazi Kama hauna upeo, Na hiki ndio kimesababisha mpaka ukanitumia ujumbe hautaki kazi tena wataka urudi Cassino!!??""
"" Najua hujanielewa vizuri. My Duffer! Mimi kukutoa kwenye Cassino sijakutoa kwa makusudi yangu binafsi ila Ni vile moyo wangu uliumia baada ya kukuona unakuwa katika khari hiyo na wakati bado Ni binti Mdogo!! Najua siku zote ulipenda usome ili upate Kazi na nfio ndoto yako hiyo ila Mimi nimeamua kukupatia kazi I'll ndoto yako itimie haraka!! Zaidi nikwambie tu, Nakupenda Sana My Duffer!! Kwakuwa niliamua kukusaidia sitachoka kamwee kukusaidia make sijajua hata hatima yangu itakuwaje siku za usoni!! Ila Ngoja nikuache kwa leo siku nyingine nitakueleza juu ya Wazazi wangu wapo wapi na kwanini nakaa na Ancle!!?? Imlany aliamua apumzike hapo hapo chumbani kwa Lunnah.
Lunnah na yeye aliamua akae pale huku akizidi kufikilia maneno ya Imlany alivyoongea kwa huzuni Sana alizidi kumuonea Huruma na kupata Shauku kubwa Sana angalau asikie Short store ya maisha ya Imlany na yeye aliamua kupumzika hapo.
Muda ulienda Lakini kwa Lunnah hakuwa kabisa na usingizi Alikuwa akishituka alimuangalia tena Imlany na kumuona Akikoroma aliamua kuchukua shuka nakumfunika Kisha na yeye aliegama kwenye kitanda akawa kapitiwa usingizi mpaka kunakucha.
Ilikuwa Ni Asubuhi Kama saa mbili. Ratifa aliamua akamuone Kwanza Lunnah Baada ya tibwili la Jana, Alifika Hadi Chumbani kwa Lunnah na kukuta Mlango uko wazi aliingi huku akiita Lunnah!! Lakini alishangaa baada ya kukuta watu wamelala huku Alvin akiwa na bandage kwenye paji la uso na kwa Lunnah anabandage kwenye kidole chake. Aliamua kumuamsha Kwanza Kakake.
"" Kaka Imlany!! Nini kimewakuta lakini!!??
Imlany Ndio kwanza anajigeuza lakini kelele za Ratifa zilimfanya aamke.
"" Daaaah!! Mbonaa kichwa kinauma hivi!! Aliamua kushika kichwa baadae Ndio anamtizama Lunnah!! Kwa pembeni akiwa bado amelala alisogea na kumshika kidole chake!!
"" Duffer!! Amka uone kidole chako hakipo tenaa!!""
Lunnah Baada ya kusikia kidole chake hakipo aliamka kwa hofu.
"" Duffer hakipo kimeenda wapi!? Maskini kwa Sasa Sina kidole tenaa!!!"
Ratifa na Imlany waliangua kicheko.
"" Twakutana tu!! Pole mwaya lakini kimevimba!! Naona Jana mlango ulizania Ni mjusi Ndio ukabana!!! Imlany alitania.
"" Aah!! Umeanza ee!! Jana Wewe ulikuwa wapiga confue na mlango Ndio maana uso umekuwa chapati.
Utani wa hapa na pale uliendelea baina ya Marafiki wa Kweli. Ratifa aliamua kuondoka na kuwaacha make ndio maisha Yao walikuwa wamezoeana kuishi hivyo na hii Ndio Ilikuwa Ni furaha Yao siku zote, pale wanapoikosa furaha walizidi kumisiana.
¶¶¶¶¶¶¶¶¶
Ilipita miezi mitatu baada ya Lunnah kurudi kwenye kampuni Tena, kwa muda Huu Alikuwa tayari keshakuwa mzoefu wa kazi na urafiki wako ulizidi kupamba Moto.
Huku kwa Imlany Alikuwa Ofisini kwake baada ya kukamilisha kazi zake alichukua simu yake na kuanza kutizama Any new zilizokiki kwenye mitandao ya kijamii,
"" Ngoja nifungue kisigizo Kwanza make sio kwa joto hili ili nizidi kuenjoy zaidi hapa Sina kazi ya kufanya. Wakati anazidi kupekua alikutana na picha ya Lunnah Intagram kapost akipromo kampuni. Imlany alizidi kuitazama ile picha na kubaki akitabasamu TU huku akiongea peke yake!!
"" Lunnah!! Wewe Ni Duffer wangu siku zote Lakini Why Nakupenda kiasi hiki vipi Rayna akijua Nakupenda itakuwaje!! Huyu shetani anayeninyemelea ashidwe kabisa Mimi tayari Nina mke!!""
Muda kidogo Lunnah na yeye alikuwa anaingia na file zake, Alifika kuingia Kasi hati kwa Imlany Kisha alifika file mezani.
"" Duffer!! Saini twende Nyumbani! Muda umeisha hivyooo!!""
Imlany yeye Alibaki ametulia Tu, akili yake Ilikuwa mbali sana, Mtu aliyekuwa akimfikilia leo Ndio anakuja mbele yake.
Lunnah ilibidi amtizame Kwanza Imlany!! Why yupo kimya ile anatazama TU anakutana na kifua Cha Imlany, Aliona Aibu ilibidi ainamishe kichwa Chini Kisha aliomba Samahani huku akiondoka.
"" Sorry Duffer!! Sikujua Kama nitakukuta upo hivi!!
Imlany alimvuta mkono na kumsogeza Karibu yake Kisha alimwambia TU.
"" Duffer Nakupenda Wewe!!!""
Lunnah Alishituka kidogo make hata upande wake mapigo ya moyo yalikuwa juu. Imlany alizidi kumsogelea huku akizidi kumtizama, Alimuuliza Tena.
"" Vipi na Wewe!! Nikizidi kukutazama kwa ukaribu huu unaonekana tayari na Wewe una hisia za mapenzi!!""
"" Aaa!! Hapana Duffer!! Acha Basi utani. Aliamua kujinasua toka mikononi kwa Imlany na kuelekea Hadi Ofsini kwake, Alifika na kuchukua maji na kunywa kisha alishusha pumzi Ndefu!!
"" Imlany usitake kuniingiza huku!! Mimi pia najua Nakupenda ila Sitaki nikupende tayari unaelekea kufunga Ndoa!! Harafu umejuaje kuwa na hisia na Wewe!??""
Muda kidogo Rich aliingia.
"" Oyaa Lunnah time is over!! Leo walala Ofsini Duffer kakusubili nje muende nyumbani!!""
Lunnah Ndio anaangalia masaa kumbe muda ulikuwa umeisha na umepitiliza Kama nusu saa.
Alifika kwenye Gari na kupanda huku Imlany Alikuwa akisikiliza mziki Taratibu. Alhakikisha Lunnah kapanda Kisha aliwasha gari nakuondoka, lakini aliamua kumuuliza Lunnah!!""
"" Duffer!! Mbonaa Leo hutaki kukaa na Duffer wako Karibu Hadi umekaa nyumaa??""
"" Hapo Ni kwa Rayna!! Mimi siku zote nitakuwa nakaa huku nyuma!; Nimeona nianze mapema kupazoea naona Ni Kama miezi miwili imebakia Rayna aanze kukaa Karibu yako!!"
"" Sawa!! But unaongea Sana pasipo hata kuniuliza unayoongea Wewe na Mimi ndio nataka!! Siku zote rafiki was Kweli kwenye mapenzi huwa anasehemu kubwa Sana!! Haijalishi nitaoa lakini Wewe bado una nafasi kwangu!!""
"" Ayaaa!! Na Wewe unaongea sana!!"
Imlany aliamua kufunga break Kisha alipaki gari lake pembeni, Alimgeukia Lunnah na kumkuta katoa jicho.
"" Njoo sehemu yako!! Mimi sijazoea kuwa naongea na mtu kanikalia nyuma!! Wewe si Duffer!! Naamini Duffer hufanya kitu kile Duffer wake anapenda!! Na hii Ni ahadi yetu!!!"
"" Lakini Duffer Mimi,,,,,,,!!
"" Duffer Nini!!! Aya shuka Basi uje ukae sehemu yako!! Huku akifungua mlango wa Gari ashuke....
,,,,,, Itaendelea,,,,,,,,
Usikose sehemu ya 07.
Mambo hayo yameanza ✍️ Harusi tunayo hatunaa??🤷🤦.
Like, comments zenu Ndio nazitaka tujue hatimaa....
