MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: , 11 "0746638941"what'sup"
SONGA NAYO.
"" Ahsanteni sana Vijana, lakini pole Sana Jolvin mwenyezi Mungu akuponyee na Uongee tenaa!!"". Cheaf alimpatia mkono Jolvin. ENDELEA.
Baada yakumaliza kula, Walinzi walifika kuwachukua Joanyther na Ibrahimu tayali kuwapeleka kwenye nyumba Yao.
Upande wa wageni walioingia siku hiyo walitoka kidogo wakizungukia maeneo ya Kijiji Cha Cheaf huku wakiangalia bustani na mashamba Makubwa yalioteshwa miti na kuonekana Kama msitu.
Mzee Cheaf aliamua awaache kidogo wageni wake waendelee kufanya utafiti huku yeye akiaga na kuondoka ili aendelee na majukumu yake.
Huku porini kulibakia na Mzee Omario Kama alivyojitambulisha. walianza maongezi Yao huku wakishauliana;
"" Hivi Jolvin una uhakika Joanyther hajakufahamu sura yako make amekuwa akikudadisi Sana Kama vile anakufananisha!???"" Collin aliuliza.
"" Hapana hawezi nifahamu na hii mindevu niloiweka ya bandia, Daaah Hapana, Hivi wajua Razack yeye ndio kavunja rekodi tena kawa mbabu ka' Mzee mwenyewe Omario.""
""" Mimi naomba hii tiriki tuifanye haraka, hapa Kwanza nmechoka muda wote kuwa na ekit sauti ya Mzee Hadi mandevu yananichosha na hii rungu ndo kabisa!! Ka Mzee Omario kwelii, Si Bora hata Mimi ningeekit Kama Jolvin yeye mpka anataka tambulika kwa sura Ila na Wewe unachangamoto kosa kuongea tu ndio itakuwa shida!!""
"" Mimi swezi haribu bhana nipo kikazi lakini kumbukeni tufanye ndani ya siku tatu tu tukamilishe, hapa tumebakiza siku mbili za kumtorosha Joanyther, Sasa sijui tunampataje tumdokeze Siri hii yeye atufahamu."" Jolvin aliuliza.
""" Sasa hapo itabidi Jolvin Wewe ndio usimamie Hilo make naona Kama anakufananisha Joanyther, hili naomba tukuachie Wewe. "" Razack' na Collin waliunga mkono.
Siku iliyofuata Joanyther Alikuwa amepumnzika ndani Kama majira ya mchana. Ibrahimu Muda wote Alikuwa akiangalia TV aliweka season moja ya love story alipendelea Sana kuiangalia "" Name's of LOVE" Ilikuwa ikimbuludisha Sana na kumpelekea kuingiwa na chembe chembe za mapenzi.""
Baaadae usingizi ulianza kumuelemea ikabidi ajipumnzishe sebuleni. Joanyther usingizi ulimuisha Alisimama na kuelekea sebuleni na kumkuta Ibrahimu kalala, alichukua remote na kuzima TV huku akifoka kwa sauti;
"" Ibrahimu Wewe mtu gani unaweka season zako sauti ya juu mpaka humu hakulaliki, mbona msumbufu Wewe!!""
Ibrahimu ndio Kwanza alizidi kujigeuza na kuendelea kuongoroma huku akiota ndoto iliyomfanya aanze kutabasamu tu huku akisumbuliwa mto wake.
Joanyther Alisimama na kuchukua maji Kisha alimumwagia kwa kumnyunyuzia machoni baaadae Ibrahimu ndio akaamka.
""" Joany!! Wewe!!! Mtu gani mkorofi hutaki wenzako walale, nikilala tu unakuja kuniamusha ngoja tuone na Wewe usiku Kama utalala!!""
"" Sasa' Wewe usingizi gani huo wa mchana?? Halafu unaanza kuota ndoto wajicheka mwenyewe, sijui unamatatizo Wewe!!??""
"'' sawa bhana!!! Na matatizo ndio!!! ""hebu nirudishie season yangu niendelee kuiangalia Kama utapenda karibu tujumuike wote!!""
"" Mimi nataka nitoke Nje leo nimechoka kukaa humu ndani Muda wote Kama wafugwa.""
"" Huko Nje Wewe wafata Nini?? Kila kitu kimo humu ndani au kwakuwa ulisikia jina la Jolvin Jana ndo wazani ndio yule mwanaume wako kajaa!!""
"" Wewe Ibrah!! Una kisirani ee Mimi kutaka kutoka ndio namfata Jolvin, hafu nikwambie Jolvin siogi Mzee Kama yule, Sema huku twakaa porini hamna amshaamsha za watoto matajili kule kulikuwa na watoto wa matajili sio huku."""
""" Kwahiyo unachotaka Nini?? Au nikusaidieje??""
"" Umechukia ee!! Nilitania tu naona Leo ndio wanioneshea kuwa una hasira na Mimi Basi samahani et!! Sitatoka naomba tuangalie wote.""
Ibrahimu alichukizwa Sana na maneno ya Joanyther aliamua kuondoka pale na kwendaa kulala kitandaoni.
Joanyther aliamua kumfuata huku akimbembeleza;
"" Ibrahimu usiwe hivyo jamani Mimi nilitania tu, mbona Sasa umechukia lakini!! Nisamehe Basi!!!'' naomba tukaangalie wote season jioni twende mtoni tukavue samaki!!""
"" Joanyther Unataka kuniuzi Sasa tangu nikae na Wewe hujawahi niuzi Ila kwa Sasa ukiendelea Hivi utaniuzi kupita kiasi!!""
"" Sirudii bhana!! Nimesikia!!' Hebu inuka Sasa twende sebuleni!!', Huku akimpatia mkono!!""
Walifika Hadi sebuleni na kuweka season waendelee kuangalia waliangalia Kama vipande vitano huku kila mtu akiwa kimya akifuatilia kwa makini.
Ukimya ulizidi, Ibrahimu aliamua kufunguka na kusema;
"" Inaonekana Hawa baadae watapendana si sawaa!!""
"" Ndio wanapendana Hadi Sasa Wewe huoni kwanii??""
"" Halafu Joanyther nimekumbuka kitu leo nahitaji kuzungumza na Wewe!! Sijui Kama upo tayali niongee!!""
""Aaah!! Kuzungumza Nini tenaa!!!'' Mpaka twende mtoni Kwanza ndio utazungumza.""
Mida kidogo walijiandaa na kuwaaga walinzi wataelekea mtoni kuvua samaki, watawahi kurudi.
Safari Yao ilifika tamati. Joanyther Alikuwa amemis Sana kuogelea alifika na kubadilisha nguo ili aweze kuogelea alimuita Ibrahimu amfundishe kuogelea Muda wote yeye hakuwahi kuogelea.
Ibrahimu Alikuwa Ni Mwoga Sana hata alipoingia mtoni alitoka mbio huku akipiga kelele anakufa, lakini Joanyther alimshawishi mpaka akaingia majini Japo alikaa mwanzoni huku akiogopa maji mengi.
Joanyther aliamua kumrudia Ibrahimu na kumpeleka kwenye maji marefu Japo mwili wote ulikuwa ukitetemeka kwa hofu, lakini Joanyther alimtoa hofuu;;
"" Ibrahimu!! Wewe Mwoga hivyo?? ""naomba mikono yako uikusanyie kiunoni kwangu Mimi ndio nitakuwa naogelea nataka nikupeleke kwenye maji Yale ya blue. "" Sawa!!!?""
Ibrahimu alifanya vivyohivyo Lakini baada ya kumshika tu kiunoni. Joanyther alihisi khari ya tofauti Sana na kubaki akimtazama Ibrahimu machoni, feeling zilienda mbali Sana alianza kumuona Ibrahimu kwa mtazamo Mwingine alianza kujadili uso wake ulionekana unavutia Sana nakusema "" Kweli Wewe Ni Handsome""
Ibrahimu na yeye alizidi kumshangaa Joanyther, na kumuona Ni mrembo Sana na Alikuwa ashaanza kumpenda siku nyingi, alizidi kumkumbatia kwa hisia Kweli.
Baadae Joanyther ndipo anazinduka kwenye dibwi la fikira, alimwachia Ibrahimu na kumsukuma pembeni, moja kwa moja Ibrahimu alianza kuzama kwenda chini na Muda huo hakujua kuogelea alianza kunywa maji.
Joanyther alijitosa Hadi chini kumsaidia Ibrahimu, Alifika Hadi chini akiangaza Huku na kule hamuoni mpaka pumunzi zilianza kumuishia ilibidi arudi Tena Hadi juu kuvuta hewa na kurudi Tena kumtafuta.
Juhudi zake zilizaa matunda Baada ya kumuona Ibrahimu kaegama kwenye jiwe huku akiwa kakata Moto , Alimchukua na kutoka nae Hadi juu Kisha alimtoa kwenye maji na kumpeleka sehemu yenye hewa na kuanza kutoa msaada wa kwanza.
Alimtolea maji kwa kukandamiza kifua chake baada ya hapo alimwangalia na kuona pumunzi Bado hazimtoshi vizuri, Aliinama na kugusanisha midomo yake huku akimpulizia pumunzi, wakati anafanya hivyo Ibrahimu aliamua kutoa sapoti na yeye!
Upande wa Ibrahimu baada ya kukandamizwa kifua maji yakamtoka, alijisikia vizuri Ila aliamua amtege Joanyther akiisubili romance mdomo kwa mdomo apate pumunzi nyingine na hio ndio Ilikuwa furaha yake siku hiyo.
Joanyther alimsukuma Ibrahimu na kuanza kumurushia ngumi za usoni.
"" Unanitania kumbeee!! Mimi ndio wakukufanyia hivyo Wewe hafu ndio uning'ang'anie??""
"" Wewe hicho tu ndo umeumia!!?""
umesahau aliyeanza uchokozi Ni Nani??, kwahiyo ulizamilia leo kuniua kwenye maji??'' naona ugomvi umeanza toka mchana Visa vingi ili uende kwa Jolvin mpaka ukataka kuniua kwenye maji!!, Kwanini usiende kimya kimya pasipo kunidhuru Mimi, kwanini unanichukia hivyo Joanyther??!""
Ibrahimu aliamua kuondoka huku nguo zikiwa Bado zimelowa na maji.
Joanyther alichukua nguo na kuanza kumkimbilia Ibrahimu, Huku akizidi kumbembeleza.
"" Ibrahimu naomba nielewe basi, sio dhamira yangu hiyo naomba ubadilishe Basi mavazi kwanza kabla hatujafika nyumbani itakuwa hatari kwetu!!!"
"" Hatari ganii!!?" Si umetaka iwe hivyo leo!!'' umeamua kuharibu siku yangu!!!' SIVAI•``
Joanyther alishidwa kujizuia aliamua kuanza kulia Kisha alikaa chini huku akiwa kakumbatia begi lake la nguo.
""" Ni maisha gani haya Mimi nitaishi siku zote mtu hutaki kuombwa msamaha, huoni unanipa wakati mgumu Leo hii nitaenda kusema Vipi familia yako ikanielewa, basiii!!! Kama Ni kutoroka nitatorokea hapa!! Siwezi nikafika Hadi Nyumbani!! """
Ibrahimu alizidi kusonga mbele baadae Alikuja kugeuka nyuma hakumuona Joanyther Tena, Aligeuza mbio huku akimrudia alifika na kumkuta kajikunja huku baridi ikimpiga.
"" Nimerudi bhana kuvaa!! Sasa mbona unalia??
Alichukua begi na kuchukua nguo zake akaenda kuvaa, baadae alirudi na kumkuta Joanyther Bado kajikunyata na Baridi.
"" Sa' mbona Wewe wachukia hivyo hutaki hata kuongea na Mimi wakati Mimi ndio ilibidi nikununie please kavae Basi twende nyumbani wataanza kututafuta!!"
Joanyther alibadili mavazi yake na Safari iliendelea Hadi Nyumbani.
¶¶¶¶
Huku upande wa Jolvin, Collin na Razack' walikuwa wakimfatilia Joanyther tangu mtoni mpaka wanafika nyumbani, matukio yote walikuwa wakijionea mbele ya macho Yao. Na jitihada zao walitaka waongee Ana kwa Ana na Joanyther wamfahamishe kuja kwao.
Jolvin muda huo Alikuwa na maswali mengi akijiuliza moyoni;
" Joanyther Hivi wajua kuwa nakupenda lakinii??'' inaonesha tayali umezama kwa Ibrahimu, kumbuka hapa nimekuja kwaajili yako nikurudishe!! Vipi huwa unanipenda lakini!!??""
,,,,,, Itaendelea,,,,,,,,,,
Usikose sehemu ya kumi na mbili.
Nini kitafuata Kati ya Watu Hawa Ibrahimu, Jolvin na Joanyther?? Je Joanyther ataondoka amuache Ibrahimu ikiwa tayali kaanza kuonesha kumpenda??
Usisahau👍 Like, comments, Share.
MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: , 12 "0746638941"what'sup"
SONGA NAYO.
Jolvin muda huo Alikuwa na maswali mengi akijiuliza moyoni;
" Joanyther Hivi wajua kuwa nakupenda lakinii??'' inaonesha tayali umezama kwa Ibrahimu, kumbuka hapa nimekuja kwaajili yako nikurudishe!! Vipi huwa unanipenda lakini!!??"" ENDELEA.
Collin alimsogelea rafiki yake na kumbembeleza. Aliona rafiki yake anampenda Sana Joanyther, Japo na yeye huwa anampenda.
"" Usiwaze hivyo Wewe amini Joanyther tutarudi nae ""
Razack' aliamua kumtania Jolvin.
"" Sasa Jolvin!!! Unaumia Nini na wakati hujawahi hata kumwambia kuwa unampenda!! Inaonekana jamaa imeoa hiyo!!""
"" Wewe Razack' acha hizo utaua watu na Nyoyo zao jamani, Mimi nimegundua toka zamani Jolvin anapenda bhanaa!!!"". Hivi mwajua leo ndio siku ya pili Hakuna hata tulichokifanya na kesho ndio siku ya mwisho ndio tulivyoongea na Cheaf tunafanyaje hapaa!!?? ""
"" Hapa inabidi tuandike vitu tulivyovipenda hapa halafu tutaomba atuongezee siku mbili ili tufanye masoko Kwanza tuulizie miti inavyonunuliwa na bei yake!! "" Jolvin alitoa hoja.
"" Hii kazi ngumu lakini!! Hebu fikiria Mimi nimesomea Afya leo tena nianze utafiti wa miti jamani!!! Daaaah!! Hizi kazi zina wenyewe. Razack' aliongea na kuwafanya wenzake waangue kicheko.
"" Naomba tu tusikate tamaa!! Siku tukikamilisha kazi yetu ya kumrudisha Joanyther Chuoni naona tayali tunaenda kuwa millionea!!"" Collin aliongea.""
"" Nyie mnawaza tu kuwa millionea tukifanikisha kumpeleka, halafu hamuwazii kuhusu Mimi nitaishije baada ya Joanyther kupelekwa kwenye chuo Cha Utafiti!! Vipi Kama watagundua kitu kinachotafutwa miaka yote kipo mwilini mwake huoni kama atamilikiwa na Chuo hicho yaweza akapoteza maisha kabisa!!"" Alikuwa Jolvin.
"" Sasa na Wewe usimpende Kwanzaa, mpende siku akikamilisha project yetu akikutwa Hanaa!! Mchukue Tena Oa'' kabisa!!!"" Alikuwa Razack'.
"" Lakini Collin,,,!!, Mbona na Wewe huwa unampenda!!! Au Ni kitu gani wakiplan kutoka kwake. Jolvin aliuliza.
"" Wewe hujui tu, " Kila mwamba ngoma hujivutia kwakee!!! Basi twendeni tusishitukiwe!!
¶¶¶¶
Huku ndani upande wa Joanyther na Ibrahimu baada ya kufika kila mtu Alikuwa amechoka Sana waliamua kupumzika siku hiyo.
Ibrahimu Alikuwa akiweweseka ndotoni tena akiota huku akipiga makelele. Joanyther baada ya kusikia kelele hizo alinyanyuka kitandani kwake na kwenda Hadi kitandani kwa Ibrahimu.
Ibrahimu Alikuwa akiota huku akiongea kwa huzuni Sana huku machozi yakimtoka pasipo kujua.
"" Joanyther naomba usiondoke katika Kijiji hiki naomba ubaki na Mimi, hata Kama utaondoka naomba usirudi Chuoni""
Joanyther hakuelewa Ibrahimu anamanisha Nini, tena Alikuwa akionesha uhalisia wa kitu anachoongea. Aliishia kumtizama tu Kisha alimfuta machozi na kumfunika blanket na kumuacha akiendelea na usingizi.
Kisha alielekea kwenye kitanda chake na kukaa huku akikumbuka maneno ya Ibrahimu na kuanza kuwaza Sana.
"" Kila siku Ibrahimu anaweweseka usingizi akiota ndoto za ajabu, Hivi Kuna Nini Kati Kati Mara hataki kusikia Jolvin, Mara Unataka kwenda kwa Jolvin kakuijia!! itabidi nichunguze vizuri.""
Muda kidogo Ibrahimu aliamka na kumwangalia Joanynther Muda wote Alikuwa amekaa kitandani kwake alimfuata na kukaa nae.
"" Vipi Joany!! Mbona haulali leo!!??"
"" Nitalalaje wakati Wewe unaweweseka usiku na Ndoto sijui una tatizo gani??""
"" Nilikuwa naota kwanii!!?? "
"" Ndio!!! "
"" Huenda Kweli, nimekuwa na hofu juu yako, au ulitaka kunitoroka!!?? "
"" Nikutoroke niende wapi!!??""
"" Si kwa Jolvin!!""
Joanyther Alisituka kidogo baada ya kusikia jina la Jolvin, alianza kuunganisha matukio ya nyuma na maswali mengi, "" Kwanini Ibrahimu Muda wote anamtaja Jolvin!!?? ""
"" Mbona una hofu hivyoo??" Vipi, nimekuuzi?? Basi nikuache Mimi nikalale lakini nakuomba pia na Wewe ulale!! "" Ibrahimu aliuliza.
"" Sina usingizi leo!! Naomba tuongee tu mpaka kupambazuke""
Ibrahimu alikubaliana nae alisogea na kukaa nae kitandani, Kisha aliuchukua mkono wake mmoja na kuuweka shingoni na kumwambia;
"" Jana uliniahidi tukienda mtoni!!! utanipa Muda wa kuzungumza na Wewe, lakini haikuwa hivyo, vipi Naweza kuzungumza!!?? ""
Joanyther alimshika mkono Ibrahimu na kuutoa Kisha aliuweka kitandani Kwanza.
"" Sawa waweza zungumza!! "" Lakini mkono wako mzito nitakuwa na kibiongo bhanaa!! ""
Ibrahimu alicheka tu, Joany, Nuru yangu siku zote una maneno mengi Sana , Hebu nione mikono yako kwanza. Huku akiishika shika.
Mikono yako inaonekana ina bahati na unanyota nzuri.
Okay nisipoteze Muda kitu chenyewe ninachotaka kukwambia tu.
"" Nakupenda Joanyther naomba nikuoe rasmii!!"
Joanyther alibaki akimwangalia Ibrahimu pasipo kumjibu chochote, akiwa haamini kitu alichozungumza.
Ibrahimu alimuona Joanyther kaduwaa Kama anataka kusema kitu, alimuwahi kwa kumkumbatia Kisha alimwambia.
"" Naomba usizungumze kitu chochote Kwanza, Wewe pokea ombi langu lifanyie kazi, Kisha alimwachia na kumbusu kwenye paji la uso.""
Joanyther alibaki akiduwaa huku macho yake akiyatizama chini ili kumuepuka Kumtizama Ibrahimu machoni.
Ibrahimu Alisimama na kumuaga tena Joanyther.
"" Uwe na usiku mwema kwako!!", Naomba kwa Sasa jisimamie peke yako''' sitakubana tenaa, ukitaka kutoka toka Ila kumbuka maneno yangu na uyafanyie kazi.""
Siku iliyofuata Joanyther alijaribu kumuepuka Ibrahimu alitoka zake Nje na kukaa huku akipungwa upepo. Ibrahimu alimfuata na kukaa nae alikuwa na kitu Cha kuongea nae.
"" Joany naondoka kidogo nmeitwa huko kwa Cheaf nitarudi jioni naomba jisimamie peke yako!! '''
"" Sawa bhanaa!!! Ani Muda wote wanambia nijisimamie pekee kwani Mimi sijui bhanaa!! Wewe Nendaa tu!! ""
Ibrahimu alicheka tuu Kisha alichuma machugwa matatu mtini na kumrushia.
"" Kula bhanaa!! Muda wote umekaa hapo, wamsubili Athuman aje akuchumiee!! ""
Joanyther alidaka kwa Awamu kila chugwa, Kisha alianza kumenya na kula.
"" Daaaah!!! Ulijuaje kuwa namsubili Mathew na Athuman hapa waniangulie, ubarikiwe mwayaa!! ""
Muda kidogo Ibrahimu anatoka alipishana na vijana Watatu wakiwa wanaelekea kwake alisalimiana nao na kuagana nao.
Ibrahimu aliingiwa na hofu baada ya kuwaona wageni wale, aliwafahamu toka siku Ile kawaona Nyumbani kwa Cheaf, lakini aliwapotezea na kuendelea na Safari yake.
Wageni wale walifika Hadi kwa Joanyther waliongea na walinzi na kuwaomba wawache kidogo wana mazungumzo ya faragha
Joanyther aliwakalibisha Hadi ndani na kuandaa kinywaji huku wakiendelea na stori, Muda huo Alikuwa Bado hajawatambua.
Baaadae Jolvin alitoa kofia yake na zile ndevu Kisha alimgeukia Joanyther na kumuita.
"" Joanyther umenisahau hata Mimi!!""
Joanyther Alisituka baada ya kumuona Jolvin aliamua kuuliza.
"" Jolvin Ni Wewe Kweli??"" Alisimama na kumkumbatia. " Nilihisi tangu zamani utakuwa Ni Wewe!! Hafu mpo wote Ma prince isipokuwa Alvin???""
""" Sawa usilopoke tenaa, hapa tumekuja kwa ajili yako naomba ujiandae kesho njoo mtoni majira ya asubuhi tuondoke wote tutakuwa tukikusubili huko, Hivi unakumbuka tulitoka tumeijenga Nyumba yenu hata haujaikalia, nakuomba fanya hivyo.""
Razack'na Collin na wao walizidi kukazia, mpaka wakawa wameelewana, Kisha waliaga na kuondoka.
Siku iliyofuata asubuhi yake Joanyther alikuwa akijiandaa maandalizi ya hapa na pale huku Ibrahimu Alikuwa kakaa kitandani akimtazama, baadae Alimuuliza;
"" Joany Safari imeiva??" Mbona huagi??""
"" Safari ya wapi tenaa na Wewe??"
Ibrahimu Alisimama na kumsaidia kupanga nguo yeye alionesha kuwa na furaha tu mpaka Joanyther alibaki akimshangaa, Ibrahimu Alimuuliza.
"" Sasa mbona waniangalia tu, si siku yako ya furaha uliyosema waitaka ndio leo!!'' Vipi una uhakika lakini utakuwa na furaha huko uendako??""
"" Ndioooo!! Maswali mengi ya Nini Wewe??"
"" Sawa!!! Twende nikutoe Walinzi wasikuzuie.""
Waliongozana moja kwa moja Hadi mtoni. Ibrahimu alifika na kuwasalimia Kisha aliwakabizi.
"" Nina mkabizi kwenu Joanyther mikononi kwenu, naomba mkamtunze siku zote awe na amani asijute kuondoka huku, hakikisheni anapata elimu yake vizuri, Sina Cha ziada zaidi niwatakieni Safari njema. Kisha aliondoka.
Joanyther alishidwa kujizuia alimfuata Ibrahimu Huku akilia alifika akamkumbatia lakini Alikuja kugundua Ibrahimu nayeye machozi yalikuwa yakimtoka, walikumbatiana wote huku wakizidi kulia mpaka kina Jolvin, Collin na Razack' waliingiwa na huruma kuona wanawatenganisha Watu wapendanao Lakini na wao hawakujali kwa sababu Ilikuwa Ni kazi.
Ibrahimu alimwachia Joanyther na kumwambia.
"" Naomba ujisimamie mwenyewe kwa Sasa utakuwa Mbali namimi Ila Mimi,""Sitàacha kukupenda!!!""
Joanyther hakuwa Na chaguo zaidi. Safari iliendelea mpaka majira ya usiku walifika kijijini kwao Joanyther, walifikia moja kwa moja hadi kwao alifika na kuanza kushangaa jengo llilokuwa kubwa limesimama alibaki akishangaa tu.
Baadae walitokea mabinti wawili walichukua mizigo na kuiingiza ndani kisha walimkalibisha Hadi ndani baadae walifatia kina Jolvin na wao walikula chakula Cha usiku na kulala.
Kesho yake asubuhi. Joanyther aliamka mapema huku akisalimia majirani zake baadae wajukuu waliosalia wa Bi Emma walikuja na kuanza kuongea na Joanyther kuhusu Bibi Yao kwa Muda ule walikuwa wamekuwa Binti wakubwa, Joanyther Aliamua kuwaambia ukweli Bibi Yao alikufa kwa malazi huku akiwaficha.
Siku iliyofuata Joanyther Alikuwa safarini akielekea Chuoni kuanza masomo yake rasmi Tena kwa mhula wa kwanza huku akiwa ameambatana na prince Watatu.
Siku hiyo Chuoni waliandaa part kubwa ya kuwakalibisha wao lakini mgeni mlegwa Alikuwa Ni Joanyther. Mpaka yeye alistaajabu kwa sherehe iliyokuwa ikifanyika siku hiyo, zawadi nyingi ziliandaliwa na kutolewa kwake ikiwa Ni miongoni mwa sale za shule pamoja na madaftari na baadhi ya mahitaji mengine.
Wakati Sherehe ikiendele, mkufunzi wa Chuo alipigiwa simu na kumfanya atoke kidogo kwenye kelele huku wakizungumza na mpigaji wa simu.
Lakini majibu yake baada ya kuongea nae Muda wote Alikuwa akimsikilizia tu baadae alijibu kwa kifupi;
"" Ndio kila kitu kipo tayali na nimeshaandaa.""
,,,,,,,,, Itaendelea,,,,,,,,,,,
Usikose sehemu ya kumi na tatu.
Ni Nini kilikuwa kinaongelewa hapo?
Share, like , comments tukutane tenaa.
MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: , 14 "0746638941"what'sup"
SONGA NAYO.
Leo upande wa Ibrahimu Alikuwa kakaa na Cheaf wakijadili kuondoka kwa Joanyther kijijini. Cheaf Muda wote Alikuwa akimlaumu Sana Ibrahimu kwa kumwachia Joanyther, lakini Ibrahimu hakuwa na maneno mengi ya kuongea siku hiyo aliwajibu tu;
"" Joanyther Alikuja kijijini kumtafuta Mdogo wake Lakini Nyie mkamkatalia akae huku, Kama Mimi nimepona mwacheni aendelee na maisha yake siku akitukumbuka atarudi huku, make hajaondoka kwa shari na Mimi ndio niliemsaidia kumuondosha huku!! ""
Mzee Cheaf Baada ya kusikia maneno ya Ibrahimu alichukia sana aliwaamuru walinzi wamchukue Ibrahimu na kwendaa nae porini kumfunga kwa siku tatu alale njaa Kama adhabu ya Cheaf.
Ibrahimu alipelekwa Hadi porini na kufugwa huku njaa ilizidi kumuuma japo alizidi kujikaza lakini haikusaidia kutokana na maisha aliyozoea kuishi.
Muda kidogo alikuja Mathew na Athumani, walifika pale na kumwonea huruma Sana. Mathew alimtizama Ibrahimu huku kashikilia kibuyu Cha maji, Athumanii aliitikia kwa kutumia ishara ya kichwa.
Ndipo Mathew alichukua kibuyu kile na kumnywesha maji.
"" Kuwa makini muda mwingine usiwe unasema ukweli, bora hata ungekana kuwa alikutoroka ona Sasa wakati huu unateseka kweli!! ""
"" Mathew Ni sawa tu, acha niseme ukweli!! Joanynther mwacheni aendelee na maisha yake Kama Ni adhabu acha niitumikie hafu, muda mwingine msinisaidie mtaharibu kibarua chenu!! ""
Mathew na Ibrahimu hawakuwa na budi ya kuendelea kukaa hapo waliamua kuondoka ili wanusuru vibarua vyao.
¶¶¶¶¶¶
Ilikuwa Ni siku nyingine tena alionekana Kijana mmoja wa makamo hivi alikuwa akikimbizwa na vijana wane, walikuwa wamejazia vifua vyao tena na maumbo yao yalikuwa ya miraba, walionekana Ni vijana wanaopenda Sana mazoezi na wakakamavu.
Vijana Hawa walikuwa wakimukimbiza kijana huyo, huku wakijali Sana maisha ya kijana huyo, lakini kwa bahati Mbaya kijana aliwapoteza kwenye Msitu na kujificha huku akihema Sana na kusema:
"" Ni mwaka mmoja nipo kifungoni kwa kosa ambalo halijulikani tangu watu Hawa walipoteketeza nyumba yetu kwa Moto sijajua hata wanataka Nini, Ee Mungu ninusuru kwa janga hili!! ""
Vijana wale walitawanyika huku na kule wakimtafuta, kijana mmoja aliwaita wenzake kwa kupiga mrusi, Kisha walikimbia eneo husika.
"" Mwoneni kijana mwenyewe huyo hapo katulia kwenye kichaka Kama haoni.
Walianza kupongezana kwa furaha huku wakiachia cheko ya ushindi na kuanza kushushia Mvinyoo, waliokuwa wameandaa na kuweka kwenye vibuyu.
Upande wa kijana huyo hakuwa mwingine bali alikuwa Ni Movick, mdogo wake na Joanynther, aliekuwa kapotea kwa muda mrefu pasipo taarifa zake kupatikana.
Movick baada ya kuona , vijana waliokuwa wakimfatilia wametulua huku wakinywa pombe za jadi, aliamua atoke pale huku akinyata ili aweze kunusuru maisha yake.
Lakini kabla hajatoka kijana mmoja alishituka na kumnasa mshale mguuni.
"" Dogo tulia unazani hapa hatukuoni, hujui hapa tukikupoteza Wewe, Dili letu litaenda kuharibika, umetutoa Mbali Sana na leo tunakuludisha kwenye chuo Cha Utafiti na sisi tupate pesa yetu then tulale mbele.""
Movick baada ya kunaswa na upinde mguuni jeuri yake iliishia hapo!! alianguka chini huku akilia kwa maumivu Sana, huku akijalibu kuuvuta ule mshale Hadi akautoa.
Kijana mmoja alisimama na kumfuata Movick Hadi pale chini alipokuwa, Kisha aliuchukua ule mshale na kumchoma nao mkononi huku akitikisa kichwa chake.
"" Wewe!! Ni mtoto tu huna namna ya kufanya kwa Sasa, Tayali mikono yako ina jeraha, na ukiendelea nitakutoboa hayo macho yako yote!! Kisha alimwacha na kuendelea kunywa pombe na wenzake!!""
Usiku uliingia tena, kuamkia siku ya tatu Ibrahimu amalize Adhabu yake, leo walinzi wa Ibrahimu, Waliamua tena kumrudia Ibrahimu kumwangalia khari yake huku wakiwa wamemuandalia uji na chakula Cha kutumia.
Kadili walivyozidi kwenda, kwa mbele kidogo waliona Moshi ukifuka, na Moto ukiendelea kuwaka.
Waliamua kufatilia ule Moto, walipokalibia waliona Kuna watu wane,.wamekaa huku wakipiga stori, na kuandaa nyama ya pori wakiichoma.
Ibrahimu na Mathew walisogea kidogo wasikie wanna ajenda gani pale. Lakini kwa mbele walimuona kijana mmoja yupo kwenye mti kafugwa kamba mikononi na miguuni alionekana kalegea sana.
Ndipo kijana mmoja alisikika akisemaa;
"" Zoezi tumekamilisha, kesho mapema tumchukue kijana wetu tumtoe katika Kijiji hiki, tukifika mjini tuchukue gari Mpaka kwenye chuo kile Cha Utafiti.""
Kijana wa pili aliamua kuwauliza wenzake.
"" Hivi kwanini kijana huyu wanamhitaji Sana kwenye kile chuo!! Unajua najiuliza Mpaka kutoa mkwanja mrefu hivi sio bule!! ""
Kijana wa tatu na yeye alijibu.
"" Hayooo!! Watajua wao kikubwa sisi tumepiga mkwanja inatosha, Lakini nilisikia pia kwenye kile chuo Cha Utafiti Kuna dada'ke na yeye anahitajika pia. ""
Kijana wa nne.
"" Daaaah!!! Watafiti wakiamua kufanya vitu huwa Ni hatari!! Na Tena kitu kikiingiliwa na mtu mweupe daah!! Tutapandikizwa Hadi virus vya Corona!!
Muda huo Mathew na Athumani walikuwa wakisikiliza hoja zile, lakini Mathew aliamua kumshilikisha mwenzake alikuwa na jamboo:
"" Hapa Kuna kitu kinaendelea, naomba tufanye kitu, tumkomboe kijana huyo hafu tuondoke nae Hawa tupambane nao, Kisha tutamhoji kijana kila kitu atatuambia.""
Mathew aliamua kumuuliza:
"" Vipi ule unga wa usingizi unao!! Hapa uwezo wa kupambana nao hatuna naona wamejazia Sana, tuingie pale tuwapake ule unga uwazimishe, na sisi ndio tukimbie na kijana!! ""
"" Wazo zuri naomba tulifanye vivyohivyo!!!""
Muda ule Movick alikuwa na machale Sana, alihisi Kuna watu wanakuja sehemu hiyo, alijua Ni watu wabaya alianza kunusuru maisha yake tena!! Kwa kufungua kamba miguuni na mikononi Mpaka alipofanikisha, alimaliza kufungua Kisha akarudishia kamba Kama zilivyokuwa, huku akiisubili watu wale wajitokeze ndipo na yeye akimbie.
Muda huo huo, Mathew na Athumani walitokeza pale huku wakiwa tayali wameandaa Unga wao, walifika pale na kuwapakaa usoni Japo walijitahidi kufurukuta lakini jitihada zao ziligonga mwamba, Dawa tayali Ilikuwa Imeanza kuwalegeza, wakawa wameshiwa nguvu na kuzimia pale pale. ""
Baada ya kumaliza Kukabiliana na vijana hao, na kuhakikisha wote wamezima ndipo wanageuza jicho upande wa pili wakimwangalia Movick, lakini walikuwa tayali wamechelewa Movick alikuwa kashaondoka na kutokomea.
Upande wa Movick, Alijitahidi kukimbia huku akiuvuta mguu wake uliokuwa umechomwa mshale na maumivu makali alizidi kuyasikia lakini alizidi kujikaza.
Jitihada zake za kukimbia zilimfikisha kwenye kichaka kimoja aliamua kupumzika ajifiche hapo, lakini kabla hajaingia kwenye kile kichaka alisikia sauti ya mtu akilia huku alihitaji msaada!!
Alisogea Mpaka akaifikia sauti iliyokuwa ikisikika pale, ndipo alimuona Ibrahimu kafugwa kwenye mti, Movick alimhurumia Sana kijana huyo, akili yake ilimtuma na yeye atakuwa miongoni mwa watu wanaotafutwa.
Alianza kumfungulia kamba pale Kisha alimaliza na kumwambia;
"" Tafadhari tukimbie wale watu wanatuijia tena, hawapo Mbali na sisi wapo karibu, tuondoke Tafadhari!!! ""
Ibrahimu alikuwa bado kalegea mwili wake hakuwa na Nguvu hata za kukimbia, alimgeukia Movick na kumwambia;
"" Wewe nenda tu Mimi Adhabu yangu naimalizia usiku wa Leo!! Ni masaa kadhaa yamebaki naomba niache nimalizie adhabu hii!! ""
"" Hapana siwezi kukuacha nakuomba tuondoke, adhabu hii haikufaa iwe yako kwani umekosea Nini Mpaka uazibiwe?? Mimi pia sijawakosea waoo!! ""
Movick Alimchukua Ibrahimu huku akimkokota taratibu na kuondoka sehemu ile, walitembea umbali kidogo Kisha walifika kwenye kichaka na kuamua watulie hapo.
Movick alitoa kkibegi chake kidogo, alikuwa kahiifadhia chakula alitoa chupa ya chai na kikombe Cha plastic Kisha alimimina ile chai na kuchukua siles mbili za mkate Kisha alimpatia Ibrahimu ale.
Ibrahimu alichukia mkate ule, alikula kwa pupa Sana huku Movick akimwangalia Sana na kuanza kucheka.
"" Vipi ulikuwa na njaa ee!!! ""
Ibrahimu hakumjibu baadae aliona kwa pembeni Kuna nyama ya kuchoma alichukua na kuanza kula kwa pupa Tena, baada ya kushiba ndipo Ibrahimu alimjibu;
''" Nashukuru Sana, kumbe! Njaa ndo huwa inauma hivii!!!, Leo ningekufa et!! Basi ngoja nilale tutaongea keshoo!!"
Upande wa Mathew na Athumani, walizidi kumtafuta Movick pasipo majibu yoyote.
Waliamua kuachana nae, ikabidi waendelee na kazi Yao waliokuwa wamefata, walifika Hadi sehemu aliokuwa kafugwa Ibrahimu lakini hawakumuona mtu pale.
Walianza Tena kumtafuta huku na kule, mwishowe walichoka na kuamua kupumzika Kwanza watamtafuta asubuhi.
Kulipopambazuka asubuhi, Ndipo Ibrahimu anaamka aliangalia huku na kule haoni mtu, akili yake ilienda mbali Sana.
""" Hivi nilikuwa naota!! Jana si nilikuwa na ka kijana kadogo kadogo Hivi kameenda wapi?? Hapa nakumbuka ndio kalinileta mbonaa!!"
Muda kidogo Movick alitokea huku akiwa ameshikilia sungura wa kuchoma alifika pale na kuweka chini, Kisha alimuuliza Ibrahimu.
"" Ulikuwa na hofu Sana juu yangu?? Make naona unanitizama tu Kama Kuna kitu wataka kusema!!!?? ""
"" Walaa!!! Kwani Wewe Ni Nani?? Na umetoka wapi?? Na kwanini uko hapa!! Hafu kwanini ulinisaidia?? ""
"" Umeuliza maswali mengi Sana!! nitakujibu pia na Wewe nitakuuliza; "" Mimi niite Movick!! Wewe nikuite nanii??"
"" Niite Ibrahimu!! Sasa!!, Wewe Ni Nani lakini!!??""
"" Kula kwanza bhanaa!! Wewe naona bado unanjaa!!! ""
Ibrahimu aliendelea kula lakini Muda wote alionekana alimtizama Sana Movick.
Movick na yeye Alisituka baada ya kutizamwa Sana, alimuuliza Ibrahimu;
"" Mbona wanitizama Sana hivyo!! Au huniamini Mimi kuwa na Wewe!!??
"" Kumbe!! Umeniona!!??, Basi tu!! Nakufananisha na Mwanamke mmoja, niliwahi kuishi nae miaka ya nyumaa!!! "
"" Ndio Mimi wa kufananishwa na Mwanamke wakati Mimi Ni wakiume, mbona unadhalau Sana Ibrahimu!!! ""
""" Samahan bhana!!; Sikuwa na maana hiyo!! Umenitafsili vibaya tu. ""
"" Kwani umeoa ??? ""
"" Aaa aaah!! Hapanaa!!! ""
Muda kidogo Athumanii na Mathew waliwafuma pale, wakiwa wamekaa wakipiga stori zao, huku wakiendelea kula.
,,,,, Itaendelea,,,,,,,,,
Usikose sehemu ya kumi na tano.
Kipi kitafuata baada ya Ibrahimu na Movick kukamatwa, na vipi kuhusu Movick baada ya kufikishwa kwa Cheaf, Je, Atapokelewa!!!??.
Like, comments, Share. Nitume chap!!!
MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: , 13 "0746638941"what'sup"
SONGA NAYO.
Wakati Sherehe ikiendele, mkufunzi wa Chuo alipigiwa simu na kumfanya atoke kidogo kwenye kelele huku wakizungumza na mpigaji wa simu.
Lakini majibu yake baada ya kuongea nae Muda wote Alikuwa akimsikilizia tu baadae alijibu kwa kifupi;
"" Ndio kila kitu kipo tayali na nimeshaandaa."" ENDELEA...
Baadae mkufunzi alirudi na kuendelea kusherekea sherehe hiyo Mpaka ilipomalizikia.
Siku nyingine tena, Joanyther alikuwa darasani akiendelea na masomo yake. Leo upande wa Three princess walimtembelea kwa pamoja.
Ancillah alikuwa Ni mzungumzaji mkubwa siku hiyo.
"" Joany naomba Leo tutoke wote twende party tukasherekee kidogo kwa pamoja make tulikumisi Sanaa!!"
Joanyther hakuwa mgumu aliwakubalia kuwa watatoka wote siku hiyo.
Muda kidogo alifika Jolvin na kumuomba atoke kidogo na Joanyther. Walielekea kwenye darasa moja lilikuwa wazi, waliamua kupumzika hapo wakipiga stori.
Jolvin alikuwa na vitabu vichache alikuwa navyo, alitoa pale na kuviweka juu lakini kwa bahati Mbaya anatoa alikuwa na syringe kaandaa ya 2cc.
Joanyther aliiona Ile sindano na kuamua kumuuliza.
"" Vipi Jolvin siku hizi wajali Sana masomo Mpaka unatembea na bomba la sindano??.""
"" Aaaah!! Hapana nimejisahau tu Jana nilikuwa kwenye practical nikawa nimesahau.""
"" Sa' mbona unakuwa na kauoga Tena, au hukutaka kuwa nayo hapa!!!?""
"" Hapana bhanaa!! Kawaida tu, Naomba tuachane na hilo, Vipi lakini Safari yako Ilikuwa na Amani huko??"
"" Ushaanza bhana!!, Mwanzoni Ilikuwa na Huzuni Baada ya kumpoteza Bibi yangu Lakini baadae nikawa na Amani Baada ya Kumzoea Ibrahimu.""
""" Kwani!!, huyo Ibrahimu Ni Nani??
"" Maswali yako bhanaa!! Ni mtoto wa Cheaf, unajua simulizi yake inasikitisha Lakini sijui hata nimemuacha Ana khari gani, nayeye anajali Kama Wewe tu unijalivyo!! ""
"" Hivi Joanyther!!! Mimi huwa wanichukuliaje Kwanza kwako?? ""
"" Mhuu!! Ni rafiki Mwemaa!! "
"" Rafiki Mwemaa tu ' Basiiiii!!!! "
"" Yaaah!!, Kumbe hivyoo tu!! ""
"" Wewe je, wanichukuliaje Mimi!! ""
"" Rafiki zaidi ya rafiki, means Mpenzi!! ""
"" Mhuuu!! Tusome bhanaa!! Utani uachee!!"
Jolvin alichukua Ile syringe na kuishikilia huku akiitizama kwa makini Kisha aliiweka chini. Huku Joanyther akiwa anamtizama pasipo majibu yoyote aliamua kumuuliza;
""" Leo una Nini Jolvin!! Lakini??
Jolvin aliamua kumjibu.
"" Vipi Kama nitakuwa nimetumwa kuuondosha uhai wako, utanisamehe!!?""
"" Wewe una Nini Lakini leo??", huku akimnusa kutafiti Kama kanywa pombe, "" Mbona hata hujalewa Lakini una maswali ya ajabu!!"
Jolvin alimsogelea Joanyther akiwa kashikilia Syringe, Kisha alimshika mkono ili aweze kutoa damu. Alimuuliza Tena;
"" Vipi Kama nitachukua damu yako, Wewe utanichukuliaje??""
Baadae ndipo Joanyther anakuja kutambua kuwa Jolvin yupo siliazi na kitu anachotaka kukifanya. Alimpiga kwa teke na kuanguka chini Kisha Alitoka pale anakimbia huku akiwa anahema kwa Kasi ya ajabu Sana.
Mbio zake zilienda kuishia kwenye mikono ya Alvin Baada ya kudakwa huku akiwa hoi akielekea chini kuanguka.
Alvin alichukua kitambaa na kumfunika Joanyther usoni, akiwa amenyunyuzia dawa ya usingizi, alimbeba na kumpeleka Hadi chumbani kwake Kisha alichukua Syringe ya 5cc alichukua na kufyonza damu Kisha aliachia tabasamu kubwa usoni na kujisemea.
"" Nilijua Jolvin huwezi fanikisha kitu Wewe ukitaka kufanya kitu punguza maneno mengi, unamuua nyani huku watizama machoni na unaunganisha feeling za Mapenzi!! Wewe bado Sana!!.""
Alvin Baada ya kuchukua damu alitoka haraka kuelekea Sehemu ya Maabara kupeleka Ile sample, Alifika na kumpa Specialists aliekuwa anahusika pale Kisha alimpa maelekezo na kuanza kuifanyia kazi Ile sample.
Upande wa Jolvin Baada ya kuzinduka pale Baada ya kipigo Cha Joanyther aliamka pale na kuanza kumtafuta Joanyther huku na kule baadae alifika Hadi chumbani kwa Alvin na kumkuta Joanyther kalala usingizi huku hajitambui, mkononi aliona kawekea plasta ilizihilisha tayali damu imechukuliwa.
Alimsogelea pale kitandani huku alkimhurumia Sana Kisha alikaa na kuanza kumtizama tu, Huzuni na huruma ilimuingia na kuanza kumtengenezea nywele zake.
"" Joanyther sikudhamilia iwe hivi, nilijua kazi hii sitaweza nitashidwa tu, natamani kukulinda Ila nafosiwa na watu waliombele yangu. "" Vipi ukiamka ukanikuta nipo mbele yako utanisamehe!!?""
Jolvin alizidi kuwaza baadae aliamua kuondoka pale ili isiwe msala baada ya kukutwa hapo. Lakini kabla hajatoka pale Joanyther aliamka na kumshika mkono.
"" Mbona unaniacha tena katika khari hii!!?? Ni kweli niliyoambiwa na Ibrahimu nikae Mbali na Wewe ndio hivyo inatimia!! '"
Jolvin ilibidi arudi akae ili azungumze vizuri na Joanyther.
"" Joanyther nisamehe Mimi!!! Sikuwa na kusudio la kufanya hivyoo!! Hii Ni kazi tu natumikishwa na Mimi!! ""
Lakini Joanyther alimtizama na kumjibu kwa upole tu.
"" Hata Wewe unayenipenda leo wanifanyia hivyoo!!?? Kumbe kunijali kote huko ulikuwa wataka univute kwako niwe karibu na Wewe halafu ukamilishe kazi yakoo!!? ""
"" Nisikilize Kwanzaa!!! Joany!!!""
"" Haina maana kwa Sasa damu yangu mshachukuwa tayali!!. ""
Joanyther alisimama pale Japo alionekana Mwili wake hauna nguvu baada ya kuchomwa sindano Ile, alitembea kwa kuyumbayumba, muda huo Jolvin alikuwa akimtazama tu.
Baadae aliamua kumsaidia kwa kumshikisha ili atembee, lakini kadili alivyozidi kutembea nguvu zake zilizidi kumuisha, ndipo Jolvin alimbeba na kumpeleka Hadi chumbani kwake akimpatia huduma ya Kwanza.
Alichukua drip ya maji na kumtundikia ili apate nguvu Kisha alimchoma sindano kwenye paja ya kumuongezea nguvu "x.pen'' na kumuacha huku kapumnzika.
Baadae alimretea chakula na matunda, alifika akaweka mezani na kumuomba ale ashibe, Muda huo Joanyther alikuwa kashaamka akimtizama Jolvin anavyomenya matunda pasipo kusema chochote.
Jolvin alichukua kipande Cha Chungwa na kumpatia Joanyther;
"" Tafadhari naomba kula Kwanza ili dawa ifanye kazi!!"
Joanyther alitikisa kichwa tu akiashilia hayupo tayali kula.
Jolvin alimsogelea na kumshika mkono Tena.
"" Damu inaenda kukuishia hivyo nakuomba Tafadhari kula upate afya!! Kuna watu bado wanakuhitaji uishi, bado Wana nafasi kwako!!""
Joanyther alionekana akisusa tena kwa kusukuma kile chakula nusra kidondoke chini lakini Jolvin akawa amekiwahi, Baadae aliamua kuondoka huku Akimwambia;
""" Naomba ujisimamie mwenyewe Mimi sitaweza tena kukusimamia!! ""
Joanyther alisimama pale huku akijitahidi kujisaidia mwenyewe. Lakini Muda huohuo Alvin aliingia moja kwa moja na kumsaidia Joanyther kumsimamisha Kisha alimkalisha chini.
""" Joanyther!! Kwa Sasa haupo vizuri naomba ule Kwanza ushibe ndio utaweza kujisimamia mwenyewe!!"
Joanyther alionekana kukubali, Alvin alichukua chakula na kuanza kumlisha Taratibu huku akijaribu kumchekesha Joanyther, lakini Joanyther alimuuliza Alvin.
"" Hata Wewe Unaweza ukanichoma sindano!!? ""
Alvin alishituka kidogo baada ya swali la Joanyther.
"" Sindano ya Nini tenaa!! Kwani umeandikiwa na Dokta sindano za masaa!!!??""
"" Hapana!!!, niliuliza tu nipate majibu, but hamna tatizo!!"" Kisha aliendelea kula lakini hakili yake ilimtuma Alvin hajui chochote, lait angejua kuwa yeye ndio kahusika hata kuchukua sample sijui ingekuwaje tu.
Upande wa Jolvin aliamua arudi ili amuone mgonjwa wake anaendeleaje, lakini alifika na kushangaa baada ya kukuta Alvin na Joanyther wanacheka kwa furaha.
Alijikaza na kusogea kusikilizia kipi walikuwa wakizungumza Mpaka kukawa na furaha Ile.
Joanyther alipaliwa chakula baada ya kucheka Sana akiwa na chakula mdomoni, Alvin alichukua maji na kumnywesha huku akiwa anampoza kwa kumpiga mgongoni na akimwachia maneno ya kumsindikiza;;
"" Katoto, kazuri, karembo kamepaliwa jamani shetani huyu naona yupo mawindoni akikatafuta kaumie!!""
Ndipo Joanyther anaachia tabasamu akicheka kwa furaha na kuanza kumpiga kwa kulushiana chakula Kama kamchezo.
Jolvin aliona ule mchezo na kuzidi kuumia aliamua kuondoka pale asizue balaa jingine make mhusika Alikuwa tayali kajisafisha hivyo mzigo uliangukia kwake hakuwa na budi kuubeba.
,,,,,,, Itaendelea,,,,,,,
Usikose sehemu ya kumi na nne.
Kipi kitafuata katika mkasa huu Kati ya Jolvin na Alvin, na Vipi kuchukuliwa kwa damu ya Joanyther itakuwaje??
Like, comments, Share. Tusonge mbele.
MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: 15 "0746638941"what'sup"
ANZA NAYO.
Safari ya kuelekea kwa Cheaf ilianza Lakini Movick alikuwa na hofu Sana na Safari ile, moyoni mwake alianza kukiuliza, Kumbe!! Nimemsaidia mtu tofauti na Mimi, nilijua Ni miongoni mwa watu waliopo katika kitengo Cha Utafiti kumbe sivyoo kabisaa.
Baadae Ibrahimu aliingizwa moja kwa moja kwa Cheaf wa Kijiji huku akiwa ameambatana na Movick.
Movick alikuwa haelewi elewi, alifika pale na kumwangalia Ibrahimu anavyosalimia na yeye alifata vivyo hivyo.
Cheaf aliamua kumuuliza Movick ujio wake katika Kijiji hicho, naye aliamua kujibu.
"" Mimi kwa Majina naitwa Movick!! Hapa nimefika hata Mimi sielewi, nakumbuka Kama miezi kumi na mbili imepita nlichukuliwa na watu wasiojulikana majila Kama ya usiku waliniteka na kunipela kwenye chuo Cha Utafiti Japo sijui kipo wapi, make muda huo natekwaa walikuwa wamenifunga kitambaa mpka nafikishwa.
Katika Chuo hicho Cha Utafiti Muda wote wamekuwa wakinidunga sindano na kutoa damu yangu kila siku, ndipo siku moja niliamua kutoroka na kuja Hadi kijijini kwetu lakini kabla sijafika niliona Kuna watu wananifukuzia na Mimi nikawa nimekimbilia huku.
Ndio usiku wa kuamkia leo niliona wale Vijana wananikimbiza nikawa nimejificha sehemu wakawa wameniona, na Kati ya wale Vijana Kuna mmoja alininasa mshale mguuni Baada ya kuniona nataka kukimbia ndipo wakatokea vijana wako kunisaidia.
"" Ilikuwaje tena ukataka kumtorosha kijana wangu tenaaa!!!?? ""
"" Sikuwa na Nia ya kumtorosha lakini nilimuona pale kafugwa na kamba nikajua na yeye Ni miongoni mwa watu tuliokimbia, make siku hiyo tulitoroka Kama watu wanane Hivi, namimi ndio nikaamua nisaidie nikatafuta sehemu ya kupumzika Kwanza, kupambazuke ili kesho tuone utaratibu, lakini kulipopambazuka ndipo vijana wako wakawa wametuona, Naomba usiniadhibu kwa kutaka kumtorosha kijana wako.""
"" Sawa!!! Sitakuadhibu kwa Hilo, Kwanza umeonesha kumjali Sana kijana wangu, nitakupa ruhusa ya kukaa hapa mpaka utakapoamua kuondoka.""
"" Nashukuru Sana Cheaf, kwahilo lakini naomba ulinzi wako wale watu wasinichukue nahisi bado wako hapa!! Wanaweza kurudi.""
"" Usijali kwa hilo!!! Utaenda kukaa na Mwanangu Ibrahimu, kwenye Nyumba yake ulinzi upo wa kutoshaa, Wewe kaa utulize akili Kwanza huku ukiwa wawatafuta ndugu zako!! ""
Ibrahimu Alimchukua Movick na kwendaa kuishi naye, na maisha mapya yaliendelea Kati ya Ibrahimu na Movick.
Siku moja Ibrahimu Alimchukua Movick na kwendaa nae Hadi mtoni, alifika na kukaa nae huku wakiendelea na sitori za hapa na pale, alimuuliza Movick.
"" Vipi na Wewe!! Huwa Ni muogeleaji!?? ""
"" Ngoja nikuoneshe Kwanza, ujionee make ndio kitu ulichokuwa wataka nikujibu.""
Movick alivua nguo na kujitupia kwenye maji Kama samaki, alizama kwa Muda mrefu Kama robo saa ndio akaenda kuibukia ng'ambo, Huku Ibrahimu alibaki kushangaa, huyu mtu abauwezo gani wa kuogelea mpaka robo saa kazama, "" Mbona anaogelea Kama Joanyther!!!??""
Ndipo Movick aliamua kutoka kwenye maji na kujianika kwenye jua, huku akiwa amevua shati lake, Ibrahimu alimsogelea pale na kuanza kumwangalia mwilini lakini alimuona Ana makovu mengi ya vidoti vidoti mwilini.
"" Mbona Mwili wako upo na madoa Hivi kulikoni?! ""
"" Wewe achaa tu, Mambo mengi siyo ya kusema, Kile chuo Wallah!! Wanaharibu miili ya Watu yaani Muda wote Ni sindano na Muda mwingine wanakukata vinyama wanaondoka navyoo, Daaaah!!! Bora tu niliwatoloka!!""
"" Polee bhana!!; Kwani Wewe Ni mtoto wa ngapi kuzaliwa!!?? ""
"" Mie wa pili na ndio wa mwisho kwa babangu sijajuwa lakini kwa mama huko aliko Kama ashatuongezea kenginee!! ""
"" Huyo wa Kwanza Ni wakike au kiume?? Kwanini unasema Ni wakwanza na wa mwisho!!?? ""
"" Mie nae nitakuwa naongea Sana Lakini wa Kwanza Ni wakike, sijui hata kwa Sasa atakuwa wapi make muda ule Alikuwa chuo natekwa, ila nitaenda kumtafuta, nahisi atakuwa bado hajamaliza!! ""
"" Baba , mama!!!' wao wako wapi??""
"" Ibrahimu maswali mengi tuondoke bhana!! Nisije chukuliwa na wale Vijana wenye miraba minne naona watakuwa wananitafuta!! ""
Ibrahimu hakupata majibu, Kuna kitu Alikuwa akidadisi ajue, make taswira ya Joanyther Muda wote Alikuwa akiiona kwa Movick. Aliamua atalifanyia Utafiti.
¶¶¶¶¶¶
Leo Chuoni Tena kulikuwa na wageni wametembelea chuo Cha Nursing, walikuwa Ni watu wa Damu salama. Siku hiyo walifika na kutoa semina Kwanza Kisha watu walijitolea kutoa damu zao ili zikawe msaada kwa watu wasiojiweza.
Lakini katika ugeni huo, kulikuwa na msimamizi wa kitengo hicho Alikuwa ameshikilia picha ya Joanyther, akijaribu kuulizia kwa baadhi ya wanachuo alitoa Oder! Joanyther aletwe.
Upande wa Joanyther siku hiyo Alikuwa Hana hili Wala Lile, siku hiyo Alikuwa ametoka na Alvin, Collin na Razack' pamoja na Three princess wa shule walienda kufanya manunuzi ya mahitaji yao ya shule.
Taarifa za kutafutwa kwa Joanyther zilimfikisha Jolvin, Jolvin alipozipokea taarifa hizo aliamua kupiga simu kwa Alvin na kumuuliza Kama watawahi kurudi, kwa majibu aliyoyapata yalimpa furaha Sana moyoni mwake, yalikuwa Ni majibu watakawia kurudi mpka jioni.
Jolvin aliamua kufanya upelelezi Kwanza, kwanini Joanyther anatafutwa na Hawa Watu wa Damu salama, Mbona nilijua Ni Mkurugenzi wetu was chuo ndio anashilikiana na kitengo Cha Utafiti iweje tena na Hawa wanamtafuta wakati hata hawana uhusiano na Watu wa Utafiti.
Jioni, majira Kama ya saa moja, kina Joanyther ndio walikuwa wakiingia Chuoni wakiwa wamehemea vitu kadhaa.
Jolvin alipigiwa Simu na Razack' kuja kuwasaidia kushusha mzigo, Jolvin akawa amefika pale, Ile wanashuka tu Ancillah alikimbia na kumkumbatia Jolvin huku akimpolomoshea mabusu kadhaa.
"" Jolvin kwanini lakini hukuambatana na sisi tukaenda wote!! Hivi unajua Ni zawadi gani nimekuletea.
Ancillah alitoa Chocolate na kumpatia Jolvin,
"' Najua hiki ndio wapenda, Japo sikuwa karibu na Wewe lakini ukila hii Chocolate itauvuta ukaribu wako kwangu!!""
Joanyther aliwatizama huku akiangalia vituko vya Ancillah, alibaki kuwaangalia tu Kisha alichukua vitu vyake na kuondoka.
Alvin ilibidi amuwahi ili amsaidie mzigo, make aliona Kama vile kaboeka.
"" Mbona umebadilika ghafura!! Hujafurahia kitendo Cha Ancillah kwa Jolvin, wale waache wawili wapendanao wasikuumize kichwa!! "
"" Walaa!! Mimi wivu kwa Jolvin utoke wapi!!? , mie Ancillah huwa ananiboa mashauzi yake tu!!! ""
"" Ohoo!!! Muache huyo!! Sie twamjua vizuri Sanaa!! ""
Jolvin hakufurahishwa na kitendo Cha Ancillah kujigonga Sana kwake, Aliamua kumvumilia tu asimuoneshee kwa wenzake. Siku hiyo aliamua kumuita Ancillah faragha wazungumze;;
"" Ancillah Mimi kukuita hapa Kuna kitu kinanisibu moyoni mwangu itabidi tu nikwambie!!""
"" Kitu gani tenaa hicho huenda leo umeutambua Upendo wangu kwako!! Ayaaa niskie kitu hichoo!!!! ""
"" Kupenda na kupenda!! Tatizo Wewe upendo nilionao Mimi kwako!!! sio upendo ulionao Wewe kwangu, kwa kifupi Mimi nakupenda Kama dadangu, pia familia zetu Zina umoja na zinashare katika makampuni, Mimi swala la kukupenda wewe Badoo moyo haujawa na chuguo kwa Sasa, Naomba uniwie kwa radhi kwa maneno yangu huenda mbeleni tenaa Kama Ni mipango ya Mungu tukawa wote.
"" Kwanini lakini Jolvin!! Hunipendi Mimi au Mimi Nina kasoro gani?? Kama Ni familia zetu zinaheshimiana kwanini!; Tusiwe wote I'll tudumishe heshima hiyo!! Nipende basi Jolvin!! Mimi nipo tayali kuolewa na Wewe. Ancillah Alikuwa akilia Sana kutetea upendo wake kwa Jolvin!!
"" Nimekuambia kuwa na subira!!, Wewe ukinifos Mimi nikupende, nitakuumiza, Muda wote nitaishi na Wewe pasipo na Feeling zozote huoni Kama nitakuwa naukatili moyo wako???""
"" Sawa nimekubaliana Jolvin, kumbe hujawahi hata kunipenda Mimi hata kidogo Muda wote najipendekeza kwako kumbe Wewe hata huniwazii sawa si unampenda Joanyther!! Kwa Sasa umeleta ugomvi na Mimi hata huo muungano wa familia zetu nitauvunja!!!
Kisha Ancillah Alisimama na kuondoka kwa hasira huku amefura kifua chake, Aliondoka moja kwa moja Hadi kwa Joanyther.
Joanyther Alikuwa amekaa zake darasani akipitia vitabu vyake, Alikuja kusitushwa kwenye kitabu chake akiona mabaki ya dagaa na ukoo, ile anainua uso wake alikutana uso kwa uso na Ancillah, akiwa anataka kumkaba shingoni.
Joanyther alizidi kuumia baada ya kuona kitabu chake kikizidi kulowana alikisogeza pembeni Kisha alimnyanyua Ancillah na kumtupa kwenye meza na kujigongeza kwenye paji la uso huku damu zikimchulizika, Alimsogelea Tena na kuchukua kiti na kumbondea mgongoni huku akiwa amechafukwa na hasira.
"" Nishajua Wewe Ni adui yangu tangu nimekanyanga hapa Chuoni umekuwa ukinikandamiza!! leo nitakuua kwa mikono yangu mwenyewe, Hapa Sina baba, mama, Wala kakaa!! Kwa Sasa najisimamia mwenyewe!! ""
Alvin alifika pale na kumvuta Joanyther na kumsukuma kule, Kisha Alimchukua Ancillah na kumbeba begani na kuondoka nae, pasipo kuangalia Joanyther atakuwa kwenye usalama ganii!!, Lakini kwa bahati Mbaya alienda kujigongeza kisogoni na kumpeleka damu zianze kumvuja puani.
Muda huo huo Joanyther anaugulia maumivu Kuna kipande Cha ubao kililushwa kutoka sehemu, Joanyther alikiona kwa Muda huo Alikuwa Hana hata nguvu ya kutoka pale alifumba macho kusubili kimgonge.
Jolvin alikuwa tayali kafika pale akija kwa mbio kutoa msaada!! Aliona ule ubao unakuja kwa kasi, alikimbia kwenda kunusuru maisha ya Joanyther, Alifika pale na kumkumbatia Joanyther, ule ubao ukawa umemfika yeye, moja kwa moja kwenye uti wa mgongo na kuanza kutapataba kwa maumivu huku akilia na Nguvu zilianza kumuisha.
Joanyther ile anakuja kufungua macho yake, Mara baada ya kusubili kwa Muda mrefu ubao umpate umechelewa kumfikia, ile anatizama hakuamini kumuona Jolvin mbele yake akiwa amemkumbatia na ubao ukiwa umemchoma mgongoni. Jolvin alimwangalia Joanyther kwa Mara ya mwisho nakusema.
"" Nisamehe Mimi Joanyther!! Muda wote nakuwa mkosaji kwa Mara nyingine Tena, nikuombe kuwa karibu yangu ili niweze kukusaidia!!! "" Kisha alianguka na kuzimia papo.
,,,,, Itaendelea,,,,,,,
Usikose sehemu ya kumi na sita.
Je, Nini hatima ya misukosuko ya Joanyther???
Like, comments, share. Nilete Mwendelezo.
MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: 16 "0746638941"what'sup"
SONGA NAYO.
" Nisamehe Mimi Joanyther!! Muda wote nakuwa mkosaji kwa Mara nyingine Tena, nikuombe kuwa karibu yangu ili niweze kukusaidia!!! "" Kisha alianguka na kuzimia hapo. ENDELEA...
""" Hapana Jolvin usifanye hivyo!! Mbonaa Sasa!! Umekuja kunisaidia Lakini, ungeacha tu nife nisahau haya maisha!!"
Lillian Alikuja huku akiwa analia, Alifika pale na kumsukuma Joanyther akaanguka pembeni.
"" Jolvin nisamehe!! Sikukusudia kufanya hivyoo!! Mimi Nilitaka kumuazibu Joanyther kwa kitendo alichokuwa kamfanyia Ancillah, amka basi nikwambie!! Sio Mimi lakinii!!!
Muzdalpher na yeye alifika hapo akiwa ameambatana na Razack' na Collin, walifika pale na kumchukua Jolvin na Joanyther Muda huo walikuwa bado hawajitambui, Muzdalpher alimgeukia Lillian,
"" Sasa!!! Unalia Nini kabla tusaidiane kuwabeba wakapate huduma ya kwanza, unaishia kulia, hayo machozi yako umeona Ni ponyo!!?? ""
Harakati zilizidi kuendelea kwa Madaktari bigwa!! Ili kunusuru uhai wa wagonjwa, huku dawa mbalimbali zilizidi kuongezeka na drip kadhaa zikiongezwa kwa wagonjwa!!
Muda kidogo alionekana Daftari wa kike aliingia kwenye chumba Cha Joanyther akiwa na Syringe kaandaa, Alifika akamdunga sindano Joanyther kwenye paja na kusukumia dawa Kisha aliondoka kwa Siri Sana!!
Daktari wa zamu Alikuwa ametoka kidogo, Ile anarudi alikuta khari ipo tofauti vitu vilikuwa vimevurugika aliamua kuviludisha sehemu yake na kuanza kumkagua mgonjwa wake.
Lakini alishangaa baada ya kumuona Joanyther damu inazidi kumvunja masikioni na mdomoni.
"" Mbona khari imebadilika ghafura Kuna mtu nahisi aliingia humu. ""
Alichukua Simu na kupiga kwa Daftari mkuu na kumtaka aje kumuona mgonjwa wake.
Daktari alifika pale na kuchukua vipimo Kisha, alipima mapigo ya moyo na kuona yapo chini, ilibidi atafute hewa mbadala ya kumsaidia kupumua '0²'.
Upande was Ancillah khari yake Ilikuwa Mbaya, fahamu zilianza kumrudi!! ndipo anakuja kuzinduka aliutizama mwili wake, na kuona bandage karibia mwili mzima zimenzunguka, Hapo hapo alizidi kulia akitaka msaada..
Wazazi wake walikuwa wamezunguka, kitandani wakimwangalia, mamake Alikuwa akimwonea huruma Sana, alimsogelea pale kindani na kumshika shavu kumtoa wasiwasi.
"" Mwanangu!! Usilie kiasi hicho!!, Mimi mamako na babako tuko hai, lazima utapona na tutahakikisha unakuwa salama!! ""
"" Mamaaaaaa!!! Kwani Jolvin yeye anaendeleaje?? ""
"" Anaendelea vizuri!! Lakini itamchukua Muda mrefu kuponaa!!
"" Kwanini iwe Muda mrefu!!! Ina maana hataponaa kabisa!!!? Na vipi kuhusu Joanyther??""
"" Jolvin atapona!! Shida Ni ule mti ulienda kumchoma kwenye uti wa mgongo, imempelekea kuwa na shida ya ukaukaji wa maji katika uti was mgongo na tatizo hili litapelekea kila mwezi kuchomwa sindano kwenye Uti wa mgongo ili aweze kutembea, but kwa sasa atakuwa Ni wa kitandani, kuhusu Joanyther khari yake Ni Mbaya na yeye anapumulia mashinee!! ""
'"" Mungu wangu nilikosea Mimi kuleta vulugu kwa Joanyther!! Lakini kwanini anikatae Mimi Jolvin!!, Halafu chanzo Ni Joanyther kasababisha haya yotee lazimaa nitamuua kwa mikono yangu miwili, tenaa!! Atafia humuhumu wodini. Ancillah aliongea kwa hasira huku akiwa ameng'ata meno yakee!!
Baba'ke na Ancillah, alisogea kumbembeleza mwanae.
"" Mwanangu kuwa na huruma hafu usilipe kisasi kiasi hicho, Jolvin Kama hakupendi achana nae mbona Alvin anakupenda Muda wote yupo karibu nawewe, halafu yule Binti Usimguse tazama Hana Wazazi, Wala familia Ni yatima!! naomba umuache aishi tu.""
"" Baba!!, Mamaaaa!!! Hayo yote niachieni Mimi nitafanya kitu kile Moto unapenda'' Naomba mniachie Mimi, Joanyther kuwa mzima labda Jolvin apone na Mimi niponee!!! ""
πππππ.
Yapata siku tatu kupita leo Joanyther ndio alipata fahamu baada ya siku tatu mfululizo akitumia mashinee ya hewa kupumulia. Leo alitolewa ile mashinee na kuanza kupumua vizuri, aliangalia sehemu ile Kama kutakuwa na mtu, alisogea karibu huku akivuta meza iliyokuwa na glass ya maji ya kunywa anywe. Lakini kwa bahati Mbaya ile anavuta meza glass ilianguka na kupasuka,
Kelele ya mpasuko wa glass ilipenya mbali ilimfanya mhudumu afike pale kutoa msaada.
"" Mungu mkubwa!! Joanyther umeamka!!?? ""
"" Maji ya kunywa!!" Ndio jibu lililosikika kinywani kwa Joanyther.
Muda huo Razack' na Collin walifika pale, baada ya kupata taarifa maendeleo ya Joanyther.
"" Joanyther unaendeleaje!!! Umepona ee, Alikuwa Ni Razack'na Collin waliongea kwa furaha.
"" Naendelea vizuri!! Vipi kuhusu Jolvin na Ancillah, waoo wanaendeleaje, nataka nikawaonee Kwanza!!! '"
Muda huo huo Nurse!! Aliingia mule wodini, hakuwa Ni mwingine Bali Alikuwa Ni yule yule aliyemdunga sindano Joanyther kwenye paja.
Kitendo Cha kumkuta Joanyther kakaa, anaongea kilimsitusha sana!! Ilibidi atoke kwa kubabaika Sana.
"" Ooh!!! Endeleeni kumuona mgonjwa nitakuja kumuona baadae.
Razack' ilibidi amufatilie yule Nurse baada ya kumuona Ana wasiwasi Sana, alijua moja kwa moja itakuwa katumwa. Kadili alivyozidi kumfatilia Nurse yule alizidi kupita chocho baadae alifika Sehemu nakutoa simu yake kupiga Upande wa pili.
"" Ile mishe yetu naona inaenda kufeli, nimemkuta mgonjwa kachangamka, wakati na ile sindano Mimi nilimdunga!! Sasa itakuwaje tenaa!!!
Razack' Alikuwa akisikiliza maongezi Yao, Japo hakusikia Upande wa pili kipi alijibiwa, aliamua aanze kumfatilia Nurse yule ajue hiyo kazi kaagizwa na Nani!!""
Nurse yule alifika sehemu akavua gwanda lile na kubakiwa na nguo ndani Kisha alichukua tax na kuelekea kwenye jumba kubwa, Mbaya Zaidi alipofika pale aliona kapokelewa na Mlinzi wa pale getini Chuoni kwao na kubaki akishangaa.
"" Siamini macho yangu Mlinzi yule hohe hahe ndio anahusika kwa hili, nahisi na yeye atakuwa nyuma ya mtu itabidi nianze kumfatilia boss wake nimjue hapa itakuwa Ni watu wawili wanatumikishwa!! ""
Razack' aliamua kurudi baada ya kuona Utafiti wake umezaa matunda, Muda huo Upande wa Collin walikuwa bado wakimsubili Razack' aludi.
""" Vipi mlinisubili Sanaa!!! Nilitoka Muda ule kuongea na Nurse lakini kwa bahati Mbaya nimekutana na principal akanipatia kazii!!! """
""" Ooh!! Pole Sana!! Joanyther alinisumbua umekawia Sana kurudi, Muda wote anataka akamuone Jolvin na Ancillah.""
"" Sijachelewa Sanaa!! Naona pia huu Ni muda wa kwenda kuwaona wagonjwa, Basi tuongozanee!! ""
Waliongozana Hadi wodini kwa Jolvin.
Jolvin muda huo Alikuwa anaendelea vizuri Japo hakuwa na uwezo wa kuinuka.
Joanyther Alifika pale alishangaa Sana kumkuta Jolvin yupo katika khari ile,
"" Jolvin huwezi kutembea Kweli!!! "
"" Daaaah!!! Usiwaze bhana!! Nitatembea tu!! Sema itachukua Muda but nitakuwa Sawaa!! Vipi Wewe waendeleaje Lakini?? Sogea Basi nikuone karibu.
"" Wewe naee!! Kama hunioni!! Ila utapitia wakati mgumu kwa Sasa!! Pole Sana. ""
Jolvin alimsogelea, karibu Joanyther.
"" Kumbe!! Uliumia Sana kichwani??' "Nasikia wamekushona Nyuzi Saba!!""
Muda huo huo Jolvin alikuwa akimkagua Joanyther kidonda chake, Ancillah Alikuwa akiingia Wodini kumuona Jolvin, Aliwakuta katika khari ile wakiwa wametizamana.
Ancillah alifurahia Tena kwa hasira huku akipolomosha maneno machafu.
"" Wewe mwamke muuaji umekuja Tena hapa!! Wataka umumalize kabisa Jolvin, kwa Sasa umempa ukilema umeona hautoshi wataka kumuua tenaa!!!!""
"" Ancillah una uhakika kuwa Mimi Ni muuaji hapa aliyetaka kuua Ni Nani, yaani Ni kijimtu unatoka huko na hasira zako kuja kuleta ugomvi na haya yote umesababisha Wewe!!! "" Joanyther nayeye hakuwa dhaifu kivile.
"" Wewe lazima nitakuua tu lazima nitakufutilia mbali, siku za usoni!!
Jolvin hakutaka makelele aliwaamuru rafiki zake wamludisha wodini asilete ugomvi wodini,
"" Ancillah naomba ukapumnzike naona kichaa Cha ugonjwa bado kipo kichwani, halafu muda wote ukitaka kuja kuniona njoo kwa heshima siaki makelele, kwa Sasa kitu ninachokitaka Ni utulivu tu. ""
Ancillah ilibidi arudishwe wodini kwake akapumnzike Baada ya kuleta fujo pale, Daktari aliwaomba Wazazi wa Ancillah wasimruhusu Kwanza kutoka mpaka atakapokuwa anaendelea vizuri.
Upande wa Joanyther Alimchukua Jolvin kwenye wheelchear na kutoka nae nje huku Razack' akiwa anamsukuma, mpaka Muda wa kusalimia wagonjwa ulipoisha.
Razack' ilibidi abaki akiongee na Jolvin kwanza kuhusu tukio la Yule Nurse, Jolvin aliamulu Joanyther apatiwe ulinzi pia afatilie swala Hilo I'll waweze kutambua Nani anayehusika, na yeye anataka Nini kwa Joanyther.
,,,, Itaendelea,,,,
Usikose sehemu ya Kumi na Saba.
Like, comments, share.
MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: 17 "0746638941"what'sup"
SONGA NAYO.
Siku zilizidi kusonga mbele Afya ya Joanyther na Ancillah zilikaa vizuri wakaendelea na masomo lakini kwa Jolvin Alikuwa akitembelea wheelchear.
Joanyther alijitahidi Sana kuwa upande wa Jolvin lakini Ancillah Alikuwa Ni kikwazo kikubwa kwake, Siku hiyo aliamua kumfuata Jolvin aongee nae. Alimchukua Jolvin huku akimkokota kwenye Wheelchear ake nakutoka nje kidogo ya shule, huku wakiongea stori za hapa na pale.
Jolvin aliamua kumuuliza Joanyther swali baada ya kumuona anamuepuka Sana.
"" Hivi Joanyther waweza kunambia Kuna sababu gani inakufanya uniepuke, hutaki mazoea na Mimi! Shida hasa Ni Nini?? ""
"" Bora hata umeniuliza!! Make kukuleta kwangu huku ndio kitu Nilitaka kukwambia, "" Kweli Jolvin hapa natafuta njia ili niweze kukuepuka kwa Sasa nataka uwe mbali na Mimi, mazoea ya urafiki wangu na Wewe yaishee!! "
"" Utakavyofanya hivyoo!! Wewe utafaidika na Nini?? Hivi umefikilia swala hilo kabla hujasemaa!!? ""
"" Ndio!! Mpaka kukuita hapa ujue nimeamua'' Kwasasa sitaki kufa naona Ancillah ataniua Mimi, na akishidwa!! Bado Kuna Muzdalpher na Lillian, wote wanna hasira na Mimi kisa kukufanya uwe hivi!!! ""
Jolvin alimwangalia Joanyther na kubaki kucheka Kwanza.
"" Kweli jogoo wa shamba hakosi kamba mguuni, bado unawaza kulogwa Wewe!!" Hebu zinduka ulipo hakuna mtu anayekuchukia hivyo Hadi awaze kukuua!! ""
"" Naona hatuelewani ila ndio hivyo Mimi nishamaliza kukwambia, Naomba nikurudishe Kwanza hostel.""
Joanyther Alimfikisha Hadi hostel, nakumsindikiza Hadi chumbani kwake huku akimsaidia kumlaza kitandani, Kisha alimfunika blanket na kuondoka.
Jolvin alimtizama Joanyther Kisha alimshika mkono na kumvutia usoni kwake.
"" Wewe tu ndio utakaebakia upande wangu lakini kwa hao wengine usiwaamini, But!!! ''ulivyoniambia kipindi tupo kule!! naomba usichukue maamuzi hayo!! Muda wote njoo unione, pale ninapokuhitaji usisite kuitikia wito wangu!!! "" Kisha alimwachia mkono.
Joanyther alibaki akitoa macho asiamini ule ukaribu uliotokea na Jolvin.
Jolvin alimwona bado anaduwaa aliamua kumuuliza.
"" Vipi wataka uje ulale??? "
Joanyther hakumjibu!! zadi ya kuikusanya mikono yake na kuiweka kifuani na kutoka, Alifunga mlango na kutoka lakini wakati huo huo anatoka alikutana na Ancillah akiwa na Lillian wakiwa wanakuja kumwangalia mgonjwa. Muda huo Ancillah hakuongea kitu, ila Lillian alimpiga kikumbo na kumkwalua na pen aliyokuwa nayo mkononi.
"" Wewe Villa girl!!! Ni lini utaacha kujipendekeza kwa wanaume Muda wote!! Ushaambiwa hakupendi lakini hutaki!!""
Joanyther Aliamua kukaa kimya huku akiwaza mambo mengi kichwani.
"" Jolvin hikihiki ndio kinachonifanya nizidi kukuepuka!! Laah!! Hivyo nitauwawa huku nipo naona.""
Lakini Maneno ya Lillian yalipenya Hadi masikioni kwa Jolvin na kubaki akimhurumia Sana Joanyther.
"" Kumbe!! Ndio maana waniepuka kisa hiki, leo ndio nimejua ila nitahakikisha hawakuzuru!!""
Ancillah na Lillian Muda huo walifika huku wakiwa wamebebelea mazaga ya mgonjwa.
Walifika na kumpa Jolvin, Japo alionekana Ni mnyonge Sana siku hiyo. Ancillah aliamua kumuuliza.
"" Vipi mbona mnyonge hivyo!! Leo au Joanyther kakuuzi!!??""
"" Bora hata Joanyther alikuwemo humu ndani nilikuwa na furaha!! Lakinii,,,," Kisha alichukua Maji na kuanza kunywa!!""
"" Polee!! At, Japo hujakamilisha sentensi yako!! Huenda alikuuzi Sana ila Muda Mwingine nitahakikisha haukwaziki na vikwazo vya Joanyther, Halafu vipi mwezi kesho likizo Wewe unaitumia likizo ukiwa wapi?? Ancillah aliuliza.
"" Kwani Wewe na Lillian mtakuwa wapi?? ""
"" Sisi likizo yetu tumepanga tutakuwa Ulaya Kwanza Kuna vitu tutaenda kufanya manunuzi na vitu vya shule!!''
"" Ani Jolvin Wewe husemi utakuwa wapi hafu sie tu ndo watuuliza!!" Lillian aliuliza.
"" Oohooo!!! Mimi bila Shaka khari yangu mnaiona jinsi nilivyo hapa nitakuwa Indian kwa matibabu zaidi siku nikiwa sawa narudi, Japo itanichukua mwezi kurudi, lakini khari ikiwa nzuri kwa huduma Kama itamalizika wiki moja, mbili nitawawahi!! ""
"" Daaaah!!! Mwenyezi Mungu akupiganie uwahi kurudi, Daaaah!! Masikini Joanyther sijui likizo yake ataenda wapi, Bora hata angekuwa hajakuumiza Hivi tungemuangalia na yeye angalau hata akaone Ulaya ilivyo!! ""
Lillian aliangusha kicheko Cha kumsapot Ancillah, Huku Jolvin akiwa anawatazama tu.
"" Hahahaahaaa!! Yaaani tena hata kule kijijini Hana ndugu, Tena atushukuru sisi kumjengea hata hiyo nyumba itamsaidia kujihifadhi, au ataenda kuwinda sungura kijijini kwao!!""
"" Bora hata sungura, Tena ataenda kuvua wale samaki wa mto wapo Kama sori ya kiatu Cha bi Emma, si ulikiona siku ilee!!!!?? ""
"" Na kilivyokuwa kinaachama duuuh!!! Ndo maana Alvin alikiogopa Hadi akaenda gongwa na Nyoka!! Wewe kiatu kimekaa kama jamiii ya Nyoka wa mwituni.""
"" Nyie Wanawake hamumalizi kuongea!! Bora hata mwenzenu anayeishi kijijini muda wote anafuraha na maisha, hawazi kula, na bata Kama zenu zinazowahangaisha akili Muda wote kutafuta matoleo mapya!! Okay, Naomba mniache Kwanza nipumnzike. Kisha alivuta shuka na kujifunika!! "
Ancillah na Lillian waliondoka kwa aibu huku wakijikanyaga kanyaga.
"" Wewe unaongea sanaa!! Hadi Jolvin kachukia"""
"" Atajua bhana!! Yeye huwaga Ni mtu mwenye hasira Sana!! Atabadilika tu siku moja, Ani mtu mkimya sijui ndio kaanza mapenzi na Joanyther!! "" Alikuwa Ni Lillian.
¶¶¶¶¶
Ilikuwa Ni siku nyingine tena, leo wanachuo walikuwa wakijiandaa kurudi makwao kupumzika baada ya kupata likizo.
Upande wa Joanyther Leo alikuwa na furaha Sana, baada ya kupata likizo ya kwenda kwao, muda wote alikuwa anaona masaa Kama yamechelewa, alifungasha vitu vyake na kutoka nje aangalie wenzake waliokuwa tayali wameanza kuondoka na kubaki akijisemea moyoni.
"" Bora hata kesho ingekuwa leo namimi ningeondoka siku ya leo but nitakuwa mvumilivu tu kesho itafika mapema tu naondoka!! ""
Muda kidogo aliona gari la kifahari linaingia getini walionekana Ni Wazazi wa Ancillah walishuka huku Ancillah alikimbia moja kwa moja kuwapokea. Kisha alianza kupaki mizigo yake kwenye gari.
Upande wa Jolvin na wenzake walikuwa tayali wakijiandaa kuondoka lakini kabla hawajaondoka Alvin aliamua aonane na Joanyther Kwanza.
Walitafuta Sehemu wakakaa huku sitori zinaendelea. Alvin alimuuliza Joanyther.
"" Vipi Kama Joanyther likizo yako tukaitumia wote, naomba ubaki na Mimi Kuna sehemu nataka nikupeleke.""
"" Hapana!! Bhana!! Mimi nimekumbuka nyumbani kwetu nataka nikasalimie ndugu zangu waliipo huko, usijali lakini na siku nyingine, si likizo bado ipo!!"
"" Aaaah!!! Siku nyingine Tena!!! Wazani tutakuwa bado tupo pamoja, Anyway nisikufos Sana, Kuna kitu nimeandaa kwaajili yako.
Alvin alitoa saa na kumvisha Joanyther mkononi, ilionekana Ni saa yenye thamani Sana.
'' zawadi yenyewe ndio hi!! Naomba uitunze pia zingatia muda, pia usisahau kufanya kitu kwa muda, Kumbuka siku hazigandi naomba pangilia mambo yako mapema, muda wote uwe tayali.""
"" Wewe!! Nae maneno mengi hivyoo, Nitazingatia lakini umeongea maneno mengi nahisi muda mwingine yatakuwa na maana, lakini nitayatafakalii!! ""
"" Sawaa!! Pia yafanyie kazi, ngoja Mimi nikuache Leo nitaondoka Mimi na Razack 'na Collin, Jolvin yeye Kuna form bado hajamaliza kuzisaini kutokana na khari ya afya aliyokuwa nayo.""
Siku ya pili iliwadia huku Joanyther alikuwa akimalizia kuweka vitu vyake sawa aondoke.
Alichukua begi lake huku akilibuluza chini taratibu, huku akikiangalia chumba chake Mara mbili mbili.
"" Daaaah!!! Chumba hiki kimekuwa mkosi kwangu, Japo naondoka lakini Haijalishi kilikuwa na mkosi kiasi gani lakini muda mwingine kimenipa furaha, huko ninakoenda Sina Wazazi Wala mdogo wangu, huzuni ikinijaa nitakumbuka hata uwepo was hapa!! Au niende kijijini kwao Ibrahimu nikawasalimie Bora hata huko Kuna furaha."""
Baadae alitoa begi lake huku akielekea mlangoni, alipiga jicho Hadi mlangoni lakini alishangaa baada ya kumuona Jolvin akiwa kwenye Wheelchair akimgonja mlangoni.
"" Jolvin Ni wewe tenaa!!!!?" Hivi bado hujaondoka hata wewe!??"
"" Ningeondoka usingeniona, ila kwa kuwa bado nipo ndio maana nipo hapa karibu yako!!!
Joanyther Aliamua aweke begi lake Kwanza pembeni Kisha alimsogelea Jolvin karibu huku akimkokota kumuelekeza kitandani Kisha alikaa huku wakiwa wametizamana huku Jolvin akiwa kwenye Wheelchair.
"" Ila Jolvin una machale kweli unajua ndio nlikuwa naondoka hivyo, na hapa nikienda nataka niende Hadi kule kijijini kwao Ibrahimu.""
"" Hivi Joanyther unampenda Ibrahimu??
"" Wewe nae nampenda ndio so Ni rafiki yangu, wewe wazani likizo nitaenda wapi Sasa!!"
"" Sawaa!!! Hivi Ni kweli hujawahi tambua mi nakupenda, au nifanye Nini ujue nakupenda ok nikutakie Safari njema ila kumbuka Mimi pia na moyo wa kukupenda. Kisha Aligeuza Wheelchear na kuondoka.
Joanyther alimfata huku akijalibu kumsimamisha tenaa!!
"" Sasa ndo wachukia hivyo!! Ibrahimu Ni rafiki yangu Kama wewe tu, ndo upaniki kiasi hicho lakini!!! ""
"" Siku ukijua kutofautisha kati ya rafiki na mpenzi ndio utanielewa huwa namaanisha Nini nikisema nakupenda!!""
"" Ayaaa!! Nimekuelewa!! Nishajua una wivu na Ibrahimu hutaki nimtaje!! Sawaa simtaji Tena make hapa nikiongea tu Ibrahim na sura unakunja!! ""
"" Kama ushaanza kutambua hayo yote kuwa nachukia kuhusu Ibrahimu vizuri!! Itafikia hatua utanielewa tu. Halafu naona mkononi unasaa!!!!
"" Hii kanipatia Alvin janaa!! Pindi anaondoka, vipi Ni nzuri kwanii?? ""
"" Mhuuu At umepewa na Alvin tenaa!!!!?? ""
"" Naweee umezidi!! Hukutaka nipewe na Alvin tenaa!! Au nachukiza kuivaa??? Hafu naona nawewe mbona unasaa Kama ya Alvin tena Ni mpyaa!! Kumbe wote mnapenda saa Kama hii hafu wachukia hivyo!! ""
Jolvin alibaki alimtizama Joanyther pasipo majibu yoyote lakini alianza kumfikilia Alvin.
"" Lakini Alvin ananitaka Nini Mimi!! Kumbe ile siku nimemtuma saa akaninunulie Kumbe alienda kununua saa mbili hafu kaniwahi akampatia Joanyther Daah!! Kweli "Love is circle"
Joanyther alimwangalia Jolvin akajua amemkwaza kwa majibu yake ndipo na yeye alianza kuwaza.
" Kumbe Jolvin!! Hutaki kuniona nakuwa na Alvin karibu, hupendi kuniona nakuwa na Ibrahimu karibu!! Sijui umekuwaje tu Mpaka nashidwa kukuelewa!! ""
"" Joanyther naomba nikuache!! Pia nikutakie Safai njema tu, lakini ukimaliza likizo yako sijui Kama utanikuta nimerudi nahisi nitachelewa ila nahitaji likizo yako ikawe ya furaha, naomba kwenye kuomba kwako usinisahau na Mimi nahitaji kupona ili Kuna vitu vingine nataka kufanya nikiwa natumia mwili wangu!! Lakini nashidwa!! Okay niliandaa saa Kama zawadi yako kwa kuwa Alvin kukupatia na Mimi nitakupatia na hii swezi Rudi nayo tenaa!! "
" Nashukuru Sana!! Hafu zote nimezipenda, Inaonekana wewe na Alvin mna moyo mmoja hii itakuwa Ni Double love!! "
,,,,,,,,,Itaendelea,,,,,,,,,,
Usikose Sehemu ya Kumi na nane.
Mambo Ni kuchuana!! Sijui kwa ndugu msomaji utapenda Couple gani kwa upande wa Joanynther awe na Nani??"
Like, Comments, Share.
MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: 18 "0746638941"what'sup"
ANZA NAYO.
Leo Joanyther alikuwa tayari kafika kwao, alipokelewa na wajukuu wa Bi Emma kwa furaha Sana, hata ilipofika siku ya kesho yake walikuwa wamemwandalia tafrija ndogo ya kumkaribisha, Ndugu wa karibu pamoja na majirani siku hiyo walijumuika kwa pamoja wakisherekea ujio wa Joanyther.
^^^^^^^
Turudi kidogo leo Kijijini kwao Ibrahimu, Alionekana Ibrahimu na Movick walikuwa wamekaa wakipiga stori za hapa na pale walionekana kuzoeana Sana.
Siku hiyo Movick alimwomba Ibrahimu akamuombee ruhusa kwa Cheaf wa Kijiji siku ya kesho alitegemea arudi kijijini kwao Baada ya kuona Wale Vijana hawakurudi Tena kumtafta, aliona usalama utakuwepo.
Ibrahimu Baada ya kupokea ombi la Movick alisononeka sana, alifikilia jinsi alivyomzoea na kubaki akijiuliza mambo mengi Sana.
"" Kwanini inakuwa hivi kila mtu ninae mzoea leo ananikimbia, Nilimzoea Joanyther nayeye akanikimbia, leo hii tena Movick na wewe Unataka kunikimbia. ""
Movick alitambua Hilo kuwa Ibrahimu hakulipokea ombi lake kwa furaha, alimsogelea karibu na kukaa pembeni yake.
"" Ibrahimu naomba usinikunjie moyo ukasababisha nisiondoke!! Niruhusu kwa moyo wako mmoja niende nikatafute ndugu zangu!! Tizama kwa Sasa Ni likizo nataka niende kijijini huenda dadangu atakuwa kaja Nyumbani!!! Nikimkuta kaja!!' ndio nitajua kuwa Ni mzimaa.""
"" Walaa!! Usiwaze Mimi pia napenda upate familia yako!! Kinachoniuma leo, ngoja nikwambie muda wote nakumbuka uliwahi kuniuliza Kama nishawahi kuwa na mwanamke, leo!! Nitakwambia Kuna kitu nataka nijue kutoka kwako.""
"" Kitu gani tenaa!!! Ka Ibrahimu, wataka ujue kutoka kwangu!!?""
"" Okay!!! Miaka ya nyuma Kuna Binti alikuja hapa kijijini alikuwa kaambatana na Bi mmoja hivi walitokea Kijiji Cha kusini! Walikuja hapa wakiwa wanamtafuta mdogo wao kwa majina walisema anaitwa Movick!! Muda wote nimekuwa nikikutizama Sana tangu siku ile nimekuona, Hadi siku ile tumeenda mtoni kuogelea niliamini huenda akawa ndugu yako, yaani jinsi ulivyokuwa waogelea na yeye alifanya vivyohivyo,,""
'" Huyo mwanamke alifananaje Kwanza!! Ana nywele ndefu?? Hafu mweupe?? Na huyo Bibi Ni mnene hivi au?? Kwani hawakujitambulisha majina au yule Binti anaitwa Nani??""
"" Walijitambulisha Lakini kwa upande wangu nlikuwa Kama gerezani sikuweza kumuona huyo Bibi ila Binti nimekaa nae Kama nusu mwaka, ila kwa yule Bibi aliuwawa!! ""
"" Aliuwawa tenaa!!! Na hao waliomuuwa Ni kina Nani?? Kwani na huyo Binti anaishi?? Na anaitwa Nani??"
"" Binti yule atakuwa anaishi lakini niliona Ana maadui wengi Sana wamezunguka, hata siku anatoka hapa Kuna watu waliingia kwa Siri katika himaya yetu wakawa wamemchukua kwa kumtorosha Lakini Mimi nilifanikiwa kujua kilichokuwa kinaendelea, nikawa nimemruhusu kwa moyo mmoja akawa ameondoka!! ""
"" Lakini Ibrahimu!! Inaonekana hata jina lake humkumbuki kwelii?? Na unaaminije Kama atakuwa anaishi!! Kama watu walikuja kumchukua kwa siri, inamaana hawakumzuru Kweli!!!??? ""
""" Naamini atakuwa anaishi!! Muda wote huwa nafanya Dua kwaajili yake ili aishii tu, Kisha Ibrahimu alitoa picha na kumupatia Movick !! Vipi unamjuaa ??? ""
Movick alibaki kaduwaa.
"" Mbona Ni Da Joany!!!""
"" Unamfahamu ???""
"" Maskini dada aliwahi kuishi huku!!"" Kwanini aishi huku tenaa!!! Ndio alikuwa mkeo unayesema siku zote!! ?""
"" Joanyther Ni rafiki yangu wa karibu Sanaa!! Japo niliambiwa nimuoe lakini haikuwa matwaka yetu!! Japo wao walijua tumeoana lakini haikuwa hivyo tuliheshimiana tu ""
"" Kwani ililazimu Nyie muoanee??"
"" Daaaah!!! Ngoja nikueleze ilivyokuwa Mpaka Mimi nikaishi na Joanyther. Baada ya ujio wa Joanyther katika kijjiji chetu ilikuwa hivii,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,""
Alimaliza kusimulia.
'" Daaaah!!! Mbona Ni Kama simulizi unayonisimulia, Vipi unampenda Joanyther?? ""
"" Kawaida tu!!!"
"" Naomba unipeleke kwa Cheaf nataka nikamuage niende nikaione familia yangu!! ""
Waliongozana moja kwa moja Hadi kwa Cheaf. Movick alifika akajieleza kwa Cheaf akawa kampatia likizo, lakini kwa Ibrahimu alimsihi Sana baba yake wangeongozana wote waende halafu ka wiki moja ikipita Ibrahimu atarudi lakini Cheaf alimkatalia Sana zaidi ya kumwambia atamwandalia Movick Walinzi kuhakikisha anafika salama.
Siku iliyofuata Movick alikuwa tayari kaandaa kibegi chake alichokuja nacho tayari kuondoka.
Muda huo alikuwa akimsubili Ibrahimu aje waagane aendelee na Safari lakini hakutokea zaidi ya Walinzi walikuwa wakimsubili nje.
Aliamua kuachana nae ili aendelee na Safari yake. Muda kidogo alitoka nje ili waanze Safari, Lakini alishangaa Cheaf kafika hapo akiwa na Ibrahimu.
"" Movick!! wewe Ni Kama mwanangu ila kuondoka kwako hapa kijijini kumemfanya mwanangu asononeke sana!! Nikuombe tu utakwenda na Ibrahimu ila wiki moja hakikisha anarudi, Na Nyie Walinzi hakikisheni mnarudi kabla ya lisaa kupita hiyo wiki ikifika!!! ""
Movick alibaki kushangaa hakuamini Kama Cheaf anaweza badilisha maamuzi haraka hivyo, alijiuliza kipi kimempata Mpaka amruhusu lakini hakujali yote hayo alikimbia na kumpongeza Ibrahimu.
"" Mimi pia nilitegemee tuambatane na wewe!! Nimefurahi Sanaa!!! ""
"" Usijali!!! Tuondokeni!! Mnataka Cheaf abadilishe maamuzi!!!
¶¶¶¶¶¶
Upande wa Joanyther siku hiyo alitokana wajukuu wa Bi Emma kwenda kufua mtoni, lakini siku hiyo alionekana Ni mtu mwenye furaha Sana alikuwa akiimba nyimbo za hapa na pale Mpaka wenzake walimuuliza,
"" Joany!!! Mbona leo una furaha Sana!! Tangu tufike hapa Ni wewe na nyimboo kulikoni??" Alikuwa Ni Ancile.
''" Unajua Muda mwingine unaamka umekosa tumaini, huna mtu wa kumueleza unaamua tu ujieleze mwenyewe halafu unabaki ukicheka mwenyewe!! "
"" Kwahiyo na wewe ndio umefanya hivyo!! Sikujua Aliuliza.
"" Ndivyo hivyo bhanaa!!! Basi tuondokeni bado mapema tusing'atwe na majoka porini.
Siku iliyofuata Joanyther Alikuwa yupo jikoni akiandaa Chakula kainjika viazi. Mdogo wake Sikujua Muda huo Alikuwa anatoka shuleni( Darasa la sita) aliwaona Kuna vijane wane wanakuja huku wamebebelea mzigo, aliwahi nyumbani na kufika kumsitua Dada yake akiwa jikoni.
""" Dada Joany!! Nimeona Kuna watu wengi leo, wanaingia Kijijini wamebebelea mizigo mingi hafu wengine wananyama, hafu wamepanda farasi. ""
"" Sikujua mdogo wangu una maneno mengi Sanaa!!! Kwani Ancile Yuko wapi.""
"" Atakuwa bado yupo shule( form Three) Make sijawaona wakipita shuleni kwetu.
"" Basiiiii!! Badilisha nguo uje ule Kwanza!!
Muda huo Ancile Alikuwa akitoka shule lakini alisikia ikiitwa!! Ilibidi ageuke nyuma. Hakuamini kumuona Movick mbele ya macho yake alitupa garoli lake na ufagio, Kisha alikimbia moja kwa moja nakumkumbatia Movick, Kisha alianza kumkagua kagua.
"" Movick!!! Ni wewe Kweli!! Kumbe bado unaishi, ulipotelea wapi lakini??"
"" Ancile!! Ni wewe Kweli!! Ila umekua karembo Kweli. Ilibidi amkumbatie Mara mbilimbili kwanza Kisha alimkiss shavuni.
"" Nilikumisi Kweli mpenzi wangu!! Waooo!!! Leo Joanyther sijajua tu leo atakuwa na raha gani, make tokea Jana Alikuwa na furaha Kweli sijui mlimwambia ujio wenuu!! ""
"" Unaongea mno!! Mwishowe uwasahau wenzangu kuwasalimia!!, salimia kwanza mengine tutayaongea!!"
Baada ya kusalimia Ancile aliwaelekeza wageni moja kwa moja Hadi Nyumbani. Alifika na kuanza kumuita Joanyther, lakini Muda huo Alikuwa ametoka kidogo, Alitokeza Sikujua.
"" Wewe Sikuu!!! Kama vile huoni hebu njoo upokee mizigo hapaa!!
Sikujua ndio anagutuka.
"" Ka Movick Ni wewe!!! Alikimbia na kumkumbatia.
"" Sikujua umekuwa Kweli, yaani naona siku hizi utakuwa umeacha tabia ya kubebelea mahindi ya kuchomaa kwenye mbegi!! ""
"" Kaka nawee!! Unaniabisha hivyoo!! Mbele ya wageni et!!
Walipumnzika kwenye viti huku Ancile na sikujua wakiandaa chakula mezani.
Muda kidogo Joanyther Alikuwa akiingia ndani huku kubebelea samaki mkubwa mkononi huku akiimba nyimbo zake, Alifika Mlangoni na kushangaa viatu vimekuwa vingi.
"" Kina Nani tenaa wamekuja!!! Nipo najiimbia Kumbe wananisikia si et!! Alikuwa akijiuliza.
Alifunua pazia la sebuleni huku akiwa anachungulia kwenye upenyo, aliona sura ya Movick na Ibrahimu na wale Walinzi Mathew, na Athuman.
Ndipo alipoita kwa sauti! Movick!; Movick!!! Huku akimkimbilia kumkumbatia, kwa pupa aliyokuwa nayo alijikuta akijikwaa kwenye meza na kuangukia moja kwa moja kwa Ibrahimu! Nakubaki amemtolea machoo!!
"" Ibrahimu!! Ni wewe Tenaa!!! Hivi umerudi kwaajili yangu!!?!""
"" Uwe mwangalifu!! Siku zote nakwambia jisimamie mwenyewe!! " Kisha alimwachia na kumuonesha siti ya kukaa!! ""
Joanyther aibu zilimuingia Mpaka akashidwa Tena kumkumbatia Movick. Ilibidi tu waanze kuulizana.
"" Ulikuwa wapi Movick!! Siku zote nakutafuta hauonekani kila sehemu!! Kukutafuta kwako kumefanya Bibi apoteze maisha., Kisha machozi yalianza kumtoka.
"" Samahani Dada!! Mimi pia sikupenda itokee hivi!! Nimesikia na baba alipoteza maisha tenaaa!! ""
"" Wewe Nani nakwambia!!? ""
"" Ibrahimu bhana!! Hujaona nimeongozana nae.
""" Unataka kunambia upo Safari moja na Ibrahimu?? ""
"" Ndio!!!! Wewe maswali mengi ya Nini?? Tutaongea bhana, nataka kujua habari za baba kwanza!! ""
"" Baba Alifariki, Akiwa hospital akipata matibabu!! Lakini Baada ya kuzinduka alijikuta na majeraha akaamua kujilusha dirishani na huo ukawa mwisho Wa uhai wake, sijajua vipi kuhusu wewe!! Uulikimbilia wapi siku yenyewe!!""
"" Maskini Baba!! Mimi sizani Kama Kweli ile ilikuwa Ni akili yake Mpaka imefikia kaamua kujilusha, hapa Kuna kitu kilifanyika Mpaka akajilusha!!""
"" Kwanini unasema hivyoo??"
"" Hapa nakumbuka!! Siku Moto unaunguza nyumba Kuna mtu aliingia chumbani kwa baba akiwa amevalia nguo nyeusi na barakoa Alipofika chumbani alimchoma sindano baba na kutoa damu yake!! Mimi nilipoona hivyoo nilipiga kelele huku nikiwauliza, mnapeleka wapi hiyo Damu?? Ndipo mbaba mmoja aliniziba mdomo na macho!! Kisha alinichukua na kunipeleka Hadi kwenye gari, Kisha nilisikia tu sauti "" Choma moto kila kitu hakikisheni ushahidi wote haubakii.
"" Sasa walikupeleka wapi? Joanyther Aliuliza.
Muda huo watu wote walikuwa wakimsikiliza Movick kwa makini. Upande wa Ibrahimu Alikuwa akijiuliza maswali mengi. "" Kwanini Joanyther ulinificha yote hayaa yotee!!;??""
,,,,,,,,, Itaendelea,,,,,,,,,,,,
USIKOSE KUFATILIA sehemu ya kumi na Tisa.
Je, Movick alipelekwa wapi?? Like comments, Share.
Majibu kipande kinachofuata.
MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: 19 "0746638941"what'sup"
SONGA NAYO.
"" Sasa walikupeleka wapi?? "" Joanyther alimuuliza Movick. ENDELEA...
"" Sikujua hata Ni wapi, ila Safari yetu ilichukua siku mbili kufika lakini pindi nikiwa njiani Kuna sindano nilchomwa nikawa nimepitiwa usingizi Kama siku ya Tano ndipo nilipata Kumbukumbu. Nilikaa siku zote nikiwa natolewa damu inapimwa muda wote!!
Kuna siku nilichoka baada ya kuchomwa sindano, ikanifanya miguu yangu ipalalise, nilianza Taratibu kutafuta njia ya kutorokea ili niweze kutoka katika kitengo hicho.
Nilichukua baadhi ya nguo zilivokuwa kwenye kapu nikabadilisha, make muda wote nilipewa nguo ya kijani nikawa navaa Kama sale ya pale, Siku hiyo nilivua na kuvaa tshrt na jeans Kisha niliingia kwenye chumba kimoja kulikuwa na Watu wakijadili kwa pembeni kidogo niliona picha ya Joanyther imewekwa ukutani Tena karibia kila kiuongo kilitenganishwa; mbavu, moyo, utumbo ,mifupa na vinginevyo na walikuwa wakijadili huku wakitumia picha ya vile viungo.
Baada ya kuona hivyo nilitafuta sehemu nyingine ya kupitia, nilisitushwa na mtu alinishika bega huku kavalia nguo nyeusi juu Hadi chini, kisha aliniuliza.
"" Vipi Unataka kutorokea??? ""
Nilimjibu kwa hofu Sana huku nikitikisa kichwa. "" Hapanaa!! ""
Alinitizima Muda mrefu Kisha alinishika mkono ishara nimfuate. Alinipitisha chocho za hapa na pale na kunifikisha Hadi dirishani Kisha alininyanyua juu na kunirusha Hadi chini na kunipungia mkono huku akitabasamu na kusema.
"" Nenda wewe!! Uishi!! Wewe Badoo Ni kijana mdogo, sie tumeshayazoea haya maisha ila kumbuka kurudi kutusaidia endapo ukifanikiwa kutoka salama.""
Niliondoka kwa hofu huku nikiwa Ni mtu mwenye wasiwasi Sana huku nikiyatafakali maneno ya yule kijana.
"" Kwanini kunisaidia mimi!! mbona kanitendea wema kiasi hicho?? Kwanini kaniomba tena nije nimsaidie!! ""
Niliwaza Sana Lakini niliona Ni Kama nazidi kupoteza Muda!! Niliondoka na kuelekea Hadi stand Kisha nilianza kuwauliza watu hapa Ni wapi?? Waliniambia nipo kibiti ilibidi moja kwa moja nilianza kuulizia gari za kunifikisha kijijini kwetu.
Nilipanda moja kwa moja Hadi Nyumbani lakini nilipokalibia nyumbani kufika niliona gari moja ilikuwa inanifukuzia, ilinibidi nisimamishe hiace, Kisha nilishuka na kuanza kukimbia porini na Muda huo kiza kilikuwa kimeanza kutanda.
Nilitembea porini Kama siku mbili!! Huku nikiwa nakula matunda mbalimbali ndio hiyo siku nilikuwa nimelala zangu!! Kumbe, wale watu walikuwa karibu yangu ndipo waliponiona na kunifunga kamba ilikuwa usiku. Kwa bahati nzuri hiyo siku hiyohiyo ndio nilipata msaada himaya ya kina Ibrahimu!! walinipokea vizuri lakini kwa baadae waliniambia ujio wako kufika kwenye kile Kijiji.
Movick alimaliza kusimulia mkasa wake Kisha alishushia kikombe Cha maji na kunywa.
Muda huo huo mlango ulisikika ukigongwa. Sikujua alitoka na kwendaa kufungua, Ile anafika Mlangoni tu alikutana na vijana wane huku wakiwa wamebebelea siraha walimpiga ubapa wa panga na kuwafanya watu wote waliokuwa ndani wasituke!!
Joanyther alimtizama Movick Kisha alimkumbatia huku akilia Sana.
"" Movick Mdogo wangu!! Leo tu nimekuona nikawa na furaha leo tena tunaenda kutenganishwa! Naomba jisimamie Mdogo wangu hakikisha unakuwa mzimaa!! ""
"" Wewe!! Pia Da Joany!! Naomba ujisimamie mwenyewe!! Hata hivyo nimefurahi kukuona Tena ukiwa hai!! Nitahakikisha nakuwa mzimaa, hata kwako lazima uwe mzima!! ""
Vijana wale walizidi kuingia ndani!! Hadi walipofika sebuleni waliwakuta wametulia tu wakisubili liwalo na liwe.
Kijana wa Kwanza!! Alicheka kwa dharau huku akisema.
"" Ama Kweli Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu!! Hafu leo jiwe moja linaua Ndege wawili kwa mkupuo, Hakika hii Ni bonge la surprise!!""
Kijana wa pili alitoa pingu na kuwafunga!! Ibrahimu, Movick, Mathew na Athuman huku Joanyther alionekana akisumbua Sana huku akikataa kufugwa ndipo kijana mmoja alimnasa kibao kikampa wenge!! Na kuanguka wakawa wamefanikiwa kumfungulia pingu.
Muda huo huo!! Gari Ilikuwa imeandaliwa walipelekwa kwenye Gari Kisha gari iliwashwa kwa spidi Kali.
Nyumbani alibakia Ancile Muda huo Alikuwa amejificha kwenye uvungu wa meza, baada ya kuona kimya alijifunua na kutoka hadi Mlangoni, alimkuta Mdogo wake Sikujua ndio anazinduka, alimsaidia kumtoa pale huku wakiwa wanakimbilia barabarani kutizama gari ile ndipo waliona vumbi tu linaishilia walizidi kukimbia huku wakilia wakiita, " Da Joany!!! Movick!!! Lakini wapi ilibidi warudi Hadi Nyumbani huku wakilia Sana.
Ancile ilibidi ambembeleze Mdogo Wake huku akimtia moyo.
"" Usilie Sikujua!! Kaka, Dada wote watarudi tu!! Halafu wale watu pindi umezimia waliniambia wanawachukua kwa muda wa wiki moja wanawaludisha!! ""
"" Hapanaa!! Dada!! Mimi nilikuwa nafatilia mazungumzo ya Ka Movick!! nimemuelewa vizuri!! Wanaenda kuuwawa kwenye kile kitengo, wewe dada hujali kumbe!! ""
"" Ungejua naumiaje, Hapa Movick nilimumisi sanaa Kuna mambo mengi tuliahidiana kuoana na mambo mengi! Ona Sasa!! Kaniacha tena huku nikiwa bado namhitaji!! ""
"" Poleee Dada!! Jikazee sa mbona unalia kiasi hichoo!! Nyamaza basii!! Wewe ukilia Mimi nitafanya!!""
Ancile ilibidi amkumbatie tu Mdogo wake huku wakisaidiana kulia!! Waliamua kurudi nyumbani huku wakijivuta Taratibu, walifika na kufunga mlango huku kila mtu alikaa na pozi lake akitafakari mambo ya nyuma pindi wakiwa na Bibi Yao!! Na maisha waliyoishi wakiwa na Movick, na Joanyther na kujikuta machozi yakizidi kumwagika Kama maji!! Usingizi hawakupata Tena mpaka kulipotimia asubuhi siku hiyo hata hawakwenda shule walielekea kwa Mwenyekiti wa Kijiji na kumueleza kilichowasibu usiku wa kuamkia siku hiyo na kuanza kulifanyia upelelezi tukio Hilo.
^^^^^^^^
Huku njiani upande wa wasafiri, Safari ilizidi kuendelea mpaka usiku wa manane, Wakwanza kuamka siku hiyo Alikuwa Ni Joanyther aliamka na Kumtizama Mdogo wake Movick alikuwa kalala, alipiga jicho akiwatazama Walinzi wa Ibrahimu nao walikuwa usingizini.
Alimtizama Tena Ibrahimu na kumkuta Muda wote yupo Macho Alikuwa akitazama nje akisoma ramani ya mazingira wanapopelekwa.
Joanyther Aliamua kumkanyanga mguuni Ibrahimu amsitue ili aamke!! Ibrahimu alimgeukia Joanyther na kubaki akitabasamu tu Kisha alimsogelea na kumnong'oneza sikioni ili watu wasisikie wakawashitukia.
"" Vipi!!! Umeona uwezekano was kutoroka naona wale wababe wamepitiwa usingizi hapa kinachofuata naomba tushuke!! ""
"" Sasa!! Tutashukaje Sasa wakati gari inatembea!! Na wakitushitukia unazani itakuwaje Kama siyo kuuwawa, kwani wenzetu wanajua kuwa tunataka kushuka?? ""
"" Hapa wenzetu wote wanajua!! Na hapa hawajalala wapo macho ila wanamzuga Dreva!! Hawa Walinzi Watatu tumeshawazimisha na ule unga kuamka badala ya masaa Ishirini na mane ndo wataamka Sasa chakufanya, Nataka tumzime Dreva hafu wewe ukaendeshe gari make sisi sio wazoefu kuendesha ndo maana Muda wote tumekusubili wewe uamke tufanye utaratibu huo, tuliogopa kukuamsha make wewe huwa mlopokaji mno, naomba nifanye hivyo na wewe ufanye hivyo.
Joanyther hakuamini Kama Ibrahimu angewaza kujikomboa kwa njia hiyo, alimtizama Kisha aliachia tabasamu huku akiitikia kwa kutumia kichwa ishara ya kukubali.
Ibrahimu Muda huo Alikuwa tayali kafungua pingu. Muda huo huo Dreva aliingia na hofu kwa ukimya uliokuwepo aliamua kugeuza kichwa chake nyuma kuangalia usalama Kama upo, aliona watu wote wamepitiwa usingizi.
Aliamua kuita
"" Kamanda GP mbona kimya kwahiyo mmelala Mimi nasikia usingizi umeanza kunielemea au tupumnzike wote Kwanza hata nusu saa!! ""
Alisubilia majibu ajibiwe lakini kimya, Alifunga break ili asimame, Muda huo huo Ibrahimu alipoona kafunga break alifurahia na kusema.
"" Hapa kazi tiyari mmeturahisishia alisogea na kumpulizia unga na kumfanya Taratibu usingizi umpitie.
Baada ya kukamilisha zoezi hilo walisaidiana haraka kuwashusha Kisha Joanyther alichukua gari Ile na kuiondosha kwa Kasi, na kuanza Safari isiyojulikana mwelekeo zaidi ya kusonga mbele tu.
Movick ilibidi amuuluze Dada yake.
"" Hivi Da Joany!! Hebu funga break Kwanza tuangalie Kama Kuna camera huenda Ina rekodi kila kitu humu!! ""
Joanyther alisimama na kuanza kukagua, ndipo Kweli walibahatika kuiona Camera!! Waliifungua na kuona mkanda uliokuwa umerecord kila kitu kilichokuwa kinafanyika kwenye kile kitengo.
Ibrahimu aliwaomba waache Kwanza kuangalia Camera maana wapo kwenye hatari. Lakini upande wa Movick alizidi kukagua kwenye kila seat na kupekua. Mwishowe aliona boksi lipo chini ya Seat aliamua kulifungua huku akipenyua, aliona Books limejaa syringe za kila Aina na dawa za kutosha pamoja na Sample zenye damu zikiwa kwenye books Lile, alikausha na kutomwambia mtu huku akizidi tena kupekua kwa pembeni tena kulikuwa na books jingine alilifungua Taratibu Huku asiamini macho yake baada ya kuona books limejaa pesa!!
Alitabasamu kwa furaha huku akiwa anaona Ni mshindi katika mtihani huo.
Joanyther yeye hakujua kilichokuwa kinaendelea kwa Movick. Yeye Alikuwa macho take yamelenga mbele na usukani huku pembeni Alikuwa kakaa Ibrahimu akimpa kampani. Aliamua kumuuliza Ibrahimu.
"" Unajua mpaka Sasa!! Najiuliza hizo akili Wewe ulizitoa wapi, mpaka tumetoka kwenye himaya Yao?? ""
"" Wewe nawee!! Nakuomba endesha usiwe hivyo usijihisi kuwa umshindi wakati mpaka Sasa twatembelea himaya yao!! Tayari gari lao tunao Wewe huoni bado tupo nao!! Mimi nafikilia tukikalibia mjini gari tuliache tutembee kwa miguu make wakianza kutufatilia wakiuliza watatupata kwa wepesi Sana kwa hili gari!! Au Wewe unaonaje ??! ""
Movick Muda huo Alikuwa akiwasikilizia, ndipo wazo lilimuijia hapa Ibrahimu Ana wazo zuri sana, ilibidi atoe books Lile la pesa na kuwaonesha.
""" Hizi pesa nimeziona zipo humu kwenye Gari, Mimi ninasaport maneno ya Ibrahimu tufanye hivyohivyo na hizi pesa zitatusaidia kufika Mbali, pia tutaendeshea maisha na hapa itabidi tuhame Nchi kabisa' tukaanzishe maisha mapya sehemu nyingine. ""
Joanyther na Ibrahimu hawakuamini Kama ingetokea bahati kubwa kiasi hicho.
Muda ulizidi kwenda hatimaye kukapambazuka Tena!! Walizidi kusonga huku wakiendelea na Safari yao Lakini kwa Mbali walianza kuona Mnara na Nyaya za umeme zimepita, ilibidi washuke wafanye Kama walivyopanga waiache Gari.
Muda huo huo wanashuka walisikia King'ora kinalia huku sauti ikiwaelekea Kuna gari inakuja ilibidi wakimbie msituni huku wakiwa wamebeba kila kitu na kujificha!!
Muda kidogo Gari ilifika pale na kupaki walishuka Askari Game huku wakiwa wameshikilia siraha zao mkononi, walianza kukagua Gari ile lakini hawakuona Kama Kuna mtu.
Mkuu wao alitioa agizo watafutwe watu walioingia porini kwa uwindaji haramu pasipo kibali chochote hafu Mbaya zaidi Gari Ilikuwa haina Prate Number, ndipo msako ulianza papo wa kuwasaka.
,,,,,,,,, Itaendelea,,,,,,,,,
Usikose sehemu ya 20.
Nini kitafuata baada ya Askari Game kuanza msako huo huku. Upande wa Kina Joanyther na wao wamejificha porini happy.
Like, comments, Share then Sambaza link ya Group wadau waburudike na simulizi.
https://www.facebook.com/groups/263417295228138/?ref=share.
MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: 20 "0746638941"what'sup
SONGA NAYO.
Mkuu wao alitioa agizo watafutwe watu walioingia porini kwa uwindaji haramu pasipo kibali chochote cha serikali, hafu Mbaya zaidi Gari Ilikuwa haina Prate Number, ndipo msako ulianza papo hapo.
Upande wa Kina Joanyther baada ya kusikia hivyo ilibidi watafute kichaka kizito wajifiche!! Walikusanyika kwa pamoja huku kila mtu alimwomba Mungu wake, amnusuru na msala huo.
Wale Askari Games, walitafuta Mpaka wakachoka waliamua kutoa ufunguo wa Gari na kuondoka nao, wakijua wamewameza.
Baada ya kuona wale Askari Game wameondoka ndipo na wao walijitokeza huku kila mtu akiwa anapumua kwa Kasi Sana.
Ibrahimu aliongoza msafara wa kuingia mjoni huku wakiwa bado wamebebelea Lile books la hela.
Movick aliwaamuru wenzake watulie kwanza Sehemu aiingie Kwanza mjini akanunue nguo make Upande wa Athuman, Ibrahimu wote walikuwa bado wamevaa nguo za pori. Walitafuta Sehemu ya kujihifadhi Kisha aliwaacha na kutoka na Joanyther kwenda moja kwa Hadi mjini.
Baada kukamilisha mahemezi yote, waligeuza Hadi Sehemu walipowaacha wenzao Huku wakiwa wamewabebea chakula, walikula na kubadilisha mavazi Kisha Safari ilianza moja kwa moja Hadi kwenye hotel kubwa walikuwa tiyari wamebook vyumba.
¶¶¶¶¶¶
Leo katika kitengo Cha Utafiti.
Baada ya kusubili siku nyingi bila kufanikisha watu wao waliokuwa wamewaagiza!! Waliamua kutuma watu wengine wakawafatilie Tena kwa Mara nyingine.
Mkuu wa kitengo alitoa vifaa vingi na kuwapatia vijana wake wawili, make Ni vijana aliokuwa akiwaamini Sana'' Andrew na James, kesho waondoke.
Siku ilifika, James na Andrea walianza Safari ya kuelekea kijijini tena kwao Joanyther.
Safari ilikuwa ndefu!! Hatimaye walifika kwenye hoteli iliyokuwa karibu na mji kidogo, waliamua kuchukua Chumbani na kupumzika siku hiyo ili kesho waendelee na Safari.
Siku hiyo James aliamua akae kidogo nje akipungwa upepo huku akitafakali kazi aliyopatiwa na Boss wake. Muda huo huo amekaa alimuona mtu Kama Movick kapita chap na kupotelea mbele, Aliamua kumfatilia Lakini hakumpata tenaa.
"" Hivi mbona Kama naota vile!! Nimemuona Movick kapita au kwa vile namfikilia Sana!!"
Macho ya James hayakuwa yamekosea sema ni wenge tu alikuwa nalo, Hotel waliokuwa wamefikia na kina Joanyther walikuwa hapohapo pasipokujuana.
Kesho yake asubuhi Movick!! Alijidamka asubuhi huku akifanya mazoezi ya kukimbia, Baaada ya kumaliza mazoezi yake alipitia bombani na kunywa Maji, Lakini kwa Mbali aliona Kuna mtu anakuja pale pale bombani kuchota maji aliiona sura ya James akiwa anakuja, alivyoniambia tena zaidi kwa nyumake alimuona Andrew kavalia track nyeusi Kama kawaida yake. Alianza kuwaza tenaa.
"" Hawa wapo hapa wanamtafuta Nani so itakuwa Ni Mimi!! Au ndo wanaelekea kijijini kwetu tenaaa?? Mbona Andrew siku yenyewe alijitahidi kunitorosha halafu tena na leo Yuko hapa tenaa!!! ""
Uamuzi aliouchukuwa aliamua kuondoka na kwenda kujificha huku akijaribu kuwafatilia kwa Siri sana, Lakini aliwaza tenaa, sawa Mimi nitajificha vipi Joanyther akionekana maana picha yake ipo kule lazima tu watamfahamu, aliona aachane nao Tena na kwenda Hadi kwa Joanyther na kuanza kuzungumza.
""" Da Joany!!! Huwezi amini Tena wale watu wa kile kitengo nimewaona leo wapo hapa!! Na tumelala hotel moja nikuombe usitoke Nje!! Make ukitoka tu hapa watakupata make sura yako ipo kwenye kile kitengo na imebandikwa kila Sehemu kwenye ofisi zao. ""
"" Sasa itakuwaje?? so tuondoke Lakini!!??' Vipi wewe wakikujua si nitakukosa tenaa!! ""
"" Usijali!!! Mimi nitakulinda Wewe na wenzako naomba usiogope!!""
Muda huo alitokea Ibrahimu, alionesha alikuwa akiwasikia pindi wanaongea.
"" Lakini Movick Kama yule Jamaaa!! Mwingine alikusaidia pindi unataka kutoka!! Huyo atakuwa mwema inabidi tufanye njia ya kumteka Kwanza inaonekana Kuna kitu anafatilia katika kitengo hicho angekuwa mtu Mbaya asingekutorosha!! ""
"" Daaaah!! Umesema point vipi Lakini njia gani ya kumteka ifanyike!! Joanyther Aliuliza.
"" Nyie Hawa Watu hamuwajui tu!! Ukiingia kwenye hicho kitengo Kuna kitu huwa wanakuwekea Kama ki Dira! Kwenye mwili kila unapoenda wanakuwa wanakusarch kwenye mitandao yao!! ""
"" Kwahiiyo na Wewe unachoo??? Joanyther alijikuta Aliuliza kwa hamaki ya kupata jibu.
Movick alimshika mkono Dada'ke!!
"" Ndio ninachoo!!! ""
"" Mbona hujasemaa!! Kwanini tumeyafanya haya yote, jitihada zote za Nini!! Si Bora tu twende kwenye hicho kitengo tukatumikie!! Tuache haya maisha ya kukimbia kimbia!! Hapa si ningekuwa nishamaliza hata kusoma, make wanna chuo Chao wanasomesha!! Mbona hata Wewe umekuwa Dokta now.
""" Ee!!! Unapenda kusoma kumbeee!! Pasipo kuangalia afya yako!! Muda wote nakwambia jisimamie kwanza Wewe!! Ibrahimu aliongea.
"" Hapanaa bhana!!! Niliwatania tu!!, Siku ya kuwekewa Mimi hiyo Dira!! Ndio ilikuwa siku hiyo Mimi natoroka so ningebaki tu hiyo siku mimi ningekuwa tayari mikononi mwao!! "" Ndio maana hata leo Hawa wanakoenda wanapajua ile Dira ishawaonesha walipo ndio wataenda kuwachukua.""
Zile Dira walizowekewa begani hufanya Kama kuvutana na kufanya wajue ule ukaribu wao na zinahesabu muda na masaa yamebaki mangapi ili wakutane, pia muda wote usafiri wao hufunga camera Kama Tahadhari ya kujua mazingira na kurecord kila kazi itakayofanyika.
"" Sasa!! Tutafanikishaje kumteka huyo kijana!!?
"" Joanyther ee!! Tulia Basi hili swala tuachie sisi Wewe hakikisha hautoki ndani kwanza Mpaka ruhusa yangu!! Movick Aliondoka kuchungulia usalama Kwanza huku ndani akamuacha Ibrahimu na Joanyther.
Joanyther aliinamisha kichwa chini huku akijaribu kukumbuka maisha anayoyapitia, Mawazo yalienda Mbali na kumpeleka akumbuke hata mama yake, alianza fikilia malezi ya baba na mama!! Huenda wangelelewa pamoja na Wazazi wawili hayo yote yasingetokea, aliamini utengano wa Wazazi ndio ulisababisha yote hayo.
Ibrahimu alimuona Joanyther Hana raha ilibidi asogee amtie moyo kwa nyakati anazozipitia.
"" Unawaza Sana Mpaka unafikia Mbali hebu kuwa na Amani haya yote yataisha tu, Kisha alimuegemeza kichwa kwenye bega lake huku akizidi kumbembeleza. ""
Movick alirudi tena na kumkuta Joanyther na Ibrahimu wapo katika mkao was kubembelezana, aliishia kutabasamu tu na kujisemea.
"" Kumbe kweli, Joanyther ulimpenda!! Ndio maana ulisononeka Sana pindi amekuacha!! Lakini huu Muda sio salama!! Tukamilishe Kwanza usalama wetu mengine yatakuja tu!!.""
Muda huo Ibrahimu ndio anazinduka kwenye mawazo make akili yake ilienda mbali Sana, baada ya kukaa na Joanyther, Ukweli alimisi Sana ukaribu wake tangu atoke kijijini hajapata hata Muda wa kucheza wote na kutaniana Yale matani ya hapa na pale!!
"" Aaaah!!; Movick umerudi??! Huku akiwa anamuachia Taratibu Joanyther na kumlaza kitandani.
"" Nimefanikisha swala letu!! Tayari nimeshajua chumba walicho, Lakini Mimi naona ngumu bado make nikisogelea tu yale mazingira Badoo kile kidude kwenye mitandao na Mimi nitaonekana make nitakuwa karibu nao chakufanya!! Wewe mteke Andrew mpeleke kwenye chumba chako Kisha mwambie kile kidude akipoteze direction kisisome kwa muda yu wapi?! Hafu mwambie Movick anataka kuzungumza nae!! Hafu utanipigia simu.
Ibrahimu alikubaliana na Movick, Kisha alitoka Taratibu na kwendaa Hadi nje huku akiisubili jinsi ya kumpata Andrew
Upande wa Andrew Alikuwa akitoka kutembea zake huku Taratibu akiwa kavalia track ake nyeusi na mzura na huku kaweka Earphones akipata mziki laini.
Ibrahimu alizidi kumnyemelea mwishoe, Alimvaa na kumpakaa unga wausingizi Kisha Alimchukua kiulaini Hadi chumbani kwake, akiwa hajitambui.
Alichukua maji na kumumwagia usoni, kumtoa wenge la usingizi Kisha alimbana shingoni na kumuwekea kisu.
"" Naomba Zima Dira yako kwanza Kuna kitu nataka niongee na Wewe kwa amani tu.""
Andrew alimuuliza kwanza.
"" Ingekuwa kwa amani ungeniteka!! Mimi nitakuamini Vipi Kama Wewe Ni mtu mwemaa!!!""
Ibrahimu alimsogelea na kumnong'oneza sikioni.
'' Samahani anayekuhitaji hapa Ni Movick tu!! ""
Andrew baada ya kusikia Movick. Alizima haraka kidude chake.
"" Kwani yeye Yuko wapi??
Ibrahimu alichukua simu na kumpigia Movick, Kisha alifika sehemu hiyo.
Ile Andrew anageuka hivi hakuamini kumuona Movick mbele Yake , alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha Sana.
"" Vipi Movick!! Kumbe!! Uliishi tenaa. Alimkumbatia tena!! Kwa furaha,na kumwambia.
"" Kwanini upo hapa!! Nawakati unajua ujio wetu Ni kukutafuta Wewe halafu nimemuona Joanyther na yeye upo nae huoni unakosea, umesahau kuwa yeye ndio anahitajika Sana kwenye kile kitengo?? ""
"" Sasa naenda wapi na wakati!! Sioni mbele Wala nyuma, niambie Wewe pa kwendaa!!??""
"" Ukiwa unatafutwa huku unakosa si huwa unabanza sehemu ili adui asikuonee!! Halafu tayari na huyu kijana!! Ushamwingiza kwenye hatari tenaa!! ""
"" Kijana gani Tenaa huyoo !!??""
"" Ulie nae hapa!!!, Kuna alama nimeziona kwakee na alama hiyo inatafutwa sana'' nikuombe kaa mbali na Watu wa kitengo hiki, ila nimefurahi Sanaa kukuona na imani siku moja utarudi kutukomboa na Mimi nitakuwa kampani yako. Kisha alimuaga na kuondoka.
,,,,,, Itaendelea,,,,,,,,
USIKOSE KUFATILIA sehemu ya 21.
Mambo yanazidi kupamba Moto. Ni kitu gani hicho kipo kwenye mwili wa Ibrahimu, na itakuwaje hatima Yao.
Like, comments, Share. Hakikisha una join kwenye Group ili upate simulizi zote. Sambaza Link kwa Magroup mengine ili kuburudika na wenzako.
https://www.facebook.com/groups/263417295228138/?ref=share
MTUNZI: TINNER ROBER. SIMULIZI: GLOOMY SUNDAY SEHEMU: 21 "0746638941"what'sup
ANZA NAYO!!
Kijijini kwao Ibrahimu.
Leo Cheaf was Kijiji baada ya kuisha wiki moja na siku tatu alikuwa akimsubili Ibrahimu aweze kurudi na jopo lake. Ilikuwa ni majira ya asubuhi Mpaka kulikucha tena pasipo majibu yoyote, Siku iliyofuata aliwaita baadhi ya Walinzi wake warudi tena Kijijini kwao Joanyther wafatilie kipi kimewapata huko kimewakawiza.
Siku iliyofuata Walinzi wane waliongozana Hadi kijijini kwao Joanyther. Iliwachukua Kama Siku tatu kufika.walifika kwa kuulizia Kwanza kwa mwenyekiti huku mazungumzo yakiendelea.
"" Samahani Cheaf!! Tumeingia hapa kijijini kwenu pasipo utaratibu!! Lakini Ni kwa amani Sana, tumekuja kuulizia wageni wetu walikuja hapa wakiwa wameambatana na Joanyther, na makubaliano yetu yalikuwa ni wiki moja wangerudi Lakini hatujafanikiwa kuwaona, sijui Ni Nini kimewakawiza Cheaf. ""
"" Vijana wangu nashukuru pia kwa kufika hapa, kwa kuwa mmefika naomba tujadiliane tuone tunalifanyiaje kazi swala hili, Wageni wenu walifika wakiwa wa tatu, Huku Movick akiwa Ni wanne. Siku hiyo walifika na kupokelewa vizuri! Huku salaam ziliendelea ndani Lakini kulitokea na watu wanne waliingia ndani na kuwavamia wakawa wameondoka na usafili wao!! Majira Kama ya usiku, tangu siku hiyo hawajaonekana Tena, na Wala haijulikani wako wapi?? ""
Baada ya kupata majibu wale Walinzi waliamua siku hiyo kwenda moja kwa moja Hadi kwao Joanyther. Kuangalia mazingira na usalama Kama upo.
Siku ya kesho yake kulionekana gari ilikuwa ikiungia moja kwa moja hadi mlangoni kwa kina Joanyther, baadae alionekana James na Andrea wakishuka kwenye gari.
Waliingia moja kwa moja Hadi ndani na kuwakuta Sikujua na Ancile wamekaa huku wakijisomea na pembeni walikuwepo watumishi wa Ibrahimu walikuwa wakijadili jinsi ya kuwapata ndugu zao.
Andrew na James walifika na kukaa na kuanza kuwahoji kutoweka kwa Joanyther na Ibrahimu na wale Walinzi, mwishowe walifikia Hatima na kuamua kuondoka kila mtu alirudi makwao.
¶¶¶¶¶¶¶¶
BAADA YA MIAKA MITATU KUPITA.
Leo katika kampuni kubwa Nchini Urusi alionekana kijana mmoja amekaaa akiwa anasaini documents zake huku akiwa na mtoto kambeba miguuni akimpatia dawa, Kijana huyu Alikuwa mwenye mawazo Sana huku akinung'unika moyoni na kusema;
"" Haikuwa matakwa yangu Mimi leo niishi hivi, Mbona Ni mapema Sana nilijua moyo wangu siwezi kuuwekeza kwako Leo hi umenifanya niwe mtu wa kumlea huyu mtoto!! Kwanini Ancillah ulikuja kwangu, Kumbe ujio wako ulitegemea niwe mzima tazama Leo siwezi kutembea umeamua kuniachia na huyu mtoto.
Muda kidogo alifika mtumushi mmoja akiwa na hofu Sana.
"" Dokta!!! Jolvin, Mkeo huko anakufaa!! Fanya haraka ukatoe matibabu!!
Ndipo Jolvin Alionekana yupo kwenye Wheelchair akizidi kukokota mkokoteni wake Hadi kwenye chumba Cha matibabu alichoitiwa, Alifika na kusogea karibu na kumfunua mkewe ambae kwa muda huo alikuwa Ni Ancillah. Alichukua file la mgonjwa na kupitia Kisha alimuuliza;
"" Kipi kimekupata tena mpaka hapa umerudi ukiwa katika khari hii kwanini uliamua kumkimbia mwanao akiwa na miezi mitatu, nimemlea kwa shida mpaka kafikisha miaka miaka miwili, halafu leo hii unarudi ukihitaji msaada wangu!!!""
Ancillah alikuwa kwenye khari mbaya alinyanyua kichwa chake huku akimtizama Jolvin na kumnyoshea mkono.
"" Nisamehe Mimi!! Sikulizia kuwa na mwanaume kilema katika maisha yangu, pia naomba huyo mtoto(Gift) nataka nimpatie baba yake, nisamehe kwa kuwa sikuwa mkweli kwako huyo mtoto Ni wa Alvin na ndio baba'ke halisi, siku zote nilikuwa nikitoka nae!! ""
"" Ancillah!!! Ancillah!!! Sitaki kusikia habari hizo, siamini Kama leo hi Wewe ndio unataka kuniadhibu kwa uchungu kiasi hiki!! Kwanini!!! Huyu mtoto ulimuacha na ulishidwa kumpeleka kwa babake!! Alvin Mdogo wangu tumelelewa familia moja na Wewe umenisaliti mimi!! Hakika huyu mtoto uhai wake utaishia hapa!!"
""" Please!! Please!! Jolvin!!! Mtoto Hana makosa, hajakukosea Wewe muache aishi!! Bora uniazibu Mimi kuliko mtoto.""
Muda huo huo!! Mabishano yalizidi kuendelea huku wakivutana pande mbili. Mara walisikia sauti upande wa pili ikisema;
"" Jolvin!!! Hupaswi kufanya hivyo Gift ataishi, huyu ni damu yangu na Ni mwanangu pia!! Suruhisho sio kumuua mtoto ila Ni Wewe kupata mtoto!!!""
Jolvin aligeuka akisikiliza sauti hiyo hakuamini Kama ndio ndugu yake Alvin alikuwa akiongea.
"" Alvin!! Alvin!!! Ni Wewe Tena unakuja mbele yangu ilikhari umenikosea vyakutosha bado una maneno mengi hafu wazidi kunitolea kweli!!!!??""
"" Tafuta Hatima ndugu yangu!! Mimi nilichohitaji Ni kufanikisha kila mpango!! Japo umeenda sivyoo Mimi nilimleta Ancillah kwako! I'll ahakikishe kampuni yote inakuwa mikononi mwetu kwa habari ya mtoto alinificha na kusema Ni wako, hapa nmefanya tafti zote mpka nimepima DNA ya mtoto na Mimi hapa Ikamerch bado Tena Ancillah hapa anakiumbe changu anataka kukitoa!! Hapa Ni Wewe ndio utachagua Ancillah afe na mtoto tumboni wote. Make kwa dawa alizotumia tiyari mtoto kashikilia roho ya mama, na ukitaka aishi utaalamu wa kumrudisha mtoto akakaa vizuri kwa hapa barani Africa utaalamu huo unao Wewe, Kama utachagua Ancillah usimuone tena, kisa ugomvi wa kugombania mtoto basiii, It's up to you!!.Kisha alimbeba mwanae na kuondoka.
Jolvin alijaribu kujivuta na Wheelchair yake huku akimsogelea Alvin. Alvin alijua Kuna mtu anamfuata aliamua kutoa Bastora yake na kumgeuzia Jolvin.
"" Kuna kitu kingine bado unataka!! Useme nikiwa bado sijachukua maamuzi mengine!! "
Jolvin aliishia Kumtizama ndugu yake asiamini Kama kabadilika kiasi hicho na kuwa katili, aliamua kumuuliza tu.
"" Unajua na kufikilia Sana!! But sipati majibu, unaweza kunambia tayari unafanya kazi na kile kitengo ndio wamekuchoma zile sindano mpaka umekuwa katili kiasi hiki!!??" Anyway!! Sipaswi kujua vipi Joanyther na Movick wapo wapi??!""
"" Jolvin!!! Mimi nilifata pesa!! Na pesa ndio kila kitu, unavyozidi kuuliza maswali mengi ndio unazidi kupoteza muda wa Mimi kwenda kumalizia mishe yangu, Joanyther na Movick wote tunao katika kitengo. Kitu kinachotufelisha Ni ile Group la damu AB la kumerch pale tukamilishe project yetu ndio bado hatujapata, ila Kuna kijana alikuwa na Joanyther inasadikika ndio analo Lakini na yeye alikimbia muda mrefu haijulikani Kama atakuwa wapi??""
"" Alvin please!! nakuomba usimzuru Joanyther Tafadhari Kama umechukua mwanao nikuombe uniachie Joanyther please, Wewe njoo umchukue Ancillah uende nae tu!!""
"" Ancillah!! huyo atapoteza maisha punde tukizidi kupotezeana muda hapa atakufa!! ""
Jolvin hakuwa na budi Zaidi ya kuachana na Alvin, alianza jitihada za kunusuru maisha ya Ancillah Kwanza Kisha mengine yatafuata taratibu.
Aliwaamuru wafanyakazi wake wamchukue na kumpeleka Chumba maalumu, matibabu yalianza kufanyika huku yakiwa kwenye uangalizi maalumu wa Jolvin!! Yalichukua Kama masaa6 kukigeuza kile kiumbe kirudi katika mfuko wake wa uzazi baadae walifanikiwa na kumuacha mgonjwa kupumzika Kwanza.
Siku nyingine katika Chumba Cha Ancillah, leo ndio fahamu zake zilianza kurudi taratibu, huku akimuita mwanae;; Gift!! Gift!!
Muda huo Jolvin alikuwa kakaa karibu yake huku akiwa anamtizama Ancillah kwa hasira Sana. Huku akijisemea moyoni, "" Sipaswi kulipiza baya kwako!! Kama ningeamua leo maisha yako yalikuwa Ni mikononi mwangu!!;""
Ancillah ilibidi aangaze macho yake huku na kule ndipo alipomuona Jolvin kakaa mbele yake akiwa na Chupa ya uji alimimina kwenye kikombe Kisha alianza kuipoza taratibu, Alivuta pumzi ndefu na kumuuliza.
"" Vipi Ancillah!! Kwa Sasa unaendelea??
Ancillah aliingiwa na woga!; Na kubaki ametoa macho yake asiongee kitu!! Alishika tumbo lake Kwanza na kumuuliza Jolvin;
"" Mwanangu tenaa bado anaishi!!??" Kwanini umenisaidia mtoto huyu aendelee kuishi tenaa!! ""
Lakini Jolvin alizidi kumsogelea Hadi kitandani kwake. Kisha aliinua kijiko Cha uji na kumupatia Ancillah.
"" Kunywa Kwanza Uji!! Hayo maswali nitakujibu baada ya kumaliza kikombe hiki!!; ""
Ancillah alimtizama Mara mbili mbili, Jolvin hakuamini kwa yote aliyomtendea bado anakuwa karibu yake tena!! Alijaribu kuukataa uji huku akili yake ikimtuma Mambo mengi Sana huenda Jolvin kamuwekea sumu ili afe anaona kabisa tatizo lake lilianzia wapi, alikuta anakataa ule ujii.
Jolvin alishusha kile kikombe Cha uji Hadi chini Kisha Alimkazia jicho na kumuuliza.
"" Kwani hayo maisha yako kwa Sasa yapo mikononi mwa Nani?! Mimi ndio muamuzi wako mpaka kufikia hapa uishi au usiishi!! " Kisha alinyanyua kikombe tena na kumupatia uji.
Ancillah hakuwa na majibu Zaidi ya kunyamaza tu, na kubaki na majibu moyoni mwake. "" Wewe Ni mtu mzuri nimeamini Kama ungetaka Mimi nisiishi tena!! Usingenisaidia!! Kwa Sasa nataka nikuamini tu, make Sina chaguo sahihi kwa Sasa!!""
Jolvin alimaliza kumpatia uji Kisha alijivuta kwenye Wheelchair yake aondoke!!
Ancillah alimuwahi na kumshika mkono Kisha alimuuliza.
"" Jolvin!! Ahsante kwa msaada wako, ila na swali nataka nikuulize, Gift yupo wapi kwa Sasa!!?""
"" Hupaswi kuuliza maswali mengi kwa Sasa!! But yupo na wafanyakazi Nje!! Muhimu kwa Sasa angalia maisha yako na kiumbe kilichomo ndani!! Halafu punguza stress kwa Sasa!!
Kisha aliondoka.
Ancillah alibaki akifurahia na kuzungumza pekee.
"" Jolvin Kweli Ni Careling , pia Ni romantic boy!! Na kumuuzi kote huku bado yupo na Mimi itakuwa Kumbe alinipenda toka zamani ila aliuficha upendo wake asinioneshee ila hapa kwa Sasa ndio nitazidi kujidekeza ili nizidi pata huo upendo uliojificha!!""
,,,,,,Itaendelea,,,,,,,,,,,
USIKOSE SEHEMU YA 22.
Unazani Nini kitafuata je? Ancillah anavyofikili ndivyo itakavyokuwa kwa Jolvin, Atarejesha penzi lake kwa Ancillah!!!!.
Like, comments, share.