Karibu uweze kuendelea kuburudika na story kemkem usisahau kuacha comments yako pendwa kabisa ya Lugembe Tv
MWANDISHI; CHRIST AMAD. SIMULIZI; DON’T CRY ANOTHER LOVE. SEHEMU YA ; 03.
****Ukimya ulitanda mahali pale kila mtu aliwaza na kuwazua asijue mahali pa kuanzia. ``baba Tinnah`` aliinua kichwa chake kwa kusema wanangu napenda sana kila mtu atimize ndoto zake, Tinnah mwanangu shule lazima uende, ili utimize ndoto zako pamoja na Tommy na yeye lazima asome ili plan yake aliyoweka nayeye atimize ndoto zake. Ilikuwa ni sauti ya baba Tinnah iliyojaa simanzi kwani aliwataka wanawe wafikie malengo yao.*****
***MAANDALIZI YA TINNAH KWENDA SHULE YAWADIA. **Ilikuwa ni jumamosi moja alfajili, Tinnah alikuwa tayali kashajiandaa na maandalizi ya kwenda shule, alimsubili baba yake amusindikize stend ya mabasi kwani alimuahidi atamsindikiza pamoja na Tommy. +++Muda si mrefu baba Tinnah’ aliingia,, alikuwa kabebelea zawadi nyingi, kamletea binti yake kama ukumbusho pindi aendapo shule zitamsaidia. Tommy alimwandalia[ Diary] kumbwa lililokuwa na Hadithi mbalimbali ambazo, aliweza kutunga Tinnah, ikiwa ni Tamthiliya, mashairi na vichekesho. Muda mwingi Tinnah alitumia muda wake akiwa free, alijibuludisha kwa kuandika hadithi pamoja na vichekesho kwani alipenda sana kuwa mwandishi wa vitabu japo aliifanya kama kazi ya ziada kwake, aliamini siku moja atakuja kuitumia fun yake ingemsaidia.+++ ```Tommy’’ Alifanya hivyo, hakutaka dada yake apoteza kipaji chake , kwani hadithi za dadake alizipenda saana, na muda mwingine alikuwa akimtungia hadithi kuhusu maisha yake ya mbeleeni akifanikiwa. Na hii ilikuwa zawadi tosha kwa Tommy. ****
***Ndugu,jamaa na marafiki walifika kumuuaga Tinnah’’ na kumpa zawadi mbalimbali na kumtakia masomo mema, kwani walimpenda saana Tinnah kwa ucheshi aliokuwa nao hivyo hawakuona budi kumuunga mkono. Tommy alikuwa mwenye ukiwa saana ,machozi yalimdondoka, baba alimtia moyo Tommy,lakini haikusaidia kitu, Tinnah aliwapungia mkono, huku machozi yakidondoka,,, alimtazama``baba, na mdogo wake Tommy ,,ndipo huzuni ilimwingia nakujikuta machozi yakibubujika,alitamani hata asiende shule,`` Ndipo anapokumbuka aliweka ahadi ya kusoma kwa bidii ili mbeleni aje kuwa mtu mkumbwa; haraka alifuta machozi na kusema mimi siku zote ni shujaa tu sijawahi kufeli wala kukata tamaa. ********
***** Tinnah aliingia kwenye gari,alichagua seat ya dirishani, ghafura`` alisikia sauti iliyokuwa ikimuita,Tinnah; Tinnah; alisituka na kumwangalia,alikuwa ni mkaka mmoja sura yake haikuwa ngeni sana, kama aliwahi kumuona sehemu Fulani, kumbukumbu zake hazikuwa vizuri; kaka Yule alikuja kashikilia bahasha akampatia Tinnah’’ nakuondoka zake, Tinnah alipokea ile bahasha na kuiweka kwenye pochi yake. Safali ilianza kama masaa mawili yalipita, Tinnah; alipitiwa na usingizi,ile anagutuka usingizini ndo anakumbuka bahasha ile aliyopewa , anaiangalia, anakuta juu ya bahasha imeandikwa ```DON’T CRY ANOTHER LOVE’’Ni maneno yaliyokuwa mazito kwa Tinnah,hakuelewa kwanini aliandika vile, halafu ni kijana asiyemjua, na sura ile kama alishawahi kuiona mara moja sehemu , na kwanini aandike vile,ni yeye kweli au katumwa na aliyemtuma ni nani=.++++Tinnah aliamua kuifungua ile bahasha ndani alikuta kuna barua moja imeandikwa kwa maandishi ya kiarabu, na yalikuwa yametafisiriwa kwa Kiswahili, Daaaaaaaa,’’ Tinnah—‘’ hakuamini macho yake````** Je, Tinnah aliona Ujumbe gani; ***********************USIKOSE SEHEMU YA 4’
BY CHRIST AHMAD .