Ni katika nyuso za huzuni pande za Mwanzugi sura za watanzania waliokuwa wakihudhuria kila siku kila saa mpaka kufanikisha kuokolewa kwa miili ya wavuvi waliozama majini katika bwawa la Kijiji hicho lijulikanalo kama MWAMAPULI DAME. Hao walioko pichani ni wananchi wakikusanyika kwa ajili ya kushuhudia miili ya wapendwa hao iliyoonekana ikielea baada ya kumaliza muda wa takribani siku tatu ndani ya maji na hatimaye ikaonekana ikielea Pembezoni mwa bwawa hilo ambalo pia licha ya kutumiwa kwa shughuli za uvuvi linatumika katika shughuli za kilimo cha Kilimo Na Umwagiliaji. #MWAMAPULI_IRRIGATION_SCHEME
Ni bwawa linalotegemewa kiuchumi katika wilaya ya Igunga na hata Mkoani Tabora kiujumla.
Tags
Kitaifa