Ni Fahari kwa Tanzania! Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga Ateuliwa Kuongoza AMECEA

 Na Fredy William

Ni Fahari kwa Tanzania: Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga Achaguliwa Kuwa Rais wa AMECEA

Kanisa Katoliki nchini Tanzania limepokea kwa shukrani habari ya kuchaguliwa kwa Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga kuwa Rais wa Chama cha Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki (AMECEA).


Uchaguzi huu unaonesha imani ambayo Maaskofu wanachama wa AMECEA wameweka kwa Askofu Mkuu Nyaisonga ili kuongoza na kuratibu shughuli za Chama hicho katika kipindi kijacho. Ni pia ishara ya mchango wa Kanisa la Tanzania katika maisha na utume wa Kanisa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

AMECEA ni chombo kinachowaleta pamoja Maaskofu wa nchi za Afrika Mashariki na baadhi ya nchi za Afrika ya Kati kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kichungaji, uinjilishaji, haki na amani, pamoja na maendeleo ya watu kwa kuzingatia mafundisho ya Kanisa Katoliki.

Waamini nchini Tanzania wanaungana na Kanisa zima kumshukuru Mungu kwa uchaguzi huu na kumwombea Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga ili Roho Mtakatifu amjalie hekima, busara na nguvu katika kutekeleza kwa uaminifu dhamana aliyopewa kwa ajili ya kulijenga Kanisa na kulitumikia Taifa la Mungu.

“Bwana amwongoze na kumtia nguvu katika utume wake mpya, ili kupitia huduma yake, Kanisa liendelee kuwa chombo cha umoja, matumaini na upendo katika Afrika Mashariki.”


Source: Vatican News

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi