Vatican Yasisitiza Msimamo: Ndoa Ni Kati ya Mwanaume na Mwanamke Pekee

 Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, amesisitiza kuwa hakutakuwa na mabadiliko yoyote katika mafundisho rasmi ya Kanisa Katoliki kuhusu masuala ya ndoa za jinsia moja na watu wanaojitambulisha kama transgender.



Papa huyo amesema wazi kuwa msimamo wa Kanisa bado unabaki ule ule wa muda mrefu, kwamba ndoa ni muungano kati ya mwanaume na mwanamke, na hivyo Kanisa halitabariki ndoa za jinsia moja.


Kauli hiyo inakuja wakati mjadala wa kimataifa kuhusu haki za watu wa LGBTQ+ ukiendelea kushika kasi katika jamii mbalimbali duniani 🌍

Kwa msisitizo huo mpya, Vatican inaonyesha kuendelea kushikilia misingi ya mafundisho ya jadi ya Kanisa Katoliki kuhusu ndoa na familia.


FOLLOW kukata kiu ya Habari 


#LugembeVoiceOnline

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi