Na Helima Saida
Waswahili husema mkaa bure si sawa na mwenda bure, hii inadhihirika kupitia uwepo wa kipindi maalumu kinachoangazia masuala mbalimbali yanayohusu Elimu mahusiano na mapenzi kikilenga vijana zaidi.
Siku kadhaa zilizopita mara baada ya Meneja wa kitengo cha Rasilimali Watu (Human Resource Manager) ndugu Timotheo SD kukamilisha ile kazi ya uchambuzi wa kabumbu ndani ya Chuo kikuu Cha Dar Es Salaam sasa amekuja na kitu kingine kabisa ambacho hakika kimegusa kwa kiasi kikubwa maisha ya vijana kwa asilimia kubwa zaidi.
Ndg Timotheo SD maarufu kama Timmy the Creative wakishirikiana na mwanadada kutoka Taasisi ya Chuo Life hivi karibuni wameanzisha program yao maalum inayoenda mjini YouTube kupitia THE REAL VOICE 255 ikifahamika kama the INSIDE TALK ambapo mapokezi yamekuwa makubwa kiasi kwamba Lugembe Media tumekuwa tukifuatilia ni kwa namna gani kipindi hiko kinakubalika na wadau wana maoni yapi na jana LUGEMBE MEDIA tulipokea mrejesho kutoka kwa wafuatiliaji wawili ambapo walianza kwa kuwapongeza Timmy na Chicca kwa kugusa maisha halisi ya vijana kwani yapo mambo ambayo vijana hufanya pasipo kujua mwisho wake ni upi.
Pili waliongeza kuwa kupitia kipindi hicbo wanapata wasaa mzuri zaidi kutoa madukuduk yao na kuyafikisha kwa wengine ili kuwafundisha kuwa ukiacha curaha kuna upande wa pili wa hiyo furaha na hii inasaidia kwa walio single kufahamu namna wanaweza kuhandle changamoto za mahisiano yao watakapoingia katika mahusiano.
Ahsante kwa muda wako usisahau kumwalika jirani aka-like na kusubscribe Lugembe Voice