Wataalamu
mbalimbali wamefasili dhana ya Uchapishaji na Uchapaji kama ifuatavyo.
Kwa
mujibu wa Mulokozi (1993) Uchapishaji ni mbinu ya usambazaji wa habari, maarifa
au fasihi kwa maandishi yaliyopigwa chapa au kunakiliwa katika nakala nyingi.
Tuki
(1981) wanafasili Uchapishaji kuwa ni kazi ya kushughulika na utoaji wa vitabu
na kuvitawanya kwa kuviuza kwa watu. Pia Wanafasili dhana ya Uchapaji kuwa ni
kazi ya kutumia mashine au mitambo kutolea maandishi, mfano gazeti au vitabu.
Pia
Ndalu na Babusa (2014) wanasema Uchapishaji ni hali ya kutoa maandishi kwa
kutumia mtambo. Wanafasili dhana ya Uchapaji kuwa ni hali ya utoaji wa nakala
za maandishi kwa kutumia mitambo maalumu.
Pia
kwa mujibu wa kamusi teule ya Kiswahili wanafasili maana ya Unenaji kuwa ni
jinsi ya kusema maneno.
Historia
ya Uchapishaji na Uchapaji.
Itakumbukwa
kuwa Uandishi ulivumbuliwa Sumeria na
Misri ambapo Wasumeria walitumia Cuneiform na Wamisri walitumia michoro ya
picha ambayo baadae ilichanganywa na ishara za kifonetiki. Baadae taaluma hii
ilienea mpaka china na kuanza kuandika kwa michoro na kuenea mashariki ya mbali
kama Japani na Korea. Mnamo karne ya 11 Nchi za mashariki ya mbali China,
Korea, na Japan ziligundua uchapaji wa maandishi yanayohamishika.
Mwaka
1440, Johannes Guternberg wa Ujerumani
aligundua namna ya kutengeneza herufi na michoro kwa kutumia taipu za
metali zinazohamishika, ugunduzi ambao haukuwa tofauti sana na ule wa Wachina
ila ulienea haraka zaidi na kutumika kwa mafanikio katika biashara. Ugunduzi
wake ulisababisha utengenezaji wa herufi zinazohamishika na ambazo zingeweza
kutumika kuchapa vitabu vingi.
Yafuatayo
ni mambo yaliyochochea kuanzishwa kwa Uchapishaji na Uchapaji kutoka katika
unenaji.
Dini.
Uwepo
wa dini mbalimbali ulichochea kuibuka kwa uchapishaji na uchapaji. Mfano, Kitabu
cha dini ya Buddha kiitwacho The Diamond
Sutra ambacho kwa mujibu wa mtandao wa livescience kimehifadhiwa katika
makumbusho ya mjini London, Uingereza kinaeleza namna mahubiri na maandishi ya
dini ya Buddha ya zamani yalivyohifadhiwa. Kitabu hiki kiliandikwa mwaka 868
wakati wa enzi ya mtawala wa China aliyeitwa Tang na kilitengenezwa kwa mbao
ngumu na mtindo huu ulitumika pia Korea na Japan tangu karne ya 8. Kitabu hiki kiliandika mambo ya kidini
na mikataba mbalimbali pamoja na historia.Hata wakati wa Gutenberg karne ya 14
na 15 masuala ya dini yalichochea kwani hata yeye mwenyewe aliweza kuchapisha
mamia ya Biblia zilizoitwa Biblia za Gutenberg ambazo zilikuwa na mistari
isiyozidi 40 kwa kila sura.
Shughuli
za kiuchumi.
Kwa
mujibu wa Joseph Needhem (1945) anaeleza kuwa Mnamo karne ya 11 mkulima mdogo
raia wa China aliyeitwa Pi Sheng alitumia mbao kutengeneza hati hamishiki ambazo
alitumia kuwapasha wakulima wenzake habari mbalimbali zinazohusu kilimo.
Kupitia ugunduzi huo alimtumia mwanasayansi aliyeitwa Shen Kuo kuzalisha mamia
ya nakala ya hati hamishiki.Vilevile serikali ya China walitumia madini ya
shaba kutengeneza na kuandika maandishi katika sarafu katika karne ya 14 na 15.
Maendeleo
ya Sayansi na Teknolojia.
Kwa
mujibu wa Mulokozi (1993) anafafanua kuwa Kadri siku zilivyozidi kwenda
wanadamu walijighulisha kuboresha maisha yao ikiwemo kuboresha kazi za
uchapaji. Ugunduzi wa maandishi ya shaba huko China na Korea karne ya 14 na
mwanzoni mwa karne ya 15 ulirahisisha kazi ya Uchapaji hali iliyopelekea
kuchapwa kwa nakala nyingi zaidi kazi na vitabu ambavyo vilisambazwa na hivyo
kupelekea uchapaji kuendelea.
Kuendelea
kwa Mifumo ya Kiutawala na Kisiasa.
Kwa
mujibu wa Shen kuo anaelezea kuwa ikumbukwe kuwa tangu enzi na enzi maisha ya
binadamu yamekuwa yakipitia mifumo tofauti tofauti hasa katika masuala ya
kiutawala. Masuala ya kiutawala yalikuwa yameendelea zaidi katika nchi za Ulaya
na Asia.Watawala hawa walitumia Uchapishaji ili kupata nakala nyingi ambazo
zingewasaidia katika kueneza itikadi zao au hata taarifa mbalimbali za
kiutawala. Kwa mfano; katikati mwa karne ya 15 iligundulika michoro iliyochorwa
juu ya mbao katika Bonde la Rhine mpakani mwa Ufaransa na Italia. Wataalamu
wanadai kuwa michoro hii ilionyesha mipaka ya nchi hizo na maeneo mengine ya
Iberia Peninsula na ilitumiwa na
serikali ya Ufaransa kutatua migogoro ya
ardhi. Vilevile wakati wa utawala wa Kijamaa wa Yuan nchini China karne ya 14,
ugunduzi wa Pi Sheng uliisaidia sana serikali kwa kueneza sera zake na hata
mipango yake ilienezwa kwa watu kupitia uchapishaji wa hati hamishiki ya mbao.
Maendeleo
ya Elimu.
Kwa
mujibu wa Parlemo (2014) anafafanua kuwa tangu kugunduliwa kwa maandishi yapata
miaka zaidi ya 5000 iliyopita, wasomi mbalimbali walijishughulisha na namna
ambavyo wangeweza kuyahifadhi maarifa yao na hata pengine kuyahamishia kwa watu
wengine. Jambo hili lilipelekea kwa mbinu ya Uchapaji na Uchapishaji yapata
miaka zaidi ya 500 huko Ulaya mashariki na Asia ya mashariki ya mbali. Kwa
mfano; miaka zaidi ya 2000 katika nchi ya Ugiriki kuliibuka Wasomi na
Wanafalsafa mbalimbalia kama Aristotle na Plato ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni
kuwafundisha watu katika jamii zao juu falsafa mbalimbali za Ulimwengu na
jamii kwa ujumla kupitia maandishi na
michoro katika mbao ngumu kwa kuandika na wino. Hata hivyo suala la elimu
linatajwa kuendelea tangu karne ya 12 katika nchi za Ulaya ambapo vyuo
mbalimbali ikiwemo kile cha Paris nchini Ufaransa walichapisha taarifa za
kitaaluma katika vitambaa vigumu vilivyoandikwa kwa rangi.
Pamoja
na kuwepo kwa sababu nyingi zilizopelekea kuanzishwa kwa Uchapaji na Uchapishaji,
Uchapishaji na Uchapaji ulipitia nyakati tofauti tofauti na katika maendeleo ya
ngazi tofauti tofauti. Mwanamama Elizabeth Palermo katika kitabu chake cha Who invented Printing Press anasema
uchapashaji na uchapaji ulianza yapata miaka 600 kabla ya kuzaliwa kwa Johhanes
Gutenberg. Elizabeth anaendelea kutueleza kuwa, watu mbalimbali hasa viongozi
wa dini walitumia mbao ngumu kuchora michoro na maneno mbalimbali yahusuyo dini
katika mbao hizo kama ilivyoelezwa katika hoja iliyotangulia ya namna dini
ilivyochochea uchapishaji.
Kwa
maana hiyo zipo hatua na vipindi
mbalimbali ambavyo vilipitiwa katika maendeleo ya Uchapishaji na Uchapaji. Zifuatazo
ni baadhi ya hatua hizo:
Mwaka
50,000 Kabla ya Kristo.
Katika
historia ya Uchapaji na Uchapishaji ni muhimu kukumbuka kuwa uchapishaji
ulianza kwa binadamu kuchora michoro mbalimbali ambayo pengine iliwakilisha
sauti au matendo fulani. Katika kipindi hiki jamii nyingi hasa za Kiafrika
ziliishi maisha ya Kijima na jamii nyingi zilitegemea uwindaji. Hoja hii inathibika
kwa uwepo wa michoro mbalimbali katika sehemu za Afrika kama Irangi Kondoa
Afrika mashariki na Bonde la Rhine Ulaya ya kati. Katika michoro ya mapangoni
huko Irangi, kunaonekana michoro inayoonyesha watu wakiwinda wanyama ambayo
imechora katika mwamba mgumu na pia michoro iliyopo Rhine ilionyesha mipaka ya
ardhi kwa wakati huo.
Mwaka
3400-3200 Kabla ya Kristo.
Katika
mwaka wa 3400 Kabla ya Kristo nchi ya Misri ilkwishakuwa na hati ambayo
waliweza kuiandika. Katika mwaka huu Wamisri walitumia michoro ya picha
iliyoitwa Hierographics wakati maandishi hasa yalivumbuliwa huko Mesopotamia
(Iraq) ambapo baadhi vyanzo vya habari vinadai kuwa maandishi haya yalikuwa ni
kwa ajili ya kuonyesha mipaka yake na Syria, Iraq na nchi za jirani mpaka karne
ya 4 baada ya Kristo. Pia inasadikika kuwa hata jina “Mesopotamia” lina maana
ya “Ardhi” kwa Kigiriki. Baadhi ya Wataalamu wa historia kama Finkelstein 1962
anadai kuwa tangu mwaka wa 5300 Kabla ya Kristo tayari Mesopotamia walikuwa
katika kipindi cha zama za chuma na walitumia zaidi shaba kuunda maandishi yao
ukiachilia mbali suala la kuchonga sanamu mbalimbali.
Mwaka
wa 3200 K.K - 1088 B.K
Katika
kipindi hiki sehemu nyingi ulimwenguni hasa nchi za Ulaya na Asia zilikuwa
zimepiga hatua kubwa katika Uchapishaji. Katika nchi kama China tayari
kulivumbuliwa hati hamishiki ambazo ziliweza kupangwa katika kuandika maandishi
mbalimbali ingawa maandishi haya yaliandikwa katika vipande vya mbao lakini
tayari hawakuwa wakitumia michoro bali herufi. Shen Kuo akinukuliwa na Joseph
Needham 1954 katika kitabu chake kilichoitwa The Dream Pool Essays anadai kuwa kupitia hati hizi hamishiki
kulichapwa mamia ya nakala ambazo zilihusu kilimo na watu wakazisoma. Vilevile
nchi mbalimbali kama vile Ethiopia, Mexico, India, Misri, Syria na kwingineko
katika kipindi hiki tayari kulivumbuliwa hati ambazo ziliwekwa katika maandishi
ya kisasa yaani abjadi na picha.
Mwaka
1088 B.K - Karne ya 15 (Wakati wa
Gutenberg ).
Kama
watangulizi wake waliotangulia ambao tumewatazama hapo awali Bi Sheng, Wang
Chen, Baegun na wengine , Johannes Gutenberg alitamani kuiboresha kazi ya
Uchapishaji na Uchapaji huku akitaka kujikita zaidi katika namna ambao kazi hii
inaweza kufanyika kwa umaridadi na wakati mfupi zaidi ingawa alijua kuwa
kunahitaji umuhimu mkubwa. Wanahistoria wanamwelezea Gutenberg kuwa ni kijana
aliyetokea katika familia ya wahunzi wa vifaa vya dhahabu na chuma katika mji
mdogo wa Strasbourg nchini Ujerumani. Yeye aliandelea na mfumo wa watangulizi
wake wa kutumia mbao ingawa alizikata katika vipande vidogo vidogo kulingana na
herufi na alama mbalimbali za uandishi.
Baadaye
Gutenberg alikata vipande vya chuma na kuzichonga herufi moja moja na
kutengeneza hati hamishiki. Baada ya kufanikiwa katika hili, aliweza kugundua
kuwa kumbe angeweza kutengeneza wino kwa kutumia rangi na mafuta tofauti na
watangulizi wake wakina Bi Sheng, Shen Kuo na wengine ambao walitumia maji
pamoja na rangi.
Kadri
siku zilivyokwenda Gutenberg alifikiri kuboresha kazi yake ya uchapishaji, safari
hii alikuja na wazo la kuziunganisha zile herufi za chuma katika mstari mmoja
kwa kupitia skuruu na kuwa kama sentensi kabla kugundua kuwa angeweza kupaka
wino juu ya zile herufi katika mstari kisha akachuku karatasi na kuibandika kwa
juu na kuitoa ikiwa ina maandishi yanayosomeka.
Kwa
ujumla kutokana na hatua hizi zote mpaka wakati wa Gutenberg, jamii zilipata
uzoefu na namna ya kutengeneza maandishi na kufanya kazi ya Uchapaji na
Uchapishaji kwa ufanisi. Ingawa ugunduzi wa Gutenberg ulionekena kama ni hatua kubwa
zaidi kuwahi kufikiwa, Uchapaji huu wa Gutenberg haukupendwa kutumiwa na
mataifa mengi ya Ulaya na Asia. Hii ilitokona na sababu kuu tatu.
Kwanza,
kwa wakati huo jamii za Ulaya na Asia zilikuwa na hati nyingi hivyo kutumia
mbinu ya Gutenberg kungetumia muda mrefu kuandaa vitabu na machapisho.
Pili,
kwa kuwa aina hii ya Uchapishaji ilitumia chuma, jamii na watu wa nchi hizi
waliogopa kutumia gharama. Tatu, kwa kuwa Uchapishaji huu
ulitumia nguvu za mikono, nguvu nyingi ilitumika pia vitabu viliuzwa ghali
sana. Hali hii ilipelekea jamii nyingi kupendelea zaidi mfumo ule wa awali wa
kuandika juu ya mbao na vitambaa.
MAREJELEO
Finkelstein, D.
(1962). Social Justice in the Ancient
World. Amazon: Greenwood Publishing
Group.
Mulokozi, M. M.
(1993). Fasihi, Uandishi na Uchapishaji.
Dar es salaam: Dar es salaam
University Press.
Ndalu E. A.
& Babusa H. (2014). Kamusi teule ya
Kiswahili. Kilele cha Lugha. Kenya:
East African Educational
Publishers Ltd.
Palermo, E.
(2014). Who Inveted Printing Press.
Washington: Washington University Press.
Shen Kuo.
(1088). The Dream Pool Essays. China:
Sichuan People’s Publishing House 2008.
TUKI. ( 1981). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es
Salaam: Oxford University Press.