Watu ni stori na stori ni watu. Tunaweza kujifunza mengi tunapopata bahati ya kukutana na watu mbalimbali na hii ndio maana halisi ya msamiati watu katika maisha.
Imehaririwa na Sadick Msigwa ( UDSM)
Soma kisa hiki kisha itapendeza zaidi kama utaniandikia maoni yako juu ya kijana huyu
"Ipo hivi mimi ni kijana wa miaka 28 sasa.
Nilipokua chuo mwaka 2018 nikisomea course ya IT nilibahatika kupata mdada ambaye niliishi nae kama mchumba na kumpa mahitaji yote na tulikubaliana tuzae.
Basi nikampa kweli ujauzito huku nikimhudumia kwa kila kitu bila wazazi wangu kujua na hakuwahi kukosa kitu alichohitaji kwangu japo sikuwahi kuomba msaada kwa mtu, ila niliendeleza life langu kwa mishe zangu za kitaani(kwa wanaoelewa IT huwa hatukosi mishe za hapa na pale).
Ilipofika mwezi mmoja na nusu kabla ya binti kujifungua alisema anaenda jifungulia nyumbani.
Sikumkataza kwa vile na mimi niliona sitaweza ghaili masomo nisaidie malezi. Hivyo nikamruhusu aende na kumpatia vitu vyote muhimu alivyohitaji kwa ajili ya safari na mambo mengine.
Basi yule binti akaanza safari mpaka akafika. Siku zikakata mpaka akajifungua.
Mwisho wa siku nakuja pata habari kuwa alienda kujifungua kwa mwanaume wake aliyempa ujauzito. Nilishtuka ikanibidi nifunge safari mpaka alipo kwenda kumuona, cha ajabu mtoto nusu anafanana na mimi nusu anafanana na huyo anayesemekana ni baba yake.
Sikuelewa. Nilipoomba nikapime DNA na mtoto nilikataliwa.
Ikanibidi niwaache na maisha yao nikapiga moyo konde nikaanza safari ya matumaini. Walibahatika kuoana pia baada ya mtoto kuzaliwa.
Maisha yameenda na cha ajabu yule binti ananisumbua mpaka hii leo anahitaji turudiane huku akidai kuwa mtoto ni wangu licha ya kuwa aliwahi nikana kuwa sio mtoto wangu hapo awali. Kiukwel nampenda sana ila tatizo ni kuwa ameshaolewa na hajaachwa kwa talaka ila wamepishana kauli tu na mumewe tangu mwaka jana mwezi wa saba. Najiuliza nirudiane nae? na itakuaje kwa mtoto? haitaleta utata zaidi?".
Anonymous, #WatuNiStory
Pakua App yetu leo
Uyo tema kabisa harud kwa mumewe kwa nin aseme uongo
JibuFutaKatika maisha unapaswa kuchukulia mambo katika Hali zote mbili yaani kupata na kukosa, pia Kama ilivyo kwangu hutokea kwako pia. Kikubwa Kama unampenda jitahidi ujue sababu ya kupishana kwa mme wake wa awali kabla ya kufanya taratibu za kumrejesha, kwani Sheria humfunga yeyote. Yeye kutaka mrudiane sio Jambo la kuzingatia kwani mihemko ya mda mfupi hupelekea maamuzi ya haraka na yasiyo sahihi, hivyo ng'amua sababu ya kupishana kwako, na kujua wametengana kwa namna gani kwa kuzingatia mustakabali wa usalama wako kabla haujamrejesha.
JibuFutaIla kwamba nimehariri Mimi, mhhh inahitajika maombi maana makosa ya kiuandishi Ni mengi Sana na lugha iliyotumika haijawa specialized Aina ya rejesta uliyoichagua
JibuFuta