Binti Msahaulifu Full Episodes

 Tinner 1: SIMULIZI: BINTI MSAHAULIFU.         MTUNZI: TINNER ROBER.                        SEHEMU: 01. 0746638941 Whtsup.


ANZA NAYO.


Katika Jumba kubwa pembezoni na mji mkubwa uliokuwa umezungukwa na kisiwa, Kulionekana Kuna majadiliano Kati ya pande mbili Huku wakizidi kuvutana Huku na kule.


Mama mmoja wa makamo alikuwa akimfokea Mmewe Huku akimulaumu Sana.

   "" Baba Ndalu!! Kwanini umeamua Kumsaidia huyu binti!! Unajua familia yake anakotokea!! Ni Bora ungemuacha akasaidiwa na wengine isije ikawa Ni Jini umelisogeza Ndani!!!"


Muda huo huo Akiwa anaendelea kuongea, Kuna vijana watatu walifika wakimuulizia binti Huyo!! Walitoa picha nakuwapatia Kama watakuwa wanamjua Huyo Binti.


Mama huyu Alimtizama Mmewe baadae ya kuona anasita kuongea Ilibidi amuulize.

   "" Baba Ndalu!! Mbona husemi kitu!!?"


 Baadae Mmewe aliamua kuzungumza.

  "" Vijana wangu Huyo mtu mnaemtafuta naona hatumfahamu, labda mjaribu kuulizia sehemu nyingine!! Kwani Binti Huyo kafanyaje!?"


  "" Tungempata ndio tungewaambia kwanini tunamtafuta kwa juhudi!!?"


Wale vijana waliondoka nakuwaacha mke na mme wakiendelea kujadili.

  "" Kwanini unamficha Binti huyu!! Si ungewaambia tu, kuwa tupo nae?? Ayaa kamhudumie mpaka azinduke Mimi simo kwenye kesi za kujitakia!!"


  "" Mkewangu acha kuwa na roho Mbaya kiasi hicho!! Naona Binti huyu anahitaji msaada kwanza!! Acha apone harafu tutamhoji ujio wake huku!!'


Baba Ndalu aliingia Ndani kumuangalia Binti yule!! Alinyanyua simu yake nakupiga kwa Doctor mmoja akihitaji msaada. Baadae Doctor alifika nakumcheki afya yake aligundua Kuna kitu kizito alipigwa kichwani ndio kikamfanya azimie.


Alitumia jitihada zake kunusuru Maisha ya Binti huyo, Baadae alimuita Baba Ndalu Huku akionekana kuwa na huzuni Sana.

   "" Baba Ndalu!! Naona khari ya mgonjwa sio Nzuri!! Inatakiwa apelekwe hospital kwa uchunguzi Zaidi naona Kuna damu imegandamia kwenye ubongo hivyo inatakiwa akafanyiwe upasuaji!!


Jitihada zikaendelea wakawa wamefanikiwa kumpeleka hospital! Alienda kuwekwa moja kwa moja kwenye chuma Cha ICU kwa uchunguzi Zaidi.


Huku Nyumbani kwa Mama Ndalu!! Aliingia kwenye Chumba kimoja katika nyumba yake! Kilikuwa Ni Chumba Cha Siri, Kulionekana Ni Chumba Cha muhimu Sana, Chumba hiki kilikuwa kimejaa nguo za mtoto wa kike mwenye umri Kama wa miaka ishirini. Mama huyu alisogea ukutani Kisha alichukua picha kubwa iliyokuwa mezani Kisha alianza kuitizama Huku akibubunjikwa na Machozi.

  "" I'm sorry my Son!! Naimani Huku uliko Bado wanikumbuka vizuri Mimi mama yako!! Bado Nakupenda Sana japo nimiaka  nane sijakuona kwenye mboni ya macho yangu ila naamini upo salama!!


Wakati akiendelea kulia alisikia Sauti ya mmewake akifokea.

  "" Mama Ndalu!! Nishakwambia Hupaswi kuingia kwenye Chumba hiki!! Muda wote umekuwa ukimkumbuka huyu mtoto tayari ameshatangulia mbele za haki, Hupaswi kulia tenaa!!"


   "" Hapana!! Najua Mwanangu Bado anaishi!! Kama amekufa kwanini hutaki nichome nguo zake!! Hivi Ni wapi ulimpeleka Mwanangu!!!?" Mama alizidi kufoka Huku akimlalamikia Mmewe.


Huku hospital Juhudi ziliiendelea kunusuru Maisha ya Binti, Baadae alitolewa nakupelekwa kwenye Chumba Cha kawaida, fahamu zilianza kurejea taratibu, baadae alifungua macho yake Huku akiangaza Huku na kule.


Kuna Dokta alifika pale kumtizama Baada ya Kumuona alishituka Sana, alitoka nje kumuita mganga mkuu wakawa wamekuja moja kwa moja Kumuona Mgonjwa. Daktari alimchukua kipimo Tena baadae Aliona khari yake inaendelea vizuri Ilibidi akae chini kwanza angalau azungumze nae kwanzaaa alimuuliza;


   "" Vipi waendeleaje!!!?! Kichwa hakiumi teenaa!!? Na Vipi waitwa Nani jina lako!!?"


Binti alibaki kaduwaa Huku akizidi kumtizama Dokta, Lakini kwa Dokta aliona Bado khari yake haipo sawa aliamua kumuacha kwanza Kisha alimpatia dawa za maumivu Huku akimuachia maelekezo Nurse aliyekuwa ameingia zamu.

   "" Naomba muangalie mgonjwa huyu kwa umakini Sana!! Chochote kile kitatokea Naomba uniambie!!"


Baadae Aliondoka na kupiga simu moja kwa moja kwa Baba Ndalu,

  "" Hello mheshimiwa!! Naona mgonjwa wetu anaendelea vizuri kwasasa anajitambua  ila hawezi kuongea!!"


   "" Sawaa!! Vizuri Sana Naomba endelea kumhudumia, hakikisha anazidi kuimalika harafu akiongea kitu chochote niambie!! Tumia njia yoyote Ili mradi aongee!! Nahisi hawezi kuongea hebu jaribu kumpatia daftari na kalamu harafu muulize maswali huenda anaweza kukujibu kwa njia ya kuandika.


  "" Sawaa mheshimiwa nitafanya hivyoo!!!"


Majira ya Mchana Dokta alirudi Tena Wodini Kisha alimchukua Binti nakumpeleka Kwenye Chumba Cha Siri Huku Akiwa amembebea chakula!! Alifika na kumpatia chakula Huku akijaribu kumlisha, baada ya kuona Kashiba alianzisha sitori za Hapa na pale mpaka zikamfanya Binti huyo atabasamu, baadae alimpatia Daftari na kalamu Huku akimuuliza maswali.


  "" Wewe Ni Binti mzuri Sana ila Sasa sijakufahamu Majina yako!! Waweza niandikia Majina yako kamili!!?""


Binti alichukua kalamu Huku Akimtizama kwa makini Daktari baadae aliandika Majina yake kwenye Daftari, muda huo Daktari alikuwa akifatisha kila herusi ya jina libaloandwikwa baadae Alirudia kwa kulisoma " TINNAH"


   "" Kwahiyo Wewe Ni Tinnah!!?'


   "" Aliitikia kwa kichwa Ishara ya kukubali!!"


Baadae Doctor alimuuliza Tena!!

 "" Kwani Nyumbani kwenu Ni wapi!!? Au Kuna kitu chochote wakumbuka Huko Nyuma!! Yaani ulikuwa ukiishi wapi na kwanini upo Hapa.


Binti Alitikisa kichwa Ishara ya kwamba hakumbuki chochote, isipokuwa anachokumbuka Ni jina lake TU.


Doctor alitoka nje kupiga simu kwa Baba Ndalu kumpatia information mpya, majibu yalitoka kwa Baba Ndalu.

   "" Okay!! Hakikisha asiwe anakutania!! Kama hakumbuki Basi iwe kweli!!"


Majira ya usiku Tinnah alikuwa kapumnzika Lakini alianza kupata njonzi za kutisha zilimpelekea kichwa kuuma Sana baadae alianza kulia mpaka kukawafanya wale wagonjwa wengine washituke na kubaki wakimuangalia jinsi anavyoweweseka Usingizini.


Mgonjwa mmoja alionekana kuwa na unafuu ilibidi ashuke kwenda kumuita Doctor wa zamu baadae Alikuja Kumuona.

   "" Vipi Tinnah!! Cha mno Nini!!?


Tinnah Alibaki akishikilia kichwa chake Huku akizidi kuugulia maumivu. Doctor alibaki Akimtizama kwa khari aliyokuwa nayo Aliondoka Huku akiongea pekee.

  "" Hii serious case!! 


Alichukua file la mgonjwa Nakuanza kulipitia angalau ajue chanzo Cha ugonjwa kwanza. Mgonjwa anaitwa Tinnah!! Alifanyiwa upasuaji.. inaonekana alipigwa kichwani na kitu kizito kilichosababisha damu kuganda kichwani ikabidi afanyiwe upasuaji... Mchana alifanyiwa checkup inaonekana Hana uwezo wa kuzungumza ila anaweza kuandika na hii imesababishwa na shida ya upasuaji uliofanyika ikampelekea kushidwa kuzungumza.... Uwezo wake wa kuzungumza utakuwa Unarudi taratibu endapo ataweza kumbuka Kumbukumbu za Nyuma!!!"


Doctor baada ya kumaliza kusoma file na mgonjwa tayari alikuwa amepata majibu. " Inaonekana tatizo libalomsumbua Ni Kumbukumbu zinazokuja na kupotea Ndio zinamfanya apate maumivu makali. Alichukua Dawa ya maumivu na kwenda kumchoma baadae alitulia.


Ilikuwa Ni majira ya Asubuhi Huku Nyumbani kwa Mama Ndalu, alikuwa ameamka Huku akifanya usafi wa nguo, baadae mmewe alipita akitoka ndani kuelekea Nje, Mama Ndalu ilibidi asitishe kufua kwanza nakubaki akimwangalia mmewe, baadae alimuuliza.

   "" Lakini Baba Ndalu!! Maisha haya tutaishi mpaka lini!!? Tazama tuna kila kitu ila Nyumba yetu Haina furaha!! Muda wote twaishi Mimi na Wewe kwenye jengo kubwa namna hii!! Hakuna hata mtu wakuongea nae nikuombee basi niletee hata mdada wa kazi angalau niwe naishi nae!! Au kachukue Basi mtoto kwenye kituo Cha kulelea Watoto yatima angalau azibe pengo la Ndalu.


Mmewe aliishia kumtizama baadae Alimjibu Huku akiondoka.

  "" Una uhakika utapata furaha ukipata mtu wa kuishi nae!? Okay nitalifikilia. Kisha alipanda gari na kuondoka.


   ******


Yapata wiki mbili kupita leo Tinnah alikuwa akihamishwa hospital na kupelekwa kwenye Nyumba iliyokuwa mbali kidogo na mji, Wakati maandalizi yakiendelea kulionekana Kuna mtu mmoja alikuwa akifatilia kila hatua iliyokuwa ikiendelea pale, muda wote alikuwa na laptop yake ilimsaidia kunote kila kitu kilichokuwa kikiendelea.


Baadae Utaratibu mzima ulikamilika wa Tinnah kuondolewa pale, ilikuwa Ni majira ya Usiku Ndio ratiba ilipagwa ifanyike vile.


Yule mtu alizidi kufatilia mpaka akajua majira ya kuondoka pale!! Aliamua kufatilia utaratibu wa usafiri watakaotumia aliona Kuna gari ilikuwa imepakiwa Nje!! Alifanya utaratibu wa kutafuta ufunguo Kuna kazi alitaka aifanye.


Aliangaza Huku na kule baadae Aliona gari hiyo imeegeshwa vibaya!! Alitafuta Mlinzi mmoja aliyekuwa akilinda pale!! Alipiga stori nae baadae alimwomba apumnzike kwanza kwa kuekit Ana mgonjwa pale muda mrefu wamekuwa wakifukuzwa na kulala Nje hivyo muda huo Kama atautumia kupumzika itakuwa Ni vizuri.


Mlinzi alimuamini Sana ilibidi amkabizi funguo baadae yeye aliendelea kuzunguka zunguka akiimalisha Ulinzi. Kijana Yule baada ya kuingia Ndani alichukua sale za walinzi zilizokuwa humo Kisha alivaa na kutoka Nje. Alichoamua Ni kumfata moja kwa moja Doctor aliyekuwa akihusika kumhudumia Tinnah.

   "" Doctor kwema Lakini!!!! Naona Gari yako umepaki vibaya!! Waweza ilekebisha ukaipaki vizuri!!!"


Muda huo Doctor alikuwa Busy Sana!! Ilibidi ampatie funguo ya Gari Huku akimuelekeza aipaki vizuri.


Kijana Yule alichukua funguo Kisha Alielekea kwenye gari, Alichofanya Ni kufungua nakuingia kwenye gari Kisha alitegesha Camera vizuri, sehemu iliyokuwa imejificha kwa kutizama Haraka huwezi kuiona!! Alimaliza kufunga Camera Kisha alipaki gari vizuri na kurudisha ufunguo.


Baadae Alibadilisha mavazi na kuvaa nguo zake Huku Akiwa amebeba begi lake mgongoni, Ile anatoka nje alikutana na mabinti wawili walipishana nao Huku Akiwa busy na Mambo yake.


Mabinti wale walibaki wakimtizama mpaka anaishilia, baadae walianza kumujadili.

   "" Huyu Mkaka inaonekana Ni mgeni hapa naona hii itakuwa ni siku ya tatu Kumuona!! Ila naona yupo busy Kweli na laptop yake!!! Ila anajifanya yupo serious Sana!! Mpaka anachukiza japo Ni HB Kweli!!"


   "" Umeanzaaa mambo yako Rose ya kuchunguza chunguza kila wakaka wageni wanaokuja!! Harafu kwani yupo word namba Ngapi au Ni Daktari bigwa yupo kwenye jengo lao!!!"


   "" Sijui Bhana!!! Kesho tutamfatilia angalau tumjue Zaidi.


   .... Itaendeleaa....


Usikose Sehemu ya 02. 


UNAIPATA YOTE KWA KIASI CHA TSHS 2000/=

[3/26, 16:43] Tinner 1: SIMULIZI: BINTI MSAHAULIFU.                                             MTUNZI: TINNER ROBER.                        SEHEMU: 02. 0746638941 Whtsup.


ANZA NAYO.


Huku kwa Tinnah alifikishwa kwenye jumba kubwa lililokuwa limezungushiwa fence kubwa pia kulikuwa na Ulinzi mkubwa!! 


Baadae Doctor Alikuwa akimuelekeza mazingira ya pale, Mara kidogo walitokea watoto watatu went umri was miaka saba, walikuja pale kumsalimia Tinnah. Mtoto mmoja alimuita Doctor.

   "" Doctor!! Na huyu ndie Dada yetu ulikuwa unamsema atakuja!!?"

  "" Yaaah!! Ndio Dada yenu Ambae mtakuwa mkiishi nae kwa Sasa!!"

   "" Mbona haongei Sasa!!?""

  "" Anaumwa ila ataongea TU!!"

  "" Ila atakuwa Ni Dada mzuri!!??"

Doctor alisogea karibu Kisha alimshika kichwani Tinnah Huku akiongea nae.

  "" Naamini utakuwa sawa hii Ni familia yako kwasasa nimekukabizi jisikie uko huru muda wote!!


Tinnah aliitikia kwa Ishara ya kichwa, baadae Doctor alimpatia kaunta mbili na kalamu Kisha alimkabizi Huku akimuomba Kama atakuwa na shida yoyote Ile anaweza kuandika nakuwapatia wanzake.


Baadae aliwaita watoto waliokuwa pale, Muda huo  Tinnah Aliitwa na yeye ili aweze kuungana nao alibaki akisikiliza maelezo yaliyotolewa pale make alikuwa akisikiliza.


Baadae Aliamua kuondoka pale na kwenda kwenye bustani iliyokuwa sehemu hiyo, alikaa Huku akitizama mazingira Yale moyoni alikuwa na Mambo mengi Sana akijiuliza.

  "" Mbona Kama sikumbuki kitu!! Hawa watoto Ni wa Nani!?"


Muda kidogo Alikuja Binti mmoja mwenye umri sawa na wake, muda huo alikuwa amepatiwa information zote kuhusu Tinnah, Alifika na kumuuliza Tinnah Huku akimpatia kibegi kilichokuwa na kaunta pamoja na kalamu.

   "" Waweza tumia begi pamoja na vitu vilivyomo ili kurahisisha mawasiliano.


Tinnah Alifungua Begi Kisha alichukua kalamu nakumuandikia kwenye karatasi maandishi yaliyosomeka hivi.

  '" Kwanini mnafanya haya kwangu!!? Kuna umuhimu wa Mimi kuandika!!?'


 "" Nafanya kwaajili yako!! Naona umpweke kweli natamani tushare furaha kwa pamoja!! Niite Naomi kwanzaa!!" Harafu Wewe Ndio Tinnah!!?"


   "" Sawaa!! Una kitu wataka tuzungumze na Mimi' Tinnah Alimjibu kwa kuandika make alikuwa akisikiliza vizuri maongezi ya Naomi!!"


  "" Natamani kuzungumza mambo mengi Sana kuhusu Wewe!! Ila nikubalie kwanza umekubali niwe rafiki yako wa karibu!!?"


  "" Nimekubali.."


Naomi Alimchukua Tinnah Huku akiendelea kumzungusha mazingira ya pale. Baadae Alisitushwa na wale watoto wawili walikuja Huku wakikimbizana.

   "" Dada!!! Dada!!!' Dada Yule mwingine Anaumwa ndanii!!!'


Ilibidi watoke Haraka kwenda Kumuona Ndani!! Kwa like jengo lilikuwa kubwa Walitumia Kama robo saa kufika kwenye kill chumba, kipindi wamefikia kile chumba Naomi alimgeukia Tinnah Kisha alimwambia  amsubilie nje kwanza, baadae wale watoto waliondoka na wao Huku wakiongozana na Tinnah.


Naomi aliingia kwenye kile chumba kilionekana kuwa na Giza Sana, alichukua torch Huku akimulika ili apate Nuru. Alifika Hadi Kitandani na Kukaa Huku Akimtizama vizuri Baadae alimuita.

   "" Ndalu!!! Unaumwa Nini tena!!! Nimeambiwa unalia!!?"


Ndalu Alliinuka kisha Alimshika mkono Naomi Huku akimuuliza.

  "" Ni lini nitatoka kwenye chumba hiki!! Nifungulie leo nitoke Hapa!! Tazama imekuwa Ni Miaka nane nipo Hapa Ni lini nitatoka!!?"


Naomi Alimshika mkono huku akijaribu kumtia Moyo.

  "" Kwasasa muda wote utakuwa huru!! Naona Kuna Binti kaja!! Ila nahisi Kuna kitu ndani yake japo kwasasa simuelewi vizuri!!""


  "" Kwani Ana Nini anacho huyo Binti umeona!! Anaweza kunisaidia Mimi!!?"


  "" Sijajua vizuri ila yeye Ni Binti msahaurifu!! Hakumbuki chochote na hawezi kuzungumza kwa njia ya mdomo ila anaelewa kila kitu utakachomuuliza Lakini anajibu kwa kuandika.""


   "" Sawaa!! Mfatilie vizuri utakuwa unaniambia!! Tatizo muda mwingi hauji kuniona kwa wakati!! Ndio maana nimewatumia wale watoto Baada ya kuona wanapitapita huku!! Walisogea Hadi mlangoni wakawa wameniuliza Wewe Ni Nani nikawaambia Dada!!" Nikawaomba waje kukwambia kuwa naumwa!!;"


  "" Sasa umeanza kuzingua huoni hawa watoto watamwambia Doctor kuwa wamekuona Huku!! Kipi tunaenda kukifanya kwa Sasa!!?"


  "" Kawaonye wale watoto wasije kusema!! Watishie vikali Sana naamini hawawezi kusema!!!"


Naomi alitoka kwenye Chumba kile Kisha Alielekea kwa wale watoto aliwakuta wapo wakila. Alitazama kwa pembeni alimuona Tinnah Kasimama Huku Akiwa na Daftari lake Kuna Picha alikuwa akichora.


Naomi alimsogelea Tinnah Kisha alibaki akimtazama, Ni kitu gani anakifanya baadae alizichukua Daftari na kulisogeza karibu huku akizidi kuitazama picha baadae alimuuliza.

  "" Hi picha Ni ya Nani umechora!??"


Tinnah Alibakia kutabasamu tu, Huku Akimtizama Naomi baadae aliamua kumjibu kwa kuandika.

  "" Ndicho ninachokumbuka kwa Sasa!! Ila simkumbuki vizuri naona Ni mtu aliyekuwa upande wangu muda mwingi!!"


   "" Ni Kaka yako!?" Mara ya mwisho ulimuona wapi!?"


   "" Hospitali!!, Kuna Siku moja nilimuona kaja kuniona!! Ndio Kumbukumbu zangu ninavyoziona!!"


  "" Sawaa!! Basi endelea kukumbuka Vizuri!! Ila njoo kwanza tupate!!"


Tinnah aliwahi kumshika mkono Naomi baadae alimuandikia kikaratasi Kisha alimpatia, Naomi alikichukua Kisha alikisoma.

   "" Kwenye kile Chumba!! Ni Nani aliyekuwa mle akihitaji msaada wako!!?"


Naomi alishituka kidogo, aliamua kumjibu.

   "" Usijali siku nyingine nitakueleza, ila sio wakati huu.


  "" Wakati gani utanieleza.. kwanini isiwe Sasa!!!??"


Naomi alifanya kumkaushia Kisha alimshika mkono nakwenda nae sitting room. Waliendelea kupata chakula Lakini Tinnah alikuwa Bado Ni mtu mwenye Mawazo Sana alichukua karatasi Tena Kisha alimwandikia Naomi.

   "" Njia gani naweza itumia Kumbukumbu zangu zikarudi tena awali!!?"


   "" Ruhusu ufahamu wako uwe wazi kila ukijaribu kukumbuka achilia fikra zako zote ziwe hewani!!"

°°°°°°°°°°°°°°°°


Majira ya Usiku Tinnah alikuwa kasinzia Huku akikumbuka maneno ya Naomi yakijirudia Mara mbilimbili, Ruhusu ufahamu wako wa akili uwe wazi!! Alijaribu kuvuta Kumbukumbu Huku akifunga Macho kama ataweza kumbuka Lakini aliona Giza lenye Nyota Nyota zikiwaka kwa kubadili kila Aina ya rangi, baadae alifungua macho na kubaki akicheka mwenyewe Hapa nafanya ujinga juu ya ujinga, Anyway Sitaki tena kukumbuka.


Huku Nje kidogo na mji ule, Katika Chumba kimoja alionekana Kuna kijana alizidi kuchezea computer yake huku akizidi kuangalia location na ile Camera, baadae Alizima Computer nakubaki akizunguka Huku na kule kana kwamba Kuna kitu ameshidwa kukikamilisha.


Aliwasha Tena Computer Huku akizidi kuchezea computer yake Lakini alibaki akiongea pekee.

   "" Lazima nitafanya kwaajili yako ili uwe salama!!'


Muda kidogo Alikuja Kijana mmoja aliingia Ndani Kisha alimuuliza jamaa yake.

   "" Ni kweli Aniseth.. umekosa mwaka wakumsaudia Tinnah!!?"


   "" Nahisi wametushitukia ile Camera niliyotegesha kwenye gari!! Naona hainasi tena matukio!! Nahisi itakuwa imetolewa!!"


   "" Sasa tunafanyaje!! Ila nakuamini Wewe kwenye maswala ya Network upo vizuri!! Kama utashidwa Wewe tayari Tinnah utampoteza..!! Au tusitishe Jambo hili.


  "" Acha utani Leonard!!! Mambo ya serious usichukulie utani!!! Kumpata kwetu Tinnah mambo yetu yatafanikiwa!! Hapa kesho naomba twende moja kwa moja tukafatilie tukiwa huko...


   """ Hebu sogea kidogo kwa computer, Hivi unaona Ulinzi uliopo hapa, Walinzi wapo wakutosha unataka tukafie huko.""


   "" Haaaaa!!! Ama kweli hapa inatakiwa akili ifanye kazi, muda wote tucheze na mtandao vizuri tujue tunamsaidiaje Tinnah!!"


Siku iliyofuata Aniseth na Leonard walikuwa wakielekea kwenye Jengo alilokuwa Tinnah, Uchunguzi uliendelea kufanyika muda kidogo waliona gari ikipaki pale, alionekana Ni Baba Ndalu pamoja na Doctor wakishuka.


Anseth aliamua kutafuta upenyo Baada ya kuona Walinzi wakizubaa aliingia taratibu akijificha kwenye gari, baadae alifanikiwa kuingia kwenye jumba Hilo kazi aliyoifanya nikuzima camera zote ili zisimulike, Kisha alichukua simu yake nakumpigia Leonard Huku akimpatia information ya mambo yote alimsihi awashe Computer yake Kisha aliunganisha mawasiliano yote yatakayoendelea pale.


Alitafuta sehemu nakukaa Huku akizidi kuchunguza vizuri, baadae Alimuona Tinnah akiwa anapita sehemu yake, aliamua kumnyapia taratibu Kisha Alimvuta na kumziba mdomo Huku akibaki kumtizama baadae alimuuliza.

  "" Unanikumbuka!!!?"


Tinnah Alibakia Akimtizama TU, Ishara ya kuwa hamkumbuki, Aniseth Alirudia Tena kumuuliza.

   "" Tinnah!! Wanikumbuka?? Mbona huongei!!!!?"


Ilibidi Tinnah Amuandikie Chini, "" Sikukumbuki kwani Wewe Nani!!?"


Aniseth Alisoma maandishi Yale Kisha alimtizama Tinnah usoni, Kisha Alinyanyua mkono wake nakumshika Tinnah Rip's za mdomo Huku Akiwa haamini kwanza alimuuliza.

  "" Ni kweli huwezi kuzungumza tenaa!?"


 Tinnah aliitikia kwa Ishara ya kichwa kuwa hawezi zungumza.


Aniseth Ilibidi amuachie Kisha alimruhusu Aende ila alimsihi asimwambie mtu yeyote Kama kamuona mtu ila alimsihi kumsaidia. 


Baadae Aniseth alizidi kupandisha juu huku Akiwa Bado anawaza mambo mengi Sana.

  "" Tinnah... Hivi Ni kweli haongei tenaaa!!? Nini kimemkuta Binti Huyu!!?"


Kutokana na Stress za hapa na pale alipamia ua lilokuwa limetengenezwa kwa Shaba likawa limeanguka chini na kupasuka, kelele ziliwasitua Walinzi wakawa wamekimbia moja kwa moja kuangalia kitu gani kimeanguka. Mlinzi mmoja alitoa Sauti akisema Huyo huyo mkamateni, Huku wakizidi kumuandama Aniseth kwenye jumba Hilo.


   .... Itaendelea....

Usikose Sehemu ya 03.


Nini kipo Nyuma ya pazia. Kwanini Tinnah alifatiliwa Sana, na Je Aniseth atakuwa mwema? Na kwanini Wanamuwekea Ulinzi mkubwa, Na vipi kuhusu Ndalu kipi kinaendelea Kati yake na Babake!!?"




















Tinner 1: SIMULIZI: BINTI MSAHAULIFU.               MTUNZI: TINNER ROBER.                        SEHEMU: 03. 0746638941 Whtsup.


ANZA NAYO.


Kutokana na Stress za hapa na pale alipamia UA lilokuwa limetengenezwa kwa Shaba likawa limeanguka chini na kupasuka, kelele ziliwasitua Walinzi wakawa wamekimbia moja kwa moja kuangalia kitu gani kimeanguka. Mlinzi mmoja alitoa Sauti akisema Huyo huyo mkamateni, Huku wakizidi kumuandama Aniseth kwenye jumba Hilo. ENDELEA...

Aniseth Alizidi kukimbia Huku akijaribu kutetea maisha yake, bahati nzuri Kuna mtu alitokea chap akawa amemvuta nakumuingiza Chumbani.


Walinzi walizidi kumtafuta Lakini hawakufanikiwa baadae walirudisha majibu kwa Doctor kuwa wamemkosa!! Aliwaamuru watumie Camera kumpata Lakini walipotezana waligundua Camera zilikuwa hazinasi matukio muda ule Ilibidi wakae chini wakijadili kwa kina.


Upande wa Doctor alikuwa amekaa na Baba Ndalu Ilibidi kila mtu afikilie kwa makini ilikuwaje mtu aweze kuingia nakuzima Camera itakuwa Ni mtu mwenye uwezo Sana wa kutumia Mtandao. Lakini Baba Ndalu Alitoa hoja.

  "" Inaonekana mtu huyu anatufahamu vizuri huenda kila kitu kilichokuwa kikiendelea hapo nyuma Anafahamu!! Ila sijajua kwanini alikuwa anafanya Hivi kipi anachohitaji kwetu!!!"


   """ Ooh!! Umewaweza vizuri Sana Hapa inabididi tuanze kufatilia pindi Tinnah akiwa hospital wording,' ngoja nimcheki Doctor Isaac atuangalizie Kwenye Camera.


Doctor alipiga simu kwa Doctor Isaac Kisha alimpa maelekezo Baadae Aliingia kwenye Computer Huku akifatilia location ya Chumba kimoja ndipo wanagundua. Baada ya siku tatu Tinnah kufikishwa hospital Kuna mtu Aliingia akiwa amefunika uso wake na Muda huo Aliingia Kama Doctor Huku Akiwa amevaa sale ya kidokta, Mtu huyu alionekana kuingia Huku akijaribu kukwepa Camera japo Camera ilifanikiwa kumnasa, Alifika Kitandani kwa Tinnah nakuchukua Dawa furani akawa amepaka mikono ili kuondoa ushahidi. Kisha alimshika usoni Tinnah Lakini alionekana Ni mtu mwenye huzuni Sana Baada ya Kumuona Tinnah kafugwa Bandage kichwa kizima baadae Aliondoka.


Baba Ndalu alimkatisha kwa kumuuliza.

  "" Ngoja kwanza nikuulize"!! Muda huo kaenda kumtizama Tinnah, Je Alikuwa akijitambua!! Au hakuweza Kumuona yeye huyo mtu!!?".


   "" Ngoja nivute Sura yake kwanza!! Inaonekana Tinnah alikuwa amelala na Muda huo Hakuwa na fahamu kwahiyo hakumfahamu!!!"


"" Sawaa!! Ahsante kwa Ushirikiano Doctor!!"


Baadae walibaki tena wamekaa wakijadili. Inawezekana mtu huyu Ni mtu wa karibu Sana na Tinnah!! Hapa inabidi tumuulize yeye mwenyewe atupatie majibu.


Muda kidogo Alifika Naomi Huku Akiwa amebeba Vinywaji, aliweka mezani Huku akitaka kuondoka lakini Doctor alimuuliza.

   "" Vipi!! Hakuna kitu chochote kilichotokea kwa Tinnah!!? 


   ""Aaa!! Labda Kuna Picha alikuwa akiichora!! Naona ndio kitu kipya!!!"


   "" Waweza ifata...!!?"


Naomi Alileta Ile picha Kisha alimpatia.


Walianza kuifanyia kazi. " Inaonekana Ni picha ya kijana wakiume!! Inaonekana Ni kijana ambae atakuwa chini ya miaka therathini!! Inaonekana kuwa Ndio mtu ambae Ni wa karibu na Tinnah na mtu huyu huyu Alikuja pale hospital!! Na Kama amekuja Hapa inaonekana kaja kumchukua Tinnah!! Na kijana huyu sizani Kama atakuwa ametoka kwenye Jumba hili nahisi atakuwa amebanza sehemu!! Na Hapa lazima tutampata TU kikubwa Ulinzi uimalike getini make hamna njia nyingine atakayotumia kutokea, Akiruka fence lazima atapigwa short ya umeme Hapa tukasisitize Ulinzi TU.


Walimaliza majadiliano Yao wakawa wameondoka.


Huku kwa Aniseth alikuwa kwenye Chumba Cha Giza kilichokuwa kikimpatia hofu Sana Lakini kila akimtizama mtu aliyemsaidia hakumuona vizuri!! Ilibidi amumulike kwa kutumia simu yake. Baadae aligundua kuwa Ni Binti aliyemsaidia ilibidi amuulize.

  "" Wewe Ni Nani!!? Kwanini unakaa kwenye Chumba kilicho na Giza muda wote? Kwanini Wewe hapo umenisaidia mimi!!?"


   "" Una maswali mengi!!! Najua umekuja kumsaidia Yule Binti msahaurifu naomba kabla hujamsaidia Yule Binti!! Nisaidie kwanza Mimi!! Huyo Binti utamsaidia baadae!!" Ndio maana Mimi nimekusaidia Wewe kwanza kabla hujamsaidia Yule Binti!! Kwahiyo fanya kunitoa hapa angalau univushe pale getini nipite Kisha uniache na Mimi nitajua pa kwenda!!"


Aniseth Alibaki akimtizama Binti huyo, Kisha aliamua kumjibu.

   "" Ni sawa!! Umefanya vizuri kunisaidia Ila kwasasa sijui kwanini upo hapa!! Sijui ulipatwa na Nini katika maisha yako!! Ila utanisamehe siwezi kukusaidia kwasasa labda mpaka nitoke Hapa nikafanye Upelelezi ndio nitarudi kukusaidia Wewe!!! Naomba unikutanishe na Tinnah kwanza nimchukue Ila nitarudi kulipa fadhira kwa kile ulichonitendea!!!"


   "" Ndio wamaanisha Kweli huwezi nisaidia!! Ila Kama utafanikiwa kurudi naomba usisahau kurudi kwaajili yangu!! Ila kwa Majina yangu naitwa 'Ndalu' hata ukienda nenda ukifanya Upelelezi kuhusu Ndalu!!"


"" Sawa Nakuahidi!! Nitafanya hivyo!!!" Njia gani nitapita maana jengo hili Ni kubwa!!"


"" Subili kwanza!! Leo usiku naimani Binti msahaurifu atakuja kupeleleza kuhusu Chumba hiki naona anamashaka na hiki Chumba Basi akifika Ndio utaongozana nae!! Ila najua kwasasa kutakuwa kumuwekwa usalama wakutosha kwahiiyo kuwa makini!!"


Mnamo majira ya usiku Kama walivyotabili Tinnah alikuwa Chumbani kwake muda huo alikuwa kashikilia touch Huku akifikilia chakufanya.

   "" Lazima niende kwenye kile Chumba nikajue kipi kinaendelea!"


Alisimama Nakuanza kutembea Mdogo Mdogo Hadi kwenye Mlango, Alisogea nakusikilizia Lakini kulikuwa kimya make muda huo walikuwa tayari wamesikia vishindo, ikabidi wakae kimya kusikilizia.


Tinnah Alikuwa akifikilia kitu gani atumie kuingia kwenye Chumba Hicho, Lakini akili ilimtuma atumie Sauti ya Naomi ili aingie kwenye Chumba Hicho. Ile anataka kuita tu Alisitushwa na Sauti ya Naomi akimuita na Muda huo alikuwa kafika pale.


   "" Tinnah!! Kipi unakifanya hapa!! Naomba tuondoke Haraka! Alimchukua nakuondoka nae.


Huku kwa Aniseth Alibaki akimtizama Ndalu baadae alimuuliza.

  "" Kipi tunaenda kukifanya!!?' Nani aliyemchukua Tinnah tenaa!!?""


  "" Kaa kimya!! Muda huu atarudi, na akirudi naomba  ukakae kwenye kolido hakikisha asisitukie Kama uko Hapa!! Mimi nitakueleza Hadi kwenye Chumba Cha Tinnah ukamsaidie!!"


Muda huo huo Naomi Aliingia Kisha alikaa Kitandani ili aongee na Ndalu.

  '" Huyu Binti msahaurifu sijui anafanya Upelelezi ganii!! Nimemkuta yupo mlangoni anataka kuingia Huku!! Harafu Kuna kijana kaingia hapa na yupo kwenye jengo hili inaonekana kaja kumtafuta huyu Binti.""


    "" Hawezi kukamatwa Kweli!!? Make Baba si mtu wa mchezo mchezo!!"


"" Daaah!! Namuonea Huruma!! Akikamatwa hapa sizani kama atatoka salama!! Na inaonekana bado yupo ndani ya Jengo hili!!"


"" Kwahiyo akipatikana itakuwaje!!? 


"" Hata akitaka kuondoka itakuwa hatari make kila Sehemu Camera zimetegeshwa ili kumpata mtu huyu!! Kwa umakini alioutumia labda ajaribu tena!!"


"" Kwahiyo Vipi Tinnah!! Tunamsaidiaje kwasasa!! Upo radhi kumuacha aondoke na mtu huyo!!?"


"" Hapana!! Tinnah nimewaza Kuna namna Nataka tumtumie katika jengo hili hivyo bora azidi bakia kwanza!! Mpka kufikia akatoke hapa!! Kuna vitu atakuwa ametutengenezea'' Wao wamtumie na sisi tutamtumia kivyovyote vile!!"


"" Utanishilikisha Sasa!! Kila hatua Lakini Ni kheri!!?"


"" Kikubwa usalama wa maisha yako!! Wewe ukitoka salama!! Tinnah atakuwa na faida gani kwako? Okay uwe na usiku mwemaaa!!"


Naomi Aliondoka Huku akimuacha Ndalu akifikilia maneno yake Lakini asielewe Ni mbinu gani anataka kuitumia. Upande wa Aniseth na yeye alisikia yote ilibidi asogee nakumkaba Ndalu.

   "" Kumbe nyie Ni wauaji!!? Ni kitu gani mnae plan mwataka kumuangamiza Binti wa Watu!! Nasema niache nikamsaidie Tinnah kwasasa!!"


Aniseth Alitoka pale Nakuanza kutafuta Chumba ambacho atakuwepo Tinnah, Ila aliamua kutembea kwa Tahadhari ili Camera zisimnase aliamua kutafuta Setting nzima ilipo Huku akizidi kufatilia Nyaya zote zinapoelekea baadae zilimufikisha kwenye Chumba kimoja aliona Ni Mlango uliokuwa umefungua kwa kufuri Ilibidi atafute namna yoyote ili aweze kufungua mlango huo!! 


Bahati nzuri alibahatika kupata Chuma baadae alirudi kuvunja kufuri akawa ameingia Ndanii, alikuta Kuna Aina ya kila mitambo ilibidi atazame switch ya kuzima Camera kwanza!! Baadae Alizima nakuchukua mkanda uliokuwa ukinasa matukio Hadi Nje!! Kisha alichukua simu yake nakumpigia Leonard ili amshirikishe mipango iliyoendelea wakawa wamekubaliana kuwa atamsubili nje na usafiri ili akitoka tu Safari ianze. Baada ya hapo aliamua kutoka kwenye Chumba Hicho huku akitafuta Chumba Cha Tinnah.


Kwa bahati nzuri alimuona Tinnah kakaa kwa nje Huku Akiwa na Daftari lake na kalamu, ilibidi asogee taratibu pasipo yeye kujua kisha alianza kumtizama kipi anaandika. Muda huo Tinnah alikuwa akichora ramani ya Jengo Zima huenda na yeye alikuwa na plan yakutoroka pale.


Lakini Aniseth alifikilia kitu Kama ramani ya Jengo Zima Tinnah analo kwake atakuwa Ni msaada tosha wakutoka kwenye jengo hilo!! Aliweka plan endapo taa zitazima Walinzi wote watatoka getini Nakuja kutafuta chanzo Cha kuwa na Giza wao Ndio wataitumia njia hiyo kutoka.


Ilibidi amsogelee Tinnah Kisha alimziba mdomo!! Baadae alimuachia nakumruhusu amtamtazame.

  "" Tinnah najua nishajua kitu unachoplan Ila Nataka tutoke hapa mapema ninachoomba Ni saport yako make hapa nitaenda kuzima taa zote!! Kwakuwa Wewe ushakuwa mwenyeji hapa naamini utakuwa ukiongoza Njia!!


Tinnah aliitikia kwa ishara' kuwa yupo tayari!!"


Aniseth Alirudi Hadi kwenye kile Chumba kilichokuwa na Network Kisha alifanya kuzima baadae Alirudi hadi alipomucha Tinnah. Plan yake ilienda sawa Walinzi wote walikimbilia ndani wakawa Wameacha geti wazi wakawa wamefanikiwa kutoka nje kiulaini.


Muda huo walimkuta Leonard akiwa mlangoni kawasubili na usafili wake ilibidi wapande nakuondoka sehemu haraka sehemu hiyo..


   ,,, Itaendeleaa....


Usikose Sehemu ya 04.


Like comments and Share 🤝🙏.




















 Tinner 1: SIMULIZI: BINTI MSAHAULIFU.          MTUNZI: TINNER ROBER.                        SEHEMU: 04. 0746638941 Whtsup.


ANZA NAYO.


Aniseth Alirudi Hadi kwenye kile Chumba kilichokuwa na Network Kisha alifanya kuzima baadae Alirudi hadi alipomucha Tinnah. Plan yake ilienda sawa Walinzi wote walikimbilia ndani wakawa Wameacha geti wazi wakawa wamefanikiwa kutoka nje kiulaini.


Muda huo walimkuta Leonard akiwa mlangoni kawasubili na usafili wake ilibidi wapande nakuondoka haraka sehemu hiyo. ENDELEA.


Walifika Hadi kwenye jengo lililokuwa pembezoni mwa mji Kisha waliweka makazi yao. Lakini muda huo Tinnah alibaki kimya Huku akiangaza mazingira ya hapa na pale Huku wakiwa wamekaa Sebuleni, baadae alimugeukia Aniseth Kisha alimwandikia kikaratasi.

   "" Wewe ndio Aniseth!!?"


   "" Ndio!!! Umenikumbuka!!?"


   "" Alitikisa kichwa ishara hamkumbuki, baadae alimuandikia tena. "" Si Ulikuwa kwenye Lile jumba la kina Naomi!!?"


""  Ndio!! Hujakosea!!!"


Baadae Walimuandalia sehemu ya kulala, Kisha walibakia Sebuleni Wao Kama wao wakijadili.

     "" Inamaana kwamba kweli Tinnah hakumbuki!!?' Kipi tunaenda kukifanya kwasasa ilimradi Kumbukumbu zake zikarudi tena!!?" Aniseth alihoji.


"" Daaah!! Labda tumrudishe kwao!!! Huenda atakumbuka!!" Harafu"" Kwanini Lakini Aniseth Unafanya haya yote kwaajili ya Tinnah.


"" Kwaajili ya Kakangu tu! Ndio maana nafanya hivi!! Haijalishi Kakangu alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha ila aliniambia nimlindie huyu mwanamke!!"


"" Hivi wazani Tinnah!' fahamu zake zikimrudia huoni wewe itakuwa ngumu kumuelewesha!!"


"" Nitamuelewesha!! Najua atanielewa TU.


Asubuhi kulipambazuka Tinnah Aliamka Huku akisaidiana na wafanyakazi waliokuwa pale baadae alimuona Aniseth alikuwa akipita pita Ilibidi amfuate. Aniseth na yeye asimame baadae alimgeukia Tinnah Huku akimuuliza.

   "" Vipi wataka kuongea na Mimi'!!


   "" Aliitikia kwa ishara' ya kichwa.


   "" Sawaa Lakini baadae nimalizie kazi moja nataka niifanye Kwanza!!"


Huku kwenye Jumba la Doctor muda wote kulikuwa na msako wa hapa na pale kumtafuta Tinnah pamoja na Aniseth. 


Upande wa hospital waliendelea kumtafuta Aniseth kwenye CCTV camera. Baadae Alifika Rose kwa Doctor aliyekuwa akishilikiana na Baba Ndalu.

   "" Samahani Dr. Najua Wewe Ndio umetoa time table yakuingia zamu!! Kuna mkaka mmoja tulimuona  ile siku nilikuwa Mimi na Jamila kwa bahati Mbaya aliangusha picha!! Make nimemtafuta kweli nataka nimrudishie picha yake sijui yupo word namba ngapi!!?''


Doctor alichukua ile picha Kisha aliiangalia Lakini aliona Ni picha ya muda kidogo, wapo watu watatu yaani Tinnah na Kaka wawili waliofanana Sana!! Baadae aliiweka ile picha Kisha alimuuliza Rose.

  "" Kijana huyo yukoje kwanii!!?"


  "" Ni mrefu mwembamba!! Alikuwa kavaa gwanda jeupe la udokta, mkononi alishikilia laptop, sura yake aliificha kwa proova nyeusi pia alivaa miwani.


   " Sawaa waweza iacha ataikuta Ofsini!!"


Rose aliondoka pale Huku akimuacha Doctor kwenye tafakuri nzito Sana. Alinyanyua simu yake akawa amempigia simu Baba Ndalu kumpatia information alizozipata kwa Rose!! Baada ya mawasiliano Yao kuisha walipeana maelekezo sehemu ya kukutana wazungumze.


Huku kwa Tinnah jioni alitoka na Aniseth angalau wazungumze. Walikaa sehemu Kisha waliagiza juisi Huku sitori ziliiendelea. Muda huo Tinnah alikuwa kaandaa daftari lake Huku akihitaji kujua vitu vingi kwa Aniseth.


Aniseth muda huo alikuwa na maswali mengi ya kujiuliza kila akizidi mtizama Tinnah' inaonekana Kuna mambo mengi Sana alikuwa kamficha baadae alimuuliza.

  "" Vipi Tinnah!! Kuna kitu wataka kuniuliza make naona upo serious Sana!! Okay uliza!!?"


Tinnah Alichukua kalamu take na daftari lake Kisha alimwandikia.

  "" Wewe Ndio Albert au Ndie Aniseth!!?"


Aniseth Alishituka kwanza Kisha alichukua juice nakumimina kwenye Glass Kisha alikunywa, muda wote Tinnah alikuwa akimtizama alichana karatasi ndogo Kisha alimpatia Tena Aniseth Huku Akiwa ameandika. "" Wewe ndie Albert!!?"


Aniseth Ilibidi akae vizuri Kisha Alimtizama Tinnah uso kwa uso Kisha Alimjibu.

   """ Kumbukumbu zako zimerejea!!?"


   "" Simkumbuki hataa!! Ila kwenye ufahamu wangu nakuwa naona sura yako IPO Mara mbilimbili harafu Kuna jina jingine linakuja Albert!! Nilitaka unifafanulie vizuri Aniseth na Albert Ndio kina Nani!!?" Alimaliza kuandika Kisha alimpatia.


   "" Hapana huenda Kuna Kumbukumbu zinakuijia ila Albert Ndio Aniseth!!" Naona kwasasa unawaza mbali Sana.. endelea kukumbuka Vivyohivyo naimani muda si mrefu ufahamu wako utarudi!!"


   "" Nina Swali Tena....!!


   "" Niandikie...!!


   "" Lini utaenda kumtoa Ndalu kwenye Jumba lile? Maisha yake yapo hatarini kwa Sasa!! Fanya kitu kumuondoa pale!!"


"" Sawaa Nakuahidi nitafanya hivyo!! Ila Nawewe niahidi siku tukipotezana hakikisha utarudi kuniulizia kwenye jumba hili make kwasasa maisha yetu yapo hatarini Sana!!"


"" Sawaa muokoe kwanza Ndalu!!"


Maongezi Yao yaliendelea baadae Aniseth alimurudisha Tinnah Nyumbani. Majira ya Jioni Aniseth na Leonard walichukua usafiri kurudi kwenye Jumba kumkomboa Ndalu.


Wakati wamefika karibu na jengo Hilo waliona Kuna gari inatoka pale, Ilibidi waanze kuifatilia taratibu!! Iliwafikisha Hadi kwenye jengo Kubwa lilionekana Kuna Ulinzi wa kutosha Ilibidi wakae sehemu I'll kutizama kitu kinachoendelea,,, 


Walizidi kuangalia kwa makini Ghafura waliona Kuna mtu alikuwa amebebelewa Huku Kafunikwa nguo nyeupe, Mwishoni kabisa alionekana Naomi akishuka kwenye gari Huku akilia, Sauti ya Mwisho iliyosikika Ni Ndalu umeniacha mapema mnooo!! Huku ikifatiwa na kilio kikubwa.


Mlinzi mmoja Alikuja kumchukua Naomi Huku akijaribu kumnyamazisha!! Kilio hicho kilipelekea hata Aniseth na Leonard washituke Sana!!

   "" Daaah!! Tayari Ndalu katangulia.... Maskini nitamwambia Nini Tinnah.


Leonard alimshika mkono rafiki yake Kisha Alimuomba watoke sehemu hiyoo..

   "" Tuondoke hapa!! Tupo hatarini Sana, tutaenda kuongea mbele ya Safari!!"


Aniseth alisimama kwa Unyonge Sana, walielekea kwenye gari Huku kila mtu Akiwa haamini kitu kilichotokea.


   ++++++


Ilikuwa Ni mwaka mmoja Baada ya kutokea Tukio la Ndalu kupoteza maisha. Leo Katika Gereza kuu la Tanzania kulionekana baadhi ya Wafungwa walikuwa wakiachiliwa kuwa huru Tena.


Kuna mfugwa mmoja Baada ya kuwa huru alionekana akilia Sana mpaka baadhi ya washikaji wake walimwendea Huku wakimuuliza.

  "" Oyoo!!! Mbona una umama mwingi Sana au hukutaka kuwa huru!!? Shauli yako watakurudisha tena usote Ndani.


Mfugwa huyo Alinyanyua kichwa chake Huku akitaka kumjibu.

   "" Ni kheri Wewe!! Unatoka Huku ukipokelewa na Ndugu zako Tena kwa usafiri private!! Je, mimi?  Ni Nani anayeweza kuniona wa thamani Sana katika Dunia hi!! Sikufanya Tukio kwa kukusudia ila ilinilazimu iwe hivyo!!"


Jamaa aliamua kumpotezea make kila mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake, Ilibidi ampigepige bega Kama kumtia nguvu Kisha alimwachia maneno kadhaa.

   "" Kosa sio kosa ila kosa ni kurudia kosa!! Wewe kampane kutafuta maisha, hakikisha taswira iliyopo katika Jamiii unaibadilisha upya na iwe Kama ya Mwanzo.


Katika Wafungwa haohao alionekana kijana mmoja aliekuwa kapanda hewani, yeye muda wote alikuwa Ni mtu wakutafuna big G Huku akiambatanisha masihara mengi, pia alikuwa Ni mtu wakucheka na wenzake muda wote. 


Mkuu wa Gereza pamoja na wafanyakazi wenzake, walimuita Kisha alimpatia mkono Huku akimtakia kila la kheri kwenye maisha mapya ya kijamii tena!! Alimuita Mara mbilimbili.

   "" Albert!! Albert!! Niwakati wako mpya wakwenda kuanza maisha upya Tena!! Ila uwe unakuja kutusalimia angalau Mara moja moja uwepo wako tunajivunia!! Ulikuwa Ni mtu mzuri Sana!!"


Albert Aliishia kutabasamu Kama kawaida yake Huku akiendelea kutafuna big g!! 

  "" Kila Weekend nitakuwa naja kuwasalimia jamaa zangu!! Ila na nyie mpunguze kutupiga na hizo rungu!!"


Walicheka wote kwa furaha Huku wakimsindikiza kwa macho, huku kila mtu akitathimini yaliyo ya Moyoni kwakee..

  "" Ni kijana mzuri Sana.. sizani Kama hata Hilo kosa alifanya ila alikubali kutumikia kifungo bila ridhaa yake!! Ni baadhi ya maneno ya mkuu wa Gereza aliyatafakari.


Huku Getini Albert alikuwa akiwasalimia wenzake Huku akijaribu kuwaaga, baadae Alitoka Hadi getini Kisha Alisimama nakusoma maneno yalioandikwa pale " GEREZA KUU LA WAFUNGWA" Huku akiyarudia maneno Yale Yale marambili.


Wakati yupo pale alisitushwa na Sauti ikimuita,, Ilibidi ageuke kumtizama!! Alikuwa Ni Askari alikuwa Ni rafiki yake wa karibu Sana, Alifika pale nakumpatia kimfuko kidogo Kisha alimwambia.

   "" Ondoka mazingira haya!! Unaweza kukamatwa tena!! Nimekupatia kiasi kidogo Cha fedha kitakachokusaidia hapo baadae..!!"


Albert Alichukua usafiri wa hiace maana Gereza lilikuwa mbali kidogo na mji, Alipita mjini kununua Nguo kwa baadhi ya zile pesa alizopewa Kisha alichukua Hotel moja kupumzika siku hiyo. Huku akitafakali mambo Mia kwa sekunde moja.

"" Kuna wakati Unatamani kufanya kitu ila nafsi inakuuma tenaa..  Lakini sikutumikia kifungo bure pasipo kuwa na kosa lazima nitalipa hata muda niliopoteza haijalishi Ni sekunde lazima watalipa!!"



.... Itaendelea....


Usikose Sehemu ya 05.


Like, comments and Share.

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi