Mtunzi: Jenipha Namfua
Story: Maumivu ya Moyo
Episode: I
MAUMIVU YA MOYO
Moyo umebeba mambo mengi Sana , yaweza kuwa mazuri au mabaya hakuna mtu yoyote anayefahamu moyo wa mwenzie umebeba nini!? Kila mtu ana historia yake kwenye maisha haya ,,,usimhikimu mtu Bila kufahamu
Ni asubuhi njema kabisa ndege angani wanafurahia na kushangilia,anga la bluu huku mawingu yakipishana kama magari yanavyopishana kwenye barabara ndogo. Jemima alivuta hewa nzuri ya asubuhi hoyo huku akifurahia,jua la asubuhi lenye vitamini c hakuwa na hofu wala shida yoyote kwenye maisha yake aliyafurahia maisha anayoishi, anayaona ni maisha yenye amani na Furaha Sana aliyapenda maisha ya ndoa yake hakuwaza chichote zaidi ya kumwaza mme wake kipenzi. Erick Anderson ni kijana wa miaka 28 ni mwanaume mwenye muonekano mzuri Sana kila mwanamke atakaye kutana nae lazima avutiwe na muonekano wake maana alikuwa na sura nyembamba na rangi nyeusi inayoteleza kama mtoto mdogo aliyetoka kuzaliwa ,weusi wa sura yake ulifanya aonekane maridadi zaidi,alikuwa anamiliki kampuni ya baba yake inayoitwa shughulika na usambazaji wa bidhaa mbalimbali nchini na nje ya nchi.Ilikuwa kampuni kubwa Sana ambayo kila siku inaingiza mamilioni ya pesa ,kwahiyo maisha yao yalikuwa bora Sana kila mtu alikuwa anawaonea wivu kutokana na maisha wanaoishi........
Kipi kinafuata....usikose