Ikawe Heri 9 na 10

 SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER .                            MTUNZI: TINNER ROBER.                          SEHEMU: 09. 0746638941 (Wtsp).


ANZA NAYO.


Aliamua kuwasha music kwa kuachia sauti ya Chini huku akizidi kusikiliza Mdogo Mdogo Hadi kukapambazuka. ENDELEA.


Kulikucha asubuhi Junior aliamka asubuhi na kuandaa chai kisha aliweka mezani na kuelekea bafuni kuoga!! Lunnah Ndio anaamka alishangaa Baada ya kuona chai iko mezani!! Aliamka na kuanza kumtafuta Junior!!!

  "" Wewe Junior hauendi kazini kwako bado TU unajizungusha hapa kwangu!! Unataka kuniletea balaa!!??""


Muda kidogo Junior ndio alikuwa anatoka bafuni na taulo lake alikuwa akifuta nywele zake!! Mkononi alishikilia simu!!

  "" Oyoo!! Walalama Nini Lakini Okay!! My Duffer!! Anapiga simu!! Sijui Ndio Nani huyo au Ndio mmeo??""


   "" Wewe let's bhana unauliza Nini?? Simu ilikata akaamua kumpigia Tena simu.

 "" Hello My Duffer!! Sorry bhana simu ilikuwa chumbani!! Vipi umefika wapi??""


   "" Njiani bhana nipo nakuja!! Kufikia jioni nitakuwa hapo unajua uniandalie Nini??""


   """ Sijui bhana!! But nitafanya Kama Wewe unavopenda si samaki mkavu na ndizi?? Au ushabadili!!!??""


    """ Waooo!!! Naona umo mule mule unachezea!! Okay mida basi!!!""


Lunnah akawa amekata simu!! Junior muda wote alikuwa busy akila Lakini maongezi yote aliyasikia!!

  "" Lunnah!! Huyo Ndio mmeo?! Okay naondoka ila jioni nitakuja kumsalimia angalau tujuane!! Okay see you later!!""


    "" Sasa unaondoka na Koti lako unamuachia Nani??""


"" Kwani ile Siku nilikupatia koti likiwa bichi!!?? Okay usiku naliijia!! Nikute umepass harafu uniwekee Yale marashi yako!!!"" Alichukua pikipiki yake na kuondoka.


"" Yaani Junior sijui mtu gani tu, et uijie usiku Wallah ukirudi sitafungua mlango!! Utakaa hapo mpaka ukome!! Tena bahati Nzuri leo weekend hamna Kazi ngoja nimtafute Duffer wangu!!"'


Majira ya jioni Lunnah alikuwa kakaa Huku akizidi kuandaa chakula Cha usiku, Mara simu yake iliita na kumfanya aachane na shughuri zake apokee simu!!

  "" Najua huyu Ni Imlany tu!! Lakini mbona no ngeni!! Hello Duffer!! Umefika wapi??""


  "" Muone wazani mimi Ndio Duffer wake!! Naona Ni kiasi gani mmezoeana kwa sauti uliyoniongelesha tu inazihilisha mahusiano Ndani yake!! Okay isave no yangu!!!""


  "" Sasa Nani kakupatia namba yangu!!??


  "" Leo usiku uliposinzia na simu yako ilisinzia!!??""


   "" Ayaa!!! Mme wangu anakuja Sitaki usumbufu!! Kupata namba yangu isiwe tabu ya Wewe kunikwaza sawa!!""


  ""Okay!! Mapishi mengi ila usinisahau na Mimi usiku nakuja kula na kuchukua Koti langu!!!""


Lunnah Aliamua kumkatia simu Huku akizidi kulalama!!

  "" Mtu msumbufu!! Hadi anakera!!! Sijui Junior kazaliwa wapi huko!! Mtu msumbufu kila Mara!!""


Kidogo alisikia Get linagogwa. 

"" Mungu wangu!! Missed call hapa!! Hata sijasikia huyu Junior ananichanganya mno!! Huyu Ni Imlany kafika.


Alitoka na kuelekea Hadi Getting na kufungua mlango alishangaa kumuona Imlany akiwa anaingia na mfanyakazi wake mmoja wa kampuni yake alikuwa kamleta.

  "" Waooo!! Imlany hatimae umefika Tena!! Unajua nilikamisi Kia's gani??


   "" Sawa!! Weka mizigo Kwanza Ndani!! Tutaongea bhana!!! Ngoja niongee na mfanyakazi wako Kwanza make kaja kunipokea na gari la kampuni!!""


Muda kidogo Imlany alimaliza kuongea na yule mfanyakazi Kisha aliingia Ndani na kumkuta Lunnah akiandaa chakula!!

  "" Duffer!! Hujaivisha tu bado?? Na Njaa bhana!! Sijui Nile TU pasipo kuoga!!""

   

   "" Kaoge Bhana!! Ndio tupate kula Mimi sili na mtu anayenuka petroli!! Na bado ananuka gari gari!!"


   """ Umetosha!! Okay naoga basiiiii!!


Baadae walikaa mezani na kuendelea kula!! Mara kidogo simu ya Imlany iliita alikuwa Ni Rayna akipiga video call!!

   "" Vipi umefika salama!!! Mpatie simu Lunnah nimsalimie!!! Alifanya kumpatia.


"" Waooo Lunnah now ur so beautiful!! Okay sogea mbali kidogo niongee na Wewe!!! Nilitaka kukwambia TU Mlinde Duffer wako kumbuka kwa Sasa Ni mme wa mtu!! Kwahiiyo muepushe na mazoea ya huko na hii Kazi nakupatia Wewe!! Naomba mpelekee simu!!""


"" Nambie Rayna!! Mnanisema na Lunnah?? Why asogee mbali ili muongee!!?? Aya week kesho narudi!! Na Wewe usiwe mpweke kiasi hicho sawaa!!! But Nakupenda tu!!


Huku kwa Lunnah Aliona awe Busy kula make sitori za wanandoa hazikumhusu!! Lakini simu yake ilipigiwa aliangalia aliempigia alikuwa Ni Junior!! Aliimute ile simu na kuifunika kioo kiwe chini. Junior aliamua kupiga tena simu mpaka Imlany Alimwambia apokee!!


   "" Vipi Lunnah!! Ukiwa na Mmeo Ndio hupokeiii simu!! Mpatie mmeo simu niongee nae!!""


Lunnah alishidwa amjibu Nini Alimtizama Imlany.

  '" Let's niongee na Mmeo!! Mbona waogopa hivyo!! Imlany alichukua simu nakuongea nae!!


"" Vipi jamaa!! Naona mkeo anaogopa kuongea na wewe sijui bado hajakuzoea!! Shida rafiki yangu huyu huwa kanisoea Sana mimi!! Nikusihi uwe waenda nae taratibu!! Ila usimchezee Duffer wangu!! Nitakufanya Mbaya!!!


Junior Baada ya kuhakikisha kaongea na Imlany alijawa na furaha tele."" Yaani Lunnah muongo Kweli et Mme wangu!! Kumbe Ni rafiki yake na kamsave Duffer!! Afadhari nimejua Ukweli Lunnah nitakuwa Karibu yako tu, one day utanielewa ninachokitaka kwako Ni upendo TU!!


Huku kwa Lunnah alikuwa kachukia Mbaya.

   "" Ani Duffer!! Unachukua simu tu na kuanza kuongea et Junior mme wangu Nani kakutuma!! Ukweli umeniuzi!!""


    "" Duffer nimekuuzi Wewe!! Aya Junior Mimi simjui Ndio nasikia hapa!! Kwanza naona jamaa anakupenda Kweli mpaka kunipigia simu anataka kujizihirisha tu!! Mimi Ni Nani kwako hata hivyo anaonekana Ni kijana mzuri Kweli hafu HB na nimeona gwanda hapo!! Hongera pia kwa uchaguzi!!""


  "" Utajua Wewe!; Aya Junior nmemjua juzi TU Lakini Ni pasua kichwa muda wote ananisumbua Mara aijie koti lake,,, Mara atakujaa usikuu,,,,


Imlany alijisikia vibaya na kumkuta jichooo. 

   "" Aje kulala!! Aijie koti!!!! Aje kulaaa... Okay Hongera Mimi napumnzika wapi ngoja nikuache na Junior wako!!!""


Lunnah Alimchukua Imlany na kumpeleka Hadi chumbani kwakee!!

 "" Ayaa!! Shuka hii hapo!! Usiku mwema Mimi nalala sebuleni!!""


  "" Ndio wanizihirishia kabisa, Junior anakuja kulala sebuleni na Wewe!! Tangu lini ukawa waniogopa!! Sasa hivi unacheche za upendo na mtu mwingine!! Mimi Ni Duffer wako tu siku zote!! Hebu njoo ulale!!""


   "" Duffer!! sio hivyo ushaanza kuchukia kisa simu ya Junior, ayaa!! Unajua Rayna ananichukuliaje Mimi kuwa Karibu na wewe?? Anavyonichukia na Mimi ndio Nataka niwe mbali na Wewe!!""


  "" Ayaa usiku mwema kesho wahi mapema kuamka!! Ni muda wa kazini!!""


Usiku Lunnah Aliamua kupumnzika sebuleni, Lakini alikuwa na huzuni Sana Baada ya kumuona rafiki yake kamuuzi kiss Junior ambaye hata hamuelewi muda wote anampgia kelele TU.


Kulipopambazuka aliamka asubuhi na kujiandaa na Imlany alikuwa Tayari alikuwa keshamaliza kujiandaa.


Walielekea Hadi Ofisini na kuendelea na Kazi Huku Imlany alikuwa kamkunjia Lunnah!! Lunnah na yeye alizidi kutafuta namna ya kumfanya rafiki yake awe na furaha!!


Lunnah Alitoka nje na ofisi na kurudi kabebelea bahasha yenye chakula alifika Hadi Ofisini kwa Imlany na kuweka mezani.

   '" Duffer!!  Nakupenda Sana!! Hivi unajua Ni muda gani nilikumisi!! Nilitegemea kuja kwako Ndio kutanifanya niwe na furaha Lakini imekuwa tofauti hata ahadi yetu hukumbuki kabisa, " kuwa Duffer!! Hatokubali aone chozi la Duffer wake akilia!!! Kwanini leo unataka kufanya hivi!!!""


   "" Oooh!! Nishakuumiza muda mrefu sema nilimisi kusikia ahadi za urafiki wetu Kama unakumbuka!! Basi sogea tule kwa pamoja!! Japo nilipanga tutoke out angalau nifahamu huu mji ulivyo!!""


  "" Usiku bhanaa!! Now Ni muda wakazi tutaongea baadae!!!"


Huku kwa Junior alikuwa akimpigia Lunnah simu Lakini zilikuwa hazitoki alibaki akifikilia Mambo mengi Sana aliamua kumtafuta rafiki yake na kutoka nae na kuelekea kwenye hotel moja  angalau amsaidie kimawazo!!"

   "" Anord!! Hivi na Wewe huwa inakutokea hivi!! Unajua kile kibinti ki Lunnah nakipenda Sana Lakini kinanichukia Hutaamini kwa sasa kimebrock namba zangu zote!! Mpaka hapa nimekata tamaaa kabisa Mimi naona niachane nacho TU hapa kitanisumbua mno akili!!""


   "" Tatizo na Wewe jamaaa angu huwa wakata tamaa mapema!! Huenda Binti bado hajakuelewa vizuri!! Kwani umewahi kumwambia unampenda!! Basiii siku ukimwambia wampenda akikubrock Ndio ujue Hana habari na Wewe!! Hapa anakuchukulia TU ka msumbufu hivi!! Harafu hujawahi nionesha mtu mwenyewe yupoje!!""


 Junior alizidi kutumia pombe Huku akijaribu kufuta kumbukumbu za Lunnah azizione kabisaa!!.


Huku Upande wa Lunnah na Imlany walikuwa wakielekea Hadi kwenye hotel jilani, walifika na kuagiza chakula Huku wakieendelea na sitori za hapa na pale!!


Huku kwa Anord muda wote alikuwa akiwatizama Lunnah na Imlany, Aliamua kumuasha Junior.

   "" Wewe Amka Basi nikupe mchongo wa pesa Kuna Manzi kaingia happy naona yupo na mkaka sijui Ndio boyfriend wake!!! Unajua nilikuwa namumendea yule mtoto nimtongoze kumbe anajaamaa tenaa!! Siku moja nilienda kuchukua mkopo pale kwenye kampuni yake alionekana kuwa Ni mcheshi Kweli! Oyaa Muone Basi kwanza alivyo Mrembo wewe acha kulala!!!""


Junior kutokana na wenge la pombe Aligeuza shingo amtizame mtu anayezungumziwa pale.

  "" Mbonaa kafanana na Lunnah!! Kwani Wewe wamjua??!""


   "" Nishakwambia namjua!!! Tena Ni mteja katika kampuni Yao!!!""


Lunnah hakuwa na habari kabisa!! Alimuaga Imlany kuwa anaenda uwani. Baada ya kubaki pekee muda wote alikuwa akiitizama meza jilani make tangu wafike pale jicho lilikuwa kwao!! Aliamua kuwafuata Kwanza.

   "" Oyoo!! Mbonaa jicho muda wote lipo kwetu au mnapanga baadae mtuibie!! Nitaita policy hapa wawakamate!!"


Anord aliamua asizue mengi make aliona hata akiita police wao Ndio watawazuia!!  Hakutaka kuonesha Kazi Yao!!

   "" Sio hivyo!! Huyo Dada Kuna siku nilifika ofsini kwake kimaongezi zaidi!! Hapa nilikuwa namuonesha rafiki yangu siku moja afike na yeye apate huduma!! So nice hivyo TU Kaka!!!""


Imlany alisogea Karibu na kumtizama Junior. Lakini aliingiwa na hofu kidogo na kuamua kuondoka, lakini kwa Anord na yeye alimuita Junior jina lake alitaka waondoke.


Huku kwa Lunnah Ndio Alikuwa anaingia lakini kwa bahati Mbaya alipamiana na Junior, Muda huohuo Imlany na yeye alikuwa akiwatizama jinsi walivyoondoka!! 

  "" Hawa wanataka kumfanya Nini Tena Duffer wangu!! Aliamua kusogea na kumchukua Lunnah Kisha walikaa na kuendelea kula.


Lakini kwa Lunnah alikuwa Tayari kamuona Junior na kuamua kuvunga tangu muda wote wafike!! Alifanya hivyo ili kumfanya Junior asichukie tenaa!!!!.


   ,,,,,, Itaendelea,,,,,,,,,

Usikose Sehemu ya 10.


Nini Hatima ya mkasa huu Kati ya Junior na Lunnah!! Navipi kuhusu Imlany na Rayna kwa Lunnah???

SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER .                            MTUNZI: TINNER ROBER.                          SEHEMU: 10. 0746638941 (Wtsp).


ANZA NAYO.


Walifika Hadi Nyumbani, Huku Imlany alikuwa busy akifikilia mengi Sana aliamua kumuita Lunnah!! I'll wazungumze ratiba ya Kazi.

  "" Lunnah!! Naona utendaji Kazi wako upo vizuri!! Zaidi zidi kupambana!! Harafu Nina kitu kizuri kwako!! Kilichonileta Huku Ni pamoja na ununuzi wa Nyumba yako!! Ancle alinipigia simu nikuletee hati ya Nyumba pia kwenye hili kampuni kwasasa utakuwa Ni Meneja Wewe Ndio utawaongoza wote waliopo hapa watakuwa chini yako!!""

 

   "" Kwanini Sasa inakuwa hivyo!! Mbonaa Ni mapema mno!! Harafu Nyumba Mimi sijataka mninunulie kwani Mimi nitakuwa nakaa Huku Miaka yote?? Au Ndio mmenihamishia mazima!!??""


   "" Duffer!! Ni Jambo jema hata hivyo Mimi binafsi nimefurahi Baada ya kuona Ancle anakujari Wewe!! Cha Mwisho Kadi yako ya harusi hi hapa!!!""


Lunnah Alichukua ile Kadi na kuanza kuisoma taratibu, Alimaliza kuisoma na kuirudisha mezani!! Lakini alibadilika kidogo Baada ya kuisoma.

   "" Okay!! Hongera Duffer kwa hatua, Ila naumia et!!!""


   "" Waumia tenaa!! Hupendi Duffer wako nipate jiko!!? Acha roho mbayaa!!""


"" Wewe wasema!! Ila nilivyokuzoea na ukioa itakuwa urafiki wetu unachuja taratibu!! Sioni Kama tutakuwa twatoka out!! Nacheka na Wewe muda wote but IKAWE KHERI MY DUFFER!!""


"" Najua Duffer wangu!! Nikiasi gani unaumia hata ulipokuwa wasoma Kadi nimeona maumivu yako, uliyokuwa nayo moyoni!! But sitakuacha kamwee na sitataka kuona unakuwa mnyonge kiasi hicho!! kuoa kwangu kusinitenganishe Mimi na Duffer wangu!!""


Lunnah machozi yalianza kumtiririka ilibidi amkumbatie Imlany ili kuufariji moyo wake!! Kwa Imlany na yeye aliamua kumpa saport na ukiangalia na yeye tayari alikuwa na cheche za upendo Ndani yake wakawa wamekutana wote Japo Walikuwa hawajawekana wazi juu ya upendo wao Ni zaidi ya Urafiki.


Matani ya hapa na pale yaliendelea Sehemu hiyo!! Imlany alimuuliza swali la kizushi Lunnah!!

  """" Vipi kwenye harusi yangu umeniandalia zawadi gani??""


   "" Ani wataka nije niumie moyo TU!! Kuna MC wana mbwebwe Kweli!! At Bwana harusi amubebe Bi harusi!! Weweee Nani aanguke na presha siku hiyo!! Kwakweli sitakuja ila nitaleta zawadi TU!!!""


   "" Mbonaa una wivu kiasi hicho Lunnah!!?? Vipi, Unampenda Duffer wako!!??"


   "" Swali hilohilo jiulize na Wewe moyoni!! Vipi unampenda Lunnah/ Duffer wako!!? Naamini jibu ulilonalo Wewe Ndio limekufanya uniulize Mimi Hilo swali!!??""


   "" Mhuuuuuuuuuuu 🤔Maswali hayo Okay!! Nikijibu na Wewe unijibu. "" Mimi huwa nampenda Duffer wangu!! Tangu siku nyingi!! Ila sijui nilichelewa wapi ningekaoa Moja kwa Moja toka kwenye Cassino siku I'le!!!"


   """ Wewe nae Duffer kweli! Vivyo hivyo na Mimi huwa nampenda Imlany Ni mtu wa muhimu Ndio kanifanya Mimi niwe hapa!! Naona Ni zaidi ya kumpenda tu!! Ni afadhari yupo Karibu yangu!!""


  """ Ni sawa!! Ila vipi kuhusu yule MJeder mna ukaribu gani?? Make naona anateseka kwaajili yako mpaka kaenda kukunywea pombe!! Vipi na yeye Ni Duffer wako??""


  "" Wewe umemuonea wapi kwani??" Na umejuaje kuwa kaninywea pombe??""


  "" Nishajua Wewe Siku hizi wamficha Duffer wako!! Ila Mimi nakuamini Wewe!! Nasitaki uendelee kunificha, kwanini Jana hukuniambia kuwa yule kijana kwenye hotel Ndio Junior!!!??""


  "" Ningekwambia vipi wakati nikitaja habari za Junior wachukia!! Sawa tuachane nayo Ni lini nitarudi Nyumbani kwenu kwanza??""


  "" Mimi pia natamani nikae Karibu na wewe ila Ancle kakufanyia suprise Kweli yaaani Nyumba kukujengea!! Ila kesho atakuwepo hapa na Mimi nikimaliza TU kukuhamisha naondoka!! Ndio ubakie mwenyewe!!!"


  "" Nitakaa peke yangu kwelii Basi nitafutie mtu wa kukaa nae au Mdada wa Kazi!!""


 "" Wewe si utakaa na Junior!!!""


"" Umeanza!!!!""


"" Si Kweli!! Mbonaa Alikuja kukaa hapa na akalala Kama ulimlaza ukiwa umepanga sembuse kwako si atahamia kabisaa!!""


 "" Una kisilani Wewe sio bure!! Una lako Jambo!!!"


"" Now Duffer wangu, Ana Duffer wawili Junior na Imlany! Daah! Kukaa mbali na Duffer kunafanya na Wewe upate Duffer mwingine!!""


  "" Kwahiiyo na Wewe!! Una Duffer mwingine??"


  "" Kama Wewe TU ulivyompata Junior!!""


  "" Ni sawaa TU!""


Siku nyingine tenaa leo Lunnah alikuwa anahamia kwenye Nyumba yake!! Huku walikuwa wakisaidiana na Imlany kuhamisha baadhi ya vitu. Siku hiyo Ancle aliamua kuongea na Lunnah.


  "" Lunnah kwasasa haya Ndio yatakuwa Ni makazi yako!! Sitaki nije kusikia tena unamfata fata mwanangu!! Harafu nije kusikia umeleta habari za Cassino tenaa!! Nitakutoa roho!!""


  "" Ancle Sitaki Kukaa Nyumba ya masimango muda wote nitakuwa nakaa nikikuhofia Wewe!! Kwasasa Nina mshahara wangu naweza kutafuta chumba na nikaishi vizuri TU okay hapa Mimi siishii!!""


  "" Sawa Ondoka naona hautaki fadhira Wewe!!! Ukiamua Rudi Cassino huenda twasumbuka na mtu ambae keshazoea kujiuza!!""


Lunnah Alichukia na kuamua kubeba begi lake na kuondoka kurudi kwenye ile Nyumba aliyokuwa akiishi!; Huku kwa Ancle alimpgia Simu Imlany na kumpa taarifa za Lunnah kuondoka Nyumbani!!


Imlany alichukua Gari ya Mjomba wake na kuamua kumtafuta Lunnah!! Alijaribu kumtafuta kwenye simu kila muda lakini kwa Lunnah alikuwa Tayari kazima simu yake aliangaza Huku na kule lakini wapi, Aliamua arudi Sehemu aliyokuwa akiishi mwanzo ndipo anashangaa kumkuta Lunnah kaweka begi lake pembeni Huku kajikunyata kwa kibalaza analia!!


Alifika pale nakuchukua begi na kuweka kwenye gari Kisha alimrudia Lunnah na kumpakia kwenye gari na kuelekea kwenye hotel moja na kuchukua chumba Cha kupumnzika!!! Aliamua azungumze na Lunnah kwanza;

  "" Duffer!! Nini kinakufanya ushidwe kukaa kwenye ile Nyumba!! Kipi hujafurahishwa nayo!! Au Wewe na Ancle Kuna shidaa??""


  "" Ni sawa!! Mimi Malaya najiuza Cassino!! Huenda ningebaki kule ningekuwa na furaha!! Siku ile nakwambia niache kazi kwanini ulikataa nisiache kazi hapa ningekuwa nishazoea!! Leo naacha kazi rasmi kabisa Nataka niwe na business zangu nikushukuru TU kwa kunifadhiri!!""


  "" Shida Nini Mpaka unaamua hivyo!! Wewe na Ancle naona hampatani tangu siku ile kafika Nyumbani ile umemuona tu ulianza kutetemeka Shida Nini Duffer!!??"" 


   "" Sisitahili kukaa kwenu Ndio Shida harafu Mimi mtu wa Cassino!! Muda mwingine nawaza kwanini shangazi aliamua kunileta kwenye Cassino nikae hapo!! Nahisi kwake Ndio lilikuwa nichaguo sahihi!! Hata kama Alikuwa na madeni alitaka alipwe!! Najua  hakunufaika chochote kile tangu unisaidie Wewe!!, umefanya Deni la Shangazi lizidi kuwa kubwa!! Kwasasa narudi Cassino!!!""


 Imlany alipata hasira nakuanza kumfokea Lunnah!!

 "" Duffer!! Kweli nimechoka tena nimechoka hayo yote nimefanya kukusaidia Wewe ili uishi vizuri!! Vipi Kama ungeharibiwa usichana wako na yule Mbaba leo ingekuwaje!! Huoni TU nilikusaidia!! "sawa!! Up to you!! U can Do!!"" Imlany aliamua kuondoka na kumuacha Lunnah chumbani!.


Kesho yake Lunnah Aliandaa mizigo yake hakutaka kupingana na maamuzi yake aliyoyapanga Ndio aliamua kuyatimiza, Aliamka Asubuhi na kuelekea stand na kurudi Moja kwa Moja hadi kwenye Cassino!!


Lunnah Alifika na kupokelewa na baadhi ya wahudumu wa pale!! Rafiki yake Recho alimuona na kumfuata Kisha aliamua wakae faragha waongee.

  "" Lunnah!! Kumbe hii kazi unaipenda!! Muda ule ulikuwa ukilia kumbe Ni kuigiza inaonekana hii biashara ulikuwa umeizoea!!! Hongera pia na unaonekana Mwanamke mpambanaji Sana watu twatamani kurudi ila Wewe umerudi! Na hapa Madam alivyokuwa anakutafuta sijui TU itakuwaje!! Siku yenyewe umetoweka hapa tulikula kichapo kisichoelezeka!! Sawa subili.


Habari zilimfikia Madam kuhusu ujio wa Lunnah!! Baaada ya kusikia aliamua kumuita Lunnah!!

  "" Wewe Ni wangu tu japo utanitoroka lazima ungerudi TU! Najua ulikoenda haikuwa kwenu ila Hapa Ndio kwenu!! Kitu nilichokitegemea kwako Miaka ya nyuma najua kwa Sasa hakipo tenaa!!" Ila nitakunyosha leo!!


Madam Alimchukua Lunnah na kumpeleka kwenye chumba kilichokuwa kimeandaliwa!! Alichoamua Ni kumtafutia mibaba mitatu imuingilie!! Madam aliagiza wahudumu wamuandae na kumbadilishia mavazi na kuvaa vazi la ukahaba, 

   "" Tuone Leo Kama utarudia Jeuri yako!!! Tena naona Siku hizi umenogaa Sana!! Leo hutasahau kwa unyama utakaotehdeka kikubwa wasikuzuru tu ili uzidi kuniingizia pesa!!""


Lunnah Alikuwa akisikia maongezi ya Madam na yeye aliamua litakalokuwa na liwe mbona waliopo kwenye Cassino wanaishi vizuri na wanafurahia maisha!!


Ni muda wa usiku alisikia mlango ukifunguliwa taratibu, aliamua kujifunika gubi na kuanza kulia Huku akizidi kumuita Mamake!!

  ""Mamaa!! Leo Sina chaguo jingine natamani Siku ya leo nikufate huko uliko najua mnaishi vizuri na Baba na Mimi nataka nije huko muwe mwaniagiza angalau!!""


Baadae alisikia mtu yupo kitandani na Muda wote Alikuwa akimsikiliza maneno yake, Alimfunua shuka na kumuita.

  "" Duffer!!! Duffer!!!! Ni Nini hicho unakiwaza??"


Lunnah Ndio anasituka Huku akizania Ni Ndoto.

  "" Duffer!! Ni Wewe Kweli umekuja kunifanya tena nirudi Duniani Mimi nataka niende kwa Mama na Baba leo!!""


  "" Duffer unaamua Kweli leo kuuzika mwili wako kiulaini TU, na Wewe umezamilia tayari!! Ahadi zetu ziko wapi leo za mimi na Wewe!! Kusaidiana na nilikwambia Duffer wa Kweli Ni yule ambae hatomuona Duffer wake anapata shida!! Hapa hujui tu nimefikaje hapa!! Hujui Nimetumia kiasi gani kuwalipa wale jamaa wasije kukuzuru harafu unachukulia simple simple TU!! Wewe Ni Mtu gani Lunnah!! Usie jali maisha yako!!""


  ""Sasa Ndio umeamua kunywa pombe!! Wewe kawaite TU wale jamaa kwani kinachokuuma Wewe Ni kipi?! Nikihariwa si Ni Mimi!! Kwanini kunifatafata muda wote!!?""


Imlany aliinuka na kufunga mlango na kuweka funguo mezani!! Kisha alimtizama Lunnah Huku Akiwa haamini maneno anayozungumza aliamua kumkumbatia kifuani kwake Huku Chozi la Huruma likimtoka.

 "" Duffer Ni afadhari nikuzulu Mimi kuliko uzuliwe na watu wasiojulikana  matokeo yake upate magonjwa bure!!!" Leo nitakwambia!! Ninafanya haya yote kwasababu gani!! Ni Siku nyingi nimekuwa na hisia zenye mapenzi ndani yake Tena ni  zaidi ya Urafiki ( Duffer). Niseme tu Nakupenda Sana!! sana!! Duffer!! Ndio maana maisha yako wewe Ni maisha yangu Mimi!!""


   "" Aah aa!! Lakini Duffer Ni na  aa Rayna,,,,,,"

 

   ""Najua Sitaki uzungumze kitu Ni hisia zangu!! Leo Nimeamua kunywa pombe ili niongee ya moyoni, najua Siku zote mtoto na mlevi huwa wanazungumza Ukweli na Mimi siwezi kurudi Utoto Ndio maana Nimeamua kunywa pombe!! Harafu kesho tunarudi wote kazini kwako lazima nikurudishe!!


Imlany aliamua kuzima taa, mpaka Asubuhi kukapambazuka Ndio Wanasituka usingizini, Wakwanza kuamka Ni Imlany Baada ya pombe kumuisha kichwani aliamka na kuelekea bafuni kuoga,  Alivaa haraka Huku akigubikwa na wimbi la aibu aliamua kutoka Nje na kuingia kwenye gari akimsubili.


Lunnah Ndio anaamka na kuangalia pembeni yake hakuna mtu!! Aliamka na kutembea mdogo mdogo Hadi bafuni!!

  "" Imlany!! Hivi Kweli usiku nimepumnzika na Wewe vipi kuhusu Rayna akijua si atanifanya Mbaya!!""


Alimaliza kuoga na kushika simu Yake, baada ya kuona sauti ya message ikiita,  Altoa pattern na kukuta Kuna Ujumbe wa Imlany.

   "" Duffer!! Nakusubili kwa Nje kwenye gari!! Njoo tuondoke wote!!""


   " Okay!!"" 


Kidogo Tena simu Yake kuliingia Ujumbe  kutoka kwa Junior.

  "" Hellow Lunnah!! Nashukuru kwa kuruhusu simu zangu ziingie kwako! Endelea  kuwa na moyo huo naimani tutafika TU!! Kwanini wanichukia kiasi hicho lunnah?? hukupaswa kuondoka kimya bila kuniaga!! Okay lini warudi Nina mazungumzo na Wewe!!!""


Hawa nao watanichosha Kweli harafu Junior ushaanza nilikuanbrock Jana tu Leo umeanza tenaa!!  nitakubrock tenaa. Kidogo simu yake iliita tenaa!! Alikuwa Ni Junior.

  "" Vipi Lunnah!! Hivi Ni Kweli! Wewe huwa unajiuza kwenye Cassino?? Junior alimuuliza hivyo tu na kukata simu!!""


   ,,,, Itaendelea,,,,,,,

Usikose Sehemu ya 11.


Kwanini Junior kamuuliza hivyo Lunnah!! Kipi kipo nyuma ya pazia??


Ungana nami kwa kulike, Comments na share niunganishe kipande kingine!!

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi