SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER . MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 08. 0746638941 (Wtsp).
ANZA NAYO.
Leo upande wa Imlany alikuwa kapumnzika siku hiyo aliamua kumtafuta Lunnah Alimpigia video Call.
"" Hellow Duffer!!! Inaonekana kweli haunimisi siku hizi!! Muda wote Mimi Ndio nakuwa wakukupigia simu kwelii!!!""
"" Hapana Duffer!!!! Kwasasa naogopa upo na Rayna kukupigia simu muda wote nitajenga uadui Mimi na Wewe!!""
"" Kwanini uogope?? Kwani Mimi na Wewe tuna mahusiano ya kimapenzi Mimi kwako Ni Rafiki tu, au Wewe unahofia Nini kwani!!!??""
"" Hapana bhana Duffer!! Nakukumbuka Nakumisi pia!! Hapa Nipo nimevaa Cheni yako Ila imeanza kufubaa ani!! Sijui ulinunulia wapi TU!! Vipi saa yangu iwapi make siioni hapo mkononi kwako!!!""
""" Ooh!! Hapa nimetoka kuoga but ninayo!! Iko mezani!!! Mida nitakuchomea Hapa naona Rayna kaingia hafu siku hizi anamind Mimi kuongea na Wewe!!"""
Rayna alifika na kuchukua simu Kisha alianza kukagua Imlany alikuwa anaongea na Nani muda wote ule.
"" Ushaanza Mambo yako!! Huyu Ni Lunnah kabisa, kwanini nije harafu ukate simu!!??""
"" Rayna hebu kuwa mpole basii!! Ayaa huyo Ni Lunnah!! Unachotaka kunambia Ni kipi?? Okay Duffer now Ni partiner wangu!! Bado unaswali tenaaa??""
"" Sawa TU!! Najua hunipendi TU Imlany, na muda wote wampenda Lunnah!! Rayna aliamua kuondoka na kukimbilia chumbani kwake Huku akizidi kulia.""
Imlany aliamua kumfuata Rayna Hadi chumbani na kwendaa kumbembeleza mkewe!!""
"" Rayna yote hayo huwa wasababisha Wewe!! Mbonaa una jereous kiasi hicho!! Ni Duffer wangu yule Lakini unaonekana unapenda kelele Wewe okay jiandae kesho tunaelekea Nyumbani kwenu nikamalizie mahari nikuoe haraka si Ndio wataka iwe hivyo!! Tatizo nyie wanawake huwa mnapenda kuvaa shera tu na hio Ndio Ndoto yenu!! Okay nitafanya!!!""
"" Sio hivyo Imlany!! Nahofia penzi langu!! Hapa kila mtu achunge mzigo Wake!! Harafu punguza kuniwazia hivyo Mimi sipo Kama anavyofikili unazani Mimi nimefanya shella Hapa!! Nimefata upendo wangu tu Ndio unanisumbua!! Au nakosea Kukupenda lakinii!!! ""
"" Okay!! Upendo wako usiniadhibu kiasi hicho hebu nipe Uhuru wa kufanya Mambo yangu!! Mimi najielewa Wewe una nafasi yako pia!! Hebu niamini basii niwe huru!! Ukiendelea kunifatilia utanifanya nishidwe kufanya Mambo yangu mengine!!""
"" Nimekuelewa kwasasa sitakusumbua tena!! So be fare!! Kwasasa Nataka nifocus na Mambo yangu Kwanza!! kesho naondoka utabaki salama!!""
Imlany aliamua kumkumbatia Rayna Baada ya kuona feeling zake ziko mbali kimawazo!!
"" Sorry kajiandae Basi leo Nataka nitoke na Wewe!! Vaa nguo nzuri ninayoipendaga si unaijua!!!""
Rayna aliingia Ndani na kujiandaa Kisha walitoka wote na kuelekea hoteli kubwa kupata chakula Cha usiku. Rayna kunazawadi alikuwa ameiandaa siku hiyo alimwomba Imlany afunge macho Kisha aliingiza mkono kwenye mkoba wake na kutoa saa, Kisha alimvisha.
"" Nisamehe kwa kukupotezea furaha yako kwa muda mrefu!! Najua hii saa ulipatiwa na Lunnah!! Rafiki yako hata Jana wakati anakupigia Lunnah aliulizia saa naona Ni kitu Cha muhimu kwake na Wewe ukamkumbusha kuhusu Cheni!! Ni Duffer wako unampenda na Mimi Sitaki kukuona unakuwa hivyo!! Kwasasa nitazidi kumwamini Lunnah na urafiki wenu na Mimi Nataka niwe rafiki yenu Kati ya Duffer na Duffer Wake!!""
Imlany Baada ya kusikia hivyo alibaki na furaha isiyoelezeka, alimkumbatia Rayna.
"" Hapo Ndio nimekukubali!! At wataka nikatishia urafiki wangu na Lunnah!!""
Siku hiyo ilienda vizuri baina ya Watu wawili na upendo wao uriludi Kama mwanzo tenaa!!!
°°°°°°°°°°°°°°°°°
Siku nyingine Tena upande wa Lunnah alipokea Ujumbe kutoka kwa Imlany!! Kesho nitakuja Huko Kuna Kazi ya ofsi Nataka niikamilishe!! Kesho yake Lunnah alikuwa akijiandaa kumpokea Imlany Alifanya usafi wa Hapa na pale!! Huku alijitahidi kila kitu alikiweka sehemu husika, Aliamua kutoka nje Kwanza kutafuta matunda ya kutengenezea juice.
Ile anatoka nje Alikuta Kuna gari nje imepaki pembeni, alizidi kuitazama Lakini Kumbukumbu zikaja Ni Ile gari ya Junior naona kaijia koti lake ngoja Kwanza nimfatie!!
Aliondoka na kwenda kuchukua Koti Kisha Alikuja Moja kwa Moja Hadi kunako gari lakini alishangaa Baada ya kukuta gari halipo Tena, aliamua kuondoka nalo Huku akizidi kuangaza Huku na kule Kama ataiona Ile Gari!! baadae alikata tamaa nakuanza kuzungumza pekee.
"" Yaaani Junior!! Sijui yupoje leo kaijia koti, nmelifata nimletee harafu nakuta hayupo Tena!! Bado unazidi nizurulisha na koti lako bado Ni lizito Kweli!! Una bahati tu naona Kuna kimvua Tena kimeanza kunyesha!! Na kwakuwa Ni msimu wa Mvua linazidi nisaidia Hapa nitatembea mdogomdogo Hadi Nyumbani""
Huku Njiani alionekana Junior alikuwa pikipiki akiendesha, kwa mbali kidogo alimuona mtu Kama anakoti lake aliamua kumfatilia ili ajue Kama Ni lenyewe, Alifika na kumpigia hon. Lunnah Alisituka na kumtizama.
"" Nani Wewe!! Inamaana huoni njia mpaka upite sehemu yangu!!""
Ile anamtizama vizuri alishangaa kumuona Ni Junior.
"" Junior!!!' vipi na Mvua hii unaenda wapi!! Harafu kwanini ulinikimbia wakati nilikuwa nakuletea koti lako!!""
Junior yeye alikuwa Hana habari kabisa, muda wote alikuwa akiitizama nywele za Lunnah Kama Ni zenyewe Ani ndefu, Baada ya kujilizisha Ndio akaachia tabasamu!!
"" Ooh kumbe Ni yeye!!""
Lunnah hakumuelewa' aliamua kutoa koti na kumkabithi koti lake!!
"" Koti lako hili Hapa!! Make limenitembeza Kweli nahisi ningekuwa nimekutana mapema nisingenyeshewa Mvua!! so Sitaki Tena itokee!!""
Junior aliamua kumrudishia Lile koti.
"" Siku ile majira Kama haya nilikupatia rifti lakini Nia yangu Ilikuwa nikupeleke Moja kwa Moja Hadi Nyumbani kwako lakini nilipata dharula!! Hilo koti ukinipatia Mimi!!! kwako sitakutendea haki twende nikupeleke Nyumbani kwanza ili usilowe!! Hapo Sasa hata ukinipatia koti itakuwa vyema!!!""
Junior Alimchukua Lunnah na kuelekea nae Hadi kwake Huku Lunnah alikuwa akimuelekeza sehemu anakoishi, walifika Hadi Nyumbani, Junior alipaki pikipiki yake na kubaki amesimama.
Lunnah Aliona sio vizuri mgeni Wake!! Aishie nje aliamua kumkalibisha Hadi Ndani. Junior Baada ya kufika Ndani alifika na kusimama tu, mpaka Lunnah akamuuliza.
"" Mbonaa haukaiii!!!??"
"" Nikae vipi wakati nguo Ni mbichi!!""
"" Sasa Mimi nitatoa wapi nguo za kuvaa Wewe!!! Hapa nitakupatia t-shirt je suruali!!??""
"" Nipatie track!! Kwani Wewe hauna!!"" Harafu nichukulie boksa dukani!!!""
"" Mhuuuuu!! Mimi Tena nikakununulie Wewe!! Sasa nitasemaje na pesa iko wapi!!??""
"" Tumia yako nitakulipa!!!" Harafu nioneshe bafuni wapi nikute naoga kabisaa!!""
"" Daaaa!!! Hapa nimepatikana leo!! Okay!! Bafu lipo Moja harafu chumbani kwangu Wewe utaingiaje Sasa!! Ngoja Kwanza niweke vizuri vitu vyangu!!!"
Lunnah aliingia chumbani kwake na kuhifadhi baadhi ya vitu vyake!! Vingine vilikuwa Ni vya Siri!! Alimtafutia nguo Junior na kumuwekea bafuni!!
"" Huyu Junior jamani yupoje mbona anakuwa hivyooo!! Okay uoge haraka uende kwako!!!""
"" Wewee Junior!! Ayaa njoo uoge haraka!! Nikirudi tu!! Uwe umemaliza Nataka nikusindikize haraka usiku unazidi kuingia sahizi Ni saa Moja et!!!.
Lunnah aliondoka na kuelekea Dukani kutafuta nguo!! Muda kidogo ariludi nakumkuta Junior bado yupo bafuni.
"" Wewe Junior!! Mbonaa masaa mengi yamepita hautoki humo bafuni!??""
""" Harafu niite vizuri sio Wewe Junior!! Ukisema Junior TU huriziki!! ayaaa nishamaliza kuoga hayo mafuta yako wapi!!? Bado nguo ya Ndani ulitaka nivalie juu!!!??""
"" Unazingua bhana!!! Hayaa vyote hivi hapa utanikuta mlangoni Mimi npo jikoni napika!!""
Lunnah aliendelea kupika, lakini alisitushwa kidogo na mlio wa Glass ilianguka chini, aliamua kwenda sebuleni kuchungulia, alishangaa baada ya kumkuta Junior yupo busy akisaga juice.
"" Junior jamani!! Mbona hata sitakwambia uyengeneze juice!! Unajiamulia tu humu ndani Kama Wewe Ndio baba mwenye Nyumba!!!""
"" Kwani siwezi kuwa baba mwenye Nyumba!? Okay!! Nimefanya kukusaidia TU Baada ya kuona upo busy jikoni nikaona nikupunguzie kazi!! Harafu toa hio kofia yako umeharibikia!!!"
"" Kwani yanakuhusu Nini Wewe!!??""
"" Hayanihusu ndio!! Lakini nywele tayari zimelowa hapo zitanuka!!!"
""" Eeee!! Junior!! Junior!! Unaniuzi bhana!! Kaa kimya umalize kula uondoke!!""
Junior alisimama na kumshika Lunnah na kumpeleka Hadi jikoni.
"" Kwani hii nyama wapika na Nini!!??""
"" Mimi sijui bhana!! Itakuwa twaikomba!!""
"" Ayaa Wewe kaoge!! Mimi nitakaanga nyama harafu nakaanga na chips kavu!! Ndio tukombe Sasa!! Hii kazi niachie Mimi!!!
Lunnah Aliamua kuondoka na kuelekea bafuni kuoga alimaliza kuoga na kukausha nywele zake Kisha alichukua track Yake ya dhambarau alipigilia na kumpulizia marashi kidogo Kisha Alikuja kukaa sebuleni, alikuta chakula tayari Junior kaandaa na kuweka mezani!! Lakini alianza kumwangaza huku na kule akimtafuta Junior!!
Baadae Junior aliingia akiwa anatokea Nje, alifika na kumtizama Lunnah na kubaki kaduwaa, baada ya kumuona kabadilika Ghafura, na urembo wake ulizidi kuonekana vizuri kuliko hata alivyokuwa kamzoea siku zote!!
Lunnah Aliamua kumsitua.
"" Mimi nikajua umeenda Nyumbani!! Kumbe upo bado!!!""
"" Unazani Nani anapenda kulowa na mvua!! Nilienda kupaki pikipiki yangu vizuri!! Mimi leo nimgeni wako means nalala hapa!! Okay funguo ya pikipiki hii hapa utakuwa waiangalia usiku nikilala!!!""
Lunnah Aliamua kumshika mkono wake Junior uliokuwa na Ile funguo.
"" Wewe mmewangu anakuja leo!! Utaniharibia jamanii!! Please nakuomba uondoke nitakupa mwamvuli wako!! Na koti nitakupa lakwangu!! Sawaaa Junior!!""
Junior hakuwa anajali kabisa muda wote alikuwa akimtizama Lunnah usoni.
"" Lunnah!! Kweli Wewe Ni Mrembo na hii nywele yako imezidi Kukupendeza!! Kuwa mpole Basi tuongee!!!""
"" Tuongee Nini tenaa!! Nachotaka nisikie kwako Ni unaondoka tu basiii!!!!!"
"" Lunnah hebu kuwa na utu Basi, hapo nje Kuna mvua kubwa yanyesha!! Hapa nimevaa nguo zako!! Na Mimi naishi kambini kuingia kambini kwa Sasa Ni ngumu!! Bado mavazi Ni ya kike!! Huoni nitafukuzwa Kazi!! Hebu nilindie kibarua changu leo!! Harafu kesho nitaondoka Asubuhi!! Naomba unisaidie kufua nguo ili zilale zimeanikwa!!!""
Lunnah alikakaa akifikilia baadae aliwaza kumbe Junior Ni mwema tu, walimaliza kula, huku Lunnah alimwacha sebuleni Junior akiangalia mpira na yeye alitoa nguo na kuanza kufua!!!""
Baada ya kumaliza ariludi Hadi sebuleni na kumkalibisha Junior sehemu ya kulala.
"" Junior nenda kalale chumbani Mimi nitalala hapa sebuleni!!!""
"" Aah tukalale wote bhana!! Wazani Mimi nitakusumbua!! Basi huniamini niache Mimi nilale sebuleni Wewe kalale TU Huko chumbani!!!""
"" Basi na Mimi silali Chumbani!! Mgeni gani unakataa kulala sehemu aliyoandaliwa Basi tulale wote hapa kwenye sofa!!!"""
Baadae usingizi uliwachukua na kulala pale pale kwenye sofa!!"" Junior Alisituka usiku na kumtizama Lunnah alimuonea Huruma kwa mbu walivyokuwa wakimkula alisogea Karibu yake huku akizidi kumtizama.
"" Lunnah!! Nahisi hata muda ninaopoteza hapa Ni kwasababu Nakupenda tu!! Sio kwamba siwezi kurudi kambini now Ila naweza sana, Ni vile Nimeipenda ukaribu wako tu!! Alichukua shuka na kumfunika.""
Aliamua kuwasha music kwa kuachia sauti ya Chini huku akizidi kusikiliza Mdogo Mdogo Hadi kukapambazuka.
,,,,,, Itaendelea,,,,,,,,
Usikose sehemu ya 09.
Kipi kinafuata katika mkasa huuu.
Like, comments, share.
Saport yenu ya muhimu kwangu bila saport Mimi swezi fanya kitu kwaajili yenu!! Mtie Nguvu yule anayekupa kufurahi!! Ili uzidi kufurahika Zaidi.