Ikawe heri 11

 SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER .                            MTUNZI: TINNER ROBER.                          SEHEMU: 11. 0746638941 (Wtsp).


ANZA NAYO.


"" Vipi Lunnah!! Hivi Ni Kweli! Wewe huwa unajiuza kwenye Cassino?? Junior alimuuliza hivyo tu na kukata simu!!"" ENDELEA!!!!!


Imlany Baada ya kuona Lunnah anakawia kufika aliamua kumurudia na kumshika mkono na kumpeleka Moja kwa Moja kwenye Gari.


Lunnah muda wote alikuwa akiwaza Mambo mengi baada ya kuona ule ujumbe wa Junior alitaka kumjibu lakini aliwaza atamjibu vipi? Aliamua kuweka Simu na kulala baadae Alisitushwa na sauti ya Imlany akimuamusha dirishani!!

  "" Sasa utakaa kwenye Gari mpaka Sangapi!! Karibu tunywe chai!!""


  "" Ooh!! Kumbe tumefika!!!"


Walikaa na kuagiza Vitafunwa na kuendelea kula Huku kill mtu Alikuwa kimya akimsikiliza mwenzake Kama ataanza kuongea! Lakini kwa Imlany aliamua atumie uhusika wake na kukuta wakizungumza pamoja Huku kill mtu akimuita mwenzake, "" Duffer!!!"


   "" Vipi Lunnah mbona umekaa kimya hivyoo huongei!!""


  "" Kwani Wewe ulikuwa waongea zaidi ya kuongea na vijiko?? Harafu Duffer! Kwanini uliamua kunifanyia hivyoo!!??"" Leo Mimi na Rayna! Itakuwaje??


Kabla Imlany hajajibu simu yake iliita na kupokea, baada ya kuongea alimpatia simu Lunnah!!


Lunnah Alipokea ile simu na kutoka kidogo kuongea, baadae alikata simu na kumrudishia Imlany huku Akiwa analia.

   "" Duffer!! Nilijua haya yote yatatokea unaona Rayna anavyonifokea Mimi nitakuwa mgeni wa wapi baada ya haya yote yakijulikana!!!" Lunnah aliondoka na kuelekea kwenye gari Kisha alifika na kujiinamia kwenye kiti akizidi kulia!!!


   "" Lunnah!!! Naomba Basi unisamehe!! Haikuwa hatima yangu!! Nikufanyie hivyoo Niamini Mimi Hakuharibiki kitu hata Rayna hawezi kujua ila Ni wasiwasi wake TU anakuwa hakuamini!!!""


"" Vipi kama utanirudisha Cassino!! Huoni utakuwa huru Wewe na Mwenzake wako!? Hapa kwasasa unanipeleka Nyumbani huoni Rayna anaweza kuja na kusababisha ugomvi tenaa!!""


"" Mbonaa unakuwa hivyo Lunnah!! Sitaki kusikia habari za Cassino!! Nitakupeleka kazini kwako na utaenda kukaa kwenye Nyumba yako!! Hebu niamini Mimi na uniheshimu kwa kitu ninachokitaka kifanyike basi!! Mbonaa muda wote unataka ugomvi na Mimi!!"


Siku hiyo Kila mtu alikuwa haelewani na mwenzie, Ilikuwa Ni usiku tenaa. Imlany alichukua simu yake na kumtext Lunnah.

   "" Hellow Duffer!!! Umenisamehe kwa kitendo Cha Jana!!?? Naimani Duffer wa Kweli Siku zote huwa kakaa na roho ya msamaha Ndani yake!! Pole pia kwa maumivu!!!"


Lunnah muda wote alikuwa yupo macho akifikilia kitendo Cha Jana na kubaki akitabasamu TU.

  "" Moyo wakukupenda ninao Lakini sihitaji Tena kwasasa unaenda kuniacha unaanza Safari nyingine ya maisha ila nitazidi kukukumbuka Sana Duffer wangu!! Katika maisha yangu yote tuliyoishi Mimi na Wewe sijawahi jutia uwepo wako!!! Daima nitazidi kukukumbuka.""


Muda kidogo Ujumbe wa Imlany Ndio unafika!! Aliufungua na kuusoma Kisha aliamua kumjibu.

  "" Sitaki maneno yako!! Wewe sio Duffer tenaa!! Duffer gani anamsaliti Duffer wake!!??"


   "" Kama Mimi sitakuwa na Nafasi ya Duffer tenaa!! Hebu niambie hiyo nafasi umempatia Nani?? Ila nitapenda Junior umpe nafasi ya Duffer harafu Mimi niwe Partiner wako wa moyo!!"" Imlany aliamua kumjibu Lunnah.


   "" Utajua mwenyewe bhana!! Harafu kwasasa Duffer Hana nafasi kwangu!! Na kitendo Cha Jana naomba usahau kabisaa!! Ndiyo!! Kwasasa Duffer wa Kweli Ni Junior!!!''


   "" Ahsante kwa majibu uwe na usiku mwema Duffer wangu!! Kipenzi changu!! Daima nitakumisi hata Kama nikianzisha Safari nyingine bado Nafasi yako itakuwa bado nimeihifadhi moyoni!!!  Cha zaidi! Nakupenda"


Kesho yake Ilikuwa Ni Safari ya kurejea Lunnah kazini, Alikuwa kaambatana na Imlany. Imlany alimfikisha Lunnah na kusaidiana kuweka Mambo sawa kwa muda ambao hakuwepo kazini!!


Siku iliyofuata mnamo majira ya Asubuhi Imlany Alikuwa Nyumbani kwa Lunnah akipangilia nguo zake kwenye Begi ili aondoke.


Lunnah muda huo Alikuwa akiandaa chai mezani baadae walikaa mezani Huku wakipata kifungua kinywa!! Imlany alianzisha sitori za Hapa na pale zilizozidi kurudisha ukaribu wa marafiki wapendanao.

   "" Lunnah!! Sitaki Tena kusikia habari ya Cassino kwasasa nataka nisikie habari ya  kampuni inazidi kukua na hii Ndio furaha yangu, kampuni ikue ikiwa miongoni mwa Duffer wangu ninayemuamini!!!""


  "" Usijali!! Nakuahidi haitatokea tena kusikia narudi kwenye Cassino!! Na hutaona narudi Nyumbani kwenu Mimi Siku zote nitakuwa hapa kwangu!!!"


  "" Vizuri!! But umeniuzi at hutarudi Nyumbani kwetu hapo tengua kauli sema nitakuwa naja kuwasalimia kila likizo!!!""

   

   "" Ila Ni hivyooo TU!! Sitakuja Basi  tuondoke!!! Mimi nakusindikiza Hadi stand harafu naelekea Officin.

 

Imlany Alikuwa akizidi mtizama Lunnah baadae alisimama na kuchukua Begi lake, lakini kwa bahati Mbaya mguu wake ulikuwa umekufa ganzi alishidwa kutembea na kuomba sapoti kwa Lunnah.

   "" Duffer Mguu wangu umekataa please naomba nikae kidogo!! Unisaidie na maji unimwagie kidogo!!!"


Lunnah Alichukua maji kidogo kwenye kikombe.

  "" Sasa!! Nitamwagia na hicho kiatu na hizo soksi!!??""


  "" Siku hizi waniogopa Kweli!! Nahisi Mimi kwa Sasa Sina nafasi ya UDuffer tena!! Kipindi Cha nyuma uliweza kunivalisha hata shati lakini hukuniogopa!! Basi fanya Kama mpenzi!!""


Lunnah Alimtizama Imlany na kumfanya akae kwanza!!

 "" Basi sifanyii!!! Wewe si Ndio waumwa!!!""


Imlany Alichukua simu Yale na kumpatia Lunnah!!

  "" Kwani Sasa Ni saa ngapi??! Okay Mimi nasafiri Wewe waenda ofisini!!! Hata hivyo uwepo wako nafurahia!! Basi tuzidi kukaa mpaka mguu wangu uwe sawa na hauwezi kuondoka ukamuacha mgonjwa!!!""


Lunnah Alitizama muda na kuona unazidi kwenda alisimama na kumvua viatu na soksi Imlany!! Kisha alichukua maji na kumumwagia kidogo!!

  ""Naimani kwasasa utakuwa mzima!! Basi twende.


Imlany Alimshika mkono Lunnah!! Na kumvutia kwake Huku akizidi mtizama usoni.

  "" Naomba urafiki wangu na Wewe uendelee!! Haijalishi Nini kimepita Kati Kati yetu!! Hata Mimi namisi ukaribu wako na michezo yetu!! "" Siku zote sikuwahi kutumia amri Kama nilivyotumia Hapa!! Huwa unafanya kitu pasipo kuamuliwa naomba ufanye Tena Kama zamani!!!"" Imlany alizidi kumkumbatia Lunnah huku akizidi kumuomba msamaha!!


Lunnah Aliamua kumjibu Imlany!!

  "" Nisamehe pia Mimi!! Nahisi kwasasa nakosa kujiamini nikiwa na Wewe!! Ila nitajitahidi kuwa Kama mwanzo tulivyokuwa tukiishi wote!!""


Imlany alifurahi Sana baada ya kusikia vile, waliongozana kwa pamoja na kuelekea kwenye gari!! Kisha Lunnah alimpeleka Hadi Stand na kuchukua usafiri. Kabla hawajaagana kill mtu aondoke! Imlany alitoa kiboksi kidogo na kumkabithi Lunnah.

  "" Hii Ni zawadi yako Duffer nakukabizi!! Ila Utaifungua ukiwa Nyumbani!! Sawaa!!"


  "" Ahsante Duffer!! Uwe na Safari njema pia msalimie Ratifa!! Mwambie huwa namkumbuka Sana!!!"


Baada ya kuachana kila mtu alikuwa na Safari yake!! Lunnah alifika Hadi Ofisini na kuanza majukumu yake lakini akili Yake Ilikuwa ipo juujuu ikiwaza zawadi ya Imlany!!

   "" Duffer nayeye!! At ifugue ukiwa Nyumbani!! Mimi swezi vumilia nitaifungua TU!!"


Taratibu alifungua na kukuta Ni zawadi ya saa na Ujumbe uliambatana!!

  "" Hongera Duffer!! Kwakujitunza muda wote!! Sikuwa nakuamini Kama utakuwa bado na usichana wako!! Kutokana na maneno yako muda wote watamani ukakae kwenye Cassino!! Hii imenifanya nishidwe kukuamini nikizani kuwa Wewe huenda Ni Kahaba!! Ila nitapenda zaidi kujua hhistoria ya Wazazi wako Kama  hutojari!!! Iakini kwa sasa Nazidi kukuamini na kuzidi Kukupenda Kama Duffer wangu wa moyo!! Zawadi niliyokuandalia Ni Kama Shukrani ila Kuna Siku nitafanya zaidi!!


Lunnah Baada ya kumaliza kusoma Ujumbe!! Alifurahi Kweli na kutaka kumjibu Lakini aliishia kutabasamu TU!!


Muda kidogo alisikia Kuna mtu akibisha hadi. Alimsihi aingie!! Ile anakuja kuangalia mgeni aliyeingia alishangaa kumuona Ni Junior!!!

  "" Junior!! Umenifata Hadi kazini jamani!!!"


 '"" Kwanini ulikuwa hujibu Sms zangu muda wote??? Ile Siku nilikupigia simu Video call nikakuuliza kitu hujataka hata kunijibu wala kunitafuta tangu umefika!!! Ndio maana Nimeamua nije mwenyewe!!""


  "" Ni muda wa Kazi hata hivyo!!! So ungenisubili nikatoka!!!""


  "" Nilikuja kukuarifu tu!! Kwasasa Ni saa nane mchana!! Ofsini mnatoka saa kumi na Moja'' so utanikuta Nje nakusubili Wewe!!?


Junior aliondoka na kumuacha Lunnah amekaa!! Alielekea kwenye Gari na kuingia huku akiachia mziki was Taratibu Kisha usingizi ulimchukua!!


Huku kwa Lunnah Baada ya kumaliza majukumu yake alifungua ofisi na kuelekea nje!! Lakini alishangaa baada ya kumkuta Junior yupo kwenye gari akimsubili huku usingizi ulikuwa umemchukua.


Lunnah azidi Kumtizama Junior!! Junior alionekana Ni mkaka smart Sana hata rangi yake ilivutia pamoja na muonekano wake Alikuwa Ni HB Kweli!!

Alizidi Kumtizama huku Junior alikuwa kaweka Earphones zake sikioni akisikiliza mziki wake!!  Kwa pembeni aliona Kuna hotpot lilikuwa limewekwa pembeni likiwa limefunikiwa vizuri, Aliona Bora afungue mlango na kuingia huku jicho likiwa kwenye hot pot!! Alichukua Taratibu na kufunua, huku macho yake yalitua kwenye pilau la kuku uchu wa kula ukimsaidia kumpa apatite ya kula.


Alisitushwa kidogo baada ya kusikia Junior akinyosha na kutoa Earphones zake masikioni.

  "" Lunnah!! Mtoto Joriee!! Haya nilijua utakuwa na njaa!! Nikaona nikutafutie Chakula ili upate kula!! Chukua Maji seat ya nyuma nawa ule!!!""


Lunnah hakutaka kuchelewa alinawa na kuanza kula!!

  "" Nipeleke Nyumbani Kwanza!! Watu wakiniona hapa harafu nakula kwenye Gari siyo picha nzuri!!"


Junior aliwasha gari na kuelekea Nyumbani kwa Lunnah. Lunnah alimaliza kula Ndio akili ikakaa sawa na kumuuliza Junior!!

   '" Wewe Junior!! Unanyosha Moja kwa Moja hadi kwangu!! Unapajua make sielewielewi!""


 "" Harafu nishakukataza kuniita Wewe!! Huwa washidwa kusema Junior TU!! Okay tatizo huwa wanificha!! Ukahama kimya kimya ulizani sitapajua?? Nilienda kuulizia pale ulipokuwa waishi zamani walanielekeza Hadi kwako harafu muda mwingi nimekuwa nikija kukuona lakini hukuwepo!!!""


  "'" Nishajua Junior!! Ni watu wanaopenda kufatilia maisha ya Watu!! Ayaa nishushie Hapo Nje!! Na urudi kwako!!""


   "" Nilikwambia nataka tuongee na Wewe!! Harafu nimekuuliza twaelekea wapi ukasema kwako!! Ungesema kwangu au hotelin ningekupeleka!! Kwasasa namimi siendi sehemu yoyote ile!! Nataka kwako.""


Lunnah alishuka na kufungua mlango Mlango wake!! Na kumkalibisha Junior ndani!

   '" Ayaa!! Dakika tano ongea!!! Zikiisha tu! Nakutimua.


   "" Dakika tano!! Kukaa tu zinakuwa zimeisha harafu Kama nakubana kwako!! Twende sehemu nyingine Sitaki unipelekeshe!!!"


Lunnah alipiga target zake na kutoa maamuzi.

 "" Basi tuongee hapa!! Make nyie hamchelewagi kabadilika mkiwa faragha!!""


   "" Okay!! Nipo serous kidogo!! Naomba uniambie stori yako ya maisha!! Bila kunificha chochote na Kwanini ulirudi kwenye Cassino!!?? Harafu Wewe na Ancle ako Mnaficha Nini?? Vipi kuhusu Shangazi yako ulimuacha anaendeleaje??! Kuhusu Madam wa Cassino na Shangazi yako  wana ukaribu ganii???


Lunnah Alishusha pumnzi ndefu kwa maswali ya Junior yalimtoa kijasho chembamba kilichompelekea kuchukua Glass ya maji  na kushushia Kwanza!!!


   ,,,, Itaendelea,,,,,


Usikose sehemu ya 12"


Je, Lunnah!! Atamjibu Nini Junior?? Na kipi Junior anakijua kuhusu maisha ya Lunnah!!


Like, comments, Share.

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi