Ikawe Heri 21

 SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER .                            MTUNZI: TINNER ROBER.                          SEHEMU: 21. 0746638941 (Wtsp).


ANZA NAYO.


Junior'' na Lunnah walirudi kijijini kwenda kumchukua Lunnah nakuondoka nae Hadi mjini kwenda kuunganisha Kesi ya Ancle. ENDELEA...


Siku iliyofuata walielekea mjini moja kwa moja Hadi Nyumbani kwake Lunnah.


Lunnah Aliamua kurudi mjini nakumchukulia nguo Ennah pamoja na mtoto wake huku akiunganisha na chakula Cha mtoto Kama lishe..


Ilipita Kama mwezi mmoja, Afya ya Ennah ilikuwa imeanza kuimalika pamoja na mtoto Wake, Ennah aliweza kufanyiwa upasuaji baada ya mtoto wake wa tumboni alionekana kapoteza maisha baada ya kuathiriwa na Madawa aliyokuwa akitumia kutoa Mimba, Lakini baada ya lishe na matunzo kutoka kwa Lunnah afya yake ilirudi Kama mwanzo na mtoto wake( 1yr Nasrah) alikuwa tayari anatembea..


Ni siku nyingine tena, Lunnah Aliamua kumuweka ndugu yake Ennah kwenye kampuni awe Mtumishi, Kwa Ennah alikuwa amepata taarifa zote kuhusu babayake Ndio mwenye kampuni na yupo mikononi mwa Sheria akitafutwa muda wote.


Lunnah Aliamua kumtembelea Ennah huku akijaribu kumuelekeza jinsi ya utendaji wa kazi, Alifika nakumkuta Ennah kakaa huku akishushia juice yake baridi alifika nakumuuliza.

  "" Vipi Ennah!! Kazi umeimaliza niliyokuwa nimekupatia make zile documents zahitajika twataka mahesabu yakufunga mwaka!!"


 "" Lakini Lunnah!! Hiyo kazi hata Wewe Unaweza kufanya!; Isitoshe Wewe pia upo Chini yangu!! Siku babayangu akija hakika Mimi Ndio nitakuwa director wa hii kampuni!!!"


Lunnah alibaki kaduwaa, hakuamini Kama Ennah leo anaweza kumjibu kwa kujiamini kiasi hicho.

  "" Ennah!!! Nakuthamini Sana Wewe na Shangazi yangu!! Naona kukwambia ukwelii leo wataka uanze akili Kama za babako!! Nimekukuta hujiwezi huna mbele Wala nyuma Lakini leo hii wanichukia Mimi sifai kwako!! Okay relax! Kampuni ya babako vipi wajua hata hizi Mali alizipata wapi??""


Lunnah Alitoka pale nakumuacha Ennah katulia, siku hiyo hata mood wakufanya kazi uliisha, aliamua kumpigia simu Dusky wake Junior!! Alimhitaji nyumbani kwakee na Junior alitimiza Nakuja.


  "" Dusky!! Leo sijisikii vizuri!! Hapa Ennah!! Kaanza kuniletea roho ya kumiliki Mali za babake kiburi si kiburi!! Kweli moyo wangu unauma Sana!! Tetesi za Ancle mpaka Sasa hapatikani alipo!! Wewe umefikia wapi kuhusu swala hili??"


  "" Daaah!! Hapo kazingua Sanaa!! Pole pia! Ila usijali Sana Hapa nakamilishia tu!! Sema Imlany Ndio ananiangusha hakumbuki kitu!! Ila Kuna baadhi ya matukio anakumbuka kiasi chake harafu Kumbukumbu tena zinapotea!! Ninachotaka kukifanya kwasasa nenda Ofisini kwa Ancle vunja Mlango Chukua vitu vyovyote vitakavyokamilisha  swala letu, na Hapa jioni Naenda kupokea Bahasha yenye documents kanitumia Imlany naamini ndani ya hii wiki tumepata Suluhisho Wewe nenda kazini ukafanye hivyo!!!


Lunnah Baada yakumaliza maongezi na Junior, Aliondoka nakuelekea ofsini, Alitafuta watu wakavunja Mlango Kisha aliingia Nakuanza kutafuta documents zote Lakini documents zilizopatikana Ni za kiofisi tu!!


Aliamua kusogeza meza Ili aangalie ukutani huenda alihifadhi, ile anasogeza alihisi Kuna kitu kigumu kakanyaga mguuni kwake, alinyanyua Mguu huku akitizama nikitu gani alikanyanga ndipo anagundua Kuna ubao ulikuwa umewekwa kwa sakafu aliinama nakujaribu kuubandua Ndio anagundua upo Kama sehemu yakihifadhio na unafunguliwa kwa Rock.


Aliangalia huku na kule akitafuta namna ya kufungua ndipo aliona kwa pembeni Kuna chuma kimetulia hapo!! Alichukua kile chuma nakuvunja ule Mlango bahati Nzuri alifanikiwa, Alianza kupakua bahasha moja baada ya nyingine ile alipomaliza kutoa alichukua documents zote nakuondoka nazo Hadi kwa Junior.


Walikaa na Junior Huku wakianza kukagua Documents moja baada ya nyingine, katika kupitia kwao Ndio wanakutana na picha ikiwa Ni familia ya Lunnah. Alionekana Ni Lunnah akiwa bado Ni mtoto Mdogo lakini kwa pembeni alionekana Kuna mtoto wakiume katika picha ya Pamoja, Baadae Tena walikuta Kuna picha ya Lunnah akiwa bado mtoto Mdogo akiwa na mtoto wa kiume walionekana wanamiaka sawa hivi!!


Walizidi Tena kukagua ndio wanakutana na picha ya Ancle wakiwa pamoja na Shangazi yake( mama Ennah) kwenye tabasamu la pamoja, walionekana Ni watu wapo romantic kabisa kwa love. 


Walizidi kukagua Ndio wanakutana na kile kitambulisho alichokuwa akikitafuta Imlany kwa muda mrefu.


Lunnah alibaki katulia kwanza Kama bumbuwazi hivi asiamini amini kumbe Imlany walikuwa wakifahamiana, Zaidi alijua TU Kuna mtoto alikuwa akicheza nae lakini walihama Yule mtoto akapotea na haikuwa lahisi kumtambua akiwa mkubwa kiasi kile, muda wote tangu anakuwa hakuwahi kuona picha za utoto hakuweza kabisa kukumbuka kumbe zile picha za utoto zote zilichukuliwa na Ancle, Alibaki akijiuliza Mara mbilimbili, " Ancle Ni Nani? Katika maisha yangu na katika maisha ya Imlany?? Hapa kilichobakia Ni Ancle ndie anajua ukwelii upo wapi??


Junior'' na yeye pia alikuwa akifikilia Mambo mengi Sana ilibidi tu azungumze na Lunnah!!

  "" Kumbe Kweli Duffer wako Imlany!! Anakumbukumbu nzuri!! Na Ndio maana anakung' ang'ania Kweli Imlany Ni Duffer wako toka mkiwa watoto!! Ila huyu Ancle bado sijajua Ni ndugu kwako au ndugu kwa Imlany au Kuna Nini katikati!! Hapa itabidi  tumuulize  Ancle vizuri!!!""


Walizidi kukagua Tena Ndio wanakutana kichupa kidogo Cha Dawa, walijaribu kukisoma japo maandishi take yalikuwa Ni kichina ila walikutana na 20yrs used!! Walichoamua walichukua simu kubwa nakukipiga picha Kisha walianza ku Google kwenye mtandao ndipo wanagundua ile Dawa ukichomwa inakaa Miaka 20" mwilini pasipokuwa na Kumbukumbu zozote,


Hapo Ndio wakatambua kumbe Imlany Ndio alipewa ile dawa na hapo ilikuwa imefikia Mwisho Ndio maana Kumbukumbu za Imlany zilianza kurudi Mdogo Mdogo baada yakianza kumaliza Nguvu.


Lunnah alimgeukia Junior nakumuuliza.

 "" Hapa Dusky!! Tutafanya Nini?? Kuhusu Imlany!! Mimi naona hivi vitu tulivyovigundua inatakiwa tumshilikishe kila kitu!! Make huu Ni mwaka wa Mwisho Kumbukumbu zake zinarudi, na hatachomwa Sindano nyingine ili zikiwa zinarudi awe ameshajua ukwelii asiharibike kisaikolojia au na sisi tumchome hiki kichupa kimoja kilichobakia ili Kumbukumbu zake ziendelee hizi za Sasa, mpaka zikarudi Tena Ni Kama atakuwa na miaka 45 hivi!!


  "" Hapa ngoja tuone kwanza hili swala tunalimaliza vipi?? Lakini Ancle ndie anayejua kila kitu hapa ngoja nikapokee Documents zinazotumika kwa Imlany!! Na hapa twafanya kumsaidia Imlany nakuweka Mambo sawa!! Harafu kama Ni hivyo Ancle alimuona Shangazi yako, na inaonekana Ni ukumbwani na hapa naona Ancle hapo nyuma Alikuwa na maisha yake, vipi kuhusu maisha ya Imlany yatakuwa wapi sasa???"


  "" Kazi IPO!! Wewe kapokee documents Mimi naelekea nyumbani kwanzaa!! Nikakutane na hiki kivuruge kinachonipatia sumu muda wote!!!""


Waliachana pale, huku Junior alienda kupokea zile documents Nakuanza kuzifatilia, Ndio anakuta Kuna Nyaraka za Kampuni  ile anazidi kukagua Ndio anakutana na jina la baba'ke na Lunnah na jina la Imlany yapo kwenye mkataba na Majina yalisomeka Kama " AHMAD & IMLANY COMPANY CREDIT LTD.


Alizidi kusoma ule mkataba Ndio anagundua kuwa jina Imlany Ni jina la Ukoo Ndio maana alipewa Imlany Kama jina la kurithi, na Upande wa Lunnah!! Ndipo anagundua kampuni lilianzishwa na watu wawili mzazi wa Lunnah na mzazi wa Imlany, kufikia hapo picha Ndio akawa ameipata lakini ikabakia kwa Ancle!!! Who's Ancle??""


Aliamua kufunga Safari nakuelekea kwa Lunnah nakumpatia zile documents, Lunnah alizitizama kwa makini Kisha alijizihilisha vizuri!! Nakubaki akiongea pekee,

  "" Duffer is my Duffer!! Kumbe toka mwanzo tulikuwa TU marafiki hata familia zetu ziliwahi kuwa karibu!! Vipi Sasa kuhusu Ancle Ndio Nani katikati yetu!! Kweli Ndio maana muda wote ulikuwa ukinicare kumbe wanikumbuka!! Huenda Mimi nilikuwa jingajinga TU! Kumbe Wewe Ndio Yule mtoto niliekuwa nacheza nae uliehama kipindi kile!! 

Hata ile siku kwenye gari mbona Mimi sikukumbuka mapema hivyo nilichukulia Ni mtoto Kama mtoto!! Hiyo hiyo siku Ndio Wazazi wako ulitengana nao!!? 

Hata ile siku twasafili Mimi nilijua kwakuwa baba yangu Ni mcheshi walipokutana na Wazazi wako Ndio wakifahamiana siku hiyo kumbe Ndio walikuwa kwenye miradi!!?? Kwanini baba hakunileta kwenu baada ya kuhama nikawa Nakuja kukutembelea!! Angefanya hivyo nisingekusahau?? Kwanini Sasa ulibadili jina wakati Yule mtoto Aliitwa Ibrahimu lakini huku kwasasa waitwa Imlany??!""


Junior Alijua Lunnah kwasasa akili yake iko mbali, Wazo la kwanza lilimuijia kwakuwa Lunnah kashamkumbuka Imlany vizuri na Imlany akishayajua yote akili yake ataihamishia kwa Duffer na yeye kuhusu upendo wake utayeyuka!! Alimsogelea na kumbembeleza.

   "" Lunnah!!! Hebu tuliza akili yako hapa!! Tumalize mkasa wetu!! Naomba leo mtafute Imlany Mwambie kesho aje, uje umueleze kila kitu pasipo kumficha!! Tuone kwa upande wake na yeye atachukua maamuzi gani??""


Junior aliamua kuondoka na kurudi kwake, japo moyo wake ulikuwa na jeraha Sana!! Siku hiyoo hakupata hata usingizi Alikuwa akiongea pekee take TU.

  "" Kweli Dusky nampenda sana!! Sijajua yeye Ana mtazamo upi?? Je, baada yakumueleza Imlany kila kitu atarudi kwake Teena??? au anaendelea na Rayna? Si bora  Lunnah amtakie kila la Kheri Duffer wake na amtakie Ndoa njema??? Hivi Lunnah huwa una feeling Kweli Wewe???""


Hayo yalikuwa Ni baadhi! Ya maneno Alikuwa akijiuliza na kuyatafutia majibu ambayo aliona majibu yatakuwa Ni kwa Duffer na Duffer wake Ndio wangeyajibu!!!??"


Kesho yake Imlany aliitikia wito!! Alifika moja kwa moja kwa Lunnah, Lunnah alimpatia Documents zote Kisha Imlany alizipitia zote!! Baada kujua ukwelii wote kichwa chake kilianza kumuuma.


Alimuita Duffer wake amtafutie Dawa anywe!! Lunnah alimpatia Kisha alimuomba akapumnzike kwanza!! Imlany Alisimama taratibu huku akielekea Chumbani lakini kwa bahati Mbaya alihisi kizunguzungu mwili wake ulilegea nakusababisha kuanguka chini na kuzimia.


Lunnah Alimchukua haraka nakumpeleka hospital akapate huduma!! Alimfikisha nakubaki nje huku akisubili majibu kutoka kwa Doctor.


Muda kidogo Doctor alifika, 

Lunnah alipomuona TU alikimbia kuuliza khari ya mgonjwa wake, lakini Doctor alitoa majibu huku akitikisa kichwa...


   ,,, Itaendeleaa,,,,,,


Usikose Sehemu ya 22.


Kwanini Doctor katikisa kichwa je Ni habari nzuri au Mbaya???


Ungana namimi kwenye page yangu kwakunipatia sapoti ya kulike, comments na kushare kwa Duffer wote🤝✍️🙏.


https://www.facebook.com/groups/263417295228138/?ref=share.

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi