Ikawe Heri 16 - 20

 SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER .                            MTUNZI: TINNER ROBER.                          SEHEMU: 17. 0746638941 (Wtsp).


ANZA NAYO.


Imlany aliitizama ile mikono yake na kuona imetapakaa Damu!! Alichoamua Ni kumpakaa Lunnah usoni kwake Huku Akiwa na furaha sanaaa, Akichekaaa.

  "" Maumivu ya Duffer Ni maumivu ya Duffer Wake!! Na Wewe ukiiona damu yangu itakufanya uumie!! Na hapo tutakuwa tumeshere maumivu so ndivyo ilivyo hivyo!! Duffer wa Kweli!! Hukosa furaha pale Duffer wake anapokosa furaha naomba tuilejeshe furaha tena kwa mchezo huu wa kupakana Damu.!!" ENDELEA....


Hatimae Usiku ulizidi kujongea, Ukawa Ni Usiku mzuri kwao! Kulipokucha Asubuhi simu ya Imlany ilikuwa ikiita, Imlany Alikuwa kapitiwa na usingizi, Lunnah aliiwahi na kuchukua simu na kuangalia aliekuwa akipiga simu, Alikuwa Ni Rayna.

  "" Duffer!! Rayna anapiga simu pokea basii!!"


Imlany alichukua simu na kuipokea, Kisha alisikilizia kwanza ajue Rayna anaongea Nini!!

  "" Mmewangu amka kumekucha jiandae uende kazini!! Hakikisha unafanya mazoezi kwanzaa!! Hicho kitambi naona kinataka kukuotea!!!"


   "" Sawa Mamangu, Ndio naamka hivyooo!! Jiandae pia!! Kumbuka kuchemsha chai kwanza kabla ya kwendaa kazini!!! Okay Baadae Nakupenda Sanaa my wife to be!!"


Lunnah alikuwa akisikiliza maneno yote yaliyokuwa yakiongelewa kwenye simu, Wivu na hasira zilizidi kuutawala moyo Wake!! Aliinuka na kuondoka, lakini Imlany alimuwahi tenaa.

  "" Sorry Duffer!! Hata Mimi naumia Sana!! Nahisi nilichelewa kwako na Wewe ulichelewa kwangu acha nikamilishe zoezi hili nilionalo mbele yangu!! Likikamilika nitazidi kuona Kama Kuna namna nyingine tenaa!!!""


Lunnah hakumjibu aliamka na kujiandaa kuelekea kazini. Siku hiyo alifika kazini nakuingia kwenye ofisi ya Ancle!! Alifika nakuanza kufanya upekuzi Huku akitafuta kitambulisho Cha Imlany!!


Lakini kwa bahati Nzuri alipata kile kitambulisho, alichukua na kulitizama kwa Makini.

  "" Mbona huyu Ni baba na mama na huyu Ni Mimi kabisaa!! Inakuwaje Tena alipatiwa Imlany??""


Wakati Akiwa anaendelea kukitizama mara Imlany aliingia pasipo hodi!!

  "" Kwanini umeniacha Duffer!! Ulitaka leo nitembee peke yangu njia nzima!! Hayaa!! Kwenye ofisi unatafuta Nini Tena???"


Lunnah alibaki akitoa mimacho tuu Huku mikono yake Alikuwa kaiweka nyuma, Alizidi kurudi nyuma na kukiangusha chini kile kitambulisho pasipo kujua Imlany.


Imlany nae alizidi kumsogelea akifikilia Lunnah kaficha Nini? Baaadae alifika Mwisho na kumkaribia kabisa!!

  ""Duffer!! Umeanza kufanya Mambo kimya kimya! Hata Mimi Duffer wako umenificha Kweli!! Vipi umepata kitambulisho??""


Lunnah alibaki akikodoa TU,

 "" Hapana Duffer!! Sijakipata na hicho Ndio nakitafuta hapa!!!"


Imlany alimshika Shavu Lunnah!!

 "" Hakika Yule mtoto!! Alikufanana kila kitu Hadi shavuu Ni Kama yeye!! Ila nikimpata kwasasa atakuwa Ni Duffer wangu! Mrithi wa Rayna!!! Ila Hata Wewe Ni mrithi!!!" Imlany Aliamua kuondoka na kumuacha Lunnah akizidi mtizama.


"" Hapa Nina Mtihani mbona!! Tayari nishajua huyo mtoto Ndio Mimi!! Mbona Mimi sikumbuki hayo yote!! Au kwenye huo utoto nilikuwa jingajinga Sana!!" Vipi Duffer wangu siku akiiona hiki kitambulisho mahusiano yake na Rayna yatakuwaje!!!??"


Aliamua kufunga ile Ofisi ya Ancle na kutoka nje, Lakini ile anatoka tu, Ancle Ndio na yeye anaingia. Lunnah alibaki akitetemeka na kumfanya mikono yake ilegee na kuangusha kile kitambulisho.

  "" Ancle Shikamoo!!! Samahani Ancleee, Mimi nilikuwa nata......!!"


Ancle alimnyamazisha kwa kumziba na mkono, Kisha aliinama nakuokota kile kitambulisho.

   "" Lunnah!!! Ancle!!! Hivi bado mnanitafuta Nini Kwanza!!! Kila kitu nimekufanyia Lakini hauliziki, Ni Nani kukwambia uingie Ofisini kwangu na uchukue hiki kitambulisho!!!??"


""" Ancle!! Mimi niliingia kuchukua file Lakini wakati nikiwa nachukua nikaona kitambulisho kina picha ya wazazi wangu nikawa nimekichukua Kwakuwa kinanihusu Mimi!!!""


"" Wewe mtoto!! Marufuku nikusikie Tena unazoea vitu vyangu!! Laah!!! Hivyo nitakufanyia kitu Mbaya!! Mimi kuua sioni Mbaya!!"" Kisha Ancle aliondoka.


Lunnah Aliamua kumuita Ancle.

 " Ancle Samahani Kuna picha iko Hapa!! Huenda Unaweza ukawa wafahamiana nae!!!


Ancle alisogea nakuanza kuiangalia ile picha, ilimfanya asituke kidogo.

  "" Wewe!! Wafahamiana nae huyu!! Mbona Ni mama Ennah!! Unamfahamu??""


Lunnah  alifunga simu yake na kuondoka huku akimjibu Ancle.

  "" Wewe si unanitishia maisha Mimi!! Mama Ennah!! Namjua vizuri ila ulitaka nikwambie Sehemu alipo nirudishie kitambulisho Cha Imlany harafu Mfanye Imlany akumbuke Mambo ya nyuma!! Kama utaweza nitafute kwa muda wako na Mimi nikutafute kwa muda wangu!!!"


Ancle alibaki katulia tulii, Alichukua kile kitambulisho nakukiangalia kwa makini.

 "" Lunnah!! Lunnah!!! Huko unakotaka tufikie siyo kuzuri!! Tangu uje kwenye familia yangu umekuwa kichomi Sana!! Ngoja nitafanya kitu kwaajili yako naimani hautarudia Tenaaa!!!""


Ilikuwa Ni siku nyingine Tena Imlany Alikuwa Tayari keshaondoka nakuelekea kazini kwakee!! Siku hiyo Lunnah alipigiwa simu majira ya Usiku akutane na Junior, Aliwasha gari yake na kuelekea kwenye hiyo hotel.


Wakati Akiwa Njiani alifika Sehemu na kukuta Kuna gari imepaki Njiani, Aliamua kusimama na kwendaa kuchungulia kwanini wameziba njia, Ile anashuka TU hivi Kuna watu walitokea na kumpulizia Madawa Kisha walimchukua na kuondoka nae nakuelekea Sehemu isiyojulikana..


Baadae walifika kwenye msitu mrefu na kumshusha Lunnah Kisha walimfunga kwenye mti mkubwa na kumuacha, Kesho yake kulipopambanzuka Lunnah Ndio anaamka huku akihisi ubaridi wa tofauti!! Aliangalia Huku na kule akizidi kuona Ni miti mikubwa ikimzunguka!! Alifumba macho nakufumbua Tena akizania Ni Ndoto anaota!!! Ndio anasumbuka tukio la Jana ilivyokuwa Baada ya kushuka kwenye gari Ndio alitekwa.


Alianza kupiga kelele huku akizidi kuita 

 "" Duffer!!! Duffer!! Duffer!!! Duffer!!! Msaada njooo unisaidie!! Nakufa huku!!!"


Muda kidogo Ndio anatokea kijana mmoja kajazia kifua Kama baunsa hivi.

 "" Duffer!! Duffer!!! Duffer!!! Leo hamna Cha Duffer!! Duffer wako leo Ndio Mimi!!! Namimi Ndio nimekabiziwa nifanye kitu chochote kitakachonifaa!!!""


Turudi huku kwa Junior siku hiyo alizidi kumgonjea Lunnah pasipokufika, mwishowe Aliamua kuondoka na kuelekea Nyumbani kwake, Siku hiyo Aliamua kuomba ruhusa kazini na kupumzika huku akiwa kawasha redio akisikiliza matukio na akizidi kulalama kwa kitendo Cha Jana alichomfanyia Lunnah.

  "" Lunnah!! Sijui Mwanamke gani!! Kumpenda kwangu ananidharau TU, Hata nikimuhitaji anaona Nakuja kumwambia Maada ileile!! Leo ilikuwa asaign mikataba yake na hati zake upyaa serikali ianze rasmi kufatilia Ila hakuja tenaaa!!"""


Muda kidogo Kuna Message iliingia What's up na kumfanya asituke kidogo, Alikuwa Ni rafiki yake Anord alimtumia Ujumbe.

  "" Oyoo Jeder!! Umempeleka wapi yule Manzi Lunnah, naona unatafutwa huku na kituo Cha Police!! Vipi umeoa jamaaa!!??""


Junior kabla hajajibu alisikia taarifa ya habari, 

  "" Director wa BancABC! Atekwa na watu wasiojulikana, na inasadikika kuwa Alikuwa akielekea kwenye  Hotel Moja ya 🌟 star Hotel!! Kwa maelezo ya mwisho simu yake ilikutwa IPO chini ikiwa na mawasilino ya no 074663.. ikiwa imesaviwa My Dusky,, Kitengo Cha mawasilino wamejaribu kufatilia ile namba na kumjua mtumiaji wa hiyo namba ni Junior Ahmad ambae anafanya Kazi kwenye Jeshi la wananchi (JKT) akiwa na Nyota tatu!! Leo jioni atakuwa akihojiwa.


Junior Baada ya kusikia hivyo Ndio anatambua kuwa Lunnah kumbe hakufika makusudi!! Atakuwa ametekwa, Aliingia ndani nakubadili mavazi nakuamua kuelekea Moja kwa Moja kituoni, Ile anatoka tu anakutana na police wakiwa tayari wamefika kumchukua, Junior hakuwa mbidhi aliongozana nao Moja kwa Moja Hadi kituoni.


Huku kituoni Junior alikuwa akihojiwa kwa maswali kadhaa, Junior alielezea ilivyokuwa nakusema kuwa yeye hahusiki kinachotakiwa Ni kujua Lunnah yupo wapi??


Police Baada ya kujilizisha na majibu walimuomba Junior atabaki ili azidi kuwasaidia kwa upelelezi Zaidi.


Huku kwa Imlany taarifa zilimfikia na kumfanya ampigie Junior Huku akiwa kamind Kweli!!

  "" Junior!! Umeamua haitoshi TU kuniona Mimi nakuwa na Duffer wangu karibu!! Kwasasa si umeamua kumuoa kwakutumia Nguvu ya Kazi!! Nakwambia siku akijua kuwa Wewe Ndio mhusika ndio utajua kuwa Duffer nae mkorofi huwa hapendi dharau!! Hata hivyo Duffer wangu anampenda Duffer wake siku zote!! Naomba umrudishe haraka!!""


Huku kwa Junior, Aliamua kumkatia simu Kisha alichukua maji na kunywa kwa pupa Sana huku akijaribu kufikilia Mambo mengi.

  "" Ninani kamteka Lunnah!! Kwanini hii kesi na lawama zote zinamuangukia yeye!! Hili dili limesukwa na inaonekana huyo mtu alitambua tangu mwanzo kuwa Lunnah anakuja kuonana na Mimi!! Hapa lazima nijue hatima ya swala hili!!""


Junior Alichukua gari yake nakuelekea Sehemu ya tukio lilivyofanyika!! Alifika nakuangalia Kisha aliondoka na kuelekea Moja kwa Moja kwenye gari ya Lunnah aliyokuwa akiitumia siku hiyooo! Alifika nakuangalia camera iliyokuwa kwenye gari aliweza kuona kijana mmoja kwa mbali Sana muda ule alionekana akimchukua Lunnah kutoka kwenye gari nakumuingiza kwenye gari yake!!


Alichukua kile Kipande Cha mkanda nakurusha kwenye simu yake na kuwasha gari take na kuelekea kwenye kitengo kimoja kilichokuwa kikiitwa GYM GUY'S!! Sehemu hiyo ilikuwa Ni maarufu Sana kwakufanyia mazoezi.


Junior alifika pale nakuangalia mazoezi yaliyokuwa yakifanyika hapo, Baadae aliona Kuna vijana walifika pale na kushuka kwenye gari la kifahari Kisha walibadilisha mavazi Yao nakuvaa mavazi yakufanyia mazoezi, Junior alikuwa aliwatizama kwa makini akijaribu kufananisha sura zao na ile Short Video aliyokuwa kaichukua, lakini Kila alipozidi kuwatizama walianza kusemeshana wao kwa wao.

  "" Vipi huyoo jamaaa! Mbona muda wote anatutizama TU! Isije kuwa Ni mpelelezi Hapa tufanye kuondoka naona mahali Hapa SI salamaa!!""


Walianza kuondoka mmoja Baada ya mwingine, Hapo hapo Junior alijua tayari wahusika wamepatikana!! Alichoamua Ni kuimaiki plate no. Ya gari Kisha sura zao alizikalili, Kisha aliendelea na mazoezi pasipokuwa na pupa ya kuwafatilia haraka hivyooo!!"


  ,,,,,,, Itaendeleaa,,,,,,,

,

Usikose Sehemu ya 18.


Junior anaenda kufanya kitu gani Baada ya kuwajua wahusika????


Like comments and Share.

SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER .                            MTUNZI: TINNER ROBER.                          SEHEMU: 16. 0746638941 (Wtsp).


ANZA NAYO.


Kuna siku Moja Ancle alinikuta nakiangalia kile kitambulisho akawa kaniomba na hakunirudishia Tena hata nilipomuomba aliniambia kimepotea. Na hicho ndio kilichokuwa kinanisaidia, Kila nikikitizama Ndio nakumbuka sura ya yule mtoto ukweli mmefanana nae sanaaa..... ENDELEA.


  "" Duffer!! Subili kwanza Kuna kitu nataka nikuulize kwanza!! "" Unamaanisha kumbukumbu zako za Sasa sio Kama zile za Mwanzo!!??""


  """ Ndo hivyoo!! Lakini Siku nikipata kile kitambulisho naamini kumbukumbu zangu zitarejea vizuri!! Ila kwakuwa Sina Ndio maana maisha yangu yamebadilika Sanaa!! Mwanzo nilipomuona yule mtoto mpaka nakua Ndoto yangu kubwa ilikuwa Ni kumtafuta yeye ili nimuoe lakini kwasasa Sina kumbukumbu yoyote mpaka nimeamua kumtafuta Rayna Ndio achukue ile nafasi yake!!


  "" Unasema kuwa yule mtoto alifanana na Mimi!!! Vipi Kama Ndio nitakuwa Ni Mimi Utanioa!!??"


   "" Yaani!! kwasasa Sina Uhakika Zaidi!! Kuwa yule mtoto wa kwenye kitambulisho Ndio Wewe ila mmefanana Sana!! Kwakuwa Sina Uhakika Acha uwe Duffer wangu wa karibu huenda nikizidi kukaa na Wewe kumbukumbu zangu zitarejea tenaa!!!"


   "" Kwahiiyo kwa sasa Ancle unaishi nae vipi?? Harafu Kwani Ancle Hana Aunty, na watoto wake wako wapi au familia yake iko wapi?? Vipi Kuna ndugu wengine kwa upande wa Wazazi wako wafahamiana nao!!!?""


   "" Lunnah!!!! Tangu siku ile niwe mikononi mwa Ancle, sijawahi sikia Kama ndugu wamekuja kutusalimia!! Wala watoto wa Ancle!! Lakini kuhusu Aunty, Ancle aliwahi kuniambia waliachana miaka ya Nyuma akawa kaondoka na mtoto mmoja!! Ila kwa zamani Tena Alikuwa na mke akawa kafariki Ndio akamuoa huyo mwenye mtoto lakini baada TU ya kujifungua alikimbia na kwendaa kuishi sehemu isiyojulikana ila aliondokaga na mtoto wa kike na jina la mtoto Ancle alimuita Ennah!! Kama hakubadili jina Basi mtoto huyo atakuwa Ni Ennah!!.


  " Duffer!! Umesema kuwa Auntie alikimbia na mtoto na huyo mtoto Aliitwa Ennah!!? Kwanini Sasa Aliondoka??"


  "" Maongezi ya Ancle Alikuwa akimtuhumu kuwa Ancle Hajatulia anapenda wanawake wadogo wadogo!! Lakini nikimuuliza Ancle anasema kuwa Ni Wivu TU ulikuwa ukimsumbua Auntie, Watoto wenyewe walikuwa Ni wafanyakazi wa kampuni!!!""


  "" Mimi Nahisi jaribu kuongea na Ancle!! Huenda Kuna kitu anakijua kuhusu Wewe ndio maana hata alipoona kile kitambulisho kinakurudishia kumbukumbu akaona akunyanganye!! "" Daaah!!! Pole Sana Duffer!!"  Naona Ni afadhari yangu Mimi Ndio najua kilichoendelea na nikipata haki yangu nitasahau haya yote!! Kitakachobakia nitaenda pambana na Shangazi TU!! Ila kwako inakuwa ngumu hata kumbukumbu unazoishi nazo kumbe si zako tenaaa!! Daaah!!! Sijui nikuulize.....""


   "" Uliza TU!!""


   "" Bado unapenda kumbukumbu zako za nyuma zirudi?? Mimi naona uendelee kukaa kwenye hizi kumbukumbu za wakati huu ulizo nazo make zile za nyuma umekaa nazo ukiwa Ni Mtoto Mdogo!! Na hizi umekaa nazo kwa muda mrefu naukiwa wajitambua!!!""


  "" Hapana Lunnah!! Natamani nianze mwanzo kabisa!! Ili nikumbuke hata Mali za Wazazi wangu!! Nijue ndugu zangu wa karibu bado Nina mama zangu wadogo Lakini hata siwakumbuki!! Na Cha zaidi nataka nimtafute yule baba alieniachia kitambulisho, nimtafute na Yule mtoto anaefanana na Wewe!! Moyo wangu unawiwa kumtafuta yule mtoto nahisi kwa Sasa atakuwa Ni mbiti mkubwa mkubwa Kama Duffer!!""


  "" Ayaaa!! Ni sawa nahisi Ni Mimi wa kwenye kitambulisho!! Kwakuwa Wewe Ni Duffer wangu na Mimi napenda furaha yako iwe yangu nitajitahidi kutafuta kile kitambulisho na Mimi nimuone huyo Mtoto ninaefanana nae!!" Na Mimi nitakusaidia kutafuta chanzo Cha Wazazi wako kuuwawa Kama mnavyoshilikiana na Mimi kupata Mali zangu!!!!


Muda kidogo Mdada wa kazi Alifika sebuleni na kumhitaji Kuna mgeni wake yupo Nje anamsubili. 


Lunnah alisimama ili akamuone mgeni wake, lakini Imlany alimsihi aachane nae, alimwomba mdada wa kazi amwambie apite Ndani.

  "" Nahisi itakuwa Ni wateja wetu!! Wametufata Hadi Nyumbani angekuwa mtu wa kazini si angeingia wewe Mwache!! Nikusaidie kumjibu Mimi Ndio nimesababisha usirudi kazini!!"


Muda kidogo Mgeni anaingia sebuleni, walipomuona tu walibaki wameduwaa wote!! Hasa kwa Imlany Alikuwa akimumind Sana Junior!!. Lunnah ilibidi amkalibishe mgeni Wake.

  "" Junior!! Karibu Sana!! Sikujua Kama Ni Wewe!!?""


  "" Ahsante bhana!! Naona ulijua Ni wadeni zako!! Okay!!" Junior aliangalia sehemu ya kukaa akaona sio Mbaya akakae karibu na Lunnah make alikaa kwa Imlany anaweza tupiwa ngumi, Bora akae kwa Lunnah amkomeshe Imlany.


Imlany Baada ya kumuona Junior Kakaa na Lunnah, alimkata Hilo jicho Kisha alichukua remote na kuwasha Tiv ili aendelee kuangalia michezo!!""


Huku kwa Junior sitori ziliendelea..

 "" Jana nilifika Ofsini kwako kukutembelea!! Lakini sikukukuta niliambiwa na wafanyakazi wako Umetoka Wewe na Boss wako na hamkurudi tenaa!! Nikaona leo nifike nyumbani!!"


   "" Sasa Junior!! Ndio ujebila kuwasiliana na Mimi!!? Ani kimya kimya tu upo hapa!!""


  "" Kwani Kuna Ulazima wa mimi kupiga Simu!! Au unamuogopa Imlany?? " Hata hivyo Imlany na yeye Ni Duffer wako tu, na Ana maisha take na yeye kaja Kama Mimi nilivyokuja!! Harafu mkewe hana Wivu!! Ningekuwa Mimi jamanii daaah!! Na harusi imekaribia angekuwa hatoki!! Unajua kilichonileta Hapa Ni Wivu TU  ndo maana nikafika hapa."


   "" Wewe Unakuwa na wivu Kama Mimi naniyako kwanzaaa!! Nikajua hata umeniletea habari za Mahakamani kumbe Ni hicho!! Ayaa!! So ushajua tayari!! Basi uondoke!!!""


   "" Sasa Niondoke!! Niende wapi? Wewe Ndio unanifanya!! Mimi nizidi kukufatafata tenaaaa!! Juzi Ndio ulinichanganya kabisaa kwenye Lile Korch!! Kila nikilala nakumbuka vizuri!! Kwanini nikae mbali na Wewe!! Hapa nawaza kuhamia unipe chumba changu lakini kiwe humuhumu ndani Ndio nilichoamua kukueleza!!""


Imlany Japo Alikuwa amewasha Tiv lakini akili Yake ilikuwa nikusikiliza kile kilichokuwa kikiongelewa Japo Alikuwa hasikii vizuri maneno kutokana na sauti aliyokuwa kaweka lakini hata hivyo na wao walikuwa wakitumia sauti ya chinichini.


Imlany aliamua kusimama na kuelekea Chumbani na kwendaa kupumzika!!


  "" Yaaani!!! Junior'' Unaongea mno hapa Hadi Imlany kakeleka kaenda kulala!!!"


   "" Wewe Hujui tu, Najua Imlany anayewivu juu yako na anakupenda Sana!! Hapa nilikuwa naongea Alikuwa akinipiga Hilo jicho la chinichini!! Lakini tayari keshafanya maamuzi Naomba hiyo nafasi yake kwako aniachie na Mimi!! Hata hivyo Nina moyo wakupenda pia na Mimi!!""


   "" Mtajua wenyewe!! Nikuombe tu, Mwache Duffer wangu!! Kwa sasa kapumzika na bado Ana Mambo mengi Sana kichwani kwake!! Mimi Ndio natakiwa kumpatia faraja harafu na Wewe wamuongezea huzuni!!;""


   "" Okay!! Sawaa kampatie faraja, lakini Duffer wako kwa Sasa Ni wa Rayna!! Hapo utakuwa waingilia Mambo yasiyokuhusu ila Mimi Nilikuja kukuona tu, Nilimisi kukuona. " Zaidi nikutakie Usiku mwema ila kwenye kuwaza kwako Muwaze na Junior kuwa Ni mwanaume anayekupenda Sana!!!""


Lunnah Baada ya kuachana na Junior!! Aliondoka na kuelekea Moja kwa Moja Hadi Chumbani kwa Imlany. Alimkuta Imlany kapitiwa na usingizi, Alisogea Hadi kitandani na kukaaa huku akizidi kumtizama Imlany Usoni Kisha alichukua kitambaa na kumfuta jasho.

  "" Duffer!! Najua Ni kiasi gani unaumia!! Ila nitajitahidi kutafuta Suluhisho uwapate ndugu zako!! Ila kuhusu Kumbukumbu zako kurudi Hilo sitakubaliana nao!! Najua unahangaika Sana kurudi upya na kuanza Mwanzo!! 


 "" Muda wote Najua bado unatamani Sana kupata kile kitambulisho Nia yako Ni juu ya yule mtoto ambae kafanana na Mimi, Je Kama Kweli utakipata na ukathibitisha kuwa Mimi ndie yule wa kwenye kitambulisho utafanyaje!! Kabla hujapata kile kitambulisho itabidi Mimi Ndio nianze kukipata ili nijithihilishe kuwa yule mtoto Ni Nani!! Lakini sitakupatia!!"


  "" Itoshe kusema tu, Duffer!! Wangu ninampenda Sana ila kwasasa Sina namna tayari nafasi ya kumpenda kimapenzi haipo tena!! Hapa Nina nafasi ya Duffer TU!! Ila ninae wivu juu yako na kwenye harusi sitafika tenaa!! Nitafanya Kama siku yenyewe ambavyo sikufika kanisani kwenye Uchumba wako!! Japo nilikufariji nitafika ila sio hivyo nitaandaa zawadi kwaajili yako tu.


 "" Muda mwingine natamani!! Hata niondoke nikae mbali na Wewe!! Ili nikusahau tu, lakini nimeshidwa Sina budi kukutakia baraka njema kwa kusema; " Ndoa yako, " IKAWE  KHERI MY DUFFER" Nitakumisi Sana kwa Kila  Changamoto nitakayopitia kwenye mahusiano yangu yakawe Ni ya Kheri tu.


Lunnah alimaliza kuongea hivyo Huku machozi yakitiririka nakuangukia Usoni kwa Imlany. Imlany Alisituka nakukodoa macho!! Kisha Aliamua kumkumbatia Lunnah kwa hisia Kweli Kisha alumjibu.

   "" Hayo yote Ni sawaa!! Lakini Mimi pia natamani siku ukipata kile kitambulisho  nioneshe ile picha nimjue yule mtoto Ni Nani!? Hivyo vingine vyakujua Wazazi na Ndugu zangu sizitaki tena!! Hapa tayari Nina maisha yangu nanitazidi kuendelea nayo hivyo hivyoo hata kuhusu Kujua Ancle Ni Nani?! Sitaki Tena kujua ila nataka ile picha nijue yule mtoto Ni Nani?? Na yupo wapi kwa Sasa!!!??"


Lunnah Alisituka na kumuachia Imlany Huku akijiuliza maswali mengi.

  "" Kumbe hukuwa umelala Kila kitu ulisikia!! Mbona sio Siri Tenaa!! Mimi nilijua naongea kimoyomoyo kumbe nilisikika!!""


Lunnah Aliamka na kushuka ili aelekee Nje, Lakini Imlany alimuita.

  "" Najua Lunnah!! Ni kiasi gani unaumia hata huko unakoenda kulala utazidi kuumia Zaidi!! Njoo unielezee hisia zako ulivyoongea nikiwa nimelala tuchukulie Kama ilikuwa Ni Ndoto TU!! 


Imlany Alisimama na kumsogelea Lunnah!! Kisha alifika na kumkumbatia kwa nyuma nyuma.

  "" Moyo wangu na hisia zangu zote zipo kwenye taswira ya yule mtoto!! Japo mmefanana nae Kweli!! Ndio maana nilichoamua ni Hisia kuzihamishia kwa Duffer TU! Natamani nikumbuke hata theruthi ya Kumbukumbu nikiwa kwenye gari siku ile nikiwa na yule mtoto!! Je? Waweza nikumbusha??"


Lunnah ilibidi Amgeukie Imlany, make aliona Kama akili zake zimeruka Aliamua kumsukuma na kuangukia kwenye kitanda, Lakini kwa bahati Mbaya akawa kajibamiza kwenye paji la uso. Imlany aliinuka Huku mkono wake wa kulia alikuwa kashikilia kwenye paji la uso Huku akigugumia maumivu.

  "" Hiyohiyo michezo uliyonichezea leo!! Hata yuleyule mtoto siku yenyewe alinisukumia kwenye seat nikawa Nimeumia Sehemu Ile ile, na Siku yenyewe ulinibamiza kwenye mlango nikawa Nimeumia kwenye paji la uso!! Mimi naona Yule mtoto awe Ni Lunnah TU!! Ila nitakuwa namuita Lunnah wa utotoni mpaka pale nitakapopata kitambulisho nikijithihilisha sio yeye!!!  Nitaacha kukuita jina Hilo!! Na ukitaka nisikuite hivyo tafuta kile kitambulisho nikizibitisha sio Wewe nitaacha kukuita hivyo majina yetu yataendelea, "Duffer!! Ila kwa Sasa una majina mawili. " Lunnah wa utotoni na Duffer""


Imlany alimaliza kuongea Kisha Aliamua kutoa ule mkono na kukuta una damu, Nakuanza kulalamika tenaaa.

  "" Duffer umenitoa Damu!! Duffer mkorofi!! Hunithamini tenaa.""


Lunnah Ndio anajua kuwa Duffer wake kaumia, Aliamua kumsogelea na kuanza kulia tenaa.

 "" Samahani Duffer!! Sikupanga nikuumize hivyoo!! Harafu mbona Ni Wewe umetaka Mimi kukusukuma kidogo hivyo Ndio uumie Kweli!!


Imlany aliitizama ile mikono take na kuona imetapakaa Damu!! Alichoamua Ni kumpakaa Lunnah usoni kwake Huku Akiwa na furaha sanaaa, Akichekaaa.

  "" Maumivu ya Duffer Ni maumivu ya Duffer Wake!! Na Wewe ukiiona damu yangu itakufanya uumie!! Na hapo tutakuwa tumeshere maumivu so ndivyo ilivyo hivyo!! Duffer wa Kweli!! Hukosa furaha pale Duffer wake anapokosa furaha naomba tuilejeshe furaha tena kwa mchezo huu was kupakana Damu.!!"


   ,,,,,,,, Itaendeleaa,,,,,,,,,


Usikose Sehemu ya 17.


Raha ya Duffer Ni kufurahi na Duffer wake kwa pamoja. Siyo yakukosa simulizi hii, Tuungane wote kufurahi na Duffer wetu!!


Kwa kulike, comments, na kushare...

SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER .                            MTUNZI: TINNER ROBER.                          SEHEMU: 18. 0746638941 (Wtsp).


ANZA NAYO.



Walianza kuondoka mmoja Baada ya mwingine, Hapo hapo Junior alijua tayari wahusika wamepatikana!! Alichoamua Ni kuimaiki plate no. Ya gari Kisha sura zao alizikalili, Kisha aliendelea na mazoezi pasipokuwa na pupa ya kuwafatilia haraka hivyooo!!" ENDELEA....


Ilikuwa Ni siku nyingine tenaa. Junior siku hiyo alikuwa akiwafatilia wale jamaa watekaji, Siku hiyo Aliamua kudili na kijana mmoja alikuwa akimfatilia, kijana huyo alikuwa kakaa hotelin akitumia kileo chake, Junior Alifika pale na kukaa kwenye meza yake Kisha alisalimiana nae na kuagiza na yeye kinywaji Huku wakizidi kubadilishana Mawazo.

  "" Samahani nimekuingilia kwenye seat yako!! Upo na Mwenzio???""


  "" Hapana bhanaa!! Nareflesh mind since Unajua leo weekend!!!""


Junior'' Alitoa picha ya Lunnah nakuiweka Mezani Kisha alimuuliza.

 "" Wamfahamu huyu Mdada!!!""


Jamaa Baada ya kuona picha ya Lunnah ilimfanya asituke kidogo Huku akitikisa kichwa chake Huku kajawa hofu!!!

  "" Aah aaa!! Hapana!!!"


  "" Okay!!! Naomba unisaidie kumtafuta popote pale alipo nijulishe! Na Hapa nataka majibu jioni!!! Kesho Asubuhi jiandae kunipeleka alipo!!"


Junior Alitoa kitambulisho chake Cha kazi na kumuonesha, Kisha aliondoka pale nakumuacha akiwa kwenye sitafahamu!!!"



Huku kwa Lunnah!!! Muda wote alikuwa akilia Huku akimtaka Duffer wake amsaidie!! Baadae kidogo aliona wale Nyemela wamepumnzika!!! Alitafuta namna yakujisaidia ili atoke pale!!! Alihangaika kufungua kamba hatimae akawa kafanikiwa!!


Alisogea pale Huku akinyata taratibu nakuanza kupekua mabegi Yao akitafuta simu, baadae alifanikiwa kuchukua Simu nakutokomea msituni akitafuta njia yakutokea. 


Alifika sehemu nakuandika namba ya Imlany ili amjulishe kilichotokea, Kila Alijaribu kupiga anakuta namba busy!! Hasira zilimzidia nakuanza kutoa maneno makali.

  "" Et Duffer!! Duffer! gani!? Hajali kuhusu Duffer wake amepatwa na Shida gani?? Tenaa Sahiii Wewe sio Duffer tena!! Ancle yako Ndio ananifanya niteseke polini!! Duffer I heart you!!""


Lunnah alikuwa akimlalamikia Imlany, pasipo kujua Imlany muda huo alikuwa akimkolomea Junior kuwa yeye Ndio anahusika na muda huo alikuwa busy kuongea na Junior!! Baadae alimpigia mjomba Wake akimsihi azifi kumtafuta Lunnah!! Ancle na yeye alimhakikishia katuma majeshi yakumtafuta Kila Kona.


Lunnah Aliamua kutafuta namba nyingine na kupiga tenaa, Ndio anakumbuka kabla ya kutekwa alikuwa anaongea na Junior, Alijaribu kukopy namba Lakini ikawa sio sahihi ikabidi Tena aijaze upya Ndio anapokea Junior akiwa kwenye gari!! Siku hiyo Lunnah!! Jina la kwanza alikuwa akiita!!

  "" My Dusky!! My Dusky!!! Njooo unisaidie Mimi!! Nipo huku polini!! Leo nitakufa kwa wanyama wakali!! Tazama kiza kimeingia na Hapa nimewatoroka sijui hata niwapi hapa!!!"" Lunnah alizidi kulia.


  "" Usijali!! Tayari nimeshakuona nipo pembeni yako!! Nope robo saa tulia hapo hapo Nakuja Sahiii!!!


Junior Baada ya kuongea na Lunnah alibaki akifurahi Baada ya kusikia leo kwa Mara ya kwanza anaitwa "My Dusky" Alimtizama kijana aliyekuwa nae kwanza.

  """ Kwanini Ancle!! Kaamua kumfanyia hivi Lunnah!!! Harafu na nyie mnapewa kazi!! Mnafurahia TU!! Hamjui mnajiingiza kwenye Shida!! Kosa nikute Lunnah kazurika nitafawafanyia Mbaya!!! 


Junior aliona anazidi kuchelewa!! Alishika usukani nakuondoa gari kwa spid, Walifika Hadi kwenye msitu Kisha walishuka!!!

  "" Mbona husemi!! Mlimfunga wapi Lunnah!!??"


Jamaa aliongoza njia Hadi kufika sehemu walipokuwa wameweka kituo, Lakini walishangaa Baada ya kukuta hamna mtu. Ilibidi waingie polini huku wakizidi kumtafuta Lunnah walijaribu kumpigia Tena Lunnah akawa hapatikani Network ilikuwa chini Sana, walianza kumtafuta kwakubashili huenda atakuwa huku au kule.


Kadili walivyozidi kumtafuta Ndio walifanikiwa kuona Mwanga wa simu kwenye kichaka!! Kumbe Lunnah alikuwa tayari kapitiwa usingizi na simu yake ilikuwa ikiita walikuwa Ni wale watekaji wakimpigia Simu huku wakizidi kumtafuta!!!


Junior Alifika pale na kukaa pembeni kwa Lunnah huku akizidi kumtizama!!! Alimuonea Huruma Sana kwa baridi iliyokuwa imempiga na mwili wake ulikuwa umekwaluzika kwa miti!! Alivua koti lake nakumfunika!! Huku Lunnah Ndio anasituka usingizini akiwa anaweweseka huku akiomba msaada!!

  "" Duffer!! Duffer!!! Naomba nisaidie!! Mwili wangu unauma!!! Kichwaa nacho kyanigonga!!"


Junior Alijisikia vibaya Sana!! Alimtizama Yule mtekaji aliyekuwa kaongozana nae alimpatia ile Simu nakumsihi, Awapokee wenzake Kisha alimwambia.

  "" Nenda ukawe huru!!! Najua umefanya haya yote kisa Ni Njaa na khari duni ya maisha!! Kwakuwa Sasa nakujua vizuri naomba usirudie tenaa!! Nitazidi kukutembelea!! Fanya maamuzi ukaachane na hii Kazi!!!"


Jamaa alitoka pale asiamini Kama angenusurika kwenye mikono ya Junior!! Make muda wote baada yakupewa kazi na Junior siku yenyewe ilibidi aende Nyumbani nakuiaga familia yake kuwa kwasasa atakuwa kwenye kifungo Cha maisha baada yakuona deal limefeli, familia yake iliingiwa kwenye huzuni Sana!! Nakumuomba ajisalimishe TU make Haina jinsi!! Kwa Junior alikuwa akimfatilia Sana baada ya kuona katii amri Kesho yake aliamua kuja mwenyewe kujisalimisha aliona Ni mtu mwema, Ndio siku hiyo akaamua kulipa fadhira kwaaina hiyo!!!"


Baadae Junior Aliamua kumbeba Lunnah nakumpeleka kwenye gari yake, muda huo alikuwa bado kalala, ile anakuja kusituka alishangaa kuona yupo kwenye mikono ya Junior''

  "" Junior!!! Niwewe tenaaa!! Nilijua hautakuja kunisaidia hata pale unaongea nilijua wanienjoy!! Kiza kilipotanda niliogopa Sana nikawa nimefunga macho yangu nisione kitu chochote kitakachopita mbele yangu!!! Kwanini Lakini umenisaidia???""


Junior hakumjibu Zaidi yakumbeba nakuendelea kusogea kwenye gari!! Alifika nakufungua Mlango Kisha alimulaza kwenye seat nakuwasha gari akisogea Mdogo Mdogo.


Alifika mbali kidogo alimuona yule Jamaa akiwa anatembea kwa hofu Sana huku akiwa kashikilia viatu vyake mkononi akiwa Attention kwa lolote Lile likitokea atoke mbio. Junior Alifika pale nakufunga break Kisha alimruhusu aingie kwenye gari!!


Lunnah alikuwa akishuhudia Junior anavyoonesha wema kwa yule mtu!! Ile kaingia kwenye gari Ndio anageuka nakukutana na Sura ya jamaaa Ndio anapiga kelele.

  "" Junior!! Mtu Mbaya huyu!! Atatuteka!!! Nayeye Ni miongoni mwa wale watekaji!! Muache Tafadhari!!""


Junior Aligeuka nakumpiga jicho Lunnah, Lunnah nayeye sambamba Ndio anakutana na uso kwa uso na Junior Ilibidi abaki kaachama Kwanzaa!!


Hatimae walifika Hadi mjini, Junior alimpeleka Hadi Nyumbani Jamaa!! Kisha Aligeuza gari nakuelekea kwakee!! Alifika nakushuka kwenye gari Kisha alisogea nakumfungulia Lunnah Mlango huku akimuamuru ashuke.


Lunnah alijivuta taratibu huku akijaribu kushuka, Lakini alipojaribu kukanyagia miguuu yake ilikuwa ikimuuma, Junior alisogea pale nakumbeba Hadi ndani!! Nakumlaza sebuleni!!


Aliingia Jikoni nakuandaa chakula!! Baadae alimchemshia maji yakuoga, Alimpelekea Hadi bafuni!! Nakumuacha akioga. Huku kwa Lunnah baada ya kumaliza kuoga alibaki ametulia TU huku akiwaza nguo zakuvaa make zile zilikuwa zimechafuka. 


Alisikia Mlango ukigongwa, alifungua huku akijificha kwenye Kona, Junior alimrushia Nguo.

  "" Leo utavaa nguo zangu!! Kama ile siku nilivyovaa nguo zako!! Nawewe utafanya hivyo hivyo!!


Lunnah alimaliza kuvaa Kisha alimuita Junior aje kumchukua!!! Junior alimbeba na kumleta Hadi sebuleni Kisha alimpakulia msosi na kumpatia.


Waliendelea kula Huku Kila mtu alikuwa kimya. Junior alimuuliza tu.

  "" Miguuu yako ulifanyaje!! Mpaka unashidwa kutembea!!??


 "" Wale jamaaa!! Mungu awalaani TU, ningekuwa nimezaliwa kwenye maisha ya lai lai sizani hata Kama ningetembea!! Walikuwa wananichoma na miiba na chupa!!""


Junior aliinuka nakuletea Dawa Kisha alimwambia Anyoshe miguuu yake!!

 "" Muda wote nataka nikusimamie upone kwanza!! Ndio tutangaze habari zakupatikana kwako!! Mimi sijui utaanzia wapi kuwatafuta hao watu waliokuteka bila Shaka mhusika mkuu unamjua Ni Ancle yako!! Kama utataka msaada kwangu nitakusaidia!!" Ila kwa Sasa hamna kutoka Ndani mpaka upone kwanza!! Ndio utoke nje harafu Sitaki mtu yeyote ajue upo kwangu.



Ilikuwa Ni wiki Mbili imepita leo kwa Lunnah alikuwa tayari anaendelea vizuri! Alikuwa akifanya mazoezi ya kutembea tembea akiwa ndani!! Baadae alimaliza nakuanza kuandaa chakula Cha jioni.


Muda kidogo Junior Alifika Huku akiwa kabebelea matunda!! Aliingia moja kwa moja Jikoni na kumkuta Lunnah akiwa busy kukorofisha!! Alifika nakuweka matunda nakuelekea bafuni kuoga baadae walikaa Mezani.

   "" Lunnah!! Naona kwasasa upo huru naunaendelea vizuri!! Nataka nikuweke huru Sasa!! Nitangaze umepatikana!!!"


   "" Waooo!! Itapendeza pia!! Ila nilikuwa nimepazoea kwako!! 


   """ Ndio ubakie Sasa!!!""


Junior alimpatia simu yake Lunnah!! 

 "" Simu yako hii Hapa siku yenyewe watekwa!! Iliokotwa nakuletwa kituoni!! Waweza Anza kuwasiliana na ndugu zako!!"


Lunnah alichukua simu yake na kuiwasha, Ile anaiwasha TU alikutana na Message za Imlany Kama Mia kidogo, na message moja ilionesha Ina Kama dakika tano zimepita!!!


Imlany Baada ya kuona sms Imederivery Aliamua kupiga. Lunnah alipokea simu Kisha alimsikiliza.

  ""Duffer!!! Duffer!!! Ni Wewe Kweli!! Upo salama Lakini!!? Ulikuwa wapi?? Niambie Basi!! Vipi hujadhurika?? Ni Junior Ndio alikuteka??""


  """ Sitaki tenaaa uniite Duffer!!! Duffer ya wapi hiyo?? Ndio mnavyonicall na Ancle kunidanganyia kampuni kumbe mna yenu!! Kwasasa nishawajua Tena Sitaki mawasiliano na Wewe tenaaa!!" Lunnah alimaliza kuongea nakukata simu!!!""


Junior alikuwa akiwasikiliza TU, Aliamua kumjibu Lunnah.

 "" Usiwe na hasira kiasi hichoo!! Duffer Ni Duffer!!! Ancle Ni Ancle!! Kwani umejua chanzo Ni kipi??""


 "" Sitaki kujua!! Huyu Duffer gani Sasa!! Mbona hajaja hata kunitafuta!! Nimekwambia ukimuona Ancle Ndio umemuona Duffer!! Hawa Ni damu moja wanajuana!! Nachukia kwanini Ancle alizaa na Shangazi, kwanini alipanda mbegu kwenye ukoo wetu Kweli mtoto wa Nyoka na Ni Nyoka, tayari kashazaa Nyoka Tena ipo nyumbani, Kweli Ennah!! Nimejua roho mbaya umeitoa kwa Babaa!! Hata Duffer nayeye atakuwa Ni yule yule Nyoka wa ukoo!!


  "" Please Lunnah!! Nakuomba utulie Hapa bado waumwa!! Hasira zanini unataka uendelee kukaa Hapa nikuuguze tenaaa?? Ongeza kupiga kelele Tena ongeza!! Kwani wazani nimekuchoka Mimi bado natamani ukae Hapa mazima!!! Eeheee!! Unasema kwamba Ancle amezaa na Shangazi yakoo......???"


Junior Aliamua kumchokoza tenaa Lunnah Ile azidishe hasira Nia yake ilikuwa Ni Lunnah aendelee kukaa kwake.


  ..... itaendeleaa.......


Usikose sehemu ya 19.


Usikose kufatilia mkasa huu!! Nini Hatima yake!! Na vipi kuhusu Imlany atachukua maamuzi gani??

SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER .                            MTUNZI: TINNER ROBER.                          SEHEMU: 19. 0746638941 (Wtsp).


ANZA NAYO.


"" Please Lunnah!! Nakuomba utulie Hapa bado waumwa!! Hasira zanini unataka uendelee kukaa Hapa nikuuguze tenaaa?? Ongeza kupiga kelele Tena ongeza!! Kwani wazani nimekuchoka Mimi bado natamani ukae Hapa mazima!!! Eeheee!! Unasema kwamba Ancle amezaa na Shangazi yakoo......???" ENDELEA....


Siku iliyofuata habari zilienea Kila Kona kupatikana kwa Lunnah. Siku hiyo Lunnah alikuwa alielekea nyumbani kwake Huku akiwa Ni mnyonge Sana!! Kila akikumbuka habari za Ancle kumteka Ndio hasira zinaishia kwa Imlany.


Alifika Hadi Nyumbani kwake nakumkuta mfanyakazi wake wa ndani kafanya usafi wa mazingira Huku akizidi kumgonjea Lunnah!! Alipomuona tu, alikimbia nakumkumbatia Lakini alimuona anahangaika kutembea!! Alimshika mkono nakuingia nae Ndani Kisha alimulaza kapunzika sebuleni!!!.


Muda kidogo Aliingia Junior'' akiwa kabebelea dawa, pamoja na matunda ya mgonjwa. Alifika na kumwagiza Mdada wa kazi amuandalie maji ya Moto, Baada ya kumaliza alimletea Junior.


Junior Aliandaa maji nakuwekea Dawa Kisha alimkalisha vizuri Lunnah nakuchukua tambala na kumkandia miguuni. Lunnah alihisi maumivu makali nakuanza kulalamika.

  '" Junior!!! Hauna moyo wa Huruma Wewe!! Hujui naumia et!!!""


 "" Lunnah!! Nakupenda Ndio maana Sitaki kuonesha Huruma kwako!! Nachohitaji upone TU!! Najua hii Kazi nikukuachia Wewe au Mdada wa kazi lazima akuhurumie tu! Ndio maana nimefanya hivi na kila siku nitakuwa naja kukukanda nikibanana nitakuwa nakujulisha ila kuwa na Amani kwanza kwasasa relax!! Hakikisha moyo wako hauendeshwi na stress na matukio yaliyotokea nyuma!!!""


Baada ya Junior'' kukamilisha kazi yake aliyoijia Aliamua kuondoka nakuendelea na majukumu yake!!!


°°°°°°°°°°


Yapata mwezi moja ilipita Khari ya Lunnah ilikuwa tayari imekaa vizuri!! Alikuwa tayari akiendelea na majukumu yake!! Na habari zakutekwa kwa Lunnah zilikuwa zimeanza kupotea!!!


Leo alikuwa Ofsini kwake akiendelea na majukumu yake!! Muda kidogo alipokea Ujumbe kwenye simu ya kutoka kwa Imlany.

  "" Duffer!! Nimekukumbuka Sanaa!! Kwanini unaniacha mpweke kiasi hiki!! Ahadi yetu nikushikamana siku zote!! Kipi nakosea kwako!! Mpaka usitake ukaribu wangu kwako!! Niwie radhi kwa Jambo lolote unalolisadifu kuwa nimekukwaza!! Namisi ukaribu wako na utani utani wako!! Hivi Ni Wewe Kweli uliyenitungia hii simulizi nakuipa jina "" IKAWE KHERI MY DUFFER"" hio KHERI'' wazani nitaipataje kama Ndio umeanza kunitenga ikiwa Ni mapema hivi!!?? Au hisia zangu na Mawazo yangu nakuwa nayapelekea kwa Lunnah mtoto wa kwenye kitambulisho ambae niliipenda awe Duffer na Tena awe mke kumbe sio yeye!! Basi hata Kama sio yeye Basi Ni Duffer TU, Najua Duffer na Duffer! Siku zote huwa wananguzo mbili tu katikati Yao nayo Ni Nguzo ya UPENDO  na MUSAMAHA!! Bila kuwepo haya maneno Nguzo ya Duffer huwa haipo Tena!! Vipi hizo Nguzo Leo Umeziondoa kwangu!!??"


Lunnah Alimaliza kusoma ule Ujumbe, lakini moyo wake uliumia Sana!! Duffer Ni mtu wakaribu yake na yeye alikuwa ameimisi kampani yake, Alitamani amjibu kitu lakini aliamua kuikaushia.


Muda wakutoka kazini ulikuwa umefika!! Alitoka nje na kukuta Junior kamsubili!! Aliingia kwenye gari nakuelekea nyumbani, Njiani Aliamua kumuuliza Junior.

   "" Junior!! Kwasasa nimepona hata miguu yangu kwasasa naweza tembea hata kudrive naweza!! Nikushukuru tu!! Kwa muda uliokuwa pamoja namimi kunileta kazini nakunirudisha!! Ukweli Wewe Ni mtu wa pekee Sana!! Zawadi yangu nitakayotoa kwako Ni Mimi kukuita "MY DUSKY!! Kuanzia leo na Kesho nasiku nyingine make jina hili Ndio wapenda nikuite!!.


Junior Alibaki akimtizama Lunnah Kama yupo serous Kweli Ndio anagundua kuwa Hana utani tenaaa, Aliamua kumjibu.

  "" Ahsante DUSKY" 


Lunnah Aliamua kumuuliza Junior swali tenaaa!!

  "" Dusky!! Kwasasa Nina Duffer wangu Imlany!! Muda wote anapenda Sana kampani yangu!! Mimi na yeye hatuna ugomvi ila Ancle ndie ndugu yake unafikili nikwanini Ancle anifanyie hivi na Duffer asiseme kitu wazani Kuna Uhusiano gani Kati ya Hawa ndugu!!??""


  "" Duffer wako!! Sizani Kama hata anajua anayehusika namkasa huu Ni Ancle!! Nimegundua hili kwa kuangalia Lawama na shutuma zote anazileta kwangu naanajua kabisa Mimi ndie nilie kuteka Wewe!! Mpaka Sahiii!! Nakuomba muite siku moja umuweke wazi kuhusu Wewe na Ancle huwa mnaishije naamini atakusaidia pia!!!""


  " Ahsante DUSKY!! Nimeanza kuona upeo wa jina unalolitaka nikuite, Kumbe!! Linakufaa hata kwamimi pia litanifaa pia!!"


Ni usiku Tena Lunnah alikuwa amelala Huku akichezea simu take mtandaoni, Aliwasha Data nakuanza kuview Status za watu!! Mwishowe alikutana status ya Imlany!! Kaweka picha yake wakiwa pamoja Huku akiandika maneno machache TU.

  ""Duffer Kama Duffer!! Nalipenda jina hili, japo  typing.......""


Lunnah alibaki akifikilia maneno kadhaa, Sasa walipenda jina!! Hiyo japo typing... Ndonini??" Aliamua kuachana na What's up nakuingia Instagram Huku akipitia  New za wasanii!! Lakini aliona Kuna Ujumbe Tena unaingia wa Imlany. Alimtumia Short Video!! Siku ile akiwa anamvalisha kiatu Baada ya mguu wake kufa ganzi, Huku akiambatisha maneno. "" Namisi ukaribu wa Duffer!! Lini tenaa utanifanyia hivi??


Lunnah Baada ya kutizama!! Alijisahau zile hasira zote zikawa zimeisha nakuandika Emoji za kucheka Huku akifatisha maneno.

 "" Duffer!! Duffer!! Mkorofi anapenda kunifanya niwe nachukia Harafu Ndio afurahi!! Harafu Jinga Kweli kumbe ulikuwa wafanya shooting!!?""


Alimaliza kuandika nakuituma, Baada ya kuituma Ndio akili zinarudi Sasa,

 "" Mimi mjinga TU!! Mbona nimemjibu Duffer!! Wakati nilikuwa nimemnunia!! Ila kunasiku yake TU!! Harafu nakiona kinatying,,,, Sijui vidude gani hivyo!??"


Imlany Baada yakuona Lunnah!! Kamjibu alibaki alifurahia tu Huku akijisemea.

  "" Furaha yangu!! Siku zote imebebwa na Duffer wangu!! Yaaani ungejua Duffer wako alivyokuwa anakuwaza Wala usingeniuliza hiyo roho ngumu kiasi hicho!! Ona sasa Duffer wako Hapa nimepungua kilo tano kwa Stress TU!!"


Baadae aliamua kumjibu Baada yakutafakari sana!!

 "" Duffer!! Najua hasira zimeisha!! Ugomvi wa Mimi na Wewe umeisha, Ila ulivyo nakisirani najua utanikazia tenaa!! Ila fine TU!! Siku zote Ugomvi Ugomvi na hiyo minuno minuno yako huwa Ina nafasi nzuri kwa Duffer!! Na hayo Ndio mahusiano yanayohusiana na jina Duffer!! Nimemisi kukuona!! Uchukie ukiwa karibu yangu Ndio napenda na Kesho naja!! Angalau nikuage age!! Baada ya Ndoa Kweli nimeona uzito wa neno Duffer utapungua!!!"


Lunnah Alimaliza kusoma Kisha aliamua kuzima simu yake!! Katika maisha yake Ongea vyote ila neno Kuoa kwa Duffer ukiligusia moyo wake huwa unauma Sana!!!


Siku ya Kesho yake Aliamka Asubuhi huku akiwa kwenye maandalizi yakupokea mgeni!! Majira ya Jioni Imlany alikuwa tayari kaingia kwenye mjengo wa Lunnah!! Siku hiyo Aliamua kumfanyia Suprise Lunnah!!


Alifika Huku akiwa kamuandalia zawadi kadhaa!! Lakini kwa Lunnah Aliamua kumchunia siku hiyo!! 


Imlany na yeye aliamua kumkazia! Alimsalimia Kisha Aliingia chumbani kwa Lunnah Kisha aliamua kulala.


Lunnah Baada ya kuivisha aliangalia Mdada wa kazi nayeye alikuwa ametoka, Alitaka amuagize amuitie Imlany.


Ilibidi akamuite kwa shingo upande tu!!

 "" Duffer! Ani sijui ukoje!! Unaona kabisa nimeivisha harafu Ndio Waja kulala!! Nani akuamushe Sasa?!


Imlany aligeuka na kumshika mkono Lunnah.

 "" Hizi hizi kelele zako Ndio nilizimisi!! Maneno mengi unashidwa kunambia TU, " Duffer karibu chakula unaanza kurukaruka!!!"


  "" Niache Bhana!! Kumbe ulielewa? Ayaa!! Njoo tule hata hivyo nimepika chakula ukipendacho!!!"



Baada ya kumaliza kula, Imlany alimwomba Lunnah watoke kidogo Ana maongezi nae.


Imlany alimpeleka Hadi Hoteli moja, iliyokuwa ikiitwa 🌟 star Hotel!! Baadae Lunnah Ndio anashuka nakuanza kushangaa kwanza??

  "" Mbona Ndio Ile Hotel!! Siku ile Junior alinikaribisha Tukutane hapa!!"


Imlany alifika pale nakuagiza vinywaji!! Kisha Aliamua kuongea Shida iliyomfanya atake mazungumzo na Lunnah!!

   "" Duffer kwanini hukuniambia haya yote yaliyotokea, matokeo yake nikaanza kutoa lawama kwa watu wasiokuwa na hatia!! Kiss usirisiri wako!!"


Lunnah Ilibidi asituke kwanza nakuamua kumuuliza.

 "" Kwahiiyo umeshamjua mhusika aliyeniteka? Na Kama umemjua umechukua jukumu gani??""


 "" Daaah!!! Inasikitisha na inashangaza!! Kabla hata sijamjua ila nataka unipe kitambulisho changu!! Kwanini ulikipata harafu ukaamua umrudishe Ancle!! Harafu kwanini Wewe na Ancle mnazidi kushirikiana japo Ni Adui yako!! Kwanini Tena hujaniambia kuwa Ancle Ni mme wa shangazi yako?? Kwanini hutaki kunipatia kile kitambulisho nipate Kumbukumbu angalau Wazazi wangu!! Ikifeli Zaidi nataka nijue Yule mtoto ndie Lunnah!! Hicho TU Ndio nataka.


Lunnah alikuwa akimtazama Imlany Nakuona lawama zote anapata yeye!! Wakati alitegemea msaada!! Na yeye hasira zilimjaaa nakuamua kutupia ndoano mmaji angalau aokote hata perege.

   "" Duffer!!! Hizi lawama hupaswi kujilaumu Mimi!! Mimi Ndio wakukulaumu!! Kwanini ulinitoa Cassino!! Ningebakia kule haya yote nisingeyajua, Shangazi alitosha kunipa maisha yakukaa kwenye Cassino ila kwa jeuri yangu sijui kwanini nilikuwa nikikuomba msamaha!! Ni Bora siku yenyewe tungelala tu kwasasa ningekuwa nimeshayazoea maisha!!;"


  "" Duffer!!! Lunnah!!! Sitaki kusikia habari za Cassino!! Nishakwambia siku zote!! Ila hapa nazidi kutofautisha Lunnah mtoto na Lunnah mkubwa Baada ya kukua kabadilika Sana!! Kwasasa habari ya Ancle Sitaki kusikia harafu Mimi Ancle Sina imani Kama Ni Ancle yangu Kweli au ile siku alisingizia tu ili anisaidie!! Kwasasa Yule Ni Ancle wako wa damu si kazaa na Shangazi yako kwahiiyo Mimi siyo ndugu yako!! Ndiomaana Wewe na Ancle mnajengeana nyumba!!


  "" Lakini Duffer!! Mbona lawama zote zinaangukia kwangu!! Hayo yote Mimi nayajulia wapi?? Mimi nilitegemea Wewe Ndio utaniambia ukweli!! Kwanini mzigo wote unanibebesha Mimi??!


  "" Nenda kamuuliza Ancle!! Nyie mnajuana kwanza sisi tuwasindikizaji! Hivi Duffer!! Ndio Duffer Kweli!! Kweli Yule mtoto wa utotoni nilitegemea kuwa Ni Lunnah kumbe nimewafananisha TU. 


Imlany Alisimama nakuondoka huku Lunnah Alibaki kumtizama Imlany akiondoka Huku machozi yalizidi kudondoka baadae aliamua kuegama mezani huku akizidi kugonga gonga meza nakuendelea kuagiza pombe Kali.



   ,,,, Itaendeleaa,,,,,

Usikose Sehemu ya 20.


Nini Hatima ya mkasa huuu??.


Like comments Share.

SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER .                            MTUNZI: TINNER ROBER.                          SEHEMU: 20. 0746638941 (Wtsp).


ANZA NAYO.


Imlany Alisimama nakuondoka huku Lunnah Alibaki kumtizama Imlany akiondoka Huku machozi yalizidi kudondoka baadae aliamua kuegama mezani huku akizidi kugonga gonga meza nakuendelea kuagiza pombe ENDELEA....


Huku kwa Imlany alifika Hadi Nyumbani nakulala Huku akizidi kutafakari Mambo mengi Sana. Mpaka kukapambazuka ndio akili yake inatulia ndio anakumbuka Lunnah alimwacha Hotelin.


Alitoka nje nakuchukua usafiri wake na kwenda kumtafuta Lunnah!!! Alifika Hadi hotelin nakuulizia kwa wahudumu, Kama watakuwa wamemuona Lunnah! Aliulizia pasipokupata majibu yoyote, Alitoka Nakuanza kumtafuta huku na kule, baadae alimkuta kakaa kwenye swimming pool akiwa kaloweka miguu yake kwenye maji. 


Imlany alifika pale nakuvua koti lake nakumfunika Kisha alimshika mkono nakuondoka nae Hadi kwenye gari, baadae alimuomba msamaha.

  "" Sorry Duffer!!!"


Kisha aliwasha gari nakuelekea Hadi Nyumbani, walishuka nakuelekea sebuleni, Imlany alimtaka Tena msamaha Lunnah!! Baada yakuona haongei bado anahasira nae.

  "" Sorry Duffer!! Najua nikiasi gani unavyonichukia!! Hizo zilikuwa Ni hasira zangu TU! Naomba fungua kinywa chako tuongee Basi!!


Lunnah aliamua kuchukua maji kwenye Glass Kisha alikunywa Nakuanza kuongea.

  "" Duffer!!! Hukunikosea mpaka uniombe msamaha!! Najua Mimi na Wewe hatuna hatia na Hapa hakuna mtu anayejua ukwelii!! Niombe tu swala hili tulifatilie tukiwa wote!! Ancle kakimbia Baada yakuniteka Mimi!!! Na yeye ndie anayejua ukwelii ukowapi namimi nitaenda Kijijini kwetu kwa Shangazi nikamuulizie Nini hatima ya haya yote nawewe mtafute Ancle akupe ukwelii ili wote tuwe huru!!"


  "" Duffer!! Najua ila Mimi mkosaji TU kwako!! Mimi naona niachane na Mambo haya!! Sitaki Tena kufatilia, nikiujua ukwelii Nitazidi kuumia TU!! 


  '" Duffer!! Hutaki tenaa kumjua Yule mtoto wa kwenye kitambulisho?? Huenda akawa Ni Lunnah!! Sijui utafanyaje??"


  " Ewaaa!! Kama ndio Lunnah!! Hakika nitamuoa!!!! Nikishidwa ntamfanya awe Duffer wa Ndani!!!"


  "" Muone Jinga Kweli!!! Ila Duffer wangu sitakuja kamwe kumsahau kwa wema wake!! Harafu nimemisi kupakana damu!! Et alikuwa kaumia Lakini aliponaaa!!!""


  "" Ila Siku nikiwa nakuacha natamani nikuache mikononi mwa Junior!! Nahisi hapo Kuna usalama naona Junior anajitahidi kujitoa kwaajili yako Duffer!!""


  "" Ushaanza Tena!! Wataka kuumiza moyo wangu tenaa!! Wakati leo Ni siku yakurudisha furaha yetu toka siku ya Jana Kila mtu alikuwa kakis!!! Okay!! Week kesho narudi kijijini kwa Shangazi naomba nitakuacha ofsini kwangu!! Hakikisha nikiwa narudi niwe nimepata  kuhusu Ancle harafu tuunganishe matukio!!  Jukumu lakufatilia Kesi yangu kwasasa ipo mkononi mwa Junior''


¶¶¶¶¶¶¶¶¶


Ilikuwa Ni siku nyingine tenaa, Lunnah alikuwa Njiani akisafili kuelekea kwa Shangazi yake..


Alifika majira ya jioni, Alimkuta Ni Ennah akiwa anafuafua Nguo za mtoto, ilibidi ashangae kwanza Baada ya Ennah kusimama nakuona kifua chake kimejaa alijua Ni dhahiri kuwa anae mtoto. Lunnah alimsogelea nakumsalimia.

  "" Ennah!! Ni Wewe Kweli?? Vipi za Siku Lakini Mwaendeleaje??"


Ennah alimtizama Lunnah juu chini huku akimpandisha, baadae aliamua kumjibu.

  "" TU wazima!! Nambie kiliichokuludisha Hapa?? Umesahau Nini?? Naona Cassino imekung'alisha!! Umetakata!! Umepata wanaume wenye gari, leo warudi umening'iniza simu yako kubwa macho matatu hayaa sema usikike!!!"


Lunnah aliamua kumkalia kimya make alijua yeye na Ennah huwa hawapatani tangu wakiwa watoto, Alishusha mizigo yake kwenye gari nakupeleka ndani! Alifika Nakuanza kushangaa mazingira ya pale yalikuwa yamechakaa sana, hata Kochi nazo zilikuwa tiyari zimeisha!!!


Aliamua kutoka nje huku akizidi kumtafuta Shangazi yake, Alifika mlangoni nakumkuta Ennah akiwa kakaa ananyonyesha, Lunnah alimsogelea huku akimtizama Yule mtoto Baada ya kumuona TU, Alishituka.

   "" Ennah!! Huyu Ni mwanao kumbe!! Kwanini mtoto Ana afya Mbaya kiasi hiki shida Ni Nini?? Lishe au??""


Ennah Baada ya kuulizwa hivyo alijikuta akimwaga machozi Kisha alimkumbatia mwanae nakuingia Ndani.


Lunnah alibaki pale akizidi kushangaa, muda kidogo alimuona Shangazi akiwa anatoka sokoni kuhemea!! Alimuwahi nakumsogelea amkumbatie Lakini Shangazi alimgeukia mgongo Nakuanza kulia,


Lunnah alibaki akizidi kushangaa nakuingiwa sitofahamu, alichoamua nikuchukua kile kikapu chenye mboga mboga nakuingia nacho ndani, Huku Aunt alikuwa akijivuta taratibu akiingia Ndani alifika Hadi sehemu aliyekuwa kakaa Lunnah, Alipiga magoti mbele yake huku akizidi kulia;

   "" Shangazi yangu Lunnah!! Nisamehe Mimi nimekuwa Mbaya kwako nimetumia Mali zako kwa unafiki mkubwa huku nikijimilikisha!! Lakini kwasasa nimeshidwa kuzitumia vizuri!! Matokeo yake mdogo wako Ennah!! Alipata mwanaume Mali zote Hadi shamba na ile nyumba yakule kijijini alimuuzia Baadae Yule mwanaume akamtoroka nakumuachia mtoto.


Kwasasa unavyotuona Mimi na Ennah!! Hatuna kitu chochote!! Na hii nyumba tumeshaiuza na mumiliki wa hii nyumba katupa tuendelee kuishi kwa mwezi mmoja na Hii Hapa ndio hati ya mnunuzi kwasasa Ni Mali yake! Na inasadikika hata ile nyumba ya kule kijijini kainunua Tena kwa ghalama ya juu toka kwa mme wa Ennah, wakawa wamekubaliana na hii ndio hati yake ya ile nyumba wiki kesho anakuja kuchukua.


Lunnah alichukua zile hati Nakuanza kuangalia mnunuzi aliyenunua Lakini alibaki kaduwaa Baada yakuona Junior'' ndie mnunuzi wa zile nyumba, alirudi mara mbilimbili akizidi kukagua ndio anaona pasport na Sahiii yake!! Aliamua kwanza kunyamaza wasije wakawa na maswali ya kuuliza, Alizirudisha mezani nakuulizia;

  "" Huyo mumiliki anaishi wapi? Na anakazi gani??


  "" Mumiliki hatujajua kuwa anakazi gani!! Nahisi atakuwa Ni mfanyabiashara mkubwa Hapa mjini!! Hata hivyo nahisi pia atakuwa Tena Ni Mtumishi wa serikali!!""


Lunnah Alimtizama Ennah!! Nakumuona anatapika tenaa, Alishituka nakumsogelea Ennah, Kisha aliamua kumuuliza Shangazi yake;

  "" Shangazi Ennah!! anaumwa??"


  "" Daaah!; Ana Kweli hujafa hujaumbika!! Ennah Baada yakuona katelekezwa na baba wa mtoto Wake!! Aliamua kuwa mlevi na kuutumia mwili wake vibaya!! Matokeo yake kambemenda mtoto wa Mwaka mmoja kwasasa Ni mjamzito wa miezi minne!! Na hapo kanywa Kila Aina ya Dawa Mimba imekataa kutoka!!!"


Lunnah baada yakusikia hivyo Nguvu zilimuishia ilibidi akae kwanza chini, Muda kidogo alishangaa Kuna gari tatu zimefika pale, huku kukiwa na Askari wakutosha, Walifika nakushuka Kisha walisogea Hadi kwa Shangazi nakutoa vitambulisho vyao nakumuweka chini ya Ulinzi Kisha walimuomba aongizane nao kituoni kwa mahojiano zaidi.


Muda huohuo gari ya tatu Ndio Mlango unafunguliwa alikuwa Ni Junior akishuka huku akiwa kapigilia pamba kali, Lunnah alipomuona Junior alibaki kushangaa, 

  "" Junior!! Mvaa pens!! Leo kavaa kiboss boss! Namna hii!!!??""


Junior aliwapita watu wote Kisha alizidi kusogea kwa Lunnah!! Alifika nakumkumbatia huku akimuachia maneno kadhaa.

   ""Kwaajili yako Dusky!! Nipo radhi kufanya kitu chochote kilicho ndani ya uwezo wangu!! Yote hayo nikuhakikisha unakuwa na amani tele!! Na hii Ndio kitu Duffer wako Imlany huwa anapenda!! Hata hivyo na Dusky wako Junior!! Nae anapenda vivyohivyo!!"


Junior alimuachia nakumshika mkono!! Nakuondoka nae Hadi kwenye gari yake Kisha aliwasha gari nakuongoza njia. 


Lunnah alibakia katulia TU, aliona Ni surprise ya Nguvu ambayo hakutegemea Kama ataipata, Alimuuliza Junior;..

   "" Kwani twaenda wapi?? Harafu tumemuacha Ennah!! Akiwa analia!!""


  "" Usijali!! Ennah atakuwa vizuri TU!! Ngoja kwanza hili nalo liishi ili uendelee na maisha mengine!!"


Walifika moja kwa moja Hadi kituoni Shangazi siku hiyo alikuwa akihojiwa, Huku Ennah na Junior nao walikuwa sambamba wakisikiliza.


Mwanasheria wake na Lunnah!! Alitoa memory card iliyokuwa ikimuonesha, Shangazi siku hiyo Aliingia jikoni akiwa anakichupa kidogo alitia sumu kwenye mihogo, muda huo huo mamake Lunnah alikuwa akiingia jikoni baada yakumuona Lunnah katoka jikoni, Alisimama pembeni nakuchukua video baada yakumaliza alichukua ile memory card!! Nakwenda kuiweka kwenye bahasha iliyokuwa inadocument za hati ya nyumba huku akiambatanisha Ujumbe wa karatasi.

  "" Kwaajili yako Lunnah!! Natamani nikuache pekee ili uzidi kugundua Mambo mengi, uzidi tambua adui zako Ni wale unaokaa karibu nao!! Nipo Tayari kufa kwaajili yako ili uwatambue adui zako!!"


Shangazi baada yakuona ile video alibaki akitetemeka!! Nakuanza kulia.


Baadae Hakimu alichukua memory card, nyingine nakuweka kwenye screen Kisha! Alimuuliza Shangazi.

  "" Kabla sijaweka!! Naomba uniambie siku ile kwanini ulitia sumu kwenye Glass ya juice!! Harafu ukawahi kusingizia Ni Lunnah kamuua mamake kwanini ulifanya hivyo!!??"


Shangazi alianza kulia pasipo hata kuiona ile video, Alipiga goti Nakuanza kulia Huku akiomba msamaha kwa Lunnah!!

   "" Nisamehe Mimi Lunnah!! Nipo Tayari kutumikia adhabu!! Yakumuua mamako kwakumuwekea sumu!! Kwenye chakula!! Yote hayo Ni uchu wa Mali baada yakumuona Kakangu kafariki Niliona wifi yangu atanufaika na hizo Mali nikaamua  nimuue!!"


Hakimu alimtuliza huku akiwaza Mambo mengi.

 "" Hata hivyo nilijaribu kukutega TU kwamawasiliano kuhusu kuweka sumu kwenye juice hata hiyo video sikuwa nayo!! Nilitumia uzoefu wa kazi kutokana na maelezo ya pande mbili!! Kwakuwa umesema ukwelii kwasasa utapatiwa hukumu.""


Baada ya maelezo yote kulinganisha sehemu mbili, Shangazi alipatiwa hukumu ya kifungo Cha maisha na Kesi yake ikawa imeishia hapo.


Junior'' na Lunnah walirudi kijijini kwenda kumchukua Lunnah nakuondoka nae Hadi mjini kwenda kuunganisha Kesi ya Ancle.


   ,,, Itaendeleaa,,,,,,


Usikose sehemu ya 21.


Like, comments, Share....

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi