SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER . MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 12. 0746638941 (Wtsp).
ANZA NAYO.
Lunna alishusha pumzi kidogo na kijidho chembamba kilimtoka kutokana na maneno ya Junior! Ilibidi achukue Glass ya maji na kushushia Kwanza ili amjibu!! ENDELEA...
"" Junior!! Maswali mengi ya Nini?? Hivi umetumwa!!? Au Ni Nini wakitaka kwangu!??"
"" Please!! Nataka Ukweli mtupu kwako!! Hebu relax kwanza!! Nina Nyaraka zako na Ukweli mtupu kuhusu wewe!! Nataka nikusaidie!!! Junior Alitoa baadhi ya Documents na kuziweka mezani, Kisha alimgeukia Lunnah!! "" Just continue........!!!!
Lunnah alipitia Zile Documents!! Baada ya kumaliza kusoma zilimfanya aanze kulia Huku akikumbuka maisha ya nyumaa yaliyowahi kumkuta....
Ni siku Moja katika familia Yao walikuwa wamekaa yet na mamake. Kuna wageni walikuja kuwatembelea!! Alikuwa Ni Shangazi na Ennah!! Walifika kuwatembelea, Ni Mara TU Baada yakupotelewa na Baba'ke Lunnah kwa maradhi ya moyo!!
Siku ya meieho wa Uhai wa Babake na Lunnah!! Ilikuwa Ni Siku Moja alikuwa safarini akipeleka dhahabu kiwandani kuuza Ghafura kwa mbele alikuta Kuna ajari kubwa imetokea na watu waliuwawa vibaya sana! Alipata mshituko wa moyo nakupelekea kushidwa kupumua kwa Kasi na Hapo hapo Ndio Safari yake ilimalizikia hapo.
Enzi za uhai wa Babake na Lunnah alikuwa Ni mfanyabiashara wa madini na aliwahi kuwekeza rasiliamali Sehemu mbalimbali!! Katika usekezaji wake siku zote hakupenda kushirikisha familia yake zaidi ya kumshirikisha Dada'ke ( mama Ennah )Na Ndio mtu aliyekuwa anajua Kila kitu kuhusu Mali za Kaka'ke.
Siku hiyo alihudhuria msiba Lakini kwa upande wa Mamake Lunnah!! Alipoulizwa kuhusu Mali za mme wake alisoachiwa alidai Ni Nyumba TU, vingine alikuwa hafahamu. Shangazi Baada ya kuona hivyo vitu vingi hafahamu wifi yake aliamua kukaa kimya na kuingiwa na uchu wa Mali na kuanza kupanga mipango yake mingine ya kuzimiliki Mali zote!!
Aliamua kwenda kwa Mganga wa kienyeji na kupatiwa Dawa ya kumuua Mamake Lunnah ili aweze kumiliki vizuri hizo mali,. Siku hiyo alifunga Safari na kuelekea kwao Lunnah!! Baada ya kufika Upande wa Mamake Lunnah na Lunnah walijawa na furaha Sana Baada ya kuona wageni, hasua kwa Lunnah Baada ya kumuona shangazi alifurahi na kumuona Kama Ndio Babake yupo hai bado. na Upande wa Shangazi yake alikuwa akimpenda sana Lunnah!!
Siku hiyo Shangazi Aliomba awapikie, Kwakuwa walimuamini Sana hawakuwa na pingamizi chakula Cha Mchana alikiandaa wakawa wamekula vizuri Lakini Chakula Cha usiku Lunnah Ndio aliandaa.
Mamake Lunnah!! Alimuita Binti yake na kumwagiza akanunue mihogo Ndio atatumia siku hiyo ili aweze kumuenzi mmewe kwa kuwa Alikuwa Ni mtumiaji mzuri wa mihogo Mara TU Baada ya kupata maradhi ya moyo!!
Lunnah alifanya Kama alivyoagizwa na mamake, Aliandaa ile mihogo na Huku Aliandaa Chakula kingine kwaajili ya wageni make wasingeweza kutumia mihogo!! Baada ya maandalizi yote Chakula kilikuwa tayari kimeiva!! Lunnah Alitoka jikoni Huku akiandaa sahani za kulia ila anatoka TU Shangazi Alikuwa akimfatilia Kila kitu alichokuwa akifanya, Aliingia jikoni Huku akiwa kaandaa ile Dawa alimimina kwenye mihogo make ilikuwa Ni Dawa ya maji ilikuwa Ni ngumu kuitambua.
Baadae Lunnah alileta Chakula chote mezani na kutenga, Waliendelea kula Huku Lunnah, Ennah wao walikuwa wanapenda ubwabwa hawakuwa na ratiba ya mihogo hata kwa shangazi na yeye alikata na kuendelea kushambulia nyama!!
Mamake Lunnah Baada ya kula mihogo miwili alianza kulalamika !!
" Lunnah!! Leo mihogo umenunulia kwa Nani?? Mbonaa michungu hivi??.
Lunnah hakujari na yeye alimjibu Mamake kwa kumtania. "" Mama nae naona mate yako machungu TU! Sasa siuache kula'' ule ubwabwa!!?" Mwishoe Yakuuguze itakuwa yameshinda juani Siku nzima na yule mama kwa kupenda pesa hajambo!! Kasoro aboreshe mihogo ili nizidi mpelekea wateja!! Shauri yake!!!.""
Mama Lunnah baadae tumbo lilizidi kumvuruga nakumsababishia kaharo ya Mara kwa Mara!! Mpaka ikampelekea nguvu kumuisha na kupelekwa hospital!! Alipata matibabu Baada ya Siku mbili akawa amerudi Nyumbani!! Lakini muda wote alikuwa anapata maumivu makali ikabidi Tena kurudi hospital na kufanyiwa Nutrasound!! Matokeo yake ilionekana utumbo tayari umeoza itabidi awekewe wa plastic ili kunusuru maisha yake.
Jitihada ziliendelea kwa uangalizi zaidi Lakini Kuna mtu alionekana akiingia hospital Akiwa ameficha sura yake!! Alifika na kumpatia Mama Lunnah juice na kumsimamia ainywe yote lakini akawa kabakisha kidogo na kuiweka mezani, Baada ya kuhakikisha kanywa aliondoka kimya kimya pasipo Mamake Lunnah kumtambua vizuri.
Lunnah alifika kumuona Mamake!! Lakini alimkuta Ana khari Mbaya akikohoa. Lunnah aliangalia Huku na kule pasipo kuona Maji kwa pembeni Ndio anaona ile Juice imebakia akamua kumpatia. Baada ya kumpatia tu!! Khari ikazidi kuongezeka.
Mama alimshika mkono Binti yake Baada ya kuona khari imekuwa Mbaya!! Kisha Alimwambia.
"" Binti yangu nakuacha ukiwa mdogo!! Nakuomba nenda Chumbani kwangu Kuna bahasha chini ya kitanda naomba uitunze hiyo itakusaidia kwa baadae!! Hakikisha huipotezi Siku ukiwa mkubwa nikusihi ipeleke popote kwa Mwanasheria atakusaidia!!!
Lunnah alimshika mamake kwenye Shavu nakumsihi.
"" Mama Ngoja nikaichukue Kwanza ila Naomba unisubili Kuna kitu nataka kuja kukwambia Kwanza!!! Usikohoe Tena usije ukaumia kifua!!!""
Kabla hajaondoka shangazi yake Aliingia Huku Akiwa anahema kwa pupa Huku kaambatana na Dokta. Alifika na kumkuta Mama Lunnah anakohoa!! Aliangalia na kuona Glass yenye Juice Kisha alimgeukia Lunnah na kumuuliza.
"" Vipi umempatia Mama hii juice!! Harafu mbona ya baridi hivyo na Wewe utakuwa wataka kumuua mamaa!!""
Lunnah alimgeukia Shangazi yake Kisha Alimtizama mama yake Akiwa anakohoa kwa shida. Mama alimpatia Ishara aende Nyumbani akafanye kile kitu alichomwambia!!
Huku kwa Shangazi alichukua ile Juice na kumpatia Dokta Huku akiomba ichunguzwe kwanini mama kakohoa hivyo ili Siku nyingine wasirudie kumpatia tena ikamzuru.
Dokta alirudi Huku akiwa na Daktari wawili!! Alifika na kutoa majibu.
"" Tumejaribu kufanya Uchunguzi Lakini inaonekana hii juice Kuna sumu Ndani yake!! Na sumu hii inaenda kugandisha Kila chakula kilichokuwa kimeingia ndani!! Na mgonjwa wenu muda mrefu atapoteza maisha!!!""
Shangazi baada ya kusikia hivyo aliendelea kulia kwa sauti Huku akimraani vikali Lunnah!!
"" Leo unamuua mamako!! Kisa wataka Mali zote ziishe maskini Mimi kakangu!! Nimempoteza na wifi Tena nampoteza!!!"
Daktari mmoja aliwatizama wale wenzake na kubaki wakijiuliza.
"" Inakuwaje mtoto mdogo hivi aue Wazazi wake!! Na hata ukiangalia Hana akili ya kuzimiliki zile Mali, Hapa Kuna kitu.
Ilibidi wafanye Kazi Yao tu, Make haikuhusiana na Utafiti!!
"" Mama pole Sanaa!!! Hata hivyo tuzidi kumuomba Mungu anaweza fanya njia pasipo na njia Lakini hata hivyo Badoo anapumua na siyo kapoteza maisha!! Inakuwaje Wewe unalia Kama katangulia tiyari???""
Shangazi alijishitukia kidogo na kumchungulia Kama bado anaishi!! Alijisemea chini chini.
"" Mimi nae mjinga Kweli bado anapumua Lakini nalia et kafariki!! Nisije shitukiwa hapa!!! Lakini hata hivyo ana nusu saa tu ya kuishi!!!"
Lunnah alifika Nyumbani na kufanya Kama alivyoagizwa!! Alichukua ile bahasha na kuificha kwenye begi lake la nguo katikati Kisha Alitoka nje ili aweze kurudi tena hospital.
Lakini alishangaa Baada ya kuona watu wanakuja Nyumbani Huku wametanda nguo kichwani wengine wanatandika mikeka hapo hapo Ndio anagundua tayari mama kapoteza maisha!!
Siku hiyo ilikuwa Ni Siku Mbaya kwake kwani alipoteza wazazi wawili Ndani ya mwezi mmoja!!
Huku msibani tuhuma zote ziliangukia kwa Lunnah!! Kuwa yeye Ndio kusababisha kumuua mamake kwa kumpatia mihogo michungu pamoja na kumpatia Juice yenye sumu!!
Msiba Uliendelea mpaka ulimazilika. Ilibidi Lunnah achukuliwe na Shangazi yake na kwendaa kulelewa huko!!
°°°°°°°°°°°°°°°°°°°
Lunnah Alimaliza kusimulia Huku akizidi kuangua kileo.
Junior alimkumbatia TU, nakumsihi atamsaidia!!!
Lunnah Alijikaza na kunyamaza Kisha alimuuliza Junior.
"" Hii bahasha umeitoa wapi?? Muda mwingi nilijua nitakuwa nimeipotezea Cassino na Ndio maana Kila muda natamani niende kule nikaitafute!! Tangu mama aniambie niitunze sijawahi ifunua hata nikajua Kuna Nini Ndani yake!!""
"" Kukufahamu kwangu Ni juu ya hii bahasha but Sorry lakini bahasha niliifungua na kuipeleka kwa Mwanasheria Kama ilivyokuwa imeandikwa kwa mtu atakae iokota aipeleke kwa Mwanasheria, Na Mimi nimefanya hivyo na kwa Sasa inazidi kufanyiwa kazi!!""
"" Anyway!! Kuna Siku Moja nazani huenda na Wewe ulikuwepo!! Ni Siku Imlany anakutoa kwenye Cassino!! Ile mnafika Nyumbani katika kushusha Begi kwa bahati Mbaya Zipu ya beg haikufugwa vizuri, Bahasha iliweza kuanguka na kuokotwa na watoto wa mtaani wakawa wanachezea picha zilizokuwa kwenye bahasha!!"
Siku hiyo nilikuwa Mimi na rafiki yangu Anord!! Tukiwa twatembea kwenye gari kwa pembeni kidogo Ndio tuliona wale watoto wakichezea hiyo bahasha lakini Baada ya kutuona walikimbia, na sisi ikabidi tushuke kwenye gari ili tuone kilichokuwa kinaendelea pale!! Jamaaa angu yeye aliwahi kushuka na kumkamata mtoto mmoja Ndio akatupatia maelekezo jinsi walivyoipata ikawa tumefatilia mpaka tukapata Sehemu bahasha ilivyopatikania.
"" Kwahiiyo muda wote nilichukua Zile Documents na kuzitizama mpaka picha zako na za Wazazi wako nikawa nimegundua kitu nikaamua kukufatilia!! Mungu si Athumani nikawa nimekupata siku hiyo kwakukupatia rift Siku ile Mvua yakunyeshea pasipo kujua Ni Wewe!! Namimi nilipokuona TU nikawa nimeingiwa na hisia tofauti nikatamani TU nikupakie.
"" Sio Siri muda wote ulipokuwa umekaa kwenye gari Kuna hisia zikawa zinanijia za kukupenda Ghafura TU, Hata tulipoachana niliamua nimushilikishe rafiki yangu! Jinsi tulivyonana na pia sikumficha juu ya hisia zangu yaaani Nakupenda Wewe!!
Rafiki yangu akanishauli nitafute muda wa kuongea na Wewe!! Japo hata mawasilino yako sikupata ikabidi nitafute kazi na kazi nilipata Kweli ilibidi nifanye Nikawa nakuja mitaa niliyokuleta kukutafuta Japo nilikuwa sijakukalili vizuri!! Baada ya kukuona Siku yenyewe una koti langu!! Ndio nikakupata vizuri!!!""
" Nakumbuka Siku hiyo Baada ya kunileta kwako ulipotoa Koti na kuvaa Zile track usiku!! Ndio nikakukumbuka vizuri kumbe ninayemtafuta muda wote Ni huyu Lunnah!!!"
"" Siku hiyo Baada ya kuondoka na kuelekea Nyumbani kwangu nilifika nikapitia Zile picha zote nikajua sijakosea hata jina lake Ni Lile Lile tangu Siku nakutana nawewe ukawa umekaa kwenye gari ulinijibu waitwa Lunnah!!!" Japo hukuniambia la baba, nikawa nimejua ukweli wote Ni Wewe nikutafutae!! Harafu Nzuri zaidi juhudi zangu nilikuwa nakutafuta Kama mtu nimpendae lakini hata kwa hili Ndio limetimiza hatima yangu kwangu na kwako pia.
Lakini nilikuwa nawaza!! Kwanini ulinifungia simu zangu!!! Nikaona siyo Mbaya nitaanza kukufatilia Wewe maisha yako na kwanini upo hapa!! Na kwanini uliuzwa kwenye Cassino!! Itoshe TU kusema!! Nishajua kila kitu na kuhusu Ancle kwenda kwenye Cassino nishajua Ukweli wote na kuhusu Shangazi yako Ana mahusiano gani na Madam wa Cassino yote nishajua!!!!
Baada ya Junior kumaliza kuongea!! Lunnah Alibaki kimya katulia Kama kapigwa bumbuazi, Huku Akitafakari kwanini Junior tenaaaa,,,,,,,,,,,,!!!!!!!
,,,,,,,,, Itaendelea,,,,,,,,,,,
Usikose Sehemu ya 13.
Lunnah atachukua uamuzi Upi kwa maneno ya Junior!!??
🎤🎤🎤🔉🔊 Kwako Msomaji, Mshauri kitu Lunnah!! Napitia Comments zenu hapa!!!
SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER . MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 13. 0746638941 (Wtsp).
ANZA NAYO.
Baada ya Junior kumaliza kuongea!! Lunnah Alibaki kimya katulia Kama kapigwa bumbuazi, Huku Akitafakari kwanini Junior tenaaaa,,,,,,,,,,,,!!!!!!! ENDELEA.
Junior Alimurudishia ile bahasha Kisha aliamua kuondoka na kuendelea na majukumu yake Tenaa!!.
Huku kwa Lunnah alichukua zile bahasha na kuanza kukagua Huku akifikilia vitu vingi Sana katika maisha yake!! Aliamua kuchukua simu yake na kumtafuta Duffer wake angalau aweze kumpunguzia stress. Baada ya kumpigia Aliona simu yake hapokei Tena aliamua kumtumia message What's up!!
"" Hellow Duffer!! Naomba ukiwa hewani unitafute!! Sa' unakaa kimya hivyo kumaanisha Nini Lakini??""
Alituma na kukaa muda kidogo Aliona Ujumbe umefika, Na Imlany alikuwa akityping. Baadae aliona Kuna picha, Aliamua kufungua na kukutana na Pete mbili za Uchumba! Huku zikiambatana na Ujumbe.
"" Sorry Duffer!! Sikupokea simu yako nilikuwa naandaa Pete za Uchumba kwa sonara!! Si unajua Tena harusi mwezi ujao tu!! Harafu wiki kesho ndio Natangaza Uchumba, Naimani utakuwepo!! Ookay!! Vipi Lakini zimekaa powa!!!??""
Lunnah alisoma Ujumbe wa Imlany ulimpelekea akose Raha kabisa!! Alitafuta jinsi ya kumjibu Lakini alikosa namna jinsi ya kumjibu!! Baadae aliamua TU kumjibu.
"" Zipo powa bhana!! Harafu Mimi sizani Kama nitakuja!! Kazi zimenibana!!!"
Imlany Alisoma Ujumbe wa Lunnah!! Alijua dhahiri atakuwa kaumia.
"" Wewe Njoo bhana!! Mimi sipendi kuwa nafanya tukio kubwa kiasi kile harafu Wewe ukosekane sitapenda kweli!! Ofisi zote wanajua Kuna tukio!! Itakuwa maajabu wafanyakazi wenzako waje harafu Wewe usije!! Ayaa jioni njema!!""
Lunnah alibaki akilalama peke yake.
"" Yaani!! Duffer!! Hujui naumia Sana!! Nije kweli kushuhudia Aah!! Hapana siji kwa kweli, Bado kwenye harusi tenaa!! Moyo unauma na Nina wivu juu yako!! Lakini sijui kwanini naumia hivyo wakati huyu Ni Rafiki yangu TU, Ila si Rafiki tenaa naona Kuna kitu kimezaliwa upyaa!! Ni sawa Nitaona lakiniii!!""
Hatimae ilikuwa Ni siku ya jumamosi. Lunnah alikuwa kakaa Huku akifikilia kwendaa kwa rafiki yake Imlany Angalau akatoe ushirikiano!! Alichoamua Ni kuzima simu yake!! Mpka siku tukio litakapoisha.
Siku ya Tukio Lunnah!! Moyo wake ulikuwa ukimsukuma kuwasha data aone kilichojili, Aliingia What's up Status na kukutana na picha ya Imlany katupia kimkoti cheusi na kiatu chake Cha gold kilichokuwa kiking'aa misili ya koboko Akiwa na rafiki yake Rich. Lunnah Aliamua kuview status na kuandika. "" Nawaona mapacha wangu!! Huku akiongezea Emoji ️💞.
Baadae alikutana na picha ikiwa Ni Imlany na Rayna!! Rayna alikuwa kamshika mkono Imlany. Lunnah Aliamua kuizoom ile pichaa Mara mbili, Alichoamua Ni kuzima Data na kuweka simu mezani na kuwasha Tiv angalau apunguze Mawazo!!
Huku kwa Imlany Baada ya tukio Alikuwa Kakaa sebuleni Huku akijaribu kupitia picha za tukio!! Aliamua kuchukua picha baadhi na kupost kwenye mtandao wa Facebook kwa Account yake na kuandika "Couple 2021".
Baadae Aliingia What's up na kukutana na Ujumbe wa Lunnah!! Akiwa kaandika "" Nawaona mapacha💕" Imlany alizidi kutizama picha zingine na kukuta Lunnah kaview Lakini hajaandika chochote! Alibaki akijifikilia Mambo mengi Sana kichwani!!
"" Najua kweli Duffer!! Ni kiasi gani unaumia Lakini hakuna kitu kisichokuwa na Mwisho!! Ila kwangu bado utakuwa Ni Duffer wangu siku zote nitabaki upande wako!! Ukiwa na Shida yoyote naomba unishilikishe!! Kwani Badoo Nakuhitaji! Na ninakupenda pia!!"" Haya Ni baadhi ya maneno aliyokuwa akifikilia na kuwaza.
Huku kwa Lunnah!! Siku iliisha vibaya Sana Baada ya kuona picha, Hata alipojaribu kuingia Fb alikutana na pichaa za Uchumba!! Siku hiyo aliamua kuzima simu yake kubwa na kubaki na simu ndogo.
Muda kidogo Alisikia simu yake inaita ilikuwa Ni namba ngeni!! Alipokea na kusikiliza, Ilikuwa Ni simu ikimuhitaji mahakamani.
Baada ya kufika Mahakamani!! Alikutana na Mwanasheria mmoja na kuanza kuongea nae!! Muda kidogo Aliingia Junior Huku akiwa kabebelea karatasi yenye maandishi alifika na kumkabizi Mwanasheria Kisha alikaa pembeni Huku akisikiliza.
Mwanasheria Baada ya kuongea na Lunnah!! Alimkabizi Form Moja ajaze Kisha alimuelekeza sehemu ya kusagn baadae alimwambia.
"" Lunnah!! Kwasasa Mshukuru Sana Junior kwakutumia muda mwingi kukupambania kwasasa unae furaha Mali zako zinaenda kurudi mkononi mwako!! Nikuombe uzidi kunipa ushirikiano Kila ninapokuhitaji!! Naamini Mambo yatakaa sawa!!!
"" Nashukuru Sana kwa Msaada wako!! Nitawaletea baadhi ya Nakala ikifika jumatatu zitakuwa Tayari!!""
Lunnah alisimama na kuaga Huku alielekea Nje kutafuta usafili!! Junior alifika pale na gari lake Kisha alimfungulia Mlango.
"" Oyoo!! Twende Basi au unatembea??""
Lunnah Aliingia kwenye Gari Kisha alimpatia maelekezo Ampeleke Nyumbani. Huku Kwa Junior Ilikuwa Ni kawaida yake kusikiliza music!! Aliamua kumsemesha Lunnah;
"" Mbona leo unae hasira hivyo!!? Au Ni kwakuwa Duffer wako kamvalisha mpenzi wake Pete ya Uchumba!!?""
""Wewe Junior!! Niache bhana!! Mimi niwe na hasira Duffer anaoa!! Hivi unanichukuliaje kwanza na hizo peans zako!! Umevaa Mahakamani!! Sijui Hata wazipendea Nini??"
"" Junior Aliamua Acheke kwanza; "" Harafu nishakukataza kuniita Wewe Junior!! Huwezi niita Junior, hiyo Wewe ukaiacha?? Anyway una hasira kumbe!! Swala la kuvaa peans linahusiana na Nini kuhusu swali langu!!? Nishakusoma kumbe unasumbuliwa na
Wivu!! Au mlishawahi kudate na Duffer wako??"
"" Junior!! Sitaki kelele bhana nitashukia hapa!!!""
"" Shuka uone Mvua itakavyokunyeshea leo!! Hivi hujaona Hilo wingu na hapa Sina mkoti Nina peans TU na tshrt!!"" Harafu simu kubwa mbona leo hauna??"
Lunnah Alichukia na kumpatia simu kubwa Junior!!
"" Ayaa!! Simu hii hapa!! Kagua!! Tumia uwezavyo!! Lunnah alishuka na kuelekea ndani make muda huo Alikuwa Tayari wamefika!!
Junior Aliamua kumfuata Hadi Ndani!! Alifika na kukaa Huku Lunnah yet alipigilia Hadi chumbani na kuoga baadae alirudi sebuleni na kumkuta Junior kawasha simu akiwa anapitia picha za Imlany.
"" Oooh!! Kumbe umeumia sana!! Naona kwenye picha za Imlany umeview Moja TU! Imlany akiwa na Rich ukacomment kwanini hii Imlany akiwa na Rayna hukucomment??""
Lunnah Aliamua kukaa kimya nakuelekea jikoni kuandaa Chakula Cha jioni! Baadae alileta Mezani na kuanza kula, Ilibidi Amshukuru kwanza Junior.
"" Junior!! Nashukuru kwa msaada wako!! Unajua muda mwingi Kuna kitu kinaweza kutokea kwenye maisha yako kikakufanya ukose amani kabisa!! Imlany Ni mtu wangu wa Karibu Sana tangu nifahamiane nae!! Kanifanya nifikie kwenye maisha mengine kabisa!!
"" Ukweli Nimeumia!! Na nimefurahi pia Baada ya kuona Duffer wangu anafikia hatua nyingine ila kwangu naona ule ukaribu Wake kwangu utapungua!! Nafasi yake kwangu Nitazidi kuimiss Sana!! Muda mwingi nilipokuwa Sina furaha nilimfanya kuwa mfariji wangu!! Naona kwasasa nafasi aliyokuwa anaitumia kwangu, Sasa Ni wakati wake kuitumia kwa Rayna!!
"" Kanifanya nijue maisha Hata jinsi yakuishi na jamii yangu inayonizunguka, Hata katika Kazi zangu za kiofisi amekuwa Upande wangu!! Pia kanifanya niyajue maisha kwa ujumla!! Daima nitamkumbuka Sana Duffer wangu!! Hats kwenye Safari ya maisha yake namtakia maisha yenye Amani TU!! Na Kila la KHERI.
Lunnah Alimaliza kuongea Huku machozi yakitiririka, baadae alishidwa kabisa kuendelea kula ikawa nikilio TU!!
Junior Ilibidi jukumu libakie kwake alianza na kumbembeleza Huku akimtia moyo.
"" Lunnah!! Najua Imlany mmetoka nae mbali!! Hata haya machozi yako kweli yanamaanisha Ni jinsi gani unaumia ila kumbuka! Hakuna kitu kisichokuwa na Mwisho Baada ya Ndoa Kuna maisha itafika hatua Wewe utazoea, naamini Hata Imlany na yeye bado anakukumbuka huko aliko!! Kwake ulikuwa na nafasi Hata akikumbuka ile nafasi yako kwake Ilikuwa Ni ya muhimu!! Usilie tenaa huenda katika ufahamu wa ubongo uliweza Jenga kitu kingine kwa Imlany Baada ya kuwa nae kwa muda mrefu!! Muache kwanza kwasasa swala la Ndoa Ndio limetawala ufahamu wake wa akili!!!"
Lunnah Baada ya kusikia maneno ya Junior alifarijika kiasi chake!! Alichukua Juice na kumumiminia Junior.
"" Basi tunywe kwa furaha tenaaa!!!"
Junior Alichukua Juice na kinywa fundo Moja Kisha alishusha Glass chini Huku akimtazama Lunnah!! Aliamua kumuuliza.
"" Vipi Lunnah!! Siku zote umezoea kuniita Wewe Junior!! Vipi leo Kama utatoa neno "Wewe'' na "Junior" ukaweka Dusky!! Angalau TU limech Kama la Duffer wako Imlany mnavyoitana na Mimi nikawa Dusky huoni litaleta Mantic??""
"" Oooh!! Junior!! Now uwe Dusky!! Ni jina zuri lenye maana ya rafiki wa Kweli na Ndani ya urafiki Kuna uhusiano!" Mimi haya majina kwasasa nayaogopa Sana hasa kinapozalishwa kitu Uhusiano Ndio kinamfanya mtu azidi jutia!! "" Kama uliwahi fatilia season 'BEYHADH" Bila Shaka uliona haya majina yalivyotumika kwa wahusika walivyokuwa wakihangaika!! Itoshe TU kusema nitakuita " Junior"" na Sio "" Wewe Junior!!""
'" Ni sawa Lakini!! Bado Nina Swali Moja kwako!!" Nikuulize?"
"" Uliza!!""
"" Umewahi kuwa na hisia na mtu yeyote!!??"
"" Maswali gani Sasa hayo!!!?"" Eee!! Nishawahi!!!
'" Uliwahi fikisha hisia kwake na Ulipomwambia alikujibuje!!!?"
Lunnah alifikilia chakujibu lakini aliamua kukaa kimya Huku akijiuliza,
"" Je! Ni Imlany Why!! Sijawahi mwambia, huenda ningekwambia angenipa majibu mazuri TU!!"
Junior Aliamua kumsitua, make muda wote alikuwa kimya asijibu chochote!!
"" Najua Ndio una hisia na mtu!! Lakini nishajua dhahiri unampenda Imlany na yeye anakupenda ila hawezi kukwambia kwakuwa kwasasa yupo na Rayna na anaenda kuoa!! Isitoshe nikwambie TU, Mimi Hisia zangu zipo kwako toka muda mrefu!! Nataka nikuoe Wewe ila nitafanya hili Baada ya kukamilisha umepata vitu vyako vyote ulivyozurumiwa!!"
"" Aaah!! Harafu kwanini Junior unafanya haya you kwangu Nini maana yake make umekuwa ukifatilia maisha yangu toka awali!!!?"
"" Kukutafuta kwangu Ilikuwa Ni nje ya maisha yako!! Kumbuka Hata siku Nakuona!! Nilikupenda pasipokujua kuwa Wewe Ndio mwenye ile bahasha!! Namimi nilipoleka ile bahasha nilipewa agizo la kukutafuta mpaka nikupate ili upate hakiyako ya msingi!! Na nilipogundua mwenye bahasha Ni Wewe na Ni mtu nimpendae Ndio nikalipa kipaumbele swala lako ili nikamilishe hatima yako!!
Natamani Siku Moja na Mimi unipende Kama Duffer wako ulivyokuwa ukimpenda!! Natamani Hata Mimi leo unione Kama Duffer wako Imlany mlivyokuwa mkiishi na Mimi natamani maisha yenu yalivyokuwa!! Naomba unipe nafasi hiyo kwako!!
"" Vipi tenaa kwanini Sasa umeanza kulia tenaa?? Au Maneno yangu yanakuuzi Wewe!!??
,,,,,, Itaendeleaa,,,,,,,,
Usikose Sehemu ya 14!!
Nini kinaenda kutokea tenaa kwenye mkasa huu.
Like, Comments, Share.
Mnaniangusha kwa Sapoti jamanii 🤔 wale mnaopenda kusoma Hata like hamna Wala comments!! Huwa mwanikatisha tamaa kabisa!!!👿😨😫
SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER . MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 14. 0746638941 (Wtsp).
ANZA NAYO.
"" Vipi tenaa kwanini Sasa umeanza kulia tenaa?? Au Maneno yangu yanakuuzi Wewe!!?? ENDELEA.
"" Hapana Junior!! Naomba unipe nafasi kwanza!! Akili yangu kwasasa inaniuma Kweli!! Ngoja nikapumnzike Kwanza tutaongea baadae!!"
"" Sawa kapumunzike!! Nitakuja kesho kukuona ila punguza stress!! Upe moyo maamuzi sahihi na pia angalia maisha yako ya mbeleni hatima yake!!"
"" Sawa!!! Usijari hata hivyo nipo okay!!"
Ni siku nyingine tena kwa Lunnah alikuwa zake ofsini!! Meneja wake alifika na kumtaka Kuna Ujumbe wake kwa Ancle anamhitaji.
Lunnah Baada ya kusikia hivyo alikosa ujasiri kabisa na kumfanya aende kishingo upande!!! Alifika na kumwamkia Ancle Kisha Aliketi.
"" Ancle nasikia unanihitaji!! Nini wito wako!!??""
"" Nimekuita hapa nipitie mahesabu ya Mwisho wa mwezi!! Kingine leo Madam kutoka Cassino atakuwa hapa!! Na Mimi Sitaki akukute hapa nikuombe leo hautakuwa kazini na kesho!! Itabidi utulie nyumbani kwako!!!! Ni Hilo tu waweza kuondoka!!!
"" Ancle si ulisema Wewe!! Unajiamini namimi nataka kuonana na Madam ili nimuthibitishie kuwa Nina Kazi yangu na kwenye Cassino hataniona tenaa!!!
Ancle alichukua simu yake na kumpigia Meneja!! Muda huo alifika na kumchukua Lunnah na kumtoa pale Hadi nje!! Lakini alibaki akifikilia Mambo mengi Sana!!
"" Ancle na Madam nahisi huwa wanna ukaribu Zaidi haiwezekani Kama Ni biashara za kwendaa kuchukua watoto wadogo Ndio kujenge ukaribu kiasi hiki!! Au Wanachukuana na Madam!!""
Lunnah alitaka ashuhudie Nini kipo nyuma ya Ancle na Madam, alimwambia Meneja wake amuache Kwanza!! Ataenda pekee!!
Baadae aliona Kuna gari ilikuwa inaingia eneo Lile!! Aliiamua kubanza sehemu Huku akitaka ashuhudie mtu anayeshuka hapo Ni Madam kweli!!
Kuna kijana Alishuka huku akiwa kavalia kofia Na peans!! Lunnah alipomuona alishituka Sana! Kidogo Ndio anamuona Madam na yeye anashuka.
"" Mbona Ni Junior tenaa!! Kwanini kavaa nguo za mitaani hivyo japo kuvaa peans Ni kawaida yake!! Ila kajiachaniza hivyoo!!"" Na vipi anaukaribu gani na Madam!!"
Lunnah aliondoka pale akiwa amechoka Sana, alijivuta mdogo mdogo Hadi barabarani huku akisubili usafiri wa kumpeleka Hadi kwake!! Siku hiyo alisubili Sana pasipo kuona usafiri wowote!! Baadae Aliona gari ya Meneja wake ilifika pale na kumchukua.
"" Vipi Lunnah!! Mbona haupo kwenye mood leo!!!"
"" Kawaida TU Frank!!! Siku huwa hazilingani at!! Nipeleke Kwanza hoteli Nzuri nikatafute Chakula!!!
"" Lakini Lunnah!! Nina swali!! Nataka nikuulize Wewe!!?""
"" Uliza!!!"
"" Hivi Ancle yako huwa wanabiashara gani Na Madam wa Cassino!!? Make Ni muda mrefu huwa anakuja anakaa Kama siku mbili, tatu akiwa ofsini!!! Na muda mwingine huwa anafanya Kazi za kiofisi!!"
"" Mhuuuu!!!! Hadi za kiofisi tenaaa??"
"" Ndio hivyoo!! Baadae huwa wanaondoka wote!!"
"" Vipi kuhusu huyo Dreva tax aliyeingia huwa wamfahamu!!!?
"" Yule Dreva!! Huwa nashidwa kumuelewa make Kuna muda nilimuona sehemu akiwa kavaa gwanda la jeshi!! Nikajifanya kumshobokea Lakini alinikanya Mara mbili mbili nisiendelee kumfatilia Tena akanipa onyo nilivyomuona nisimwambie mtu yeyote anaweza kunidhuru!!! Namimi sinaga habari na tenaa!!!"
"'' sawaaa!!! Naomba nipeleke Nyumbani TU!! Hapa Sina mood Tena wa kula!!""
Lunnah alifika Hadi Nyumbani na kukaa Huku akifikilia Mambo mengi Sana kichwani kwake!! Aliamua ajipumnzishe ili aweze kutafakari Jambo Hilo kwa kina Zaidi!! Ikiwezekana Basi aoteshwe hata Ndoto juu ya Jambo Lile!!!
Alilala kidogo na kusitushwa na simu ya My Duffer!! Akimpigia video call!!
"" Hellow Duffer!!! Mbona umenitenga kiasi hicho!!! Kipi nimekuuzi!!!?"
"" Sijakutenga bhanaa!! Majukumu TU, vipi Lakini process zenu zaendeleaje harafu Ancle yupo wapi??""
"" Mhuuuu!! Maswala ya Ancle Mimi sijui bhana!! Nina muda sijaongea nae nahisi yupo kwa pilika zake!! Mimi ninachotaka kujua khari yako TU!!! Unajua nimekumic at!!!""
Lunnah Aliamua kukata simu, Kisha aliizimaa!!!
"" Duffer!! Ancle!! Junior!! Madam!! Rayna, Shangazi yangu!! Ni walewale TU!! Hamtaniona nawasiliana na Nyie tenaa!!!
Siku mbili zilikata kimya kimya pasipokuwa na mawasilino yoyote!! Upande wa Imlany aliwaza mbali Sana!!
"" Najua Duffer!! Una wivu na Mimi na Ndio kitu kinakusumbua!! Nitafunga Safari kwaajili yako!! Nataka uniambie Ni kipi kimekufanya usihudhurie kwenye Sherehe yangu!! Mimi Sitaki Duffer anayeshidwa kushirikiana na Duffer wake at unajitenga!!!""
Huku kwa Junior nayeye Baada ya kumtafuta Lunnah asimpate kwenye simu Aliamua kuchukua usafiri na kuelekea Hadi kwakee.
Alifika na kumkuta Mdada wa kazi alikuwa akifua fua pale!!
"" Dada!! Umzima?? Vipi Lunnah!! Nimemkuta!!!??"
Dada!! Alifikili Cha kumujibu huku akikumbuka maneno ya Lunnah!! "" Akija mtu yeyote kuniulizia Sitaki umwambie nipo!! Mwambie katoka kidogo!!"" Ndipo Aliamua kumjibu.
"" Samahani Kaka!! Lunnah Alitoka kidogo!! Ila atarudi midaa!! ""
"" Okay Sina haraka!! Hata hivyoo Mimi mwenyeji wake Sanaa!! Ukimwambia Junior TU, hatakuwa na swali tenaa!! Ngoja nikute namsubili sebuleni hapa!! Huku akiingia Ndani.
Huku kwa Dada wa kazi alibaki kaduwaa asiamini Kama Mgeni wake angeingia Ndani!!
"" Hapa nitafanya Nini Lakini!! Ngoja nikimbie Ndani nikwambie Lunnah Kila kitu kuhusu mgeni wake!!
Huku kwa Lunnah hakuwa anajua kipi kinaendelea hapo alikuwa alitoka Chumbani kwake akielekea nje huku akizidi kumuita Mdada wa kazi!!" Dada!!! Dada!!! Dadaaaa.....!!
Alipita sebuleni pasipo kujua Kama kuna mtu!! Make Junior alikuwa katulia huku akichezea laptop yake!! Baada ya kumuona Lunnah alimpiga jicho la chinichini!! Huku akizidi tafakali Mambo mengi.
"" Lunnah!! Wewe Ni Mdada Mrembo Sanaa!! Naona umejiachia kinyumbani nyumbani!! Harafu umeniiga kuvaa peans na t-shirt leo!!"
Huku kwa Dada wa kazi alikuwa tayari kafika!! Hadi mlangoni!! Alifika na kutua jicho kwa Junior akiwa busy na laptop hapo hapo Ndio anagundua huenda Lunnah! Hakumuona Junior!!
"" Dadaa!! Mgeni yupo Nyuma yako!!!"
Lunnah Ndio anageuza shingo nakumuona Junior yupo zake busy na Laptop. Baadae alifunika laptop yake na kumkalibisha Lunnah!!
"" Duffer wa Imlany!!! Karibu Sana Nyumbani kwako jisikie unae furaha!! Japo haunayo amani mpaka muda wote wazimaa simu!! Unazani kuzima kwako simu Ndio kusov Tatizo!!?? Anyway Mambo ya Ng'oswe mwachie Ng'oswe!! Sembuse Mimi Mazoea!!!"
Lunnah Alimtizama Mdada wa kazi!!
"" Samahani tupishe kidogo!! Wewe endelea na kazi zako!! Huyu Ni Junior!! Ni rafiki yangu!! Namjua vizuri usije ukajihisi vibaya, naona umeogopa hebu kuwa na amani tu!!"
"" Ayaaa!! Junior!! Umeona uje kimya kimya!! Si hapa kwako? Mazoea zoea TU unanifanyia!!!""
"" Sasa Ndio unisimamie!! Wewe huwezi ukakaa ukaongea umetulia!! Wataka tufokeane au Tuchambane!!! Naona umevaa peans leo!! Hakika tumemech!!"
Lunnah Aliamua kukaa Huku akijitenga pembeni akiwa na hasira za Junior kumuona kwenye gari akiwa na Madam!! Aliamua kufunga mdomo Wake akimsubili Junior aongee!!!
Junior alichoamua!! Alisimama na kuelekea Hadi sehemu aliyokaa Lunnah na yeye akabanana hapo hapo, Kisha alinyosha mkono wake na kuuzungusha shingoni kwa Lunnah na kumvutia kwake huku wakitazamana Ana kwa Ana usoni!!!""
""" Lunnah!!! Najua Wewe!! Ni Mwanamke mpambanaji na una Mambo mengi yakufanya!! Lakini unafeli kitu kimoja unapoona kitu kimeenda kinyume fanya kuuliza ili utatuliwe tatizo!! Kwanini Wewe unapopatwa Shida unaamua kukaa kimya nakuchukua maamuzi ya kuzima simu!! Najua una wasiwasi na Mimi tangu unione juzi nashuka kwenye Tax nikiwa na Madam!! Na hicho Ndio kimekufanya unichukie!!!
Nilitegemea utaniuliza Baada ya kuona hivyo!! Lakini ukaamua kuzima Simu!! Hata hiyo akili yakujiuliza kazi yangu na Udreva tax unaambatana na Nini!! Wewe huwazi!! Sawaa Basi fanya kitu kwaajili yangu!! Junior Aliamua kumuachia na kuchukua Laptop yake akaendelea kufanya kazi yake!!
Lunnah alibaki katulia TU huku maneno ya Junior yalikuwa yamemuingia kichwani!! Aliamua kusimama aondoke Lakini Junior alimvuta na kumrudisha kwenye seat!!
"" Lunnah!! Unae hasira?? Kwaajili yako hii kazi naifanya Lakini bado wanichukia Mimi!!! Hivi Ni lini utanipa kipaumbele Kama Imlany unavyomthamini!!!""
Lunnah!!! Alizidi kukaa kimya pasipo kumjibu tenaaa!! Kitendo hicho Junior kilimkasilisha Sana!!! Ilibidi asimame na kuondoka kwa hasira!!!
Lunnah na yeye alifanya Kama alivyomfanyia Junior!! Alimvuta na kumkalisha chini Huku akibaki yeye kusimama, Huku Junior na yeye aliona sio Mbaya abaki akisimamiwa alimvuta Lunnah nakumkalisha miguuni kwake Huku wakizidi tazamana wote wakawa wamepigwa bumbuwazi!!!
Junior Aliamua kumvuta Lunnah na kumsogeza karibu na rips zake na kukutanisha ndimi zao!!
Muda kidogo Lunnah Ndio anasituka Huku akijinasua kwa Junior na kusimama huku akielekea bafuni!! Alifika bafuni na kunawa uso wake huku akizidi kutizama kwenye kioo.
""" Daah!!! Hivi nilipatwa na Nini leo!! Kipi kimenikuta leo?? Ani Junior kanikiss kwelii!!!""
Huku kwa Junior alibaki kakaa huku akizidi kutafakari Mambo Mia kwa sekunde Moja huku tafakuli yake kubwa ilikuwa Ni Siku Moja kumumiliki Lunnah!!! Na hii Ndio ilikuwa Ni Ndoto yake kubwa!!!!
Lunnah Ndio anarudi pale!! Huku akiwa na aibu aibu!! Huku kwa Junior nae Baada ya kumuona Lunnah Ndio anazidi kuchanyikiwa kabisa!! Aliamua kuaga na kuondoka.
"" Lunnah!!! Nimeitwa kidogo kazini!! Nikipata muda nitakuja kukuona tenaa!! Naomba Basi leo!! Washa simu zako huenda kukawa kuna Jambo zuri linakuja!! Harafu Niite Basi Dusky!!!"
"" Ayaaa!!! Wewe nenda tu!! Mpaka uniage at mida unarudi!! Badoo nikuite Dusky!! Dusky!! Kila Siku unaimba Wimbo uleule!! Okay Safari njema Dusky!!! Ila Duffer wangu Ni Imlany TU!!!""
,,,,,, Itaendeleaa,,,,,
USIKOSE kufatilia mkasa huu Sehemu ya 15.
Like, comments and Share. Sapot yako Ndio Nguzo ya Mtunzi, kuzidi kuandaa kazi nzuri zaidi!!!
SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER . MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 15. 0746638941 (Wtsp).
ANZA NAYO.
"" Ayaaa!!! Wewe nenda tu!! Mpaka uniage at mida unarudi!! Badoo nikuite Dusky!! Dusky!! Kila Siku unaimba Wimbo uleule!! Okay Safari njema Dusky!!! Ila Duffer wangu Ni Imlany TU!!!"" ENDELEA.
Ilikuwa Ni Siku nyingine tenaa leo Imlany alikuwa safarini Akielekea kwa Lunnah!! Huku kwa Lunnah siku hiyo alikuwa mahakamani kapeleka vitambulisho vya kushughulikia kesi yake! Muda kidogo alipokea simu kutoka kwa Meneja Wake!! Imlany alikuwa tayari yupo ofsini akimhutaji.
Lunnah Baada ya kukamilisha Mambo Yake!! Aliwasha gari lake na kuelekea hati Ofisini, alimkuta Imlany kakaa na teamwork wakiwa na kikao Cha dharula. Lunnah ilibidi afike na kukaa Huku akiendelea kusikiliza kikao!!
Mwisho kabisa Baada ya kikao kuisha Imlany alikuwa amekuja na Kadi za mwaliko alikuwa akigawa kwa watu waliokuwa wamemaliza mchango!! Baada ya kumaliza kugawa wafanyakazi walisambaa na kuendelea na majukumu ya kiofisi!!
Huku kwa Lunnah muda wote alikuwa akisikiliza TU, Baadae alichukua ile Kadi aliopatiwa na Imlany na kuanza kuisoma baadae alimaliza nakuiweka kwenye mkoba wake!! Kisha Alielekea Ofisini kwakee na kuendelea na kazi.
Muda kidogo alipokea Ujumbe wa message kutoka kwa Imlany.
"" Duffer!!! Bado unahasira na Mimi!! Hutaki hata tusalimiane!! Ni sawa!!!" Umenikuta nipo busy Ndio!! Basi tutoke Lunch nimemisi kula na Wewe!! Nakugonja Hapa nje!!""
Lunnah alimaliza kusoma ule Ujumbe Kisha alimjibia, "" sawaa!!" Lakini moyoni mwake Alikuwa Tayari ile Kadi ya mwaliko Ishamchanganya!!
"" Ayaaa!! Ni sawaa harusi imefika!! Kwanini Lakini naumia!! Wakati Imlany Ni wa Rayna!! Namimi sijui Ni wanani!! Au nitakuwa wa Junior!! Lakini nampenda Duffer wangu!!""
Muda ulifika walitoka na kuelekea 🏨 hotel, iliyokuwa katikati ya mji na kupata chakula!! Imlany aliamua aanze kumsalimia.
"" Duffer!! U mzima lakini?? Naona leo sijapata salamu yako!! Vipi una hasira na Mimi!!!"
"" Me mzima TU!! Hasira gani tenaa!! Ule muda nilikukuta upo kwenye kikao!! Wazani Mimi ningejitoa kiherehere TU at nije mbele kukusalimia!" Kwasasa Wewe Ni Bwana harusi mtarajiwa!! Iweje Mimi nilete mazoea kivile!!"
"" Vizuri!! But Wewe Ni Duffer wa karibu!; Muda mwingine nahitaji faraja kwa upande wangu hivi unajua Ndoa siyo ya kuiparukia!! Na hapa nikikosea kuoa Ndio nitajutia maisha yangu yote!! Sijui nitarudi kwa Duffer wangu na yeye huenda muda huo atakuwa kaniletea Kadi ya Mwaliko!!! Daaah!! Mungu zidi kuniimalushia chaguo langu siku zote!!""
"" Ayaaa!! Unawaza mno na Wewe!! Hebu relax akili yako itulie Laah!! Hivyo ukiwa na mawazo mengi utanifanya Duffer wako nayeye apate mawazo!!!""
"" Usijali!! Najua huwa unajali Sana kuhusu Mimi, ila unakosea kitu kimoja TU!! Haunipi sapoti kwenye Mambo yangu hivi waweza nambia kwanini sikukuona kwenye tangazo la Uchumba siku I'll kanisani!! Mimi nilitegemea nitapiga picha Moja ya kumbukumbu na Wewe!!!""
"" Wewe nae!! Nilikwambia Mambo mengi siku hiyo nilikuwa nimebanana!! Ayaaa!! Sikuja Ndio!" Kwani siku yenyewe hukutangaza!!??""
"" Masiala mengi tatizo!! Ila kuja kwako Wewe!!" Kwangu ilikuwa Ni faraja toshaa!! Harafu naomba isijirudie tenaa bado Nakuhitaji Wewe uzidi kuwa karibu yangu Lunnah! Na Mambo mengi yakunisaidia kwa wakati huu!!!"
"" Ni sawaa!! Lakini Mambo gani hayoo!! Mimi nitakusaidiaje?
"" Nataka ufike kwenye harusi yangu!! Japo nimesikia hautafika!!" Duffer!! Wewe Ni faraja kwangu!!! Na so hivyo TU Nakupenda!!!"
"" Duffer!!! Lakinii,,,,, !!"
Imlany aliamua kumnyamazisha kwa kumziba mdomo na mkono.
"" Muda mwingine acha Hisia!! Niziweke wazi hata Kama nitakuwa nafanya hivi nafanya kwasababu hatua yetu imefika!! Na ilikuwepo tangu zamani kabla hata hatujaonana na Wewe!! Huenda ningekuwahi kabla ningekuoa lakini kwa Sasa sio wakati wakutumia ngeli Hapa!! Itoshe TU kusema Nampenda Duffer wangu!!!' ila nitazidi kuwa na Wewe karibu!! Angalau nizidi kukuona karibu yangu TU!!! "" Vipi Lakini Umempata Kaka yangu/ Daah!! Shemeji yangu bhana nilisahau!!!"
"" Nikimpata nitakufanyia Suprise Kama Wewe! Ulivyomleta Lunnah nyumbani pasipo kunambia Kama una mtu!!! Duffer gani anaemficha Duffer wake!! Mimi naona Duffer kwa Sasa si Duffer wangu!! Keshabakia Ni wa Rayna TU!!!""
"" Umeanza kumind naona!! Okay!' sio Shari!!, Najua Duffer wako sahizi Ni Junior na umemsave " My Dusky!!" Malizia TU kuandika "Duffer" na sio " Dusky" Sahiii sipati Upendo wa Duffer wangu kisa " Dusky Junior!!""
"" My Duffer!!!" Mbona na Wewe una mind kiasi hichoo!!
"" Wewe'' Ni Duffer wangu!! Sina Duffer mwingine najua hata uliponitoa huenda ningekuwahi kahaba mkubwa leo Lakini umenifanya niheshimiwe leo!!""
Imlany aliangalia masaa na kuona muda umeenda kwelii!!
"" Duffer!! Muda umeenda kwelii hapa hamna kurudi kazini Tenaa naomba twende Nyumbani!! Hapa kazini Hadi Jumatatu.
Walielekea Hadi Nyumbani na kukaa Huku Wakiendelea na sitori. Imlany Alisimama na kuchukua kinywaji kwenye Freezer, Kisha alichukua Wayne na kumimina kwenye Glass.
"" Lunnah!! Muda mwingine akili huwa inakuwa nzito mpaka inasababisha kichwa kiwe kizito nakizidi kuuma! Ninachotaka kufanya hapa nataka nidilute angalau kichwa kiwe chepesi TU Ndio furaha yangu naona!!!
"" Kwanini Lakini!! Unafanya hayo yote najua Wewe sio mzoefu wa kunywa pombe Ndio maana hata siku ile ulikunywa pombe ulikuta unamsaliti Duffer wako pasipokujua.
Imlany alizidi kumimina pombe na kupiga Glass Kama mbili Kwa pupa, Kisha alishusha Glass yake chini akimuomba Lunnah amuongezee tenaa!! Lunnah akawa amemuongezea kidogo na kuichanganyia na Fanta.
"" Unajua Lunnah!! Wewe Ni rafiki yangu!! Ni rafiki ninaekupenda Sana Kama Duffer wangu wa karibu!! Yaani Mimi nipo katikati yenu kulia kwangu Kuna Rayna harafu kushoto kwangu Kuna Lunnah ( Duffer). Je hatima ya yote Ni Nini??
"" Imlany!! Naona pombe tayari zimeanza kukuingia!! Naomba ukalale!!"
"" Hapana Sina usingizi!! Nakuhitaji Wewe tuongee!! Mpaka asubuhi make kwasasa naenda kuwa kifungoni!! Ulivyosema kweli endapo nitaoa sitakuwa Tena na ukaribu na Wewe!! Naomba leo niongee na Wewe!! Muda mwingi nakumbuka ukaribu wako!! Muda mwingine nimeanza kuwa na wivu hata kwa Ancle nakuwa na mashaka nae!!
Kuna siku ile pindi upo kwetu!! Ilikuwa Ni usiku Nilimuona Ancle anatoka Chumbani kwako, Namimi siku hiyo nilikuwa natoka nje kufungua maji make mlikuwa mmeyafungia, ila Ancle hakuniona nikaamua kulifatilia swala hili kwa kina Zaidi.
Harafu kesho yake Ndio unanitumia message kuwa hutaki Kazi!! Na unataka urudi Cassino!! Na siku hiyo hukuja kazini na Mbaya Zaidi unaumwa Japo uliniambia Ni Koo!! Lakusumbua Mimi nikajua Ni michezo mnacheza na Ancle, Ndio maana siku nakuijia kwenye Cassino niliamua kunywa pombe ili nitoe aibu ya kitu ambacho kitatendeka!! Nikawa nimekufanyia vile! Lakini nilikuta utofauti kabisa ikabidi nianze upya kufatilia kilichofuata ya Ancle na Wewe na kwanini hataki urudi nyumbani na kwanini akujengee Nyumba kubwa ya kuishi huku!!!??""
Lunnah Ilibidi aanze kushangaa na kujiuliza maswali mengi, huenda Imlany anaelekea kujua ukweli wa Ancle ilibidi amjibu TU hafahamu hayo yote.
Imlany siku hiyo alikuwa na Jaziba alimsogelea Lunnah na kumshika shingo.
"" Duffer!!! Nakupenda, nakuamini, Nakuthamini, pia nakuheshimu naomba useme ukweli Basi kuliko kunificha!! Ukweli wako Ndio utakufanya uwe huru Wewe na uzidi kuishi maisha ya kujiamini!! Ancle Kama Ni Adui yako weka wazi!! Mimi nipo tayari kukusaidia!!;""
Lunnah siku hiyo alikipata Cha Moto kwa hasira aliyokuwa nayo Imlany, mpaka Lunnah alichanganyikiwa na kujiuliza Ni hasira TU anayo au Kuna kingine!!! Aliamua kumgeukia ili azungumze na yet angalau kumshushia hasira;
"" Duffer!! Tuongee taratibu Basi!! Unajua wanishangaza hukuwahi kusema na Mimi ukiwa katika khari hiyo!! Utanifanya niwe muoga kwako!! Kama nimekukosea naomba unisamehe basii!! Siku zote Duffer na Duffer wake huwa wanaelewana inakuwaje leo hii Duffer wake anataka kumzuru Duffer!! Cool down my Duffer!!!
Maneno ya Lunnah yalimfanya Imlany ashushe pumunzi Ndefu Kisha alimkumbatia Lunnah kwa hisia Kweli huku machozi yakimtoka na akigugumia kwa maumivu!!
Lunnah Alibaki akishangaa Baada ya kusikia Duffer wake Leo analia mbele yake Tena kwa machozi, Alimuachia taratibu na kumgeuzia mbele yake ili Amtizame vizuri!!!
Imlany Baada ya kugeuka Aliamua kuegama miguuni kwa Lunnah na kujilaza mapajani Kisha alizungumza na Lunnah.
"" Samahani Duffer!! Najua huenda nimekuuzi kwa namna Moja au nyingine nimekukaripia ila naomba unisamehe TU!!; Na unichukulie Ni hasira nilizokuwa nazo!!! Kuna siku nilitamani kujua simulizi ya maisha yako ila nimeipata toka kwa Junior!!
"" Pole kwa kupotelewa na Wazazi wako!! Pole kwa changamoto za maisha!! Pia Samahani kwa kukuharibia Usichana wako nayo pia Ni changamoto huenda Uliwahi kuwaza mwanaume wa Kwanza Ndio atakuwa mme wako lakinii Safari bado....
Lunnah Baada ya kusikia maneno ya Imlany yalimfanya akumbuke mbali Sana!!! Machozi na kilio kikahamia kwakee!! Imlany aliamua kuchukua zoezi la kumbembeleza.
"" Sorry Tena Duffer!! Huenda nimekufanya ukumbuke maisha ya Nyumaa ila maisha yako Ni Kama yangu tu! Ndio maana Mimi na Wewe TU Duffer!!!"
Siku ya leo nitakuwa muwazi kwako kwakuwa sisi tumeamua kuwa " Duffer" Tena tumekula kiapo." Maisha yako Ni maisha yangu!! Mimi na Wewe tuna makubaliano ya pamoja!! Jambo jema kwangu na kwako liwe jema!! Likiwa baya kwangu na kwako liwe baya!!
Natamani kumbukumbu zangu za zamani zinirudie nijue kuwa Mimi nilikuwa Nani kabla ya kuanza kuishi na Ancle!!!
Kila nikijaribu kutafuta kumbukumbu zangu huwa kumbukumbu zinakuja Lakini Ni kwa kuota pindi nipo mtoto Mdogo nilikutana na mtoto mwenzangu wa kike kwenye Gari nikawa tumezoeana nae kwa muda mfupi tu, siku hiyohiyo tukawa marafiki wa karibu Sana!!
Baba yake alitokea kunipenda sana!! Akawa amenipatia kitambulisho kilichokuwa na picha ya familia yake!! Lakini Kila muda nikikumbuka sura ya yule mtoto mmefanana nae kweli!! Shida Sasa kile kitambulisho kimepotelea ndani Kama Miaka miwili hivi imepita ila kumbukumbu yangu huwa inakumbuka siku yenyewe ilivyokuwa mpaka nikawa hapa.
"" Kwani Ilikuwaje Duffer???"
Siku hiyohiyo nilikuwa na Wazazi wangu ndani ya Gari tukiwa safarini!! Tulifika Mwisho wa Safari tukawa tumeshuka na yule Babake na yule mtoto waliendelea na Safari ila sisi Baada ya kushuka TU kulitokea na uvamizi mkali Wazazi wangu wakawa wameuwawa na Mimi nikawa nimejificha kwenye mtaro Ndipo kuna Gari ilifika pale Baada ya Wazazi wangu kuchukuliwa na kupelekwa hospital, Alishuka Baba mmoja na kunichoma Sindano!! Nikawa nimelala ila nilikuja kuzinduka nikiwa kwake, Baada ya kuzinduka aliniita Imlany Kama jina langu na kuniambia nimuite Ancle, na Ndie huyu huyu mpaka leo naishi nae.
Ila Mbaya Zaidi huwa sikumbuki vitu vingine huko nyumaa hata juu ya Wazazi wangu ilikuwaje!!
Muda mwingi huwa naota Ndoto Mara Moja Moja TU, Kila nilipokuwa nikiangalia kile kitambulisho mpaka nimekuwa mkubwa kumbukumbu zangu zilikuwa zinakuja nikiwa na kile kitambulisho Japo Ni Mara Moja Moja Sanaa.
Kuna siku Moja Ancle alinikuta nakiangalia kile kitambulisho akawa kaniomba na hakunirudishia Tena hata nilipomuomba aliniambia kimepotea. Na hicho ndio kilichokuwa kinanisaidia, Kila nikikitizama Ndio nakumbuka sura ya yule mtoto ukweli mmefanana nae sanaaa.....
,,,,, Itaendelea,,,,,,,,
USIKOSE kufatilia mkasa huu Sehemu ya 16.
Kwanini Imlany anamfananisha Lunnah!! na yule mtoto wa kwenye kitambulisho.
Like, comments, Share. Like zikianzia 100.... Nitakuwa naleta kwa siku vipande viwili.