SIMULIZI: IKAWE KHERI MY DUFFER . MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: 07. 0746638941 (Wtsp).
ANZA NAYO.
"" Duffer Nini!!! Aya shuka Basi uje ukae sehemu yako!! Huku akifungua mlango wa Gari ashuke.... ENDELEA
Walifika Hadi Nyumbani lakini walishangazwa baada ya kuona Kuna Gari imepaki kwenye Nyumba Yao.
Mara Ratifa Alipita pale Alikuwa anaenda kumwaga uchafu, Ile alipowaona aliiailisha kwenda kumwaga ilibidi aweke pale uchafu na kuelekea Moja kwa Moja Hadi kwenye Gari.
"" Kaka Imlany!! Rayna kaja na Mdogo wake wapo wote ndanii!!""
"" Mbonaa Ghafura hivyo Kuna Nini!! Na wakati alinambia atakuwa na likizo fupi hatoweza kufika!!!"" Imlany Alihoji.
"" Duffer!! Sio kuanza kuhoji Wewe shuka ukamuone Mchumba!! Mchumba!!""
Imlany alifika Hadi Ndani, kwa Rayna alipomuona tu mchumba alikimbilia na kumhag kwa mahaba yotee. Rayna Alimtizama Lunnah kwa nyuma Alikuwa akiwaangalia alichoamua ni kumkonyeza tu, Kisha alimwachia Imlany.
"" My leo nimeona nikufanye suprise bila Shaka umeshagazwa Sana!!""
""" Waooo!! Nimefurahi pia!! But imekuwa Ni Ghafura!!! Okay Karibu Nyumbani tena kwa Mara nyingine!!""
Muda huo huo Ancle na yeye anaingia Baada ya muda mrefu kutokuweka nyumbani. Imlany Alikuwa was Kwanza kumuona alimsogelea na kumkumbatia Ancle.
"" Waooo Ancle!! Ni muda mrefu kidogo imekuwa sikukuona!! Vipi lakini kazi ziliendaje Huko??""
"" So Good kivile!! Make nimepeleza mfanyakazi mmoja na hapa!! Nimeona nimchukue Lunnah!! Kwa Sasa si amekuwa mzoefu!!?"
Imlany Alisituka kidogo na kubaki akimwangalia Lunnah!! Muda wote na yeye alikuwa katoa jicho!! Imlany aliamua kumuachia Ancle na kwendaa Hadi kwa Lunnah Kisha alimshika mkono.
"" Usiwe na Hofu Kia's hicho!! Naamini utafanya kazi na Mimi nitakuwa upande wako!! Sawa Duffer!!!" Kisha alimkumbatia.
Rayna aliona yote hayo!! Moyo wake uliumia Sana, inakuwaje Imlany anakuwa Karibu Sana na Lunnah!! Hiki ndio kimenifanya nije kwa hii likizo. Aliamua kuondoka na kuelekea Chumbani kwake.
Imlany Ile anageuza kichwa Hivi!! Alikutana na Rayna akiwa anawatizama kwa hasira Kisha aliondoka. Imlany aliamua kumuachia Lunnah na kumkimbilia Rayna Hadi chumbani!!
"" Mbonaa unakuwa hivyo Rayna!!!??"
""" Niache!! Bhana!! Kumbe Ndio hicho huwa mwakifanya na Lunnah!! Mbele yangu kabisa unaenda kumkumbatia Lunnah!!"
""'' Wewe unaumia Nini hapo?? Lunnah she's my Duffer!! Anytime nakwambia na unajua kabisa!! Leo unapanic Nini!??"
"" Imlany!! Mimi na Wewe twaenda kufunga Ndoa hivi Karibuni!! Unavyozidisha mazoea kiasi hichoo!! Muda wote unakuwa busy na Lunnah!! Huoni kabisa huo upendo unavyozidi kuugawa kwangu hautoshi!!""
Imlany aliamua kumkumbatia tu,
"" Kumpenda kwangu Lunnah!! Simaanishi upendo wa Lunnah Ndio huo huo upendo nitakaokuwa nao kwako!! Jua basi kutofautisha upendo wetu wa Mimi na Wewe na Lunnah Ni tofauti kabisa!!!""
"" Sasa unamaanisha Nini Imlany!!??"
"" Nakupenda Wewe!! Kama mke wangu wa Ndoa na nafasi yako haiwezi kuzibwa na Mtu yeyote!! Tafadhari jiamini na uniamini pia!! Kwasasa rafiki yangu Lunnah atakuwa mbali na sisi zaidi tumuombee maisha mema tu!!!""
Huku kwa Lunnah aliingia Ndani nakuandaa nguo zake Kisha alitoka Hadi nje kumsubili Ancle atoke ndani!!"
"" Najua Ancle umefanya makusudi!! Kwakuwa Sina pakwenda lazima niende kazini tu!!""
Muda kidogo alimuona Imlany Akiwa anakuja pale alifika na kuchukua begi la Lunnah na kuweka kwenye gari Moja kwa Moja, huku Lunnah Alibaki ameegemia ukuta huku kashikilia kimkoba chake!!""
Imlany aliamua kumfuata sehemu alipomuacha alifika na kumkumbatia TU.
"" Muda wote nitakuwa Karibu na Wewe Duffer wangu!! Naamini sitakuacha kitu chochote kikuzuru Wewe!!""
""" Usijali bhana Mimi nitakuwa sawa!! Zaidi nikutakie maandalizi mema ya Ndoa!!""
"" Aah sawa bhana!! Chukua hii Chen Kama zawadi yangu!! Naomba muda wote utakuwa waivaa!! Sawa Duffer!??""
"" Ahsante!!! Naona Ancle muda wote ananisubilia tuondoke!!!""
"" Lakini Duffer,,,,,,,,,,,!!!
"" Lakini Nini tenaaa,,,,,!!""
"" Nitakukumbuka Sanaa!! But niruhusu nikuage kidogo!!""
"" Uniage tenaaa!! Hapa kwani hatuaganii!!!"
"" Wewe kubali basii!!""
Lunnah alitikisa kichwa ishara ya kukubaliana nae!!. Imlany alisogea na kumpiga kiss mdomoni Kisha alimkumbatia tenaa!!!
"" Nakupenda Duffer!! Naimani utanimisi pia na Mimi nitakumisi kila Mara nikumbukapo ukaribu wako!! Pia nitakukumbuka hata nikiwa ofisini nikitizama meza yako itakuwa wazi muda wote!! Basii!! Nikutakie Safari njema!!""
Lunnah na yeye alishidwa kujizuia aliamua kumrudia Imlany Kisha alifika na kufungua pochi yake na kutoa saa, Kisha alimkabizi.
"" Duffer!! Sitatamani niende nikiwa na zawadi yako!! Acha na Mimi nikupatie hii zawadi ili tuzidi kumbukana wote!!!""
"" Thanks Duffer!! Usingenipa ningekusema kimoyomoyo siku zote!! Na ningekuachia laana ya maisha yako yote!!""
"" Jinga kwelii!! Et laana ya kumlaani Duffer wako!! ""
Muda kidogo Rayna na yeye alifika pale Kisha Alimchukua mchumba wake na kuondoka nae!! Lunnah Alibaki akiwatizama tu Kisha aliingia kwenye gari na kuondoka na Ancle.
¶¶¶¶¶¶¶¶¶
Baada ya Miezi mitatu kupita.
Leo Lunnah alikuwa Kwenye Mihangaiko yake Baada ya kufunga ofsini, Alipita sokoni kuhemea wakati Akiwa anarudi Kuna kimvua kilianza kunyesha ilibidi akimbie na kujibanza kwenye kibanda kidogo!!!
Kuna Gari ilifika pale na kusimama!! Huku Lunnah alikuwa kajikunyata kwa baridi Kali!! Kuna mkaka mmoja ilibidi ampigie hone Lunnah Ishara ya kumgeia rifti.
Lunnah aliingia na hofu kidogo alijikausha Kama hakusikia, mpaka yule Kaka akarudia Tena Huku akimwomba amuamini. Lunnah alitoka pale Kisha aliingia na kukaa kimya. Mpaka Yule mkaka alimsemesha.
"" Dada waitwa Nani!!? Pole pia kwa kijimvua kilichokunyeshea!!""
"" Naitwa Lunnah!!!
"" Okay!! Niite Junior!! Vipi waelekea wapi nikusogeze!!'
"" Miti mirefu, Karibu na Godown!!!
"" Sawa!!!
Mara simu ya Junior iliita, alikuwa Ni boss wake alimpigia simu anahitajika kazini Kuna dharura ya kikazi.
"" Sorry Lunnah!! Nimepata dharura kidogo nahitajika kazini!! Nikikuacha hapa sio mbaya!! Chukua hili koti naimani litakusaidia kujikinga na mvua!!
Lunnah alishuka na Lile koti na kuanza kutembea mdogo mdogo!! Huku akielekea Nyumbani kwakee! Alifika Hadi Nyumbani na kukaa Kisha alivua Lile koti na kulitundika kwenye kamba na kubaki kulitizama.
"" Junior!! Junior!! Sasa mbonaa hujaniachia namba ili nikurejeshee koti lako!! Harafu unafanya Kazi gani Kwanza!!?.
Huku kazini kwa Junior alifika na kupatiwa Kazi Kuna jengo liliungua siku hiyo. Junior alichukua kikosi chake na kuelekea kazini.
Huku Njiani Junior alionekana Kama Ni mtu mwenye Mawazo sana!! Rafiki yake Anord aliamua kumuuliza.
"" Vipi leo naona haupo Okay!! Au Kuna kitu kimekupata leo?? Huwa nakwambia tafuta Mwanamke awe anakutatulia Mawazo yako!!""
"" Na Wewe umeanza!! Ila asubuhi nimekutana na Manzi mzuri kweli nikawa nimevutiwa nae!! Daaah!! Mara simu ya boss!! Njoo kazini kwa ile haraka mpaka nimesahau kuchukua namba yake sijui nitampata wapi?? ""
"" Wewe nae bado sana!! Sijui ukafudwe!! Ayaa!! Hata mtaa hajakuelekeza tuanze doria!!""
"" Mtaa nakumbuka vizuri tu!! Ila Sasa hutaamini yule Manzi sijamkalili sura yake make muda wote alikuwa kainama ila Ana nywele ndefu, zaidi nimekalili mavazi yake sijui akibadili nitampata wapi jamanii!!! ""
"" Uzembe uzembe Ndio maana yule Demu alikuacha tatizo haupo serous Sana!!""
"" Usitake kunikumbusha yule Mwanahawa mtoto wa kizaramo Baada ya kuona Nina kazi!! Mshahara wangu wote alitaka aumalizie kwao!! Ila sipendi mtu mchunaji yaani, akinipenda asipende pesa zangu!!!""
"" Kwanii yule Manzi uliyemuona wazani atakuwa hapendi pesa!!??
"" Sijajua ila anaonekana mstaarabu kweli!! Hata akipenda pesa!! kwakuwa nimevutiwa nae nitajitahidi kumbadilishaa!! Nahisi kukapenda kweli harafu kanajiita ka Lunnah!!""
"" Ayaa bhana!! Leo nimejua umekufa ukaoza hata feeling zako zaonesha okay tupige kazi kwanza!!""
°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°
Huku kwa Lunnah Leo alikuwa kazini akirecord pesa zilizoingia, Siku hiyo Ancle alimtembelea Lunnah alijaribu kukagua kazi zake!!
"" Leo nataka nipitie mauzo yako kwa mwezi Kama umefanya vizuri nitakuongezea asilimia mbili kwenye mshahara wako Kama mauzo yatakuwa yameshuka nitakukata kiwango hicho hicho.""
Lunnah alibaki kimya TU!! Akimsikiliza Ancle. Ancle alikagua Baada ya kujitosheleza alitikisa kichwa kwanza.
"" Naona unajitahidi siku hizi!! Okay hongera kwahilo!! Vipi Lakini Kama nitakupa mshahara wako na nikakuongezea pesa nyingine si utajitegemea na sitasikia habari ya kurudi kwa Mwanangu Imlany Tena!! Harafu Imlany tayari Anamchumba wake Lakini naona unamzoeazoea wataka kuharibu Ndoa ya Mwanangu!!
""" Ancle hiyo sio sababu ya kutaka kunitenganisha Mimi na Duffer wangu!! Siku zote Imlany Ndio huwa ananifanya Mimi nimzoee yeye Ila nachojua unahofia mimi nikikaa nae nitakuharibia kwa Imlany kuhusu habari zako za kwenda kwenye Cassino!! Si sawaa!!!??""
"" Ishia hapo Lunnah!! Tukiachana na Hilo kumbuka maisha yako wewe"" si huna Wazazi unaonaje ukitengeneza maisha yako Huku na ukaepuka skendo Mbaya kuwa ulikuwa wajiuza kwa Cassino!! Vipi Kama nitatangaza kwenye kampuni kuwa uliokotwa kwenye Cassino!!??""
"" Ni sawa TU Ancle!! Mimi sio maarufu kivile hapa!! hata Kama ningetangazwa Mimi kuwa na sikendo mbaya!! Vipi kuhusu Wewe boss mwenye rebo yako ya utajiri huwa waenda kununua wadada tena watoto wadogo watembea nao!! Naona huwazi kwa Hilo Ancle!!!??""
""" Lunnah!! Unanitafuta naona!! Na hapa sitakurudisha Tena ukafanyie kazi Nyumbani!! Okay Mshahara wako huu hapa!! Harafu nakuonya Kama unataka shindana na Mimi Wewe endelea,,,,,
Ancle aliondoka pale Huku akiwa na hasira, aliamua kuchukua gari yake na kuelekea Crub akapunguze Mawazo Kwanza!!!".
,,,,, Itaendeleaa,,,,,,,
Usikose sehemu ya 08.
Hakikisha unalike na kuComments pamoja na kushare kwa group na rafiki ili kukuza Group letu, Kama bado hujajoin tumia hii Link ikulete Moja kwa Moja kwa kurasa.
https://www.facebook.com/groups/263417295228138/?ref=share