MTUNZI. TINNER ROBER
SIMULIZI. ''JES'TINER''
SEHEMU. 01
Ni miaka nyuma imepita katika familia ya mzee Budagala baada ya kutoonana na binti yake Mara tu baada ya kumaliza
darasa la saba, na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha nne huko Kigoma katika
shule ya Kichangachui . Leo ilikuwa ni kumbukumbu ya kumpongeza binti yake
Jestiner haswa kwa juhudi zake alizozionesha katika mtihani wake kwa ufaulu
mzuri uliowavutia wazazi wake, akiwa ni miongoni kati ya wanafunzi waliofanya
vizuri kidato cha nne kwa waschana, akishikilia nafasi ya tano kimkoa kwa
wasichana. Na Leo ilikuwa ni siku yake
maalumu ya kumpongeza.
Jestiner (24), ni binti mcheshi japo
ni mkimya sio kama watu wanavyoamini kuwa mtu
mkimya ni mtu anayejisikia, kwake haikuwa hivyo, alipendelea kupiga
stori na kila mtu ucheshi wake, ulimfanya kujulikana sana kwa jamii. Vilevile
alikuwa na rafiki yake kwa majina alijulikana kama Jasmine, wengi walipenda
kumwita Jescar.
Jescar (23) ni binti wa mzee
Leonard, ni mchesi, muongeaji, Mollah Kamtunuku rangi ya chocolate, rangi adimu
kwa sasa kila mtu anataka awe nayo japo
kamzidi kidogo Jestiner yeye ni maji ya
kunde, na rangi hii ilimpendeza yeye angepewa Jestiner, isingempendeza na wala rangi ya Jestiner, apewe Jescar
isingependeza, rahaulaa!! Watu husema kazi ya Mollah haina makosa. Hivyo ni kwa
ufupi tu jinsi gani warembo hawa walivyokuwa wakionekana kimuonekano wa Sura
zao na nyuso zao zenye kuvutia Zaidi.
Jasmine ni rafiki mkubwa wa Jestiner,
ni marafiki walioshibana,, wamesoma darasa moja tokea darasa la kwanza, hadi la
Saba katika shule ya msingi Ushirombo yaani hii sio kuishia tu kuitana
classmate bali wamekuwa ni kama ndugu sasa,
Mara tu baada ya kumaliza darasa la Saba, Jestiner alihitajika kwenda
kigoma kwa Dadake kumsaidia kazi za hapa na pale, Mara tu baada ya kujifungua mapacha; mmoja
alijifungua kawaida na mwingine kwa operation na hii ilisababisha mwili wake
kutokuwa sawa, Jestiner ilimbidi abaki kumsaidia dada yake kazi za nyumbani.
Miezi ilizidi kujongea hatimaye matokeo
yake yalitoka akiwa ni miongoni mwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato
cha kwanza katika shule ya Upili (sekondari kama ilivyozoeleka) Ushirombo,
kutokana na afya ya dada yake kuwa mbaya ilibidi Jestiner kumchukuliwa
uhamisho, aendelee na masomo yake kigoma.
Ukiskia
mkeka kuchanwa ndio huku sasa…… Kwa upande wa Jescar ilimuuma sana kutengana na
rafiki yake, ukiangalia Marafiki hawa walishilikiana pamoja kwa kila jambo
hawakutupana mkono, walifanya sherehe mbalimbali pamoja na kumbukumbu za
kuzaliwa kwao, kupongezana kwa kufanya vizuri katika masomo wakishirikiana na
hata familia zao, ziliweza kutoa sapoti
kubwa kwa mabinti hao.
Sherehe ilizidi kupamba moto ndugu, jamaa,
marafiki walifika sehemu ya tukio ikiwa ni miongoni mwa wanafunzi mbalimbali
aliosoma nao Jestiner toka awali mpaka kidato.
Mambo yalizidi kupamba moto tena ukiangalia MC, hakuwa mzembe alizidi
kuweka nyimbo mbalimbali zilizozidi kuchangamsha ukumbi huo, huku kamati ya
vinywaji hawakuwa haba kuvutia mandhari ile Kadhalika kamati zote zilikuwa
zimejipanga vyema katika suala zima la kunogesha sherehe hiyo.
*** Upande wa Jestiner alionekana akiwa
saloon Moja maarufu sana katika mji huo, saloon hio ilikuwa ina kila aina ya
mazaga, hakika ukiingia sehemu ile ukitoka lazma uwe mpya. Sasa vuta taswira
kwa urembo wa kigori huyo na kwa kile nilichokwambia sasa kaingia saloon
kuongeza muonekano wake unadhani akitoka saluni atakuwa na muonekano
gani?.......
Jestiner, ile anapiga jicho pembeni alimuona
Jescar kashikilia gauni zuri, lililokuwa limenakishiwa na kitambaa cha hariri,
gauni lile lilikuwa likimetameta hakika lilikuwa ni gauni bomba. Jestiner alimkumbatia, ''Jescar'' ''nafurahi sana kwa
zawadi hii, sikutegemea kama ungefanya hivi, '' nisamehe kwa kua nilikuweka
mbali na mimi'' kwa muda niliokuwa masomoni, najua nikipindi kigumu haswa ulivyokumbuka
vituko vyangu tulivyovifanya na wewe, huzuni, simanzi zilikujaa moyoni
ndipo ulipochukua simu yako
nakuniandikia "Mis u my Tursky" nili enjoy sana nilipoiona sms yako
hakika nimekuja kwa ajili yako.'''lakini nashukuru Mungu kwa kuwa hata chuo
nilichopagiwa Mimi na wewe u hicho chuo zaidi tukutane " KIBITI NURSING
SCHOOL "
Jestiner, alimwachia ''Jescar'' katika
kumbatio hilo, Jescar""Alimbinya mashavu Jestiner, nakusema'' Usijali
my Tursky'',nipo pamoja na wewe hakika hakutaharibika kitu, turudi kama zamani,
hakika nilikumisi saaana"' Basi
tufurahi. “Daaaaah! Mbona waduwaa hivo utazani ndo Mara ya kwanza kuona vitu
kama hivi? " Jescar aliuliza “Noooo. nimefurahi tu, nahisi kupendeza
kabla!!!" Acha basi, na unavyojua kujishetua Leo lazima wang'akee, na hii motion
pagawisha, macho yanguuu Jescar na
Jestiner kwa pamoja walicheka kama
ishara ya kufurahia jambo Hahahahaaahaa!!!!!!!!!!
Jestiner, alijaribishia nguo ile rahaulaa!! Macho yangu,
nguo ile ilimpendeza haswa, pamoja na nywele zake zilizodesigniwa kimtindo, na
makeup iliokaa kimaridadi usoni kwake ilizidi kuipamba sura yake na kuonesha urembo
wake hasua uliokuwa umekithiri kwa watazamaji, hakika mwenyezi Mungu alimtunuku
kirangi hivi, akampa na urefu pamoja na kijishep, macho yake madogo maregevu, hakika
akikutizama tu lazima utoe chechee, japo chechee za mpishi haziwezi zima
moto""midomo yake yenye rips nene ikipambwa na meno meupe hasua
akitabasamu ndo uzuri wake ulizidi kuonekana zaidi na kupamba uso wake. Hakika Jestiner alikuwa ni binti, mrembo,
kati ya kiumbe na yeye alikuwa ni "kiumbwa" na si "kiumbwaubwa"
Muda ulizidi kwenda Jestiner na Jescar waliingia
kwenye gari, tayali kuelekea kwenye tukio, hakika wote walikuwa bombaa na kama
ni chakula basi wangekuwa keki, walipambwa, wakapambika wenye mioyo ya Agape
lazima sifa kuwasifia wenye roho za kwanini nasisi
tungejiongeza tu.
Walikaribisha, kwenye viti vyao maalumu vilivyoandaliwa maalumu kwao,
taratibu Jestiner alimshika mkono Jescar tayali kuelekea kuketi kwenye viti.
""MC aliwakatisha kwa kusema, " wageni
wetu rasmi kabla hawajakaa naomba watufungulie kwanza sherehe hii kwa mziki
mzuri" DJ weka ule wimbo wetu, moto tuuwashe, watu wanyooshe viungo
vyao"
""" Ilipigwa ngoma ya
diamond, maarufu kama moto. Jestiner, Jescar nao hawakuwa haba waliuwasha kweli
moto, huku kelele, vifijo mbalimbali vikisikika eneo hilo. Kila mtu akicheza
design yake alioijua ilimradi kuchangamsha viungo vyake. DJ, alikata mziki na
kuruhusu kila mtu akakae katika sehemu yake
husika ili kuendelea na ratiba nyingine maana muda ulikuwa unayoyoma.
"Upande wa pili kwa nje
kulioneka na gari ya kifahari yenye rangi nyeusi'' liliokuwa linaingia mahali pale, likipaki kwa
pembeni katika parking ya ukumbi ule alionekana kijana mmoja, akishuka mkono wa
kushoto, alishikilia mkufu wa dhahabu uliokuwa shingoni kwa mbwa''', mbwa yule alikuwa mweusi mwenye Doa jeupe
kwenye paji la uso wake, alionekana ni mbwa alieshiba mwenye asili ya kizungu,
na mkono wa kulia Kijana yule alishikilia box lilokuwa na rangi ya dhahabu.
''''''Moja kwa moja alizidi kusogea katika sehemu ya
tukio kwa wageni rasmi, Jestiner alikuwa bussy akiongea na mhudumu wa mahali
pale akimpa ratiba ile anageuza macho tu yaani nyuso zao zilikutana uso kwa uso na kijana
yule, alipigwa butwaaa, akataharuki!!!!!,
hapo hapo UA alilokuwa kashikilia mkononi lilianguka chini na kuachana
vipande vipande, ile anainama kuokota Ua
lile mara ghafla sauti ilisikika upande wa pili ikisemaaaaaa,,,,,,,,,,,,,,,,,
Itaendelea...........
'''''..Usikose sehemu ya pili, kwanini Jestiner
kaduwaa!!!!?? Vipi kuhusu ujio wa kijana huyoo?
Comment
Like
Share
Ili niweze kukupa utamu Zaidi
kwa kipi kiliendelea kwa mastori tu na hadithi mbalimbali tembelea ukurasa wetu
kama ilivyo katika picha hapo juu.
Thanks Joseph lugembe umenipa saport kubwa sana kwa kazi yangu mungu akubariki
JibuFutaThanks too endelea kushare link kwa magroup mengi waweze kuijua kazi yako
FutaPowa
JibuFutaThanks for your comment
Futa