Mwanahabari na mhariri wa Kituo cha redio cha Mjini Fm Joseph Lugembe leo hii tarehe 21 Agosti katika kipindi cha round about ametusanua machache kuhusu historia ya maisha yake ilivyokuwa na kuwataka vijana wanaojitafuta wasikate tamaa kwani kukata tamaa ni chanzo cha kupoteza malengo ya ndoto zao
Binafsi nimeingia Arusha 2023 mwezi wa nane na bahati mbaya zaidi nilikaa mwezi wote wa nane Mt. Meru Hospital nikiwa namuuguza kaka yangu, na hii ndio ilikua sababu kuu ya mimi kutoka Dar kwenda A Town, dada angu sikufichi watu wa Arusha ni wakarimu sana usisikie story za huku mjini. Mimi baada ya kutoka hospital tulirudi home tukawa tunaishi pale kwa bro na hadi Disemba nikamuomba kaka niende nikapange chumba changu na mimi kwa kuwa amesha- recover bro hakusita aliniruhusu nikaenda japo nilipanga chumba ni maeneo jirani na kwake na huu pia ndio ulikuwa mwanzo wa kufahamiana mimi na familia moja hapo mtaani. iko hivi nilizoea kwa bro maji shem anachota tunatumia wote but after mimi kwenda kupanga nikaanza hustle kutafuta maji yanapatikana wapi akili ikanituma nikaombe kwa majirani na jirani wa kwanza kumfuata alikuwa ni Mrs Urassa na nilimwendea tu sijui ilikuaje ila nikajikuta nafuata nikamwambia mama naomba nichote maji akanikubalia nikachota hiyo ni siku yakwanza na ikawa n muendelezo nikajikuta nimekuwa na ukaribu naye kiasi kwamba naenda nagonga geti wanafungua nachota maji natoka lakini sasa cha ajabu ule ukaribu ukazidi ikafika hatua nikawa namsaidia kazi nyumbani ko ikawa ni familia wakati huo mume wake sijawahi kukutana nae hata kidogo na simjui. Siku moja natoka hapo kwake ile nafika getini nikasikia mlio wa honi na binti wa kazi akaja kufungua nilimsalimia akaitikia sikufuatilia sana kumbe ndie baba wa familia hiyo mzee. Nilikaa muda sana ikafika wakati siku sijaingia harakati zangu nachill pale kwake siku moja nakumbuka nilikuwa nimekaa tu nipo mimi na yule mama (Mrs Urassa) akaja mzee mwenyewe akatukuta ndio rasmi nikatambulishwa ila hakua mgeni machoni pangu. Tukaendelea kukaa vile tukawa tumezoenana ila mzee nilikuwa namuogopa kinoma kuliko mke wake hata ikitokea nataka kwenda kanisani nilikua namsubiri mke wake ndio napanda gari yake ila sio mzee cha ajabu sasa tumeendelea kukaa vile ikafika muda mzee akaanza kunyanyua mjengo na mimi nilikua saidia fundi oya eeeh kote uko nimepita. Saa ngapi Urassa asimpange Engineer kwamba mimi na msela wangu ambaye kwa sasa yupo Tanga tusikose kazi. Mie ile nafika tu jioni mzee ananiambia muombe kazi Engineer kesho uchimbe msingi. Haaaaah nilishtuka kwamba leo mzee kanisemesha na mie msingi nilikua naogopa sana hadi kesho katika ujenzi nimekimbia sana issue za kuchimba msingi ila kwakua ni mzee kasema nikasema acha nikajaribu nilichimba nakumbuka ilikuwa ni mita 5 zikanitosha ili tu niendelee na kazi siku inayofuata. Na kweli Engineer aliendelea kutuweka kila siku tukapiga kazi hatimaye mjengo ukasimama jamaa yangu alitoka mapema akapata mchongo Tanga kwa hivyo nikabaki mimi na Mr. Urassa kupitia kwa mke wake aliniamini akanibadili kutoka saidia fundi nikawa msimamizi wa ujenzi wakati yeye hayupo hadi nyumba imekamilika niliendelea kusimamia kumanage issue za wapangaji na kila kitu pale licha ya kuwa ghorofa imekamilika. Mimi kwangu nilichojifunza katika utafutaji au unapoenda sehemu yoyote jitahidi kulinda heshima yako, heshimu kila mtu, alafu onesha bidii zaidi. Urassa haikuwahi kutokea mimi na yeye tukadharauliana nae hata kidogo nafikiri nikipata nafasi siku nyingine nitawapa namba yake, mimi na yeye ilifikia hatua tukawa tunacheka pamoja tunataniana ila tofauti ya mimi na yeye ilikua moja tu. Niko tayari kumsikiliza kwa vyote atakavyoongea ila sio ushauri wake katika masuala ya kimpira tu! Hilo hata yeye anajua. Kwangu mimi Urassa na familia yake walikuwa wanafahamu zaidi maisha yangu kuliko hata kaka yangu. Nilikuwa ninamheshimu na kumchukulia kama sasa huyu ndiye Mzee Lugembe wangu kwa huku ninapoishi maana nilichokipenda alikuwa mkali akiona kuna kitu sifanyi vizuri hakuacha kukemea hata kama nitawahi kwenda kulala, akigundua atanipigia simu muda wowote ule. Yeye kwangu amekuwa ni daraja la mafanikio kwa kipindi chote nikiwa Arusha. Yeye na mke wake wamenifanya nibaki hivi nilivyo sasa kupitia ushauri wao. Arusha mimi ni nyumbani, nikipata muda nitaenda. Bado ninawasiliana nae hata juzi nilikuwa na mpango wa kurudi maana main target kwangu kuja Dar ilikua nakuja kuchukua vyeti vyangu kisha nirudi Arusha.
Mhariri huyo ambaye pia na yeye ni mmiliki wa Blog amewaasa vijana kutumia muda mwingi kufanya mambo ambayo yataacha alama kwa jamii na yatakuwa yakikumbukwa hata pindi wanapokuwa wametoka eneo hilo.
Kwa emoji moja tumkaribishe kijana huyu katika studio zetu

