Safari ya Ndoto (Muendelezo)

Tinner 1: SIMULIZI: SAFARI YA NDOTO.                                             MTUNZI: TINNER ROBER.                        SEHEMU: '29' . 0746638941 Whtsup.


ANZA NAYO.


Aliamua kurudi sehemu alipomuacha Degner! Alimkuta kaegama ukutani Huku akizidi kutetemeka! Alimtizama vizuri baada ya kuona chini kumelowa, Aliishia kucheka tu Huku akimkumbatia kumtoa hofu.

   "" Umeamua ukojoe kabisa kwa hofu!? Pole lakini ila tupo sehemu mbaya naomba tukimbie! Nilichokiona sijakielewa huko nje ni kipi chaendelea!?"

ENDELEA...


Degner alimwachia Soyona Huku akitazama Upande wa pili, Kuna kitu alikumbuka ilibidi amuulize Soyona.

   "" Mti wa mkuyu uko wapi kwa hapa!?"


Soyona aligeukia Upande wa pili ndipo akakumbuka ni mti mkubwa ambao upo karibu na mlima mara nyingi Sana wakiwa vitani hupenda kuutumia kwa kupumnzikia.

   "" Wamaanisha Ndio wenzetu wapo huko!?"


   "" Ndio! Make walinipa maelekezo baada ya Mimi kukutoa hapo! Nikuulize huo mti ndo wao wataelekea huko!?


  "" Aaah! Mbona hii baraaa!! Ngwasamo pia anaujua huo mti au wao wamejipangaje!? Basi twende japo ni usiku jamanii!"


Walianza safari ya kuelekea kwenye mti wa mkuyu! Hatimae walifika make haikuwa mbali na hapo kwa mbali waliona mwanga wa Moto ukiwaka ilibidi waende kwa tahadhari! Sauti ya Alfred ilisikika kana kwamba wanajadili kitu wafanye! Ila Kuna mtu katika wale Askari aliuliza;

   ""Mbona Brighton haonekani! Mwangalieni huenda katoroka kumtafuta mkewe! Make naona akili yake haikuwa hapa!"


Maneno Yale yalisikika maskioni kwa Soyona! Kwanamna moja au nyingine Maneno yalimuingia Soyona alijua ni kiasi gani Brighton anavyompenda mpaka anashidwa kujumuika na wenzake alibaki akitabasamu tu, Degner nae aliona hilo alikuwa akimtizama chinichini Soyona nakubaki akijisemea.

   "" Hawa wameshaanza kuzoeana kumbe! Mwanzoni nilijua Soyona hamkubali Ka Brighton kivile! Mbona katabasamu!?"


Wakati Degner akizidi kuwazua kwa mbele kidogo aliona Kama mti unatikisika kwa hofu aliyokuwa nayo alikimbilia mgongoni kwa Soyona akawa amejificha.

  "" Degner Nini tenaa!?"


  "" Mti huo unacheza!!? Angalia mbele yako!?"


   "" Sasa mbona kunae mtu kaegama!? Au ni yule Binti katufuata!?"


Soyona alichukua upanga wake taratibu Huku akimnyemelea alinyanyua upanga ili amkate lakini tayari alishitukiwa mapema alishangaa upanga wake ukitua kwenye mti, ile Anakuja kutizama vizuri anamuona Brighton akiuangalia ule upanga jinsi ulivyotua, Brighton muda huo hakuwa na uharaka wa kumtizama aliyemkosa upanga make aliutambua ule upanga, alibaki akiongea mwenyewe.

   "" Hatimae nimekupata tenaa!? Nilijua utakuwa bado upo mikononi kwa Ngwasamo! Ila nilijua utarudia hii hii njia make hata siku ile ulipitia hapa hapa!! Hakika yule Binti Hodari niliyemngoja kwa muda Ndie yeye ameangukia mikononi mwangu.


Soyona alikuwa bado akimtizama Brighton Huku akijilaumu, vipi Kama angeondoa shingo ya mtu asiye na hatia kwakee ingekuwaje?' mbaya zaidi ni mtu ampendae, Alisogea taratibu Hadi kwa Brighton alifanya kumkumbatia Huku akizidi kumuomba msamaha.


Muda huo team nzima ya Alfred ilikuwa imefika baada ya kusikia sauti ya Upanga. Huku Prince Lee pamoja na walinzi wake walikuwa bado wametia team! Kwa prince Lee macho yake muda wote yalikuwa kwa Soyona yakimtizama kwa uchunguzi zaidi Huku akitafakari.

   "" Kwahiyo huyu ndie Binti Soyona toka Tokyo! Japo sijamuona vizuri sura yake lakini ngoja kupambazuke asubuhi nitamtia vizuri machoni kwangu!"


Soyona alimuachia Brighton toka kwenye kumbatio Huku akimtafuta Alfred, alipiga jicho nakumkuta kasimama na Pacie Huku kamshikilia mkono, Harafu Upande wa pili alikuwa ni Prince Lee kamshikilia mkono na yeye vilevile, alitazama ile mikono jinsi walivyomshikilia aliamua na yeye kumshika mkono Degner pamoja na Brighton Huku wakielekea sehemu kulipokuwa kumekokwa Moto.


++++++++++


Ni asubuhi kulipambazuka Kila mtu aliamka na harakati zake! Mabinti waliokuwa kwenye kundi Hilo walikuwa ni watatu tu Ani , Soyona, Pacie, na Degner! Waliungana pamoja wakaelekea Mtoni angalau kukosha miili Yao.


Huku kwa Upande wa Wanaume wao walikuwa ni wengi kidogo Upande wa prince Lee alikuwa na walinzi wake wawili yeye wa tatu, walinzi wa Pacie walikuwa Saba, Huku Askari wa Soyona na Alfred walikuwa kumi na wawili! Na wengine walijigawa kuelekea kwenye himaya ya Baba ake kwa ulinzi zaidi.


Muda si mrefu Soyona, Pacie na Degner wariludi kwa wenzao! Waliwakuta wakipata chakula Huku wakisukumizia na maji, na wao walijumuika kwa pamoja wakaendelea kula. 


Alfred alikuwa akimtizama Sana Soyona make muda wote alikuwa akicheka chinichini ilibidi amhoji.

   "" Wewe Soyona una Nini lakini!? Sisi tupo kwenye hatari harafu Wewe unacheka!?"


   "" Hahahaaa! Hata ni wewe mtu apite ana nguo nyeusi! Hafu uachwe pekee ndicho kilichomkuta Degner Ani alikojoa vibaya!"


Wote waliangua kicheko Huku Degner alibakia na aibu alimsogelea Soyona akawa amemsina Huku akimkunjia uso kwanini anamsema mbele ya watu!


Prince Lee alibaki Akimtizama Soyona na jino lake la pembeni lilikuwa limebebana lilimvutia Sana alibaki akicheka Huku akipiga makofi. Alfred alikuwa akimtizama chinichini hata kwa Pacie na yeye alimuona alimsogelea na kumnong'oneza sikioni.

   "" Safari yako ya kuja Huku ilikuwa ni kwaajili ya Soyona naona vile umedataa anii! Hafu nasikia umeoa karibuni tu na mkeo si anae ujauzito!?"


Alfred alikuwa akiangalia ukaribu wa Pacie pamoja na Prince Lee! Aliwaza Mambo mengi Sana kuhusu kuzoeana kwao na wanafahamiana vipi lakini hakuwa na majibu aliamua kukatisha sitori.

   "" Naona sitori zinazidi kuendelea hamjui kuwa tupo vitani! Kila mtu ajue thamani ya maisha yake na ya mwenzake Kama tutavamiwa hapa kwa uharaka itakuwaje!?"


"" Bora hata umeongea kiongozi! Mimi nimeacha familia yangu Nyumbani inaningoja! Na wanayo matumaini makubwa ya Mimi kurudi nikiwa mzima! Hapa tumewapoteza Askari wetu kadhaa! Hatutaki itokee tenaa!?"


Askari mmoja katika kile kikosi aliongea. Ilibidi wote warudishe akili yao vitani wakaanza kupanga mbinu za kivita tenaa! Walipanga kuvamia kikosi Cha Ngwasamo ikiwa ni pamoja na kumpata Ngwasamo.


Wakati mjadala unaendelea Kuna mjumbe mmoja toka Tokyo alitumwa kufikisha ujumbe, aliwapatia karatasi kisha aliondoka.


Alfred Pamoja na Soyona walichukua karatasi Kisha waliisoma kwa pamoja kimya kimya, baada ya kumaliza kuisoma Soyona alibaki akimtizama Alfred kipi atazungumza!


Alfred aliishia kumtizama pia Kisha alinyanyua mkono wake mmoja Huku akimpigapiga mgongoni aliachia maneno ya kishujaa.

   "" Nipo tayari kupambana na Ngwasamo uso kwa uso!"


   "" Kipi kinaendelea mbona hamusemi!? Pacie Alihoji.


   "" Barua inasema kiongozi toka Sakhalin tayari amechukua Wanajeshi wake kuelekea Mji wa Tokyo kwenda kuvamia! Pia Ngwasamo kaomba pambano na Alfred uso kwa uso atakayeshidwa atanyanganywa taifa lake! Na plan ya Ngwasamo ni kumshinda Alfred ili achukue taifa la Tokyo! Na mwisho kabisa anawaomba Pacie na Brighton wakaungane na taifa lao laaah hivyo atamuua Babake Soyona!


Upande wa Pacie pamoja na Brighton baada ya kusikia hivyo walishuka chini kwa pamoja Huku wakiwa wamelegea. Soyona alikuja kuinua uso baada ya kumaliza kusoma alimuona Brighton kapiga magoti chini ilibidi amwendee;

   "" Usiwe na hofu kiasi hicho! Kwakuwa wewe u Upande wangu na Mimi ni Upande wako naimani upo sawa ila Mimi bado nakuamini Sana hujawahi kunikosea siku zote umwema katika Upande wangu!"


Soyona alimaliza kusovu Upande wake tatizo likabakia kwa Alfred kumuaminisha Pacie yupo sehemu salama! Alfred Alimtizama Pacie Huku akitaka kumwendea lakini alikuwa amechelewa tayari Prince Lee alikuwa yupo na Pacie wakibembelezana.


   .... Itaendeleaa.........


Usikose sehemu ya 30.


Tinner 1: SIMULIZI: SAFARI YA NDOTO.                                             MTUNZI: TINNER ROBER.                        SEHEMU: '28' . 0746638941 Whtsup.


ANZA NAYO.


Pacie Alinyosha mkono juu baada ya kuona wanajeshi wake wanataka kuingilia Kati.

  "" Hapana!! Achaa tuonee kwanza Yupi atazidiwa! Ndio tutoe msaada! Jeshi letu litaingia Kati kumpambania huyo Kijana aliyewekwa Kati ila kwasasa acha tuonee juhudi zake kwanza!!"

ENDELEA.....


   "" Kiongozi! Soyona yupo chini! Huenda kaumia Sana! Degner aliongea.


  "" Basi tuingie kati! Hakikisha Degner pamoja na wenzako mnaungana kumkomboa Soyona!"


Kizaazaa kilianza upya Pacie Aliingia Kati akaruka Hadi kwa Prince Lee Huku akizidi kuonesha upanga wake, Prince Lee Alimtizama Pacie akawa amempata.

   "" Princess toka Sakhalin na wewe uko hapa!? Inaonekana kwasasa umeimalika katika upanga! Ni muda mrefu sijakuona ila umezidi kuwa mrembo! Nasikia kakako ndie anamumiliki Binti Soyona!"


Pacie alibaki akimtizama Prince Lee! Make alimjua toka siku nyingi huwa anapenda kuchimba chimba Mambo, Aliishia kucheka tu Huku akiongea.

  "" Kwasasa tupo vitani kwanza! Hafu hujaacha utani wako hata Wewe unavutia kwasasa!!?"


Prince Lee ilibidi acheke na yeye, Huku akiendelea kuwasha upanga Wake!

   "" Hakikisha unakuwa makini Pacie! Nisije nikampoteza rafiki yangu wa utotoni!"


Wakati Mazungumzo yakiendelea Soyona alikuwa tayari kachukuliwa na Degner muda huo Ndio fahamu zake zilikuwa zikimrejea taratibu, anakuja kufungua macho anamuona Degner kakae pembeni yake, alivuta taswira jinsi tukio lilivokuwa Ndio akakumbuka Kuna Kijana alikuwa nae alisimama ili aondoke akamuone lakini Degner alimshika mkono nakumrudisha.

   "" Vipi lakini Umzima! Make niliogopa Sana!?"


Soyona alibaki akimtizama Degner, alimuona kavalia mavazi ya kivita alimtazama  pembeni katika mavazi yake alichomeka upanga! Alimsogelea na kuuchomaa upanga Kisha alibaki ameushikilia mkononi akiutazama, Aliushusha chini Huku akinyanyua mkono wake wakuume akamshika shavu Huku akiachia tabasamu lililojaa maneno kadhaa.

  "" Madaam! Niko mzima Kila kitu kinaenda kuwa sawa! Nimeona Alfred kaingia kwenye ghala la kuhifadhia Ngano naimani usalama upo wa kutosha ngoja nikasawazishe kwanza kitu kilichobakia!"


Soyona Alitoka Nje alitazama mazingira ya pale yalivyokuwa yakifuka Moshi, baadhi ya nafaka zilichomwa moto! Hii ilimuumiza kiaina lakini alijipongeza kwa kazi aliyoifanya. Soyona aliwahi kufika pale alichofanya alichukua Chakula na kuhamishia sehemu nyingine pamoja na Wanajeshi wake baadhi harafu yeye akabakia pale ili kuendelea kuwazuga hata walipokuja walianza kudili na Wanajeshi baadhi Huku wakifanya kuharibu mazingira kwa kuchoma kambi yote! 


Wanajeshi wengine walijigawa wakarudi Tokyo ili kuweka ulinzi wa kutosha! Upande wa Ngwasamo alijua moja kwa moja nguvu yake yote aliweka kwenye kambi ya chakula! Alijua akiwamaliza kuwathibiti kwenye chakula ataweza kupindua utawala wa Tokyo kiulaini!


Soyona Baada ya kumaliza kutafakari Aliingia Hadi kwenye uwanja wa Vita alikuta Kuna miili mingi imelala chini alianza kukagua ndipo anakugundua tayari wamepoteza maisha! Alisimama aondoke lakini alishituka Kuna mtu alikuwa akiugumia maumivu ilibidi amfuate, Alimtizama vizuri ndipo anagundua ni Mwanajeshi wake wa muda mrefu hata siku ile kwenye msafara wake katika nchi ya Harbin alikuwepo, alichuchumaa chini Huku akimwaga machozi mbele yake.


Alinyanyua mkono wake ili ampatie make alikuwa amemnyoshea mkono, alimsikiliza;

  "" Soyona nisamehe Mimi! Pia msamehe na Ngwasamo sijui hata kaingiwa na Nini mpaka kafanya hivi! Nlijaribu kukataa kuwa Upande wake lakini alinitisha vikali hata kuahidi ataizuru familia yangu! Nlipoingia vitani niliwaza kuwa Upande wenu lakini nilichelewa make watu wa Upande wako walinichukulia ni bado mharifu hata mavazi yangu ni ya Upande wa Ngwasamo! Hivyo ilikuwa ni ngumu kutambulikaa!"


Alimalizia kuongea kwa kusuwasua! Soyona Alimtizama vizuri ndipo anagundua kajeruhiwa vibaya make damu zilikuwa zikimtoka ubavuni, alimpindua vizuri ili atizame jeraha lake alichokutana nacho ni damu nzito iliokuwa imeanza kugandamia kwenye nguo! Damu ile ilimshitua nakubaki akipiga kelele.

   "" Hapana lazima uishi! Ni mtumishi wangu ninayekutegemea Sana! Bado nakuhitaji!"


Soyona alijitahidi kumbemba lakini hakuwa na nguvu za kumbemba! Mwisho kabisa alisikia sauti ikimsisitiza japo kwa shida.

  "" Soyona jitahidi Sana uishi! Najua taifa hili bado linakutegemea wewe na Alfred! Hakikisha unapambana kufikia Safari ya Ndoto yako pamoja na Alfred! Harafu Ngwasamo amerudisha vikosi nyuma baada ya kuthibitiwa na Askari wako! Muda wowote atarudi harafu Kaangalie Usalama wa Nyumbani kwanza!" 


Alimaliza kuongea Kisha alikata roho miguuni kwa Soyona! Soyona alipata pigo jingine alinyanyuka pale Kama kachanganyikiwa, alianza kutembea mdogo mdogo akielelekea sehemu ya kuhifadhia Chakula. Muda huo Degner alikuwa akimtizama mpaka machozi yanamtoka! Alianza kumfuata taratibu Huku akijaribu kuruka ile miili ya Marehemu kutokana na uoga alionao kwa bahati mbaya alikanyaga mkono wa mtu kelele aliyopiga mpaka ikamfanya  Soyona na yeye akili yake irudi pale walibaki wakipiga kelele wote kwa pamoja.


Degner alikimbia kumkumbatia Soyona kwa uoga Huku akizidi kulia.

  "" Kweli naogopa Sana kuona miili ya Marehemu! Naogopa Dadaaa!!"


Soyona na yeye aliogopa vilevile hasa tukio la kumpoteza Askari mwenzake mbele ya macho yake hili lilimuumiza Sana Kila akifikilia ile damu ilivyokuwa ikimtoka Ndio huzuni na woga vilimkumba. Alibaki amemkumbatia pia Huku akisema;

   "" Naogopa Damu niliyoiona kwa Askari wangu! Ila siogopi hi miili ya Marehemu make katika Vita nimekumbana nao wengi!"


Alimuachia na kumfuta machozi Huku akimuomba amfuate.

  """ Kama waogopa basii funga macho yako! Utembee na Mimi kwa hisia! Ila ukifungua macho yako ukakuta Kuna damu Basi niambie na Mimi nifunge macho yangu! Kweli naogopa Damu!"


Wakati wakizidi kutembea tembea Huku wakiwatafuta wenzao! Ghafura Kuna mtu alipita mbele yao Huku akiwa amevaliwa mawazi ya kininja, walisituka kwa pamoja kutokana na hofu waliyokuwa nayo Kila mtu alishikilia tumbo lake Huku alibaki kaganda vile vile akimtizama mwenzake!

  "" Kweli usiku unatishaa! Mbona Kama sielewi! Muda wote natamani nifunge macho yangu nisione kipi kinachoendelea katika usiku!


Soyona aliongea kwa majonzi kweli.


   "" Hivi hakuna hata mtu anaejali kuhusu sisi tenaa!? Si Kaka Alfred, Brighton, pamoja na Dadangu Pacie naye kanitenga jamanii!?"


Soyona alibaki akimtizama Degner make alijua ni wakati gani anapitia na jinsi anavyojisikia. Alichomoa upanga wake awe attention kwa Kila kitu kitakachotokea angalau kilichobakia ni kulinda uhai wake tu.


   "" Huyo ni Nani kwanii!? Je, ni watu wa Ngwasamo au ni watu wetu!?"


Soyona Alimtizama Kisha alimuwekea kidole mdomoni, atulie kwanza ili ajue kipi kinaendelea.

  "" Nakuomba kaa hapa! Nakuja muda si mrefu!


   "" Aaa! Aa!! Mwenyewe!?" Hapana siwezi!"


Soyona Alimtizama Kisha alimkata jicho lilomfanya Abaki kimya.


Alimuacha pale Huku akimfukuzia yule mtu aliepita mbele yao muda ule, alifika Hadi kwenye kolido lilokuwa lipo karibu Aligundua moja kwa pamoja atakuwa pale alinyanyua upanga wake Huku akijiweka sawa! 


Yule mtu alikuwa akimpigia Target Soyona! Ile anachungulia hivi walikuta wakitazamana uso kwa uso ilibidi wavamiane uso kwa uso, Soyona alifanikiwa kumfungua kitambaa Ndio akaona uso wake, alikuwa ni Binti mmoja uso wake ulionekana kuwa bomba kabisa.


Soyona alibaki akimtizama Huku kaduwaa make alikuwa hamuelewi elewi kabisa! Na ilikuwa sura ngeni kwakee. Wakati akizidi kumtizama kwa mshangao! Binti yule alipata upenyo akamkimbia, Soyona alianza kumfukuzia lakini alimkosa.


Aliamua kurudi sehemu alipomuacha Degner! Alimkuta kaegama ukutani Huku akizidi kutetemeka! Alimtizama vizuri baada ya kuona chini kumelowa, Aliishia kucheka tu Huku akimkumbatia kumtoa hofu.

   "" Umeamua ukojoe kabisa kwa hofu!? Pole lakini ila tupo sehemu mbaya naomba tukimbie! Nilichokiona sijakielewa huko nje ni kipi chaendelea!?"


   .... Itaendeleaa.....


Usikose sehemu ya 29.

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi