Mfahamu mtunzi wa Simulizi za kusisimua na mwanamitindo maarufu Jiji la Mwanza

 

Tinner Robber

MWANDISHI; TINNER ROBER.                 SIMULIZI; UPENDO USIOTARAJIA.         SEHEMU; 01

    UTANGULIZI.

     Majina yangu naitwa Tinner "22", ni mtoto pekee kwa wazazi wangu, mzaliwa wa mwanza, Wazazi wangu wanajishughulisha  na biashara, Baba yangu ni muuza dagaa maarufu huwa anachukua dagaa, ziwani anasambaza mikoani, mama yangu ni fundi cherehani pia Ana duka la vitambaa makoroboi, anauza jumla na rejareja, Wazazi wangu wamenipa kipaumbele Sana katika masomo yangu mara tu Baada ya kumaliza kidato Cha nne, wazazi wangu walipenda Sana nikajiunge na chuo Cha uuguzi kibiti Nursing school, kilichopo Lindi. Chuo hiki walikipa kipaumbele  Sana kutokana na baba yangu mdogo ni daktari bigwa wa maswala ya "Physiology" na hii imempa umaarufu Sana kwa hapa Bugando. Na matumaini yao yalikuwa ni makubwa sana kwangu hata kama ajira zingekosekana walikuwa radhi kunipa mtaji nikajiajiri mwenyewe, Baba aliependa Sana muda wote kuniambia " Mwanangu elimu ni hadhina kubwa kama wazazi wako wakikupa  hadhina hii ihifadhi ili badae uje kuitumia mbeleni na hii itakupa ufunguo wa maisha yako.


   Nakumbuka ilikuwa ni siku moja ni siku iliyovutia machoni kwangu, kumbumbuku za furaha, na huzuni Kila ninapovuta taswira haikosi jirudia Tena, ni siku ambayo ilikuwa ni kumbukumbu yangu ya kuzaliwa ilikuwa ni tarehe 23,12 ni siku watu walikuwa wameanza maandalizi ya X-mas na mikesha hasa katika makanisa mbalimbali ya  kikristo yalikuwa yamepamba Moto, Nyumbani kulijaaa na shamra shamra za Kila aina , Mimi nlikuwa ndani na rafiki yangu Jescar, tunapiga story za hapa na pale huku tukiandaa mavazi yetu. Jescar, alikuwa ni rafiki yangu wa karibu Sana aliweza kunisapot siku ya birthday yangu kuwa kama partiner siku hiyo, na urafiki wetu ulikuwa ni urafiki wenye furaha siku zote ulijaa amani, na upendo na siku zote ulizidi kuchanua.


    "" Mara Baada ya maandalizi yetu kumaliza, tulielekea sehemu ya tukio, Kila mtu aliekuwa mahali pale kiukweli aliweza kupendeza na sherehe ilipamba Moto, muda ulizidi kwenda ilikuwa ni muda wa zawadi mbalimbali Kila mgeni alileta zawadi yake, 


"""mama aliniletea zawadi ambayo sikutegemea kabisa, walikuja na baba wameshikilia kibox Cha Kati baba,


"" akasema "" Mwanangu,, Mimi na mama yako  tunakuachia muongozo wa Vitabu hivi vikawe mwongozo wa maisha yako itabidi ufungue hapa mbele za haraiki hii Kila mtu aone zawadi hii.


  ""Taratibu nilifungua box lile nilikuta Kuna vitabu viwili Cha Kwanza ni Anatomy( kinazungumzia Sana sehemu ya mwili wa binadamu kwa ujumla), Cha pili ni Midwifery (ukunga)



  Mimi binafsi sikuamini kama wazazi wangu wangenipa zawadi hiyo, watu wote walishangaa kwa mtu ambae hakuwa mwelewa aliona kama kitu Cha ajabu sana, kwa waelewa walishangilia.


 

   Muda kitogo kuna vijana wawili walivaa nguo nyeusi, waliingia huku wameshikilia zawadi zao ikiwa ni pamoja na keki, moja kwa moja Hadi sehemu nilipokaa, waliweka mezani Kisha kuchukua mshumaa, na kuwashaa, watu wote walikuwa wakiwatazama bila majibu yoyote, Baada ya kuvuta Moshi ule wa mshumaa nilianza kuhisi mwili wangu unakuwa mzito, nikaanza kuwasikia kwa mbali wakiongea; ""mama, baba tayari huko, sijui ni kumbukumbu zangu tu nilizipelekea huko, baadae nilimuona mama povu linatoka mdomoni, na baba alikuwa pembeni damu zikimtoka puani na mdomoni. Nilisituka ghafura na kusema ""


       ''Hivi naota!!!,, Tinner hebu gutuka rudisha akili hapa nataka kuchanganyikiwa'' hivi naota??? 


     "Jescar""" hivi na wewe ninavyoota Mimi na wewe unaona hivyohivyo, hebu niambie ni ya kweli haya lakini!!!?? 



    """Baada ya kufumbua macho, yangu nilimkuta 'Jescar kanikumbatia kwa nguvu huku hofu ikiwa imetanda  neno la mwisho alisema""


 " Tinner, tukimbie mama, Baba wote wameuwawa, tutoke hapa watu wote wamekimbia wamebaki wachache tu na wao ni wafu, tuondoke, halafuuu,,,,,,,


     ""Kabla hajamaliza kuongea nilimuona mtu mwenye nguo nyeusi alimpulizia Moshi machoni Jescar" na hapohapo alizirai Kisha alinivuta kwa nguvu na kunitupia kwenye gari kama mzigo na kuwashaa gari, kwa sipidi Kali muda huohuo Baada ya kunitupia kwa gari nilijigongeza kwenye paji la uso na kuzrai. 



 "" Ile nakuja kuzinduka tayari nlikuwa Airport, na ndege muda huo inaondoka, nikaanza kupiga kelele, nilikuja kuangalia watu wote wapo busy na mambo yao wengne wanasoma gazeti, pembeni yangu alikuwepo mzungu mmoja kakaa na mwanae na muda huo yupo busy wanacheza game kwenye laptop, 



  " Ikabidi nimsemeshe  "" how are you? Mzungu yule, aliniangalia tu akatabasamu Kisha akasema "" Fine"



  " Daaah!! Moyoni nikajisemea na kutabasamu kote anaishia, fine" tu kweli watu weupe wanadharau Sana, sasa nitamuanza vipi tena, nimwambie unajua nlikotoka, au ninapoenda , au abiria wote wanaelekea wapi?? make wanafuraha Sana utazani wanaenda kwenye sherehe, mbona nikikumbuka mara ya mwisho nilikuwa kwenye gari na watu wenye nguo nyeusi au ndo nipo kwenye surprise ya birthday.



    "Wazo liniijia nikawaza ngoja nimfinye mtoto au nmkanyange niseme bahati mbaya, ili akilia Baba atakuwa busy kumbembeleza mtoto, na akishanyamaza mtoto hatakuwa na mud Tena wakucheza game, atambembeleza mwishoe atalala akilala huyu mzungu atanisikiliza vizuri make atakosa kampani Tena lazma nitafanikisha tu hapa.


  "" Nilijisogeza karibu, na mtoto nikajifanya kama nasinzia, taratibu nilimkanyanga mguuni kwa kumkwarua kucha zangu za mguuni muda wote nilipendaa kufuga,



   Mtoto kweli alilia huku akisema Daddy!! Daddy!! Huku akininyoshea kidole akinielekezea Mimi.



 Mimi, ndo nkajistua daaaah sorry, sorry, excuse me, sorry please!!


Mzungu, aliniangalia tu,,nikaona tayari nimesha muungia kingeleza ndo maana kaniangalia, na kunishangaaa tu.


 Matokeo yake nilichofikilia ndio nilifell kabisa, alimnyamazisha mwanae Tena kwa kumdanganyia acheze game la kukimbizana, na ndo game likanoga wakawa watu wakucheka tu baadae wakapitiwa usingizi wote wakalala,


    """Tayari upande wangu nkabaki kushangaa tu abiria wenzangu muda wote wanachezea laptop nikaona ngoja nilale tu sioni hata mtu anayetaka kuwa karibu yangu.



    "" Nasinzia hivi, nashangaa, mdada wa kitanzania akaja na kukaa karibu yangu, vipi Madam unanjaa? Kwa haraka kweli nilimjibu Tena Sanaa kama ukileta sato, mkubwa mkavu, na ugali ntashukuru. 


  "" Dada yule, aliondoka, hakunijibu chochote , baadae aliniletea samaki mkavu, na ugali pamoja na juice ya embe Kisha aliondoka. Akili yangu ikanituma aaah kumbe nipo Tanzania tu itakuwa naenda Dar, mbona vyakula vya Nyumbani tu wameleta na nmeagiza makusudi tu wasingeleta ningejua sipo sehemu sahihi, 



  ****** Safari ilizidi kuendelea, taratibu usingizi ulinichukua, ile naamka tayari ndege imetua Airport, muda huo natoatoa macho, sielewe zaidi ni watu wamebadilika kabisa kimuonekano, mpka mavazi kuliko watu wa kitanzania wanavyovaa, walivaa mavazi kama ya kikorea, ni mavazi yenye heshima, Tena walikuwa wanaheshimiana kweli salamu zao walisalimiana kwa kusujudiana, 



  "" Muda kidogo alitupokea mama mmoja wa makamo hivi alitoa ishara tu tumfuate, muda huo nlikuwa nmevaa gauni langu la birthday, na pembeni nilikuwa na wale vijana waloniteka japo tyari walibadilisha mavazi yao na kuvaa mavazi ya kule, niliamini tu watakuwa ndio wenyewe wamebadili nguo,.



''' Tayari tulifika kwenye jumba moja lililokuwa limepambwa vitu vyenye thamani, vilivutia muda wote na sehemu hiyo ilionesha kutakuwa na tukio litafanyika punde.



   "" Alitokea mdada mmoja ,umri kama tunalingana, alikuja kwa heshima akiniinamia, kama salamu za hapo walivyokuwa wakifanya hata kwa wengine,, akisema ""ewe  princess mtukufu,;  Mtukufu wetu markia anakuita yupo kwenye jumba la ibaada, tafadhari fuatana na Mimi princess nikupeleke.



  Nilimfuata kwa unyonge, mpaka kwa markia, nikasimama, muda Huo nimeshikilia gauni langu lilikuwa refu, ishara ya kutaka balance ya kusimama kisha,  kumtolea macho. 


   "" Markia unaniita!!??, 

   "" Keti Kwanza tuongee""


   "" Taratibu niliketi, ""Markia nakusikiliza'' 


     "" Markia aliniangalia tu hakusema chochote, alichukua birika lililokuwa na kahawa na kunimiminia Kisha alinipatia akisemaa, "" Princess"" pole na uchovu, tumia hii itakupa nguvu. 



"" Nilinyanyua kikombe nikanywa ile nakunywa tu niliibunda mdomoni kusikilizia Radha yake, ilinishinda ikabidi niiteme, ile natema tu bahati mbaya nkamtemea Markia.


 

""Haraka walikuja warinzi wa Markia kumfuta na kumpa pole

."" pole Markia, naona hajazoea, hada mavazi yake yanasadifu hajawahi tumia. 


""Muda huo, Markia alikuwa kimya tu, akijifuta. 



"" Taratibu nilianza, kuogopa na kusema, "" mbona wanamcare hivo, hafu Mimi nimemtemea sijasema hata samahani??



""" Taratibu, Nilipiga magoti mbele ya Markia, nikamwinamia huku Naropoka kwa sauti na kusema ""'samahani Mtukufu Markia, kweli ilikuwa bahati mbaya, kiukweli nakubaliana na mlinzi wako Mimi sijawahi tumia vitu hivi hata mavazi yangu ni tofauti na yenu. 



"" Markia, aliniinua kwa mkono wake mmoja kunishikisha,  "" nimekuelewa princess, sawa keti. 



"" Akaamuru nitengenezewe chai, namimi nikasapot hapo sawa Markia, huwa natumia baba yangu alipenda Sana kunitengenezea chai.



"" Hapo, hapo fahamu zilinirejea na kuanza kulia, 



""Kwanini, mmenitenga mbali na wazazi wangu, mbaya zaidi naishi nchi, hata nisiojua ni nchi gani?, Mmeua wazazi wangu naomba mnirudishe Nyumbani kwetu, Tanzania, sizani kama hii, ni nchi yangu hatuna Mila kama hizi mbaya zaidi Rais wetu nmeacha kafariki, huku naona Bado mna utawala wa kifalme.



 """ Niliendelea kulia, bila matumaini yoyote, """ basi nawataka wale vijana waliokuwa wamevaa nguo nyeusi, wanipeleke wao ndio wanapajua Nyumbani, nipelekeniiiiii!!!



   """Ikawa ni patashika sehemu hiyo, Nilivunjavunja Kila kitu Cha udongo, na maua yote nilitupa kulee.



  """ Markia, aliamuru nipelekwe ndani, nioge na nibadilishiwe nguo nifanane kama wao.



   """" Ukweli niliandaliwa, chumba kizuri, kilichokuwa na mazingira mazuri, chumba, kilijaa nguo Kila aina Tena zilikuwa na matrio ya dhahabu, muda ule zilikuwa zikimetameta.



  """ Kijakazi, mmoja alikuwa karibu Sana na Mimi tokea nilipofika kwenye jumba lile alijitambulisha""  princess niite piniety, ntakuwa mwangalizi wako muda wowote, ukiwa na shida niambie, naahidi kuwa karibu na wewe muda wote ukikosa wewe niazibiwe Mimi, na hii ndio kazi yangu niliochagua. "" Basi ukimaliza kuoga niite, nikusaidie, kukuweka sawa upendeze mi nipo jikoni nakuandalia chakula. 



     "" Samahani Tena princess, niahidi basi, kama hautatoroka utabaki, na Mimi, usiniharibie kazi nakuomba tafadhari.




 ""Muda wote nlikuwa mbali kimawazo, baadae nasituka hivi, nikakuta nmekubali "" kweli ntakaa mikononi mwako siku zote.



   ""Piniety, "alinikumbatia kwa hisia Kali na kusema ahsante Sana princess, nimefurahi kusikia hivo Basi tufurahi kwa kinywaji.




***** ****** ****** ******* ********

Upande wa Markia, alionekana akizunguza, na mwanamama mmoja umri wake ulikuwa umeeda kukoma kuzaa, mazungumzo yao yalikuwa hivi""



  

   """Markia "" Mimi tayari nimeshaanza kuwa na wasiwasi na hii kazi tunayoifanya, hivi kwa mfano prince Nillylan, akitoka masomoni akifika akampenda princess itakuwaje , na mpango wetu, tunajua hawezi kumpenda kweli mTanzania, na option ya mwisho sisi lazma tumchague binti yako aolewe awe princess, na akishaolewa tayari ntapata fungu hapo.




""Wewe usijali,  Mtukufu Markia, kwa kuwa hujapata mtoto, na hauna uwezo wa kumzalia mfalme, naamini tukifanikiwa kwa hili, Markia wa Nillylan, kumuondosha ni vyepesi, isitoshe haoni, ni kipofu.



""Markia, akadakia kwa kusema, "" hakika nakukubali Sana, kama uliweza mwagia tindikali na hakuna aliyetuhisi, lazma tutafanikiwa hata na kwa hili.



"""Vipi, kuhusu na huyu prince Nicklan, mdogo wake prince Nillylan""


 

""'hahaaaaa!! Bado mdogo Sana, si itakuwa tayari, ufalme upo mikononi mwetu, yule ni kumbeba tu.



""" Basi, usiniangushe, ngoja nikaaongee na mfalme, tuweke sawa maandalizi, imebaki wiki moja tumpokee prince, tayari masomo kamaliza, harusi ifungwee tuvute shavuu. 



"""" Markia, na mshauri wake , waliagana kwa kicheko, kilichojaa, ushindi, wakiamini tayari ufalme upo mikononi mwao. 



***** ***** ****** *******

""" Kwa upande wa mfalme alikuwa, na wake wawili, mke wa Kwanza ni Markia Cheness, hakubahatika kuzaa, hivo mfalme ilibidi aoe mke wa pili ambae ni Markia wa Nillylan au Nicklan alibahatika kuwa na watoto wawili wakiume, Mfalme Ana matatizo ya moyo muda wote yeye anashinda kwenye ufalme, zaidi nchi yake inaongozwa zaidi na mawaziri, yaani serikali ya uongozi ndio inashikilia zaidi madaraka ya kuongoza, kwa upande Wa Markia Nillylan, alipata tatizo la kutokuona mara baada ya kumwagiwa Tindikali na mhusika mkuu, ndio tumeona ni Markia Cheness na mpango mzima ni mama mshauri wake nia na malengo nikupata madaraka kumuuangusha Mfalme, prince Nillylan aoe kwa mshauri wake, kwa kuwa hakupata mtoto, atakatiwa kiasi Cha hadhina katika ufalme, je itawezekana?? Mimi na wewe hatujui Basi songa nayooo Hadi mwisho.......




****** ******* ****** ********

Upande Wa prince Nillylan, alionekana, kakaa na rafiki yake Nellyson, sitori zao zilikuwa hivii




""Nillylan, sasa naona, tumefikia, tamati hapa, tumemaliza masomo yetu, tayari unarudi, kutumikia nchi yako, na tayari mwali kaandaliwa, siamini kama unaenda kumiriki princess hafu naskia princess, mwenyewe mTanzania, hahaaaaa!!, Hivi upo tayari kumuacha princess pinty wa kifalme Tena falme yao ina nguvu, Kwanza mnajuana tangu uanze chuo, na mnamaliza wote???




""Kiukweli Nellyson, sizani Mimi ntaenda kufanya ndoa fake, hafu narudi kumchukua princess Pinty'' siwezi kuoa, Mtanzania Mimi.



Baadae alionekana Pinty" anakuja alifika na kusimama nyuma ya Nillylan, na kuanza, kumtengenezea kora ya t-shirt ake, huku akiachia maneno kwa prince Nillylan nakusema """""



""Nillylan, kwahiyo unaondoka, kweli, na utatimiza ahadi yetu??, Nimeambiwa tayari umeletewa princess wa Kitanzania, na ndio mtegewa awe ubavu wako, je utapingana na falme yako kisa, Mimi?, Kama unajua kabisa ni ngumu, niambie mapema, nianze kukusahau, namimi tayari nimeshaandaliwa prince wa kunioa, nianze kumpenda taratibu japo haitafikia kama wewe ninavyokupenda, niambie please na Nellyson awe shahidi.



   """Prince Nillylan,,, alisimama, na kuinamisha kichwa chini, alimshika mkono Pinty, ishara ya kukubaliana, "" Ndiyo ntafanya hivyo usibadili maamuzi nitakufata katika falme yako na nipo tayari kuunganisha falme yangu na yako liwe taifa moja lenye nguvu moja.



""Naahidi itakuwa ni siku moja utakapoona, karibuni Anga siku hiyo jua litachomoza, halafu kutatanda giza, na hio siku ni ya kupatwa kwa mwezi, ndio itakuwa ni siku nitakayofunga Safari nakuja kwako princess Pinty!!



""Kwa furaha walikumbatiana wote ishara ya kufurahia ahadi yao, waliagana kwa furaha na hatimaye Kila mtu alierekea kwenye falme yake, Pinty na Nellyson walikuwa wanakaa falme moja, Nillylan yeye alikuwa peke yake kwenye falme katika chuo hicho.



********* ******** ********* ******

Siku hiyo ufalme ulikuwa, umechangamka tayari, kumpokea prince takribani miaka mitatu alikuwa masomoni, na huku mipango ya harusi ikiendelea, ratiba ilikuwa ni prince apumnzike siku moja kesho yake harusi na siku inayofuata tayari kutawanzwa, na kuwa mfalme na hii kutokana na mfalme alikuwa kazoofika na maradhi na nchi kupelekea kuendesha zaidi na serikali ya kifalme na kusababisha mambo mengne hasa biashara za jirani na ufalme na falme kwa falme kusitishwa kwa kukosekana kiongozi wa kusimamia biashara hizo.



"" Upande Wa Tinner" ilimlazimu kaandaliwa kuwa princess tayari alikuwa kashajikatia tamaa, na matumaini kabisa ya kurudi Nyumbani hayakuwepo tenaa.



""Siku ya harusi iliwadia ni siku ya huzuni kwa prince Nillylan, muda wote alikuwa kavaa vazi la harusi lakini akili yake ilikuwa muda wote ikimuwaza princess Pinty, pamoja na ahadi walizowekeana, alishikilia nembo aliopewa na Pinty! Mkononi na kunuia kwa kusema""


 """Siamini princess Pinty, kwani mpka muda huu naenda kuoa sijui una khari gani huko, Mimi ni mtoto tu nafata sheria za ufalme wetu kama ntaweza kunusurika nitakuja kwako, naiweka nembo hii kwa kuifukia chini sehemu ya chumba changu kwa sasa naenda kukaa siku zote katika falme na siku nikirudi hapa nkafukua nikapata nembo hii hakika nitaamini kuwa wewe ni wangu, na nisipoiona Basi haukuwa riziki yangu, nisamehe kwa maneno magumu niliyoyazungumza lakini naamini itakuwa hivyo.



"" Prince Nillylan baada ya kumaliza maagano Yale alierekea tayari kwenye jumba la kifalme kusubiri ndoa.



 """ Tayari, Princess alikuwa kashaandaliwa tayari, kupelekwa kwa prince alifungwa kitambaa machoni, asiweze mtambua prince mpka watakavyoamliwa amfunue na kwa prince ilikuwa vivyohivyo.



"" Muda urifika tayari, prince, princess, waliambiwa Kila mtu ashike kitambaa Cha mwenzake kwa nyuma afungue taratibu kwa ustadi mkubwa, na sisi tunahesabu, moja,mbili, tatu, mtafungua kwa pamoja, baada ya hapo Kila mtu amfunue mwenzake kwa wakati mmoja.


""Moja, mbili,tatu"""

Macho ya prince, na princess yaligongana kwa pamoja Kila mtu akaingiwa na fikra juu ya mwenzake, wote waliduwaaa!!!!!!


,,,,,,,,,,,,Itaendeleeaa,,,,,,,,,

Usikose sehemu inayofuata.

Je, Prince Niylan atakamilisha ahadi yake na Pinty?

 Na kuhusu Princess Tinner nini hatima yake katika nchi nyingine itakuwaje? Na vipi kuhusu malkia Cheness?

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi