UANDISHI WA MAJINA MATAKATIFU
Na
Riziki Kavishe
@The Catholic Diocese of Moshi
Ndugu Msomaji Karibu tuwe pamoja katika kuona jinsi ya kuandika majina Matakatifu na maana yake,
1. mungu - hii mungu ya herufi ndogo inamaanisha shetani/miungu, rejea ( 2CORINTHO 4:4, 2 WAFALME 1:2).
√ MUNGU/ Mungu - Tunamaanisha hapa ni Mungu mwenyewe, muumba wa Mbingu na Nchi, nafsi ya kwanza ya Utatu Mtakatifu. Rejea (YOHANE 3:16, LUKA 1:26).
2. bwana - tukisema neno bwana linamaanisha Mume, bosi au mkubwa wako wa kazi.
√ BWANA/ Bwana - maneno haya ya herufi kubwa hapa tunamaanisha ni Mungu mwenyewe. Rejea (MATHAYO 22:37)
3. roho - tukisema roho kupitia herufi ndogo tuna maanisha roho zetu, au roho za mashetani, wanyama nk.
√ ROHO/ Roho - Tunamaanisha ni Mungu mwenyewe nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu. Rejea (YOHANE 14:26).
4. yesu - hili linamaanisha yesu yule ambaye ni mchawi aliyetabiriwa katika Biblia maarufu kama Bar - yesu. They come apon a certain magician. Rejea (MATENDO YA MITUME 13:6)
√ YESU/Yesu - Hapa linamaanisha ni Mwana wa Mungu aliye hai, nafsi ya tatu sawa na Baba na Roho Mtakatifu. Rejea (MATHAYO 1:16).
Ndugu zangu watu wengi wamekuwa wakitumia god, mungu, yesu katika kubariki, hatuwezi kubarikiwa na mungu au yesu, anayestahili kutubariki ni MUNGU/Mungu au Yesu/YESU tuwe makini na uandishi wa maneno.
Kosa lingine Kanisa Katoliki hatuna Bikila Malia, wala Loho Mtakatifu, hawa labda ni wa makanisa mengine.
Kanisa Katoliki tunaye Bikira Maria ambaye ni Mama na mwombezi wetu. Pia tunaye Roho Mtakatifu ambaye ni Mfariji wetu.
Tuepuke hayo makosa.
Walio wangu waisikia sauti yangu na kuizingatia.
Makala hii imeandaliwa na Riziki Kavishe kutoka Jimbo Katoliki la Moshi na Kuchapishwa kwenu na Joseph E. Lugembe Jimbo Kuu Katoliki Dar Es Salaam.
WENU KATIKA KRISTO
@PHILOSOPHER OF WISDOM