Chongolo apokelewa na mabango Kigoma.

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo amewasili katika Mkoani Kigoma na anafanya mkutano mkubwa wa hadhara hii leo Julai 26,2023 katika Uwanja wa Mwanga Center, Kigoma mjini.

Katika mkutano huo unaotarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wanaCCM na wananchi kwa ujumla, kutoka mkoa huo na maeneo ya jirani, ambapo Chongolo na ujumbe wake wataelezea hatua kwa hatua kuhusu uamuzi wa Serikali kuingia makubaliano ya uwekezaji wa kuboresha uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Uelimishaji huo unalenga kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma kwa ufanisi mkubwa tofauti na ilivyo sasa na katika msafara huo ameambatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Stephen Wassira.

Wengine ni Katibu wa NEC Oganaizesheni, Usi Gavu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo, Naibu Waziri wa Ujenzi na  Uchukuzi, Atupele Mwakibete na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Jerry Silaa.


Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi