Mwanahabari mkongwe na mchambuzi wa masuala ya michezo ambaye pia ni mtangazaji katika kituo cha habari cha TvE na Efm anayefahamika kwa jina la Oscaroscar wengine wakimwita Baba Mzungu na wengi wao wakimuita Mzee wa Kaliua amewataka watu waache kubeza pindi mtu anapotunukiwa shahada ya udaktari huku akitanabaisha aina na namna ambavyo watu hawa wanapewa inakuwa kitu gani kimeangaliwa sana.
Katika ukurasa wake wa Facebook nguli huyo aliandika hivi
"UDAKTARI wa Heshima hapewi tu mtu yoyote ndiyo maana Baba yako hana. Doctorate Degree, Doctorial Studies au PhD ina maeneo makubwa mawili. Moja ni Heshima ya Kitaaluma ambayo huwa anatunukiwa mtu baada ya kufanya Tafiti na kutupatia Knowledge mpya na ya Pili, ni heshima ambayo huwa wanapewa watu baada ya kufanikiwa kupitia Application ya hizo Research zenye Academic qualification.
Hawa watu wote wanapaswa kupewa heshima sawa. Kuna watu ni wazuri sana kwenye Theories lakini kwenye application ni Sifuri. Kuna watu ukiwapeleka Shule ni Sifuri lakini kwenye application wako Super. Na wengi wao ndiyo Mabosi zetu. Na wengi wao ndiyo Matajiri zetu. Doctorate nyingi za Qualification, zimeajiriwa na Doctorate za heshima.
Kuna mtu ana PhD ya pale University of Dar es Salaam lakini ameajiriwa na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma. Kuna mtu ana PhD ya mambo ya Biashara, halafu kuna Mzee Said Salim Bakhresa. Kuna mtu ana PhD ya Muziki wa Kizazi Kipya, halafu kuna Diamond Platinumz. Kuna mtu ana PhD ya Soka, halafu kuna Mbwana Ally Samatta. Tuache kudharau Degree za Heshima wanazopewa watu. Hizi Degree haziji kwa bahati mbaya. Ukiona mtu wa Darasa la Saba anakuwa Mbunge mbele ya Maelfu ya watu wenye PhD huogopi? Kuna watu wana Phd za Biashara lakini hawawezi hata kuuza Duka. Udaktari wa Heshima hapewi tu mtu yoyote ndiyo maana Baba yako hana.
Watu wenye Phd as an Academic qualification, wanastahili kupewa heshima kwa sababu kufanya Tafiti na kuleta new knowledge sio kazi ndogo. Pia watu wanaotumia hizo new knowledge kama Mzee Bakresa, Mohammed Dewji, Mbwana Samatta, Diamond Platinumz, just to mention a few wakipewa Udaktari wa Heshima wala siwezi kushangaa. Wote wanastahili heshima. Udaktari wa Heshima hapewi tu mtu yotote ndiyo maana Baba yako hana. Naheshimu sana Phd zinazotokana na Academic qualification lakini pia, sidharau hata kidogo Doctorate za Heshima. Sidharau kwa sababu kama ingekuwa ni rahisi hata Baba yangu angekuwanayo.
Kuna watu Wanajenga sana M" alimalizia