Mhe. Gulamali amlilia Padre Fransis Kapurure Chuwa

 Na mwanahabari wetu



Ilikuwa tarehe 24 Feb 2021 Mbune wa Jimbo la Manonga Mhe. Seif Khamis Gulamali katika ukurasa wake wa Facebook aliweza kutoa yake ya moyoni na kuonesha ni kwa namna gani alivyoguswa na msiba wa aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Usongo (Kanisa Katoliki) iliyopo chini ya Jimbo Kuu Katoliki Tabora ambalo lipo chini ya Mhashamu Askofu Mkuu Paul Runangaza Ruzoka mara baada ya kupata taarifa za kusikitisha za kifo cha Paroko huyo ambaye amewahi kufanya kazi katika Parokia ya Igunga mjini akishikiria nafasi baada ya kifo cha Padre Alberto Bolle mwanzilishi wa St Margareth Maria Alokok Igunga. Mheshimiwa Gulamali katika ukurasa wake wa facebook ameandika hivi:




Ni taarifa ya kusikitisha lakini hakuna Namna ya kuikwepa na kuikubali kwa Kuondokewa na Baba Paroko Fransis Kapurure Chuwa
Nilipata nafasi ya Kuzungumza na wewe kwa Muda Mrefu sana Nyumbani kwako Ussongo.Ulinipa Historia ndefu na ya kina.Ulinipa Ushirikiano katika kipindi chako cha Utumishi.
Oooh Pole sana Pole sana kwa Kanisa,Pole kwa Ndugu,Pole kwa Waumini Parokia ya Ussongo na Wana Ussongo na Nyandekwa wote,Pole kwa Wana Jimbo na Jamaa wote,Pole kwa Waumini wote
Mwenyezi Mungu aiweke Roho yake Mpendwa Wetu Mahala Pema.

Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe. 

 Hakika Parokia ya Usongo imepata msiba mkubwa na wana jimbo la Tabora kwa Ujumla 

Joseph

Karibu tuweze kujadili na kupakua habari mpya zilizojili Afrika, Tanzania na pia hata Kidunia kwa ujumla

Chapisha Maoni

I, (taja jina lako/indicate your name)

Mpya zaidi Nzee zaidi